Search This Blog

Wednesday, September 30, 2020

TAASISI YA HABARI YAMTOLEA UVIVU TUNDU LISSU, YAMTAKA AACHE KUTOA KAULI ZA KULIGAWA TAIFA

 


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


TAASISI ya Habari Development Association imekutana na waandishi wa habari kwa lengo la kukumbushana wajibu wao katika kukemea kauli zisizokuwa za kujenga Taifa zinazotolewa na baadhi ya wagombea wa Urais hususan Tundu Lissu ambaye anakiwalisha Chadema.


Imesema Lissu amekuwa akitoa kauli zisizokuwa za kiungwana na zenye kujenga mpasuko mkubwa kwa Taifa ikiwemo ya kujitangaza kuwa ni mshindi halali wa Urais akiwa katika kampeni zake katika Mkoa wa Geita na mikoa mingine mbalimbali ya Mara, Shinyanga na Mwanza.


Taarifa ya Taasisi hiyo waliyoitoa leo Septemba 30,2020 kwa vyombo vya habari imesema kuwa Lissu pamoja na viongozi wenzake wamekuwa wakitoa mastamshi ambayo taasisi hiyo inaona ni matamshi yasiyoijenga Tanzania bali yapo kwenye tafakuri ya kuleta mpasuko kwa jamii.


"Tunaona na tunaamini vitendo na kauli anazotoa Tundu Lissu sio nzuri na zinazusha taharuki kubwa kwenye jamii hasa wakati huu ambao nchi iko kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.Sisi Taasisi ya Habari Development tunaiomba Tume ya Uchaguzi Nchini (NEC) kusimama na kutoa kauli kulingana na sheria za uchaguzi kuwa vitendo anavyovifanya Lissu sio vizuri na vipo katika misingi ya kuleta mpasuko kwenye jamii.


"Tunaamini huu ni wakati wa kila mwandishi wa habari kuwa imara na kupinga kauli hizi au kuvipuuza vitendo hivio ambavyo vina lengo la kuibomoa nchi na kuteteresha amani ya Tanzania ambayo imejengwa kwa nguvu kubwa,"imesema taarifa hiyo.


Taasisi hiyo kupitia taarifa hiyo imeongeza kila mwanasiasa anapaswa kuilinda amani na achunge ndimi zake kwa kuwa uhuru na amani ilioko ni tunu kubwa na anapokuja mwanasiasa anayesema kuwa yeye ndio mshindi kwa kigezo cha kujaza watu katika mkutano mmoja si jambo nzuri na tunalikemea kwa nguvu zote.


Pia imesema kuna umuhimu mkubwa wa kukemewa suala hilo na wanaiomba NEC kuchukua hatua kwa mgombea yeyote anayekwenda kinyume na taratibu za nchi kwa kuwa vitendo na kauli wanazotoa zinahatarisha amani.


"Kutokana na hali hiyo, Taasisi ya Habari Development Association tunamsihi na kumuomba Tundu Lissu afahamu ana dhamana kubwa ya usalama wa nchi yetu ambayo yeye kama mgombea tunamuomba amwage sera zake na jukumu la nani mshindi litatolewa na Tume ya Uchaguzi baada ya wananchi kumaliza kupiga kura,"imesema taasisi hiyo.


Pamoja na hayo imefafanua kama mjuavyo hivi


sasa nchi yetu ipo kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambao ni takwa la kikatiba na kidemokrasia kila ifikapo miaka mitano, nchi inafanya uchaguzi mkuu, hivyo huu ni wakati muhimu na waandishi wa habari kama wadau ni wakati wao kujitafakari kwa kuitumia vyema kalamu yetu kuelekea uchaguzi mkuu.





RC SINGIDA AWATEMBELEA WAZEE WANAOISHI MAKAZI YA SUKAMAHELA WILAYANI MANYONI

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia Wazee wa Makazi ya Sukamahela.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt ..Rehema Nchimbi pamoja na Kamishna kutoka Ustawi wa Jamii, Naftari Ng'ondi wakikabidhi chakula kwa wazee hao.
Wazee wa makazi ya Sukamahela wakimsikiliza mkuu wa mkoa.
Wazee wa makazi ya Sukamahela wakimsikiliza mkuu wa mkoa.
Jengo jipya la utawala lililopo kwenye makazi ya Sukamahela.


Na Ismail Luhamba, Manyoni.

KATIKA kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametembelea makazi ya Wazee mkoani hapa yaliyopo Sukamahela Wilayani Manyoni na kuzungumza nao.

Akizungumza na Wazee hao juzi, Dkt. Nchimbi alisema Wazee ni tunu kwa Taifa kwani mawazo yao ndio yanayopelekea mafanikio makubwa hapa nchini.

Alisema kupitia serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli imejikita kuimarisha uchumi kwa lengo la kuwasaidia wananchi wakiwemo wazee ndio maana serikali ilianzisha makazi kwa ajili ya wazee ili iweze kuwatunza.

"Tarehe 01 oktoba kila mwaka ni siku ya wazee Duniani siku hii ikatukumbusha kuwatunza wazee wetu. familia zetu ziwatunze wazee wetu,kama unachangamoto ya kumtunza mzee wako nenda kwa viongozi wako,nenda kwa mkuu wa wilaya toa taarifa ili serikali iweze kukusaidia." alisema Dkt. Nchimbi. 

Aidha Dkt.Nchimbi aliwakabidhi wazee hao zawadi mbalimbali ikiwemo mafuta ya kula,mchele,ndoo za maji, sukari, mbuzi kwa ajili ya kitoweo na sabuni huku akiwaambia kuwa serikali inatoa matibabu bure kwao,hivyo kama kuna baadhi ya madaktari kwenye Zahanati,Vituo vya afya na Hospitali za mkoa huo hawatekelezi jambo hilo watoe taarifa ili kutatua changamoto hiyo ikiwemo kuchukua hatua za kisheria.

"Serikali inawapenda sana ndio maana mpo na hapa tumeona imefanya ukarabati wa majengo yetu,tunahitaji mawazo kutoka kwenu ili na sisi tufike hapo mlipo." alisema Dkt. Nchimbi.

Awali akisoma taarifa ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Kamishina wa Ustawi wa Jamii Naftari Ng'ondi alisema mpaka sasa serikali inatoa matunzo kwa wazee 281 katika makazi 13 ya wazee nchini ambapo eneo la Sukamahe ni moja ya makazi hayo.

"Hapa Sukamahe tunatunza jumla ya wazee 15, Wizara inajivunia kupata mafanikio katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma kwa wazee tunaowahudumia hapa nchini." alisema Ng'ondi.

Alisema serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya majengo ya makazi ya wazee kwa kufanya ukarabati wa majengo yaliopo na kuanzisha majengo mapya ambapo kwenye makazi ya Sukamahe serikali imejenga jengo la utawala kwa lengo la kuimarisha mazingira mazuri ya kazi kwa watumishi wa makazi hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Makazi ya Sukamahela, Andrea Yohana aliishukuru serikali kwa kuendelea kuwajali na kuwatunza wazee,na kuiomba serikali isichoke kuwatunza licha ya kuwa hawana uwezo wowote wa kuilipa.

"Tunaliombea taifa letu liweze kuvuka salama kwenye kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kama alivyotuvusha kipindi cha Corona ili tuendelee kuishi kwa amani." alisema Yohana.


RUVUMA YAPATIWA BILIONI 4.5 KWA AJILI YA SEKTA YA AFYA

 

SERIKALI imesema, inaendelea kuimarisha na kuboresha huduma za afya ikiwemo kuongeza dawa na vifaa tiba kwenye zahanati,vituo vya Afya na Hospitali zake ili kuhakikisha hakuna mwanachi atakayepoteza maisha kwa kukosa  huduma ya matibabu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mganga Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Jairy Khanga, wakati akiongea na wananchi wa vitongoji  vitatu vya Madaba (A) Madaba(B) na  Changarawe kijiji cha Liula wanaoendelea kupata matibabu baada ya kunusurika kifo kufuatia kukumbwa na mlipuko wa kuhara damu baada ya kunywa togwa inayodhaniwa kuwekwa sumu.

Dkt Khanga alisema,  Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuri imeupatia mkoa wa Ruvuma zaidi ya bilioni 4.5 ambazo zimetumika kuimarisha na kuboresha huduma za Afya katika maeneo mbalimbali.

Alisema, katika awamu zote serikali ya awamu ya tano ndiyo inayoongozwa kwa kupeleka fedha za kuimarisha sekta ya afya katika mkoa wa Ruvuma ambapo  mbali na fedha imeleta madaktari 24 ambao wamepelekwa katika wilaya zote za mkoa huo na kuwataka wananchi kuendelea kuiamni na kuiunga mkono serikali yao  iliyopo madarakani.

Aidha Dkt Khanga  na wataalam kutoka Hospitali ya wilaya Songea wamekwenda  katika kijiji hicho kwa lengo la kutoa elimu ya Afya,kudhibiti kuenea kwa madhara pamoja na kutoa majibu ya vipimo vilivyochukuliwa kwa ajili ya kutambua aina ya  sumu iliyowekwa katika kinywaji hicho.

Dkt Khanga alisema,kimsingi mlipuko huo umetokana na  uchafu katika  maandalizi ya tongwa kwani  hayakuzingatia kanuni za usafi ndiyo chanzo cha kupata maradhi yanayofahamika kwa kitaalam(Bacillary Dysentry).

Dkt Khanga alisema,ugonjwa wa kuhara na kuharisha damu  mara nyingi usababishwa na bakteria anayefahamika kwa jina la Shigella ambaye  utokea katika maeneo yenye ukosefu wa maji safi na salama,watu wasiokuwa vyoo bora,wasionawa mikono kwa sabuni mara wanapotoka kujisaidia,na kundaa chakula katika mazingira bila kuzingatia usafi.

Kwa mujibu wa Dkt Khanga, mtu(watu)wanapokosa vyoo  au kujisaidia porini kinyesi uzalisha Inzi ambao uingia katika chakula na vyombo na kuacha uchafu ambao ni hatari kwa afya ya binadamu.

Alitaja dalili za kuharisha damu ni mtu kupata homa inayoambatana na baridi kali,maumivu ya kichwa,kutapika,kuharisha na kichwa kuuma ambapo madhara yake ni kuishiwa  maji mwilini na kama mgonjwa hatapata dawa ni rahisi kupoteza maisha.

Adha, amewapongeza wahudumu wa Afya wa zahanati ya Matimila na Liula kwa kazi kubwa waliyoifanya kuokoa maisha ya wananchi kwani mara baada ya kutokea mlipuko huo walifanya kazi usiku na mchana bila kuchoka.

Hata hivyo,amewataka wananchi kuhakikisha wanakuwa na vyoo bora na kuzingatia kanuni bora za Afya ili kuepuka magonjwa mbalimbali ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu na kuharisha.

Awali Mganga mkuu wa wilaya ya Songea Dkt Geofrey Kihaule alisema, jumla ya watu 102 walipata ugonjwa wa kichwa na kuhara damu ambapo hadi sasa hakuna aliyepoteza maisha.

Dkt Kihaule alisema, kazi iliyofanyika mara baada ya kufika katika kijiji hicho ni kutoa elimu ya afya ili wananchi waelewe namna ya kuchukua hatua pale milipuko inavyotokea na kuwaondoa hofu kuhusiana na tukio hilo na Imani ya kishirikina na kuwafuatilia wale walio karibu na wagonjwa ili nao kufahamu afya zao na kuwapa kinga ili wasipate maradhi hayo.

Baadhi ya wananchi wameipongeza Serikali kupitia mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma  kwa kuchukua hatua ya haraka kukabiliana na mlipuko huo hali iliyosaidia kuokoa maisha ya watu walioathirika na ugonjwa huo.

Mmoja wa wananchi Moses Luambano alisema, kama wataalam wangechelewa kufika kwa wakati ni dhahiri kuwa madhara yangekuwa makubwa zaidi kwa watu kupoteza maisha.

  Mganga Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Jairy Khanga akimjulia hali mkazi wa kitongoji cha Madaba B kijiji cha Liula wilaya ya Songea anayeendelea kupata matibabu baada ya kupata na ugonjwa wa kuharisha damu kutokana na kunywa togwa  inayodhaniwa kuwa na sumu kwenye sherehe kijijini hapo.

Mratibu wa Huduma za maabara Hospitali ya wilaya Songea mkoani Ruvuma akimpatia dawa ya kujikinga na ugonjwa wa kuharisha mmoja kati ya watoto Hamisa Chuma(6)ambaye alinusurik katika mlipuko wa ugonjwa wa kuhara damu uliotokea katika kijiji cha Liula baada ya wananchi wa kijiji hicho kunywa togwa inayosadikiwa kuwa na sumu.





MAASKOFU NA WACHUNGAJI WAZINDUA KITABU CHA UONGOZI ULIOTUKUKA WA RAIS JOHN MAGUFULI.

 


Askofu Mkuu wa Makanisa ya Naioth Gospel Assemblies of God ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania, Dkt. David Mwasota.(kushot) akiwaongoza Maaskofu na Wachungaji kwenye  maombi ya kukiombea Kitabu cha Uongozi Uliotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki.


Maombi ya kukiombea kitabu hicho yakiendelea kufanyika.

Muonekano wa kitabu hicho.

Bishop Sedrick Ndonde wa Kanisa la Restroration Bible ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo walioandika kitabu hicho,

Askofu Mkuu wa Makanisa ya Naioth Gospel Assemblies of God ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania, Dkt. David Mwasota., akizungumza na Maaskofu  na Wachungaji kwenye  maombi ya kukiombea Kitabu cha Uongozi Uliotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki.


Uzinduzi wa kitabu hicho ukifanyika.





Na Dotto Mwaibale


MUUNGANO wa Maaskofu zaidi ya 15 na Wachungaji 100 mwanzoni mwa juma walizindua kitabu kinachoelezea uongozi uliotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.


Kitabu hicho kimeandikwa na Mtendakazi katika shamba la Bwana, Restoration Bible Church Kariakoo jijini Dar es Salaam.


Uzinduzi wa kitabu hicho kiitwacho Uongozi Uliotukuka, JPM ni Kiongozi wa Kisiasa na Kiroho, uliofanyika jijini Dar es Salaam uliongozwa na Askofu Mkuu wa Makanisa ya Naioth Gospel Assemblies of God ambaye pia ni katibu Mkuu mstaafu wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania, Dkt. David Mwasota.


Mwasota alisema lengo la kuandikwa kitabu hicho ni kutazama uongozi wa Rais Magufuli kwa pande za kisiasa na kiroho.


Askofu huyo alisema katika utendaji kazi wake, Magufuli anamtegemea Mungu hivyo kumfanya aonekane anaiongoza nchi kwa upande wa kiroho.


“Imani ya Mheshimiwa Magufuli katika kushughulikia janga la Corona kiroho limefanya kuinua imani ya watu wengi kwa kulisaidia kanisa ambalo ndiyo kazi yake kubwa kuwajenga watu kiimani,” alisema askofu huyo.

 

Mwasota aliwaomba maaskofu, wachungaji na waumini wote kuendelea kumuombea Rais Magufuli kwani ndiyo yalikuwa maombi yao kwa miaka mingi kwa Mungu atuletee kiongozi kama yeye.


“Tunamshukuru Mungu aliyejibu maombi yetu kwa kutuletea kiongozi tuliyemuomba miaka mingi ambaye ni Magufuli anayeliongoza taifa letu kisiasa na kiroho,” alisema Mwasota.


Askofu huyo aliongeza kuwa katika nchi yetu hatukuwahi kumpata kiongozi wa juu anayemtaja Mungu wakati wote na kuwaagiza watendaji wake kila anapowaapisha wamtangulize na kumtegemea Mungu.


Naye Bishop Sedrick Ndonde wa Kanisa la Restroration Bible ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo walioandika kitabu hicho, alisema lengo la kitabu hicho ni kuelezea ukweli kuhusu Rais Dkt. John Magufuli ili kufahamu zaidi nini alichobeba mbali ya wadhifa wa urais alionao na kulikumbusha kanisa na watumishi wa Mungu kuutafakari uongozi wake.


“Umuhimu wa kitabu hiki ni kuwakumbusha watumishi wa Mungu kuwa na muda wa kutafakari uongozi wa JPM kwa yote aliyoyafanya kwa upande wa kiroho,” alisema Askofu Ndonde.


Aliongeza kwa kumtegemea Mungu amefanya mambo makubwa kama kujenga miundombinu ya barabara, umeme, maji, shule, hospitali na kuwawezesha watanzania kunufaika na madini, mbuga za wanyama ambapo awali waliokuwa wakinufaika walikuwa watu kutoka nje.


 “Magufuli ni mfalme anayekiri ufalme wa Mungu kutawala taifa letu,” alisema Ndonde.


Ndonde aliongeza kuwa kuna umuhimu wa kukisambaza kitabu hicho kwa waumini wao na wananchi wengine kwa ujumla  bila kujali dini wala madhehebu wanayotoka ili waweze kuwa na mtazamo chanya.



UBALOZI WA TANZANIA - KOREA KUSINI WAANDAA SHINDANO LA 'SHOW ME TANZANIA PHOTO CONTEST EVENT' KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

 

.
Balozi wa Tanzania Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka, akimkabidhi zawadi ya kinyago huku akitoa maelezo mafupi ya maana ya kinyago hicho Bw. Donghee Choi, katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Seoul.
Mhe. Balozi Matilda Swilla Masuka akimkabidhi zawadi ya Tingatinga mshindi wa kwanza wa shindano la “Show Me Tanzania” Bw. Donghee Choi, katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Seoul.
Balozi wa Tanzania Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, Seoul wakibalishana mawazo na Bw. Donghee Choi jinsi ya kuitangaza zaidi “Destination Tanzania”. Bw. Donghee Choi ni “Travel blogger” maarufu hapa Seoul na amekuwa akisafiri nchi mbalimbali duniani.
Balozi wa Tanzania Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka akikabidhi zawadi ya vikombe vyenye kutangaza utalii wa Tanzania na kahawa kutoka Tanzania kwa mshindi wa pili wa shindano la “Show Me Tanzania” bwana Suho Lee, katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Seoul.
Balozi wa Tanzania Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka akikabidhi “Plaque of Appreciation” kwa mshindi wa kwanza wa shindano la “Show Me Tanzania” Bw. Donghee Choi, katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Seoul
Mhe. Balozi Matilda Swilla Masuka akimkabidhi zawadi ya Tingatinga mshindi wa pili wa shindano la “Show Me Tanzania” Bw. Suho Lee, katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Seoul.
Mshindi wa pili wa shindano la “Show Me Tanzania” bwana Suho Lee, akipiga picha ya vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Tanzania kwa ajili ya kuzitumia katika mitandao yake ya kijamii. Bw. Suho Lee ni Mwandishi maarufu wa habari za kitalii hasa utalii wa nchi za kiafrika. 


====== ======== ======== ========

“SHOW ME TANZANIA PHOTO CONTEST EVENT”

Katika juhudi za kuwavutia watalii zaidi kutembelea Tanzania, Ubalozi wa Tanzania, Korea Kusini ulibuni Shindano la “Show Me Tanzania” ambapo Wakorea waliowahi kutembelea Tanzania walikuwa wanatuma picha walizopiga wakiwa katika vivutio vyetu mbalimbali kupitia Akaunti yetu ya Instagram- tanzaniaembassykorea

Shindano hilo lililokuwa la siku 10, kuanzia Agosti 31 hadi Septemba 10, lilikuwa la mafanikio makubwa kwa kuwavutia washiriki 154 ambao waliposti zaidi ya picha 1100 na kupata likes zaidi ya 37,000. Kwa maana nyingine katika muda wa siku hizo kumi Ubalozi uliweza kuongeza wafuasi wapya 300 katika mitandao yetu ya kijamii na kuwafikia zaidi ya watu 37,000 ambao waliziona picha hizo zenye kuonyesha uzuri wa vivutio vyetu vya utalii, ubora wa huduma za mahoteli, vyakula, na ukarimu wa Watanzania. 

Aidha, shindano hilo limewachagiza hata wale waliowahi kutembelea Tanzania kuweka nia ya kurejea tena nchini kwa kuona kwamba kumbe kuna sehemu nyingine nzuri pia ambazo hawakuweza kutembelea na hivyo kuwapa hamasa upya ya kutembelea tena Tanzania. 

Kwa upande mwingine picha zilizokuwa zikitumwa zimedhihirisha dhana ya 3600 kwani ziligusa maeneo mbalimbali yakiwemo Mlima Kilimanjaro, Beaches za Zanzibar, Dar es Salmaam, Bagamoyo, Safari za Mbugani, Spice Tour, Maeneo ya Kihistoria kama Kilwa, Stone Town nk. Kwa uhakika shindano lilifana sana na kujidhihirisha Destination Tanzania inajitosheleza. 

Kwa ujumla wake, shindano hilo limeongeza hamasa ya watalii kuja kutembelea Tanzania, limetuongezea wafuasi wetu katika mitandao ya kijamii, limefanya baadhi ya makampuni ya utalii kuanza kushirikiana nasi kama Ubalozi ambapo tumepata timu ya bloggers na influencers ambao tunaweza kuwatumia tunapotaka kuwafikia watu wengi zaidi kuhamasisha suala zima la Utalii. 

Kupitia Shindano hili Ubalozi umeendeleza juhudi za kuwavutia wageni hawa kuja kutembelea Tanzania. Juhudi zingine ni Pamoja na: Ufunguzi wa Blog ya Kikorea kupitia mtandao wa Naver, ambayo inawafikishia Habari kwa lugha ya Kikorea; na pia Media FAM Tour iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo kampuni 10 (Media, Bloggers and Influencers) walitembelea Tanzania na kujionea vivutio vya utalii na baada ya kurudi kuandika Makala kwa muda wa miezi sita. 

Makala hizo zimekuwa chachu na hamasa kubwa kwa umma wa Wakorea. Tunaamini, kwa kupata Safe Travels Stamp na uwepo wa Standard Operating Procedures (SOPs), hali ikitengamaa kwenye hizi nchi za wenzetu, tutaanza kupokea wageni wengi zaidi katika eneo hili la utalii.


Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...