Search This Blog
Monday, September 30, 2019
Rais Magufuli afanya teuzi mbalimbali
Rais John Magufuli amefanya teuzi mbalimbali za Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) na Uhamisho wa Wakurugenzi wa Halmashauri.
Madiwani Tanzania waagizwa kutoa Majina ya Mitaa
Serikali imewataka madiwani wote nchi nzima kutoa majina ya mitaa ili kufanikisha utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akifungua mafunzo ya kujenga uelewa kuhusu umuhimu na manufaa ya kutekeleza mpango wa anwani za makazi na postikodi kwa madiwani, viongozi wa Serikali na watendaji mbali mbali wa Mkoa wa Kigoma yaliyofanyika wilayani Kibondo yaliyotolewa na wataalamu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
“Madiwani tupeni majina ya mitaa ili vifurushi, barua na vipeto viwe vinakwenda moja kwa moja kwa wananchi, tufanye biashara mtandao na kuimarisha ulinzi na usalama,” amesema Nditiye
Ameongeza kuwa biashara mtandao ni nzuri, tunataka kifurushi cha mtu kiletwe anapoishi na tayari nchi nzima kata zote zina postikodi, madiwani tupeni majina ya mitaa ili tuweke vibao na namba za nyumba ili wananchi watambulike
“Unaweza kupata postikodi ya kata au wadi yako kupitia simu yako ya mkononi kwa kupiga *152*00# kisha chagua 3 (ajira na utambuzi), 3 (TCRA – Postcode) endelea kufuata maelekezo hadi kupata postikodi ya kata yako”, amesema Nditiye
Amefafanua kuwa utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi nchi nzima unalenga kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na anwani yake ya mahali alipo iwe mahali pa kazi, nyumbani au ofisini ili kuwezesha mwananchi kuhudumiwa kwa urahisi.
Ametoa rai kwa madiwani wote nchi nzima kutoa majina ya mitaa ili Wizara iweze kuweka nguzo zenye majina ya barabara na namba za nyumba au majengo katika maeneo yao kwa kuwa tayari kata zote nchi nzima zina postikodi
Ameeleza kuwa kuna maneno yamezoeleka kuwa Dunia ni kama Kijiji, ili dunia iweze kuwa kijiji kunategemea uwepo wa mfumo wa utambuzi wa makazi na wakazi kwa ajili ya kurahisisha utoaji na ufikishaji wa huduma kwa wananchi ambapo anwani za makazi na postikodi zinawezesha utambuzi husika na nchi zilizoendelea zilishafika hatua hii na zinaendelea kunufaika na matunda ya utambuzi husika kijamii na kiuchumi
Naye Mkuu wa Kanda ya Kati wa TCRA, Antonio Manyanda wakati akitoa mafunzo hayo amesema kuwa mpango wa anwani za makazi na postikodi utaongeza ajira kutokana na fursa za kusambaza bidhaa za wateja katika maeneo yao na mahali walipo; kurahisisha biashara mtandao hivyo kukuza uchumi; kuongeza mapato ya Serikali kwa kuwa mamlaka zinazohusika na ukusanyaji wa mapato zitakuwa na taarifa ya mahali walipo walipa kodi au wananchi hivyo kuwezesha ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi.
Rais Magufuli amteua Mkurugenzi mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
Rais Magufuli amemteua Dkt. Wilson Mahera kuwa Mkurugenzi mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) akichukua nafasi ya Athuman Kihamia ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo Mahera alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Arusha
Walimu wametakiwa kujiendeleza kielimu
Na Thabit Madai, Zanzibar
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Hassan Khatib Hassan amewataka walimu wa Shule za msingi katika Mkoa huo kujiendeleza kielimu ili kuongeza mbinu mbali mbali za ufunishaji nakuongeza ufaulu wanafunzi.
Wito huo ameutoa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya walimu wa shule za msingi ndani ya Mkoa Mjini Magharibi uliofanyika katika ukumbi wa kituo cha walimu Bububu Mjini Unguja.
Mafunzo hayo kwa walimu yameandaliwa na Taasisi ya Rafiki Elimu.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema suala la kujiendeleza kielimu kwa walimu litaongeza kasi ya mabadiliko na ukuwaji wa sekta ya elimu nchini hatua ambayo itaongeza wataalamu wa fani mbalimbali na kuwa na taifa lenye wasomi.
"Kazi hiyo ya ualimu ni kazi ambayo inahitaji mabadiliko hususan katika suala la kuongeza uwezo wa kitaalamu kujiendeleza ni jambo la msingi ili muweze kuwaanda vijana wetu wapende elimu na skuli na wapunguze mda wa kubaki nyumbani".
Aidha Hassan alisema Serikali ya Mkoa huo itaendelea kusimamia kwa karibu maendeleo ya sekta ya elimu Mkoani humo ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya matokeo mazuri kwa wanafunzi wa ngazi zote.
"Suala la kuimarika kwa elimu katika nchi hii ni jambo la kipao mbele hata Mheshimiwa Rais suala la Afya na Elimu ni vitu ambavyo anavitilia mkazo sasa pamoja na hatua zilizofikiwa za kuimarikakwa elimu basi na mimi nitaongeza kasi," Alisema Hassan.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa alisema serikali ya Mapinduzi kupitia wizara ya elimu imekuwa ikiimarisha maendeleo ya sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya madarasa na vifaa vya kufundishia.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi Rafiki Elimu Hussen Hassan alisema Taasisi yao imekuwa ikijishuhulisha zaidi katika suala la elimu nchini ikiwemo utoaji wa mafunzo kwa walimu pamoja na ukarabati wa ujenzi wa madarasa ambapo madarsa 29 wamejenga na 30 wamekarabati katika Mkoa Mjini Magharibi.
"Taasisi yetu imesajiliwa kisheria na tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi pamoja na Wizara ya elimu katika kusaidia sekta ya elimu nchini," alisema Mkurugenzi Hassan.
Mafunzo hayo yana lengo lakuwajengea uwezo walimu hao shule zote za msingi katika Mkoa wa Mjini Unguja.
Kigogo CUF atimkia CCM
Mwanachama Mkongwe wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Singo Kata ya Gongoni katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Hamisi Mwami (53) amekihama chama hicho na kujiunga CCM.
Mwami ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo kwa miaka 20 sasa amesema kuwa ameamua kuhamia CCM kwa utashi wake mwenyewe baada ya kusoma alama za nyakati na kuridhika na utendaji wa Rais John Magufuli.
“Nimesoma alama za nyakati, upinzani hauna la kusema sasa hivi ndio maana nimeamua kuhamia CCM kwa utashi wangu na sio kwa kununuliwa au kushawishiwa na mtu kwani nina uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika siasa sasa nimekuwa kiongozi wa Serikali hivyo nina upeo wa kuona mbali”, amesema.
Aidha amesema uroho wa madaraka unaokitafuna chama cha CUF na vyama vingine vya upinzani ni miongoni mwa mambo ambayo yamedhoofisha upinzani hapa nchini na hivyo kushindwa kuwa watetezi wa wananchi, ndiyo maana ameamua kujiunga na timu ya watu makini wanaojali sana maslahi ya wananchi.
Mwami amepinga wanaodai kuwa amenunuliwa na CCM akihoji kwa nini hawakudai amenunuliwa na CUF kipindi alipojiunga nao ambapo alisisitiza kuwa aliingia na kuondoka kwa utashi wake na hivi sasa ameamua kuingia CCM kwa utashi wake pasipo kushawishiwa na mtu.
Makamu wa Rais akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark, Ufaranza na Qatar hapa nchini
Naibu Waziri Mabula Ataka Majina Ya Watumishi Wa Ardhi Waliokacha Kwenda Mafia
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza kupatiwa majina ya watumishi saba wa sekta ya ardhi awaliopangiwa kuhamia halmashauri ya wilaya ya Mafia mkoani Pwani lakini wameshindwa kuripoti katika kituo chao kipya cha kazi.
Dkt Mabula alitoa agizo hilo jana mwamzoni mwa ziara yake ya siku mbili katika wilaya ya Mafia mkoani Pwani kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi, kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki, kukagua Masijala ya ardhi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi.
Kauli ya Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inafuatia kuelezwa na Mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma kuwa wilaya yake ina mtumishi mmoja wa sekta ya ardhi jambo linaloifanya wilaya hiyo kushindwa kutekeleza majukumu ya sekta hiyo ipasavyo.
Dkt Mabula alisema, Wizara yake italifanyia kazi suala hilo mapema kwa kuwa ni vigumu wilaya kufanya kazi vizuri katika sekta ya ardhi kwa kutegemea mtumishi mmoja hasa ikizingatiwa sekta hiyo inahitaji kuwa na wapimaji, wathamini pamoja na wataalamu wa mipango miji.
‘’Mafia mna mtumishi mmoja wa sekta ya ardhi? Suala hili inabidi lifanyiwe kazi mapema na wizara yangu italifanyia kazi kuhakikisha wilaya inakuwa na watumishi wa njanja zote katika sekta ya ardhi’’ alisema Dkt Mabula
Awali Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alimueleza Naibu Waziri Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa, changamoto kubwa inayoikabili wilaya yake kwa upande wa sekta ya ardhi ni kukosekana watumishi wa kutosha ambapo wilaya hiyo imekuwa na mtumishi mmoja wa sekta hiyo kwa muda mrefu baada ya mtumishi mmoja wa Uthamini kupangiwa majukumu mengine.
Kwa mujibu wa Nnunduma, jitihada za wilaya yake kufuatilia upatikanaji Watumishi wa sekta ya ardhi zimeonekana kukwama kwa kuwa hadi sasa hawajapata mtumishi mwingine jambo linaloifanya wilaya hiyo kushindwa kutekeleza vyema majukumu ya sekta hiyo.
‘’Watumishi saba walipangiwa kuja Mafia lakini wameshindwa kuripoti na hapa unavyotuona tuna mtumishi mmoja, hatuna wataalamu kama wangekuwepo wangesaidia upangaji. Wilaya ni kama imesimama katika sekta ya ardhi’’ alisema Nnunduma
Nnunduma alisema, ujio wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaweza kuwa faraja kwao kupata watumishi kwa kuwa tangu kuteuliwa kwake na Rais John Pombe Magufuli kuongoza wilaya ya Mafia ndiyo anashuhudia Waziri wa kwanza wa sekta ya ardhi kwenda wilaya hiyo aliyoieleza kuwa kama itatumiwa vizuri basi itaiwezesha serikali kuingiza mapato mengi kupitia sekta ya utalii.
Mbunge wa jimbo la Mafia Mbaraka Dau alimueleza Dkt Mabula kuwa, pamoja na changamoto nyingine lakini Wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa la Baraza la Ardhi la nyumba la wilaya jambo linalowalazimu wananchi kufunga safari hadi katika Baraza la Mkuranga kitu alichokieleza kinawafanya baadhi ya wananchi kushindwa kwenda na hivyo kupoteza haki zao.
Waziri Jafo Awataka Wakuu Wa Shule Kutojihusisha Na Udanganyifu Wa Mitihani.
Na Faustine Gimu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) SELEMANI JAFO amewataka wakuu wa shule za msingi kutojihusisha na suala la udanganyifu wa mitihani kwa kuwa linaporomosha elimu ya Tanzania.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) SELEMANI JAFO amewataka wakuu wa shule za msingi kutojihusisha na suala la udanganyifu wa mitihani kwa kuwa linaporomosha elimu ya Tanzania.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo jana jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara.
Amesema wao wanadhamana kubwa katika kusimamia sekta ya elimu nchini hivyo ikitokea uvujaji wa mitihani hauleti picha nzuri katika Taifa.
Akizungumzia suala la elimu bila ya malipo amesema matumizi ya fedha hizo yameimarika tofauti na ilivyokuwa mwanzo walipoanza ambapo kulijitokeza changamoto mbalimbali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania bara(Tapsha), REHEMA RAMOLE ameipongeza serikali kwa uboreshaji wa miundombinu jambo ambalo limepunguza msongamano wa wanafunzi darasani.
Kauli mbiu ya mkutano huo inasema Uwajibikaji na Usimamizi makini wa Rasilimali katika elimu ndio Msingi wa Elimu Bora.
"Mwanamke Mnene Hana Swaga" - Gigy Money
Staa na mrembo maarufu Gigy Money, ametoa ya moyoni kuhusu kupungua kwa muigizaji Wema Sepetu, pamoja na masuala yake ya urembo na urafiki na kinachoendelea kwenye mahusiano yake kwa sasa.
Gigy Money ameieleza EATV & EA Radio Digital, wakati wa sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa mrembo Wema Sepetu, iliyofanyika usiku wa kuamkia Jumamosi ya September 28, 2019, katika ukumbi wa starehe uliopo Masaki Jijini Dar Es Salaam.
"Nam 'support' sana kwa sababu Mwanamke mnene hana ladha, hana swaga,unaweza kufanyiwa upasuaji ili upunguze mwili ila ni pesa yako tu, haina madhara, kwahiyo mwanamke akiwa lele mama mwili unamuelemea, hata mimi niliwahi kuwa mnene na nikapungua" amesema Gigy Money.
Aidha Gigy ameeleza nia yake ya kununua gari kabla ya huu mwaka kuisha na kwamba yeye ndiye msanii anayevaa nywele halisi za bandia na huzivaa mara moja na akizivua huwa anazigawa kwa watu wake wa karibu.
Akizungumzia suala la mahusiano yake, Gigy amesema kwa sasa hayuko tayari kuyaweka hadharani.
Kina Dada, Kwani Kuolewa ni lazima?
Nimeuliza hili swali kwa sababu kwenye jamii yetu baadhi ya kina dada ambao hawajaolewa hadi umri fulani wanakuwa 'desparate' na kupelekea kuchukua maamuzi yanayoshangaza au hata kuwaumiza.
Ingawa ni wachache sana wanaokiri kwa maneno frustrations zao kwa watu, tumekuwa tukishuhudia wengi wao wakikiri kwa matendo yao.
Tunashuhudia kina dada wakisacrifice heshima zao na 'kulazimika' kufanya vitu vya ajabu ili tu kumridhisha mchumba.
Tunashuhudia kina dada wakifyatua mimba kila siku zilizotokana na 'kutii' hamu ya wachumba ambao wanaishia kuwatelekeza
Tunashuhudia kina dada wakiingia katika mahusiano na wanaume lukuki kwa sababu tu wanataka ku-maximize chance ya kuolewa.
Tunashuhudia kina dada wakivunja mahusiano na wanaume wanaowapenda kwa sababu wamekutana na aliye tayari kuoa hata kama hawapendani...
Mbaya zaidi wapo wadada wanaoona kabisa unreliability ya ndoa wanazoingia lakini wanasema "bora tu niolewe mwaya, hata nikiachika nitakuwa nimetoa mkosi!!!!"
Kama Mungu kakujaalia uwezo wa kufanya kazi na kuingiza kipato cha kukuwezesha kujikimu na kuwakimu wanaokutegemea, kwa nini uumize kichwa na kuingia kwenye ndoa za mateso na za kukudhalilisha, ili na wewe uonekane umeolewa?
Kina Dada, Kwani Kuolewa ni lazima?
Ingawa ni wachache sana wanaokiri kwa maneno frustrations zao kwa watu, tumekuwa tukishuhudia wengi wao wakikiri kwa matendo yao.
Tunashuhudia kina dada wakisacrifice heshima zao na 'kulazimika' kufanya vitu vya ajabu ili tu kumridhisha mchumba.
Tunashuhudia kina dada wakifyatua mimba kila siku zilizotokana na 'kutii' hamu ya wachumba ambao wanaishia kuwatelekeza
Tunashuhudia kina dada wakiingia katika mahusiano na wanaume lukuki kwa sababu tu wanataka ku-maximize chance ya kuolewa.
Tunashuhudia kina dada wakivunja mahusiano na wanaume wanaowapenda kwa sababu wamekutana na aliye tayari kuoa hata kama hawapendani...
Mbaya zaidi wapo wadada wanaoona kabisa unreliability ya ndoa wanazoingia lakini wanasema "bora tu niolewe mwaya, hata nikiachika nitakuwa nimetoa mkosi!!!!"
Kama Mungu kakujaalia uwezo wa kufanya kazi na kuingiza kipato cha kukuwezesha kujikimu na kuwakimu wanaokutegemea, kwa nini uumize kichwa na kuingia kwenye ndoa za mateso na za kukudhalilisha, ili na wewe uonekane umeolewa?
Kina Dada, Kwani Kuolewa ni lazima?
Yanga yaangukia kwenye milioni baada ya kuzikosa bilioni za CAF
Unaambiwa kama Yanga wangefanikiwa kuiondoa Zesco United katika Ligi ya Mabingwa Afrika juzi Jumamosi, timu hiyo ingejinyakulia dola za Kimarekani 550,000 ambazo ni sawa zaidi ya bilioni 1.5 za Kitanzania.
Licha ya kuzikosa dola hizo, lakini kwa kuwa inaendelea na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga sasa inaweza kuambulia dola 275,000 ambazo ni zaidi shilingi za Kitanzania, milioni 774.
Yanga ilitupwa nje ya michuano hiyo kwa kipigo cha bao 2-1 juzi Jumamosi na kufanya jumla ya matokeo hayo pamoja na mechi ya raundi ya kwanza iwe ni mabao 3-2.
Yanga itatwaa dola 275 endapo kama itatinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kamanda Aeleza, Jambazi wa Muda Mrefu alivyouawa
Mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni jambazi, ameuawa kwa kupigwa risasi katika majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi, tukio lililotokea majira ya saa 7:30 mchana eneo la Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Ilala, Zuberi Chembela amesema kuwa mhalifu huyo alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu na kwamba alianza kufukuzwa kuanzia eneo la Magomeni.
''Hilo tukio naomba mmpigie Afande Mambosasa kwasababu huyo mhalifu alikuwa anakimbizwa kutokea Magomeni, kwahiyo alivyofika hapo akazingirwa na ndipo kikatokea hicho kilichotokea na hilo tukio limehusisha mikoa miwili, Ilala na Kinondoni hivyo ni vyema mkamtafuta Mambosasa atalizungumzia vizuri zaidi'', amesema Chembela.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa, amethibitisha kupokea taarifa ya tukio hilo akisema, ''ni kweli tukio hilo limetokea, askari wetu walikuwa wanapambana na huyo jambazi, alikuwa anafuatiliwa na hiyo milio iliyosikika walikuwa wanapambana naye na tumefanikiwa kupata Bastola moja'', amesema SACP Mambosasa.
Aidha Kamanda Mambosasa amesema kuwa atatoa undani wa tukio hilo, punde tu atakapopokea vielelezo vyote.
Harmorapa Adai Anadate na Dada wa Jay Z
Msanii Harmorapa asiyeishiwa na vituko hapa nchini, ametoa kali ya mwaka baada ya kubebwa kwenye machela wakati wa uzinduzi wa filamu 2 za Duma, zilizofanyika Mlimani City na kusema kuwa watanzania wasimbeze kwani anayo mahusiano mazuri na nyota wa HipHop duniani Jay Z.
Akiwa mbele ya waandishi wa habari, Harmorapa akazungumzia muonekano wa mavazi yake katika tukio hilo.
“Mimi ni mnyamwezi siku zote unajua , imenigharimu kiasi kikubwa sana halafu vitu vyangu vinakuwa 'Proffesional' sana na sio 'local' ila nahisi watu hawajawahi kuniona na huu muonekano”amesema Harmorapa.
Kwa upande wa mahusiano yake na mwanaHipHop maarufu duniani Jay Z, Harmorapa amesema
“Jay Z ni shemeji yangu na nina kolabo kubwa ya dunia ambayo nafanya naye inakuja, kwa sasa tupo katika mchakato wa kufanikisha hilo na itatoka muda si mrefu” amesema Harmorapa.
Kufuatia Kolabo hiyo Harmorapa anataka kuwaonesha watanzania kwamba anachokifanya anakijua na kwamba waache kumchukulia poa kwa kuwa hajakurupuka.
Duma amjibu Nay wa Mitego kuhusu Mabaunsa
Siku moja baada ya msanii Nay wa Mitego ku-post video Instagram akiwaponda wasanii kuwa na mabaunsa wa kuwalinda, msanii wa filamu Duma amepingana na kauli ya Nay wa Mitego baada ya yeye kuonekana na mabaunsa watatu usiku wa uzinduzi wa filamu yake.
"Mabaunsa hawa wananilinda kwa ajili ya tukio hili kubwa na la kihistoria, nikaona sio mbaya nikaingia na watu wakani 'support' kwa namna moja au nyingine ni kitu kizuri lakini huwezi kujua watu wanaweza wakakuvamia kwa sababu hapa watu ni wengi na wengine wanaweza wasiwe wazuri kwa upande wangu".
Kupitia ukurasa wake wa instagram Nay wa Mitego aliandika, ''sasa hivi kutembea na mabaunsa imekuwa 'fashion' sio kama usalama wa mtu, maana naona hata 'video queen', wadangaji, DJ's na wao wana mabaunsa, pia wasanii wengine hawana sababu ya kutembea na baunsa kwanza hawana hela".
Baada ya kipande hicho cha video kukiachia, kilionekana kupendwa na watu wengi na ndani ya muda mfupi kilikuwa na watazamaji 124,426 , kilipendwa (likes) 36,293, pamoja na maoni ya watu 2,235.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...



































































