Search This Blog

Friday, May 31, 2019

Taarifa Nyingine Mbaya Kutoka Nigeria Kuhusu Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines, Mzee Obasanjo na Wenzake 393 Wanusa Kifo


Ikiwa ni miezi miwili tu imepita tangu shirika la ndege la Ethiopian Airlines ndege yake ya Boeing 737 MAX kuanguka, Bado mzimu wa ajali unaendelea kulikumba shirika hilo kwani imeripotiwa kuwa juzi Jumatano usiku ndege moja ya shirika hilo imeponea chupu chupu kuanguka Jijini Lagos nchini Nigeria, baada ya kushindwa kutua mara tatu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Muhammed.


Shirika hilo la ndege limethibitisha taarifa hizo na kuydai kuwa ndege hiyo ni Boeing 777-300 na ilikuwa inatoka Addis Ababa na ilishindwa kutua kwa zaidi ya mara tatu kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya jambo lililopelekea ndege hiyo kutotua katika uwanja huo.

Ndege hiyo iliyokuwa na abiria wapatao 394, imeelezwa kuwa alikuwemo Rais Mstaafu wa Nigeria, Mzee Olusegun Obasanjo ambaye alikuwa akitokea nchini Ethiopia.

Ajikata Kidole Baada ya Kupiga Kura Chama Ambacho Hakukidhamiria


Mpiga kura mmoja nchini India amekikata kidole chake baada ya kugundua kuwa alikitumia kupigia kura chama cha siasa ambacho hakukidhamiria.

Kupitia video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii, mpiga kura huyo, Pawan Kumar, alisema kwa bahati mbaya aliishia kukipigia kura chama tawala cha Bharatiya Janata (BJP).

Alisema alitaka kukipigia kura chama kingine lakini alichanganya alama nyingi zilizokuwa kwenye mashine ya kupigia kura.

Kila mpiga kura kidole chake cha shahada huwekwa alama kwa wino baada ya kupiga kura katika taifa hilo.

Kumar alipiga kura yake wakati wa uchaguzi mwezi uliopita katika eneo la Bulandshahr jimbo la Kaskazini la Uttar Pradesh.

”Nilitaka kupiga kura kwenye alama ya Tembo, lakini nikapiga kwenye alama ya Ua kimakosa,” alisema Kumar.

Alielezea alama za vyama zilizokuwa kwenye mashine sambamba na jina la kila mgombea.

Uchaguzi huu unapitia awamu saba, huku kura zikiwa zimekamilika kuhesabiwa Mei 23.

Nchini India kuna wapigakura 900, wanaofanya uchaguzi wa India kuwa mkubwa kuwahi kushuhudiwa duniani.

Wakati BJP alama yake ni Ua, Tembo ni alama ya chama cha Bahujan Samaj (BSP), ambacho kimeungana na vyama vingine viwili kupambana na chama tawala.

Alama za vyama zina nafasi kubwa kwenye uchaguzi wa India kwa kuwa ni rahisi kutambulika kwenye nchi yoyote ambayo yenye watu wengi wasio na elimu.

Lakini pia kuna vyama mbalimbali na muungano wa vyama ambavyo huwachanganya wapiga kura.

Wema Sepetu Learns Her Lesson the Hard Way And Now Keeps her Love Life Top Secret




Tanzanian actress, Wema Sepetu has been in and out of relationships and she blames it all on publicizing her love affairs.

She affirms that she has learnt her lesson the hard way.

Wema Sepetu "You owe no one an explanation for anything you do… Learn to live your life for you and not otherwise… Outfit by @chapa1collection"
   
This she expresses during a recent interview with Wasafi Media failing to disclose any details of her current dating life.

Sijui kama niko single, au kama niko kwenye mahusiano.

Wema does not feel the need to inform the public about her private life because it would not add to anything.

Mi naona hakuna haja.

Mimi mbaka watu wajue sasa hivi niko na nani kwenye mahusiano, watahangaika sana.

According to the model, the minute the public becomes a part of your love triangle, it is bound to be shaky and most probably collapse.

Nimeregret sana.

Kwa sababu once ukishayaweka mahusiano yako, out in the open, unawakaribisha watu waanze kuyajudge.

Inakuwa tena sio watu wawili.

The world suddenly sets the rules and ensures it´s demands are met.


The beauty´s most recent relationship took a turn after sharing a steamy video between her and lover.

A move that saw the government ban her from her acting role.


Therefore compelling her to address the press and give her public apology on the same.

The ban lasted a whooping 5 months before the government could lift it, something that must have been heavy for the model.

However, for her, it is part of life´s lessons and appreciates having gone through such phases.

Ni phase ambayo kila binadamu anastahili kupitia.

Unaexperience, unajifunza, unapojifunza, ni vizuri.

Bora mtu ajifunze mwenyewe kuliko kufundishwa.



R Kelly Akabiliwa na Mashtaka Mapya 11


Mkongwe wa muziki  nchini Marekani R Kelly ameshtakiwa kwa makosa 11 ya unyanyasaji wa kingono kwa mabinti waliokuwa chini na umri wa miaka 16.

Kwamujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani, Mahakama imeripotiwa kuwa vitendo hivyo vilifanywa kwa watoto wa umri kati ya miaka 13 na 16 na ikiwa itathibitika kufanya kitendo hicho atakabiliwa na adhabu kali kuliko adhabu nyingine anazokabiliwa nazo.

Mwanzoni mwa mwaka huu kellz alikabiliwa na mashtaka kumi ya unyanyasaji wa kingono, alikana kuhusika na vitendo hivyo na akaachiwa kwa dhamana.

Hata hivyo R kelly anaimani kubwa ya ushindi dhidi ya mashtaka yake kumi yanayo mkabili, huku kesi zake kuanza kusikilizwa hivi karibuni mjini Chicago.

Licha ya kesi ya unyanyasai wa kingono msanii huyo anakabiliwa na kesi ya ukwepaji kodi na kusafirisha wanawake kwaajili ya kufanyanao ngono.

Makubwa..Mama Mjamzito Ajipasua, Amtoa Mtoto


Mwanamke Joyce Kalinda (30) amezua taharuki kwa wakazi wa Kirando mkoani Rukwa, baada ya kudaiwa kujichana tumbo kwa kitu chenye ncha kali na kumtoa mtoto akiwa hai.

Tukio hilo limetokea jana, baada ya mwanamke huyo kufika kituo cha Afya cha Kirando majira ya saa tisa alfajiri na kuanza kupiga kelele akimtaka muuguzi aliyekuwa zamu ampe huduma za kumsaidia kujifungua.

Imeelezwa kuwa kutokana na kuwepo kwa wagonjwa wengine kituoni hapo, muuguzi alimshauri mama huyo kusubiri kidogo na baadaye atamhudumia lakini aliporejea hakumkuta mgonjwa huyo.

Baada ya muuguzi kutomkuta pale alipomuacha aliamua kwenda getini na kumuuliza mlinzi ambaye alimjibu kuwa mama huyo alitoka nje ya kituo bila kuaga anakwenda wapi.

Kwa mujibu wa Dk. Hashi Mvogogo ilipotimu saa 11 alfajiri mama huyo alirudishwa hospitalini hapo akiwa amepasuka sehemu ya tumbo, huku watu waliomfikisha hospitalini hapo wakiwa wamebeba mtoto mchanga, kwa maelezo kuwa alikuwa amejipasua tumbo na kumtoa mtoto tumboni.

“Tumbo lilionekana kuwa limepasuliwa na kitu chenye ncha kali, alipofika aliwekewa dripu tatu za damu ili kuokoa maisha yake kwani alikuwa amepoteza damu nyingi, lakini pia mtoto amepewa matibabu kutokana na kutolewa tumboni bila kufuata utalaalamu” amesema Dk. Mvogogo.

Hata hivyo Dk. Mvogogo ambaye ndiye mganga mkuu wa wilaya ya Nkasi amesema bado uchunguzi unaendelea kufanyika na tayari wamewaachia Polisi kuendeleza uchunguzi huo ili kubaini iwapo ni kweli alijifanyia upasuaji mwenyewe au alifanyiwa na mtu mwingine.

Aidha amesema uchunguzi utakaofanywa pia utahusisha mtaalamu wa ugonjwa wa akili ambaye atachunguza na kubaini kama mamahuyo ambaye ni uzao wake wa nne ana ugonjwa wa akili au la.

Wakuu wa Mikoa Waonywa Kuhusu Matamko Wanayoyatoa


Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara amewaonya wakuu wa mikoa ambao wamekuwa wakitoa matamko ambayo yako tofauti na maagizo ya serikali.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma baada ya mkuu wa mkoa wa Iringa, Ali Hapi kutoa tamko la kuwataka waandishi wa habari kuwa na vitambulisho vya wafanyabiashara ndogo ndogo vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Amesema kuwa tamko lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuhusu makundi yanayotakiwa kupewa vitambulisho vya Wafanyabiashara wadogo si la Serikali.

Aidha, mezitaja sifa za Mfanyabiashara anayetakiwa kupewa kitambulisho kuwa awe na mapato ghafi yasiyozidi Tsh. Milioni 4 kwa mwaka, awe hajawahi kuandikishwa na kupewa namba ya kitambulisho cha mlipa kodi (TIN), pia, awe anatambulika kama Mfanyabiashara ama mtoa huduma mdogo kupitia ofisi ya Mtendaji wa Mtaa ama Kijiji kwa mujibu wa sheria

“Ninatoa wito kwa Wakuu wote wa Mikoa, Watendaji wote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali kuhusu ugawaji wa vitambulisho vya Wafanyabiashara na watoa huduma wadogo.”amesema Waitara

Hata hivyo, ameongeza kuwa vitambulisho 1,176,305 vimegawiwa kwa Wafanyabiashara na watoa huduma wadogo na tayari Tsh. Bilioni 23.5 zimeshakusanywa.

Harusi Tunayo! Rayvanny´s Baby Mama Drops Hint of their Wedding Date


Bongo sensation, Rayvanny´s longtime lover, Fahyma has hinted their wedding is set for July the 7th, 2019.


Up on her status update, the baby mama put a photo of the two, and a wedding gown alongside captioning:
 Save the date 7/7/2019

Seems Sunday the 7th of July, 2019 is the set date for the fashion model to walk down the isle and exchange vows with lover, Rayvanny.

A white wedding gown, a couple holding hands and a date to be spared.

What else would the African baby be hinting on?

History
It has been a year and a half since the duo welcomed their baby boy and another is on the way.

The two graced the dating scene without even officiating it.


Like every other celebrity love life, both have faced cheating allegations before re-merging and are now announcing their wedding date.

We do wish them well!



Nyota Zenu Leo Jumamosi 01 Jun 2019

NYOTA ZENU LEO JUMAMOSI 1/JUNI/ 2019

MAPACHA (  May 21- Juni 20)
Tumia siku ya leo kufanya mambo yako mwenyewe yale yote ambayo unayaona ni ya muhimu. Jitahidi kujenga umoja wako na wa familia yako.

KAA ( Juni 21- Julai 22)
Leo fikiria kuhusu maisha yako, yaweke kando mambo ambayo unayaona hayana maana maisha yako ni bora zaidi  kuliko jambo lolote jingine linalokukabili.

SIMBA (Julai 22-Agosti 22)
Kuwa makini kwa siku Siku mbili za weekend, Utakutana na  jamaa ambaye atakuhitajia sana umsaidie katika jambo la muhimu. Mpe anachohitaji kwa sababu na wewe utapata.

MASHUKE  (Agosti 23-Sep 23)
Leo una uwezo wa kufanya jambo lolote unalotaka kulifanya na hutopata pingamizi zozote. Ni siku nzuri ya kujumuika na watu na kuwasaidia watakaohitaji msaada wako

MIZANI  ( Sep 23-Oktoba 23)
Jitahidi kukamilisha  mambo  uliyowaahidi watu wako.. Kama ikiwa ni vigumu kwako kutimiza ahadi basi waome wasubiri lakini kamwe usiache

NGE (Oktoba 23-Nov  22)
Leo Kuna mambo muhimu ya kwako na ya watu wengine ambayolazima uyafanye ila tumia  busara. utapata msaada wa watu wengine.

MSHALE (Nov 22- Desemba 21)
Kaa na mtu wako wa karibu na unayemuamiani  mzungumze yaliyo moyoni kwako ili ipatikane suluhisho. utapata majawabu kwa matatizo yanayokukabili.

MBUZI ( Desemba 21- Jan 20)
Fanya kila njia usiwe mpweke. Kuwa  karibu na jamaa zako wape fikra zako na wasihi wakupe ushauri kutokana na changamoto  zinazokukabili.utafanikiwa

NDOO ( Jan 20- February 19)
Leo Jishughulishe na mambo mengi siyo jambo moja matatizo uliyonayo hivi sasa ni makubwa. jambo la muhimu kwako ni kuwa makini

SAMAKI ( February 20- March 20)
Leo Shirikiana na watu kwa sababu unaweza kupata maarifa ya kufanikisha mambo muhimu ila kuwa macho waongo ni wengi na wanafikiria namna ya kukudanganya

PUNDA ( March 20-April 20)
Leo itakuwa siku ya bahati mipango yako itakwenda kama unavyotarajia, Hali ya kukwama kwako ni ya muda tu baadae mambo yatakuwa mazuri.

NGOMBE( April 21- May 20)
Leo Usiwe na na hasira na usikasirike  hovyo bila  ya kuchokozwa na mtu yoyote. jizuie kushiriki katika magomvi na yoyote. Ni afadhali uonekane mjinga hasira hasara. 

                                              SHEIKHE ISAYA ANAWASHUKURU MWENYE Mungu kwa kumpa karama na uwezo wa kufundisha na kuwaombea dua viumbe wake. na anawashukuru wote mliorudi kutowa shukrani kwake. wengine mlioko nje ya nchi. shekhe isaya anatabiri nyota. kuondoa nussi mikosi. kutoa majini wabaya. kutafsiri ndoto. kumvuta na kumrundisha mmeo ama mkeo. kupata kazi. kupata cheo. kushinda kesi. kufaulu masomo nk na kama unaitaji kufatiria nyota yako kila siku. ingia katika pager yetu ya>>> Facebook >>tumaini tiba asili << au fika ofisini magomeni msikiti wa kiyungi simu au whatsapp +2557454951

www.tumainitibaasili.co.tz

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya June 1




TANGAZO: TATIZO LA KUTOKUONEKANA KWA PICHA LIMEKWISHA RASMI


Tunaomba radhi kwa tatizo la kuto kuonekana kwa picha kwa Baadhi ya watumiaji wetu wa App ya Muungwana Blog.

Tunapenda kuwataarifu kuwa tatizo hilo limekwisha Rasmi, kama bado unatatizo hilo basi ingia PLAY STORE kisha andika MUUNGWANA BLOG kisha UPDATE App yetu.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza katika kipindi hiki chote.

Kwa Maoni au maswali wasiliana nasisi kupitia namba hizi 0719788949 - 0789547574




MAGAZETI YA LEO 1/6/2019





























Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...