Search This Blog

Sunday, June 30, 2019

Hivi ndivyo Okwi anavyoisumbua Simba


Mshambuliaji wa Simba na timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi ameendelea kuuwasha moto katika michuano ya mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Misri.


Okwi ambaye alimaliza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita kwa mabao 16, amekuwa msaada mkubwa katika kikosi cha Uganda 'Cranes' ambacho kimefanikiwa kushinda mechi moja na kutoa sare moja katika michuano ya AFCON, huku mwenyewe akifunga mabao 2 mpaka sasa.

Hali hiyo imezidi kuwatamanisha mabosi wa Simba ambao wanamuhitaji mchezaji huyo katika msimu ujao wa ligi, ambapo mpaka sasa wanahangaika kupata saini yake, huku mkataba wake ukiwa ukingoni kumalizika ndani ya Msimbazi.

Inaelezwa kuwa tayari mabosi wa Simba wametua nchini Misri ili kumalizana na mchezaji huyo, ambapo mwenyewe amekuwa akisita kuweka wazi endapo ataendelea kubakia Msimbazi msimu ujao au ataondoka, akisisitiza kuwa hawezi kusema chochote hivi sasa michuano ikiwa inaendelea.

Simba imewasainisha mikataba mipya wachezaji wengi waliokuwa nao msimu uliopita wakiwemo, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Shomari Kapombe, John Bocco, Mohamed Hussein na Jonas Mkude, huku kikwazo kikubwa kikiwa ni kwa Okwi ambaye bado hajaridhia kumwaga wino katika klabu hiyo.

Usiku wa leo majira ya saa 5:00, Uganda itaingia dimbani kuvaana na wenyeji Misri katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano hiyo. Endapo Uganda itapata ushindi au sare yoyote katika mchezo huo itakuwa imejihakikishia kufuzu hatua inayofuata ya 16 bora.

'Tundu Lissu Amevuliwa ili Asigombee Urais' - Mashinji


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimedai kuwa hatua ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge na kuzuiliwa kugombea Ubunge kwa miaka 5 inalenga kumzuia kutowania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2020.


Kauli hiyo ya CHADEMA imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha hicho, DR Vincent Mashinji wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya maamuzi ya Spika kumvua Ubunge Tundu Lissu kwa kushindwa kuhudhuria Bungeni.

"Kuna ibara inamfunga Lissu kugombea ndani ya miaka mitano, na inambana hawezi kugombea Urais wa Tanzania kama hana sifa za kugombea Ubunge Tanzania, naomba tutafakari tukiwa tumebakiza mwaka mmoja kwenda Uchaguzi Mkuu 2020", amesema Mashinji.

"Muda wote ambao Spika anadai Lissu hajui alipo, Bunge limekuwa likimlipa mshahara, hili jambo si la kawaida, na watanzania wote wanajua Mama Samia Suluhu alikwenda kumsalimia Lissu Nairobi, na alienda kumpatia salamu za pole kutoka kwa Rais.", ameongeza Mashinji.

Mapema Ijumaa ya wiki iliyopita, Spika Job Ndugai alitangaza kumvua Ubunge Tundu Lissu kwa kile alichokidai kiongozi huyo kuwa na mahudhurio hafifu ndani ya Bunge.

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo (AQRB) Yawajengea Uwezo Waandishi wa Habari.

MONDULI MAASAI MARATHON YANOGA

MWANARIADHA Magdalena Shauri akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon yaliyofanyika juzi wilayani hapo.(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
MWANARIADHA Marco Joseph akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon yaliyofanyika juzi wilayani hapo.
MWANARIADHA Asha Samwe akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya pili yaliyofanyika juzi wilayani hapo.
MWANARIADHA Josephat Joshua akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya pili yaliyofanyika juzi wilayani hapo
MWANARIADHA Mayselina Mbua akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya tatu yaliyofanyika juzi wilayani hapo
MWANARIADHA Fabiano Joseph akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya tatu yaliyofanyika juzi wilayani hapo
Mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu akizungumza katika mashindano hayo mara baada ya kukabidhi zawadi washindi walioongoza katika mashindano ya riadha 
Mmoja wa waandaaji wa Monduli Maasai Marathon Meja Humphrey Nyuchi ambaye ni mkurugenzi mwenza alisema lengo hasa za mbio hizo kuimarisha michezo ,elimu na afya na mbio hizo zililenga katika kutangaza vivutio na fursa zilizopo Monduli.
Kikundi cha ngoma kabila maarufu la kimaasai kikitoa burudani katika mashindano hayo,
Mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba akitoa zawadi shilingi elfu ishirini kwa mama aliyeshiriki mashindano hayo ya riadha huku akiwasii wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki michezo
Mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba akiwa katika picha ya pamoja na watoto walioshiriki mashindano hayo,amabapo alidhamini Zawadi za watoto zenye thamani ya shilingi laki tatu
Kikundi cha Arusha runners wakishangilia zawadi ya mbuzi (2)walizokabidhiwa mara baada ya kutajwa kuwa wahamasishaji wa zuri wa shindano hilo



Na PamelaMollel,Monduli

Mashindano ya riadha maarufu kwa jina la Monduli Maasai Maradhon imekuwa kivutio kikubwa kwa wananachi waliojitokeza kuangalia shindano hilo lililowashirikisha wadau mbalimbali 

Mashindano hayo ya riadha yaliyofanyika juzi yanatajwa kuwa mashindano ya kwanza kufanyika Monduli na kufanya washiriki mbalimbali walioshinda kujinyakulia zawadi 

Wanariadha Marco Joseph na Magdalena Shauri wamefanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon 

Kwa wanaume waliokimbia kilomita 21 Joseph Kutoka talenti alitumia Muda wa saa 1:19:27 akifuatiwa na Josephat Joshua Kutoka Polisi kwa muda wa 1:05:54 huku nafasi ya tatu akishilia Fabiano Joseph kutoka JWTZ kwa muda wa saa 1:06:13.

Kwa wanawake Magdalena Shauri aliongoza kwa muda wa saa 1:19:27 akifuatiwa na Asha Samwe kwa muda wa saa 1:20:16 huku nafasi ya tatu ikimwendea Mayselina Mbua kwa muda wa 1:20:32.

Zaidi ya wanariadha 200 walishiriki mbio hizo za km 21,km 5 na km 2.5 ambazo ziliongozwa na mkuu wa wilaya Monduli Idd Kimanta ambapo washindi walikabidhiwa Zawadi za fedha na medali na tishirt.

Washindi kwa kilomita 21 kwa wanaume na wanawake ,Mshindi wa kwanza Alipata shilingi laki 500,000 na ,mshindi wa pili 300,000 na Mshindi wa tatu 200,000, Mshindi wa nne 150,000 na Mshindi wa Tano 100,000 pamoja na katoni za vinywaji huku Zawadi za mbuzi mnyama zilitolewa kwa baadhi ya washindi wengine.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu aliwapongeza waandaaji na washiriki,huku akisistiza kuwa michezo ni fursa ya ajira na pia inaimarisha mwili

Alitoa wito kwa wazazi kuwahimiza wototo michezo na badala yake waache kubeza watoto wanaofanya vizuri katika michezo.Mmoja wa waandaaji wa Monduli Maasai Marathon Meja Humphrey Nyuchi ambaye ni mkurugenzi mwenza alisema lengo la mashindano hayo kuibua fursa zilizopo katika eneo hilo pamoja na kuimarisha michezo

Alisema ni Mara ya Kwanza mbio hizo zinazinduliwa na matarajio mbio hizo zitakuwa endelevu kwa ila maana ya kuwa zitafanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi Juni .Naye mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba ambaye walidhamini Zawadi za watoto zenye thamani ya shilingi laki tatu alisema kupitia michezo watotonwanaweza kufanya vizuri zaidi

Alisema serikali iweke mkazo zaidi kuwekeza katika michezo kuanzia ngazi za chini ili kuweza kuwa na vijana watakaofanya vizuri baadae na kuliwakilisha taifa vyema.


MKUU WA WILAYA ARUMERU JERRY MURO ANUNUA MBUZI WA KISASA KUFANIKISHA HARAMBEE YA KUNUA VIFAA VYA MUZIKI

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

MKUU  wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amekabidhi mbuzi watatu wa kisasa ambao amewanunua katika mnada wa harambe ya kuchangia ununuaji wa vyombo vya muziki kwa kwaya ya vijana ya Kanisa la AMEC Usharika wa Manyata Halmashauri ya Meru

Muro amenunua mbuzi hao alipokuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo mbali na kuchangia Sh.milioni moja katika harambee   hiyo pia amewanunulia  kina mama wawili wajane mbuzi wa kisasa

 Pia amempatia mtoto mmoja yatima mbuzi kama sehemu ya mbegu aliyopanda katika kuwafariji na hali ya ujane na uyatimawaliokuwa nao

 Aidha Muro amewataka wananchi kutenga muda wa kuwafariji na kuwasaidia watu wasiojiweza katika maisha  kwani kwa kufanya hivyo Mungu atawafungulia milango ya baraka.

"Unajua hata katika vitabu vya dini vinaelezea kusaidia yatima na vinausia kusaidia yatima na ukifanya hivyo utabarikiwa na pia utaongezewa hivyo napenda kuwasihi wananchi kuweni na tabia ya kusaidia, "amesema Muro

Akipokea msaada huo mmoja ya wajane hao alimshukuru  mkuu huyo wa wilaya kwa msaada huo na kueleza kuwa utawasaidia kuendesha maisha kwani watawazalisha na kuuza maziwa.
Picha ya pamoja
Mkuu wa wilaya ya Arumeru akimkabidhi mtoto yatima mbuzi 
Mkuu wa wilaya Jerry Muro akimkabidhi mama mjane Neema Kaaya mbuzi ambae atamsaidia kujikimu .


Chadema Watoa Tamko Tundu Lissu Kuvuliwa Ubunge


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimedai kuwa hatua ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge na kuzuiliwa kugombea Ubunge kwa miaka 5 inalenga kumzuia kutowania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2020.

Kauli hiyo ya CHADEMA imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha hicho, DR Vincent Mashinji wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya maamuzi ya Spika kumvua Ubunge Tundu Lissu kwa kushindwa kuhudhuria Bungeni.

"Kuna ibara inamfunga Lissu kugombea ndani ya miaka mitano, na inambana hawezi kugombea Urais wa Tanzania kama hana sifa za kugombea Ubunge Tanzania, naomba tutafakari tukiwa tumebakiza mwaka mmoja kwenda Uchaguzi Mkuu 2020", amesema Mashinji.

"Muda wote ambao Spika anadai Lissu hajui alipo, Bunge limekuwa likimlipa mshahara, hili jambo si la kawaida, na watanzania wote wanajua Mama Samia Suluhu alikwenda kumsalimia Lissu Nairobi, na alienda kumpatia salamu za pole kutoka kwa Rais.", ameongeza Mashinji.

Mapema Ijumaa ya wiki iliyopita, Spika Job Ndugai alitangaza kumvua Ubunge Tundu Lissu kwa kile alichokidai kiongozi huyo kuwa na mahudhurio hafifu ndani ya Bunge.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu 1 July


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu 1 July


Tetesi: Muda wowote Simba SC kumtangaza Ibrahim Ajibu kama mchezaji wao


Inaripotiwa kuwa kuanzia leo Ibrahim Ajibu Migomba ni mchezaji halali wa Simba SC ambapo mkataba wake na Yanga SC umemalizika rasmi jana.

Taarifa zinaeleza kuwa Simba SC ilikuwa inasubiria kumtangaza mchezaji huyo mara baada ya mkataba wake na Yanga SC kumalizika.




RITA yazitaka bodi za wadhamini kufanya marejesho


Serikali kupitia Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA), imezitaka Bodi mbalimbali za wadhamini kufanya marejesho kwa mujibu wa sheria ya muunganisho wa wadhamini kwa muda sahihi kila mwaka.

Bodi hizo za wadhamini ni pamoja na vyama vya siasa, taasisi mbalimbali zisizo za serikali (NGOs), taasisi za kuabudu zikiwamo makanisa, vilabu vya mpira wa miguu na nyinginezo.

Hayo yamesemwa jana na Wakili wa Serikali  Mwandamizi, Edna Kamara, katika viwanja vya maonesho sabasaba ambapo amesema bodi nyingi zinafanya vizuri lakini zipo ambazo zinasuasua hivyo kuepuka sheria kuchukua mkondo wake wafanye marejesho haraka iwezekanavyo.

“Bodi ya wadhamini inatakiwa kufanya marejesho kila mwaka tarehe husika kwa kujaza fomu namba T.1.5  na kulipia ada ya Sh, 50000 kwa mujibu wa sheria ya muunganisho sura ya 318 toleo 2002 kuepuka kulipa faini.

“Hapa sabasaba huduma hizo zipo zinaendelea kwa wanaoona uvivu kufika katika ofisi za RITA wafike hapa tuwahudumie haraka,” amesema Edna.

Aidha amesema kuwa taasisi za dini zinafanya vizuri kwa kufanya mrejesho zikifuatiwa na vyama vya siasa.

“Vyama vya siasa vipo makini kufanya mirejesho yao hasa wakiongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), faili lao safi kabisa, lakini na vyama vingine wasipofanya hivi nafikiri watabanwa na Tume ya uchaguzi huko kwenye uchaguzi huu unaokaribia,” ameongeza Edna.



RC Ayoub azitaka Mamlaka za bima kusambaza elimu kwa jamii


Na Thabit Hamidu,Zanzibar

Uongozi wa mamlaka ya Bima Tanzania umetakiwa kutoa elimu kwa jamii kukata na kutumia bima kutoka kwa watoa huduma waliosajiliwa na mamlaka husika ili kuongeza pato la taifa pamoja na kudibiti watu waoghushi huduma hiyo.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud ametoa wito huo wakati akiungungumza na viongozi ,wadau na wananchi katika maadhimisho ya siku ya bima Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya kumbukumbu kisonge mjini unguja.

Alisema endapo makampuni na wataalamu wa bima watakuwa na utamaduni wa kutoa elimu ya mara kwa mara wananchi watapata uelewa juu ya umuhimu wa huduma Bima na  hawatasita kununua huduma hiyo.

"Kwa sababu mamlaka ya bima ni chombo cha ushauri kwa serikali kuhusu masuala ya soko la bima,ni matumaini yangu wananchi sasa watanunua huduma za bima,na endapo kutatokea migogoro au kutoelewana kati ya kampuni ya bima na mteja ninauhakika mamlaka yenu itakuwa tayari kulitatua na kulipatia ufumbuzi"alisema Ayoub.

Aidha Mkuu wa Mkoa amesema serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi inathamini jitihada  za mamlaka za Bima na wadau wake katika kuendeleza maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwasogezea wananchi huduma za bima kupitia makampuni,madalali,mawakala na wakadiria hasara wanaosajiliwa na mamlaka hiyo.

"Kulingana na ripoti ya mwenendo wa soko la bima nchini ni dhahiri kwamba juhudi za mamalaka pamoja na wadau wote wa bima zinazaa matunda kwa ongezeko la ukuwaji wa kiwango cha asilimia 7% kwa sekta ya bima inaonesha wazi kwa kushirikiana na wadau, Mamlaka inafanya kazi kwa bidii kwa lengo la kukuza soko la bima nchini'amesema Mkuu wa Mkoa.

Katika hatua nyengine Mhe Ayoub amezitaka taasisi za serikali kuwa mstari wa mbele kuvikatia bima vyombo vyao ili kuenda samabamba na mabadiliko ya sheria na maelekezo ya serikali juu ya matumizi ya bima kwa  chombo mbali mbali.

Akizungumza katika maadhimisho hayo kamishna wa Mamlaka ya Bima Tanzania Ndugu Mussa Juma amesema kuwa kila mwananchi ana haki ya kupata fidia endapo atapata ajali za barabarani zitokanazo na vyombo vya moto ambapo lengo la maadhimisho hayo ni kutoa elimu ya bima kwa jamii na kuwapa miongozo ya kupata haki zao za bima pale watakapopatwa na ajali.

Alisema  mamala ya Bima imekuwa na mikakati mbali mbali ili kuhakikisha inaonmgeza wateja kwa kutumia sekta za kibenki zitakazotoa huduma za upatikanaji wa bima kwa gharama nafuuu pamoja pamoja na kuzitaka kampuni zinazoingiza bidhaa chini kukata bima hapa Tanzania na si nje ya nchi kama ilivyokuwa zamani.

"Sasa hivi tumekuwa na utaratibu wa kuziagiza kampuni mbali mbali zinazoagiza bidhaa zao nje ya nchi kukata bima hapa nchini kwetu kwa mujibu wa sheria zilizopo na sio kule wanakoagiza biashara zao kama ilivyokuwa zamani" alisema ndugu Juma.

Aidha Kamishna Juma ameongeza kuwa maamlaka hiyo imekuwa na utaratibu wa kusaidia na kuchangia katika huma za kijamii ikiwemo afya ,elimu na watu wenye mahitaji maalumu kwa kutoa msaada wa mahitaji na vifaa mbali mbali kwa watu wenye mahitji maalum.

Mapema Naibu kamishna wa mamlaka ya usimamia wa Bima Tanzania Bi Khadija Issa Said amesema wamekuwa na mikakati mbali mbali ya kuhakikisha wanayafikia maeneo tofauti kutoa elimu kwa jamii na kuona wanapata uelewa wa kutosha na kuzitumia fursa zinazopatikana katika mamlaka zao.

"Nikiri zamani wananchi walikuwa na uelewa mdogo kuhusu bima kwani walijua bima ni kwa ajili ya vyombo vya moto tu kama gari lakini kutokana na mikakati yetu ya elimu tunayoitoa kwa makundi mbali mbali watu wengi wanafika katika mamlaka zetu kuleta malalamiko yao na tunawasaidia na wananpata haki zao"alisema Bi Khadija.

Katika maadhimisho hayo ya siku ya Bima Zanzibar Mkuu wa Mkoa aliongoza matembezi yaliyoanzia katika viwanja vya BAJA na kumalizia uwanja wa kumbukumbu vya muembe kisonge pamoja na kukagua shughuli za mawakala wa bima.

Watu 228 wafariki Australia kwa homa


Takribani watu 228 wameripotiwa kufariki nchini Australia kutokana na homa ya mafua huku wengine 100,000 wakiuguza virusi hivyo, idadi kubwa ikilinganishwa na mwaka wa 2018 ambapo vifo 58,824 viliripotiwa.

Mkuu wa afya nchini humo amesema virusi hivyo vimeendelea kusambaa licha ya chanjo iliyotolewa kwa zaidi ya watu milioni 11 na kuongeza kuwa taifa hilo linapitia wakati mgumu kutokana na msimu wa baridi na wanatarajia hali hiyo kuboreka kati ya mwezi wa Julai na Septemba.

Waziri Bashungwa awajia juu wanaobeza ubora wa Korosho


Waziri wa Viwanda na Biashara ,Innocent Bashungwa amekemea baadhi ya Watanzania wanaopotosha  na kukandia kuwa korosho ya Tanzania iliyopo kwenye maghala ,haina ubora ambapo amewapasha kuacha propaganda zisizo na tija kwa Taifa.

Aidha ameielekeza DAWASA na TANESCO kukimbilia fursa ya kutoa huduma ya maji na umeme kwa wawekezaji pasipo kuwakwamisha huduma hizi ili wazalishe zaidi na serikali ipate mapato makubwa.

Akitembelea kiwanda cha korosho Terra cashew kilichopo ,Tanita wilayani Kibaha mkoani Pwani, Bashungwa alieleza watu hao hawalitakii mema Taifa.

Aliweka bayana kwamba, tayari kwa sasa kuna korosho ya kutosha na yenye ubora katika maghala 37 nchini .

“Nchi yetu inategemea zao hili la kibiashara wakitokea watu wapotoshaji inakuwa haileti maana na kushusha sifa ya nchi katika biashara ya zao hilo”.

“Nilitembelea maghala hayo na wataalamu wangu, tumejiridhisha ,korosho yetu ni nzuri kwa grade ya I na ya II na ipo katika thamani”alisisitiza Bashungwa.

Akizungumzia suala la ubanguaji korosho ,Bashungwa alibainisha ,watu wanapata ajira katika ubanguaji na kukuza pato la Taifa,kuelekea katika uchumi wa kati.

Alisisitiza ubanguaji wa viwango na ubora kwa wakati ili kuwa na korosho yenye ubora.
Wakati huo huo ,Bashungwa alitembelea kiwanda cha KEDS ambacho kinazalisha soft care (pempas) na sabuni za unga na kutajiwa changamoto ya upungufu wa umeme na maji ya uhakika.

“Endapo wakibaniwa huduma hizi uzalishaji unapungua tuvutie wawekezaji,hii ni biashara sio kama tunawapa msaaada mjue kama hawa hawazalishi basi na serikali inakosa mapato”.

Nae mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka alisema, mpango uliowekwa na serikali kwenye maghala na kuhakikisha wakulima hawapunjwi ni mpango mzuri kwa maslahi ya wakulima na Taifa.

Koka alieleza ,hao wanaopotosha juu ya korosho iliyopo kwenye maghala zimeoza na kuharibika wapuuzwe.

Awali Ofisa Utawala wa Terra Cashew ,Peter Christopher alitaja changamoto zinazowakabili ni ucheleweshaji wa kutolewa makontena ya mitambo na vipuri bandarini kwa takriban miezi mitatu  na zaidi.

Pia tatizo likiwa kupewa taarifa zisizo kamilika mara kwa mara kuhusu nyaraka wanazozihitaji .
Peter alisema kwa sasa kiwanda hicho kina ajira rasmi 120 na ajira zisizo rasmi 300.

Simba SC wapatwa na msiba


Uongozi wa Simba SC umeeleza kuguswa na kifo cha Mwenyekiti wa Tawi la Simba Damu Fans (SDF), Alfred Kehongo.



Walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi kukuza ufaulu nchini


Walimu wa masomo ya  Hisabati  na Sayansi nchini wametajwa kuwa chachu ya kuendelea kukuza kiwango cha ufaulu katika masomo hayo na hivyo kuchochea ujenzi wa dhana ya uchumi wa viwanda.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa mwaka wa chama cha walimu wa Hisabati na Sayansi   Jijini Dodoma Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera Uratibu na Uwekezaji) Bi Dorothy Mwaluko amesema kuwa walimu wa masomo hayo wamekuwa wakifanya kazi kubwa yakuwaandaa vyema wanafunzi wanaochukua michepuo ya sayansi na hivyo kuchochea ufaulu kuongezeka.

“ Nawapongeza na kuwataka muongeze juhudi katika kuhakikisha kuwa tunasaidia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda kwani unategekea wataalamu wa Hisabati na Sayansi ili azma hii ya Serikali ya Awamu ya Tano iweze kutimia kwa wakati” Alisisitiza Bi Mwaluko.

Akifafanua amesema kuwa walimu wa masomo hayo wamekuwa wakijitoa kwa dhati kutekeleza majukumu yao ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kupenda masomo ya Sayansi na Hisabati na hatimaye kukuza kiwango cha ufaulu.

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mkutano huo ambaye pia ni mwanachama wa chama cha walimu wa Hisabati na Sayansi Bi Masika Lazaro amesema kuwa changamoto kubwa kwa walimu hao ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi wanayapenda na wanaongeza jitihada katika kujifunza.

Aliongeza kuwa kama chama wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali za kuwawezesha wanafunzi kujifunza na kupenda masomo hayo hali inayoongeza ufaulu .

Chama cha walimu wa Hisabati na Sayansi kimekuwa na manufaa makubwa kwa walimu wa masomo hayo kwa kuendesha mafunzo yakuwajengea uwezo zaidi wanachama wake kote nchini ili kukuza masomo hayo.

Mkutano wa chama cha  Walimu wa Hisabati na Sayansi umefanyika Jijini Dodoma ukiwa ni mkutano wa kwanza wa chama hicho tangu kilipoanzishwa kikiwa na dhamira ya kukuza na kuendeleza masomo hayo hapa nchini ili kutoa mchango unaostahili katika uchumi.

Serikali yashirikiana na Kampuni za simu kusaidia watoto na Wanawake


Serikali imesema itaendelea kushirikiana na kampuni za simu ili kuwasaidia wananchi katika mambo mbalimbali ya kijamii yakiwemo ya Afya, Elimu  na Miundombinu.

Akizungumza  katika hafla ya uzinduzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Naibu  Waziri wa  Tamisemi,  Joseph Kandege amesema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ili kuwawezesha Vodacom kuwafikia watanzania wote wenye mahitaji .

 Waziri kandege Amesema Vodacom wanafanya kazi ambazo zinagusa jamii kama afya   na kuwasaidia watoto wa kike kwenda shule kwa kuwapatia vitaulo vya kujihifadhia katika hedhi, pia wameendelea kuwasaidia kina mama juu ya ugonjwa wa fistula ambayo inawapelekea wamama wengi kutengwa na jamii.

“ Serikali itahakikisha inaimarisha miundombinu ili kuhakikisha vodacom inawafikia  watu wenye uhitaji na pia tumeona jinsi walivyoweza kuwasaidia watoto wa kike na wakinamama wenye fistula juu ya kupata matibabu  ya ugonjwa huo na kugawa vitaulo kwa watoto wa kike wenye uhitaji, ambao wanakosa kwenda shuleni pindi wawapo kwenye hedhi”.

Amesema matarajio yake ni kuwa  kazi inayofanywa na vodacom  iweze kufanywa na mashirika mengine kwa kushiriki jambo kama hilo au kwa kujiunga pamoja na vodacom kufanya jambo hilo.

“ Matarajio yangu kazi hii inayofanywa na Vodacom isiwe yao na  hayo mashirika wanayoshirikiana nayo, kwani hili ni jambo la kitaifa, hivyo ni vyema mashirika mengine hata ya watu binafsi wakaendeleza juu ya hili, au wakaanzisha mambo kama haya ilikuweza kusaidia jamii zenye uhitaji kwa ujumla” .

Aidha  Mkuurugenzi wa  Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation  na Afisa Uhusiano,   Rosalynn Mwaria  amesema wamekuja kuonyesha matokeo chanya ya kazi walizokuwa wakizifanya kuanzia mwaka 2014 hadi 2017, wakiambatana na sekta binafsi pamoja serikali kwa kuwasaidia watoto na kinamama kwenye mambo mbalimbali .

Amesema hadi kufikia hapa wameshawekeza sh bilioni 11 ambazo zimewawezesha kufikia wanawake  kwa upande mkubwa  na kwa watoto wa kike kwenye sekta ya  Elimu , Afya na pia kuwawezesha kiuchumi katika mambo tofauti ili kuiendeleza Tanzania na  kuifikia jamii.

Kwa mwaka 2019 hadi 2021, Mkurugenzi huyo amesema wamejikita  katika miradi ya  watoto katika  Elimu  na pia kufanya maendeleo ambayo yatawasaidia kutunza mazingira ya Tanzania nzima.

DIT YASEMA MAGARI 217 NCHINI YAFUNGWA MFUMO WA KUTUMIA GESI ASILIA, YATAJA FAIDA ZAKE

Na Said Mwishehe, wa Michuzi TV

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam DIT imesema imeshafunga mfumo wa Gesi asilia katika magari 217 yakiwamo UBER huku akielezea faida lukuki zinazopatikana kwa kutumia gesi hiyo.

Pia DIT imesema iko haja kwa vijana wakitanzania kwenda kujifunza kuhusu namna yakufunga mfumo wa gesi asili nakufanya sevisi kwenye magari hayo kwa lengo la kuhakikisha Tecknolojia hiyo inasambaa katika maeneo mbalimbali nchini na hasa inayopayopatikana gesi kwa wingi.

Akizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam leo Mhandisi Bosinge ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi wa taasisi hiyo ametumia nafasi hiyo kueleza baadhi ya faida kwa magari yaliyofungwa gesi asilia.

Mhandisi Bosinge ambaye ndio msimamizi wa karakana ya kufunga mfumo wa gesi asilia kwenye magari katika taasisi hiyo amesema wameaza kufunga mfumo huo mwaka 2008 na hadi sasa wameshafunga magari 2017 na siku chache zijazo wanatarajia kufunga magari 250 kwani muamko umekuwa mkubwa.

Akizungumzia faida zinazopatikana kupitia mfumo huo Mhandisi Bosinge amewaambia wananchi waliokuwa wamejitokeza kwa wingi katika Banda la DIT kuangalia mfumo huo ambao umekuwa kivutio amesema faida ya kwanza ni gesi asilia ni mali ya watanzania hivyo badala ya kuagiza kutoka nje inapatikana hapa nchini.

Pia amesema matumizi ya endeshaji wa gari mfano yenye cc 2000 unaweza kutumia kilo moja ni Sh.1500 na tunaweza kwenda kilometa 20 mpaka 25 lakini kwa lita moja ya petrol ambayo gharama yake ni 2300 na kwa gari yenye cc 2000 inaweza kwenda kilometa nane na mpaka tisa na hivyo unaweza kuona tofauti ya gharama.

"Ndugu wanahabari kwa mfano gari yenye cc chini ya 1500 ,mtungi wake wa gesi unaulizwaa Sh.19500 ambayo utachukua kilio 13 na unaweza kutembea kilometa 270 ni tofauti na hiyo 19500 ukijaza petrol unatembea sio zaidi ya kilometa 90." Amesema mhandisi Bosinge

Ameongeza kuwa kwa mazingira hayo tunaona namna ambavyo unapunguza gharama kubwa ,na kufafanua kuwa hivi sasa wanauona huduma za usafiri jijini Dar es Salaam kama UBER wengi walikuwa wanatumia hadi Sh.60,000 kea siku kufanya mzunguko wao lakini baada ya kuwafungia gesi asili wanatumia wanatambua zaidi ya kilometa 270 kwa gharama ya msingi mdogo wenye thamani ya sh. 13500 tena kwa siku nzima badala ya 60,000.

Kuangalia hapo tunaona kuna akiba ya Sh.40000 ambayo hiyo inamuwezesha kuitumia katika mahitaji mengine na hivyo kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Mhandisi Bosinge amesema faida ya tatu ni kwenye jijini kwani unapotumia petrol kuna kitu kinaitwa Salfa na Lead na hivyo kusabisha injini kuchoka kwani mafuta yanakuwa yanaganda sana ,hivyo kusabisha injini kuchoka na kufanya sevisi kila baada ya kilometa 3000 lakini ukitumia gesi unaweza kufanya sevisi baada ya kutembea kwa zaidi ya kilometa 9000.

Pia amesema Kwa mazingira inasaidia sana kwani gesi asilia ni rafiki wa mazingira tofauti na kutumia katika magari na kufafanua dunia inapambana kuondoa ozoni leya.

Akizungumzia kuhusu muamko amesema mhandisi Bosinge amesema kimsingi kama Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam wameanza kufunga magari tangu mwaka 2008 na mwanzoni wakipata changamoto kwenye muamko lakini siku za karibuni muamko umekuwa ukingezeka na wananchi wameanza kuelekea.mwanzoni walikuwa wanaogopa kea kudhani gesi italipuka ndani ya magari lakini waliamua kutoa elimu kueleza tofauti wa gesi asili inayotumika kwenye magari na ile ya majumbani LPD.

Amefafanua kuwa gesi hiyo ambayo inatumika kwenye magari ni NCAG ambayo inachimbwa na haina tabia ya kulipuka na kwamba anaendelea kutoa elimu kueleza kuhusu gesi hiyo na ndio maana hivi sasa wameshafunga magari 217 na wanaamini hadi wiki ijayo wanaweza kufunga magari 250.

Kuhusu mwito wake kwa wanaotumia vyombo vya usafiri wa moto yakiwemo magari, mhandisi Bosinge amesema pamoja na faida zote anaamini kwa wananchi hasa wanaoishi Dar es Salaam kupitia maonesho yanayoendelea viwanja vya 77 jijini Dar es Salaam waone umuhimu na faida ya kutumia gesi asilia kwa kuyapeleka magari yao DIT ili kufunguliwa gesi.

Kuhusu gharama za kufunga gesi asilia kwenye magari Mhandisi Bosinge amesema kwa kuanzia CC 0 hadi CC 2000 ni Sh.milioni 1.8 na magari kuanzia CC 2700 mpaka cc 4000 ni Sh.milioni 2.5 na sio zaidi ya hapo na kwamba nimejipanga kupeleka teknolojia hiyo kwa vijana ili waweze kusambaa nchi nzima hasa mikoa yenye ili kuweza kufunga teknolojia hiyo.

"Tumejipanga kufundisha kozi mfupi fupi ambazo DIT inatoa kwa ajili ya kuwaelimisha vijana ikiwa pamoja na kuyafanyia sevisi magari yanayotumia gesi asilia na kufunga mfumo huo." Amesema Mhandisi Bosinge

Amewakaribisha vijana na watu walio tayari sasa kutoka kupata elimu ya kufunga huo mfumo na kisha wakafungue karakana zao.
 Msimamizi wa Karakana ya kufunga magari mfumo gesi asilia katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) Mhandisi Geturu Bosinge akielezea mfumo wa gesi asilia unavyofanya kazi .Gari hiyo iliyofungwa gesi asilia ipo kwenye banda la DIT katika Maonesho ya Biashara Sabasaba yanayoendea jijini.
 Baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la DIT wakipata maelezo kuhusu faida zinazopatikana kwenye magari ambayo wamefungwa mfumo wa kutumia gesi asilia
 Mmoja ya watalaam wa DIT akionesha mtungi wa gesi asilia ambao umefungwa kwenye gari  ndogo iliyopo Banda la DIT katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Gari inayotumika gesi asilia ikiwa imeegeshwa kwenye banda la DIT lililopo katika viwanja vya Sabasaba ambako yanafanyika maonesho ya biashara ambayo yameanza Juni 28,2019
 Baadhi ya wananchi wakiangalia maelezo ya gharama ambazo zinatumika kwa waliofunga mfumo wa gesi asili na zile ambazo zinatumika mafuta ya petrol
Mhandisi Geturu Bosinge wa DIT  akifafanua namna ambavyo mfumo wa gesi asilia unavyofanya kazi


Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...