Search This Blog

Sunday, January 31, 2021

Breaking News: Treni yapata ajali vingunguti Dar

 


Imetokea Vingunguti Dar Es Salaam ikihusisha lori lililokuwa limebeba sukari na treni ya abiria. Taarifa zaidi zitafuata hapa hapa endelea kufuatilia muungwana blog.

Watendaji wa vijiji wilayani Kaliua wapigwa marufuku kutoza elfu moja ya ushuru wa ng'ombe wanaopelekwa mnadani


UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua imepiga marufuku kwa Watendaji wa Vijiji kuwatoza shilingi 1,000/= wafanyabiashara wa mifugo wanapokuwa wanapeleka minadani.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri hiyo Jerry Mwaga wakati Baraza la Madiwani alipokuwa akijibu hoja ya Madiwani waliolalamika Watendaji wa Vijiji kuwatoza wanyabiashara wa mifugo gharama za usafirishaji wa ng’ombe kabla hajauza ng’ombe wao.

Alisema mfugaji haruhusiwi kutozwa kiasi chochote cha fedha kipindi anaposafisha mifugo kwenda mnadani kwa ajili ya kuuza ng’ombe na pale anapokuwa anarudisha ng’ombe ambazo hazikununuliwa.

Mwaga alisema mifugo inatakiwa kutozwa kwenye eneo la Mnada husika na sio vinginevyo na kuwataka Watendaji wa Kata kusimamia utekelezaji wa agizo hilo ili wafugaji wasitozwe fedha kinyume cha utaratibu.

Aliwaomba Madiwani kuangalia maeneo ambayo wanadhani yanafaa kwa uanzishaji Minada ili waweze kutuma Watalaamu wa Halmashauri kwenda na kufanya utafiti na pindi watakapobaini kuwa kuna tija waweze kutoa vibali.

Mwaga alisema suala la uanzishaji wa minada ni muhimu liibuliwe na wananchi wa eneo husika kwa ajili ya kuuwezesha kuwa endelevu na kuewezesha  Halmashauri kuwa na chanzo cha uhakika cha mapato.

“Kama kuna wananchi wanataka kuwepo kwa mnada katika eneo lao wapeleke wazo katika Halmashauri ya Kijiji nayo itapeleka wazo hilo katika kikao cha Maendeleo ya Kata (WDC) ambacho nacho kitaandika kwa Halmashauri ya Wilaya na sisi tutawatuma wataalamu kwa ajili ya kuangalia eneo na kutoa kibali kwa ajili ya uanzishaji wa shughuli za minada” alisisitiza.

Alisema Minada ni muhimu katika uongezaji wa mapato ya Halmashauri lakini ni vizuri kama wazo litaanzia kwa wananchi katika eneo husika.



Kaliua waanza kulinda kisheria eneo la kihistoria la makumbusho ya mtemi milambo


HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imeanza mpango wa kuwekea mawe ya utambuzi wa eneo la mipaka ya makumbusho ya Mtemi Milambo kwa ajili ya kulilinda kisheria ili lisiweze kuvamiwa na kupoteza histoaria yake.

Hatua hiyo inalengo la kuhakikisha kuwa eneo hilo lenye Historia kubwa hapa nchini linaendelea kuwa endelevu kwa ajili ya manufaa ya wakazi wa Kaliua na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri hiyo Jerry Mwaga wakati Baraza la Madiwani alipokuwa akijibu hoja ya Madiwani waliotaka maeneo yote ya vivuto vya Kihistoria na utalii kutunzwa kwa ajili ya kuongeza mapato ya ndani na Taifa  kwa ujumla

Alisema mbalimbali na eneo hilo wataendelea kuainisha maeneo yote ya kale na yenye vivutio kupitia vigezo vinavyotakiwa ili yaweze kutambuliwa na kulinda kisheria kwa lengo la kuwavutia watalii wa ndani na nje.

Diwani wa Kata ya Usimba Benjamin Masanja alishauri kuwa  maeneo ya kihistoria yaliyopo wilayani Kaliua yanatakiwa kuboreshwa na kuweka watu wanaoweza kuelezea kwa ufasaha historia ya eneo husika kwa ajili ya kuwavutia watu mbalimbali wanaofanya utafiti na wale watalii kuyatembelea.

Alisema  hatua hii itaiwezesha Halmashauri kupata mapato na baadhi ya wananchi kupata ajira ya kuongoza Watalii na watafiti watakaopenda kujifunza kuhusu utajiri wa historia ya mambo ya kale yaliyopo wilayani humo.

Naye Diwani wa Kata ya Kazaroho Haruna Kasele alishauri kuwa wakati umefika kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ikaanza kuwekeza katika maeneo ya historia za kale ili kuvutia watalii wengi kutembelea maeneo husika.

Alisema hatua itawezesha Halmashauri hiyo kuongeza vyanzo vipya vya mapato ya ndani na kupata fedha kwa ajili ya kupeleka huduma za kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo utoaji wa huduma za afya , elimu na zile za ugani.

Kasele alisema Halmashauri ikiwekeza fedha kuboresha  Makumbusho ya Mtemi Milambo, eneo la kunyongea watumwa ambalo lilikuwa maarufu kwa jina la  Iselamagazi na njia ya Wajerumani  ambayo inaanzia Ndorobo wilayani Urambo kupitia Kazaroho wilayani Kaliua wataongeza mapato ya ndani.



Wanamgambo wa Al-Shabab wavamia hoteli Mogadishu, Somalia


Wanamgambo wa Al-Shabab nchini Somalia wamehusika katika makabiliano ya polisi na vikosi vya usalama katika hoteli moja iliyopo mji mkuu wa Mogadishu.

Kundi la Al-Shabab limekiri kutekeleza shambulizi hilo katika hoteli ya Afrik ambalo lilianza na bomu lililokuwa limetegwa kweye gari Jumapili mchana.

Hadi kufikia sasa, haijafahamika ni watu wangapi waliojeruhiwa lakini shirika la habari la AFP limeripoti kuwa karibu watu watatu wamefariki dunia.

Kundi hilo ambalo linahusishwa na kundi la wanamgambo la Al-Qaeda, mara nyingi hutekeleza mashambulizi dhidi ya serikali.

Inasemekana kuwa gari moja liligonga eneo la mbele la hoteli hiyo na kulipuka kabla ya mshambuliaji aliyekuwa amejihami kwa silaha kuvamia jengo la hoteli, kulingana na maafisa na wengine walioshuhudia shambulizi hilo.

"Mlipuko huo ulifanya hoteli hiyo ikaanza kutetemeka wakati tukiwa ndani tunaendelea na mzungumzo. tulishutuka, tusijue la kufanya," aliyeshuhudia Ahmed Nur amenukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Maafisa waandamizi wa usalama Mohamed Dahir ameliambia shirika la AFP kuwa raia wawili na afisa mmoja wa usalama wamethibitishwa kufariki dunia, "lakini idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka."




Ndege 750 waangamia kwa kutokana na homa ya ndege katika hifadhi ya Senegal


Ndege 750 wameripotiwa kuangamia katika mbuga ya hifadhi ya kaskazini mwa Senegal kutokana na homa ya ndege.

Waziri wa Mazingira Abdou Karim Sall , alitangaza kwenye kituo cha redio cha Rfm kuwa ndege 750 waliangaia kutokana na homa ya ndege mnamo Januari 23, katika hifadhi ya ndege ya Djoudj iliyoko eneo la Saint-Louis.

Sall alisema kuwa hifadhi hiyo ilifungwa kwa wageni na kutoa onya kwamba ugonjwa huo unaweza kuenea haraka sana kutokana na msimu wa uhamiaji.

Hifadhi ya ndege ya Djoudj, ambayo iko kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), inatoa hifadhi kwa aina 400 za ndege katika eneo la ukubwa wa hekta elfu 16.

Katika hifadhi hiyo, ndege 750 waliangamia mnamo Januari 23, kwa sababu isiyojulikana na mizoga yao ilipelekwa kufanyiwa uchunguzi.



Jeshi la Myanmar limetangaza hali ya dharura na kuchukua madaraka


Jeshi la Myanmar limetangaza hali ya dharura likidai udanganyifu wa kura katika uchaguzi, baada ya kuwakamata viongozi kadhaa akiwemo Aung San Suu Kyi.

Jeshi la Myanmar limetangaza hali ya dharura kwa muda wa mwaka mmoja na kumuweka jenerali wa zamani kama rais, kimetangaza Jumatatu kituo cha televisheni cha Myawaddy kinachomilikiwa na jeshi.

Jenerali wa zamani Myint Swe, ambaye awali alikuwa makamu wa rais, ametangazwa kama kaimu rais.

Hata hivyo, katika hali hiyo ya dharura kamanda mkuu wa jeshi Min Aung Hlaing amechukuwa udhibiti kamili wa nchi hiyo.

Tangazo hilo la jeshi limetolewa kufuatia kukamatwa kwa kiongozi wa Myanamar Aung San Suu Kyi baada ya siku kadhaa za mivutano nchini humo iliyozua hofu ya kutokea mapinduzi.

Rais Win Myint na viongozi kadhaa wa ngazi za juu wa chawa tawala pia wamekamatwa mapema Jumatatu, amesema Myo Nyun msemaji wa chama hicho cha National League for Democracy .

Akizungumza kwa njia ya simu na shirika la habari la dpa, Nyun amesema wakati wowote naye anaweza kukamatwa na wanajeshi hao.

Tangu wiki iliyopita jeshi la Myanmar limekuwa likitishia kufanya mapinduzi kwa madai kwamba kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi uliopita wa mwezi Novemba uliokipa ushindi chama cha Suu Kyi cha NLD.



Watu zaidi ya 1,643 wawekwa kizuizini kwenye maandamano wakitaka kuachiliwa huru Aleksey Navalny


Kulingana na takwimu zisizo rasmi, watu wasiopungua 1,643 walizuiliwa katika maandamano yaliyoendelea nchini Urusi wakitaka kuachiliwa huru kwa mpinzani wa Urusi Aleksey Navalny.

Maelfu ya watu, haswa wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu, walihudhuria maandamano yaliyopigwa marufuku katika miji mingi ya nchi, licha ya tahadhari za polisi.

Kulingana na mashirika ya haki za binadamu nchini Urusi, watu 1,643 pamoja na mke wa Navalny, Yuliya Navalnaya, walikamatwa, ambapo 338 kati yao walikuwa katika mji mkuu wa Moscow.

Wakati huo huo, waandamanaji wengine walikusanyika karibu na Gereza la Matrosskaya Tishina, ambapo Aleksey Navalny alizuiliwa,  na kupiga kelele wakitoa wito kwa serikali.



Barcelona yasikitishwa na kuvuja kwa mkataba wa Messi


Barcelona imesema kuwa itachukua "hatua za kisheria" dhidi ya gazeti la Uhispania la El Mundo baada ya kuchapisha maelezo kuhusu mkataba wa mshambuliaji, Lionel Messi wa pauni milioni 492.

Barcelona ilikanusha kuhusika kwa namna yoyote ile katika uchapishaji wa taarifa hizo.

Kwa mujibu wa El Mundo, mkataba wa Messi wa miaka minne ulikuwa wa thamani ya takriban euro 555,237,619 hadi Juni 30, 2021.

Hii inamaanisha kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 33, atakuwa anapokea pauni milioni 123 kwa msimu.

Barcelona imesema katika taarifa iliyotoa kuwa "inasikitishwa na uchapishaji wa maelezo hayo". Na kuongeza kuwa: "FC Barcelona haihusiki kwa namna yoyote ile katika uchapishaji wa taarifa hiyo na itachukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya gazeti la El Mundo, kwa uharibifu wowote ule ambao huenda umetokea kwasababu ya taarifa hiyo.

"FC Barcelona imeonesha kumuunga mkono Lionel Messi, hasa katika jaribio lolote la kumdhalilisha na kuharibu uhusiano wake katika klabu hiyo ambako amefanyakazi na kuwa mchezaji bora duniani na katika historia ya soka."

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina Messi alijiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13 lakini akatuma ombi la kutaka aruhusiwe kuhamia kwingineko mnamo mwezi Agosti.

Bado haijafahamiki ikiwa atabaki katika klabu hiyo wakati mkataba wake utakapomalizika.

Messi ni mchezaji wa Barcelona aliyeweka rekodi katika ufungaji wa magoli mengi na ameshinda makombe 10 ya La Liga, Ligi ya mabingwa mara nne na tuzo ya Ballon d'Or - alipewa tuzo mara sita ya mchezaji bora duniani.

Ombi lake la kutaka kuondoka Barcelona lilifuatiwa na kutoelewana kati yake na rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu, aliyeacha kazi hiyo mnamo mwezi Oktoba.

Messi, anayeelezea utawala wa Bartomeu kama "janga", alisema mnamo mwezi Desemba "Bado sijajua nitakachofanya."



MAGAZETI YA LEO 1.2.2021

















 

Utekelezaji miradi ya umeme mto Rumakali na Ruhudji, umefika patamu waziri wa nishati afika eneo la mradi

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Katika kutekeleza azma ya serikali ya kuhakikisha upatikanaji umeme nchini unakuwa wa uhakika na kuwapunguzia wananchi mzigo wa ghalama za umeme pamoja na kukuza uchumi wa viwanda,serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali ya kuzalisha umeme.


Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa Rumakali uliopo wilayani makete utakaozalisha megawati 222 pamoja na mradi wa Ruhudji uliopo mjini Njombe utakaozalisha megawati 358 na kufanya onezeko kubwa la nishati ya umeme huku mkoa wa Njombe ukiwa ni wa kimkakati huku ukiwa ni mkoa wa pili kwa uzalishaji mkubwa wa nishati ya umeme.


Waziri wa nishati Dkt,Medard Kalemani amebainisha hayo januari 30,2021 alipofika mkoani Njombe pamoja na kutembelea eneo la maporomoka yam to Rumakali uliopo kata ya Kipagalo wilayani Makete na kubainisha kuwa mradi huo utakaozalisha 222 MW ,tayari utekelezaji umeanza na serikali imeshatoa shilingi bilioni 899 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.


Kalemani amefafanua kuwa msukumo wanaoweke katika utekelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme ni kwasababu uzalishaji wake ni wa ghalama nafuu na kupelekea wananchi kupata bila changamoto kubwa ukilinganisha na aina nyingine ya umeme.


“Uzalishaji wa umeme kwa maji ni ghalama nafuu kulinganisha na vyanzo vingine,kuzalisha umeme kwa maji Unit moja inaghalimu kiasi cha sh.36 tu huku vyanzo vingine ni zaidi y ash.103 na kuendelea.Mradi wa Mwl,Nyerere utakapokamilika utawapunguzia wananchi mzigo wa bei za umeme na bei zitashuka sana”alisema Kalemani


Aliongeza “Utekelezaji wa mradi wa Rumakali na Ruhudji umekwishaanza,timu ya kutekeleza mradi huu imeshaundwa na kimsingi timu hiyo imenza na shughuli za matayarisho ya kuanza miradi tajwa na kufika Julai 02,2021 ujenzi rasmi wa miaradi ya Rumakali na Ruhudji utaanza”aliongeza Kalemani


Mbali na hayo amesema katika mradi wa Rumakali kitajengwa kituo cha kupokea umeme na utasafirishwa hadi Mwakibeta jijini Mbeya umbali wa kilomita 150 na vijiji vyote vitakavyopitiwa na njia ya kusafirisha umeme vitapatiwa nishati hiyo.


Aidha amesema bado mikakati ya ukamilishwaji wa kazi ya kupeleka umeme vijijini unaendelea na taratibu zote za kufikisha umeme vilivyosalia nchini zimekamilika ambapo februari 05 mwaka huu wakandarasi wataanza kuingia kazini ili kukamilisha vijiji vilivyosalia ndani ya miezi 18 kwa kuwa tayari serikali imeshatoa shilingi bilioni 851 kwa ajili ya kazi hiyo huku akiwataka wananchi ambao ambao bado vijiji vyao havijapatiwa huduma kuwa wavumilivu.


Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Rumakali,meneja uendelezaji wa vyanzo vya umeme kutoka shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mhandisi Toto Zedekia amesema,wamejiridhisha baaday kufanya utafiti na tathmini ya kina kuwa maporomoko yam to Rumakali una maji mengi na yakutosha kuzalisha umeme.


“Tumejiridhisha vya kutosha mto huu una maji mengi na kutosha kwa kuwa una mita za ujazo 13 kwa sekunde” na kuongeza kuwa


“Litajengwa bwawa lenye urefu wa mita 870 kutoka kingo moja kwenda nyingine na urefu wa kwenda juu utakuwa ni mita 70 na litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji takribani lita 280”


Awali akitoa tarifa ya hali ya upatikanaji wa umeme mkoani Njombe,kaimu meneja wa kanda ya Nyanda za juu kusini Maghalib Mhandisi Yusuph Salim amesema,hali ya umeme mkoani humo imeimarika zaidi tofauti na miaka ya nyuma na hali hiyo imechangiwa na kukamiilika kwa mradi wa Makambako hadi Songea.


Aidha mhandisi Yusuph amesema upatikanaji wa umeme mijini na vijijini ni wa uhakika na kupitia miradi ya umeme vijijini (REA),takribani vijiji 293 vya mkoa wa Njombe vimefikiwa na huduma ya nishati huku vikisalia 88 ambavyo vyote vimeingizwa katika mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili huku 90% ya miradi ya REA ikiwa imekamilika.


Baadhi ya wananchi wa kata ya kipagalo wamefurahishwa kuona mwanga wa kuanza kwa mradi wa umeme katika mto Rumakali kwa kuwa wamekuwa wakisubiri tangu miaka 40 iliyopita huku wakiamini kupta fursa za kiuchumi mradi huo utakapoanza rasmi.


Katika ziara hiyo waziri wa nishati Dkt,Medard Kalemani ameongozana na maafisa waandamizi kutoka wizara ya nishati na shirika la umeme Tanzania (TANESCO)



Congo, Brazaville: Chama kikuu cha upinzani kususia uchaguzi wa Machi 21

 


Chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya Congo kimesema kitasusia uchaguzi uliopangwa kufanyika Machi 21. Kwenye uchaguzi huo Rais Denis Sassou Nguesso aliyepo madarakani kwa miongo kadhaa anawania kuchaguliwa tena. 


Nguesso mwenye umri wa miaka 77 ameshikilia madaraka kwa miaka 36 sasa na hivyo kuwa mmoja wa viongozi waliodumu kwa muda mrefu madarakani ulimwenguni. Katibu wa kwanza wa chama cha upinzani cha Pan-African Union for Social Democracy (UPADS) Pascal Tsaty Mabiala amesema kufanyika kwa uchaguzi huo wa urais isiwe sababu ya kuligawanya taifa kama ilivyokuwa zamani na hivyo chama chake kimeamua kutoshiriki katika uchaguzi huo. 


Chama hicho cha UPADS cha aliyekuwa rais wa zamani Pascal Lissouba ndicho pekee cha upinzani chenye uwakilishi bungeni. Congo Brazaville imo kwenye mgogoro mkubwa wa kiuchumi uliosababishwa na kushuka kwa bei ya mafuta, deni la muda mrefu pamoja na athari za janga la corona.



Maandalizi ya uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Manyara yapambana moto

 


Na John Walter- Manyara

Kamati ya maandalizi ya Uchaguzi wa marudio wa Chama cha Soka mkoa wa Manyara (MARFA) imetangaza majina yaliyopitishwa kugombea nafasi za mbalimbali za uongozi wa chama hicho.


Majina hayo yamepatikana baada ya usaili uliofanyika kwa wagombea hao januari 23,2021.


Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji. 


Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa  na Katibu wa Kamati Mussa Rehani, imetaja majina ya wagombea na nafasi ya mwenyekiti ni Gerald Mtui na Fratern Kwahhison, Makamu Mwenyekiti yupo Victor Kijazi.


Katika nafasi ya Katibu mkuu, mgombea ni  Wilhelmon Mayo na mgombea  katibu msaidizi ni Denis Bakuza.


Mweka hazina aliechukua fomu ya kugombea ni mtu mmoja pekee Jumanne Dotto.


Mjumbe Mwakilishi Vilabu Albert Ferdinand, mjumbe mwakilishi mkutano mkuu TFF Hassan China na mjumbe mwakilishi soka la wanawake Rose Mkindi.


Nafasi nyingine ni wajumbe Kamati ya utendaji ambao ni Charles Mligo, Wilfred Mwanyika, Charles William pamoja na Nuru Mkireri.


Katibu wa Kamati ya maandalizi ya uchaguzi wa marudio wa chama cha soka mkoa wa Manyara Mussa Rehani amesema uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Februari 13,2021 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara.



Pentagon yasimamisha utoaji chanjo kwa wafungwa wa Guantanamo

 


Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema itasimamisha mpango wake wa kuwapa chanjo dhidi ya COVID-19 wafungwa wa makosa ya ugaidi wanaozuiwa kwenye kambi ya Guantanamo kufuatia kuongezeka kwa malalamiko katika wakati ambapo nchi hiyo inajikakamua kuwachanja kwanza watumishi wa afya na wazee. 


Msemaji wa wizara hiyo John Kirby ameandika hayo kupitia ukurasa wa twitter akisema hakuna mfungwa yoyote kwenye kambi hiyo ambaye tayari amechanjwa. 


Kirby amekiri akisema ni kweli rais Joe Biden amesema ana mpango wa kutokomeza virusi vya corona katika siku yake ya kwanza ofisini lakini hakusema atawapa chanjo magaidi kwanza kabla ya Wamarekani. 


Kambi ya Guantanamo iliyoko Cuba inawazuia washukiwa wa makosa ya ugaidi ikiwa ni pamoja na Khalid Sheikh Mohammed, mfuasi wa kundi la Al-Qaeda anayedaiwa kupanga shambulizi la Septemba 11.



Urusi yajiandaa kwa maandamano makubwa ya mpinzani utawala wa Urusi Alexei Navalny

 


Mamlaka nchini Urusi zimefunga vituo vya treni na basi vya abiria na kuzuwia shughuli za watu katika mji mkuu wa nchi hiyo Moscow kabla ya mkutano maandamano makubwa yakiyopangwa kwa ajili ya kumuunga mkono kiongozi wa upinzani na mkosoaji wa utawala Urusi Alexei Navalny.


Migahawa mingi na maduka katikati ya mji huo vitafungwa na usafiri wa treni wa chini ya ardhi utabadilishwa.


Zaidi ya watu 4,000 walikamatwa kote nchini Urusi wakati wa mikutano wiki iliyopita.


Bw Navalny alifungwa jela aliporejea nchini Urusi baada ya kupona jaribio la kumuua kwa sumu inayoua neva.


Mpinzani huyo wa serikali ya Urusi alitakamtwa tarehe 17 Januari kwa kutotimiza masharti ya hukumu iliyoahirishwa dhidi yake. Alikuwa ndio amewasili tu kutoka mjini Berlin, ambako aliishi kwa miezi kadhaa akiendelea kupona shambulio la sumu ambalo nusura limuue.


Mamlaka nchini Urusi zinasema kuwa alipaswa kuripoti polisi kwasababu ya kesi yake ya ubadhilifu wa mali ya umma iliyoahirishwa.


Bw Navalny alipinga kukamatwa kwake jambo ambalo anasema "ni ukiukaji wa sheria ", na kuongeza kuwa mamlaka zinafahamu fika kwamba alikuwa akitibiwa mjini Berlin kutokana na sumu ya Novichok , ambayo alipewa Urusi mwezi Agosti mwaka jana.


Maandamano makubwa ya kumuunga mkono Bw Navalny yameanza kufanyika nchini Urusi , licha ya onyo jipya kutolewa na polisi kuhusu mikusanyiko ya watu ambapo polisi wanawashikilia watu zaidi ya 250 , kwa mujibu wa kikundi cha maandalizi ya maandamano hayo OVD-Info protest monitoring group. Maandamano katika mji mkuu Moscow yanatarajiwa kufanyika baadae leo.


Washirika kadhaa wa Bw Navalny wamekuwa wakifungwa tangu juma lililopita na wengine , akiwemo kaka yake na mwanaharakati wa kikundi cha Pussy Riot Maria Alyokhina, ameweka katika kifungo ha ndani.



Aliyetelekezwa na mume kisa mtoto mwenye ulemavu asaidiwa na Meridian bet

 


Siku chache zilizopita baada ya baadhi ya vyombo vya habari kufanya kipindi na Zuhura Shabani (32) ambaye ni mama mwenye mtoto mmoja aliyetelekezwa na mume wake kwa kile kilichodaiwa kuwa ni ulemavu wa mtoto wake hatimaye apewa msaada na MERIDIAN BET


Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Mkuu wa Utawala wa kampuni ya michezo ya kubashiri MERIDIAN BET Cornelius Boenman amesema kampuni yao imekuwa ikishiriki katika jamii kwa lengo la kuwasaidia wenye uhitaji.


Naye Meneja ustawi wa MERIDIAN BET Amani Maeda amesema wao kama kampuni wameguswa na matatizo aliyonayo Zuhura Shabani hivyo wakaamua kumsaidia mtaji wa biashara.


Kwa upande wake Zuhura ameishukuru Kampuni ya Meridian Bet kwa msaada huo ambapo amesema utasaidia kumuwezesha kufungua saluni ya kike ambayo iasaidia kumlea yeye pamoja na mtoto wake.


‘Naishukuru sana Kampuni ya Meridian Bet kwa moyo mlioonesha wa kunisaidia kiasi hiki cha pesa, naahidi pesa hii mliyonipatia nitaitendea haki, nitafungua Saluni kama nilivyosema najua saluni itanisaidia kuendesha maisha yangu na mwanangu na kunipunguzia kutembea mtaani na kuomba omba msaada, Mungu awabariki muendelee na moyo huo huo”. Alisema Mama huyo


Zuhura Shaban amebahatika kupata mtoto wa kiume anayeitwa Eklam ambaye alizaliwa na matatizo ya utindio wa ubongo na kusababisha kushindwa kukaa, kusimama wala kufanya chochote jambo lililofanya mume wake kumtelekeza yeye na mtoto.



Maandamano mapya yafanyika nchini Ufaransa kupinga sheria ya usalama wa taifa

 


Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza katika miji kadhaa nchini Ufaransa kupinga muswada wa usalama ambao wanasema utawazuia watu kurekodi na kuchapisha video zinazohusiana na ukatili wa polisi.


Kulingana na waandaaji wa maandamano hayo, kulikuwa na mikusanyiko zaidi ya 55. Wanaharakati wa vuguvugu la Fulana za Manjano lililoshika kasi kwa zaidi ya mwaka mmoja nchini Ufaransa pia walishiriki kwenye maandamano hayo.


Kutokana na maandamano ya mara kwa mara, kifungu chenye utata cha 24 kulingana na sheria ya usalama wa taifa kitafanyiwa marekebisho ambapo waandamanaji hao wanapinga rasimu ya sheria hiyo ambayo itazuia shughuli za upigaji picha au kuwarekodi polisi. Raia wa Ufaransa pia wanapinga utumiaji wa zana za ufuatiliaji kama ndege zisizo na rubani na kamera zinazowafuatilia watembea kwa miguu.


Wanaharakati wanataka kifungu hicho cha 24 kifutwe kabisa lakini chama kinachotawala cha LREM cha Rais Emmanuel Macron kinakusudia kuipitisha sheria hiyo.


Video iliyosambazwa ikiwaonesha polisi wazungu wakimpiga mtayarishaji wa muziki mweusi katika studio yake ya mjini Paris mnamo Novemba 21 ni tukio lililochochea hasira za watu juu ya sheria hiyo mpya, inayopingwa na wengi wanaosema inaashiria kuwa rais Macron anageukia siasa za mrengo wa kulia. 


Serikai ya Ufaransa yasemaje

Serikali ya Ufaransa imesema sheria iliyopendekezwa inahitajika kwa sababu maafisa wa polisi wamekuwa ni walengwa, wanashambuliwa na miito ya vurugu dhidi yao imeongezeka kwenye mitandao ya kijamii. Serikali imesema sheria hiyo itawalinda vyema polisi.


Kwa upande wake vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema mpango huo wa utekelezaji wa sheria hiyo mpya ya usalama wa taifa unatumiwa kuvizuia vyombo vya habari kutangaza juu ya maandamano ya kupinga serikali.


Sheria hiyo ambayo tayari imeidhinishwa na bunge, itapelekwa kwenye baraza la Seneti, ambalo ni tawi la juu la bunge la Ufaransa, mnamo mwezi Machi.


Mnamo mwezi Januari, maelfu ya watu waliandamana kupinga sheria hiyo katika mji mkuu wa Paris na katikamiji mingine kote nchini Ufaransa.



Binti akiri kudanganya kubakwa, aliyemtaja afungwa jela miaka 60

 


Siha Amezongwa na majuto akikumbuka kile alichokifanya miaka mitatu iliyopita.


Maria Sanga (20), mkazi wa kijiji cha Kilingi Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, ameamua kuiangukia Serikali kutengua hukumu kwa kijana aliyemsingizia kuwa alimbaka na kumpa ujauzito mwaka 2017.


Kijana huyo alikuwa kidato cha nne huku yeye akiwa kidato cha pili, na baada ya kesi kusikilizwa mwaka 2018 katika kesi namba moja ya mwaka 2017, Tumaini Frank hatimaye alikutwa na hatia ya kumpa ujauzito Maria na kisha kufungwa gerezani miaka 60.



KKKT kama TEC, yatoa waraka wa angalizo


Wiki moja baada ya Kanisa Katoliki kutahadharisha, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) nalo limetoa waraka kuwataka waumini wake kujihadhari na ugonjwa wa corona.


KKKT imewakumbusha waumini wake na Watanzania kwa ujumla kuzingatia maelekezo ya kujikinga na mamabukizo ya virusi vipya ambavyo vimeshambulia nchi kadhaa duniani.


Waraka huo umetolewa na mkuu wa kanisa hilo nchini, Askofu Frederick Shoo na kupewa jina la ‘tusimjaribu Mungu kwa kutokuchukua tahadhari’ kwenda kwa maaskofu wa dayosisi zote na wajumbe wa halmashauri kuu ya kanisa hilo.



TAMBUA DALILI ZA KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUME UUME MFUPI NA TIBA YAKE ,NA TAMBUA DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE

  


Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo kikamilifu shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili,homon,Neva,misuli,hisia na miriji ya damu


CHAZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME KUWA MFUPI


  • Kuwa na halemu (cholesterol) na shinikizo la damu( B,P,)au ugonjwa wa motorcyclelUaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
  • Kisukari,
  • Umri hasa wazee
  • Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
  • Tabi za kujichua kwa mda mrefu ,kutopata usingizi
  • Ngiri, vidonda vya tumbo,
  • Tumbo kuunguruma na kukosa choo
  • Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibu magonjwa Kama vile, kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari


DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


1kuwahi kufika kileleni,2kukosa hamu ya tendo 3kushindwa kurudia tendo la ndoa 4uume kusimama kwa uregevu au kushindwa kusimama 5 kuchoka Sana baada ya tendo la ndoa


TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME


dawa ya MJN ni dawa ya asili isiyokuwa na mkemikali yoyote dawa hii ipo kwenye mfumo wa kunywa na kuchua pia dawa hii ni tamu Sana kwani imechanganywa na asari ni tofauti na  ulizowahi kutumia usaidia ata wazee wenye miaka 80 pi uboresha uume wa mwanaume ulioingia ndani na kuwa mfupi


MTN ni dawa  inayosaidia wagonjwa wa kisukari dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge na unga 


Ndugu mteja epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahii kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO 


WASILIANA NAMI TABIBU DITTU KWA SIMU 0714448999 AU Whatsapp +255714448999 ofisi ipo mbagara sabasaba  na morogoro mwanza yupo wakala  walio nje ya mkoa  au nnje ya nchi utatumiwa sehemu yoyote ulipo



Wachezaji wa Simba SC watakaoikosa TP Mazembe


Kuelekea mchezo wa Simba Super Cup leo Januari 31, 2021 kati ya TP Mazembe dhidi ya Simba SC kwenye uwanja wa Mkapa, hawa ndio wachezaji wa Simba SC ambao hawatakuwa sehemu ya mchezo huo.


Kwa mujibu wa meneja wa timu ya Simba SC Abbas Ally, wachezaji wa timu hiyo ambao walikuwa na timu ya taifa kwenye michuano ya CHAN kama Aishi Manula hawatacheza licha ya kujiunga na kambi ya Simba SC.


Wengine ni Shomari Kapombe, Said Ndemla, Ibrahim Ame na John Bocco, ambao nao watakosa mchezo wa leo dhidi ya TP Mazembe. 


Mchezo huo pia utatangazwa mubashara kupitia East Africa Radio na watangazaji Mtaalam wa Soka Ibra Kasuga na Abissay Stephen kuanzia saa 9:30 mchana ambapo studio watakuwepo David Kampista na Tigana Lukinja.



Uingereza yaanzisha pasi mpya ya kusafiria kwa raia wa Hong Kong

 


Hatimaye raia wa Hong Kong sasa wanaweza kuomba uraia nchini Uingereza kuanzia hii leo baada ya visa mpya zinazotolewa na nchi hiyo kuwapatia fursa ya kuwa raia, kufuatia Beijing kuanzisha sheria mpya ya usalama wa taifa katika jiji hilo kitovu cha biashara barani Asia mwaka jana. 


Hatua hii inachukuliwa wakati China na Hong Kong zikiwa zimesema hazitaitambua tena pasi ya kusafiria ya Uingereza, kama hati halali ya kusafiria kuanzia leo. 


Uingereza inakisia kwamba kupitia viza hiyo huenda watu 300,000 pamoja na jamaa zao wataingia nchini humo. 


Uingereza na China zimekuwa zikizozana kwa miezi kadhaa juu ya sheria hiyo ambayo London na Washington zinasema ni hatua inayolenga kubana uhuru wa kujieleza kwa wakosoaji jijini Hong Kong baada ya maandamano ya wanaounga mkono demokrasia yaliyofanyika kati ya mwaka 2019 na mwaka jana.



Ndege ya Rais wa Ecuador yatua kwa dharura

 


Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli, ameagiza Bi. Elizabeth Sarali mwenye miaka 90, mkazi wa Manyoni mkoani Singida kurudishiwa umiliki wa eneo lake ambalo alipokonywa na kumilikishwa mfanyakazi wa idara ya ardhi.


Rais Magufuli ametoa maagizo hayo akiwa njiani kurejea Dodoma leo Januari 31, 2021, aliposimama Manyoni mkoani Singida na kusikiliza kero mbalimbali, ikiwemo ya mgogoro wa ardhi baina ya mkazi mmoja na Halmashauri.


''Hili eneo ambalo nimeambiwa amepokonywa bibi Elizabeth Sarali mwenye miaka 90 kisha akamilikishwa mfanyakazi wa idara ya ardhi ambaye amepangisha Mnara wa Vodacom, hiyo hati ifutwe na arudishiwe umiliki huyo bibi aanze kulipwa pesa yake  ya pango na hao waliopanga'' - Rais Magufuli

 

Aidha amewaagiza Mkuu wa mkoa, Wilaya na Ofisa Ardhi pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni, kutatua mgogoro huo na mingine ya ardhi mara moja.


''Inaonekana Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni hauna 'information', utadanganywa na watendaji kuhusu mambo mengi ya ardhi, shirikiana na Madiwani kutatua migogoro hii ya ardhi, sipendi madiwani ambao ni 'Yes man' kwenye kila kitu huwa sio wazuri'', amesema Rais Magufuli.



Serikali imeokoa shilingi milioni 389-Dkt. Gwajima

 


Wizara ya Afya imeokoa takribani shilingi milioni 389 katika ujenzi wa jengo la Idara ya huduma za wagonjwa wa dharura linalojengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora- Kitete ambalo limewekwa jiwe la msingi na Rais Dkt. John Magufuli.


Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt. John Pombe Magufuli, Dkt. Gwajima amesema ujenzi wa jengo hilo litakalo wahudumia wakazi wa Tabora, mikoa ya jirani na hata nje ya nchi kutokana na barabara kuu zinazopita mkoani hapo kwakuwa jengo hilo litakua na uwezo  kuwahudumia wagonjwa 50 hadi 60 tofauti na awali ambapo walikua wakihudumia wagonjwa 3 hadi 5.


"Tumepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Rais mimi pamoja na wizara yangu tutayafanyia kazi ikiwemo kuongeza madaktari bingwa, kuwafuatilia wale walioondoka pamoja na jengo la huduma la mama na mtoto kwa ajili ya kujifungua na ICU", amesema Dkt. Gwajima.


Miradi mingine ya ujenzi wa Idara ya huduma za wagonjwa wa dharura nchini ambayo wizara inashirikiana na Global Fund inatekelezwa na ipo hatua mbalimbali za kukamilishwa katika mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Mara na Tanga.



Mlipuko katika duka la mikate Iraq

 


Watu 26, 3 kati yao wakiwa mahututi, wamejeruhiwa katika mlipuko kwenye duka la mikate kwa sababu ya kuvuja kwa gesi huko Iraq.


Jengo ambalo duka hilo lilikuwepo liliporomoka Kwa sababu ya vurugu za mlipuko katika duka la kuoka mikate katika jiji la Divaniye.


Mlipuko huo umesababisha hasara kubwa na uchunguzi umeanzishwa kufuatia tukio hilo.



Saturday, January 30, 2021

Barrick yatoa matumaini kuhusu deni kwa Serikali

 


Mjumbe wa bodi ya kampuni ya madini ya Twiga, Casmir Kyuki amedokeza kuwapo kwa matumaini ya Serikali ya Tanzania kulipwa deni lake la Dola200 milioni ( sawa na Sh463 bilioni) ambazo inaidai kampuni ya Barrick, ikiwa mwenendo wa soko la dhahabu duniani utaendelea kuwa mzuri kama ulivyo sasa.


Fedha hizo ni sehemu ya Dola 300 milioni (Sh695 bilioni) ambazo Barrick iliahidi kuzilipa kama fidia, kutokana na kampuni yake tanzu ya Acacia kudaiwa kodi na tozo mbalimbali na mamlaka za serikali ya Tanzania


Malipo ya fedha hizi zilikuwa miongoni mwa makubaliano kati ya Kampuni ya Barrick na Serikali ya Tanzania ya uendeshaji wa shughuli za madini yaliyosainiwa Julai, 2019 na baadae kuanzishwa kwa kampuni ya madini ya Twiga, Oktoba, 2019.


Kampuni ya Barrick ilishatoa kiasi cha Dola100 milioni (Sh231 bilioni), ambapo kiasi cha Dola200 milioni inatakiwa kuzilipa katika miaka minne ijayo.


Kyuki na Rais wa Barrick, Mark Bristow juzi walizungumza na waandishi wa habari kwenye mgodi wa Bulyanhulu ulioko mkoani Shinyanga na kueleza mafanikio ya mwaka mmoja ya uendeshaji wa pamoja wa migodi ya dhahabu kwa ubia chini ya kampuni ya Twiga.


Alisema katika kipindi hicho kumekuwa na mafanikio makubwa katika mwaka uliopita hasa ikichangiwa zaidi na bei nzuri ya dhahabu kwenye soka la dunia,


Aligusia kitendo cha kulipwa kwa kodi na tozo mbalimbali za Serikali na kutolewa kwa gawio kama makubaliano ya uanzishwaji yanavyoelekeza, kunaashiria mwelekeo mzuri.


Kyuki alisema kutokana na mwenendo huo mzuri wa kimapato, kuna uwezekano kwa Barrick kukamilisha deni lao mapema hata kabla ya wakati uliopangwa.


“Unajua Twiga imeleta ufanisi mkubwa katika uendeshaji wa sekta ya dhahabu, na katika mwaka mmoja uliopita kodi, tozo na gawio vimelipwa,’’alisema.


Imeandikwa na Samson Mfalila, Mwananchi Mwananchipapers@mwananchi.co.tz



Arusha DC yataja sababu za kutofikia malengo ya ukusanyaji mapato

 


Halmashauri ya Arusha imetaja sababu zilizochangia kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2020/21,ikiwa ni pamoja na kokosekana kwa ulipaji kodi wa hiari kwa wafanyabishara na kuyumba kwa bishara ya utalii.


Hayo yamesemwa Januari 29, na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Saad Mtambale, akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani.


Amesema halmashauri hiyo ilijiwekea makisio ya makusanyo ya Sh billioni 59.188 ila hadi Desemba 31 mwaka jana ilikuwa imekusanya zaidi ya Sh bilioni 21.837.


Ametaja sababu hizo ni kukosekana kwa ulipaji kodi wa hiari kwa baadhi ya wafanyabiashara na kuwa bila kusukumana wengi wao hawatoi kodi ambapo wamejipanga kama watendaji kutembelea maeneo mbalimbali na kuhakikisha kila anayepaswa kulipa kodi analipa na kwa kiwango kinachotakiwa.


Amesema changamoto nyingine ni kushuka kwa biashara ya utalii ambapo amesema kuwa uchumi wa Arusha unategemea  sana utalii na kutokana na janga la corona lililokumba dunia hali ya utalii bado haijawa nzuri hivyo kuchangia kushuka mapato.


“Watalii wanapokuja kwa wingi biashara nyingi zinachangamka  ushuru wa huduma tupata hapo na ushuru huo ni sehemu ya mapato hivyo tumekutana na changamoto hizi  lakini kuna jitihada mbalimbali  tunaendelea nazo kama watendaji na tutafikia malengo tuliyojiwekea,”amesema Mkurugenzi


Amesema kutokana na sababu hizo wamebuni vyanzo vingine vya mapato ikiwemo shule ya mchepuo wa kingereza ambayo imeshaanza kupokea wanafunzi,urasimishaji ardhi ambapo kwenye kijiji cha Kiserian kilichopo kata ya Mlangarini, hadi Januari 25, 2021 viwanja zaidi ya 3,000 vilitambuliwa na kupimwa ambapo katika mradi huo watapata zaidi ya Sh milioni 400.


Ametaja mkakati mwingine ni kuja na wazo la kuanzisha kituo cha Radio ambacho kitawasaidia kujitangaza na kuondoa changamoto ya wakazi wa halmashauri hiyo.


“Kuna wafanyabiashara wengi waliopo eneo la mita 200 upande wa halmashauri yetu lakini kwa kutokuifahamu halmashauri hiyo wanaenda kulipa kodi halmashauri ya Jiji la Arusha na ili tuweze kujitangaza tumeona tuanzishe radio yetu na tayari tumeshaanza kulifanyia kazi,”ameongeza Mkurugenzi huyo.



Diamond aibuka na sakata mtoto wake kupewa mwanaume mwingine

 


Wakati sakata la yupi baba mzazi wa msanii wa muziki, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz likiwa bado vichwani mwa watu, msanii huyo ameibuka na kufunguka kuwa hata yeye ana mtoto ambaye mzazi mwenzie amegoma kumpatia na huenda ameshapewa baba mwingine.


Diamond alisema hayo kupitia mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha The Switch cha Wasafi FM, Januari 28 baada ya kuulizwa anadhani ana watoto wangapi.


Akijibu, Diamond alisema anachojua ana watoto sita, tofauti na watu wengi wanavyofahamu kwamba ana watoto wanne ambao ni Tiffah na Nillan aliozaa na Zarina Hassan “Zari”, Dylan aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto na Naseeb Junior aliyezaa na mwimbaji kutoka Kenya, Tanasha Donna.


“Watu wengi wanafahamu mtoto wangu wa kwanza ni Tiffah, lakini ninao wengine wawili ambao walizaliwa kabla yake. Kuna mmoja yuko Mwanza, mama yake amegoma kunipa, pia juzi kati nimeletewa mtoto mwingine wa kike hapa hapa Dar es Salaam, lakini sijawahi kumuona.


“Mama wa huyo mtoto yuko katika mahusiano mengine na mwenye mahusiano naye anajua ni mwanae. Mambo yale...kwa hiyo yule mama anaogopa kuniletea mtoto kwa sababu akikutana na mimi mtoto ataenda kusema kwa baba yake tumeenda kwa Diamond. Kwa hiyo mtoto yupo, inatafutwa timing siku moja kumuona, lakini mama yangu amemuona na akaniambia, mwanangu, yule mtoto ni wako, mmefanana sana,” alisema mkali huyo wa wimbo “Waah”.


Alisema ikiwa watoto hao wawili ni wa kweli, Tiffah atakuwa mtoto wa tatu kwa kuzaliwa.


Sakata la nani baba mzazi wa msanii huyo lilipoanza kuvuma mapema mwezi huu, mama mzazi wa Diamond aliweka bayana baba wa msanii huyo ni mzee anayefahamika kwa jina la Salum Iddi Nyange na sio Abdul Juma kama ilivyokuwa inafahamika awali.


Jambo hilo liliibua mjadala kwa mashabiki na wafuatiliaji wa matukio ya kuvutia ya familia hiyo ikiwemo huenda hakukuwa na uhusiano mzuri kati ya mama Diamond na baba mzazi wa msanii huyo ndiyo maana akamkabidhi mtoto kwa baba mwingine ambaye ndiye huyu mzee Abdul.


Hii inamaanisha matukio yanajirudia ukilinganisha na hiki kinachotokea sasa kwa Diamond kutopewa mtoto wake ambaye anadai yupo Dar es Salaam.


Diamond alifafanua kuwa “Mama akiniambia kitu huwa hadanganyi kwa sababu macho yake ni kama teknolojia inayotumika viwanjani kuhakiki usahihi wa mpira ulipo (VAR), alipomuona aliniambia ni wangu, nasubiri nimuone,” alisema.


Diamond pia alielezea kuhusu sakata la nani baba yake halisi kwa kusema kuwa “Nimefahamu kuwa mzee Abdul siyo baba yangu tangu mwaka 2000, alienieleza ukweli alikuwa mama yangu mkubwa (mama yake Rommy Jones).


“Nilikuwa napenda sana kumtajataja baba yangu, kipindi hicho alikuwa ameshaondoka nyumbani, ametuacha Tandale. Sasa ilikuwa inawaudhi watu akiwemo mama mkubwa kwa sababu alikuwa hatuhudumii wakati alikuwa vizuri kiuchumi. Enzi hizo alikuwa na magari na pesa za kutosha.”


Hilo siku moja lilimkera mama yangu mkubwa na ndipo kwa hasira akamueleza ukweli kuwa baba yake mzazi sio Abdul anayemtajataja kila kukicha, bali ni mtu mwingine anayeitwa Salum Iddi au Salum Bubu kwa jina la utani.


“Ndipo akaniambia kama unakata kuthibitisha nenda pale Tandale sokoni wanapouza mchele wa jumla. Kamuulize mtu anayeitwa Salum Bubu, halafu mwambie mimi mwanao.” alisema.


Diamond alisimulia kwamba alienda huko na kweli akakutana na baba yake.


“Baba akanipa mchele na shilingi mia mbili. Nikapeleka mchele nyumbani mia mbili nikatumia. Na tangu hapo huo ndiyo ukawa mchezo wangu. Nikawa naenda kazini kwa baba mara kwa mara.” Alisema ile kwenda mara kwa mara kwake ikarudisha ukaribu wa mama yake na Salim Nyange na baadaye mzee huyo akampeleka Diamond nyumbani kwake Kariakoo alipokuwa akiishi kwenda kumkutanisha na ndugu zake.


Diamond alifafanua kuwa hata shughuli zake za muziki alianza akiwa Kariakoo alipokuwa akienda na kuishi mara kwa mara kwa baba yake.




Hofu ya bomu kwenye msikiti Uswidi

 


Kisanduku kinachofanana na bomu kimepatikana kwenye mlango wa msikiti mmoja uliopo katika mji mkuu wa Stockholm nchini Uswidi.


Imam wa Msikiti wa Stockholm, Mahmoud Khalfi, alitoa  maelezo kwenye kituo cha SR cha redio ya serikali nchini Uswidi na kusema kwamba walikuta kisanduku kinachofanana na bomu kilichowekwa kwenye mlango wa kuingilia msikitini na kuzua hali ya wasiwasi.


Khalfi alisema,


“Tulipofika kwenye sala ya asubuhi, tuliona kisanduku kiinachofanana na bomu mlangoni. Nyaya zote 3 kutoka kwenye kisanduku hicho ziligandishwa mlangoni. Tuliwajulisha polisi haraka ambao baadaye walitenganisha kisanduku na nyaya zake na  kuchukua ili kufanyia uchunguzi.”


Akibainisha kwamba misikiti yake imekuwa ikishambuliwa mara kadhaa, Khalfi alisema kuwa wao wamekuwa walengwa wa mashambulizi ya kibaguzi zaidi ya mara mbili kwa mwaka.


Msemaji wa Polisi wa Stockholm Per Fahlström, aliarifu kugunduliwa kwa mtu aliyeweka vifaa hivyo kupitia kamera za usalama na kwamba uchunguzi unaendelezwa.



Askofu Shoo amvaa meya aliyewavua watu barakoa

 


Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu kuwaamuru wananchi waliokuwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kuvua barakoa.


Askofu Shoo, ambaye pia ni mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya kanisa hilo, alisema kitendo cha meya huyo kuwalazimisha wananchi wanne kuvua barakoa ni kukosa hekima na uwajibikaji wa kiwango cha juu kama kiongozi wa kisiasa.


“Itoshe tu kusema nimesikitishwa sana na kitendo cha huyu meya, kuwalazimisha watu kuvua barakoa, ni kukosa hekina na uwajibikaji kwa kiwango cha juu,” alisema Askofu Shoo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kujikinga.


“Kuna barua nimesaini iende kwa viongozi na washarika wote wa KKKT. Kutokuchukua tahadhari ni sawa na kumjaribu Mungu. Kuchukua tahadhari ni wajibu si upungufu wa imani na si dhambi wala si kosa la jinai.


“Tusitawaliwe na hofu, bali tuzidi kumuomba Mungu na kuchukua tahadhari za kujikinga na kuzuia maambukizi kama tulivyofanya wakati ugonjwa ulipolipuka,” alieleza. Ugonjwa wa corona uliingia nchini kwa mara ya kwanza Machi, mwaka jana.


Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani maalumu kwa ajili ya kupitisha bajeti ya Halmashauri hiyo, Meya huyo aliwasimamisha wananchi wanne waliokuwa wamevaa barakoa na kuwamuru wazivue.


Uvaaji wa barakoa, ni moja kati ya njia zinazoelekezwa na wataalamu wa afya hapa nchini na Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa ajili ya kujikinga na kusambaa kwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.


Kabla ya kuanza kikao hicho juzi, Meya huyo alisema “Kuna kitu nimekiona hapa (ukumbini) hakijanifurahisha kabisa. Nyie mliovaa barakoa simameni. Nyie mliovaa barakoa, vueni barakoa zenu. Vueni barakoa tuko sehemu salama.


“Nitumie nafasi hii kuwakaribisha kwenye kikao. Manispaa iko shwari. Hayo mabarakoa yenu mnayoyavaa hayo hali iko shwari. Yaani nyie mliovaa ndio mnajipenda zaidi na akivaa mwingine askari mumtoe nje,” alisema Meya huyo.


Kana kwamba hiyo haikutosha, baada ya kumaliza kikao na kutafutwa na wanahabari ili afanunue amri yake hiyo, Meya Raibu, alishikilia msimamo wake huo akisema amefanya hivyo kwani uvaaji barakoa ni kuwatia hofu wananchi.


“Corona ipo tunaweza kujikinga lakini manispaa ya Moshi haina corona na ndio maana nikawaambia vueni barakoa na msikilize kikao kama ambavyo tunaamini kwamba tunapaswa kujikinga lakini tusitiane hofu,” alisema Meya huyo.


“Na ninaendelea kuwaelekeza katika eneo la langu la Manispaa sitaruhusu mtu yeyote aingie na barakoa katika kikao changu kwani tunaamini tuko salama salmini,” alisisitiza meya huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bomambuzi CCM.


Kauli ya meya huyo ilikuja siku moja tu baada ya Rais John Magufuli akiwataka Watanzania.


Tuendelee kumtanguliza Mungu wetu huku tukichukua tahadhari za kiafya kadri tutakavyokuwa tunaambiwa na wataalamu wetu lakini tujihadhari sana,” alisema Rais Magufuli alipokuwa akizindua shamba la miti la Silayo lililopo Chato.


Rais Magufuli aliwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya ikiwa ni pamoja na kujifukizia, akisema “Unajifukizia huku unamuomba Mungu unasali, unaswali.”


Aliongeza, “huku unapiga zoezi la kufanya la kulima mahindi la kulima viazi ili ule vizuri ushibe ili corona ashindwe kuingia kwenye mwili wako. Mtatishwa sana ndugu zangu Watanzania lakini simameni imara.”


“Ninajua wako baadhi ya Watanzania hata wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine na kwenda kuchanjwa na walikochanjwa huko wamekuja huku (Tanzania) wametuletea corona ambayo ni ya ajabu ajabu”


Rais Magufuli aliitaka wizara ya afya kuwa makini na chanzo hizo akisema nyingine hazifai na kuitaka kuacha kukimbilia chanjo na sio kila chanjo ni ya maana kwa taifa la Tanzania akisema baadhi ya chanjo zina madhara.



NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA

  


DOCTOR MBOJE,


NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA


MAGONJWA NINAYO TIBU NI 


A,_KISUKARI na tibu kwa miti shamba  kunywa na kupona kabisa


B,_TEZI DUME_natibu kwa miti  kunywa na kupona kabisa bila kufanyiwa upasuaji


C,_NGUVU ZA KIUME 

  Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa natibu kwa miti shamba na kupona kabisa


D,_kutibu magonjwa mbalimbali Kama uzazi) (miguu kuvimba na kuwaka Moto) (Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu) (mgongo,   kiuno)


MHERA JIGURHU ni dawa ya miti shamba inatibu kisukari na kupona kabisa kwa mda wa siku 16 

Sukari iwe kubwa kabisa lakini iwe normal 5.1  


NNKOROBHIJE ,ni dawa ya miti shamba inayotibu  TEZI DUME bila kufanyiwa operation na kupona kabisa kwa siku 14 na kibaki history 


NHUNGHU MAPANDO Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa au kama unahisi kupungukiwa tumia nhunghu mapando ni dawa inatibu na kupona kabisa tatizo kwa mda wa siku 4 tu


 NTURURU ni dawa ya miti shamba inayotibu uzazi chango kwa wakina mama wasio kua na watoto inatibu na kumaliza tatizo kabisa na mfumo wako wa Heath Kama umevulugika inatibu kwa mda wa siku 18


MWICHE,ni dawa ya miti shamba inayotibu Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu kurunguia kiuno kuuma mgongo na kupona kabisa kwa mda wa siku 7


PIIA UNAWEZA KUNIPATA KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA 

CALL AND WHAT SAAP

+255744922982

+255737585753 


HUDUMA ZANGU ZINAPATIKANA DUNIA NZIMA KWA OFISI NI DAR ES SALAAM NA MOROGORO KWA ULIE MBALI DAWA NAKUSAFIRISHIA MPAKA INAKUFIKIA KWA WALE WA DAR NA MOROGORO KAMA HUWEZI KUFIKA OFISINI NAKUAGIZIA DAWA INAKUFIKIA MPAKA ULIPO



MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 31/2021


















Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...