Search This Blog

Tuesday, June 30, 2020

Waziri Ummy : NHIF Tatueni Malalamiko Ya Upatikanaji Wa Baadhi Ya Dawa

Na.WAMJW,DSM
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imetakiwa kutatua malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa wananchi wenye bima ya afya.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kikao na Menejimenti ya Mfuko huo katika ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini, Dar es Salaam.

“Kumekuwepo na malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa watu wenye kadi za bima pia ucheleweshaji wa malipo ya watoa huduma za afya” Alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ameutaka mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa katika vifurushi vya bima ya afya.

“Tatueni malalamiko yote kwa wakati ili wananchi wafurahie vifurushi vyote watakavyojiunga navyo”.Alisisitiza Waziri Ummy

Kikao hicho pia kiliangalia mwenendo wa utoaji wa huduma za bima za afya zinazotolewa na mfuko huo ambapo kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Benard Konga, Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, na Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi.


Baba Levo Awakataa Watoto Wake "Nina Watoto Wengi Mtaani ila Mama zao Walikuwa Hawajatulia Lazima DNA Kwanza"


Msanii na aliyekuwa Diwani wa Mwanga Kaskazini Kigoma Ujiji, kupitia chama cha ACT Wazalendo Baba Levo, amesema ana watoto wengi hadi wengine amewakataa kwa sababu mama zao walikuwa hawajatulia pia ana mpango wa kwenda kuwapima DNA.

Akipiga stori na Big Chawa kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Baba Levo amesema yeye ni baba bora kwa watoto wake ila kwenye suala hilo anahitaji vipimo vya DNA ili kuthibitisha.

"Napenda sana watoto japokuwa nina watoto wengi, lakini wengine nimewaweka pembeni kwa sababu wakati natafuta hiyo mimba mama zao walikuwa hawajutulia, walikuwa wana rukaruka leo katembea na huyu kesho katembea na yule, halafu akipata mimba anakwambia ya kwako, kwahiyo mpaka nikawapime DNA nitawachukua na mchakato utaanza baada ya kumaliza kampeni".


Bilionea Mpya Mjini Laizer Awatolea Nje Warembo Mastaa Waliojipendekeza Kwake Apite Nao


HII inaitwa sitaki shobo! Bilionea mpya Bongo, Saniniu Laizer ambaye wiki iliyopita alitangazwa kuwa bilionea mpya wa madini nchini, amewakataa ‘live’ mastaa wa Kibongo wanaomtajataja mitandaoni.

“Unajua mimi siyo mtu wa mitandao kabisa kwa sababu huwa siangalii sana, lakini kingine watu ambao wanasema najuana nao, siyo kweli. Mimi ninawajua zaidi watu wa Mererani tu,” anasema Bilionea Laizer alipokuwa Akifanya Mahojiano na Ijumaa.

Mzungu Akamatwa Kwa Kusambaza Ukimwi Kwa Wadada Warembo Makusudi


Jason Pope raia wa marekani amekamatwa na police kwa kusambaza VVU kwa makusudi akilenga wanawake weusi.

Mpaka anashtukiwa alikuwa ameumiza zaidi ya wanawake 600 wenye asili ya bara la Africa.

Wengi wao wanawake hao aliwapata kupitia mitandao ya kijamii na wakionana jamaa alikuwa na styles zake alizohakikisha lazima aambukize virusi vya Ukimwi kwa kila tendo moja la ndoa.

Wengi wa wanawake hao aliwashauri wafanye mapenzi kinyume na maumbile na alikuwa anajiweka mkavu muda wote ili patokee michubuko mingi wakati wa tendo la ngono. Kila aliyekutana naye alimwambukiza VVU.

Alifanya hivyo kwa kuamini kuwa wataueneza zaidi kwa wanaume weusi kwani wanapenda ngono kupita maelezo.

Bado msako zaidi unaendelea ili kuwabaini wanawake wote waliotembea na huyu bwana kwani siyo wazima kwa sababu waliojitokeza kwa mamlaka za usalama wote wana VIRUSI VYA UKIMWI.

Nini maoni yako? https://www.youtube.com/watch?v=KWlXQGl0O9Y

Msanii Timbulo Afunguka Siri ya Baba yale "Baba Yetu Alituzaa 46, Kwa Wake Tofauti"


Msanii wa BongoFleva Timbulo amefunguka kuwa huwa anamuona baba yake kama babu yake kwa sababu kwao wamezaliwa watoto wengi sana hadi kufikia hatua ya mzazi wake huyo kuwachanganya na watoto wengine.


Timbulo amesema kwao walizaliwa jumla ya watoto 46 kwa mama tofauti japo wengine wameshafariki, baba yake alikuwa na wake wanne na kwa upande wa mama yake yeye ni mtoto wa mwisho kati ya 13 waliozaliwa baba mmoja na mama mmoja.

"Baba yangu alikuwa na watoto wengi hadi kuna muda alikuwa anatuchanganya, tulizaliwa 46 kwa wake zake wanne tofauti, mimi mpaka najitambua tulikuwa tupo 34 japo kuna wengine walitangulia mbele za haki, mimi kwa upande wa mama yangu tulizaliwa watoto 13 na mimi ndiyo nilikuwa wa mwisho, mimi naona kama ni mjukuu kwa baba yangu kwa sababu alikuwa amezeeka" ameeleza Timbulo


Mwanamuziki Nandy Afunguka Kumwibia Bwana Wema Sepetu 'Inauma"


“Huwezi amini, mimi na Wema hatujawahi kugombana kabisa, nilikuwa nashangaa wanavyosema eti nilimuibia danga lake kitu ambacho hakina ukweli wowote, siwezi kufanya hivyo halafu kwa nini tuibiane?. Kwani wanaume wameisha hapa mjini? Watu huwa wanaongea sana halafu wanaongea mambo wasiyokuwa na uhakika nayo, nampenda Wema na sitaacha kufanya hivyo, zaidi tunasapotiana sana kwenye kazi,” Nandy




Mwili Waokotwa Ziwa Victoria, Padre Aelezea Tukio


Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera Inspekta Hamis Dawa, amesema kuwa taarifa za mwili wa mwanaume mmoja kuelea Ziwani zilitolewa na Padre Deritius Rwehumbiza wa Kanisa Katoliki Bunena mkoani humo ambalo liko jirani na Ziwa.

Inspekta Dawa ametoa kauli hiyo wakati akieleza taarifa ya Jeshi hilo, kuopoa mwili wa mwanaume mmoja ambaye bado hajafahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 hadi 35, aliyezama ndani ya Ziwa Victoria na kisha mwili wake kuelea.

"Sasa hatujui kama ni mvuvi ama ni muogeleaji na sasa Ziwa letu limejaa sana na tumejaribu kutoa elimu kwa wananchi, kutowaachia watoto wao kwenda Ziwani" amesema Kamanda Dawa.

Imeelezwa kuwa mwili wa mwanaume huyo, umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kuwataka wakazi wa Mkoa huo, kuacha mara moja tabia ya kuogelea Ziwani kwa sasa sababu Ziwa hilo limejaa sana.

Rais Magufuli Arejesha Fomu za Kugombea Urais Kupitia CCM....Wanachama Zaidi ya Milioni 1 wa CCM wamdhamini



Jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 wa  chama cha Mapinduzi, CCM wamejitokeza kumdhamini Mwenyekiti wao Rais Magufuli katika fomu za kuwania kupitishwa na chama hicho kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 30 Juni 2020 makao makuu ya CCM, Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally wakati wa hafla fupi ya  kuzipokea Fomu za Kugombea Urais wa Tanzania Zilizowasilishwa na Rais Magufuli

Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM, Serikali na wanachama wa chama hicho wakiwemo wenyeviti wa chama hicho nzima waliowasilisha kila mmoja fomu za udhamini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa, Dk. Bashiru amesema, jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 walijitokeza kumdhamini  Rais Magufuli kutoka mikoa 32 na jumuiya zake tatu za wazazi, vijana na wanawake.

Amesema, leo Jumanne saa 10 jioni ndiyo siku ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji fomu za urais ndani ya chama hicho. Aliyechukua ni mmoja tu ambaye ni Rais Magufuli.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano July 01





















Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano July 01


ENEO LA WAZI BONDENI MARUFUKU KUPAKI MAGARI,BADALA YAKE RUKSA WANANCHI KUPUMZIKA-RC KIMANTA

Na.Ashura Mohamed -Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mheshimiwa Idd Hassan Kimanta amepiga marufuku kuegesha Magari katika  eneo la  wazi la bondeni badala yake Eneo Hilo  litatumika kama eneo la kupumzikia wananchi wote wa Arusha.

Akizungumza Mara baada ya kufanya ziara katika Eneo Hilo Kimanta alisema kuwa Eneo Hilo la wazi litatumika Kama bustani ya kupumzikia, wananchi kwa kuwa Ni Eneo ambalo linamilikiwa na Serikali.

"Eneo hili litatumika kwa ajili ya wananchi kupumzika na haya ni maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli siku aliyotuapisha”.

Aidha Kimanta amewata  wananchi ambao wanaegesha magari  katika eneo hilo kuondoa magari yao ifikapo Julai Mosi,2020 ili kuliacha eneo hilo wazi kwa ajili ya wananchi kupumzika baada ya shughuli zao za kila siku.

Amesema serikali inampango wa kuliboresha eneo hilo vizuri na kuwa la mapumziko kwa wananchi, kwani eneo hilo linamilikiwa na serikali na ni lawazi.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuaminiana kwa  kuwa mkoa huo,utajengwa na wanaarusha kwa maslahi mapana ya mkoa huo.

Nae mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini  Kenani Kihongosi alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Dkt.John Pima kuhakikisha kuwa Eneo Hilo halikusanywi Ushuru kuanzia July Mosi kutoka kwa mtu yeyote badala yake libaki kama lilivyo.

Kihongosi amelitaka jiji la Arusha kukaa chini na kuja na mpango mkakati ambao utaamua Eneo Hilo litafanywa Nini  ili wananchi waweze kupumzika na kulitumia.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.John Pima alisema kuwa amepokea maelekezo yote kutoka kwa mkuu wa wilaya na kuanzia July Mosi Eneo Hilo litafungwa na kufanyiwa marekebisho ili pawe pazuri na wananchi waweze kupumzika.

"Ninachoomba wananchi wa Jiji la Arusha mtuunge mkono ili tuweze kutekeleza yake ambayo mnatamani yawe hapa Arusha,kwa vitendo na kwa ushirikiano wa Pamoja"alisema Pima.
Kuanzia tarehe Mosi

Eneo hilo  lililopigwa marufuku kwa ajili ya  maegesho ya Magari lipo karibu na Msikiti wa Bondeni uliopo Jijini Arusha.

Pia Kimanta amefanya ziara fupi katika Jiji la Arusha na kukagua baadhi ya maeneo ya miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari ya Terrati.
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta katikati akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Kenani Kihongosi na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha dkt.John Pima.
Pichani mkuu wa wilya ya Arusha Mjini Kenani Kihongosi akiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha dkt.John Pima akiwa wanapokea  Maelekezo katika baadhi ya Mradi katika Jiji la Arusha.


WANAFUNZI SHULE YA MSINGI DODOMA MLIMANI WAFURAHIA KUANZA MASOMO, WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

 FURAHA! Kufuatia agizo la Rais Dk John Magufuli kuruhusu masomo yaendelee kuanzia Juni 29, Wanafunzi wa Shule ya Msingi Dodoma Mlimani wameelezea furaha yao ya kurudi shule huku wakimpongeza Rais kwa kuruhusu masomo kuendelea.

Wakizungumza shuleni hapo, wanafunzi hao wamesema waliwakumbuka walimu wao kwa ufundishaji wao mzuri huku wakisema muda wa kucheza kwa sasa haupo zaidi ya kuzingatia masomo.

Wanafunzi hao wanarejea shuleni baada ya miezi mitatu kutokana na serikali kufunga shule na vyuo nchini ikiwa ni jitihada za kujikinga na ugonjwa wa Covid19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Akizungumzia kurejea kwa wanafunzi mashuleni Mwalimu Mkuu wa Shule Teonila Mgulunde amesema anafurahi sana kufunguliwa kwa shule kwani kwa kipindi cha miezi mitatu wanafunzi kukosa masomo kilikua kigumu na imewaumiza kwa kiasi kikubwa.

‘’ Tunaishukukuru sana serikali kwa uamuzi wake huu ,kwani idadi ya watoto waliorudi shuleni ni wengi licha ya kuwa kuna mmoja tumempoteza lakini hakuuumwa ugonjwa huu alikuwa na matatizo mengine, hivyo kwa sasa tunajikita kuwafundisha wanafunzi wetu na kuwaandaa wale wa madarasa ya mitihani," Amesema Mwl Mgulunde.

Jumanne June 16,2020 wakati akitoa hotuba yake ya kuvunja Bunge la 11, Rais Dk John Magufuli alitangaza rasmi kufunguliwa kwa shule zote zilizofungwa kutokana na ugonjwa huo na June 29 ndiyo ilikuwa tarehe rasmi ya wanafunzi kurejea shuleni.

‘’Tuliwakumbuka sana walimu wetu kipindi tulichokuwa nyumbani,muda mwingi umepotea, kwa sasa tumerejea shuleni  sio muda wa kucheza tena, tutasoma kwa bidii na tutafaulu.

Lakini tunamshukuru sana Rais wetu Dk John Magufuli kwa kuamua kuruhusu masomo yaendelee na kututoa hofu kwani amesema hofu nayo husababisha kinga za mwili kupungua," Amesema Hemedi Shaban wa Darasa la Saba.

Naye Elizabelth David ambaye pia yuko Darasa la saba amesema amerejea tena shuleni hivyo atasoma kwa bidii ili aweze kufaulu mitihani yake vizuri.

‘’ Tuliwakumbuka sana walimu wetu,tumekaa nyumbani muda mrefu na hivi sasa tumerejea shuleni nitasoma kwa bidii,nakumbuka wakati niko nyumbani nilikuwa na muda wa kujisomea kupitia madaftari yangu na kupitia runinga kwenye Darasa huru’’ Amesema Elizabeth.

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Dodoma Mlimani wakiendelea na masomo yao kama kawaida baada ya kurejea shuleni kuendelea na masomo yao.


IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO JULAI 1,2020


  
 
 
 
 


Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...