Search This Blog

Friday, July 31, 2020

Kombe la FA limerejea London!

WIKIENDI hii pazia litafungwa kwenye moja ya mashindano maarufu Uingereza na Ulaya, Kombe la FA. Fainali ya kombe la FA itafanyika katika uwanja wa Wembley kuanzia saa 7:30 wakati mahasimu wawili Arsenal na Chelsea watakuwa wakiwania Taji la mwisho kwa msimu huu. Klabu zote zimezitoa timu mbili imara kwenye hatua ya nusu fainali za kombe la FA –United na City.

Timu ya Mikel Arteta iliwaondosha Manchester City kwa goli 2-0 katika hatua ya nusu fainali, wakati kwa upande wa Chelsea iliwatoa Manchester United kwa 3-1 katika hatua hiyo hiyo ya nusu faianali. "The Gurners" mara ya mwisho kufika fainali za kombe la FA ilikuwa mwaka 2017 na kupata ushindi dhidi ya Chelsea, wakati Chelsea ikiwa ni timu iliyoshinda mara nane FA Cup ilifanikiwa kufika fainali kwa mara ya mwisho mwaka 2018. Vilabu vyote vimefika katika ratiba hii vikiwa vinahistoria ya kushinda michezo ya mwisho ya ligi dhidi ya Watford na Wolves katika michezo ya ligi kuu.

Ukija kwenye mchezo wa leo Chelsea wamepewa nafasi ya kushinda kutokana na kiwango walichokuwa nacho kwenye ligi alama 10 ziliwatenganisha na Arsenal katika ligi kwa msimu huu. Odds nzuri kwa Chelsea ni 2.20, wakati Arsenal akipewa 3.25

Mpaka sasa Arsenal na Chelsea wamekutana mara 20 katika kombe la FA. Arsenal ameibuka mshindi mara tisa, Chelsea mara tano, wakati wakitoka suluhu katika michezo sita.

Ni timu gani iko katika hali nzuri kuelekea katika debi hii? Takwimu zinaonyesha mechi itakuwa "ngumu" siku ya fainali, kwasababu  timu zote zipo katika hali nzuri. Arsenal wamepata ushindi mara tatu na kufungwa mara mbili katika mechi tano zilizopita. Kinachovutia ni kwamba Chelsea wana matokeo kama hayo pia.

Na wewe unasemaje?Unajizatiti na Arsenal pamoja na kuwa na takwimu mbovu katika Ligi msimu huu? Au ni shabiki kindaki ndaki wa Chelsea, unayependelea mtanange dhidi ya arsenal? Kama ni hivyo weka bashiri yako katika sehemu sahihi, Bashiri jamvi lako na Meridianbet!

Ukiwa na Meridian, ubashiri wa mtandaoni haujawahi kuwa mwepesi na rahisi kama sasa.  
Jisajili tu na meridianbet hapa www.meridianbet.co.tz na furaha itaanzia hapo. Pakua App ya Meridianbet kwenye simu yako na uanze kubashiri kwa uhuru nyumbani kwako. Pia unaweza kuweka pesa kwenye akaunti yako kupitia KwikPay, M-PESA au Airtel Money.  Kumbuka daima hauwezi kupoteza tiketi yako ya kwanza ukiwa na Meridianbet, Tuna Bonasi ya 100%  inakusubiri.

Milipaji wa Meridian – Nyumba ya nonasi kubwa na odds bora!  



Kombe la FA limerejea London!

WIKIENDI hii pazia litafungwa kwenye moja ya mashindano maarufu Uingereza na Ulaya, Kombe la FA. Fainali ya kombe la FA itafanyika katika uwanja wa Wembley kuanzia saa 7:30 wakati mahasimu wawili Arsenal na Chelsea watakuwa wakiwania Taji la mwisho kwa msimu huu. Klabu zote zimezitoa timu mbili imara kwenye hatua ya nusu fainali za kombe la FA –United na City.

Timu ya Mikel Arteta iliwaondosha Manchester City kwa goli 2-0 katika hatua ya nusu fainali, wakati kwa upande wa Chelsea iliwatoa Manchester United kwa 3-1 katika hatua hiyo hiyo ya nusu faianali. "The Gurners" mara ya mwisho kufika fainali za kombe la FA ilikuwa mwaka 2017 na kupata ushindi dhidi ya Chelsea, wakati Chelsea ikiwa ni timu iliyoshinda mara nane FA Cup ilifanikiwa kufika fainali kwa mara ya mwisho mwaka 2018. Vilabu vyote vimefika katika ratiba hii vikiwa vinahistoria ya kushinda michezo ya mwisho ya ligi dhidi ya Watford na Wolves katika michezo ya ligi kuu.

Ukija kwenye mchezo wa leo Chelsea wamepewa nafasi ya kushinda kutokana na kiwango walichokuwa nacho kwenye ligi alama 10 ziliwatenganisha na Arsenal katika ligi kwa msimu huu. Odds nzuri kwa Chelsea ni 2.20, wakati Arsenal akipewa 3.25

Mpaka sasa Arsenal na Chelsea wamekutana mara 20 katika kombe la FA. Arsenal ameibuka mshindi mara tisa, Chelsea mara tano, wakati wakitoka suluhu katika michezo sita.

Ni timu gani iko katika hali nzuri kuelekea katika debi hii? Takwimu zinaonyesha mechi itakuwa "ngumu" siku ya fainali, kwasababu  timu zote zipo katika hali nzuri. Arsenal wamepata ushindi mara tatu na kufungwa mara mbili katika mechi tano zilizopita. Kinachovutia ni kwamba Chelsea wana matokeo kama hayo pia.

Na wewe unasemaje?Unajizatiti na Arsenal pamoja na kuwa na takwimu mbovu katika Ligi msimu huu? Au ni shabiki kindaki ndaki wa Chelsea, unayependelea mtanange dhidi ya arsenal? Kama ni hivyo weka bashiri yako katika sehemu sahihi, Bashiri jamvi lako na Meridianbet!

Ukiwa na Meridian, ubashiri wa mtandaoni haujawahi kuwa mwepesi na rahisi kama sasa.  
Jisajili tu na meridianbet hapa www.meridianbet.co.tz na furaha itaanzia hapo. Pakua App ya Meridianbet kwenye simu yako na uanze kubashiri kwa uhuru nyumbani kwako. Pia unaweza kuweka pesa kwenye akaunti yako kupitia KwikPay, M-PESA au Airtel Money.  Kumbuka daima hauwezi kupoteza tiketi yako ya kwanza ukiwa na Meridianbet, Tuna Bonasi ya 100%  inakusubiri.

Milipaji wa Meridian – Nyumba ya nonasi kubwa na odds bora!  



Ndege za Kenya zazuiwa kutua Tanzania

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesitisha kibali cha ndege za Kenya (KQ) kutua nchini rasmi kuanzia leo, Agosti 1.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Kenya kutoa orodha ya nchi ambazo raia wao wataruhusiwa kuingia nchini humo kwa ndege kuanzia leo watapofungua mipaka yao ya kimataifa.

Orodha hiyo haikuwataja Watanzania hivyo kupelekea Tanzania ambayo ilikuwa inaruhusu ndege za Kenya kuingia nchini kusitisha (nullify) ruhusa hiyo.

Ndege za Kenya hazitoruhusiwa kutua katika uwanja wa ndege wa JNIA – Dar es Salaam, KIA – Kilimanjaro, wala AAKIA – Zanzibar.

Kenya imetangaza kufungua anga lake kuanzia leo baada ya kulifunga kwa zaidi ya miezi minne ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.



Waziri Mkuu: Wanasiasa Waeleze Watakayo Fanya Kuliko Kubeza Yaliyofanyika


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu mara kampeni za Uchaguzi Mkuu zitakapofunguliwa ili kuepuka vurugu zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani

Majaliwa amesema ni muhimu kwa wanasiasa kueleza yale waliyopanga kuwasaidia wananchi kuliko kubeza yale yaliyofanywa na wengine na kukashfu

Amefafanua, “Tujiepushe na lugha za uchochezi, tujiepushe na lugha za kubeza, tujiepushe na lugha za kashfa, kazungumze kile ambacho utawatendea wananchi”

Amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuimarisha amani na mshikamano nchini kwa kutoa mawaidha yenye kujenga

Aidha, amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge kuunda Tume maalum kuchunguza matukio ya kuungua kwa moto mfululizo kwa shule za msingi na Sekondari zinazomilikiwa na taasisi za dini ya Kiislamu nchini

Huawei Yaizidi Samsung Kwa Mauzo ya Simu Kwa Mara ya Kwanza


Ripoti iliyotolewa na Shirika la Canalys imesema Kampuni ya Huawei imeipita Kampuni ya Samsung kwa mauzo ya simu baada ya kuuza simu Milioni 55.8 kati ya Aprili-Juni huku #Samsung ikiuza simu Milioni 53.7

Imeelezwa kuwa ushindi wa #Huawei usingewezekana bila janga la #CoronaVirus ambalo limepelekea kampuni hiyo kuuza takriban 70% ya bidhaa zake China ambako Samsung ina soko dogo

Hata hivyo, Mchambuzi wa Shirika hilo, Mo Jia amesema itakuwa ngumu kwa Huawei kubaki namba moja uchumi wa dunia ukianza kutengemaa kwasababu ina nguvu kubwa China pekee



Mtoto wa Kifalme Apoteza Fahamu Miaka 14 Baada ya Kupata Ajali, Baba Akataa Achomolewe Mashine


Pichani ni mmoja wa watoto kutoka katika familia ya kifaIme Prince AIwaIeed bin KhaIeed ambaye yupo kitandani akiwa amepoteza fahamu kwa muda wa miaka 14.

Kijana huyo aIikuwa anasoma katika chuo cha kijeshi nchini Uingereza aIipata ajaIi ya gari aIiIokuwa akiendesha kwa mwendo kasi nchini humo mwaka 2oo5 akiwa na umri wa mkaka 18 na kupoteza fahamu mpaka sasa.

Mwaka 2015 madaktari waIishauri familia ya kifaIme kumuondoIea mashine zinazomsaidia kuendeIea kuishi Iakini baba yake aIikataa akiamini mungu yupo na ipo siku mwanaye ataamka tena.

Mbinu Zitazokusaidia Kufikia Malengo ya Mafanikio

Umbali uliopo kati ya malengo yako na mafanikio ni mrefu sana, na una vikwazo vingi sana, nafahamu fika ya kwamba hilo unalitambua vizuri sana.Umbali huo ambao upo baadhi ya watu ambao wana Mafanikio wameweka mikakati thabiti ambayo imewafanya wameweza kufanikiwa.

Pia kwa upande watu ambao hawajafanikiwa kwa kiwango cha juu na wao katika malengo yao wameweka mikakati, ila wengi wao hukata tamaa njiani katika utekelezaji wa mambo mbalimbali yatayowalete mafanikio.

Hali hiyo hutokea kwa sababu wengi wao hushidwa kuhimili changamoto ambazo hujitokeza katika safari hiyo ya kutoka katika malengo hadi Mafanikio.

Kama na wewe ni miongoni mwa watu ambao hukata tamaa katika safari yako ya kuelekea mafanikio, naomba nichukue nafasi hii kuweza kukaribisha katika makala haya ambapo tutazungumzia masuala ya kupanga malengo yako hadi kufikia mafanikio.

Kwani Wengi hujikuta wakishindwa wakiishia njiani katika safari yao ya mafanikio hii ni kutokana kutokujua namna ya kuzitambua mbinu za kukuza malengo hadi mafanikio.

1. Malengo ni lazima yaandikwe.

Malengo lazima uyaandike sehemu ambayo inaonekana, hapa ni maana ya kwamba uandike sehemu ambayo inaonekana, kufanya hivi kutakuwa kuna kutakufanya malengo hayo uwe unayakumbuka na kujua namna ya kuayatekeleza.

Unaweza ukayaandika malengo hayo kuyaweka katika simu yako katika (screen saver), kioo ambacho unakitumia kujitazama asubuhi na sehemu nyingine ambayo utayaona malengo hayo.

2. Weka vipaumbele katika malengo yako.

Inawezekana fika ukawa na malengo mengi, yaandike malengo hayo katika makundi matatu.
Kundi la kwanza jua yapi ni malengo ya muhimu yapi si malengo ya muhimu, yapi ni malengo ya haraka na yapi sio malengo, na tatu andika malengo ambayo sio ya muhimu sana.

Endapo utagawa malengo hayo utajua ni kipi kinatakiwa kuanza na kipi kinatakiwa kufuata na kwa muda gani.

3. Anza kwa kuanza na hatua ndogo.

Siku zote kama ilivyo ukuaji Wa kiumbe chochote chenye uhai huanza ukuaji wake katika hali ya chini. Kama ilivyo kwa kiumbe yeyote katika ukuaji hata katika ukuaji wa mafanikio yako huanza katika ngazi za chini.

Kitu cha msingi ni kuweza kupanua wigo mpana kwa ajili ya kupata mafanikio zaidi kwa kila jambo ambalo unalifanya. Na kwa kuwa mafanikio hayana ukomo hakikisha ya kwamba kila iitwayo leo unapata kiu ya kutaka kufanikiwa zaidi.

4. Malengo ni lazima yawe chanya.

Mara kadha watu huwa na ndoto nzuri sana, na pia wengi wao hupanga mambo mazuri kwa ajili ya utekelezaji wa ndoto hizo, ila changamoto kubwa ambayo huwa inakuja ni pale ambapo linakuja suala la utekelezaji wa jambo hilo.

Hapo sasa ndipo utakapoanza kumsikia mtu anasema aaah hivi nitaweza kweli, inatakiwa uondokane na kukata tamaa, vinginevyo kufanikiwa utaendelea kusikia kwa akina Donald Trump.

5.Malengo lazima yawe katika muda maalumu.

Ni lazima uweke muda kamili kwa ajili ya kutekeleza malengo yako, ifike mahali Malengo yako yafananishe na makampuni yanayohusika ujenzi kwani wao kabla ya kuanza kwa mradi huwa wanafanya mahesabu ili kujua mradi huo wa ujenzi utachukua muda gani mpaka ukamilike.

Ukiishi katika utaratibu Wa kuweka mbinu hiyo itakuwa ni rahisi kwako kutekeleza mambo ambayo unataka kutekeza. Kwa mfano lengo lako ni kujenga nyumba unaweza ukaandika katika lengo lako ya kwamba baada ya muda fulani inabidi uwe umekamilisha ujenzi huo.

Kupanga malengo bila kujua muda Wa kutekeleza malengo ni sawa na bure. Hivyo ni vyema ukajua ya kwamba muda ni mali katika kufanikisha malengo yako kwa wakati sahihi.

6. Malengo ni lazima yawe na mbinu za utekelezaji.

Watu wengi wana malengo ya kusema kwa mdomo tu. Lakini nikwambie ya kwamba ukitaka kufa maskini basi endelea na utaratibu huo Wa kuweka malengo mdomoni.

Kama kweli unataka kufanikiwa hakikisha ya kwamba malengo ambayo umejipangia umeyaandika na kuandika mbinu au njia kwa ajili ya utekelezaji wa malengo hayo.

Kufanya hivi kutakusaidia kujua jinsi ambavyo utayatekeleza malengo hayo ili kupata mafanikio. Kwa mfano kama malengo yako ni kujenga nyumba basi huna budi kuandika mbinu ambazo zitakusaidia kutengeza nyumba hiyo, pia hapa huenda sambamba na bajeti ya utekelezaji wa malengo yako.

7. Malengo ni lazima yapimike.

Kila malengo ambayo umejipangia Ni lazima yaweze kupimika. Kama nilivyoeleza hapo awali ya kwamba malengo ni lazima yawe na muda maalum kwa ajili ya utekelezaji.

Hivyo ni lazima upime malengo yako ni wapi ambapo umefikia? Katika muda ambao umepanga kuyatekeza malengo hayo je unahisi utafikia malengo hayo?

Pia uchunguzi yakinifu juu ya malengo yako ni lazima ufanyike ili kujua fursa na changamoto ambazo zimejitokeza katika kutekeleza malengo yako.

Mpaka kufikia hapa sina la ziada, tukutane siku nyingine.

Dalili kuu 7 zinazoonyesha mtu ambaye atachelewa sana kufanikiwa



1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi,ana pesa za kununua nguo  lakini hana PESA za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.

2. Siku Zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia Movie, kusoma magazeti na Kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana MUDA wa Kusoma kuhusu taaluma yake ama mambo ya kumuongezea ujuzi.

3. Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wana bahati katika maisha. Huwachukia na hataki kujifunza Kwao.

4. Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea, kulaumu uchumi, wazazi, serikali au amerogwa.

5. Siku Zote Hujiona anajua Kuliko Mtu Yeyote Yule na hapendi Kujifunza kwa wengine. Huongea sana Kuliko Kusikiliza.

6. Kila anachoingiza anatumia, ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.

7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.

Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo? Amua kubadilika ishi au fanya ukijua kesho ipo .... NDOTO YAKO INAWEZEKANA, CHUKUA HATUA.

Dogo Janja: Amwagia Sifa ‘Baby’ Wake "Huyu Mwanamke Amenifanya Nimewasahau Wengine"



Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Abdulazizi Chande almaarufu “Dogo Janja” amefunguka kuwa mchumba wake yupo tofauti na wanawake wengine aliyewahi kuwa nao kipindi cha nyuma.

Akizungumza na gazeti la Risasi Dogo Janja amsema kuwa amewahi kuwa na uhusiano na wanawake tofauti tofauti ila kwa huyu wa safari hii  amegonga mwamba.

“ huyu mwanamke amenifanya  nimesahau hata kama nishawahi kudate na wanawake wengine najionaaa kama nimekuwa mpya tena yupo tofauti sana na wanawake wengine hakika anajielewa”,alisema Dogo Janja ambaye aliwahi kufunga ndoa na muigizaji wa Bongo Muvi Irene Uwoya.

Stori: Khadija Bakari

MAGAZETI YA LEO 1/8/2020












Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi August 01

















Mama Wema Sepetu Afungukia Wema Kuzimia


MAMA mzazi wa msanii wa filamu nchini Wema Sepetu, Miriam Sepetu amefungukia ishu ya mwanaye kudaiwa kuanguka na kuzimia.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, uvumi ulienea kwenye mitandao ya kijamii kuwa staa huyo wa filamu, alipatwa na hali hiyo akiwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar.



“Hiyo juzi wanayoisema wao, mwanangu alizimia mimi nilikuwa naye kambini akimalizia kushuti tamthiliya yao season ya pili.
“Jana pia niliongea naye kwa muda mrefu sana na kama angekuwa amepatwa na hilo tatizo, angeniambia.
“Watu wameona mwanangu yupo bize sasa hivi na mambo yake, wameanza kumchokonoa,” alisema Miriam kwa ukali.



Wachokonozi hao, anaowataja mama Wema, juzi kati waliposti kwenye mitandao ya kijamii kwamba staa huyo wa filamu, amekimbizwa hospitalini baada ya kupatwa na sintofahamu ya afya.

Ujumbe katika ukurasa mmoja wa Instagram (jina linatupwa) ulienda mbali zaidi na kudai si mara ya kwanza kwa Wema kuanguka na kupoteza fahamu na kudai kuwa amekuwa akipatwa na hali hiyo mara kwa mara.



Inadaiwa kuwa, tangu apungue mwili, msanii huyo amekuwa na matatizo ya kiafya jambo ambalo Wema hajaweka wazi wakati wowote kukabiliwa na mgogoro wa afya yake.

“Jamani juzi Wema alizimia pale kwake na inavyosemekana, walimpeleka hospitali akaambiwa dawa alizotumia kupunguza mwili, sasa zimeanza kumzidi nguvu.

“Wanasema dawa hizo zimenyonya mafuta mengi mwilini, mpaka imekuwa hatari kwa afya yake,” mtu mmoja aliandika kwenye ukurasa wa Instagram.



Ishu ya Wema kupungua mwili, ilikuwa gumzo miaka miwili iyopita ambapo upunguaji huo ulitajwa kutokana na upasuaji wa kukatwa utumbo, jambo ambalo mwenyewe amekuwa akilikanusha.

Mwandishi wetu alipomtafuta Wema ili kujua hayo ya mtandaoni anahusika nayo au ndiyo wabaya wanamzushia, hakuweza kupatikana baada ya simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.

Stori: Memorise Richard

Mauya atua Yanga,nafasi ya Tshishimbi mashakani


Uongozi wa klabu ya Yanga umekamilisha usajili wa kiungo mkabaji Zawadi Mauya kutoka klabu ya Kagera Sugar


Kiungo Zawadi Mauya (Kati kati) akiwa na viongozi wa Yanga, Hersi Said ambaye ni makamu mwenyekiti kamati ya mashindano(Kushoto) na Kaimu Katibu wa klabu hiyo Patrick Simon (Kulia) wakati wa ukamilisho wa usajili.

Mauya amemwaga wino wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria wa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara.

Nyota huyo amesaini mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Mhandisi Hersi Saidi ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa kamati ya mashindano wa Yanga.

Kutua kwa Mauya ambaye anacheza idara ya kiungo, ni ishara mbaya kwa nahodha wa timu hiyo Papii Kabamba Tshishimbi ambaye amezua gumzo kufuatia kupishana na viongozi wa wanajangwani hao juu ya makubaliano ya mkataba mpya.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Mwanasheria Patrick Simon alisema hawatomlazimisha Tshishimbi kusaini mkataba mpya iwapo anaona ofa waliyompatia haimfai, na wapo tayari kusaka wachezaji wengine ambao wana uwezo kama wake.

Vile vile mapema leo zilisambaa katika mitandao ya kijamii picha za mlindalango wa Kagera Sugar Ramadhan Charamanda akiwa ameshika kinachoonekana kuwa mkataba wa klabu ya Yanga.

Bado hakuna taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa Yanga kuthibitisha kama Charamanda amesajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria.

Kwani hakuonekani kuwa na changamoto katika eneo la golikipa, Metacha Mnata, Farouk Shikhalo na Ramadhani Kabwili wanaonekana kutosha.

Magereza Yaruhusu Wananchi Kuanza Kutembelea Wafungwa



Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
kufuatia kupungua kwa maambukizi ya virusi vya COVID 19 Jeshi la Magereza nchini limefuta masharti ya katazo la huduma ya kuwatembelea wafungwa na mahabusu na huduma mbalimbali katika magereza ikiwamo huduma ya chakula kwa mahabusu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma msemaji wa Jeshi la Magereza SSP Amina Kavirondo amesema kutokana na serikali kuruhusu shughuri mbalimbali kuendelea Jeshi la Magereza limeondoa katazo hilo kuanzia Augusti 1, 2020.

''Jeshi la magereza limelegeza masharti ya katazo kuanzia 01/08/2020 huduma za kuwatembelea wafungwa na mahabusu kwa huduma mbalimbali magerezani zimerejeshwa'' amesema Amina.

Aidha jeshi la Magereza limewataka wageni wote pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya jeshi na Wizara ya Afya wakati wa upokeaji wa huduma hiyo wageni watatakiwa mambo ikiwamo mfungwa au mahabusu atatembelewa na ndugu wasiozidi wawili kwa siku za jumamosi na jumapili.

Pia limebainisha kuwa mazungumzo yatatakiwa kuto zidi dakika tano na wale wenye vibali vya kuleta chakula italazimika kuletwa na mtu mmoja tu, pia mgeni atatakiwa kukaa umbali wa mita moja kati ya mfungwa au mahabusu huku wakitakiwa kuvaa barakoa na kunawa kwa maji tiririka huku likibainisha kuwa mazungumzo ya kisheria kati ya wakili na mteja wake yasizidi saa moja.

Aidha amebainisha kuwa kwa kipindi ambacho jeshi liliweka katazo hilo wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwamo baadhi ya wafungwa kukosa haki zao ambazo zilikuwa zinahatarisha au kusababisha kusambaa kwa virus vya corona katika magereza lakini wamekuwa wakiwaelimisha lengo la kufanya hivyo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi August 01















Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi August 01


Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...