Search This Blog
Saturday, July 31, 2021
Mambo yatakayowasaidia kuweza kuboresha mahusiano ya kimapenzi
Kama ilivyo kwenye bustani hata mahusiano yenu yanaweza kuwa mazuri yenye kuwapa tulizo au mabaya kuendana na kujitoa kwenu kuyatunza na kupambana na changamoto zozote zile kwenye vipindi vya shida na raha.
Ndani ya mahusiano kuna chanagamoto nyingi sana ambapo kimsingi kama wahusika hawatakuwa makini na yale wanayoyasikia na kuyaona ni kwamba mahusiano yao hayatafika mbali sana.
Watu wataleta choko choko za kuwagombanisha kama mhusika fulani hata kuwa makini kwamba mtu anaweza kujikuta anamuacha yule ampendaye pasiyo kufanya uchunguzi wa kutosha juu wa yale aliyoyasikia.
Asikwambie mtu wangu wa nguvu, Inachosha sana pindi we unahangaika kuyapalilia, kumwagilia mahusiano yako ya kimapenzi ili yastawi, halafu watu wengine wanakuja kwa kasi kubwa kwa ajili ya kung'oa mazao badala ya magugu. Inauma sana.
Hivyo ni wajibu wako kuanzia sasa kujua namna sahihi ya kuitunza bustani yenu ya mahusiano ya kimapenzi ili mahusino yenu yaweze kudumu daiama, Ni wajibu wenu kuhakikisha mnalinda mahusiano yenu kila itwapo leo,
Afungwa miaka 30 jela kwa kukutwa na bangi
Mahakama ya Hakimu mkazi Pwani (Kibaha) imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Ridhiki Omary Marimbwa kwa kosa la kusafirisha kilo 21.86 za dawa za kulevya aina ya bangi.
Hukumu hiyo ilitolewa tarehe 29 mwezi Julai 2021 na hakimu Mhe. Joyce Mushi baada ya mtuhumiwa kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha Dawa za kulevya aina ya bangi
Akisoma hukumu hiyo mheshimiwa Joyce Mushi amesema kwamba, upande wa Jamhuri umethibitisha kosa hilo pasi na kuacha shaka hivyo imemtia mshtakiwa hatiani. Kwa kuwa, makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya yamekithiri mkoani Pwani, hana budi kumpa mshtakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Wakati akijitetea mshtakiwa aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani ana familia yenye watoto wadogo wanaomtegemea.
Pamoja na hukumu hiyo Mhe. Mushi aliamuru kutaifishwa kwa pikipiki iliyotumika kutekeleza uhalifu huo pamoja na kuteketezwa kwa bangi iliyokamatwa.
Mshtakiwa alikamatwa tarehe 18 mwezi Agosti mwaka 2020 kwenye hifadhi ya wanyamapori ya Selous mkoani Pwani akisafirisha dawa hizo.
Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya mwaka 2015 kama ilivyorejewa mwaka 2019.
Usajili wa Wakulima washika kasi
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma.
Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Serikali za Mitaa zinaendelea na usajili wa wakulima kwenye mfumo wa M-Kilimo ili waweze kutambuliwa, kutoa huduma kwa njia ya simu na pia Serikali kutoa huduma zingine kwa urahisi.
Mpaka sasa hivi zaidi ya nusu ya mikoa yote Tanzania Bara, Mikoa 14 imeweza kusajili na kufikia asilimia 50 au zaidi kwenye mfumo huo wa M-Kilimo.
Akizungumzia hali ya usajili wa wakulima mpaka hivi sasa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof. Siza Tumbo amesema kuwa Mikoa 12 bado ipo chini ya asilimia 50 kwenye usajili wa wakulima.
Prof. Tumbo ameeleza kuwa Mikoa minne (4) ambayo ni Njombe, Arusha, Simiyu na Singida imeweza kufikia lengo la asilimia 100 na zaidi. Wizara ya Kilimo inaipongeza sana mikoa hii kwa kufikia hatua hiyo.
Amesema kuwa Mikoa ya Shinyanga, Kagera na Dar-es-Salaam bado wapo chini ya asilimia 30, hivyo kuwasihi kuongeza kasi ili kufikia malengo ya Serikali.
Pia, Wizara ya Kilimo inatoa shukrani za dhati kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Watendaji Wakuu na Wakati kayika ngazi ya Mikoa na Wilaya/Halmashauri na Maafisa Kilimo na Wagani wote kwa kazi kubwa ya kuwezesha, kuhamasisha na kusajili wakulima kwenye mfumo wa M-Kilimo.
OKOA NDOA YAKO NA SUPER MIHAYO MPYA
SUPER MIHAYO MPYA .
WHATSAP NO +255 746 758 853
Ni dawa bora ya kutibu na kumaliza matatizo yote ya nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile,
- kuwahi kufika kileleni dakika moja ushakojoa
- maumbile kusinyaa na kulegea wakati wa tendo
- kukosa hamu ya tendo la ndoa
- kushindwa kurudia tendo la ndoa
- uume kusimama kwa kulegea
- uume kulegea katikati ya tendo
- kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu
- kuishiwa nguvu kutokana na punyeto.
Epuka aibu hii leo kwa kutumia SUPER MIHAYO. kiboko ya matatizo haya.
Pia kuna SUPER MIHAYO. Kiboko ya uume mdogo inaboresha maumbile ya uume kwa kurefusha na kunenepesha kwa saizi uipendayo haijalishi umri hata kwa walioathirika na upigaji punyeto
Kwanza fahamu sababu zinazopelekea kuwa na upungufu wa nguvu za kiume na uume mdogo.
(1) kujichua (punyeto) kwa muda mrefu maana hupelekea misuli ya uume kulegea.
(2) ngiri
(3) kuugua chango la uzazi kwa muda mrefu.
(4) kupungukiwa hormone za testosterone.
(5) ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na visivyo na virutubisho vya kutosha.
(6) kutokufanya mazoezi na mwenendo wa maisha.
(7) kisukari.
(8) tumbo kuunguruma na kujaa gesi.
(9) maumivu ya kiuno nk.
Kwanini uhangaike? Kwanini uhuzunike?
Hii ni spesho kwa waliotumia madawa mengi bila kufanikiwa hakika hautajuta kuitumia.
WASILIANA NA:
DR. HASSANI
SIMU NO:
📞0746758853
WHATSAP NO +255746758853
Popote ulipo huduma hii inakufikia
Tetesi za Soka Ulaya leo 31.07.2021
Real Madrid wataanza mazungumzo na Paris St-Germain majuma kadhaa yajayo kwa ajili ya mshambuliaji Kylian Mbappe,22, ambaye mkataba wake utakwisha msimu ujao wa majira ya joto. (90min)
Aston Villa watampa ofa ya mkataba mpya kiungo wa kati Jack Grealish, 25, wa thamani ya pauni 200,000 kwa wiki ili aendelee kusalia na klabu hiyo na kumzuia asielekee Manchester City,ambayo imetangaza dau la pauni milioni 100 kumnasa mchezaji huyo. (Star)
Kiungo wa kati wa Manchester Paul Pogba,28, ambaye kwa kiasi kikubwa amehusishwa na taarifa za kuhamia Paris St-Germain, anaweza akashuhudia mustakabali wa muda mrefu Old Trafford, lakini Mfaransa huyo anaweza asisaini mkataba mpya na mashetani wekundu. (Sky Sports)
Tottenham imetangaza ofa kwa Atlanta ya pauni milioni 43 kwa ajili ya Muajentina Cristian Romero, 23, na timu hiyo ya Italia wako tayari kupokea dili kama wanaweza kuwa na muda zaidi wa kumpata mbadala wake. (Sky Sports Italia, via Mail)
Kiungo mchezeshaji wa Colombia James Rodriguez amesema hana uhakika kama atasalia Everton lakini mchezaji huyo mwenye miaka 30 amekataa kurudi Real Madrid. (Mail)
Kiungo wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Florian Neuhaus, 24, amesalia kuwa lengo la kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, lakini Reds hawatakuwa tayari kufikia gharama ya karibu pauni milioni 34.(Sport1 - in German)
Liverpool imejiunga na Juventus na Arsenal katika mbio za kumnasa kiungo wa kati Manuel Locatelli, 23, wa Sassuolo.(Gazzetta dello Sport, via Mail)
Southampton imekataa ofa ya pauni milioni 25 kutoka kwa Aston Villa kwa ajili ya kiungo wa kati James Ward-Prowse, 26. (Athletic - subscription required)
Chelsea wanajiandaa kushusha gharama ya pauni milioni 40 kwa ajili ya mashambuliaji wa Kiingereza Tammy Abraham, ambaye anaivutia Arsenal, West Ham na Aston Villa. (Sun)
Everton bado hawajaamua kuhusu mlinzi wa Uholanzi Denzel Dumfries, 25, anayekipiga PSV Eindhoven.(Liverpool Echo)
Vyanzo vya juu huko Liverpool havikatai uhusiano na mshambuliaji wa Kiingereza anayekipiga West Ham Jarrod Bowen. (Star)
Arsenal wanajiandaa kumpa mkataba mpya kiungo wa kati Granit Xhaka, 28, baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi kuhusishwa na taarifa za kuhamia Roma.(Athletic - subscription required)
Leeds United wako kwenye mazungumzo ya awali kuhusu kumsajli kiungo Lewis O'Brien, 22, wa Huddersfield Town. (Football Insider)
Crystal Palace, Brentford na Watford wamehusishwa taarifa za kutaka kumnasa mchezaji kiungo Matthew Garbett, 19, anayecheza klabu ya Uswidi. Falkenbergs. (Sun)
Mwanariadha wa Kenya aondolewa nje michuano ya Olimpiki
Mwanariadha wa Kenya Mark Otieno Odhiambo ameondoshwa nje ya mashindano ya Olimpiki ya Tokyo baada ya vipimo kuonesha ametumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni
Kijana huyo wa miaka 28 alikuwa ametakiwa kushindana katika mbio za mita 100 za wanaume Jumamosi lakini alishindwa katika hatua ya vipimo na kubainika alitumia dawa za kusisimua misuli.
Kwa mujibu wa mkuu wa msafara huko Tokyo Waithaka Kioni: "Hata hivyo amekataa kutambua madai ya ukiukaji huo na kuomba uchambuzi wa sampuli yake ya mkojo ."
Kipimo kilifanyika tarehe 28 mwezi Julai wakati mwanariadha huyo alipokuwa Tokyo, kabla ya hapo alikuwa kwenye kambi ya mazoezi nchini Japan kati ya tarehe 15 na tarehe 24 mwezi Julai.
Otieno Odhiambo alishiriki kwenye Mashindano ya Dunia ya 2017 na Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2018.
Ni mwanariadha wa pili wa Kiafrika kuondolewa kwenye michuano hiyo baada ya Mnaijeria Blessing Okagbare.
Kioni alisisitiza kwamba maafisa wa michezo na bodi zinazosimamia michezo nchini Kenya wameazimia kuendeleza vita yao dhidi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni
''Haya ni mambo ambayo labda yanaweza kuepukika hii ndio sababu inaendelea kuwasiliana na mashirikisho ya michezo na ADAK kwa hivyo tunaendelea kutoa elimu juu ya kupambana na dawa zilizopigwa marufuku kwa wanariadha wetu, "aliiambia BBC Sport Africa.
"Lakini sio kwamba wanariadha hawajui na ndio sababu tunachukulia kuwa hana hatia hadi tutakapochunguza tena sampuli B ya mkojo.
"Nilizungumza naye mchana huu na ananiambia hawezi kukumbuka kama alitumia kitu chochote ambacho kitatoa matokeo ya aina hiyo.
"Kinachonisumbua ni kwamba Kenya tayari imekuwa kwenye orodha ya waliowekewa alama nyekundu na tulitarajia tutatoka katika orodha hiyo lakini tukio kama hili linaweza kuvuruga mpango wa kujinasua.''
Naibu Waziri Kundo amtumbua meneja wa TTCL Kagera, Shirika la Posta Kagera kuchunguzwa
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew ametengua uteuzi wa Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wa Mkoa wa Kagera Bi. Irene Shayo kuanzia tarehe 30/07/2021 kwa kile kilichobainika kuwa taratibu za uteuzi wake zilikiukwa na utumishi wake umekuwa wa kusuasua, amekuwa akikwepa ziara za viongozi katika eneo lake pamoja na kupika taarifa za mapato na matumizi
Mhandisi Kundo ameyazungumza hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Kagera ambapo alitembelea ofisi za TTCL na Shirika la Posta Tanzania (TPC) na kuona kuwa Meneja wa TTCL katika Mkoa wa Kagera hatoshi kuwa katika nafasi hiyo ukizingatia Kagera ni mkoa wa kimkakati kwasababu unapakana na nchi takribani nne hivyo Meneja wake anatakiwa kuwa na uwajibikaji wenye ufanisi mkubwa
“Ninaagiza Meneja wa Mkoa wa Kagera aondoshwe mara moja katika Mkoa wa Kagera na kuanzia leo asitambulike kama Meneja wa Mkoa wa Kagera, taratibu zifuatwe na apangiwe kazi zingine kulingana na wasifu wake kitaaluma ili aweze kufanya kazi vizuri kwasababu majukumu ya sasa hana uwezo nayo”, alizungumza Mhandisi Kundo
Ameongeza kuwa wao kama Wizara kupitia kwa Waziri mwenye dhamana Dkt. Faustine Ndugulile wana kasi ya kutaka kuona matokeo ya kile ambacho Serikali imedhamiria kukifanya kwa watanzania katika Sekta ya Mawasiliano
Amesisitiza kuwa ili kufanikisha hilo ni wajibu wao kufanya maamuzi ya kuhakikisha taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo zinaimarisha mifumo ya utendaji kazi katika ngazi za mikoa na utoaji wa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya watanzania
Katika hatua nyingine Mhandisi Kundo alitembelea na kukagua ukarabati wa Ofisi za Shirika la Posta Bukoba zilizogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 78,801,000 na kutorudhishwa na kiasi cha fedha kilichotumika kwasababu hakiendani na hali halisi ya ukarabati uliofanywa na kuagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini gharama halisi zilizotumika katika ukarabati huo
“Nimetoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Moses Machali aunde kamati itakayohusisha wataalam wa Ujenzi, TAKUKURU na Ofisi ya Usalama wa Taifa (W) ili wakafanye tathmini na kujiridhisha kile ambacho kimefanyika na iwapo ikibainika kuna watu ambao wamefanya ubadhirifu wa fedha za umma watachukuliwa hatua za kisheria
Sambamba na hilo ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL na PostaMasta Mkuu wa Shirika la Posta kuhakikisha mameneja wao wa Mikoa ambao hawana vigezo na uwezo wa kuongoza Mikoa hasa ile ya kimkakati wanaondolewa na kuwekwa watu wenye uwezo na vigezo vya kuongoza katika Mikoa hiyo
Mhandisi Kundo yupo katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kukagua miundombinu ya mawasiliano na upatikanaji wa huduma za mawasiliano ambapo ametembelea katika wilaya ya Muleba, Bukoba na Misenyi na amepanga kuendelea katika Wilaya za Kyerwa, Karagwe na Ngara. Ziara yake katika Mkoa huo ilianza tarehe 29 Julai hadi tarehe 2 Agosti 2021
Ilemela shida ya maji itakuwa historia - DC Masalla
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Elias Masalla amesema kuwa shida ya Maji ndani ya wilaya hiyo itakuwa historia baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa inayotekelezwa wilayani humo ukiwemo ule wa ujenzi wa Tanki la Maji la mlima wa Kwa Mkuu wa wilaya kata ya Buswelu uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni Tano.
Hayo ameyabainisha wakati wa muendelezo wa ziara yake ya kata Kwa kata kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo, kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 na kujitokeza kwaajili ya chanjo pindi zitakapowasili wilayani humo, kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kisha kuzipatia ufumbuzi akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, wakuu wa idara za manispaa ya Ilemela, wataalamu wa taasisi za TARULA, TANROADS, TANESCO, NIDA na RITA ambapo akawahakikishia wananchi wa kata ya Mecco waliojitokeza katika viwanja vya Jerry’s kumsikiliza, Kuwa anatambua wilaya hiyo kukabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa Maji ya uhakika hasa maeneo ya milimani na yenye sura ya vijiji kwamba Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe Samia Suluhu Hassan imekwisha toa fedha kwaajili ya ujenzi wa mradi huo mkubwa wa Maji na kwamba Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kwa mwaka huu zimeweka jiwe la msingi na Mapema mwezi septemba mradi huo utakuwa umekamilika
‘.. Kufikia mwezi septemba shida ya Maji itakuwa imeisha kama sio kupungua Kwa kiasi kikubwa, Sisi hatuwezi kukaa ofisini kama wananchi hamna Maji ..’ Alisema
Aidha Mhe Masalla akampongeza Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula Kwa namna anavyoshiriki katika kushughulikia kero za wananchi huku akilishukuru jeshi la polisi wilayani humo Kwa namna linavyofanya kazi kwa weredi
Kwa upande wake Mhandisi Josephat Ilunde kutoka mamlaka ya Maji safi na Maji taka jijini Mwanza MWAUWASA akafafanua kuwa Jiji hilo linahitaji Lita milioni 150 za Maji, wakati zilizopo ni Lita milioni 90 hivyo kuwa na upungufu wa Lita milioni 60 ambazo zitapatikana baada ya kukamilika Kwa chanzo Cha Maji Cha Butimba kinachogharimu zaidi ya bilioni 77 na kukamilika kwa miradi mingine inayoendelea ndani ya wilaya ya Ilemela
Nae kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Ndugu Shukran Kyando mbali na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu huyo wa wilaya amezitaka mamlaka za kata ya Mecco kuheshimu mipaka ya kata hiyo iliyotangwa mara ya mwisho katika gazeti la Serikali sanjari na kuiagiza kampuni inayofanya kazi ya urasimishaji makazi mtaa wa Mecco Kusini kuhakikisha inawasilisha ramani ndani ya siku 14 zilizotolewa na Mkuu wa wilaya hiyo Kwa wananchi Ili kuwaondolea usumbufu katika Zoezi la umilikishaji na kuikosesha Serikali mapato.
Zahanati zilizokwama miaka 17 zakamilika Sumbawanga - RC Mkirikiti
Zahanati mbili za vijiji vya Fyengeleza na Kankwale zilizoanzishwa ujenzi wake na wananchi na kukwama kwa zaidi ya miaka 17 sasa zimekamilika na zitaanza kutoa huduma kwa wananchi mwezi Octoba mwaka huu baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuzikamilisha.
Akiwa katika ziara ya kukagua miradi katika Manispaa ya Sumbawanga, jana (29.07.2021) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Joseph Mkirikiti ameipongeza halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kazi nzuri ya kukamilisha miradi hiyo ya zahanati zilizokwama kwa kipindi kirefu.
Taarifa zilizosomwa katika miradi hiyo ya zahanati kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa zilieza kuwa Zahanati ya kijiji cha Kankwale ilianza kujengwa miaka kumi na Saba (17) iliyopita pale wananchi walipoanzisha ujenzi huo mwaka 2004 huku ile ya kijiji cha Fyengelezya ikichukua miaka minane (8) kukamilika kutokana na sababu nyingi ikiwemo usimamizi usioridhisha wa miradi na ukosefu wa fedha.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa zahanati ya Kankwale imegharimu kiasi cha shilingi 81,068,000/- kukamilishwa kati ya hizo nguvu za wananchi zinazotokana na michango ya fedha tasilimu na nguvu zao kiasi cha shilingi milioni 24 na Manispaa kupitia mapato yake ya ndani imetumia shilingi milioni 10 na kiasi cha shilingi milioni 50 kimetoka serikali kuu.
Imeelezwa kuwa Zahanati ya Fyengerezya hadi kukamilika imegharimu kiasi cha shilingi milioni 75 kati ya hizo Manispaa imechangia kiasi cha shilingi milioni 25 kutoka mapato yake ya ndani na shilingi Milioni 50 zimetolewa na serikali kuu.
Baada ya kukagua miradi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Joseph Mkirikiti ameeleza kufurahishwa na ukamilishwaji wa Zahanati hizo zinazotoa jibu la ukosefu wa huduma kwa wananchi waliosubiri kwa muda mrefu na kuhoji miaka 17 nini kilikwamisha.
“Ninawapongeza viongozi wa Manispaa hii kwa jitihada na ubunifu wa kukamilisha majengo yaliyoanzishwa na wananchi kwa muda mrefu mfano zahanati ya Kankwale ilianza kujengwa mwaka 2004 huku ile ya Fyengeleza mwaka 2014 leo tunaona uongozi wa Manispaa wa sasa ukikamilisha kazi hii na kuwa mwezo Octoba huduma zitatolewa, ninachojiuliza ni swali hili, kwa nini miaka 17 hizi zahanati zilikwama? Ni ukosefu wa fedha kweli au ni usimamizi?”. alisema Mkirikiti.
Mkirikiti aliongeza kuwa jitihada za Manispaa hiyo kukamilisha ujenzi wa majengo ambayo yalijengwa na wananchi lakini hayakukamilika unatoa suluhisho la upungufu wa miundombinu ikiwemo shule mpya ya msingi Ntendo “B”, maabara za sayansi shule za sekondari Kalangasa na Ntendo.
“Wito wangu bado tunao mzigo ni mkubwa ndani ya manispaa yetu na mkoa wetu wa Rukwa ,hivyo tunapaswa kuongeza kasi zaidi ili kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na kuweza kunufaisha wananchi huku tukizingatia ubora na matumizi sahihi ya fedha za umma”. alisisitiza Mkirikiti.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya alisema mafanikio yaliyowezesha kukamilishwa kwa miundombinu hiyo ni ushirikiano waliopata toka kwa wananchi na watumishi wa halmshauri hiyo .
“Siri ya kukamilisha miradi hii imetokana na ushirikiano wetu ndani ya Manispaa wakiwemo Madiwani wetu na pia usimamizi wa miradi shirikishi pamoja na uwepo wa fedha toka Serikalini” alisema Mtalitinya.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Fyengeleza Frolence Masanja aliishukuru Serikali kwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho uliokuwa umekwama miaka mingi.
Masanja alisema kukamilika kwa zahanati hiyo kutasaidia wananchi hususan akina mama wajawazito na watoto kupata huduma karibu zaidi na makazi yao tofauti na ilivyo sasa ikihusisha kusafiri kwenda mjini Sumbawanga.
Mkuu huyo wa Mkoa ambaye amehamishiwa Rukwa kutoka Mkoa wa Manyara hivi karibuni alibainisha lengo la Mkoa wake kuwa ni kuhakikisha majengo ya shule na zahanati yaliyokwama ujenzi wake yanakamilika kabla ya mwezi wa Octoba mwaka huu ili kuweza kuruhusu utoaji huduma za elimu na afya.
Mbunge Kunambi akagua ujenzi wa madarasa anayotekeleza ujenzi wake Kata ya Mchombe
MBUNGE wa Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi amefanikisha azma yake ya kumaliza changamoto ya Maji katika Shule ya Sekondari Nakaguru iliyopo katika Kata ya Mchombe.
Kunambi amekamilisha ahadi ya kupeleka maji katika Shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha sita ikiwa ni matunda ya ziara yake aliyofanya Februari mwaka huu ambapo wanafunzi wa shule hiyo walimlalamikia changamoto hiyo.
Awali wanafunzi wa shule hiyo walikua wakisafiri umbali wa kilomita moja kufuata maji lakini sasa watachota maji ndani ya eneo la Shule hiyo.
Kunambi pia amefanikisha upatikanaji wa Bomba la maji mserereko kwa wananchi wa kijiji cha Nakaguru katika kata hiyo ya Mchombe.
Katika ziara hiyo pia Kunambi ametembelea Shule mbili moja ikiwa Shule ya Msingi Ngai ambayo amefanikisha kuanza kwa Ujenzi wa Darasa ambapo awali wanafunzi wa darasa la sita walimlalamikia kusoma kwenye darasa la wazi.
"Ni furaha yangu kuona nimekamilisha ahadi yangu kwa Sekondari ya Nakaguru ya kuwaletea Maji hapa lakini pia kufanikisha kuanza kwa Ujenzi wa Darasa hapa Ngai ambapo mwanzo walikua wakisoma kwenye darasa la wazi ambapo wanafunzi waliteseka nyakati za Mvua.
Ziara yangu hii pia nimekagua ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Nakaguru ambayo yameshakamilika pamoja na madawati yake na sasa wanafunzi watasoma bila tabu,"Amesema Kunambi.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mchombe, Bathelomeo Swala amemshukuru Mbunge Kunambi kwa kufanikisha ahadi zake hizo ambapo amesema ujenzi wa madarasa hayo vitakua chache kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii.
Nae mmoja wa wanafunzi wa Sekondari ya Nakaguru Imelda John amemshukuru Mbunge Kunambi kwa kuwaletea maji kwani ilikua ni changamoto ya muda mrefu kwao hivyo sasa wana uhakika wa kupata maji safi kwenye Shule yao.
RAS Arusha akerwa waamuzi kuibeba JKT Mbweni mchezo wa mwisho ligi kuu netiboli
Waamuzi Masumbuko Matata wa Mwanza na Enock Akyoo wa Mtwara ambao walichezesha pambano la mwisho la Klabu bingwa ya Netiboli kati ya TAMISEMI QUEENS na JKT Mbweni ambalo lilimalizika kwa timu ya JKT Mbweni kushinda kwa magoli 40-39 wamelalamikiwa vikali na wadau wa mchezo huo kwa kuibeba timu mojawapo katika mchezo huo uliopigwa juzi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Katika pambano hilo kali na la kusisimua lililoshuhudiwa na mgeni rasmi Naibu Waziri, Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paulina Gekul wadau hao wameitaka CHANETA kuwachukulia hatua kali waamuzi hao kwa kuboronga kwa makusudi ili kuibeba timu ya JKT Mbweni.
Miongoni mwa walioshuhudia mchezo huo ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt Athumani Kihamia ambaye baada ya mchezo kumalizika alizungumza na waandishi wa habari na alionyesha dhahiri kukerwa na Kitendo cha Mwamuzi Matata kutoka Mwanza kushindwa kuumudu mchezo huo.
“Huyu refa aliyechezesha mchezo wa leo kutoka Mwanza mimi siwezi kumung’unya maneno hakuchezesha kihalali na tunaweza kusema ameyatia aibu mashindano haya,” amesema Dkt Kihamia.
Dkt Kihamia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Michezo mkoa wa Arusha amesema anatarajia tukio kama hilo hataliona mwakani katika mashindano ya Ligi daraja la kwanza na badala yake aliwataka CHANETA kuhakikisha kuwa mashindano hayo yanaamuliwa na marefa walio huru na uwezo.
“Kwa refa kuchezesha vile ama hana uwezo au kachukua rushwa ama timu mojawapo inamhusu, kwa hiyo mwakani tutahakikisha mambo ya namna hii hayatokei katika mkoa wetu,” alisema Dkt Kihamia.
Kwa upande wake Mhe. Gekul wakati akiyafunga rasmi mashindano hayo aliwataka CHANETA kuhakikisha inateua waamuzi bora na wenye weledi wa kuchezesha mashindano ya ligi daraja la kwanza katika michezo kama hiyo mwakani.
“CHANETA hakikisheni waamuzi ambao mnawapa jukumu la kuchezesha michezo hii wawe ni waamuzi ambao hawafumbii macho jambo lolote linalofanyika uwanjani ambalo siyo la haki, ili atakayeshinda ashinde kwa haki na atakayeshindwa ashindwe kwa haki,” alisema Mhe.Gekul.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya TAMISEMI Philbert Rwakilomba alieleza wazi kukerwa na kitendo cha waamuzi hao kuibeba timu ya JKT Mbweni katika mchezo huo kinashusha maendeleo ya mchezo huo kwani timu yake licha ya kuonyesha mchezo mzuri haikutendewa haki hasa na mwamuzi namba moja.
“tulitegemea kwa kuwa mchezo huu ndiyo uliokuwa ukiamua Klabu ipi kati ya hizo mbili kubeba ubingwa wa mchezo wa Netiboli mwaka huu, tushuhudie mchezo mzuri lakini kwa kweli nilichokiona hapa ni maamuzi ya marefarii wetu kuegemea upande wa wapinzani wetu,” alisema Rwakiloma
Kwa upande wake Nahodha wa TAMISEMI QUEENS Sophia komba alisema kuwa baada ya kuona waamuzi wameegemea upande mmoja alilazimika kupeleka malalamiko yake kwa mwamuzi wa akiba baada ya robo ya pili ya mchezo lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Miongoni mwa wananchi waliofurika kuutazama mchezo huo ni pamoja na Benson Maneno ambaye pia ni Afisa michezo wa Jiji la Arusha ambaye alisema kuwa waamuzi waamuzi hao waliipendelea JKT Mbweni huku Juma Athumani, mkazi wa Arusha yeye alisema kama siyo JKT Mbweni kucheza kibabe na Mwamuzi kuwabeba TAMISEMI QUEENS wangeifunga Mbweni JKT siyo chini ya magoli manane.
Katika mchezo huo wa mwisho wa klabu bingwa ligi daraja la kwanza timu ya Mbweni JKT ilishinda mchezo huo, huku TAMISEMI QUEENS ikishika nafasi ya pili.
Pia timu ya TAMISEMI QUEENS ilifanikiwa kutoa mfungaji bora wa mashindano hayo Lilian Jovin, Mchezaji bora wa mashindano hayo (MVP) Meryciana Kizenga na Mchezaji bora wa kati wa mashindano hayo Sophia Komba.
Jumla ya timu 13 zilishiriki mashindano hayo timu tisa za wanawake na timu nne za wanaume, ambapo washindi watatu wa kwanza wataiwakilisha nchi katika mashindano ya Netiboli Afrika Mashariki na timu sita za mwanzo zitashiriki katika kombe la Netiboli Zanzibar katika mashindano yatakayofanyika baadaye mwaka huu.
Blinken kuhusu mkataba wa nyuklia wa Iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema kuwa mazungumzo ya nyuklia na Iran hayataendelea milele.
Blinken alifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na mwenzake Ahmed Nasser es-Sabah huko Kuwait, ambapo alienda kufanya mawasiliano rasmi.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliotangazwa kwenye televisheni ya serikali ya Kuwait, Blinken alisema: "Tulikuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Wairani huko Vienna, kuonyesha nia yetu njema na ya kurudi kwenye makubaliano ya nyuklia. Mazungumzo na Iran hayataendelea milele. Mpira sasa upo kwa upande wa Iran na ndio wanaopaswa kufanya uamuzi. "
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwaiti Sabah alisema kuwa Marekani ilionyesha umuhimu unaozingatia kuhakikisha usalama katika eneo hilo.
Sabah pia alibaini kuwa wanataka kuandaa mkutano wa tano wa mazungumzo ya kimkakati kati ya Kuwait na Marekani.
Mkutano wa kwanza wa Mazungumzo ya Mkakati wa Marekani na Kuwait ulifanyika Washington mnamo 2016 na wa pili mnamo 2018, na wa tatu ulifanyika Kuwait mnamo 2019, na wa nne ulifanyika kupitia video mwaka jana.
Mazungumzo hayo, yaliyokuwa yakiendelea kwa takriban miezi 3 huko Vienna, mji mkuu wa Austria, ambayo vyama vya Ulaya pia vilishiriki, yalikwama baada ya mgombea wa kihafidhina Ebrahim Reisi kushinda uchaguzi wa urais uliofanyika Iran mnamo Juni 19.
Mkuu huyo alisema kuwa Tehran haitakubali makubaliano ya nyuklia isipokuwa vikwazo vya Marekani vitakapoondolewa kikamilifu.
Washington pia ilisema kwamba sharti hili halikubaliki na kuonya kwamba "mazungumzo hayawezi kuendelea kwa muda usiojulikana".
Yanga ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa Zesco wa Zambia
Tumu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa beki wa Zesco ya nchini Zambia, Mkongomani Marcel Kalonda ambaye anatumia guu la kushoto na ni mkali katika kukaba katika ile staili ya mtu na mtu ‘man to man’.
Uwezo wake huo unaweza kuwa kikwazo kwa viungo wasumbufu kwenye ligi kama Clatous Chama, Luis Miquissone pamoja na mastaika kama John Bocco na Prince Dube.
Kalonda, 23, mkataba wake na Zesco unatarajiwa kumalizika Desemba 31, mwaka huu hivyo huenda akaja kuchukua nafasi ya Mghana Lamine Moro ambaye tayari Yanga imetangaza kuachana naye Alhamisi.
Yanga imepanga kukiboresha kikosi chao ili kifanye vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kocha Nasreddine Nabi ndiye anayetajwa kupendekeza jina la beki huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba, kupunguza na kuanzisha mashambulizi kwenye goli la wapinzani.
“Katika kikao cha Jumatano jioni kilichowakutanisha Kamati ya Mashindano ya Yanga na kocha Nabi, jina la Kalonda lilitajwa katika mipango yetu ya usajili.
“Jina hilo lilikuja baada ya kocha na kamati kukubaliana kwa pamoja kuachana na Moro.
“Hivyo yapo baadhi ya majina yaliyokuwa yamewekwa mezani yaliyokuwa yanapitiwa na Kalonda lilikuwepo pamoja na beki raia wa Benin, Partene Counou. Hivyo mmoja kati ya hao huenda akawa mbadala wa Moro,” alisema mtoa taarifa huyo.
Akizungumzia usajili huo, Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla alisema: “Kikubwa Wanayanga wawe watulivu, tumepanga kufanya
usajili bora utakaofanikisha malengo yetu katika msimu ujao, tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa wachezaji wetu na mara baada ya kukamilika tutaweka wazi kila kitu.”
Corona yaitikisa Manchester United
MANCHESTER United imelazimika kusogeza mbele mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Preston North End uliotarajiwa kuchezwa leo Jumamosi kutokana na kutikishwa na janga la Corona.
Inaelezwa kuwa kuna wachezaji tisa wa Manchester United ambao wamepata Virusi vya Corona jambo ambalo limezua hofu na kuamua kuchukua tahadhari.
Vipimo vilivyochukuliwa kufuatia mechi ya kirafiki ya juzi Jumatano dhidi ya Brenford ambayo ilichezwa mbele ya mashabiki 30,000, vilionyesha idadi hiyo ya waathirika katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solkjaer.
Mechi hiyo ya Jumatano iliisha kwa sare ya kufungana mabao 2-2. Pia mechi ya Bretford dhidi ya West Ham inaweza isichezwe kwa kuwa Brendford nao wanafanya vipimo kutokana na kuhusika na mchezo dhidi ya United.
Taarifa kutoka United jana ilieleza kuwa kuendeleza usalama dhidi ya Corona ndiyo kipaumbele chao jambo ambalo limefanya waliopata Corona wajitenge na wengine.
"Kufuatia vipimo vya wachezaji wa kikosi cha kwanza tumepata idadi ndogo ya waathirika hiyo imefanya wengine kujitenga wakisubiri vipimo zaidi,".
Japan yakanusha madai kwamba kuna uhusiano kati ya Olimpiki ya Tokyo na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona
Japan imekanusha madai kwamba kuna uhusiano kati ya Olimpiki ya Tokyo na mwenendo unaoongezeka wa aina mpya za virusi vya corona (Kovid-19).
Waziri Mkuu Suga Yoshihide, katika mkutano na waandishi wa habari, alisema kwamba hakuona uhusiano kati ya ongezeko la kubwa la kesi za maambukizi katika siku za mwisho baada ya Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, ambayo ilianza mnamo Julai 23.
Suga alisema,
"Tunatekeleza hatua za kinga ya virusi ambazo hupunguza trafiki ya binadamu pamoja na udhibiti mkali wa mipaka ili kuzuia kuenea kwa janga hilo kutoka kwa wageni. Nadhani hakuna uhusiano wowote."
Idadi kubwa zaidi ya kesi za maambukizi tangu mwanzo wa janga huko Japan ilirekodiwa jana. Kesi za maambukizi ya virusi kote nchini ziliongezeka kwa zaidi ya 10,000 kwa siku moja kwa mara ya kwanza.
Idadi ya vifo kutokana na virusi nchini iliongezeka hadi 15,188, na idadi ya wagonjwa iliongezeka hadi 904,036. Katika vitengo vya huduma za wagonjwa mahututi, watu 539 wanatibiwa Kovid-19.
TAMBUA DALILI ZA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME NA TIBA YAKE, PIA TAMBUA DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE
TAMBUA DALILI ZA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME NA TIBA YAKE, PIA TAMBUA DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE
Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo kikamilifu shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili,homon,Neva,misuli,hisia na miriji ya damu
CHAZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
-kuwa na halemu (cholesterol) na shinikizo la damu( B,P,)au ugonjwa wa motorcycle
-ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
-kisukari,
-umri hasa wazee
-utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
-tabia za kujichua kwa mda mrefu ,kutopata usingizi
-ngiri,vidonda vya tumbo,
-tumbo kuunguruma na kukosa choo
-matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibu magonjwa Kama vile,kansa,vidonda vya tumbo,moyo,kisukari
DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
1kuwahi kufika kileleni,2kukosa hamu ya tendo 3kushindwa kurudia tendo la ndoa 4uume kusimama kwa uregevu au kushindwa kusimama 5 kuchoka Sana baada ya tendo la ndoa
TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME
Dawa ya MJN ni dawa ya asili isiyokuwa na mkemikali yoyote dawa hii ipo kwenye mfumo wa kunywa na kuchua pia dawa hii ni tamu Sana kwani imechanganywa na asari ni tofauti na ulizowahi kutumia usaidia ata wazee wenye miaka 80 pi uboresha uume wa mwanaume ulioingia ndani na kuwa mfupi
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE
1. kunywa maji mengi Sana Kila wakati
2. kwenda haja ndogo Mara kwa Mara
3. kuwa dhaifu ,kukosa nguvu na kijisikia mchovu kila wakati
4. kupunguza uzito au kukonda ata Kama unakula
5. kutoona vizuri
6. mwili kufa gazi hasa miguni
7. vidonda au majeraha sehemu ya mwili kutopona
8 kupungukiwa nguvu za kiume nk
MTN ndio dawa ya kisukari dawa hii inatibu tatizo mojakwamoja endipo ukidhingatia matumizi yake ni dawa isiyokuwa na masharti magumu kwa mtumiaji,pia zipo dawa za vidonda vya tumbo,presha,ngiri,chango la uzazi, miguu kuuma na mgongo
Ndugu mteja epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahii kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO
WASILIANA NAMI TABIBU DITTU KWA SIMU 0755028097 AU Whatsapp +255714448999 ofisi ipo mbagara sabasaba walio nje ya mkoa utatumiwa sehemu yoyote ulipo
CHUO CHA ROYAL KINATANGAZA NA FASI ZA MASOMO
Chuo cha Royal Training Institute Kilichopo Mbagala Jijini Dar es salaam kinawatangazia nafasi za masomo kwa kozi za mwezi April na Septemba mwaka huu.
Usajili umeanza na Unaendelea chuoni Royal Training Institute.
Chuo kimesajiliwa na NACTE kwa usajili namba REG/HAS/103.
Kozi zinazotolewa na Royal Training Institute ni:-
Ordinary Diploma in Pharmaceutical Sciences(Kozi ya Ufamasia) miaka mitatu. Uwe na Alama D nne zikiwemo Kemia na Baiolojia.
Ordinary Diploma in Pharmaceutical Sciences (In Service) Mwaka 1-uwe umemaliza NTA Level 5
Pia Chuo cha Mafunzo Royal kwa kushirikiana Na Mamlaka ya Elimu ya ufundi (VETA) kingependa kuwajulisha wahitimu wa kidato cha nne kwamba sasa Chuo kinatoa kozi ya msaidizi wa maabara (Certificate in Laboratory Assistants) ngazi ya 1, 2 na 3 Uwe umemaliza kidato Cha nne na kupata cheti muhula utaanza Mwezi wa nne . Wahitimu watafanya kazi kwenye mashule, viwanda na taasisi mbalimbali. Chuo pia kitatoa punguzo kwako na kukusaidia kupata kazi.
Pia chuo Cha Royal Institute kinatoa kozi ya Manunuzi na Ugavi(Procurement & Supply) ngazi ya cheti na Diploma. Uwe na ufaulu wa D 4 katika masomo ya kidato Cha nne.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na chuo Cha Royal kwa namba 0688353310, 0713325507, 0692972523, 0788083484
Au kwa barua pepe pharm_royal@yahoo.com, au tembelea tovuti yetu ya WWW.RTI.AC.TZ.
KUMBUKA KUNA PUNGUZO GHARAMA ZA HOSTELI KWA WALE WATAKAOWAHI..
Vikosi vya Rwanda vyafanya vema Msumbiji

Jeshi la Rwanda lililopelekwa Cabo Delgado nchini Msumbiji limetangaza kufanya vyema kwenye uwanja wa mapigano huku kukiwa na wasiwasi kuhusu kamanda wa kikosi hicho.
Msemaji wa jeshi la Rwanda ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanamgambo 14 wameuliwa wiki hii na wanajeshi kutoka Rwanda waliopelekwa Msumbiji.
Ronald Rwivanga amesema operesheni za kijeshi zilizoendeshwa kwenye maeneo ya Mbau na Awese,mkoani Cabo Delgado, baada ya kikosi cha wanajeshi wake kuvamiwa, zilisababisha jumla ya wanamgambo 14 kuuliwa. Rwivanga amesema ni majeraha madogo yaliowapata wanajeshi wa Rwanda kufuatia operesheni hizo.
Mapema mwezi huu, Rwanda ilipeleka kikosi cha wanajeshi na polisi 1,000 nchini Msumbiji kusaidia katika kupamabana na kundi la waasi linaloendesha mashambulizi kaskazini mwa nchi hiyo. Takriban raia laki nane waliyahama makaazi yao kwenye mkoa wa Cabo Delgado na mapigano hayo yalisababisha kampuni ya Mafuta ya Ufaransa ya Total kusitisha mradi wake wa dola bilioni 20 wa kuzalisha gesi asilia kwenye mkoa huo.
Ikiwa kupelekwa kwa kikosi cha wanajeshi wa Rwanda nchini Msumbiji kunalenga kuwasaka wanamgambo wenye itikali kali. Lakini wakosoaji wa serikali ya Rwanda wanaoishi nchini humo wanahofia usalama wao pia. Jenerali Innoncent Kabandana anayeongoza kikosi hicho, ameelezwa na wapinzani kuwa ni mkono wa rais Paul Kagame katika kuwalenga wakosoaji wake.Mtandao wa TheRwandan.com, uliandaka kuwa Meja-jenerali Kabandana alihusika na mauwaji ya maaskofu wa kanisa katoliki wa Gakurazo mwaka 1994 nchini Rwanda na vilevile kuwalenga wakosoaji wa serikali ya Rwanda nchini Marekani na Canada ambako alifanya kazi kama mwambata wa kijeshi katika ubalozi wa Rwanda jijini Washington.
Cleophas Habiyareme, mkuu wa jamii ya wakimbizi wa Rwanda wanaoishi nchini Msumbiji amesema alisoma taarifa pia kwamba kamanda huyo anahusika na kuwalenga wapinzani wanaoishi nje ya nchi. Lakini amesema hilo haliwezi kuwatisha jamii ya wakimbizi wa Rwanda nchini Msumbiji. Habiyareme amesema Msumbiji ni nchi iliyosaini mkataba wa Geneva kwa jili ya kuwapa hifadhi wakimbizi. Amesema halitokuwa jambo la busara kwa kikosi kilicho alikwa kwa shughuli malumu baadae kuanza kuwalenga wakimbizi. Hata hivyo ameiomba serikali ya Msumbiji kuhakikisha usalama wao.
Nchini Msumbiji ambako jenerali Kabandana amepewa majukumu mapya, jamii ya wakimzizi wa Rwanda ni takriban watu 4,000 ambao wamekuwa wakibughudhiwa na kuuliwa miaka ya hivi karibuni. Kisa cha hivi karibuni ni kutoweka bila maelezo yoyote hadi sasa kwa mwandishi habari na mkosoaji wa serikali ya Rwanda Ntamuhanga Cassien aliyekuwa akiishi kwenye kisiwa cha Inhaca,nchini Msumbiji.
SHANTA GOLD yapongezwa kusimamia Matakwa ya Sheria ya matumizi kwa Jamii
Na. Steven Nyamiti - Singida
Waziri wa Madini Doto Biteko ameeleza kuwa, Mgodi mpya wa Kati wa Dhahabu wa Shanta ndio mgodi pekee Tanzania unaotekeleza ipasavyo Matakwa ya Sheria ya matumizi kwa Jamii husika (Local Content).
Amesema hayo tarehe 30 Julai, 2021 alipotembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Mgodi wa Kati wa Dhahabu wa Singida (SINGIDA GOLD MINE) Shanta uliyopo wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Amesema historia ya ujenzi wa mgodi huo, kwa miaka mitano yote iliyopita Mgodi wa Shanta ndio modi wa Kati mpya uliojengwa hapa Nchini.
Akizungumzia kuhusu umuhimu wa Sheria ya Local content amesema kuwa, katika uwekezaji inawahitaji wakubwa, wa kati na wadogo ili kufanya uchumi uwe na maana.
“Kama biashara wafanye wenyeji, tulikuwa na migodi ambayo hata nyama ilitoka South Africa, lakini mgodi ambao mwaka huu tumewapa tuzo ya Local content, huu ndio mgodi ambao asilimia 100 ya walioajiriwa ni watanzania,”ameeleza Biteko.
Aidha, ameipongeza kampuni ya uchimbaji madini ya Shanta kwa kupiga hatua katika kusimamia Sheria hii ya Local content na manunuzi ya bidhaa katika migodi yao kwa asilimia kubwa ambao unategemea kuanza shughuli za uzalishaji wa dhahabu Mwezi Novemba 2022.
Naye, Meneja Mkuu Mahusiano ya Serikali wa mgodi wa Shanta, Philibert Rweyemamu amemueleza Waziri Biteko kuwa, wanashirikiana na uongozi wa Wilaya na Mkoa katika kutoa kipaumbele katika shughuli za maendeleo. Amesema wananchi wa Ikungi na Singida kwa ujumla wanapata ajira mbalimbali zinazotolewa na mgodi huo pamoja na manunuzi ya bidhaa mbalimbali.
Pia, Meneja Mkuu Shanta Mradi wa Singida Jiten Divecha akisoma taarifa ya mgodi huo ameeleza kuwa, hadi sasa mgodi unawafanyakazi 117 sawa na asilimia 70 ambao wameajiriwa kutoka vijiji vinavyozunguka mgodi.
"Tumekamilisha vyumba vya madarasa ya shule ya Sekondari Mangonyi Shanta na madawati 183," amesema Divecha.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida Binilith Mahenge ameipongeza Serikali kupitia wizara ya madini kwa mageuzi makubwa katika sekta ya madini hapa nchini. Amesema mageuzi ni mengi makubwa na utunzaji wa rasilimali madini.
“Shanta sina wasiwasi nao, sisi kama wasimamizi wa mkoa huu tutakuwa pamoja katika kusimamia mgodi huu katika kuimarisha usalama na niwahakikishie fanyeni kazi, hatutakuwa sehemu ya changamoto bali tutatatua changamoto zenu. Kuhusu miundombinu ya barabara na maji nitahakikisha kama Mkuu wa mkoa vinapatikana hapa,” ameongeza Mahenge.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Rajab Mtaturu amemueleza waziri Biteko kuwa, mgodi huo wa Shanta utachochea shughuli za uchumi kwa wananchi baada ya mgodi kuanza kufanya kazi. Amesema yeyé kama muwakilishi wa wananchi wa Singida Mashariki anatamani mgodi uanze shughuli za uchimbaji haraka ili kurahisisha maendeleo.
Waziri Biteko amefanya ziara ya kutembelea Mgodi wa Marwa Marwa and Partiners, Kukagua shughuli za uchimbaji na kuzungumza na Wachimbaji Wadogo katika kijiji cha Sambalu kata ya Mangonyi wilaya ya Ikungi. Biteko amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jery Muro na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida kuhakikisha wanafungua Vituo vya kununulia Dhahabu katika eneo la mgodi ili kurahisisha wachimbaji wadogo kupata huduma kwa haraka.
Jiko la mkaa laua tena Njombe ni baada ya mwingine kulala na jiko kwenye kibanda cha biashara
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...












































