Search This Blog

Sunday, February 28, 2021

JIPATIE KIWANJA DAR KWA 1,300,000 TU

 


Habari njema. kutoka KIUMBO REAL ESTATE. 


Tumeandaa mradi mkubwa wenye viwanja za ya 600.


Changamkia furusa hii ndugu mtanzania. 


BEI ZETU NI NAFUU SANA. 

Tsh 1,300,000/= milioni moja na laki tatu tu. 

TENA UTALIPA KWA AWAMU MBILI TU. 


Awamu ya kwanza utalipia TSHS.8, 00,000/= LAKI NANE TU baada ya hapo tutakupa Mwezi moja hadi Miezi miwili (2) KUMALIZIA NUSU ILIYOBAKIA.


mradi wetu upo VIKINDU VIANZI Maarufu KIWANDA CHA PLASTIKI /KWA MWARABU Mkoa wa PWANI/DAR ES SALAAM . 


Mradi wetu upo kilometa Tatu (3km )kutoka barabara kubwa(kilwa road).


HUDUMA ZA KIJAMII.

Huduma zote za kijamii zinapatikana kama vile.


1.Maji Tayari yapo ndani ya mradi wetu

2.Shule za serikalini na za binafsi zote zipo karibu na mradi wetu

3.Hospitali za serikali na za binafsi zipo karibu na mradi wetu

4.Umeme upo tayari ndani ya mradi ni kuwasha tu na kutumia.

5.Barabara zinapitika masaa 24 bila shida yoyo te

6.Sehemu za ibada zipo karibu na mradi.

7.Eneo lipo tambarare hakuna mabonde. 

8.Viwanja vipo kwenye mpangilio mzuri,kwa mipango miji 


UKUBWA WA VIWANJA.


1.Sqm 208(40futi & 50futi) bei yake 1,300,000/= Milioni Moja laki tatu tu, Hichi ni ukubwa wa kiwanja kimoja. 


2.Sqm 416 (40futi & 100futi) bei yake 2,600,000/= Milioni MBILI na laki sita tu, Hichi ni ukubwa viwanja viwili (2)


3.Sqm 832(80futi & 100futi) bei yake 5,200,000/= milioni tano laki mbili tu. Hichi ni ukubwa wa Viwanja vinne(4).

HABARI NJEMA NI KWAMBA UNAWEZA KULIPA KWA AWAMU MBILI.


MAUZIANO.

Mauziano yote hufanyika ofisi za serikali ya mtaa/kijiji pamoja na kupata HATI ya mauziano ya AWALI kama utalipa CASH na kama utatoa Nusu Utapewa mkataba Yetu Tunayo Tayari.

 

Habari njema Hakuna UDALALI kwenye biashara hii unanunua kwa wahusika . 


MAWASILIANO.

Tupigie Simu 0788 06 45 45 WHATSAPP/CALL 

AU 0745 94 81 60 CALL


MUDA WA KAZI.

Tunapatikana kila siku

Kuanzia asubuhi saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni kila siku.


MITANDAO YA KIJAMII.

Utatupata kupitia mitandao ya kijamii kama (Facebook, Instagram, ) kwa jina moja @kiumbo real estate. 


MAZINGATIO.

Hakikisha umekuja kupitia namba zangu hapo juu. 


KARIBU UTIMIZE NDOTO ZAKO ZA KUMILIKI ARDHI KUPITIA KIUMBO REAL ESTATE, ARDHI NI PESA ISIYOSHUKA THAMANI .













NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA

   


 DOCTOR MBOJE,

NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA


MAGONJWA NINAYO TIBU NI 


A,_KISUKARI na tibu kwa miti shamba  kunywa na kupona kabisa


B,_TEZI DUME_natibu kwa miti  kunywa na kupona kabisa bila kufanyiwa upasuaji


C,_NGUVU ZA KIUME 

  Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa natibu kwa miti shamba na kupona kabisa


D,_kutibu magonjwa mbalimbali Kama uzazi) (miguu kuvimba na kuwaka Moto) (Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu) (mgongo,   kiuno)


MHERA JIGURHU ni dawa ya miti shamba inatibu kisukari na kupona kabisa kwa mda wa siku 16 

Sukari iwe kubwa kabisa lakini iwe normal 5.1  


NNKOROBHIJE ,ni dawa ya miti shamba inayotibu  TEZI DUME bila kufanyiwa operation na kupona kabisa kwa siku 14 na kibaki history 


NHUNGHU MAPANDO Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa au kama unahisi kupungukiwa tumia nhunghu mapando ni dawa inatibu na kupona kabisa tatizo kwa mda wa siku 4 tu


 NTURURU ni dawa ya miti shamba inayotibu uzazi chango kwa wakina mama wasio kua na watoto inatibu na kumaliza tatizo kabisa na mfumo wako wa Heath Kama umevulugika inatibu kwa mda wa siku 18


MWICHE,ni dawa ya miti shamba inayotibu Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu kurunguia kiuno kuuma mgongo na kupona kabisa kwa mda wa siku 7


PIIA UNAWEZA KUNIPATA KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA 

CALL AND WHAT SAAP

+255744922982

+255737585753 


HUDUMA ZANGU ZINAPATIKANA DUNIA NZIMA KWA OFISI NI DAR ES SALAAM NA MOROGORO KWA ULIE MBALI DAWA NAKUSAFIRISHIA MPAKA INAKUFIKIA KWA WALE WA DAR NA MOROGORO KAMA HUWEZI KUFIKA OFISINI NAKUAGIZIA DAWA INAKUFIKIA MPAKA ULIPO



Mwambusi atangaza kurejea Yanga

 


ALIYEKUWA kocha msaidizi wa kikosi cha klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa kwa sasa yupo fiti kurejea ndani ya kikosi hicho, hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji wa jino.

Mwezi mmoja uliopita, Mwambusi alitangaza kujiuzulu wadhifa wake ndani ya kikosi cha klabu ya Yanga, hii ni baada ya kushauriwa na daktari kutokana na kuwa na matatizo hayo ya kiafya ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Nizar Khalfan.

Akizungumzia maendeleo yake Mwambusi amesema: “Tayari nimepata matibabu ya jino, na ni kama wiki mbili zimepita tangu nifanyiwe upasuaji, naendelea vizuri na sina maumivu kama ilivyokuwa mwanzo.

“Wanamichezo waniombee nipone ili niweze kurejea katika majukumu yangu kama ilivyokuwa awali, na endapo nitakuwa sawa basi naweza kurejea Yanga”



Polisi wakiwafyatulia risasi waandamanaji Myanmar,


Polisi wamepiga risasi na kuwaua waandamanaji 18 nchini Myanmar, ofisi ya Umoja wa Kimataifa ya kutetea haki imesema katika siku ambayo maandamano ya kupinga mapinduzi yamekumbwa na mauaji mabaya.

Vifo vimeripotiwa katika miji kadhaa ikiwemo Yangon, Dawei na Mandalay baada ya polisi kutumia risasi halisi na vitoa machozi.

Vikosi vya usalama vilianza msako uliokumbwa na vurugu siku ya Jumamosi baada ya wiki kadhaa za maandamano ya amani kupinga mapinduzi ya kijeshi ya Februari mosi.

Viongozi wa serikali, miongoni mwao Aung San Suu Kyi, waliondolewa madarakani na kuzuiliwa.

Kanda za video katika mitandao ya kijamii zinaangazia matukio ya siku ya Jumapili zikiwaonesha waandamanaji wakitoroka huku polisi wakiwakimbiza, vizuizi vya muda vya barabarani vikiwekwa, na watu kadhaa waliokuwa wamelowa damu wakielekezwa kwingine.

Oparesheni hiyo iliimarishwa siku ya Jumapili huku viongozi wa mapinduzi wakipambana kuvunja uasi wa raia ambao haujaonesha dalili ya kumalizika.

Mshauri wa Usalama wa Umoja wa Mataifa Jake Sullivan amesema utawala wa Biden unaandaa "hatua za ziada" dhidi ya wale waliyohusika na msako huo wa vurugu.

"Tutaendelea kushirikiana kwa karibu na washirika wetu kuratibu yanayoendelea katika eneo la the Indo-Pacific na ulimwengu mzima kuwawajibisha wanaohusika na vurugu," alisema katika taarifa siku ya Jumapili.

Marekani tayari imewawekea vikwazo viongozi wa kijeshi wa Myanmar tangu jeshi lilipochukuwa madaraka.



Jogoo amuua mmiliki wake


Jogoo aliyekuwa amefungwa kisu mguuni kwa ajili ya kupiganishwa na jogoo mwenzake amemuua mmiliki wake nchini India.

Tukio hilo limetokea katika jimbo la kusini mwa India la Telangana.

Kulingana na habari iliyotolewa na polisi, jogoo huyo, ambaye alikuwa amefungwa na kisu cha sentimita 8 kwenye miguu yake, alimjeruhi mmiliki wake kwenye kinena wakati akijaribu kuyakimbia mashindano.

Mwanaume huyo wa miaka 45 alipoteza maisha baada ya kupoteza damu nyingi..

Watu 15 walioshiriki katika vita vya jogoo wanatafutwa.




Trump afikiria kuwania tena Urais 2024


Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania tena Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.

Akizungumza katika mkutano wa kisiasa wa muungano wa kihafidhina CPAC uliofanyika mjini Orlando katika jimbo la Florida, mwanachama huyo wa Republican amesema huenda akajitosa katika kinya'nganyiro cha Urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Akiashiria uwezekano huo, Trump aliyeiongoza Marekani kwa muhula mmoja kuanzia mwaka 2017 hadi 2021 amesema:

"Nani anayejua. Ninaweza kuamua kuwashinda kwa mara ya tatu. Hio ni sawa?

Trump pia amesisitiza madai yake yasiokuwa na ushahidi kuwa alimshinda rais wa sasa Joe Biden katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka uliopita.

Rais huyo wa zamani ambaye amehamia katika makaazi yake ya Mar-a-Lago katika jimbo la Florida baada ya kuondoka Ikulu mnamo Januari 20, amerudia madai yake juu ya uchaguzi ulioibiwa na mara kwa mara amekataa kukubali kushindwa.

Trump anadai kuwa uchaguzi wa mwezi Novemba ulikumbwa na udanganyifu mkubwa lakini hajawahi kutoa ushahidi wowote kuunga mkono madai yake.

Trump pia alikataa wito wa kuanzishwa kwa chama kipya cha kisiasa. Alipuzilia mbali ripoti za uwezekano wa kuanzishwa kwa chama cha Trump akizitaja kama habari za uwongo.

"Tukiwa pamoja katika miaka ijayo, tutaubeba na kuupeleka mbele mwenge wa uhuru wa Marekani. Tutaongoza harakati za kihafidhina na chama cha Republican kurudi kwenye ushindi kamili. Na tumewahi kupata ushindi mkubwa. Musisahau kamwe"

Trump pia amekosoa vikali sera za Biden, hatua ambayo sio kawaida kwa rais wa zamani wa Marekani ambaye ameondoka ofisini hivi karibuni.

Rais huyo wa zamani amedai kuwa Biden amekuwa na mwezi wa kwanza mbaya katika utawala wake kwenye historia ya nchi hiyo na kumshtumu Rais huyo wa sasa kwa kutaka kuifanya Marekani kuwa "nchi ya ujamaa"

Donald Trump bado ana ufuasi mkubwa ndani ya chama chake cha Republican. Katika kura isiyokuwa rasmi ya muungano wa kihafidhina CPAC, asilimia 95 waliunga mkono muendelezo wa sera za Trump huku asilimia 70 wakitaka Trump awanie tena Urais katika uchaguzi wa mwaka 2024.

Hata hivyo wakosoaji wake hawakuhudhuria mkutano huo.

Mkutano huo wa kila mwaka hufanyika mjini Washington lakini ulihamishwa hadi Orlando kutokana na vizuizi vya Covid-19 vilivyowekwa mjini Florida.


 



Mzozo wa Tigray Ethiopia: Blinken asema Marekani inasikitishwa na ukatili unaofanyika


Marekani imelaani vitendo vya kikatili katika jimbo la Kaskazini la Tigray nchini Ethiopia, na kuutaka Umoja wa Afrika kusaidia kutafuta ufumbuzi kwa kuwa ''hali inaendelea kuwa mbaya.''

''Tunasikitishwa na hali mbaya ya kibinadamu,'' alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken.

Mgogoro uliibuka tarehe 4 mwezi Novemba 2020 wakati serikali ya Ethiopia ilipoanzisha mashambulizi ya kukiondoa chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) baada ya wapiganaji wake kuvamia makambi ya jeshi la serikali huko Tigray.

Katika ripoti iliyotolewa juma lililopita, Amnesty International imeshutumu vikosi vya nchi jirani ya Eritrea kwa kuua mamia ya watu mjini Aksum tarehe 28 na 29 mwezi Novemba, likisema kuwa mauaji ya watu wengi yanaweza kuwa uhalifu dhidi ya binadamu.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, aliliambia bunge tarehe 30 mwezi Novemba mwaka jana kuwa ''hakuna raia hata mmoja aliyeuawa'' wakati wa operesheni.

Lakini mashuhuda wameeleza jinsi walivyoanza kuzika baadhi ya miili ya raia ambao hawakuwa na silaha waliouawa na wanajeshi wa Eritrea-wengi wao wavulana na wanaume waliopigwa risasi mitaani au wakati wa uvamizi wa nyumba kwa nyumba.

Shuhuda mmoja ameiambia BBC jinsi miili ilivyobaki mitaani kwa siku kadhaa bila kuzikwa, miili mingi ikiliwa na fisi.



Tetesi za soka kimataifa


 Mmiliki mwenza wa klabu ya Inter Miami David Beckham anasema kwamba angependa kuwasajili katika klabu yake wachezaji kama vile Lionel Messi wa Barcelona na washambuliaji wa Portugal na Juventus Cristiano Ronaldo katika klabu yake katika ligi ya Marekani ya MLS. (Mirror)

Bayern Munich wamewasilisha ombi la £39m kumnunua beki wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 29. (Tuttomercatoweb, via Caught Offside)

Mkurugenzi wa kiufundi katika klabu ya AC Milan Paolo Maldini anataka kufanya mazungumzo na Chelsea kuhusu mbadala wa kubadilisha uhamisho wa mkopo wa beki wa kati Fikayo Tomori katika klabu hiyo ya Serie A kuwa wa kudumu . (Sky Sports)

Real Madrid wamejiunga na Manchester City pamoja na Juventus katika kuonyesha hamu ya kiungo wa kati wa Sassuolo na Itali Manuel Locatelli, 23. (Calciomercato - in Italian)

Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp anasema kwamba mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah ni mchezaji muhimu wa klabu hiyo na anatumai kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atasalia katika klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi. (Liverpool Echo)

Burnley na Newcastle United wanachunguza beki wa Portugal Nuno Tavares huku klabu ya Itali Napoli ikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 wa Benfica. (O Jogo - in Portuguese)

Meneja wa Everton Carlo Ancelotti anasema kwamba klabu hiyo ilimsaini kiungo wa kati Abdoulaye Doucoure, 28, kutoka Watford kutokana na pendekezo lililotoka kwa mkurugenzi wa soka, Marcel Brands. (Liverpool Echo)

Klabu ya Carlisle hujipatia £10,000 kila mara Manchester United inapomtumia kipa Dean Henderson, 23,ikiwa ni pamoja na makubaliano ya kandarasi yake wakati klabu hiyo ya daraja la pili ilipomuuza kipa huyo katika klabu hiyo ya Old Trafford akiwa na umri wa miaka 14. (Sun)




MAGAZETI YA LEO 1.3.2021





















 

Dismas Ten Hakuna kama Haji Manara

 


Afisa Habari wa zamani wa Yanga Dismas Ten amesema Afisa Habari bora kwenye vilabu vya soka Tanzania ni Hassan Bumbuli wa Yanga na Idrissa Bandari wa Ndanda FC.


Dismas Ten ambaye pia amewahi kuwa Afisa Habari wa Mbeya City amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo pia ameweka wazi kuwa kwa upande wa wasemaji hakuna kama Haji Mana wa Simba SC.


''Msemaji bora hakuna kama Haji Manara wa Simba SC haswa linapokuja suala la kuzungumza na kuhamasisha''.



Auawa na jogoo wake katika mchezo wa kupambanisha kuku

 


Mtu mmoja ameuawa na Jogoo wake aliyekuwa amefungwa kisu mguuni kwa ajili ya mchezo uliopigwa marufuku wa kupambanisha jogoo Kusini mwa India.


Mmiliki wa jogoo alichomwa kisu usawa wa kati ya tumbo na nyonga wakati kuku huyo akijaribu kutoroka. Mwanaume huyo alipoteza maisha akiwa njiani kuelekea hospitali kwasababu ya kupoteza damu nyingi.


Polisi hivi sasa wanawatafuta watu wengine 15 waliohusika kwenye tukio hilo, ambalo lilifanyika kwenye kijiji cha Lothunur jimbo la Telangana wiki hii, Kuku huyo alishikiliwa katika kituo cha polisi kabla ya kupelekwa shambani.


Polisi wamesema mnyama huyo alikuwa akitayarishwa kwa ajili ya kushiriki mpambano alipojaribu kutoroka. Mmiliki alijaribu kumkamata lakini alichomwa na kisu hicho chenye urefu wa sentimita 7 kilichokuwa kimefungwa kwenye mguu wa kuku huyo wakati wa purukushani hizo.


Wale waliohusika katika tukio hilo wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kutokusudia, kujihusisha na mchezo haramu wa kamari na kuhodhi mchezo wa kupiganisha kuku, shirika la habari la Ufaransa limeripoti.


Afisa polisi katika eneo hilo B Jeevan amesema kuku huyo atapelekwa mahakamani kwa ajili ya ushahidi, kwa mujibu wa gazeti la The New Indian Express.


Mchezo wa kuwapambanisha jogoo ulipigwa marufuku India mwaka 1960, lakini mchezo huo bado ni maarufu vijijini kama Telangana wengi hasa katika matamasha ya jamii ya Hindu wa Sankranti.


Si mara ya kwanza kwa mmiliki wa kuku kuuawa na jogoo wake, Mwaka jana mwanaume mmoja huko Andhra Pradesh aliaga dunia baada ya kukatwa shingoni na kiwembe kilichokuwa kimefungwa kwenye mguu wa jogoo.


Kwa mujibu wa Shirika la habari la CNN, mmiliki alikuwa akimchukua jogoo wake tayari kwa mpambano wa jogoo wakati tukio hilo lilipotokea.





Wakamatwa kwa kutaka kuipindua serikali China

 


Polisi wamewakamata wanaharakati 47 kwa "kupanga kuipindua serikali " katika  Kanda Maalum ya Utawala ya Hong Kong.


Imetangazwa kuwa watu hao 47 watafikishwa mahakamani siku ya kesho, Imeelezwa kuwa wanaharakati hao, wenye umri kati ya miaka 23 na 64, walikamatwa mnamo Januari na kuachiliwa baadaye.



TIBA ASLIA INAYOTOKANA NA MITI SHAMBA KUTOKA KWANGU DOKTA IZENGO MWENYE HOFU YA MUNGU NINAE TIBU MAGONJWA NA KUTATUA MATATIZO YOTE

    


Tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume  kwa vijana na wa kinda BABA limekua ni.chanzo cha ukosefu wa heshima ndani  ya ndoa  tatizo hilo  linasababishwa na Trumbo Kujaa  gesi  kupata choo kigumu  kisukari  makerere na kazalika DAWA ninayo  ya kunywa na kupona kabisa kuanzia umri12 impaka92 iitwayo SERA NIX POWER  

iko kwa wingi ukihitaji inakufikia popote  ulipo dozing siku 5 tu


Tiba ya kisukari ya kupanda na kushuka dawa yake  ni MBUKE DAWA hi inatibu kwa haraka na pia ukiwa unahisi una tatizo DAWA hi inruhusiwa kutumiwa awe mototo  mjamzito mtu mzima Haina  madhara  dozing yake ni ya mda mfupi siku 10hadi12 na ukapime 


DAWA ya tiba  ya gonjwa  la tezi dume  ni MITI 19 MIX ni dawa ya  kunywa siku14 usihangaike na operation  dawa yake ndo hi


DAWA  Male ni dawa ya kutibu uzazi kwa Wakina mama wenye matatizo ya mda mrefu  


Huduma zangu maduka ya DAWA zangu zinapatikanika, dar es salaam ,morogoro na Kahama  na mwakirishi  


Nanina vijana wakukuletea popote  ulipo zitatumwa kwa njia ya mabasi 

Kwa mawasiliano piga  

+255 713 695 655

+255 783 969 338 piga  au WHATSAPP



Shambulizi la bomu Somalia


Watu watatu wameuawa wawili kati yao wakiwa wanajeshi katika shambulizi la bomu kwenye msafara wa jeshi Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, Imetangazwa kuwa shambulizi hilo lililenga afisa mkuu wa jeshi.


Imeripotiwa kuwa afisa huyo amesema alinusurika tukio hilo bila kujeruhiwa, lakini wanajeshi 2 na raia 1 walifariki katika mlipuko huo, Hakuna mtu aliyedai kuhusika na shambulizi hilo bado.




Shambulizi la silaha Mexico

 


Watu 11 wameuawa na 2 kujeruhiwa katika shambulizi la silaha katika jimbo la Jalisco, Mexico.


Miili ya watu 11 imepatikana ndani na mbele ya nyumba, watu 2 waliojeruhiwa katika shambulizi hilo wamelazwa hospitalini.


Mnamo Februari 13, mifuko 18 iliyo na mabaki ya binadamu ilipatikana katika mji wa Zapopan wa jimbo hilo.


Kikundi cha madawa ya kulevya cha "Jalisco Next Generation" kinachofanya kazi katika jimbo la Jalisco kinajulikana kama kundi lenye nguvu zaidi katika mkoa huo.


Zaidi ya watu 300,000 wamepoteza maisha hadi sasa katika ghasia zilizosababishwa na vita ambavyo vilianzishwa dhidi ya wauzaji wa madawa huko Mexico mnamo 2006 bila mafanikio. Takriban watu elfu 40 walipotea katika kipindi ambacho zaidi ya watu 340,000 wa Mexico walihama makazi yao.


Jumla ya maiti 189 zilitambuliwa mwaka jana katika jiji la El Salto, katika jimbo la Jaliscoa.



Mfanyabiashara maarufu Arusha, afariki


Mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, Andrew Mollel ambaye alikuwa mwanzilishi  na Mkurugenzi wa kampuni mbalimbali mkoani Arusha amefariki dunia  na kuibua simanzi kwa wakazi wengi wa jiji hilo.


Akizungumza na Mwananchi leo, Februari 28, Mbunge wa jimbo la Monduli , Fredrick Lowassa amesema kifo cha Mollel  ni pigo kubwa katika jiji la Arusha kutokana na mchango wake.


Lowassa amesema taratibu za mazishi wa Mollel zinaendelea kufanywa na wanafamilia lakini, kubwa ambalo Arusha watamkumbuka ni kuandaa michoro ya mradi  mkubwa wa nyumba za PPF zilizopo eneo la Kijenge jijini hapa ambalo lilikuwa ni eneo lake.


Mollel alikuwa pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Happy Sausages ,Kijenge Animal Products Limited, Georges Center Ltd na AGM Holding  na pia mjumbe wa bodi mbali mbali hapa nchini.


Mollel pia alikuwa ni rafiki wa karibu wa Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.


Kifo cha mfanyabiashara huyu ni mfululizo wa vifo vya wafanyabiahara kadhaa katika jiji la Arusha katika siku za karibuni.



Halmashauri zitumie fedha kwa utaratibu- Mabula


Niabu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ameibana Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kurejesha fedha kiasi cha shilingi milioni 418 ilizopewa na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha viwanja katika manispaa hiyo.


Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi na wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Iringa katika kikao kazi  Dkt Mabula alisema fedha ilizopewa Manispaa ya Iringa ni mkopo kwa ajili ya kupima viwanja na siyo kwa ajili ya shughuli nyingine za halmashauri.


"Wizara imetoa fedha ili upime viwanja na kuuza na baadaye urudishe fedha lakini ninyi badala ya kurudisha fedha mmetumia kwenye mambo mengine, wenzenu Geita faida waliyopata katika mradi kama huu walinunua gari la idara ya ardhi, hatuwezi kutumia fedha kwa utaratibu huo,’’ alisema Naibu Waziri Mabula.


Waziri Mabula  alizitaka halmashauri zote zilizokopeshwa fedha na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha viwanja kuzirejesha kulingana na makubaliano ili kuwezesha halmashauri nyingine zenye uhitaji kukopa. Alisema halmashauri zitakazokaidi kuzirejesha fedha kwa wakati basi suala hilo litawasilishwa mamlaka husika ili wahusika wakatwe fedha hizo moja kwa moja.


Aidha Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa Hamid Njovu alimuahidi Naibu Wzairi wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa halmashauri yake itahakikisha inakamilisha kulipa deni hilo kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2020/2021.



Wanaswa na vipande 13 vya meno ya tembo wakisaka wateja

 


Kikosi maalum ya kupambana na ujangili katika eneo la ikolojia ya Tarangire – Manyara, kimewakamata watu wawili katika  kijiji cha Moyaka wilaya ya Babati mkoani Manyara wakiuza vipande 13 vya meno ya tembo.


Mkuu wa kikosi cha kuzuiwa ujangili (KDU) Kanda ya Kaskazini, Peter Mbanjoko leo Februari 28 amethiitisha kukamatwa watuhumiwa hao, Benard Masalu na  Yembeson Masumbuko na kupongeza kazi nzuri ambayo imefanywa na askari wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Burunge WMA na Chemchem ambao wamewekeza katika eneo hilo.


“Nimepata taarifa za tukio hili na tayari watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi la polisi na taratibu za kuwafikisha Mahakamani zinaendelea,” amesema.


Mtendaji mkuu wa Taasisi Chemchem Assosiation, Walter Pallangayo amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na taarifa za siri ambazo walizipata na wakaandaa mtego uliofanikisha kukamatwa kwao.


Taasisi ya Chemchem ambayo imewekeza hoteli za kitalii na kufanya utalii wa picha katika eneo la Burunge WMA imekuwa na mfuko maalum wa kupambana na ujangili ambapo kwa mwaka Sh400 milioni zinatumika  kufanya operesheni katika eneo hilo la ikolojia ya  Tarangire – Manyara.



UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UGONJWA WA KISUKARI NI MAGONJWA AMBAYO YAMEKUWA TISHIO KWA SASA SOMA HAPA

       

fu wa nguvu za kiume hali ya kushindwa kufanya tendo kikamilifu shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili homon ,Neva,misuli,hisia, mirija ya damu 


CHAZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUUME ,NA UUME KUWA MAFUPI NA KUSINYAA


(1) KISUKARI

(2)utumiaji wavinywaji vinavyobadili hali ya mwili

(3)tabia za kujichua kwa mdamrefu

(4)ngiri ,vidonda vya tumbo

(5)tumbo kuunguruma na kukosa choo


BAADHI YA DALILI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME AU KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUUME


(1)kuwahi kifika kileleni kabra mwenzi wako ajakojoa

(2) kukosa hamu ya tendo la ndoa

(3)kushindwa kurudia tendo la ndoa

(4) uume kusimama kwa uregevu au kushindwa kusimama

(5)kuchoka sana baada ya tendo la ndoa


dawa ya( MJN)ni dawa sahii ya mitishamba isiyokuwa na kemikali yoyote dawa hii ipo kwenye mfumo wa vidonge na unga dawa hii ni tofauti na ulizowahi kutumia usaidia ata wazee wenye miaka 80 pia uboresha uume uliosinyaa na kuwa mfupi


(MTN)ni dawa ya kisukari dawa hii inasaidia sana watu wenye ugonjwa wa kisukari dawa hii ni zuri sana endapo ukifata masharti yake ipasavyo


Wasiliana na TABIBU DITTU +255714448999

0714448999 ofisi ipo mbagara sabasaba mwanza na kahama yupo wakala mikoa mingine na nnje ya nchi tunatuma mizigo kwa uwaminifu mkubwa sana



Wafungwa watoroka gerezani Haiti: 25 wafariki

 


Watu 25 wameripotiwa kufariki wakiwemo wafungwa 6 kufuatia ghasia zilizotokea wakati wafungwa walipokuwa wakijaribu kutoroka gerezani nchini Haiti.


Kulingana na taarifa za vyombo vya habari, wafungwa ambao walianzisha ghasia katika Gereza la Croix-des-Bouquets karibu na mji mkuu wa Port-au-Prince na kujaribu kutoroka, walipambana na polisi.


Wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama, watu 25, wakiwemo wafungwa 6 kati walipoteza maisha, na zaidi ya wafungwa 200 wakatoroka gerezani.


Mamlaka ilitangaza kuwa wafungwa walishambulia raia wakati wa kutoroka gerezani, na kusababisha raia kadhaa kufariki.


Imebainika kuwa polisi wamewakamata wafungwa 69 hadi sasa katika operesheni iliyoanzishwa dhidi ya wafungwa waliotoroka gerezani.


Kwa upande mwingine, inasemekana kwamba mmoja wa viongozi wa magenge yenye silaha huko Haiti alikuwa miongoni mwa wafungwa waliotoroka gerezani.


Rais Jovenel Moise alitoa taarifa kwenye akaunti yake ya Twitter kuhusu tukio hilo na kusema,


"Tunalaani wale waliokimbia kutoka gereza la Croix-des-Bouquets na tunawasihi watu wawe na utulivu. Nimetoa maagizo yote muhimu kwa Polisi wa Kitaifa kudhibiti hali hiyo."


Gereza la Croix-des-Bouquets linatajwa kama mahali pa mfano kwa wapinzani wanaotuhumiwa kujaribu kutekeleza mapinduzi dhidi ya Rais Moise mnamo 7 Februari.




Wanachama TCCIA Pwani wataka Katiba yao iandikwe kwa Kiswahili


Wanachama wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) mkoa wa Pwani wameshauri Katiba yao iandikwe kwa lugha ya Kiswahili badala ya Kiingereza kama ilivyo sasa ili kila mtu aweze kuelewa vizuri miongozo, kanuni na sheria zinazowaongoza .


Ushauri huo umetolewa leo Februari 28 mjini Kibaha wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho wenye ajenda ya uchaguzi huku wanachama mbalimbali wakitoa mawazo yao ya kuendeleza umoja huo ili kufikia malengo yao ya kujikwamua kiuchumi.


Mkazi wa Mlandizi, Asha Saidi amesema katiba iliyopo ambayo imeandikwa kwa Kingereza inawata taabu ya kuelewa kilichoandikwa kwa sababu wanachama wengi wana elimu ya chini, jambo ambalo wamesema linapunguza ushiriki wao katika masuala mbalimbali ikiwemo kugombea nafasi za uongozi.


“Tumeshangaa msimamizi wa uchaguzi, Joseph Kahungwa kutangaza nafasi ya mtunza fedha ipo wazi hakuna aliyeoomba na nafasi nyingine yupo mtu mmoja mmoja tu wakati tunaamini kabisa wataalamu wapo  na pengine  ni watoto wetu lakini kwa kushindwa kutafsiri katiba tumekwama kujaza fomu ama hatujui majukumu, hivyo, tunaomba tuwe na katiba pia ya lugha ya Kiswahili,” amesema.


Kwa upande wake, Ally Shomari amebainisha kuwa chama hicho kina wanachama wengi wakulima ambao mfumo wa elimu waliyosoma enzi zao haulingani na sasa, kwa hiyo, TCCIA Pwani itoke ilipokua zamani kutumia kingereza ianze kutumia lugha ya Kiswahili ili kurahisisha mawasiliano.


Naye msimamizi wa uchaguzi huo, Joseph Kahungwa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa TCCIA Taifa upande wa kilimo, amebainisha kuwa uchaguzi unafanyika baada ya uongozi uliokuwepo kuvunjwa mapema Januari mwaka huu na halmashauri kuu Taifa ya chama hicho kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuvunja katiba ya umoja huo.



Mlipuko katika hospitali Ukraine

 


Mtu mmoja amepoteza maisha na 1 amejeruhiwa kutokana na mlipuko wa silinda ya oksijeni katika hospitali huko Chernivtsi, Ukraine, Mlipuko huo ulitokea kwenye ghorofa ya 2 ya hospitali. Watu 20 walihamishwa kutoka hospitali.

Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?

 


Mkasa wa hivi karibuni wa kuuawa balozi wa Italia nchini DRC, Luca Attanasio pamoja na walinzi alioandamana nao kutoka mji wa Goma - Kivu ya kaskazini, kumezusha upya mjadala kuhusu usalama au ukosefu wa usalama katika taifa hilo lililoathirika na mizozo ya ndani na vita vya miaka mingi.


Balozi Attanasio alikuwa miongoni mwa watu 7 waliosafiri katika magari mawili ya Umoja wa mataifa WFP kutoka Goma kukagua miradi ya utoaji chakula katika shule kadhaa huko Rutshuru.


Katibu mkuu Antonio Guterres ameshutumu vikali shambulio hilo na kutaka serikali ya Congo ifanye uchunguzi kwa wepesi.


Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ilifuatia taarifa hizi kwa kutangaza masharti ya usafiri.


Serikali imepiga marufuku usafiri wa mabalozi na wajumbe wakuu wa kidiplomasia nje yam ji mkuu Kinshasa pasi kuarifu mamlaka awali.


Kwa upande wake Umoja wa mataifa nao umetangaza kuwa utaidhinisha uchunguzi wa kina dhidi ya mauaji hayo.


Swali kubwa ni je hatua hizi litaibadili hali ya usalama Congo?


Mauaji yalivyojiri:

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, kundi hilo liliondoka Jumatatu mwendo wa saa tatu asubuhi.


Kundi la watu waliojihami kwa silaha lilisimamisha magari waliokuwemo balozi na wenzake mwendo wa saa nne na robo na kuwalizimisha abiria kushuka garini.


"Abiria wengine sita walilazimishwa kuingia katika kichaka kilichokuwa karibu wakishikiwa bunduki ambapo kulizuka ufyetulianaji wa risasi", WFP lilisema.


Ni katika makabiliano hayo ndipo balozi Attanasio na mlinzi wake Vittorio Lacovacci, walijeruhiwa vibaya na kufariki.


Ahadi ya Tshisekedi


Ukosefu wa usalama ni moja wapo ya changamoto kubwa anayokabiliana nayo rais Tshisekedi nchini Congo huku akijaribu kumaliza vurugu katika eneo la mashariki mwa taifa - jambo ambalo pia ni ahadi kuu aliyoitoa wakati wa kampeni zake za kuchaguliwa kuwa rais.


Wakati wa kuapishwa, rais Tschisekedi aliahidi "kujenga Congo imara, na kuifanya kuwa ya maendeleo, amani na usalama ".


Zaidi ya mwaka mmoja leo baada ya Tshisekedi kuingia uongozini, wananchi bado hawajihisi salama zaidi ya hali ilivyokuwa awali.


Wanaharakati wa haki za kibinadamu na mashirika ya kiraia wanasema kuwa ikiwa serekali itafanikiwa kutokomeza mashambulizi katika maeneo hayo, basi itakuwa ushindi mkubwa kwa Tshisekedi.


Kuendelea kuwepo kwa waasi.


Mashambulio yamekuwa yakiendelea. Jimbo la Kivu ya kaskazini sehemu ambako shambulio hilo limetokea nimojawapo ya maeneo yalio na hatari kubwa nchini Congo linalopakana na Mbuga ya kitaifa ya Virunga.


Ni eneo lililo na makundi ya waasi wa ndani na hata nje ya nchi kama vile Rwanda na Uganda.


Kundi la FDLR nimojawapo wa makundi hayo, ambalo lilitekeleza mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 na wapiganaji wake kukimbilia DRC.


Kundi jingine lijulikanalo kutekeleza mashambulio dhidi ya raia katika eneo hilo ni lile la ADF ambalo wafuasi wake ni wa kutokea nchini Uganda.


Yapo na mengine makundi madogo yalioundwa na raia kwa dhamira ya kuzikinga jamii dhidi ya mashambulio ya wasi wa nje, lakini kadri muda ulivyosogea dhamira yao ilibadilika na baadhi wakaanza kutekeleza uhalifu kwa maslahi yao.


Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ndio sehemu ilioathirika pakubwa na ukosefu wa usalama.


Shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi limetaja kwamba Zaidi ya raia 2000 wameuawa na makundi ya waasi waliojihami kaskazini na kusini mwa Kivu pamoja na katika jimbo la Ituri mwaka uliopita.


Serikali ya Congo imewashutumu waasi wa FDLR kutekeleza mauaji ya balozi wa Italia na wenziwe sita.


Hatahivyo msemaji wa kundi hilo la waasi ameieleza BBC kwamba kuna Zaidi ya makundi 100 yanayohudumu katika eneo hilo, na haelewi kwanini kundi lake ndilo lililotuhumiwa kwa shambulio hilo.


"Hatukuhusika katika mauaji hayo maovu," Cure Ngoma wa kundi la FDLR ameielezea BBC.


Kadhalika kundi hilo limeongeza kwamba uchunguzi utakaofanywa unapaswa kuzingatia kwamba eneo ambako shambulio limetokea ni sehemu ambapo majeshi ya Congo na Rwanda yalikuwa yakihudumu.


Mmojawapo ya mapendekezo ambayo yametolewa katika juhudi za kujaribu kupata suluhu la kiuslama la kudumu ni serikali kufanya mazungmzo na wapiganaji hasa wale wa kundi la ADF.


Mchanganuzi wa maswala ya kisiasa na kijamii katika mji wa Goma bwana Apollo Msambia anaamini kwamba wakati umewadia kwa serikali ya Kinshasa kuanzisha mazungmzo ya amani na utawala wa rais Yoweri Museveni wa Uganda kuhusu waasi wa ADF.


"Rais Tshishekedi anatakiwa kuanzisha mazungumzo na mwenzake Museveni na kuona jinsi waasi hawa wa ADF wanavyoweza kutoka kaskazini mwa DRC na kurejea Uganda, kwa vile sasa imeonekana kwamba wameshindwa kukabiliana nao kijeshi" asema Bw. Msambia.



Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...