Aston Villa wanatumai watafanikiwa kumzuia nahodha wao Jack Grealish , 25, kuweka katika kandarasi mpya ya mshahara wa £150,000 kwa wiki huku akiwavutia mabingwa wa ligi ya Premia Manchester City. (Telegraph - subscription required)
Juventus inataraji kwamba Cristiano Ronaldo, 36, atafanya uamuzi kuhusu hatma yake ya siku zijazo hivi karibuni kufuatia kuondolewa kwa Portugal katika kombe la Euroa 2020. Kandarasi ya mshindi huyo mara tano wa taji la Ballon d'Or inakamilika mwaka 2022. (Tuttosport - in Italian)
Manchester United ilituma skauti kumchunguza kiungo wa kati wa Ufaransa na Juventus Adrien Rabiot ,26, huku mabingwa hao wa dunia wakiondolewa katika michuano ya Euro 2020 na Switzerland siku ya Jumatatu usiku. (Star)
Adrien Rabiot
Juventus imeingia katika ushindani wa kutaka kumsajili Kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka huku klabu ya Serie A Roma pia ikidaiwa kuwa na hamu ya kumuajiri mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 aliyeiongoza Switzerland kuiondoa Ufaransa katika michuano ya Euro2020.. (Calciomercato - in Italian)
Crystal Palace, Southampton na Norwich City zinamnyatia kiungo wa kati wa Borussia Dortmund, 29, raia wa Denmark Thomas Delaney, ambaye kandarasi yake inakamilika 2022.. (Sky Germany - in German)
Kiungo wa kati wa England Jack Harrison, 24, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa kudumu katika klabu ya leeds wiki hii baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa mkopo kutoka Manchester City kwa misimu mitatu.. (Manchester Evening News)
Leeds inatarajiwa kukamilisha usajili wa beki wa Barcelona Junior Firpo, 24, baada ya kuzishinda baadhi ya klabu zaa ligi ya Premia na zile za siri A ili kumpata mchezaji huyo wa Uhispania.. (Goal)
Arsenal inatarajiwa kuwasilisha ofa rasmi kwa kipa wa Sheffield United Aaron Ramsdale, 23, baada ya kurudi kutoka michuano ya Euro 2020 akiichezea England. (Sheffield Star)
Aston Villa ina hamu ya kumsajili beki wa kati wa Manchester City Axel Tuanzebe kwa mkopo kwa msimu wa 2021-22 huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akiwahi kuichezea Aston Villa kwa mkopo . (Football Insider)
Villa pia inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 23, ambaye thamani yake ya £40m itakuwa ghali mno kwa West Ham. (Eurosport)
Mmiliki wa klabu ya Newcastle United Mike Ashley hayuko tayari kulipa dau la juu kwa wachezaji walio zaidi na umri wa miaka 27 , suala ambalo limesababisha mazungumzo na Southampton kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Gabon mwenye umri wa miaka 28 Mario Lemina , kugonga mwamba. (Mail)

No comments:
Post a Comment