Search This Blog

Saturday, October 31, 2020

Kufungwa Kwa Bar ya Last Minute ..Irene Uwoya Adaiwa Kufulia, Vyuma Vimekaza



VYUMA vimekaza! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mwanamama na staa wa fi lamu za Kibongo, Irene Uwoya, kufunga baa yake ya Last Minute iliyopo Sinza, Dar, huku sababu zikiwa hazijulikani.

Baa hiyo ambayo mbali na kazi yake ya fi lamu, ndiyo ilikuwa ikimuingizia kipato na kumpa jeuri mjini hapa mwanamama huyo, ilifungwa huku taarifa nyingi zilikuwa zikisambaa zikianisha sababu za kufungwa kwa baa hiyo.

VYANZO VINASEMAJE


Taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali zimesema kuwa, msanii huyo alikosa mtaji wa kuendesha biashara yake na ndiyo sababu akaamua kuifunga. “Hana lolote zaidi ya kufulia na kukosa mtaji wa biashara japo anafi cha tu,’’ kilisema chanzo kimoja kilichoomba kuhifadhiwa jina lake.

Haikuishia hapo mmoja wa watu wake wa karibu na Uwoya ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, aliliambia Gazeti la Amani kuwa, Uwoya kakosa kodi ya kulipia pango na hata kwenye mapato ya serikali na ndiyo maana akaamua kuifunga.

“Sababu kubwa ya Uwoya kuifunga hiyo baa ni kutokana na kukosa kodi ya kulipia hasa kwenye mapato ya serikali (TRA), maana si unajua tena huwa kuna kodi ya pango na biashara, hicho ndicho kilimshinda na ustaa wake,’’ alisema mtu wa karibu na Uwoya japo naye hakutaka jina lake lichorwe magazetini.

UWOYA AFUNGUKA

Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Uwoya ili aweze kuzungumzia ishu hii ambapo alisema kuwa, hivi karibuni ataifungua tena baa yake.


“Mimi naona biashara zangu ziko poa, Last Minute ipo na tutaifungua hivi karibuni japo Corona ilisababisha tuifunge.


“Kuhusu watu kusema nimeifunga au nimefulia, si kweli maana maneno yanazungumzwa na huwezi kuwazuia watu kuongea lile wanalotaka kuongea, mi niseme watu wasubiri waone,’’ alisema Uwoya huku akisistiza kuwa hajafulia.

KUHUSU VYANZO VYAKE VYA PESA


Baada ya kuzungumzwa kuhusiana na wapi anatoa pesa za kutanua na kula bata ilihali baa yake imefungwa ambapo alisema kuwa, ana bishara zingine.


“Maisha yangu ni ya kawaida si wkamba kuna sponsor na sijawahi kubadilika, pia nina biashara zingine ninazozifanya na zinaniingizia pesa,’’ alimalizia kwa kusema.


Mbali na kuifunga biashara hiyo, Uwoya amekuwa akisifi ka kula bata na kumiliki kiwango kikubwa cha pesa huku vyanzo vyake vikiwa havijulikani. Hivi karibuni Uwoya alizindua reality show yake inayokwenda kwa jina la I AM EVERY WOMAN ambayo inazungumzia maisha ya yake halisi.



Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili Novsmber 01



Ex wa Aunt Aibua Mambo Mtandaoni "Aunty Anapenda Sana Kutawala Wanaume"



HAYA mambo yakuachana halafu mnaanza kuongeleana vibaya mtandaoni si ushamba huu? Haya buana mapema wiki hii aliyekuwa mpenzi (EX) wa msanii wa filamu nchini Aunt Ezekiel, Alfo Alfo ameonekana kumkandia bidada kuwa hafai.

Alfo aliulizwa na shabiki mmoja huko mtandaoni kuwa kwanini aliachana na Aunt, ambapo alijibu kuwa sababu zipo nyingi ila moja ni kwamba mrembo huyo alikuwa anapenda sana kuwatawala wanaume lakini kwake haikuwezekana kwa hiyo ndio maana wakaachana.


“ Aunt like to control men, me Alfo no possible,” aliandika Alfo kwa kimombo.



MAGAZETI YA LEO 1/11/2020















 

Marapa Matajiri Zaidi Duniani Hawa Hapa



KWA hapa Bongo, inaaminika mastaa wa wanaoimba, ndio matajiri zaidi kuliko wale wa kufokafoka (Hip Hop).


Tofauti na mtazamo huo wa Kibongo, huko Marekani wapo mastaa ambao ni wa hip Hop lakini wana utajiri wa kutisha.


Twende tukaitazame Top Five ya mastaa wa Marekani lakini pia duniani kote wanaotajwa na mitandao mbalimbali kuwa ndio wanaoongoza kwa utajiri:


KANYE WEST


Kanye West ni moja kati ya marapa bora wa muda wote. Mafanikio yake makubwa ya kwenye mitindo na fasheni ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza utajiri wake. Kingine kilichochangia mapato yake, Kanye ameachia sokoni albamu 9 ambazo karibia zote zimeuza kwa kiwango cha juu (multi-platinum).


Kanye ameuza karibu nakala milioni 100 duniani kote. Miongozi mwa dili zinazomuingizia mapato ni pamoja na ubalozi ikiwemo wa kampuni ya Adidas. Kwa ujumla, Kanye ana utajiri wa Dola Bilioni 3.2 (Shilingi Trilioni 7. 4) .


JAY Z


Mkali huyu kutoka pande za Brooklyn ambaye ni mjasiriamali ndiye rapa wa kwanza kuwa bilionea katika historia. Jamaa ameweka kibindoni Dola Bilioni 1 (Trilioni 2 .3) peke yake. Lakini ukisema uchanganye utajiri wake na wa mkewe ambaye pia ni staa wa muziki Marekani Beyonce, wanakuwa na utajiri wa Dola Bilioni 1.5 (Shilingi Trilioni 3. 4)


Utajiri wa Jay Z unatokana na uwekezaji wake katika timu za michezo, studio za kurekodia kazi za wasanii, mavazi, kumbi za starehe na mambo mengine kibao.


P DIDDY


Mkongwe huyu naye hayupo nyuma kwenye marapa ambao kimsingi wamefanikiwa kutusua kwenye suala zima la utajiri. Kwenye akaunti yake benki kunasoma Dola Milioni 885 (Shilingi Trilioni 2.5) Mwana huyu mzaliwa wa New York ana majina kama yote, unaweza kumuita Puff Daddy, Puff, Diddy au Sean Combs.


Aliunda lebo yake ya Bad Boy Entertainment mwaka 1993. Mwaka 1997 aliachia albamu yake ya No Way Out ambayo iliuza kwa nakala nyingi (platinum) zaidi ya mara saba.


Mkwanja wake pia anautengeneza kupitia ujasiriamali wa mavazi, migahawa, vileo na kampuni ya miamvuli.


DR DRE


Tofauti na marapa wenzake, mwamba huyu amejiongeza kwa kufanya vipaji vingi ikiwemo uprodyuza, uigizaji na fundi wa sauti (audio engineer). Ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni kubwa ya vifaa vya muziki (Beats Electronics), Beats by Dre.


Jamaa huyu ambaye amewasaidia kwa kiasi kikubwa marapa wenzie wenye mafanikio kama vile Eminem, Snoop Dogg na marehemu 2Pac, akaunti yake benki inasoma mpunga usiopungua Dola Milioni 820 (Shilingi Trilioni 1. 9).


EMINEM


Marshall Bruce Mathers II, ndiyo jina alilopewa na wazazi wake kabla ya kujiita Eminem baada ya kujizolea mashabiki lukuki. Huyu ndiye anayekamata nafasi ya tano katika marapa wenye ukwasi wa kutosha kwani anao mpunga usiopungua Dola Milioni 230 (Shilingi Biloni 533.6)


Mafanikio yake yanatajwa kupatikana zaidi kwa kazi zake za muziki ambapo nyimbo zake zimekuwa na mafanikio makubwa sana sokoni duniani kote.



Mwanamke Amwambia Mumewe Anatamani Wanaume Wengine


 ANITA CASSIDY (40) mwanamke ambaye amekuwa katika ndoa kwa miaka ipatayo kumi, alimwambia mumewe aitwaye Marc (46) kwamba anaona maisha na ndoa ya mume na mke yamemchosha na alitaka kuwa na wenza wengine wa kufanya nao mapenzi.

Katika mazungumzo ya wawili hao ambao ni raia wa Italia, mumewe alikubali kwamba wote wawili kila mmoja angekuwa na wapenzi wengine.    Lakini, je, katika ndoa moja panawezekana kuwa na watu zaidi ya wawili?
Anita Cassidy (katikati) akiwa na mpenzi wake wa kiume Andrea (kushoto) na mumewe Marc (kulia) wakichangia penzi la watu watatu.

 “Mwaka mmoja uliopita niliweka kila kitu bayana kwenye mtandao wa Facebook kwa picha niliyokuwa na mume wangu na watoto wetu wawili.  Marafiki zangu wakaanza kuniuliza kwamba mwanamme mwingine aliyekuwa katika picha alikuwa nani.  Niliwaambia alikuwa Andrea – mpenzi wangu wa kiume.


… Watatu hao wakiwa pamoja kando ya bahari wakipunga upepo.

“Nafahamu wengi watashangaa kwani walijua Marc ndiye mume wangu halisi.   Lakini ukweli ni kwamnba nilikaa naye jikoni mwaka mmoja tukafanya mjadala  mgumu wa aina yake miaka mitatu iliyopita kuhusu maisha yetu.  Nilimwambia Marc kwamba yeye peke yake alikuwa hatoshi kumaliza hamu yangu ya mapenzi.

“Baada ya kukubaliana naye, nilianza kutafuta mpenzi mwingine kwenye mitandao na tukagunduana mimi na Andrea ambaye tulianza kukutana na hatimaye kufanya naye mapenzi.

“Nilikuwa na umri wa miaka 28 nilipokutana na Marc, hivyo wazo la kufanya mapenzi na mtu mmoja kwa miaka zaidi ya 40 ambayo ingefuata, lilinivuruga akili.  Ni kweli nilikuwa nampenda Marc lakini kimapenzi nilijiona kama nilikuwa peke yangu.  Matokeo yake nilimtambulisha Andrea kwa Marc akawa anakuja nyumbani na tunafurahi naye wote.

 “Muda si muda, Marc naye akawa na uhusiano wa wazi na wanawake wengine, akawa anaondoka kwenda kufurahi nao kwengine.  Mwanzoni nilijisikia vibaya kwani alikuwa amenionyesha wanawake hao.  Hata hivyo, sikuwa na la kufanya.

 “Sikutaka kuwaambia watoto wangu kilichokuwa kinatokea, kwani umri wao ulikuwa mdogo mno na wasingenielewa.  Tuliendelea hivyo kwa furaha hadi ikafikia mimi na Marc tukatengana na kila mtu akawa analala chumba chake kwenye nyumba ileile.  Hivi sasa tunasubiri kutengana kabisa ili niondoke na watoto.
“Tangu tutengane miezi 18 iliyopita, bado nampenda Marc na atakuwa nembo muhimu katika maisha yangu.. Ni vyema kuwa na maisha ya wazi, kuliko maisha ya kudanganyana kwa siri….”


 Wakifurahi bila ya chuki wala uchungu.

Naye Andrea anasema kabla ya kukutana na Anita alikuwa na mpenzi mwingine ambaye aliachana naye baada ya mwanamke huyo kukataa kuwa na uhuru wa kufanya mapenzi na watu wengine nje ya wao wawili.

 Hivyo,  alikazania kwa Anita ambaye walipendana na kushirikiana kila kitu likiwemo penzi kabla ya kukutanishwa na mumewe mwaka mmoja baadaye.  Mumewe alikubali kila kitu na watoto wakajua baba yao alikuwa Marc na Andrea alikuwa ‘boifrendi’ wa mama yao…



Hivi sasa Anita na Andrea wanasubiri kuendeleza penzi mara Marc na Anita watakapoachana rasmi.

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA

Makosa Makubwa Wanayoyafanya Wanawake linapokuja Swala la Kupenda..!

Je wewe ni mtu wa kupenda ghafla, yaani mwanaume anapokutamkia kwamba anakupenda huwa unamuamini kwa kiasi gani, unakuwa ni mwepesi wa kumuamini na kujitoa kwa ajili yake au unakuwa na kujivuta vuta ili kujiridhisha kabla ya kuingia katika uhusiano? Hebu fikiri kabla ya kuamua, jipe muda kwani hakuna jambo lililo jema kama subira linapokuja swala la kupenda. Subira itakuepusha kupoteza muda wako katika mahusiano ambayo hayana mashiko wakati dhamira yako ilikuwa ni kumpata mwenzi mwenye sifa muafaka, pale utakapoingia mahali ambapo sipo. Kwa kawaida kutoka katika uhusiano huo kuna gharama kubwa na kunaweza kukusababishia matatizo mengi yakiwemo ya kiafya.

Hapa chini nitajaribu kueleza makosa kadhaa ambayo wanayafanya wanawake linapokuja swal la kupenda:

1.Kumbadili mtu awe vile utakavyo:
Usije ukajidanganya kwamba unaweza kumbadilisha mtu mzima na akili zake. Kama umepata mwanaume ambaye kwa mtazamo wako unamuona ana sifa muafaka lakini anatabia ambazo huzipendi kwa mfano ulevi au kuvuta sigara vitu ambavyo vinakukera sana, usije ukajidanganya kwamba unaweza kumbadilisha na akaacha tabia hizo, anaweza kuacha kwa muda tu ili kukuvuta ukiingia kingi imekula kwako, tabia hiyo inaweza kujirudia. Ni vyema kama kuna tabia ambazo umezipenda lakini zipo ambazo huzipendi kutoka kwa mwenzi wako, basi weka uzingativu kwenye zile tabia unazozipendfa na zile usizozipenda achana nazo, kama ataamua mwenyewe kuziacha sawa lakini kama akiamua kuendelea nazo, basi zisikuumize kwani unaweza kujikuta ndoa yako inakuwa na migogoro isiyokwisha kwa sababu ya kuonekana una ghubu kwa kujaribu kumbadilisha mwenzi wako na mwisho wake upendo unakuwa haupo na kisirani katika ndoa kinaongezeka. Kitendo cha kuonekana kuwa na ghubu kinaweza kumuingiza mwanaume katika tabia nyingine mbaya ya kutotumia muda mwingi kukaa nyumbani kwake na kutafuta kampani nyingine, kama akipata kampani ambayo siyo nzuri anaweza kuangikia katika nyumba ndogo ambayo itamkubali bila masharti.


2.Njoo tuishi:
Unaweza kukutana na mwanaume ambaye ana nyumba nzuri au amepanga nyumba nzuri na ana kila kitu ndani pamoja na usafiri, anakuwa mwepesi kukupa funguo za nyumba yake ili uhamie muishi pamoja, lakini haweki msimamo wake wazi kwamba ana matarajio gani na wewe. Kabla ya kukubali kupokea funguo na kuhamia kwake jiulize kama unampenda kwa dhati au umekubali kwa sababu ya nyumba yake nzuri. Kumbuka nyumba na vitu vingine vinavyotizamika kwa macho (material things) havina mashiko linapokuja swala la kupenda. Kupenda kunahusisha vitu vya ndani kama vile kupenda kwa dhati bila masharti wala kuangalia sifa za nje, kuwa na amani moyoni kila umwonapo mpenzi wako, kuwa na furaha wakati wote mnapokuwa pamoja, kupatwa na msisimko wa mapenzi kila umwonapo au usikiapo sauti yake nk. Lakini kama utamkubali mwanaume kirahisi kwa sababu tu kakukabidhi funguo za nyumba yake wakati huna mapenzi ya dhati ni janga kubwa kwa sababu hivi vitu vya nje vinaweza kutoweka kirahisi, sasa je ikitokea si mapenzi nayo yatakuwa yamekwisha? Kumbuka kwamba kile kilichokupeleka kwake hakipo.

3.Amekuwa ni liwazo kwako
Liwazo linaweza kuwa sehemu ya mapenzi lakini hivi vitu haviendi pamoja. Unaweza kuwa na mwanaume ambaye mnapendana na mnakamilishana hii ni tofauti na mwanaume unayempenda na ukamgeuza kuwa liwazo pale unapohisi upweke. Jiulize, je ni kwamba mnapendana na mnafurahi kuwa pamoja au unampenda kiasi kwamba huwezi kuishi bila uwepo wake. Hapa nazungumzia utegemezi wa kihisia, yaani unakuwa king’ang’anizi mpaka mwanaume anakuona kero, badala ya kufurahia mahusiano yenu mwanaume anakuona kuwa ni kero kutokana na kuwa tegemezi wa kihisia. Hakuna mwanaume anayependa mahusiano ya aina hii anachoka haraka kihisia na atajitahidi kwa kila namna kukukwepa na ikiwezekana kukutosa na kutafuta ustaarabu mwingine jambo ambalo litakuumiza sana.

4.Mwanaume king’ang’anizi:
Mwanaume kutongoza na kukataliwa siyo jambo linalowashughulisha sana kwao kujaribu na kukosa ni sehemu ya maisha, lakini lipo suala la kung’ang’ania, yaani mwanaume kumfuatilia mwanamke kwa hali na mali na kujitoa ili kuhakikisha anampata mwanamke anayemtaka. Huu ni mtego wa mapenzi, kwani kwa mwanaume kung’ang’ania na kufuatilia mwanamke kwa muda mrefu bila kuchoka hata asumbuliwe kiasi gani haimaanishi kwamba mwanaume huyo amempenda mwanamke huyo. Wakati mwingine ni matamanio tu ndiyo yamemsukuma kutokana na sifa za nje alizo nazo mwanamke huyo. Kupenda kwa mwanaume kunahusisha zaidi sifa za nje kuliko za ndani na ndiyo maana mapenzi ya aina hiyo hayadumu yanaanza kama kichaa na kuyeyuka ghafla kama kipande cha barafu juani. Pale mwanamke anapokutana na mwanaume king’ang’anizi na asiyekubali jibu la hapana, kabla ya kukubali ajiulize kama anakubali kuwa na mahusiano na mwanaume huyo kwa sababu amempenda kwa dhati au kwa sababu ya uking’anga’nizi wake? Kumbuka kwamba wapo baadhi ya wanawake wanaweza kumkubali mwanaume tu kwa sababu amemfuatilia sana, anajiwa na huruma anakubali kuwa na mausiano naye siyo kwa sababu amempenda bali kwa sababu ya huruma. Ni vyema ukajiuliza kama na yeye atathamini huruma yako au akishapata alichokitaka atakugeuka na kuwa mwiba mchungu kwako? Tafakari na chukua hatua.

5.Baada ya kupanda mbegu mmea ukachipua
Umekuwa na uhusiano na mwanaume huyu kwa muda mrefu, lakini hakuwahi kukutamkia kwamba ana matarajio gani na wewe kuhusiana na swala la ndao, ghafla unakoma kuziona siku zako… Mimba hiyo! Je unafanyaje?
Kwanza naomba ufahamu kwamba, kupata mimba haimaanishi ndiyo kuolewa. Hili ni kosa ambalo wanalifanya wanawake wengi tena wa kiwango cha kutosha, wanaamini kwamba kubeba mimba kutawahakikishia kuolewa na mwanaume aliyempa ujauzito. Kwa huku kwetu sheria haziwabani sana wanaume linapokuja swal la kulea mimba na matunzo ya mtoto kwa hiyo mwanaume kumtosa mwanamke aliyebeba ujauzito siyo jambo la kushangaza. Wanawake ambao ni single mother wanajua kuhusu jambo hilo. Kwa hiyo kama unabeba mimba fanya hivyo ukiwa umejiandaa kujitwika changamoto zitakazojitokeza na usije ukajifariji ukidhani kutakuwa na masaada kutoka kwa mwenzi wako, utakuwa unajidanganya. Kama akikubali mfunge ndoa sawa, kama akikubali kulea mimba na mtoto atakeyezaliwa pia ni sawa, akikataa wala usivunjike moyo, simama imara na songa mbele na maisha kwani kuzaa kabla ya ndao siyo mwisho wa maisha, yapo maisha tena mazuri sana ukiwa na mwanao. Kwanza unaye mtu wa kukuliwaza, na pili utakuwa umajihakikishia kwamba wewe si mgumba, na tatu leo na kesho umekuwa mtu mzima unaye wa kukushika bega kuliko kutegemea ndugu zako.

6.Pesa inapokuwa sehemu katika kupenda.
Wapo baadhi ya wanawake kabla ya kumkubalia mwanaume wanaangalia anamiliki kitu gani, amesoma kwa kiwango gani, ana kazi ya aina gani, anafanya shughuli gani, anazo fedha za kutosha au yuko katika mazingira ya utafutaji yanayoashiria neema huko mbeleni. Sikatai kwamba wanawake kabla ya kumkubali mwanaume wanataka kujihakikishia usalama, na kama nilivyowahi kusema hapa mara nyingi kwamba usalama kwa mwanamke maana yake ni mtu kuwa na fedha, tofauti na zama za kale za mawe ambapo uwindaji na kilimo kilimuweka mwanaume shupavu katika nyanja hizo kukimbiliwa na wanawake. Siku hizi hayo hayapo, fedha imekuwa ni njia ya mkato katika kupata kila kitu. Kwa mwanamke fedha ni mtego umnasao kama panya na kipande cha nguru mtegoni. Siku hizi ukiwa na fedha una uwezo wa kumpata mwanamke umtakaye, fedha imekuwa kama tufani, inabeba waliomo na wasiokuwemo, hata wale watakaotokwa na povu kupinga hoja hii, nadhani hawajapata bahati ya kukutana na wanaume wenye fedha, laiti wangepata wasingeweza kusimama hapa na kupinga hoja hii. Kwa ushauri tu, si vibaya kuangalia mwanaume mwenye muelekeo wa kutafuta lakini hicho kisiwe ni kigezo namba moja, kwani kama akikuonyesha sifa hizo kabla ya kuingia kwenye uhusiano kisha ukaingia na baadaye ukagundua mwanaume huyo si mali kitu wenyewe mnaita mwanaume suruale, utaumia sana.

7. Uzuri wa kitandani
Ninaposema uzuri wa kitandani namaanisha kuridhishana katika tendo la kujamiiana, kwa kawaida wanawake ndiyo wahanga wakubwa linapokuja swala la njaa chumbani, wao ndiyo kwa asilimia kubwa hawaridhishwi na wenzi wao katika tendo. Siyo kwamba waume zao wana udhaifu, la hasha, inawezekana wanazo nguvu kama za simba, lakini kwa kawaida tendo la kujamiiana haliwi zuri eti kwa sababu tu mwanaume anazo nguvu kama za simba, bali inahitaji usanii na utundu ukiwemo werevu wa kihisia kuweza kumfikisha mwanamke kileleni. Wanaume wengi kwa sababu ya mazoea wanadhani swala la kumfikisha mwanamke kileleni ni kutwanga kwa kutumia msuli. Si kweli hata kidogo, ni kumuandaa mwanamke kwa maneno matamu kabla hata ya kuelekea kitandani. Kwa hiyo wapo wanaume wenye ufundi huo linapokuja swala la kujamiiana, nia mafundi hodari wenye uwezo wa kuwafikisha wenzi wao peponi, lakini inawezekana katika maeneo mengine ya kimaisha wakawa watupu kabisa. Siyo wawajibikaji, wanyanyasaji wakubwa, hawana staha, hawawaheshimu wenzi wao na ni wenye vurugu kichwani. Wakati mwingine mwanamke anaweza kunasa kwa sababu hiyo tu, ya ufundi wa kitandani, lakini akajikuta anaishi katika machungu kutokana na kutothaminiwa na kunyanyaswa kupita kiasi. Kinachomuweka si kingine ni ile starehe ya muda mfupi wawapo kitandani tu basi. Kuna haja ya kujiuliza, Je ni kitu gani hasa kinachokufanya umpende mwenzi wako? Kama utamkubali na udhaifu wake na una uwezo wa kuhimili hizo tabia zisizofaa kwa maana kwamba hazikuumizi kihisia (kitu ambacho si rahisi sana kwa wanawake) ni sawa, lakini kama huwezi, sikushauri kuingia katika uhusiano wa aina hiyo, kwani ni kujitafutia kaburi la mapema.

Mmea Mkubwa Unaokula Nyama....



Mmea mkubwa unaokula nyama unajulikana kama 'Montane Pitche' wa aina ya 'Nepenthes Rajah' na una urefu wa sentimita 41

Ulionekana Kisiwa cha Borneo mwaka 2011. Mmea huu ambao una kama dibwi (Pitch) unatumia majimaji yake kuwavutia na kuwanasa wadudu warukao kama buibui wakati mwingine hukamata hata mijusi na vyura

Mimea mingine inayokula nyama ni Flypaper Plant, Cobra Lily na Venus Flytrap

Katika yote hiyo uliovunja rekodi ya kula viumbe wakubwa ni huo Nepenthes Rajah ambao umeingia kwenye Rekodi ya Dunia



Marekani yafanya majaribio ya kombora lenye uwezo wa kubeba nyuklia na kusafirisha angani



Mamlaka ya Jeshi la Anga nchini Marekani imetangaza kufanya majaribio hapo jana ya kombora aina ya "Minuteman III" linaloweza kubeba nyuklia na kusafirisha angani.

Kwa mujibu wa maelezo yalitolewa na mamlaka hiyo, iliarifiwa kuwa kombora hilo lililojaribiwa kwenye kambi ya jeshi la anga ya Vandenberg iliyoko California, halikubebeshwa nyuklia wakati wa majaribio.


Maelezo zaidi yalibainisha uwezo na nguvu kubwa ya kijeshi iliyokuwa nayo Marekani, na kuthibitisha kuwa tishio kwa kipindi hiki cha karne ya 21.


Chombo cha kilichotumiwa kubeba kombora hilo hewani, kilisafiri kwa masafa ya maili 4,200 angani hadi kufikia kisiwa cha Kwajelin.


Mamlaka ya jeshi pia iliweza kuchapisha picha za urushaji wa kombora hilo katika mtandao wa kijamii.



Inasikitisha Sana Lakini Inatia Moto....Soma Kisa Hichi



Kijana mmoja wa miaka 24 alikuwa akisafiri yeye na wazazi wake, toka Ifakara kwenda Mlimba kwa usafiri wa treni. Sasa alipojaribu  kuangalia katika dirisha la treni, Mara akahamaki....... _

Akasema:

"Baba angalia, miti inarudi nyuma, tena inarudi Kwa kasi sana.....🌲🌲!!!"


Baba yake akamwangalia Kwa furaha kisha akatabasamu! 


Pembeni kidogo palikuwa na wapenzi wawili waliokaa karibu nao, Wakamuangalia yule kijana wa miaka 24  nakuanza kusemezana wenyewe: "Baby umemsikia uyo kaka, mbona ni mkubwa sana ila anatabia zakijinga ivyo?!"


"Nashangaa ata Mimi, lazima atakuwa anamatatizo ya akili, ndio maana hata Baba yake ahangaiki naye.!"


Waliongea wenyewe.


Ghafla yule kijana akashangaa tena.......!!! Akasema..... "Baba, angalia mawingu nayo yanakimbizana na sisi pia ...☁!!"


Basi wale wapenzi wawili wakashindwa kuvumilia, wakaamua kumwambia yule mzee. 


"Kwanini usimpeleke kijana wako Kwa daktari mzuri, pengine anamatatizo ya akili..?" 

Yule mzee akawaangalia kisha akatabasamu kisha akasema:

"Ndio nimefanya hivyo, hapa tumetoka Kwa daktari pale St. Fransi, ila sio wa akili..!"


Akatulia kidogo kisha akaendelea kusema:

"Mwanangu alizaliwa kipofu, na ameishi akiwa kipofu kwa miaka yote 24. Lakini leo MUNGU ameingilia kati kamfungua macho, na ndio siku yake ya Kwanza kuona kwaiyo tabia zake zinaweza kuwa zakijinga na kero kwenu, ila kwangu ni zaidi ya muujiza ambao sikutegea kabisa...asante MUNGU..!!"


Wale wapenzi wawili wakatulia tulii na kuishiwa maneno huku wakibubujikwa na machozi na aibu machoni mwao huku wameinamisha vichwa vyao chini...! 😭😢


NAKUKUMBUSHA MDAU


Kila mtu katika DUNIA hii ana historia yake, usimuhukumu mtu haraka ikiwa hujui ametokea wapi na amepitia mangapi. Kwani endapo ukijua ukweli wa maisha yake Unaweza kukushangaza, nakukuacha mdomo wazi.  Waheshimu nakuwachukulia wepesi wenzako hata kama wewe una maisha mazuri, kumbuka MWISHO wetu sote ni aridhini. (KIFO) 


NAKUOMBEA NA WEWE MUNGU AKUTENDEE MUUJIZA WA ILO TATIZO LAKO, HAIJALISHI UMEKAA NALO MUDA MREFU KIASI GANI. 

_

Sema "AMEN" Kama Umeguswa.🙏🙏  - #regrann  Reposted from @udakutz_  -  INASIKITISHA SANA LAKINI INATIA MOYO.🙏


Kijana mmoja wa miaka 24 alikuwa akisafiri yeye na wazazi wake, toka Ifakara kwenda Mlimba kwa usafiri wa treni. Sasa alipojaribu  kuangalia katika dirisha la treni, Mara akahamaki....... _

Akasema:

"Baba angalia, miti inarudi nyuma, tena inarudi Kwa kasi sana.....🌲🌲!!!"


Baba yake akamwangalia Kwa furaha kisha akatabasamu! 


Pembeni kidogo palikuwa na wapenzi wawili waliokaa karibu nao, Wakamuangalia yule kijana wa miaka 24  nakuanza kusemezana wenyewe: "Baby umemsikia uyo kaka, mbona ni mkubwa sana ila anatabia zakijinga ivyo?!"


"Nashangaa ata Mimi, lazima atakuwa anamatatizo ya akili, ndio maana hata Baba yake ahangaiki naye.!"


Waliongea wenyewe.


Ghafla yule kijana akashangaa tena.......!!! Akasema..... "Baba, angalia mawingu nayo yanakimbizana na sisi pia ...☁!!"


Basi wale wapenzi wawili wakashindwa kuvumilia, wakaamua kumwambia yule mzee. 


"Kwanini usimpeleke kijana wako Kwa daktari mzuri, pengine anamatatizo ya akili..?" 

Yule mzee akawaangalia kisha akatabasamu kisha akasema:

"Ndio nimefanya hivyo, hapa tumetoka Kwa daktari pale St. Fransi, ila sio wa akili..!"


Akatulia kidogo kisha akaendelea kusema:

"Mwanangu alizaliwa kipofu, na ameishi akiwa kipofu kwa miaka yote 24. Lakini leo MUNGU ameingilia kati kamfungua macho, na ndio siku yake ya Kwanza kuona kwaiyo tabia zake zinaweza kuwa zakijinga na kero kwenu, ila kwangu ni zaidi ya muujiza ambao sikutegea kabisa...asante MUNGU..!!"


Wale wapenzi wawili wakatulia tulii na kuishiwa maneno huku wakibubujikwa na machozi na aibu machoni mwao huku wameinamisha vichwa vyao chini...! 😭😢


NAKUKUMBUSHA MDAU


Kila mtu katika DUNIA hii ana historia yake, usimuhukumu mtu haraka ikiwa hujui ametokea wapi na amepitia mangapi. Kwani endapo ukijua ukweli wa maisha yake Unaweza kukushangaza, nakukuacha mdomo wazi.  Waheshimu nakuwachukulia wepesi wenzako hata kama wewe una maisha mazuri, kumbuka MWISHO wetu sote ni aridhini. (KIFO) 


NAKUOMBEA NA WEWE MUNGU AKUTENDEE MUUJIZA WA ILO TATIZO LAKO, HAIJALISHI UMEKAA NALO MUDA MREFU KIASI GANI. 



Watanzania Milioni 14.8 Hawajapiga Kura Uchaguzi Mkuu 2020



Matokeo ya urais yaliyotangazwa usiku Ijumaa Oktoba 30, 2020 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yanaonyesha kuwa Watanzania milioni 14.8 sawa na asilimia 49.8 hawakujitokeza kupiga kura.


 

Idadi hiyo ya watu milioni 14.8 ni kati ya Watanzania milioni 29.8 waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.


 


Uwiano huo wa watu ambao hawakujitokeza ni mkubwa ikilinganishwa na asilimia 33 ya ambao hawakujitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hata hivyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 waliojiandikisha kupiga kura walikuwa milioni 25.5.


 


NEC imemtangaza mgombea wa CCM, John Magufuli


kuwa mshindi wa kiti cha urais baada ya kupata kura 12,516,252 sawa na asilimia 84.4 kati ya kura halali 14,830,195.


Kwa mujibu wa matokeo hayo mgombea wa Chadema, Tundu Lissu amekuwa mshindi wa pili baada ya kupata kura 1,933,271 na kufuatiwa na mgombea kupitia ACT- Wazalendo, Bernard Membe aliyepata kura 81,129 na Leopord Mahona wa NRA kura 80,787.


 


Matokeo hayo yametangazwa leo usiku jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Semistocles Kaijage aliyebainisha kuwa idadi ya wapiga kura ilikuwa 29,754,699 walioandikishwa katika daftari la kudumu la NEC na lile la Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).


 


“Idadi halisi ya waliopiga kura ni 15,091,950 na idadi ya kura halali ni 14,830,195. Kura zilizokataliwa ni 261,755.”


Nec inamtangaza Magufuli mgombea wa CCM kuwa rais wa Tanzania na Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika uchaguzi wa rais uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu. Baada ya kumtangaza mshindi wa kiti cha urais sasa ni wakati muafaka kwa mawakala kusaini fomu,” amesema Kaijage.


 


Wagombea wengine na idadi ya kura walizopata katika mabano ni John Shibuda wa Ada Tadea (33,086), Muttamwega Mugaywa wa SAU (14,922), Cecilia Mwanga wa Demokrasia Makini (14,556), Yeremia Maganja wa NCCR-Mageuzi (19,969), Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF (72,885).


 


Philipo Fumbo DP (8,283), Queen Sendiga ADC (7,627), Twalib Kadege UPDP (6,194), Hashim Rungwe wa Chaumma (32,878), Khalfan Mohammed Mazrui wa UMD (3,721) na Seif Maalim Seif wa AAFP (4,635).



Waangalizi wa Afrika Mashariki: Uchaguzi wa Tanzania umefanyika kwa kufuata utaratibu zote



Rais wa zamani Silvestre Ntibantunganya ambaye ndiye Mwenyekiti wa ujumbe wa waangalizi kutoka Afrika Mashariki, amesema kuwa uchaguzi mkuu Tanzania ulifanyika kwa kufuata taratibu.




Ujumbe wa waangalizi wa EAC ulikuwa na wajumbe 89 waliosambazwa maeneo mbalimbali , kufuatilia mchakato wa upigaji kura lakini pia utangazaji wa matokeao ya kura hizo.


Bwana Ntabitunganya amesema walikutana na wadau wa uchaguzi ikiwemo tume na vyama vya kisiasa na waangalizi wengine.


Ujumbe huo umesema umeshuhudia hali ya usalama kaika maeneo mbalimbali, watu wakifanya kampeni kwa uhuru kabla ya kuanza shughuli ya upigaji kura.


Katika siku ya kupiga kura vituo vilifunguliwa kwa muda muafaka, masuala ya ya kiufundi yalifanywa kwa weledi.


Waangalizi walishuhudia wapiga kura wakitekeleza wajibu wao bila kutishwa wala hofu.


”Baadhi ya vyama vya siasa au wagombea wamelalamikia kuhusu namna uchaguzi ulivyoandaliwa na namna matokeo yalivyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi.Ujumbe wa waangalizi unatoa wito kwa vyama vya kisiasa, kufuata taratibu za kisheria kuonesha kutoridhishwa kwao na matokeo.


Tunatoa wito kwa vyama vya siasa kuweka mbele maslahi ya Watanzania, ikiwemo usalama na amani na kuepuka vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani”, alisema.


Ujumbe umewapongeza Watanzania kwa busara walioionesha katika shughuli za wakati wa kampeni na uchaguzi kwa kuzingatia kwanza masuala ya amani na usalama.


”Ujumbe unawasisitiza wagombea, vyama vya siasa na wengine wote kuendelea kuimarisha usalama na amani ”. Alisema mwenyekiti wa ujumbe huo Bw. Ntibantunganya.


Mwenyekiti wa taasisi ya EISA Pansy Ntlakula

Ujumbe kutoka taasisi ya uchaguzi na demokrasia endelevu Afrika , EISA, chini ya mwenyekiti wake, Pansy Ntlakula amepongeza serikali ya Tanzania kwa kuendesha uchaguzi wake kwa gharama zao


wenyewe. Lakini pia ripoti yao imegusia makosa ya uchaguzi, yakiwemo katika uhesabu wa kura. Pia ripoti imegusia suala la uwazi na ugumu wa kupata taarifa kipindi cha uchaguzi.


”uchaguzi wa mwaka 2020 upatikanaji wa taarifa umekua mgumu, kuliko uchaguzi uliopita,suala la kuzuia kwa baadhi ya kampeni, kuzimwa kwa baadhi ya mitandao na uhuru wa kujieleza vimebanwa ,kufungwa kwa viongozi wa upinzani, waandishi wa habari, umetengeneza hali ya uoga”. anasema Bi Ntlakula


Kupoteza kwa maisha kutokana na vurugu za uchaguzi, hususani visiwani Zanzibar ni saula ambalo limegusia pia katika ripoti yao.


Miongoni mwa mapendekeo ya ujumbe huu ni kuwa tume ya taifa ya uchaguzi iundwe kwa mfumo unaohusisha watumishi wake kupitishwa na bunge.


”Serikali inatakiwa kuhakikisha watumishi wa tume ya taifa wanachunjwa na bunge’. anasema Bi Ntlakula



Manchester United vs Arsenal, moja ya mechi zinazovutia wiki hii!!

 *Premier League Kuendelea Jumapili Hii – Red Devils kuwakaribisha Arsenal pale Old Trafford

Jumapili ni siku nzuri ikipambwa na soka lenye viwango thabiti katika Ligi ya Uingereza – EPL! Kuna kitu kizuri zaidi ya soka la Uingereza?

Jumapili hii majira ya saa 1:30 usiku moja kati ya mchezo unaovutia kwenye wiki ya 7 ya EPL ni mchezo kati ya Manchester United vs Arsenal.


Manchester United na Arsenal wameshakutana mara nyingi ndani ya miaka 10 iliyopita. Wanapimana nguvu katika viwanja vyote – Old Trafford na Emirates. 2019, matokeo ya timu zote ni kama yalikuwa yanafanana.

Tukiongelea mwenendo wa sasa, “Red Devils” hawajauanza vizuri msimu huu. Vipindi vigumu vya msimu uliopita vinaifanya timu mashuhuri kuwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi wakiwa wameshinda michezo miwili, wamepoteza miwili na kutoka sare mchezo mmoja. 


Japokuwa, lazima tukumbuke Man United wanapungufu ya mchezo mmoja ikilinganishwa na timu nyingi za EPL.


Upande wa pili, “The Gunners” kwa kiasi fulani wanahali nzuri kulinganishwa na wapinzani wao. Wakiwa na ushindi wa michezo mitatu na kupoteza kadhaa, kwa sasa wapo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi.


Japokuwa, Arsenal hawawezi kuridhika na kiwango walichokionesha mpaka sasa, hasa kama wanamalengo makubwa ambayo kimsingi ndivyo hali ilivyo.

Kutokana na kuanza msimu vibaya na kawaida ya kuziona timu hizi kwenye nafasi za juu za msimamo wa ligi, itakuwa ni jambo la kuvutia kuangalia mechi ambayo wenyeji wamepatiwa faida kidogo (1X na GG).


Kama ilivyokawaida, mashindano yakiwa yanaendelea kwenye Premier League, duka la Meridian bet ni sehemu utakayoweza kufuatilia kila kinachoendelea.


Pamoja na mchezo huu, kunamichezo mingine kibao inayochezwa katika wiki ya 7 ya Ligi ya Uingereza - EPL, unaweza kujionea odds za michezo hiyo kwa kubofya hapa.


Jisajili na Meridiabet hapa http://www.meridianbet.co.tz na furaha yako itaanzia hapo. Pakua App ya Meridianbet kwenye simu yako na uanze kubashiri kwa uhuru nyumbani kwako. Pia, unaweza kuweka pesa kwenye akaunti yako kupitia KwikPay, M-PESA au Airtel Money. Kumbuka, daima hauwezi kupoteza tiketi yako ya kwanza ukiwa na Meridianbet, tuna Bonasi ya 100% inakusubiri.


Meridian - Nyumba yenye odds bora na bonasi kubwa!




Polisi Shinyanga Wachunguza Jaribio La Kuchoma Moto Nyumba Ya Mbunge Mteule wa CCM, Patrobas Katambi


 JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio la jaribio la kuchoma moto nyumba ya Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi (CCM) iliyopo mtaa wa Ushirika Mjini Shinyanga.

Pia limemkamata aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA Salome Makamba na mdogo wake Timoth Makamba wakihusishwa na tukio hilo.

Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari  Oktoba 30,2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa sita na dakika 45.

 “Majira ya saa saba kasorobo, Mbunge Mteule Patrobas Katambi akiwa amelala  nyumbani na ndugu zake walisikia kishindo juu ya paa la choo cha nje ambacho kipo katika eneo la uzio wa nyumba hiyo ndipo walipotoka nje na kuona moto ukiwaka juu ya paa la choo pamoja na dumu lenye mafuta aina ya petroli”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Wakati  wakiendelea kuzima moto huo waliona gari aina ya Toyota Klugger lenye rangi ya silver likikimbiliwa na watu wawili na kisha watu wale waliingia ndani ya gari lile na kutoweka”,amesema Kamanda Magiligimba.

Kamanda Magiligimba amesema baada ya kufanikiwa kuzima moto huo waliona gari lile lile likipita barabara ya lami ya Shinyanga – Mwanza ndipo walipoamua kulifuatilia na dereva wa gari hilo baada ya kugundua anafuatiliwa aliamua kuingia hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na kuliacha gari hilo kisha kukimbia.

“Wakati wa kuwaweka chini ya ulinzi watu hao ilitokea purukushani ndani ya uzio wa hospitali na gari ya polisi iliyokuwa doria ilifika mapema na kufanikiwa kuwakamata watu wawili ambao ni Wilson Mhando Suluti (30) mkazi wa Bugweto na Jackson Raphael Peter (27) mkazi wa Bugweto wakiwa ndani gari hilo lenye namba za usajili T 729 DFP aina ya Toyota Klugger rangi ya Silver mali ya Salome Makamba aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA”,amefafanua Kamanda Magiligimba.

“Ilibainika kuwa watu hao tuliowakamata wao ndiyo waliokuwa kwenye eneo la tukio kulingana na mavazi waliyovaa. Baada ya mahojiano, watu hao walikiri kuwa gari hilo ni la Salome Makamba na dereva aliyetoroka ni Timoth Makamba ambaye ni mdogo wake Salome Makamba”,ameongeza.

Amesema polisi walifika nyumbani kwa Salome Makamba na kufanya upekuzi kisha kuwakamata watu wengine wawili ambao ni Justine Owesiga (35) Mkazi wa Ndala Shinyanga na Gibson Mkongwa (31) mkazi wa Iringa waliokutwa kwenye nyumba hiyo.

“Juhudi za kuwatafuta na kuwakamata Salome Makamba na Timoth Makamba ambaye ndiye dereva wa gari hilo lililotelekezwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga zinaendelea. Gari husika linashikiliwa na watuhumiwa hao wanne na watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika”,amesema.

Amesema Salome Makamba aliachiwa jana kwa dhamana baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi Oktoba 28,2020 kwa tuhuma za kumshambulia msimamizi wa uchaguzi kituo cha kupigia kura cha Bugweto B, Farida John na kumuumiza ambapo aliomba aone matokeo na baada ya kutoridhika nayo aliyachana na kuanza kumshambulia msimamizi huyo wa uchaguzi akiwa na wafuasi wake.


Marekani yafanya majaribio ya kombora lenye uwezo wa kubeba nyuklia na kusafirisha angani


Mamlaka ya Jeshi la Anga nchini Marekani imetangaza kufanya majaribio hapo jana ya kombora aina ya "Minuteman III" linaloweza kubeba nyuklia na kusafirisha angani.

Kwa mujibu wa maelezo yalitolewa na mamlaka hiyo, iliarifiwa kuwa kombora hilo lililojaribiwa kwenye kambi ya jeshi la anga ya Vandenberg iliyoko California, halikubebeshwa nyuklia wakati wa majaribio.

Maelezo zaidi yalibainisha uwezo na nguvu kubwa ya kijeshi iliyokuwa nayo Marekani, na kuthibitisha kuwa tishio kwa kipindi hiki cha karne ya 21.

Chombo cha kilichotumiwa kubeba kombora hilo hewani, kilisafiri kwa masafa ya maili 4,200 angani hadi kufikia kisiwa cha Kwajelin.

Mamlaka ya jeshi pia iliweza kuchapisha picha za urushaji wa kombora hilo katika mtandao wa kijamii.




Mshukiwa mmoja wa kesi ya shambulizi la kisu akamatwa nchini Ufaransa


Mtu mmoja anayedaiwa kuhusika na shambulizi la kisu lililopelekea watu 3 kufariki kwa kuchomwa kisu hapo jana mjini Nice,  ameripotiwa kukamatwa na maafisa wa usalama.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Kifaransa, imeripotiwa kukamatwa kwa mtu mmoja mwenye umri wa miaka 47, anayedaiwa kufanya mawasiliano na mshambuliaji wa kanisa la Notre-Dame mjini Nice.

Mwendesha Mashtaka wa Mapambano dhidi ya Ugaidi nchini Ufaransa Jean-Francois Ricard, alibainisha mhusika wa shambulizi hilo kuwa kijana wa miaka 21 kutoka Tunsia, aliyesafiri kisiwa cha Lempedusa nchini Italy tarehe 20 Septemba, na baadaye akaingia Ufaransa tarehe 9 Oktoba.

Hapo jana nyakati za asubuhi, kanisa la Notre-Dame mjini Nice lilishambuliwa ambapo watu 3 walipoteza maisha baada ya kuchomwa kisu, huku wengine wengi wakijeruhiwa.

Baada ya mshambuliaji kukamatwa, alifikishwa hospitali na baadaye uchunguzi ukaanzisha na Mwendesha Mashtaka wa Mapambano dhidi ya Ugaidi.

Nchi nzima ya Ufaransa imeweka mchakato wa kupambana na ugaidi kuwa suala la shambulio la dharura.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitoa maelezo hapo jana na kusema kuwa ataongeza idadi ya wanajeshi kwenye operesheni ya "Sentinelle" ya kushika doria, na kuimarisha usalama katika sehemu za ibada na mashuleni.




Hii hapa ratiba ya leo ya ligi kuu

 


LEO Oktoba 31 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kushika kasi ambapo mechi nne zitachezwa kwa timu nane kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.

Tanzania Prisons v Polisi Tanzania, Uwanja wa Nelson Mandela, saa 8:00 mchana

Namungo FC v Dodoma Jiji, Uwanja wa Majaliwa, saa 10:00 jioni.

Biashara United v Yanga, Uwanja wa Karume, saa 10:00 jioni.

Simba v Mwadui,saa 10:00 jioni, Uwanja wa Uhuru.



Twaha Kiduku ampiga mbabe wa Tinampay


Bondia Mtanzania Twaha Kiduku (28) amefanikiwa kumpiga TKO round ya 7 bondia wa Thailand Sirimongkhon (43) katika pambano lililochezwa uwanja wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Twaha anakuwa Bondia wa pili kumpiga TKO bondia Sirimongkhon ambaye leo lilikuwa ni pambano lake la 5 kupoteza katika mapambano yake 102 aliyocheza na kushinda 97.

Sirimongkhon ni bondia mwenye CV kubwa aliwahi kumpiga Arnel Tinampay ambaye aliwahi kucheza na Hassan Mwakinyo, hata hivyo Sirimongkhon alikubali yaishe baada ya kuumia puani lakini na bega lake kutokuwa sawa.



Twaha Kiduku Ambomoa Mthailand kwa TKO, Amtaka Mwakinyo – Video



Bondia Mtanzania, Twaha Kiduku amemtwanga bondia Sorimongkhon kutoka Thailand kwa TKO raundi ya saba








Mimba ya Aunt Hatarini!



KITENDO cha staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel kunaswa ‘club’ ya starehe ya usiku akigida pombe za hatari ilihali ni mjamzito wa kujifungua muda wowote, kimeibua gumzo kubwa juu ya hatari ya kuchoropoka kwa mimba hiyo.

Wikiendi iliyopita, Aunt alinaswa akitandika bia kama zote kwenye Club ya The Base iliyopo Makumbusho jijini Dar, usiku wa manane ambapo kulikuwa na shoo ya msanii wa Bongo Fleva anayedaiwa ndiye mwenye ujauzito huo aitwaye Salmin Said ‘Kusah’.

Bila kujali ukubwa wa kitumbo chake, pia Aunt ndiye alikuwa MC wa shoo hiyo kabla ya kuweka kambi kwenye moja ya kona na kuanza kutandika ulabu aina ya bia ambazo zina sifa ya kuwa na kilevi kikubwa.

Hata hivyo, baada ya ishu hiyo kuibua mjadala mkali, gazeti hili liliibeba hadi kwa daktari ambaye amefunguka kinagaubaga juu ya madhara ya unywaji wa pombe kwa mwanamke mjamzito kama Aunt. Dk Geofrey Charles ‘Dk Chale’ ni daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na watoto ambaye anasema kuwa, mama kutumia kilevi wakati wa ujauzito, kunaweza kusababisha mimba kutoka au kuzaa mtoto ambaye ana matatizo hivyo kwa staa huyo kunywa pombe hadharani na hata mafichoni siyo sahihi.

“Hakuna sehemu yoyote inayoruhusu mjamzito kunywa pombe hata kidogo. Ni hatari kwa afya ya mtoto aliyepo tumboni, lakini pia kuna uwezekano mkubwa wa mimba kutoka,” anasema Dkt. Chale akimtahadharisha Aunt kuachana na pombe kwenye kipindi hiki cha ujauzito na kuongeza;

“Anatakiwa aelewe kwamba pombe ni sumu kwa mtoto. Mjamzito anapokunywa pombe inaingia moja kwa moja kwenye mzunguko wa damu wa mama kisha hufika kwa mtoto kupitia kondo la nyuma (placenta).


“Pombe inapoingia kwenye mzunguko wa damu wa mtoto, huathiri uwezo wa mtoto kupata chakula, virutubisho na oksijeni ya kutosha kwa ajili ya maendeleo ya kawaida katika ubongo na viungo vingine. Hii inaweza kuathiri ubongo wa mtoto na ukuaji wa viungo vya mwili kwa jumla.

“Uharibifu huu unaweza kuathiri uwezo wa mtoto kujifunza na kufikiri pale anapozaliwa, hali ambayo itajionesha kwa matendo yake kama mtoto na kama mtu mzima.


“Utafiti unaonesha kwamba, uwezo wa mimba kustahimili kiwango cha pombe ni mdogo mno hali ambayo huathiri ufanyikaji wa viungo na ukuaji wake kwa kiasi kikubwa, hivyo kunakuwa na hatari ya mimba kutoka.

“Kama mtoto akizaliwa, madhara haya yanaweza kusababisha kifo kwa mtoto, malezi na makuzi ya taabu na hata hisia mbalimbali katika maisha.

“Kwa mjamzito yeyote, ni vizuri kuacha kunywa pombe.”

Kwa upande wake, Aunt, katika mazungumzo na gazeti hili juu ya ishu hiyo, alisema kuwa anachojua pombe inaongeza damu.


“Mimi ninachojua pombe inaongeza damu siku zote, kwa hiyo ninakunywa kwa afya na siyo kupitiliza kama watu wanavyofikiria,” anasema Aunt ambaye anatarajia kupata mtoto wa pili baada ya yule wa kwanza, Cookies aliyezaa na Moze Iyobo.



Friday, October 30, 2020

JESHI LA DAR WAONYA..."OLE WAO WANAOPANGA KUINGIA BARABARANI KUANDAMANA, KITAKACHOWATA WATAJUTA"



Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa onyo kali kwa mtu, watu au kikundi chochote cha watu ambao wanapanga kuingia barabarani kuandamana kwani halitawaachia na kitakachowatokea wasijutie.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari jioni ya leo Oktoba 30,2020 kwamba wanazo taarifa kuna watu wamekaa vikao vya siri wakipanga mipango ya kuingia barabarani kuandamana.

Amefafanua uchaguzi ulikuwa umamalizila salama na amani lakini baada ya matokeo kuanza kutangazwa vimeibuka  vikundi vya watu wengine wakiwamo waliogombea  nafasi mbalimbali ambao wanaendelea kufanya vikao ya siri lakini mipango yao ni kutaka kwanza kuingilia mchakato wa  kutangaza matokeo hayo yanayoendelea.

Pia wanajaribu kuhamasisha wafuasi wao kuingia mtaani , na jambo linaloshangaza kufanya hivyo wengine wanaopanga mipango hiyo wameshindwa Hai, wameshindwa Kilimanjaro, wameshindwa Arusha lakini wamejikusanya  jijini Dar es Salaam kama eneo ambalo ni shamba la bibi, wanataka kufanya vurugu.

"Nimekuja kwa umma kutoa onyo kwao , kipindi cha kampeni ambacho tulikuwa wastaarabu sana ,tumewapa nafasi ya kunadi sera zao, na kipindi hiko kimeshikwa ,sasa tuko katika kutekeleza dhima na dhumuni la Jeshi la Polisi ambalo ni kulinda maisha ya watu na mali lakini ni pamoja na kuwalinda viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ambao wanaendelea kukamilisha matokeo kwenye majimbo ambayo nafas ya urais yanaendelea kutolewa.

"Nitoe onyo wananchi mnaokaa Dar es Salaam wapuuzeni ,anayetaka kuingia mtaani aingie yeye, kama ana mke atangulize mke wake, kama ni mme atangulie yeye , tukutane naye tumejipanga na hatuna mjadala katika hili, tunachotaka kuhakikishia watanzania wote wanaokaa Dar es Salaam , mko salama na jeshi limesimama na linaendelea kufanya kazi yake, tumezunguka maeneo yote, tumekaa kuhakikisha mtu atakayeachiwa afanye lile analolifikiria.

"Niwaombe wale ambao watapata taarifa watu kutaka kuingia barabarani watupe taarifa mapema, tunaendelea kufuatilia lakini mahali popote watakapoanzia tutawa labda umbali wa hatua 10 na wasijutie kitakachowapata , kwasababu tumeamua kuhakikisha hatuwapi nafasi kuchezea demokrasia hii ambayo kimsingi kinachotangazwa ni maamuzi ya wananchi wenyewe,"amesema.

Amesisitiza hakuna sababu ya kwenda kugombea kama hauko tayari kushinda au kushindwa, yoyote anayeingia kwenye ushindani ategemee mawili, kupewa ama kukosa,waliokosa basi wavumilie na wanakatibishwa mwaka 2025 lakini kwa sasa mchezo wa kampeni kushawishi,kuvuruga havina nafasi."Hayo ndio maamuzi ya Watanzania ,yanayoendelea kutangazwa ni lazima tuyaheshimu na yoyote atakayepuuza asilie na kile atakachokutana nacho.Tumesimama kuhakikisha hatumuachii mtu nafasi ya kufanya lolote, na narudia tena mtu asijutie kwa lile atakalokutana nalo.

" Niwaombe watanzania wote wapuuze vitendo vya kuingia barabarani havina afya,havina baraka, lakini pia vinakinzana na demokrasia  yenyewe ,wananchi wameamua halafu unataka wagomee,unagomea ili umuongoze nani".



Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...