Search This Blog

Wednesday, June 30, 2021

Mfugale kuzikwa Jumatatu Iringa


Mwili wa aliyekuwa  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale utazikwa  Julai 5, 2021 nyumbani kwake Ifunda mkoani Iringa.

Mfugale alifariki dunia Jumanne Juni 29, 2021 saa 5 asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi, mwili wa Mfugale unatarajiwa kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam Alhamisi Julai Mosi, 2021 ukitokea Dodoma na kupelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Ijumaa Julai 2, 2021 mwili utatolewa hospitalini hapo na kupelekwa viwanja vya Karimjee ambapo wafanyakazi wa Tanroads na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi watatoa heshima zao za mwisho kisha utapelekwa Kimara Temboni nyumbani kwake.

Baada ya misa takatifu siku ya Jumamosi Julai 3, 2021 mwili wa Mfugale utasafirishwa kwenda Ifunda mkoani Iringa ambapo unatarajiwa kuwasili Julai 4 na maziko yatafanyika Julai 5, 2021 nyumbani kwake Ifunda.



Wanajeshi wa Senegal wahitimu mafunzo ya Kituruki


Kituo cha Mafunzo cha Kituruki kinachofungamana na Taasisi ya Yunus Emre (YEE) kilichoko Cap Manuel Barracks huko Dakar, mji mkuu wa Senegal, kilitoa wahitimu wake wa tatu.

Balozi wa Uturuki huko Dakar Ahmet Kavas, Kiongozi wa Jeshi la Dakar Kanali Levent Güldağı, Mkurugenzi wa YEE Dakar Merve Işık Elsıkma, Meneja wa Tawi la Mafunzo ya Kijeshi la Senegal Kanali Yahya Diop na wawakilishi wa taasisi za Uturuki walihudhuria sherehe ya kufunga na kuhitimu kozi ya tatu ya Uturuki iliyofanyika kambini.

Katika hotuba yake, Balozi Kavas alikumbusha kuwa Uturuki ina balozi 43 barani Afrika na akasema kuwa ushirikiano wa Uturuki na bara hilo unaongezeka siku baada ya siku.

Akisisitiza kuwa ushirikiano huu unaendelea sio tu kwa maana ya kibiashara lakini pia katika hali ya kitamaduni, Kavas pia alisema kuwa YEE ndio mfano bora na aliwapongeza wanajeshi ambao walipokea vyeti vyao.

Wanajeshi 25 waliofanikiwa kumaliza kozi ya miezi 9 ya Kituruki iliyoanza mnamo Oktoba 2020 walikabidhiwa vyeti vyao na Mkufunzi wa YEE Emran İpek.

Wanafunzi walimshukuru İpek na wakampa zawadi.



Xi Jinping: China haiwezi kurudi nyuma


Chama cha Kikomunisti cha China leo kimeadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake kwa kuruka kwa ndege za kivita na helikopta juu na hotuba kali ya Rais Xi Jinping wa taifa hilo.

Akizungumza kwa sauti yenye kuonesha majigambo katika moja katika hotuba kubwa ya kuadhimisha sherehe za miaka 100 ya chama tawala cha taifa lake, Chama cha Kikomunisti (CCP) huko mjini Beijing, kiongozi huyo aliuambia umma wa watu kwamba taifa hilo la Asia limeanza uelekeo wa kihistoria wa mabadiliko yasiyoweza kubadilishwa.

Amesema zile zama za China kuchinjwa na kuoneswa zimekwisha pita daima. Huku akishangiliwa kwa makofi kiongozi huyo aliendelea kwa kutoa onyo kwamba yeyote ambae atathubutu atakaejaribu kufanya hivyo dhidi ya umma wa wachina wanaopindukia bilioni 1.4 atakumbana na kizingiti kikali zaidi.

Zaidi kiongozi huyo mwenye nguvu amesema "Watu wa China, ni watu wanaopenda haki lakini hawaofii machafuko. Taifa la China ni taifa lenye hisia kali za kujivunia utaifa wake na kujiamini. Watu wa China hawajawahi kuonea, kudhulumu au kuwatumikisha watu wa mataifa mengine."

Aidha ameongeza kusema hawajawahi kufanya hivyo katika siku za nyumna, hawawezi kufanya sasa na wala katika siku za baadae. Katika hafla hiyo pia amekimpongeza Chama cha Kikomunisti kwa kufanikiwa kuwaondoa mamilioni ya raia swa China kutoka katika lindi la umasikini akisema watu wa China si tu wajuzi katika kuitokomeza dunia ya zamani lakini pia wapo vyema katika kuunda ulimwengu mpya.

Kuhusiana na suala la usalama Xi amesema taifa hilo kwa sasa linapasswa kuongeza kasi ya kufanya mageuzi ya kisasa katika ulinzi wake na jeshi. Na juu ya Taiwain anataka kufanikisha hatua ya kuungana tena na kupinga juhudi zozote za kukipa uhuru kisiwa hicho kutoka China Bara.

Tofauti na hotuba hiyo ya Rais Xi Jinping hafla hiyo ya maadhimisho ya miaka 100 Chama cha Kikomunisti cha China imefanikishwa na ushiriki wa maelfu ya waimbaji, ambao walijunga pamoja katika uwanja wa Tiananmen na kuimba nyimbo za kizalendo.

Miongoni mwa nyimbo ambayo zilizoimbwa ni pamoja na ile iliyopewa jina la "Bila ya Chama cha Kikomunisti, hakutakuwa na China Mpya." Aliyekuwa mwenyekiti wa chama na kiongozi mwenye nguvu zaidi Mao Zedong alianzisha Jamhuri ya Watu wa China mnamo 1949 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Na rekodi za sasa chama hicho kinaonesha kuwa na jumla ya wanachama milioni 95 nchini China.



Pakistan yaishutumu India kwa kuvuruga uhusiano wao na Afghanistan


Rais wa Pakistan Arif Alvi ameishutumu serikali ya India kwa kujaribu kuvuruga uhusiano kati ya Islamabad na Kabul.

Alvi alizungumza na vyombo vya habari vya India na kusema kwamba India inataka kutengeza hali ya ukosefu wa maelewano na Pakistan nchini Afghanistan.

Akibainisha kuwa India ina jukumu la kusababisha usumbufu, Alvi alisema kwamba New Delhi kwa muda mrefu imekuwa ikitaka kuvuruga uhusiano kati ya Islamabad na Kabul.

Alvi pia alitoa jibu kwa Mshauri wa Usalama wa Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani, Hamdullah Muhib, kwa taarifa zake dhidi ya Pakistan na kukumbusha kuwa nchi yake inahifadhi wakimbizi milioni 3,5 wa Afghanistan.

Akisisitiza kwamba maafisa wa serikali ya Afghanistan wanapaswa kutoa matamshi kwa umakini, Alvi pia alisema kuwa hawapaswi kulaumu Pakistan kwa makosa yao wenyewe.

Muhib, Mshauri wa Usalama kwa Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani, na maafisa wengine wa Afghanistan walitoa taarifa kwamba Pakistan ilihusika na wimbi la mashambulizi yaliyofanywa na Taliban dhidi ya vikosi vya usalama.

Pakistan, kwa upande mwingine, ilijibu maoni haya na maafisa wa Afghanistan na wakakanusha madai hayo.



Tetesi za soka kimataifa


 Huku makubaliano ya kumsaini winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho yakiafikiwa , kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice ,22, beki wa Villareal mwenye umri wa miaka 24 Pau Torres na mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane 27 , ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer (Guardian)

Sancho atapatiwa jezi nambari saba katika klabu ya Manchester United ambayo kwa sasa inavaliwa na mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34. (Metro)

United pia ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich Leon Goretzka, 26, ambaye kandarasi yake na klabu hiyo ya Bundesliga inakamilika 2022.. (Bild - in German)

Hatahivyo , United na Liverpool huenda wakamkosa winga wa Ufaransa Kingsley Coman baada ya Bayern Munich kusema kwamba anaweza kuuzwa kwa bei ya £77m. (Bild)

Tottenham imemuajiri aliyekuwa mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo kuwa mkufunzi mpya kwa kandarasi ya miaka miwili .

Nuno aliondoka Wolves mnamo mwezi Mei baada ya misimu minne ambapo alionesha umahiri wake wa kazi hiyo ambapo alifanikiwa kuipandisha klabu hiyo kutoka ligi ya mabingwa hadi kufuzu robo fainali ya kombe la Europa.

Manchester City ina mpango wa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa England Raheem Sterling kuhusu hatma yake , huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake na mabingwa hao wa ligi ya Uingereza.. (Mail)

Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi amechukua nafasi ya mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo Leonardo katika mazungumzo ya kumshawishi mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe kuongeza mkataba wake na klabu hiyo. Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 inakamilika 2022.. (L'Equipe, via Get French Football News)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ana Imani kwamba The Blues inaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 20, mwisho wa msimu huu . (Express)

Mchezaji wa timu ya Portugal ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Nuno Tavares, 21, atafanyiwa uchunguzi wa matibabu katika klabu ya Arsenal kabla ya kujiunga na The Gunners kwa dau la £7m kutoka Benfica. (Goal)

Chelsea wamewasilisha ombi la mwisho kumsaini mshambuliaji wa Manchester United Lauren James, 19, dadake beki wa Blues Reece James. (Goal)

Leicester inakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan katika kinyang'aanyiro cha kumsaini winga wa Itali na Sassuolo Domenico Berardi, 26, ambaye amewavutia the Azzurri katika michuano ya 2020. (Corriere dello Sport - in Italian)

Newcastle United wamewasilisha ombi la £1.5m kumnunua beki wa Wolves Dion Sanderson huku wakishindana na Sunderland kumsaini mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 21 (Mail)

Klabu ya RB Leipzig itamuwacha kiungo wa kati wa Austria Marcel Sabitzer kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu kwa bei ya chini huku Arsenal, AC Milan na Roma zote zikimuwania kiungo huyo mchezeshaji mwenye urmi wa miaka 27.. (Bild - in German)

Nahodha wa klabu ya Rangers James Tavernier ananyatiwa na Manchester United, Brighton, Norwich na Arsenal. Mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 29 alitia saini kandarasi mpya mwezi Aprili , inayomfanya kusalia katika klabu hiyo hadi 2024. (90min)



MAGAZETI YA LEO 1.7.2021


















 

Jifunze namna ya kumuacha mpenzi wako kistrabu

 


Inapofika mahali umemchoka mpenzi wako ni bora umwambie kwa maneno matupu tena ya bila kupindisha kwamba nimekuchoka sikutaki tena sitaki mahusiano na wewe tena nenda zako, ukieleza kifupi hivyo utaeleweka vizuri tu na kama huyo unaemwambia ana akili timamu wala hawezi kuendelea tena na mahusiano na wewe au kukulilia kama vile wewe ni mungu kwake ikiwa umemtamkia maneno mazito kama hayo.

Lakini tabia ya kuachana kwa maneno mazito yenye matusi mazito mazito yanayohusisha mpaka na wazazi na ndugu wengine ambao hawayajui hata mahusiano yenu tabia hii huwa sio nzuri kabisa, kwanza inaonyesha hujakua hata kidogo na akili yako finyu na ndogo kama tonge la ugali wa mtama.

Mwanamke au mwanaume aliekuwa ki akili cha kwanza ni lazima kinywa chake kiumbwe na maneno ya busara, hekima na adabu, no matter how/haijalishi mmeudhiana vipi katika mahusiano na mmefikia stage ya kuachana ni lazima muachane kwa busara, tabia ya kukamuliana matusi kama chunisi dume au ndimu kwenye samaki kukata shombo inaprove kwamba wewe ni zero brain kiasi gani katika maisha yako.

Busta Rhymes ameshare Video akiwa Diamond "Wewe ni Michael Jackson wa Afrika"

 


Rapa Legendary tokea nchini Marekani Busta Rhymes ameshare Video akiwa na Simba Diamond Platnumz wakiwa Studio na Kumwagia Sifa kibao ikiwemo kumuita 'Michael Jackson of Africa ' / Yaani Michael Jackson wa Afrika .

Katika Video hiyo ambayo wanaonekana kama wanasuka Mdundo wa Pamoja, wameonekana Mastaa wengine akiwemo Thereal swizzz , @hitmaka na @otgenasis .

Diamond amedai kuwa Atakua nchini Marekani kwa Muda ili kuandaa Album yake, ambayo Producer wake Mkuu anatokea nchini humo (Hakutaja Jina Lake ) .

Huu ni Muendelezo wa Harakati za Diamond Platnumz kuhakikisha anauvusha Muziki wa Afrika Mashariki Duniani 



Simba yaingia kambini kuiwinda Yanga


Kikosi cha Simba kimeingia kambini jana kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi wiki hii, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, amesema timu hiyo ilianza mazoezi jana jioni kwenye viwanja vya Mo Simba Arena na jana asubuhi kuingia kambini.



RUWASA yaombwa kuondoa tenki kwenye mkondo wa njia ya mizimu ya SABURE


Na Timothy Itembe Mara.

RUWASA wanaombwa kuondoa Tenki la maji kwenye mkondo wa njia ya (SABURE)ambaye ni mkuu wa koo ya Wanchari.

Mwenyekti wa Jumuiya ya watumia Maji Korotambe kata ya Mwema wilayani Tarime,Alphons Nyaiho alisema kuwa Ruwasa walijenga Tenki la maji kwenye mkondo wa njia ya Sabure ambaye ni mkuu (MZIMU)wa  koo ya Wanchari kabIla la Wakurya bila kuwashirikisha wazee wa milahali ambayo imechangia mradi huo kutotoa maji.

Nyaiho aliongeza kusema kuwa kufuatia hali hiyo mradi wa Korotambe umekumbwa na changamoto kubwa ya kukoswa maji licha ya kuwa mradi umekamilika na wananchi hawafaidi matunda ya mradi huo kwa mda wa zaidi ya mwaka."Mimi niseme kuwa wananchi wa Korotambe wanataabika kwa kutofaidi mradi wao wa maji ambao ulianza mwaka 2012 na kukamilika 2020 kutokana na Ruwasa kujenga Tenki la maji kwenye mkondo wa njia ya Sabure ambaye ni mkuu wa koo ya Wanchari bila kuwashirikisha wazee wa mila hali ambayo imechangia mradi kutokuwa namaji licha ya kuwa umekamilika"alisema Mwenyekiti huyo.

Baada ya hali hiyo kuwepo Kamati ya watumia maji wakishirikiana na Ruwasa waliomba kuonana na wazee wa mila ambapo wazee hao waliomba vifaa kadhaa wakadha  vya kimila ikiwemo Mbuzi wa kafara na kufanya matambiko lakini hapo pote mradi hautoi maji na badala yake mradi unaingiza hasara pale ambapo shilingi zaidi ya Alfu themanini zinatumika kwa kupambu maji kwenda kwenye Tanki na kesho yake unakuta maji yamekwisha kwenye Tenki bila kutumiwa na mtu.

Nyaiho alibainisha kuwa wanatumia zaidi ya shilingi 80,000 kupambu maji kwenda kwenye Tanki lakini kesho yake wanajikuta maji yameisha bila kutumiwa na mtu na katika kitendo hicho Jumuiya inaambulia mavuno ya maji ya shilingi 5000 tu ambayo wanauza jambo ambalo ni hasara wanaomba msaada zaidi wa kiutaalamu.

Kwa upande wake Patirisia Joseph kutoka Nyamwaga alitumia nafasi hiyo kuwatupia lawama viongozi wa vijiji na kata kwa maana ya watendaji na wenyeviti  kuwa hawatoi ushirikiano kwa jumuiya ya watumia maji jambo ambalo linasababisha mradi kukwama na kushindwa kujiendesha.

Mwana mama huyo aliwataka watu wa Ruwasa kuendelea kutoa elimu ndani ya viongozi na jamii iliyopo ili kuendelea kutoa ushirikiano kwa lengo la kufanikisha malengo ya mradi kwa manufaa ya Taifa na jamii kwa ujumla.

Naye Katibu Tawala wilaya Tarime,John Mrwa kwaniaba ya mkuu wa wilaya ambaye alialikwa kuwa mgeni rasimi katika kikao cha wadau wa Maji kilichoketi katika ukumbi wa Chuo cha walimu TTC  Tarime alisema kuwa Serikali inapotekeleza miradi kwa jamii lengwa inamaana miradi hiyo iwanufaishe wanajamii siovinginevyo.

Marwa aliongeza kusema Jamii inatakiwa kulinda na kutunza miundombinu ya mradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwa manufaa yao na vizazi vijavyo vinginevyo kama kuna anaye husika kuhujumu mradi kuna haja ya kumtambua ili kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kaimu Meneja Ruwasa,Laurenti Biseko alisema katika kuhakikisha vyombo vya watumia maji vinatoa huduma stahiki kwa mjibu wa sheria ya maji na usafi wa mazingira namba 5(2019)Ruwasa Tarime hufanya ufuatiliaji wa vyombo na shuguli zinazotekelezwa.



IMF yaindhinisha mkopo wa bilioni 2.5 kwa Sudan


Shirika la Fedha Duniani IMF limeidhinisha mkopo wa kiasi cha dola bilioni 2.5 kwa Sudan, na pia Benki ya Dunia imesaini makubaliano ya kihistoria ya kutoa unafuu wa punguzo la deni la karibu dola bilioni 50 kwa taifa hilo masikini.

Tangazo hilo linatolewa baada ya IMF kuhitimisha makubaliano ya mataifa wahisani 101, ambayo yameiruhusu Sudan kufuta kiasi cha deni cha takribani dola bilioni 1.4, hatua ambayo italifanya taifa hilo liweze kupata msaada mpya.



Basi lagonga nyumba Mwanza


Basi kampuni ya Ulamaa T 330 DGB ililokuwa likisafiri kwenda Arusha kutokea Mwanza limepata ajali alfajiri ya leo kwa kuacha njia na kugonga nyumba eneo la Mkolani darajani Mwanza.

Imeelezwa kwamba ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na Watu 6 ambapo hakuna taarifa za kifo bali Majeruhi tu ambao wamepelekwa Hospitali ya Butimba.

Chanzo cha ajali kinaelezwa kuwa ni baada ya Dereva wa Basi kulikwepa gari dogo kulikosababisha gari kuacha njia baada ya kushindwa kulimudu, taarifa zaidi kukujia.


 



MIZIZI 29 POWER NI DAWA BORA NA IMALA YA KUTIBU TATIZO LA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KAMA VILE KUSHINDWA KURUDIA TENDO NA KUKOJOA MAPEMA

                   


Tatizo hili limekuwaasili watu wengi,sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine, kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo zipo , sababu nyingi zinazosababisha, tatizo hilo baadhi ni


(i) upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN ambazo mwanaume, anapobarehe vichocheo hivi, HORMONES hizo, husaidia ukuaji wa uume


 (MNYONYO MIX ) ni dawa yenye mchanganyiko wa mafuta kadha pamoja na dawa asiri inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi iliyokuwepo mwanzo dawa hii aiongezi uume kwa mtu aliyezaliwa uume wake ukiwa mfupi


 (MIZIZI 29) ni dawa bora, ya kurudisha nguvu, za, kiume  inatibu ,kabisa na  kutoa tatizo hilo, na kukupa , hamu ya , kurudia tendo, la ndoa zaidi, ya mala nne 3 ,bila kuchoka atakama unaumli ,wa mika 80,! 


ISENYE hii ni dawa ya kisukari dawa hii ni ya mimea  asili ipo ya vidonge na unga dawa hii imeonyesha matokeo mazuri Sana kwa wagonjwa wa kisukari jaribu Leo hakika uweze kuona utofauti wake na dawa ulizowah kutumia pia ana dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno dawa zipo matazo ya hedhi kwa wanawake hedhi zisizokuwa na mpangilio vidonda vya tumbo.


huduma zetu zipo vizuri popote pale dawa utaletewa hata Kama hupo nnje ya nchi ofisi ipo mbagara sabasaba MWANZA yupo wakala


Wasiliana nami kwa simu 0782794980 Whatsapp +255782794980



Penzi Kikohozi alijifichi nakupenda Lulu bora niwe mtumwa kwako- Lavalava


Penzi halfichiki kama chafya unaweza kusema hivyo hii imetokea kwa msanii Lavalava na Lulu Diva baada ya leo Lavalava kuamua kuanika ukweli wa penzi lao kwa kusema kuwa anampenda sana na amekubali kuwa mtumwa kwake.

Mara nyingi penzi la wasanii hawa limekuwa ni la siri sana hata pale vinapovuja video au picha wakiwa kwenye mapenzi mazito huwa wakihojiwa wanakataa lakini Kupitia kwenye ukurasa wake wa instaramu Lavalava ameandika hivi;

Dah Usiku Wajana Ndosijalala Kabisa Lulu Kiukweli Achatu Ifike Mahali Mtu Aweke Wazi Penzi Kikohozi Alijifichi Nakupenda Lulu Bora Niwe Mtumwa Kwako Hakuna Jinsi inaenda Wiki Sasa Hatuelewani Naumia Binadamu Tumeumbiwa Kukosea Hakuna mkamilifu Samahani Sana Narudia Tena Samahani nisamehe Mwenzako Plz 💔💔🥺💦💦💦💦



Serena Williams ashindwa kuendelea na mchezo kisa maumivu ya mguu

 


Mcheza tenisi anayeshika nafasi ya nane kwenye viwango vya ubora Duniani kwa mujibu wa Chama cha wacheza tenisi cha Wanawake Duniani, Serena Williams ameshindwa kuendelea na mchezo wake katika michuano ya Wimbledon usiku wa kuamkia leo baada ya kupata maumivu ya mguu.

Serena ambaye ni wa Marekani alikuwa dimbani kwenye mchezo wa mzunguko wa  pili dhidi ya Aliaksandra Sasnovich wa Belarus na kufukuzana kwenye seti ya tatu wakiwa na alama 3-3 lakini nyota huyo alishindwa kuendelea na mchezo huo baada ya maumivu ya misuli ya paja lake la kulia.

Serena anayetaraji kutimiza miaka 40 mwezi Septemba mwaka huu, aliugulia maumivu hayo yaliyomlekea kujiinamia chini na kuanza kutokwa na machozi na kuonesha kushindwa kuendelea na mchezo huo jambo ambalo lilipelekea apigiwe makofi ya heshima na mashabiki ili kumfariji.

Baada ya kupatiwa matibabu ya awali na kurejea kambini, Serena aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa “Niliumia sana kuondoshwa baada ya kupata maumivu kwenye mguu wangu wa kulia”.

“Upendo na shukrani zangu zipo na mashabiki na wote waliofanya nipate faraja uwanjani. Nimepata hisia kubwa sana kuungwa mkono na umati wa mashabiki wakati natolewa uwanjani na wao wanaana kubwa sana kwangu”.

Kilichomkuta Serena Willians ni huzuni kwani alikuwa anasaka ushindi wa 24 wa michuano hiyo mikubwa ya Tenis ili kuweka rekodi ya kipekee kuwa mwanadada pekee kutwaa mataji mengi zaidi kwenye historia ya tenisi huku wengi wakisema huenda ni michuano yake ya mwisho kutoka na umri wake kuwa mkubwa na majeraha yanayomuandama.

Baadhi ya wacheza tenisi nyota kama Vile Andy Murray kwa upande wa wanaume na mwanamama Tracy Austin ambaye ni gwiji wa zamani wa mchezo huo kwenye miaka ya 1980 aliyewahi kushika nafasi ya kwanza kwa ubora duniani pamoja na kushinda Gland Slam 3.


 



Kenyata: Hakuna mkenya atakayelazimishwa chanjo


Rais Uhuru Kenyatta amesema hakuna Mkenya atakayelazimishwa kupata Chanjo ya #CoronaVirus ambayo itatolewa bure na Serikali kwa watu wazima

Amesema baadhi ya Wananchi wameibua mijadala kuhusu Chanjo na madhara yake akisisitiza licha ya kwamba hazitakuwa lazima, Elimu kuhusu suala hilo ni muhimu

Kenya inalenga kutoa Chanjo kwa watu wazima wote ambao idadi yao ni Milioni 26 hadi kufikia katikati ya 2022, huku Milioni 10 wakipata chanjo kufikia Desemba 2021



Balozi wa China: Ushirikiano kati ya Serikali ya Zanzibar na Serikali ya China utaendelea kuimarika


 BALOZI  Mdogo wa China aliopo Zanzibar Zhang Zhisheng amesema ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China utaendelea kuimarika kutokana na udugu wa muda mrefu uliopo .

Kauli hiyo ameitoa  wakati akikabidhi msaada wa  vifaa tiba kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Dkt. Omar Dadi Shajak huko ofisini kwake mnazimmoja

Amesema vifaa hivyo vitasaidia katika utoaji wa huduma mbali mbali ikiwemo barakoa pamoja na mitungi ya hewa ya oxygen    kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja pamoja na Hospitali ya Abdalla Mzee ilioko pemba.

Aidha alisema mashirikiano ya pamoja yanahitajika ili kupambana na wimbi la tatu la Covid-19, ambalo linaonyesha  kuathiri  duniani kote .

 Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Dkt. Omar Dadi Shajak alimshukuru Balozi huyo kwa kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuipatia vifaa hivyo pamoja na misaada mengine wanayoisaidia ikiwemo kuwapatia Madaktari Wataalamu wa Maradhi mbali mbali .

Aliahidi kuitumia vizuri misaada hiyo ambayo itasaidia  katika kupambana na maradhi ya covid 19 kwa wananchi wa Zanzibar .

Aliwasisistiza wananchi kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya katika kujikinga na maradhi ya korona kwa kuvaa barakoa ,kunawa mikono mara kwa mara pamoja kuepukana na mikusanyiko isio ya lazima .

Wakati huo huo Dkt Shajak alipokea msaada wa mashine ya kupumulia kutoka kwa shirika la Japiego kupitia kwa Mkurugenzi wa afya Laurel Fain kutoka  Marekeni.




Kelele na mitetemo inapelekea vifo - Dkt. Gwajima


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima, amesema kuwa kitaalamu ni kwamba kelele na mitetemo ni moja wapo ya tatizo linalosababisha vifo na magonjwa Duniani.

Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma, wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo, akitoa tamko kwa umma juu ya udhibiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kelele na mitetemo, ambapo wamiliki wa maeneo ya burudani na starehe wametakiwa kuzingatia matumizi ya vipima kelele na vizuia sauti kama ilivyoelekezwa kwenye masharti yote ya leseni zao.



IGP Sirro afanya mabadiliko madogo ya Makamanda wa Polisi


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP),  Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo kwa makamishna na makamanda wa Polisi watatu kwa lengo la kuongeza ufanisi kwenye mikakati ya kubaini, kuzuia na kukabiliana na uhalifu.

Taarifaimetolewa Msemaji wa Jeshi hilo,  David Misime imeeleza kuwa kamishna msaidizi wa polisi  (ACP) Joseph Konyo amehamishwa kutoka kitengo cha maadili makao makuu ya polisi Dodoma na kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma .

Kamanda Konyo anachukua nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma (ACP) Simon Maigwa ambaye anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro

Taarifa hiyo inaeleza kuwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (ACP) Amon Kakwale amehamishwa katika kamisheni ya operesheni na mafunzo makao makuu ya polisi Dodoma.




Zaidi ya watu 100 wapoteza maisha kutokana na joto kali Canada


Watu kadhaa wamefariki nchini Canada kutokana na joto lisilo la kawaida kupiga ambalo limevunja rekodi ya kiwango cha joto.

Polisi wa British Columbia wamepokea taarifa za vifo vipatavyo 70 tangu Jumatatu, vifo vingi vikijumuisha wazee.

Wanasema kiwango hicho cha joto kupiga katika eneo hilo kilisababisha vifo hivyo.

Jumanne, kiwango cha joto nchini Canada kiliongezeka zaidi ikawa siku ya tatu mfululizo -ilikuwa nyuzi joto 49.5 huko Lytton, British Columbia.

Kabla ya wiki hii , kiwango cha joto cha Canada hakikuwahi kuvuka nyuzi joto 45.

"Waangalie majirani zako, familia yako pamoja na wazee unaowajua ," Polisi wa Canada Mike Kalanj, ambaye yuko Vancouver wilaya ya Burnaby, alisema Jumanne.

"Hali ya hewa inaweza kuwa hatari kwa jamii ya watu ambao hawajiwezi hasa wazee na wale wenye matatizo ya kiafya," aliongeza. Ni muhimu tukawajulia hali kila mara."

Kwa mujibu wa polisi , joto hilo linaaminika kuwa limesababisha vifo vya watu 69 katika mji wa Vancouver wilaya ya Burnaby. Wengi wakiwa wazee na waliokuwa na matatizo ya kiafya.

Katika kijiji cha Lytton, mkazi wa eneo hilo Meghan Fandrich amekiambia chombo cha habari cha Globe & Mail kuwa ilikuwa vigumu hata kutoka nje.

"Hali ilikuwa mbaya sana," alisema, na kuongeza kuwa ilimbidi amuhamishe binti yake mdogo kwenda kuishi eneo jingine la British Columbia ambako joto halikuwa kali sana.

"Tunajaribu kuwa ndani kadiri tuwezavyo.Tumezoea joto lakini si kwa kiwango hiki ambacho kimezidi nyuzi joto 30, ni kingi mno yani kinafika mpaka 47 hivyo utofauti ni mkubwa sana."

Mamlaka ya mazingira Canada imetoa angalizo juu ya jimbo la British Columbia na Alberta, pamoja na maeneo ya Saskatchewan, the Northwest Territories na baadhi ya sehemu ya Yukon.

"Taifa letu ni la pili kwa kuwa na baridi duniani na kuwa na barafu," alisema David Phillips, mtaalamu wa mazingira Canada.

"Tukiongelea suala la joto kuwa kali tunaweza kusema Dubai lakini hali ya joto tunayoiona hapa ni mbaya zaidi ya Dubai."

Joto katika miji ya Marekani ya Portland na Seattle liliwahi kuvunja rekodi mwaka 1940.

Portland ya Oregon ilipiga nyuzi joto 46.1C (115F) na Seattle nyuzi joto 42.2C (108F), kwa mujibu wa mamlaka ya huduma ya hali ya hewa



MAGONJWA NINAYO TIBU NI KISUKARI, TEZI DUME, NGUVU ZA KIUME

                                            


DOCTOR MBOJE,


NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA


MAGONJWA NINAYO TIBU NI 


A,_DOCTOR MBOJE,


NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA


MAGONJWA NINAYO TIBU NI 


A,_KISUKARI na tibu kwa miti shamba  kunywa na kupona kabisa


B,_TEZI DUME_natibu kwa miti  kunywa na kupona kabisa bila kufanyiwa upasuaji


C,_NGUVU ZA KIUME 

  Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa natibu kwa miti shamba na kupona kabisa


D,_kutibu magonjwa mbalimbali Kama uzazi) (miguu kuvimba na kuwaka Moto) (Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu) (mgongo,   kiuno)


MHERA JIGURHU ni dawa ya miti shamba inatibu kisukari na kupona kabisa kwa mda wa siku 16 

Sukari iwe kubwa kabisa lakini iwe normal 5.1  


NNKOROBHIJE ,ni dawa ya miti shamba inayotibu  TEZI DUME bila kufanyiwa operation na kupona kabisa kwa siku 14 na kibaki history 


NHUNGHU MAPANDO Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa au kama unahisi kupungukiwa tumia nhunghu mapando ni dawa inatibu na kupona kabisa tatizo kwa mda wa siku 4 tu


 NTURURU ni dawa ya miti shamba inayotibu uzazi chango kwa wakina mama wasio kua na watoto inatibu na kumaliza tatizo kabisa na mfumo wako wa Heath Kama umevulugika inatibu kwa mda wa siku 18


MWICHE,ni dawa ya miti shamba inayotibu Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu kurunguia kiuno kuuma mgongo na kupona kabisa kwa mda wa siku 7


PIIA UNAWEZA KUNIPATA KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA 

CALL AND WHAT SAAP

+255744922982

+255737585753 


HUDUMA ZANGU ZINAPATIKANA DUNIA NZIMA KWA OFISI NI DAR ES SALAAM NA MOROGORO KWA ULIE MBALI DAWA NAKUSAFIRISHIA MPAKA INAKUFIKIA KWA WALE WA DAR NA MOROGORO KAMA HUWEZI KUFIKA OFISINI NAKUAGIZIA DAWA INAKUFIKIA MPAKA ULIPO na tibu kwa miti shamba  kunywa na kupona kabisa


B,_TEZI DUME_natibu kwa miti  kunywa na kupona kabisa bila kufanyiwa upasuaji


C,_NGUVU ZA KIUME 

  Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa natibu kwa miti shamba na kupona kabisa


D,_kutibu magonjwa mbalimbali Kama uzazi) (miguu kuvimba na kuwaka Moto) (Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu) (mgongo,   kiuno)


MHERA JIGURHU ni dawa ya miti shamba inatibu kisukari na kupona kabisa kwa mda wa siku 16 

Sukari iwe kubwa kabisa lakini iwe normal 5.1  


NNKOROBHIJE ,ni dawa ya miti shamba inayotibu  TEZI DUME bila kufanyiwa operation na kupona kabisa kwa siku 14 na kibaki history 


NHUNGHU MAPANDO Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa au kama unahisi kupungukiwa tumia nhunghu mapando ni dawa inatibu na kupona kabisa tatizo kwa mda wa siku 4 tu


 NTURURU ni dawa ya miti shamba inayotibu uzazi chango kwa wakina mama wasio kua na watoto inatibu na kumaliza tatizo kabisa na mfumo wako wa Heath Kama umevulugika inatibu kwa mda wa siku 18


MWICHE,ni dawa ya miti shamba inayotibu Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu kurunguia kiuno kuuma mgongo na kupona kabisa kwa mda wa siku 7


PIIA UNAWEZA KUNIPATA KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA 

CALL AND WHAT SAAP

+255744922982

+255737585753 


HUDUMA ZANGU ZINAPATIKANA DUNIA NZIMA KWA OFISI NI DAR ES SALAAM NA MOROGORO KWA ULIE MBALI DAWA NAKUSAFIRISHIA MPAKA INAKUFIKIA KWA WALE WA DAR NA MOROGORO KAMA HUWEZI KUFIKA OFISINI NAKUAGIZIA DAWA INAKUFIKIA MPAKA ULIPO



OKOA NDOA YAKO NA SUPER MIHAYO MPYA

                 




SUPER MIHAYO  MPYA .


WHATSAP NO +255 746 758 853


Ni dawa bora ya kutibu na kumaliza matatizo yote ya nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile,


- kuwahi kufika kileleni dakika moja ushakojoa 


- maumbile kusinyaa na kulegea wakati wa tendo 


- kukosa hamu ya tendo la ndoa 


- kushindwa kurudia tendo la ndoa 


- uume kusimama kwa kulegea 


- uume kulegea katikati ya tendo 


- kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu 


- kuishiwa nguvu kutokana na punyeto.


Epuka aibu hii leo kwa kutumia SUPER MIHAYO. kiboko ya matatizo haya.


Pia kuna SUPER MIHAYO. Kiboko ya uume mdogo inaboresha maumbile ya uume kwa kurefusha na kunenepesha kwa saizi uipendayo haijalishi umri hata kwa walioathirika na upigaji punyeto


Kwanza fahamu sababu zinazopelekea kuwa na upungufu wa nguvu za kiume na uume mdogo.


(1) kujichua (punyeto) kwa muda mrefu maana hupelekea misuli ya uume kulegea.


(2) ngiri 


(3) kuugua chango la uzazi kwa muda mrefu.


(4) kupungukiwa hormone za testosterone.


(5) ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na visivyo na virutubisho  vya kutosha.


(6) kutokufanya mazoezi na mwenendo wa maisha.


(7) kisukari.


(8) tumbo kuunguruma na kujaa gesi.


(9) maumivu ya kiuno nk.


Kwanini uhangaike? Kwanini uhuzunike?


Hii ni spesho kwa waliotumia madawa mengi bila kufanikiwa hakika hautajuta kuitumia. 


WASILIANA NA:


DR. HASSANI


SIMU NO:


📞0746758853


WHATSAP NO +255746758853


Popote ulipo huduma hii inakufikia




Tuesday, June 29, 2021

Amteka mpenzi wake akitaka arudishiwe hela alizo honga, amuua


Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake aitwaye Esta John (28) mkazi wa Ibamba Wilaya Bukombe Mkoani humo ambaye kabla ya kifo chake alitekwa nyara na mpenzi wake.

Katika taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe aliyoitoa kwa waandishi wa habari inasema kwamba mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake juni 13 mwaka huu akiwa na mtu aliyesemekana ni mpenzi wake.

Baada ya kutoweka kwa muda mwanaume huyo ambaye jeshi la polisi halijamtaja kwa majina yake, alianza kuwapigia simu wazazi wa mwanamke akihitaji kulipwa pesa alizokuwa akimuhudumia kwa ahadi ya kumuoa na kwamba mtuhumiwa alibaini kuwa sio mwaminifu .

Kamanda Mwaibambe amesema baada ya taarifa kufika katika vyombo vya usalama upelelezi ulianza mara moja na kufankiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na mali za marehemu ambaye alimteka nyara.

“Katika mahojiano alikiri kumteka nyara mwanamke huyo akishinikiza kulipwa gharama alizotumia kumtunza kwa ahadi ya kuoana lakini alibaini kwamba sio mwaminifu, aliposhindwa kurudisha pesa yake ndipo alichukua uamuzi wa kumuua na kumzika huko katika kijiji Masota Wilaya ya Bukombe’’ Kamanda Mwaibambe.

Aidha amesema mtuhumiwa aliwaongoza Askari Polisi mpaka eneo alikomzika ambapo hatua za kisheria zilifuatwa ikiwmo kufukua kaburi na kufanya uchunguzi wa utambuzi wa mwili wa marehemu na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea na upelelezi ukikamilia mtuhumiwa aafikishwa katika vyombo vya sheria.



Israel kuharibu dozi 800,000 za chanjo ya Covid-19


Imeripotiwa kuwa Israel italazimika kuharibu dozi 800,000 za chanjo ya corona (Covid-19), ambazo tarehe yake ya mwisho ya matumizi inakaribia, ikiwa hakuna mahitaji kutoka nchi zingine.

Kulingana na ripoti ya Shirika la Utangazaji wa Umma la Israel (KAN), utawala wa Tel Aviv una dozi 800,000 za chano ya Covid-19, ambazo tarehe yake ya mwisho ya matumizi inakaribia.

Ikiwa hakuna mahitaji kutoka nchi zingine, Wizara ya Afya ya Israel italazimika kuharibu chanjo hizi.

Ingawa ripoti haikutaja chanjo ya Israel ni ya kampuni gani, utawala wa Tel Aviv ulinunua chanjo ya BioNTech-Pfizer.

Mnamo Juni 18, Israel ilikubali kubadilishana chanjo za Covid-19 zilizokwisha muda wake na Palestina.

Chini ya makubaliano hayo, Israel ingetoa chanjo zaidi ya milioni 1 za BioNTech-Pfizer kwa Palestina.

Kwa upande mwingine, chanjo ambazo Palestina ingepokea kutoka BioNTech-Pfizer mnamo Septemba na Oktoba zitatumwa kwa Israel.

Mamlaka ya Palestina ilifuta makubaliano hayo kwa madai kuwa tarehe ya kumalizika kwa chanjo zitakazotolewa na Israel ingefika ndani ya muda mfupi.



Wabunge waombwa kuunga mkono hoja ya kuwepo na siku ya wanawake wenye ulemavu


WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameombwa kuunga mkono hoja ya kuwepo kwa maadhimisho ya siku ya mwanamke mwenye ulemavu.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kwenye mkutano wa pamoja wa wadau wa Walemavu na Wabunge ulioandaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust jijini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano huo, Dk Tulia amewaomba Wabunge hao kuiunga mkono hoja hiyo pindi itakapoletwa bungeni na Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa.

Naibu Spika Amesema uwepo wa siku ya mwanamke mwenye ulemavu itasaidia kuongeza wigo wa kujadili changamoto na matatizo wanayokumbana nayo wanawake wenye ulemavu nchini.

Dk Tulia amesema uwepo wa siku hiyo utatoa nafasi kubwa ya kujadili nafasi ya mwanamke mwenye ulemavu kwani kwa kipindi kirefu wamekua wakipata changamoto bila kuwa na sehemu ya kuziwasilishia.

" Ni kweli Walemavu wanakabiliwa na changamoto kubwa sana lakini wanawake wenye ulemavu changamoto zao ni kubwa zaidi, Kuna ambapo wanafanyiwa ukatili wa kimaumbile lakini hawawezi kujitetea, ni jukumu letu kama Wabunge kuipitisha hoja hii ili iweze kuwepo siku ya wanawake wenye ulemavu.

Niwaombe wabunge kuhakikisha kuwa hoja hiyo itakapoletwa bungeni iwe kwa kuletwa na Mbunge Stella Ikupa mwenyewe au hata Mbunge mwingine basi tuiunge mkono kwa asilimia 100, ili bunge liweze kuridhia, naamini Wabunge mmetuelewa," Amesema Dk Tulia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Ikupa Trust ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amewaomba Wabunge hao kuipitisha siku hiyo kwa manufaa ya Watu wenye ulemavu.

“Hii hoja siyo yetu pekee yetu hata wenzetu wa shirika la kimataifa la Un Woman pamoja na shirika la idadi ya watu duniani UNFPA wametuunga mkono katika hili la kuwa na siku hii rasmi," Amesema Mpanju.

Nae Mbunge Stella Ikupa amesema kupitia uwepo wa siku ya mwanamke mwenye ulemavu ni rahisi jamii kubadilisha mtazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu na kuitumia pia siku hiyo kama sehemu ya kutoa Elimu kwa wananchi dhidi ya vitendo vyenye ukatili.

" Ni ombi langu kwenu Ndugu zetu Wabunge tutakapoileta hoja hii basi iweze kupita, tunaamini kuwa na siku moja Maalum ya wanawake wenye ulemavu kunaweza kusaidia kupunguza vitendo vya ukatili Kwenye jamii yetu," Amesema Stella Ikupa.



China yaishutumu Marekani kwa kuharibu utaratibu ulimwenguni


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin aliishutumu Marekani kwa kuwa "mharibifu mkubwa" wa utaratibu wa ulimwengu.

Wenbin, katika mkutano na waandishi wa habari alioufanya alisema,

"Marekani ni mharibu mkubwa wa utaratibu wa ulimwengu kwa kuweka vikwazo na vitisho vya kijeshi dhidi ya nchi zingine."

Akieleza kwamba utaratibu ambao sheria za Marekani zinategemea ni mfumo wa kijeshi unaotawaliwa na Marekani, Wenbin alisema kuwa washirika wake wengi hawakubaliani nao.

Wenbin pia alisema,

"Utaratibu wa ulimwengu sio wa kihuni au ulioundwa na kikundi kinachoongozwa na Marekani. Nchi zote lazima zifanyie ujamaa wa kweli, kuendeleza demokrasia ya uhusiano wa kimataifa, na kujenga jamii yenye mustakabali wa kawaida kwa ubinadamu."

Akizungumzia uhusiano wa hivi karibuni kati ya Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Urusi Vladimir Putin, Wenbin alisema,

"Chini ya mwongozo wa kimkakati wa Rais Xi Jinping na Rais wa Urusi Vladimir Putin, uhusiano wa China-Urusi umeingia katika kipindi bora katika historia yao na imani kubwa ya kisiasa na masilahi ya pande zote."

Wenbin pia alikosoa Japan kwa wito wa kulinda Taiwan kama nchi ya kidemokrasia.

Wenbin alimalizi kwa kusema,

"China imehimiza Japan kutoa taarifa ya wazi ili kuhakikisha kuwa makosa hayo hayarudiwi."



Ujerumani imeliondoa jeshi lake la mwisho Afghanistan


Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Annegret Kramp-Karrenbauer ametangaza kukamilika kwa mpango wa kuwaondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan ambao ulianza Mei.

Katika taarifa yake waziri huyo mwenye dhamana ya ulinzi ametoa shukrani kwa askari wake kwa waume 150,000 ambao wamekuwa katika jukumu hilo tangu 2001, akisema wanajivunia utumishi wao.

Aidha amewakumbuka waliopoteza maisha katika operesheni hiyo, na wale ambao walijeruhiwa akisema hawatasahaulika maisha. Kwa mujibu wa jeshi la Ujerumani, wanajeshi 59 wameuwa tangu kuanza operesheni hizo.

Kabla ya kuanza kujiondoa, Ujerumani ilikuwa na wanajeshi 1,100 ambao walikuwa wakihudumu kama sehemu ya wanajeshi madhubuti 9,600 wa Umoja wa Kujihami wa NATO ikiwa na nafasi ya pili kwa wingi baada ya Marekani. Wanajeshi hao walikuwa wakishiriki katika utoaji wa mafunzo na mipango mininge ya amani. Marekani imetangaza kujiondoa kabisa ifikapo Septemba.

Uingereza, Italia na Uturuki pia zina kiwango kikubwa cha wanajeshi nchini Afghanistan, ikielezwa mataifa mataifa matano yanafanya jumla ya wanajeshi 6,000. Lakini pia mataifa yaliokuwa na idadi ndogo katika operesheni hiyo ambayo ni Denmark, Estonia, Uhispania yamekwishawaondoa wanajeshi wao.

Hali bado ni ya mashaka katika maeneo mengi.

Hatua hii ya Ujerumani inatekelezwa baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kutangaza ameanza kuwandoa wanajeshi wake baada ya kuwepo kwa miaka 20. Aprili, wizara ya ulinzi ya Ujerumani ilitangaza mpango wa kujiondoa nchini Afghanistan hadi ifikapo mapema Julai.

Hatua hiyo inatekelezwa huku hali ya kiusalama nchini Afghanistan ikitajwa kuzorota siku hadi siku. Kundi la wapiganaji wa Taliban linatajwa kuchukua udhibiti wa zaidi ya wilaya 100 miongoni mwa wilaya zaidi ya 400 za taifa hilo. Na majeshi ya kigeni nchini Afghanistan yaliingia Oktoba 7, 2001, ikiwa si zaidi ya mwezi mmoja tangu mashambulizi ya 9/11 ambayo yalisababisha vifo vya takribani watu 3,000. 



Tetesi za soka kimataifa

 


Aston Villa wanatumai watafanikiwa kumzuia nahodha wao Jack Grealish , 25, kuweka katika kandarasi mpya ya mshahara wa £150,000 kwa wiki huku akiwavutia mabingwa wa ligi ya Premia Manchester City. (Telegraph - subscription required)

Juventus inataraji kwamba Cristiano Ronaldo, 36, atafanya uamuzi kuhusu hatma yake ya siku zijazo hivi karibuni kufuatia kuondolewa kwa Portugal katika kombe la Euroa 2020. Kandarasi ya mshindi huyo mara tano wa taji la Ballon d'Or inakamilika mwaka 2022. (Tuttosport - in Italian)

Manchester United ilituma skauti kumchunguza kiungo wa kati wa Ufaransa na Juventus Adrien Rabiot ,26, huku mabingwa hao wa dunia wakiondolewa katika michuano ya Euro 2020 na Switzerland siku ya Jumatatu usiku. (Star)

Adrien Rabiot

Juventus imeingia katika ushindani wa kutaka kumsajili Kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka huku klabu ya Serie A Roma pia ikidaiwa kuwa na hamu ya kumuajiri mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 aliyeiongoza Switzerland kuiondoa Ufaransa katika michuano ya Euro2020.. (Calciomercato - in Italian)

Crystal Palace, Southampton na Norwich City zinamnyatia kiungo wa kati wa Borussia Dortmund, 29, raia wa Denmark Thomas Delaney, ambaye kandarasi yake inakamilika 2022.. (Sky Germany - in German)

Kiungo wa kati wa England Jack Harrison, 24, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa kudumu katika klabu ya leeds wiki hii baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa mkopo kutoka Manchester City kwa misimu mitatu.. (Manchester Evening News)

Leeds inatarajiwa kukamilisha usajili wa beki wa Barcelona Junior Firpo, 24, baada ya kuzishinda baadhi ya klabu zaa ligi ya Premia na zile za siri A ili kumpata mchezaji huyo wa Uhispania.. (Goal)

Arsenal inatarajiwa kuwasilisha ofa rasmi kwa kipa wa Sheffield United Aaron Ramsdale, 23, baada ya kurudi kutoka michuano ya Euro 2020 akiichezea England. (Sheffield Star)

Aston Villa ina hamu ya kumsajili beki wa kati wa Manchester City Axel Tuanzebe kwa mkopo kwa msimu wa 2021-22 huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akiwahi kuichezea Aston Villa kwa mkopo . (Football Insider)

Villa pia inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 23, ambaye thamani yake ya £40m itakuwa ghali mno kwa West Ham. (Eurosport)

Mmiliki wa klabu ya Newcastle United Mike Ashley hayuko tayari kulipa dau la juu kwa wachezaji walio zaidi na umri wa miaka 27 , suala ambalo limesababisha mazungumzo na Southampton kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Gabon mwenye umri wa miaka 28 Mario Lemina , kugonga mwamba. (Mail)





MAGAZETI YA LEO 30.6.2021





















 

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...