Search This Blog

Saturday, August 31, 2019

Baraka The Prince Anahitaji Mtu/Watu Nyuma Yake la Sivyo Anguko Lake

Hatana mashaka hata kwa uchache katika upana wa uimbaji na utunzi wa Baraka Da Prince. (Mjuzi)

Baraka toka yake ni ya upekee mno, hakuwa na muigo wa msanii yoyote kama awali za wengi. (Muziki)

Juzi, jana ya Baraka Da Prince ilikuwa ni katika mvumo mzuri mno. Maanishio letu ni Siachani Nawe, Nivumilie, Jichunge lakini Sina. (Nyimbo)

Na nyakati hizo ikumbukwe hakuwa pekee bali watu wenye kumuongoza vyema. Pia ifahamike “Wawili ni wawili tu” (Mawazo)

Leo ya Baraka ni katika anguko kuu, na uhalisia si kama hana uwezo wa kipawa, hapana bali mikakati katika upana wa soko. (Uongozi)

Baraka anahitaji kuwa na mtu ama watu katika ongoza yake. Na watu wawe ni wenye mikakati ya namna ya kuweza kumuweka Baraka sokoni. (Biashara)

Ikumbukwe “Kuimba ni mosi, biashara ni pili” Na daima biashara inahitaji wajuzi wenye ujuzi haswa. (Ufahamu)

Vivyo kama Baraka ataendelea kujiongoza mwenyewe ni wazi anguko lake ni endelevu katika soko. (Uhalisia)

Lakini akiwa chini ya genge la wajuzi hakika Baraka ni biashara yenye upekee katika soko hili la muziki. (Hakika)

Na yeye anaweza pinga kwa ukubwa kweli hii, lakini haiwezi kutushangaza yakuwa “Huwezi kuona msitu ukiwa msituni” (Tafakari)

By Tizneez

RAIS DKT. MAGUFULI NA MKEWE JANETH WASHIRIKI MISA TAKATIFU DOMINIKA YA 22 MWAKA “C” KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR

Tofauti ya Harmonize na RICH Mavoko ni Ndoto na Uhalisia


Ndoto ni mfululizo wa picha, mawazo, mihemko, na hisia ambazo hutokea akilini kwa kawaida bila kusudi. Na hii ni katika hatua fulani za usingizi.

Yaweza kuwa alfajiri, asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Lakini kile ambacho kitakuja katika usingizi wako katika onyesho/taswira ndiyo ndoto kamili.

Kimsingi ndoto na uhalisia ni vitu viwili venye tofauti. Ikumbukwe ndoto huleta dhanio, lakini uhalisia ni kile kitu/jambo ambao unaliona kwa nyakati kamili.

Na tukirejea haswa kwa Rich Mavoko na Harmonize kila mmoja ni katika simulizi ya maoni juu yao. Ambapo yote haya ni Harmonize kuonekana ni mwenye kutaka kujiengua kutoka kwenye ‘Genge’ la Wcb.

Wakati huo Rich Mavoko alishajiengua mapema mwaka 2018 kutoka kwenye Genge la Wcb.

Kelele ni nyingi mno, na wapo mahodari wenye kelele haswa. Lakini daima “Mwenye kelele hana neno”

Na hakika kelele nyingi ni za lugha kali za mashabiki lakini wachambuzi pia hofu ni tawala katika hofu kamili juu ya kweli ambayo haihitaji kona.

Kwanza haipaswi kabisa kuweka ufananisho wa Rich Mavoko na Harmonize katika hili la Harmonize.

Ikumbukwe Rich Mavoko alitoka mithili ya mtu awapo ndotoni. Si katika tafakari kuu ya kesho bali usiku wa ndoto pekee.

Harmonize ni katika uhalisia wa kujipanga na uongozi. Lakini egemeo la jamii katika mengi yahusuyo jamii. Lakini kujiongeza kila leo na kuheshimu wengi katika kesho yake.

Rich Mavoko ni katika ndoto ambayo yumwenyewe katika usiku wake. Bila genge la watu nyuma yake lakini hata kujipoteza kwa jamii katika mengi yenye uhitaji wa ushiriki.

Vivyo wenye mfananisho hawapaswi kufananisha wasanii hawa, kwa maana ni wenye tofauti kuu katika uhalisia wao, si mfanano wa ndoto.

Harmonize uwezekano wa kusonga nje wa Wcb upo kwa maana ni mwenye juhudi kamili lakini uhalisia wa nidhamu kuu katika kazi kuanzia ngazi ya mtandao hata nje ya mtandao.

Na uzuri wa Harmonize amejitengeneza yeye na Genge lake la ‘Konde Gang’ kwa upana wa mengi yenye mengi si yale ya ndoto.

Vivyo hakuna uhalisia wa anguko la Harmonize kama ana watu makini katika kesho yake. Bali endelezo lenye ukubwa zaidi.

Pia mkumbuke yakuwa “Mshale kwenda porini haukupotea” (Tafakari..)

By Tizneez

Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Kurefusha Maumbile

*MPUTURU 3POWER*/
.
*DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME NA KUNENEPESHA UUME/*
.
*๐Ÿ“ŒMPUTURU 3 POWER*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 9 yenye maajabu yafuatayo:/
๐Ÿ”–(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri ya uume ulio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
๐Ÿ”–(2)Kurefusha uume uliorudi ndani kuanzia inch 5-9/
๐Ÿ”–(3)Kunenepesha uume cm 5 ya upana itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-20 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
Unashauliwa uitumie dawa hii kama Kinga ya magonjwa sugu, haijarishi umri hata kama una umri  wa miaka 90 itumie huanza kufanya kazi dakika 30 tu na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
๐Ÿ”–(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
๐Ÿ”–(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
๐Ÿ”–(3)Ngiri/
๐Ÿ”–(4)Kama umejichua sana punyeto/
๐Ÿ”–(5)Kisukari/
๐Ÿ”–(6)Presha ya kupanda na kushuka/
๐Ÿ”–(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
๐Ÿ“Kuishiwa kwa nguvu za kiume na kuwa na uume mdogo itumie leo,๐Ÿ“Œ/
. _______________________
Bado hujachelewa Ni tofaut na ulizo wahi kutumia/
.
*๐Ÿ”–IPYULA NGUTYE*/
Ni dawa ya kumvuta mme/mke, hawara, mpenzi, mchumba wako arudi haraka na kuanza mapenzi mapya kama mlivyo anza mwanzo baada ya masaa 2 tu atarudi na kutimiza ahadi zote na atatulia ndani ya nyumba/
.
*๐Ÿ”–SHEPU EXTRA NO 8*/
Ni dawa ya kutengeneza Shepu, mguu wa bia, umbo namba 8 pia inaondoa makovu, chunisi, nk/
.
Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO NK/
._______________________
ANAPATIKANA TANGA PANGANI NA DAR ES SALAAM  AU UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO SIMU NO:/
*๐Ÿ“ž0769597778*

Taasisi nunuzi zasisitizwa kujiunga na Mfumo wa manunuzi ya umma kwa njia ya Mtandao (TANePS)

Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo kwa mmoja wa washiriki
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akiwahutubia washiriki wa mafunzo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS yaliyofanyika jijini Arusha
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo kwa vitendo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS .


Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imetoa wito kwa Taasisi nunuzi kuwaruhusu watumishi wa vitengo vya usimamizi wa manunuzi pamoja na mifumo ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kushiriki kwenye mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa njia ya Mtandao ili ziweze kuunganishwa na kufanya manunuzi yake kwa kutumia mfumo huo. 

Wito huo umetolewa jijini Arusha na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo, alipokuwa akifunga mafunzo ya siku sita kuhusu matumizi ya Mfumo huo unaojulikana kwa jina TANePS (Tanzania National e-Procurement System) kwa maafisa 110 wa vitengo vya usimamizi wa manunuzi na Tehama kutoka Taasisi 44. 

Mhandisi Kapongo amezisisitiza Taasisi nunuzi kuhakikisha zinaunganishwa na kisha kufanya manunuzi yake kwa kutumia mfumo huo wa TANePS ili kukidhi matakwa ya sheria ya manunuzi ya umma pamoja na uamuzi wa Serikali kutaka taasisi zote za umma kuunganishwa na TANePS ili ziweze kufanya manunuzi yote kupitia mfumo huo kwa lengo la kurahisisha michakato ya manunuzi kufanyika kwa ufanisi na tija zaidi na kuhakikisha upatikanaji wa thamani halisi ya fedha. 

Amezitaja baadhi ya faida za mfumo wa TANePS unaosimamiwa na PPRA kuwa ni kupunguza gharama na muda kwenye michakato ya manunuzi serikalini pamoja na kuongeza uwazi, ushindani na usawa kwa wazabuni na watoa huduma wanaoshindania zabuni mbalimbali zinazotangazwa na Taasisi za Umma. 

“TANePS inawezesha mchakato wote wa manunuzi serikalini kufanyika kielektroniki ambapo hakutakuwa na sababu ya wazabuni kutumia muda mwingi kutembelea ofisi za Taasisi za Umma pale wanapotaka kushindania zabuni, pia hawawezi kukutana ana kwa ana na watumishi wa taasisi za umma kwa kuwa kila kitu kinafanyika mtandaoni,”alisema Mhandisi Kapongo. 

Aidha, Mhandisi Kapongo ametoa wito kwa wafanyabiashara, wazabuni na watoa huduma kuhakikisha wanajisajili kwenye mfumo huo ili waweze kushiriki au kushindania zabuni mbalimbali zinazotangazwa na taasisi za umma. 

Tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2019, wataalamu kutoka PPRA wamepiga kambi jijini Arusha kwa ajili ya kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya TANePS kwa awamu tofauti, programu inayotarajiwa kuwa endelevu ili kutoa fursa kwa wataalamu wa manunuzi kwenye taasisi zote za umma kupata fursa ya mafunzo hayo. Tangu kuanza kwa programu hii kabambe jumla ya watumishi 204 kutoka taasisi za umma 75 wameshapatiwa mafunzo hayo, ambapo wahusika wanapaswa kutembelea tovuti ya mfumo (www.taneps.go.tz) au tovuti ya PPRA (www.ppra.go.tz) ili kupata zaidi maelezo ya namna kujisajili kushiriki. 

Mafunzo haya yanagharamiwa na Serikali pamoja na ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).


MAGAZETI YA LEO 1/9/2019

















BAKWATA Waishukuru Serikali ya Mkoa kufanikisha kupata hati za viwanja vyao

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akimkabidhi hati za viwanja viwili vya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania vilivyopo Manispaa ya Sumbawanga Shekhe wa Mkoa Shekh Rashid Akilimali wakati wa hafla fupi ya Makabidiano hayo.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (waliokaa katikati) pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bernard Makali (wa pili Kutoka kulia) na Shekhe wa Mkoa Shekh Rashid Akilimali (wa pili toka Kushoto) Kamati ya Ulinzi na Usalam ya mkoa pamoja na viongozi wengine wa Wilaya na Halmashauri. 

……………………………………………………………………….

Shekhe wa Mkoa wa Rukwa Shekhe Rashid Akilimali amepongeza juhudi za serikali ya mkoa wa Rukwa chini ya mkuu wa mkoa huo Mh. Joachim Wangabo kwa kuweza kufanikisha kupatiwa viwanja viwili vyenye jumla ya ekari 18 vilivyopo katika Manispaa ya Sumbawanga baada ya kupita miaka 13 ya mgogoro baina ya Taasisi hiyo na uongozi wa serikali ya mkoa.

Amesema kuwa Serikali hii ya awamu ya tano ndio inayotakiwa kwani inawajali wanyonge na kuwapa haki wale wanaostahiki kupewa haki hiyo na kuongeza kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kweli anajua kuwateua watu wake na hakukosea kumteua Mh. Wangabo kuuongoza mkoa wa Rukwa

“Kwahiyo mheshimiwa nikushukuru kwa niaba ya waislamu wa mkoa wa Sumbawanga, hili linatoka Moyoni kwangu rasmi, miaka 13 leo tunakabidhiwa hati hizi, imetugonga mioyo, imeleta farka ya jamii, unapomchangisha sadaka mtu halafu isionekane imefanya kazi fulani anabaki anajenga hoja ambayo haipo, wewe ni mfano wa kuigwa kwa wakuu wa mikoa wengine kwa jambo hili, lakini nitakuwa mnyimi wa fadhila kutokumshukuru Mkurugenzi wa Manispaa, kijana Madhubuti kabisa huyu, amejitoa muhanga akasema ardhi hii ipo na mtapata lakini kwa usimamizia wako,” Alisisitiza

Aidha, Shekhe Akilimali alitumia nafasi hiyo kuiomba radhi serikali ya mkoa kwa niaba ya waislam wa mkoa huo katika eneo ambalo uongozi wa taasisi uliwakwaza katika kufuatilia hati hizo na kuonekana ni tatizo katika ofisi za serikali.

Kwa upande wake Mh. Wangabo alisema kuwa ni dhamana ya viongozi katika maeneo mbalimbali ya kiutawala kuhakikisha kuwa hakuna migogoro baina ya serikali na wananchi wanaoongozwa na kuongeza kuwa viongozi kwa namna yoyote ile ni lazima wawe tayari kuitatua migogoro hiyo kwasababu madhara yake ni makubwa na isiposhughulikiwa kwa wakati itapelekea kukosekana kwa utulivu na amani na hatimae maendeleo yanadumaa.

“Tnapotatua migogoro ya namna hii tunawezesha serikali kupita hatua za kimaendeleo pamoja na wananchi kwa ujumla wanapiga hatua za kimaendeleo, mgogoro huu wa viwanja umekuwepo tangu miaka hiyo ya 2006, miaka mingi sana lakini sasa leo tumekata mizizi ya fitina, tunaamini kabisa kwamba kuanzia sasa hivi tutakwenda kwa amani na utulivu na madhehebu ya dini zote sit u waislamu hata wakristo ambapo nao kulikuwa na mgogoro mzito tangu 1985 ambapo nao tumekwishautatua,” Alieleza.

Halikadhalika, Mh. Wangabo alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kufanya haraka katika kuwafikisha viongozi hao wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)katika maeneo hayo ambayo wamepatiwa hati ili waweze kutambua mipaka yao huku kukiwa na muwakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga.

Awali akitoa taarifa ya mgogoro huo Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Rukwa Ust. Mohamed Adam alisema kuwa kuna wakuu wa mikoa kadhaa ambao wamepita katika mkoa huo lakini hawakuweza kujaaliwa kuumaliza mgogoro huo ambao umemalizika leo tarehe 30.8.2019 na kusisitiza kuwa jambo hilo litabaki kuwa historia kwa waislamu wa Mkoa wa Rukwa.

“Sisi Waislamu wa Mkoa huu kwa jambo hili ulilolifanya tutaendelea kukumbuka katika maisha yetu yote na Mwenyezi Mungu akujaalie sana Mheshimiwa mkuu wa mkoa kwa alama hii uliyoiweka katika mji wetu,” Alisema.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mhe. Joachim Wangabo kwa niaba ya Serikali amekabidhi hati za Viwanja viwili vyenye namba 50074 na 50075 kwa Shekhe wa Mkoa Shekhe Rashid Akilimali kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).


KAMATI YA USALAMA BARABARANI MOROGORO YAFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU WA CCM SHAKA OFISINI KWAKE

Kamati ya Usalama Barabarani mkoa wa Morogoro wamekutana na nakufanya mazungumzo na Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka ofisini kwake.

Kamati hiyo ikiongozwa Mwenyekiti wake Ndugu Johanes Kakiziba pamoja na mambo mengine waliwasisha mpango mkakati wao wa utekelezaji wao katika kipindi cha miezi sita ijayo.

“Sisi tuna makundi ya mjumuiko wa watu katika jamii, ili muweze kufanikisha majukumu wenu lazima sisi tuwe mabalozi wenu wazuri kwa vile mara nyingi hukutana nao katika shuhuli mbali mbali, vyengine kazi yenu itakuwa ngumu”

“Naelekewa zipo changamoto za usalama barabarani katika mkoa wetu Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Morogoro tuko pamoja na nanyi”

“Endeleeni nasi tutawaunga mkono ushauri wangu kwenu mipango yenu isishie kwenye makaratasi lazima mjipange vizuri katika usimamizi na utekelezaji wake, punguzeni urasimu wa kuwa mbioni kukamilika kila siku hatamfanikiwa na mwisho wa siku mtaonekana nanyi ni mizigo isiyobebeka mbele ya mamlaka hata wananchi” Shaka Hamdu Shaka.
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro.


RAIS MHE. DKT. MAGUFULI NA MKEWE JANETH MAGUFULI WAMESHIRIKI MISA TAKATIFU DOMINIKA YA 22 MWAKA “C” KATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM. SEPTEMBA 01, 2019

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar […]

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili 1 September

















Friday, August 30, 2019

Aua Mkewe Kwa kumnyonga shingo kisha kujiua kwa kunywa sumu.

Mkazi wa kijiji cha Iponya katika Halmashauri ya Mji wa Kahama, Paschal Clement (32), amemuua mkewe Ashura Paschal (30) kwa kumnyonga shingo kisha kujiua kwa kunywa sumu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Iponya.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi na kwamba kabla ya tukio hilo, wanandoa hao walikuwa na ugomvi huku mume akimtuhumu mkewe kuwa si mwaminifu kwenye ndoa.

Abwao alisema Paschal baada ya kutekeleza mauaji hayo, alijiiua kwa kunywa sumu ambayo mpaka sasa bado haijafahamika ni ya aina gani na kukutwa chumbani kwake akiwa amelala sakafuni.


Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi aridhishwa na miradi ya SUMA JKT Kanda ya Ziwa

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi amesema anaridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na miradi inayotekelezwa na SUMA JKT kanda ya Ziwa.

Dkt. Mwinyi akiwa kwenye ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na SUMA JKT pamoja na makampuni mengine yaliyo chini ya Wizara hiyo kanda ya Ziwa  tarehe 30/08/2019 katika Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga amesema kwa kiwango kikubwa ameridhishwa na kazi zinazofanywa na sehemu kubwa kazi zimekwenda kwa kiwango kinachotarajiwa na kuwa changamoto zilizopo zitafanyiwa kazi.

“Niwahakikishie Mikoa na Halmashauri zinazohusika na miradi inayotekelezwa na SUMA JKT changamoto zote zitafanyiwa kazi” amesema Dkt. Mwinyi.

Aidha, amemshukuru Mhe. Rais John Magufuli kwa kuiamini kampuni hiyo iliyo chini ya Wizara yake na ndiyo sababu ya yeye kufanya ziara hiyo ili kuhakikisha imani hiyo inadumu pamoja na kuwaomba viongozi wote wa Mikoa na Halmashauri kuendelea kuiamini.

Aidha, amewataka SUMA JKT kuongeza kazi ya ziada mara watakapopata fedha ili kukamilisha jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ambalo ujenzi wake umesimama kutokana na changamoto ya fedha.

Naye Mkurugenzi wa SUMA JKT Kanali Rajab Mabele amesema kuwa, kampuni hiyo imepiga hatua kubwa hasa katika nyanja ya ujenzi lakini pia inajihusisha na kazi nyingine mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji.

Awali, akimkaribisha Dkt. Mwinyi Mkoani hapa, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amemuomba kupitia kampuni ya SUMA JKT kuangalia jinsi ya kuwa na miradi ya kuvuna maji ili wananchi waweze kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji.

“Pamoja na kiangazi kilichopo, tunapata mvua nyingi sana na tunavuna mpunga unaoweza kulisha nchi yote, sasa tuone namna bora ya kuvuna hayo maji na tayari baadhi ya wananchi wameshaanza kuchimba mashimo makubwa ya kuvuna maji, tumeona kama Mkoa tufanye hilo ili wananchi wetu waweze kupata mpunga” amesema Telack.


UGANDA: Asulubiwa kwa kupigiliwa misumari kwenye mikono, Yadaiwa ameponzwa na kofia ya chama tawala


Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Baker Kasumba (21), ameshambuliwa na watu wasiojulikana wakati akitoka kazini kuelekea nyumbani katika eneo la Kalerwe, Jijini Kampala siku ya Alhamisi ya Agosti 29, 2019 ya wiki hii.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mjini Kalerwe,  Imeeleza kuwa Kasumba alikutwa amepigiliwa misumari ya nchi 6 kwenye mikono yake yote katika makutano ya barabara ya Kalerwe.

Taarifa hiyo, inaeleza kuwa kijana huyo alivaa kofia ya Chama cha Tawala cha National Resistance Movement    (NRM) kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni.

Kwenye maelezo yake aliyoyatoa katika kituo kidogo cha Kibe mjini Kampala, Kasumba amesema kuwa wakati akiwa njiani kutoka kazini, Alisimamishwa na watu wawili na kisha walimvua kofia na kumvuta mikono yote miwili na kuanza kumpigilia misumari kwenye mikono yake, Huku wakimwambia ‘Kofia yako imekuponza’.

Polisi nchini Uganda inaendelea na uchunguzi kuwabaini watu hao waliomshambulia kijana huyo, Kwa sababu za kisiasa.

Inasikitisha...Mtoto wa Masoud Kipanya Miaka 12 Kitandani – Video


MALCOM Ally Masoud Kipanya ni mtoto wa Sara Chande ambaye amelala kitandani kwa miaka 12 akisumbuliwa na tatizo la udhaifu wa misuli unaosababisha kushindwa kufanya kitu chochote katika maisha yake.

Pamoja na hayo yote Malcolm ni kijana mwenye mtazamo chanya katika maisha yake na fikra zake, kwani amekuwa akiamini kuwa kuacha kulalamika ndiyo mwanzo wa kuwa na furaha maishani.

Akiwa hajiwezi kitandani, bado ana ndoto ambazo anataka kuzitimiza katika maisha yake, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wagonjwa wenzake na watu wenye ulemavu na kufungua taasisi ambayo itakuwa na msaada kwa wahitaji.

VIDEO:



Polisi Pwani Yakamata Shehena Ya Vipodozi Feki

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI la polisi mkoani Pwani, linamshikilia Albert Kiwia (45) mkazi wa Kimara Dar es salaam kwa kosa la kusafirisha shehena ya vipodozi feki mbalimbali ,kwa kutumia gari aina ya Toyota Nissan.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limefanikiwa kukamata madumu saba ya mafuta ya diezel yakiwa na ujazo wa lita 20 kila moja mali inayodhaniwa kuwa ni ya wizi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani,Wankyo Nyigesa aliwaambia waandishi wa habari kuwa ,mtuhumiwa huyo amekamatwa agost 29 mwaka huu, katika eneo la Mizani ya zamani -Kibaha Mji .

Alifafanua, licha ya tuhuma hiyo ya kusafirisha vipodozi hivyo ,jeshi hilo likamtaka aonyeshe kwa TRA stakabadhi alizolipia ushuru katika mipaka ya nchi wakati akiingiza vipodozi na hakuwa navyo

Aliwataka ,wafanyabiashara wenye tabia ya kuingiza bidhaa zao nchini kwa kukwepa kulipa kodi ,kuacha mara moja .

Wankyo alisema ,wamedhibiti mianya yote kwa wale wanaojaribu kukwepa kulipa kodi katika barabara zote za mkoa na wale watakaokamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hata hivyo, akielezea kuhusiana na tukio la kukamatwa madumu ya mafuta ya diezel ,alisema madumu hayo yamekamatwa ,eneo la Misugusugu ,Kibaha baada ya mtu aliyekuwa na mafuta hayo kuyatelekeza na kukimbia baada ya kuona gari la polisi likielekea mahali alikokuwa .

Wankyo alitoa wito kwa jamii kuacha kuhifadhi madumu ya mafuta aina ya diezel na petrol ndani ya nyumba kwani ni hatari.


Mlema "Mimi ni Staa Mkubwa Bongo..Pesa Imenitembelea, Nalipa Baunsa Milioni"


MAMBO mazuri! Kama Staa wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela naye kwa sasa analindwa na baunsa ambapo anataja sababu za kufanya hivyo.Akistorisha na Shusha Pumzi, Mlela alisema kwa sasa ameamua kuweka ulinzi ambapo anaongozana na baunsa kila anapokwenda kwa kuwa maisha yake yamebadilika baada ya fedha kumtembelea.

“Mimi ni staa mkubwa sana hapa Bongo na hata nje ya nchi hivyo ni lazima niwe na baunsa, hata mastaa wa nje wanafanya hivi, isitoshe kwa sasa fedha imenitembelea, tofauti na zamani, namlipa mshahara wa shilingi laki tano mpaka milioni moja kwa mwezi, inategemeana na tumefanya kazi kwa kiasi gani,” alisema Mlela.

Mlela ameongeza orodha ya mastaa ambao wanaolindwa na mabaunsa kama Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na Lungi Maulanga.

Kim Nana Afunguka "Mimi Sijaachika na Wala Siwezi Achika Kirahisi Hivyo"

WALE mnaopenda kufuatilia maisha ya watu mpo? Haya sasa muuza nyago maarufu Bongo Lilian Kessy ‘Kim Nana’ amesema kuwa yeye kuachika siyo rahisi kama watu wanavyodhani au wanavyoomba iwe kila siku anajiamini ni msichana mzuri.


Kim Nana aliiambia Mikito Nusunusu kuwa mikwaruzano katika uhusiano lazima itokee hivyo hata yeye ametofautiana kidogo tu na mpenzi wake Tonny Albert ’T Bway’ lakini siyo kama wameachana kama ambavyo watu wanazusha na kibaya zaidi ni kwamba asilimia kubwa ya watu wanapenda kusema mambo ambayo hawana uhakika nayo.

 “Jamani eti nimeachika na kipigo juu, mimi siwezi kuachika kirahisi hivyo kama wanavyofikiria najiamini sana, sasa watu wanapenda kuongeaongea tu mambo wasiyokuwa na uhakika nayo.“Kutofautiana katika uhusiano ni jambo la kawaida sana tu, kwa sababu hata hao wanaoongea kuhusu mimi huwa wanagombana na watu wao wakaribu,” alisema.Nana haachiki kirahisi.


Msaidizi wa White House Afutwa Kazi Baada ya Kutoa Taarifa za Familia ya Trump


Msaidizi binafsi wa rais wa Marekani Donald Trump'amelazimishwa kujiuzulu kutoka White House baada ya kujulikana kimakosa kwa taarifa nzinazoihusu familia ya Trump

Madeleine Westerhout, mwenye umri wa miaka 29, aliondolewa kazini ghafla w siku ya Alhamisi baada ya rais kubaini kuwa amekuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa chakula cha jioni mwezi huu .

Alikuwa akinywa pombe na kujisifu kuhusu namna anavyoweza kumfikia rais Trump wakati wa mapumziko ya New Jersey, kimeripoti kituo cha habari cha CBS News

Bi Westerhout alifanya kazi na Trump tangu siku yake ya kwanza ya urais.

Ikulu ya White House imekataa kutoa kauli yoyote juu ya kufutwa kazi kwake.

Gazeti la New York Times, ambalo liliripoti kwa mara ya kwanza juu ya kufutwa kazi kwa Westerhout , lilisema kuwa chanzo cha habari cha White House alisema kwa sasa anachukuliwa kama "mfanyakazi aliyetengwa " na kwamba atazuiwa kurejea katika ikulu hiyo Ijumaa.

Akielezewa na vyombo vya habari vya Marekani kama mlinzi wa lango la Trump , Bi Westerhout alikuwa na ofisi yake mkabala na ofisi ya rais inayofahamika kama Oval Office katika jengo la West Wing.

Kauli zake anazoshutumiwa kuzitoa kwa wandishi wa habari alizitoa wakati wa chakula cha jioni na hazikuwa zinarekodiwa wakati alipokuwa akizungumza na maripotoa katika hoteli ya Berkeley Heights, New Jersey, wakati Bwana trump alipokuwa mapunzikoni katika klabu yake iliyopo Bedminster, New Jersey, mapema mwezi Agosti.

Vyanzo vya habari vimeiambia CBS News kuwa alikuwa akinywa pombe na akatoa taarifa kuihusu familia ya rais . Pia ameripotiwa kutoa taarifa za uvumi kuwahusu watangazaji wanaotaka kumuona rais.

haijafahamika ni vipi Trump alifahamu mazungumzo hayo yote.

Maafisa kadhaa wa Ikulu ya White House kw amuda mrefu walishuku kuwa Bi Westerhout hamuheshimu Bwana Trump, huku mmoja wa maafisa wa zamani akiiambia CBS kuwa : " Alikuwa jasusi kuanzia siku ya kwanza ambaye alitaka kutumia ukaribu wake kwa rais kuwanufaisha wapinzani wake"

kwa mujibu wa vitabu viwili vilivyoandikwa kuhusu Trump katika White House, Bi Westerhout, ambaye alikuwa msaidizi wa zamani wa kamati ya Taifa ya Republican , alikasirishwa na kuonekana akilia katika usiku wa uchaguzi ilipojulikana wazi kuwa Trump alikuwa ameshinda.

Licha ya kutofurahishwa kwake na ushindi wa Bwana Trump, alifanikiwa kupata kazi ya usaidizi wa Trump inayoripotiwa kumlipa $145,000.

Wakati wa kipindi cha mpito cha Bwana Trump, Bi Westerhout mara kwa mara alikuwa akiwasindikiza wageni katika ofisi ya Trump Tower iliyopo New York.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, alikuwa na ukurasa wake binafsi wa Instagram ambapo alituma jumbe na picha kuhusu maisha yake katika White House ana safari alizokuwa akizifanya na rais.

Katika ujumbe mmoja alitania juu ya namna alivyolazimika kuchapisha kipande cha karatasi ambacho trump alikuwa amekishikilia katika tukio la umma.

Wakati mwandishi wa habari wa siku nyingi Bob Woodward alipolalamika kwamba ombi lake la kuzungumza na Bwana Trump katika mahojiano halikufikishwa na wasaidizi wake wa ngazi ya juu kama Kellyanne Conway, Bwana Trump alisema angepaswa kuongea na Bi Westerhout.

"Madeleine ni mtu muhimu . Ni mtu anayeweza kutunza siri ," Alisema Bwana Trump.

Kwa mujibu wa CBS, Bwana Trumpamekuwa akimuelezea mara nyingi kama "mrembo wangu".

BREAKING NEWS: Watu watano Wafariki Baada ya Magari Kugongana, Moja Lawaka Moto


Watu watano wamefariki baada ya gari la Dangote lililokuwa limebeba malighafi ya kutengenezea saruji likielekea Mtwara kugongana na Gari dogo na kupinduka kisha kuwaka moto baada ya kupoteza muelekeo na kugonga nguzo ya umeme rufiji mkoani Pwani.

RPC Rufiji,  Onesmo Lyanga amethibitisha taarifa hizo.

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu za Kiume..Dr Ntobi Anayo Dawa Bora

PATA TIBA YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME.INASAIDIA KUKUFANYA URUDIE MARA.5 NA KUCHELEWA KWA DK 20.TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.BAADA YA UTAFITI WA MDA MREFU JUU YA MATATIZO YA UPUNGUFU  WA NGUVU ZA KIUME NA UKOSAJI WA HAMU YA TENDO LA NDOA AMA KUSHINDWA KURUDIA TENDO KWA HARAKA

 DR.NTOBI AMEKULETEA TIBA SAHIHI YA MATATIZO HAYO KWA KUTUMIA DAWA ZA GUMBA POWER.NI DAWA ASALI YA VIDONGE INAYOTIBU TATIZO LA UPUNGUFU AU UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.DAWA HII INAMCHANGANYIKO WA KUTOSHA WENYE KUZALISHA VICHOCHEO VINGI VYA HEMONE ZA GESTROGEN VIKIWEMO VITAMINI B6&B1.VITAMINI E.PAMOJA NA MADINI AINA YA ZINC VITAKUFANYA KUWA NA NGUVU NA MZUNGUKO MZURI WA DAMU NA KUONGEZA HAMU NA UWEZO WA KUFANYA TENDO LA NDOA ZAIDI YA HATUWA NNE AU ZAIDI .NA KUCHELEWA KUFIKA KILELENI ZAIDI YA DAKIKA 20-30 NTINJE.

INARUTUBISHA MAUMBILE YA UUME YAANI KUREFISHA NA KUNENEPESHA NCHI.4-7 UPANA CM4-6 STANDARD KIAFYA HAIJALISHI UMRI WAKO HATA KWA WAZEE UKIITUMIA MAUMBILE YAKO YATABAKI KUWA HIVYO SIKU ZOTE.PIA TUNATIBU KISUKARI SIKU7 TU.PRESHA.CHANGO.TUMBO KUJAA GESI.NGIRI.BUSHA BILA KUPASUA

TUPO TZ DAR.ESSALAAM MBAGALA KIZUIANI.

HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO MWANZA TUPO BUGARIKA WASILIANA NAMI 0754741788/0715741788/0783741788 DR NTOBI

UVCCM KATAVI WAMSHUKURU RAIS KWA MIRADI MBALIMBALI


Katibu wa UVCCM mkoa wa Katavi Theonas Kinyonto akizungumza na waandishi wa habari


Na Mwandishi wetu, Katavi

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Katavi umempongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa utekelezaji wa miradi mikubwa mkoani Katavi

Akitoa pongezi hizo Katibu wa UVCCM mkoa bwana Theonas Kinyonto amesema ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mpanda hadi Tabora unaashiria utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2015/20

Aidha kupitia mradi wa uboreshaji miji utekelezaji wa mradi wa barabara ya lami ya kilometa 7.7 katika manispaa ya Mpanda uliogharimu shilingi bilioni 8 ambao kwa sasa umekamilika kwa asilimi 97

Pia wamemsukuru Rais kwa kutoa fedha za kujenga kituo kikubwa cha mabasi halikadhalika kuboresha miundombinu ya afya katika mkoa wa Katavi sanjari na ujenzi wa Hospitali za Wilaya tatu katika mkoa wa Katavi

Katika hatua nyingine bwana Kinyonto ametoa wito kwa Vijana kujiunga katika makundi ili kupata mikopo ya Halamshauri ambapo jumla ya shilingi milioni 700 zimetengwa kwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kuwezesha makundi mbalimbali

Pia amepongeza suala la kutolewa kwa elimu bure jambo ambalo limeongeza uandikishaji wa wanafunzi mashuleni ambapo pia amewashukuru wazazi kwa kujitolea nguvu zao katika kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa

Aidha amewakumbusha vijana kuwa kupitia miradi yote inayotekelezwa na serikali ni fursa za ajira kwa vijana hivyo hawana budi kuzitumia fursa hizo vizuri


Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...