Search This Blog

Monday, August 31, 2020

Kikosi cha Simba kuanza safari kuelekea Mbeya kuifuata Ihefu FC


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji, leo Septemba Mosi kinatarajiwa kuanza safari kuelekea Mbeya kuifuata Ihefu FC.

Simba iliweka ngome mkoani Arusha tangu Agosti 28 ambapo ilitia timu siku ya Ijumaa kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Agosti 30,Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. 

Kwenye mchezo huo ambao ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara,  Simba ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa ba John Bocco dk ya 7 na Bernard Morrison dk ya 60.

Wanaanza safari ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara kwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Ihefu Septemba 6 Uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni.

Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa timu zote ndani ya msimu mpya wa 2020/21 huku Ihefu ikiwa ni msimu wake wa kwanza pia  kushiriki Ligi Kuu Bara baada ya kupanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza.



Alichosema Wakazi kutetea wasanii chipukizi

 


Wakazi ambaye ni Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya ACT-Wazalendo amesema Serikali ya Tanzania haipo katika kukuza ubunifu kutokana na Sheria ya Maudhui iliyopitishwa.

Wakazi amesema kumtaka msanii ambaye amefanya ubunifu kuwa na Laki tano ili kuiweka kazi yake YouTube itafanya wabunifu wadogo kushindwa au kuonekana wahalifu kwa kukiuka sheria.

Wakazi ametambua umuhimu wa uwepo wa Sera ya Sanaa na Wasanii ili kuwaweka wasanii katika mazingira mazuri na kukuza ubunifu.

Wakazi ameyasema haya leo wakati wa uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha ACT-Wazalendo.



Kocha mpya wa Barcelona aanza mazoezi bila Messi

 


RONALD Koeman, Kocha Mkuu wa Klabu ya Barcelona jana Agosti 31 alianza kukinoa kikosi chake kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2020/21 bila ya uwepo wa nyota wao Lionel Messi.

Baada ya kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Quique Setien, Koeman alikabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi hicho ambacho kilitoka kupokea kichapo cha udhalilishaji cha mabao 8-2 mbele ya Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 Picha ambazo zilipigwa na kuwachukua wachezaji ambao walikuwa wameanza mazoezi zilimuonyesha kocha huyo akiwa na baadhi ya wachezaji ambao wanajiandaa na kuanza kwa La Liga huku Messi akiwa hayupo.

Wachezaji wa Barcelona walipigwa picha wakiwa mazoezini ambapo winga Ousmane Demebele alionekana akikimbia huku akitumia vifaa vipya vya mazoezi vya timu hiyo.

 Pia, Gerard Pique alionekana akiwa na mpira akichezea kwenye mazoezi hayo ambayo yalifanyika bila ya uwepo wa Messi ambaye inaelezwa kuwa anahitaji kuondoka ndani ya timu hiyo na inatajwa kuwa anahitaji kwenda kucheza Manchester City inayoshiriki Ligi Kuu England.



Sugu afunguka haya baada ya kufikisha mwaka mmoja wa ndoa yake


 Mbunge wa Mbeya Mjini anayemaliza muda wake, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ametimiza mwaka mmoja wa ndoa yake.


 Sugu alifungua ndoa Jumamosi ya Agosti 31, 2019 na mpenzi wake Happiness Msonga katika Kanisa Katoliki Ruanda Parokia ya Roho Mtakatifu, Mbeya.


“LEO ni mwaka mmoja wa NDOA yetu, NAMSHUKURU sana MUNGU kwa MAISHA yetu. Pia nakushukuru wewe MKE wangu MPENZI kwa kuniongezea FURAHA na KUBADILISHA maisha YANGU, with YOU my LIFE makes more SENSE now…LOVE ALWAYS ,” ameandika Sugu kwenye ukurasa wake wa #Instagram.

Sugu na mkewe wamebahatika kupata mtoto wa kiume waliempa jina la 'Shawn' Joseph Mbilinyi.




Trump atetea wafuasi wake kuhusu makabiliano makali yaliyotokea Portland

 


Rais wa Marekani Donald Trump ametetea wafuasi wake kwa madai ya mchango wao kwenye makabiliano yaliyotokea hivi karibuni.

Amesema kwamba kijana anayeshutumiwa kwa mauaji ya watu wawili huko Wisconsin wiki iliyopita na wafuasi wa Trump walioshiriki makabiliano Oregon Jumamosi, walichukua hatua hiyo kujitetea.

Bwana Trump aliongeza kwamba mpinzani mwenzake wa chama cha Democratic Joe Biden hajawapinga wanaharakati wa mrengo wa kushoto wanaoshutumiwa kwa kusababisha vurugu.

Bwana Biden anaongoza kwenye kura ya maoni kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Novemba.

Jumatatu akiwa Ikulu ya Marekani wakati anafanya mkutano na wanahabari, Bwana Trump alimlaumu Bwana Biden na washirika wake kwa vurugu zilizotokea kwenye jimbo ambalo meya na gavana ni wa chama cha Democratic.

Mwanahabari wa CNN alimuuliza rais ambaye anatoka chama cha Republican ikiwa atashutumu wafuasi wake ambao walifyatua risasi wakati wa makabiliano na waandamanaji wengine yaliyotokea mwishoni mwa juma lililopita Portland, Oregon.

Wakati wa makabiliano hayo, mtu mmoja wa mrengo wa kulia Patriot Prayer, aliuawa na inasemekana mshukiwa amejieleza kuwa mfuasi wa kundi la antifa.

Jumatatu, polisi walimtaja mwanaume aliyepigwa risasi kuwa ni Aoron Danielson. Kufikia sasa, hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

"Naelewa kwamba kulikuwa na idadi kubwa ya watu ambao ni wafuasi, lakini hayo yalikuwa maandamano ya amani," Bwana Trump alimjibu mwanahabari wa CNN, na yeye mwenyewe amekuwa akishutumu vyombo vya habari vya Marekani kwa kupuuza maandamano yanayotekelezwa na kundi la Black Lives Matter.

"Rangi kama njia ya kujilinda rangi sio risasi.

"Wafuasi wako na ni wafuasi wako kweli, walimpiga risasi mwanaume mmoja kijana na kumuua, sio kwa rangi lakini kwa risasi. Na nafikiria hilo ni jambo baya."

Mwanahabari mwingine alimuuliza Trump ikiwa atashutumu ufyatuaji wa risasi uliotokea Kenosha, Wisconsin, ambaye inasemekana aliwahi kuhudhuria moja ya mikutano ya rais.

Kyle Rittenhouse, 17, anashutumiwa kwa mauaji ya watu watatu , Tukio hilo lililotokea wakati wa maandamano mjini humo yaliosababishwa na hatua ya Jacob Blake kupigwa risasi.

"Yote hayo tunayafuatilia," Bwana Trump amesema, "ni hali ambayo inazua maswali, mliona nilichokiona mimi, nafikiri alikuwa anajaribu kuondoka, inaonekana hivyo. Akaanguka na wakaanza kumshambulia.



Tetesi za soka kimataifa


 Lionel Messi ataondoka Barcelona msimu hii na '' inawezekana'' akaelekea Manchester City, kwa mujibu wa mgombea wa urais wa klabu hiyo, Toni Freixa. (Goal)

Barcelona inaamini kwamba njia pekee ya mshambuliaji huyo wa Argentina, 33, kuondoka kihalali bure ni ikiwa ataahidi kwamba hatashiriki katika michuano ya msimu ujao.(ESPN)

Rais wa Argentina, Alberto Fernandez, amemshauri Messi kurejea katika klabu yake ya ujana ya Newell's Old Boys. (C5N, via Evening Standard)

Chelsea imekubali kumsajili kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 21, kwa kima cha kwanza cha pauni milioni 72, na kusababisha pesa za matumizi yao kipindi cha uhamisho kuongezeka hadi pauni milioni 200. (Guardian)

Manchester United inamlenga mlinzi wa RB Leipzig raia wa Ufaransa Dayot Upamecano, 21. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 24, anasemekana kwamba wiki hii atajiunga na Arsenal kwa mkopo kutoka Real Madrid. (Guardian)

Vilabu vya Saudi Arabia na Qatar vimeonesha nia ya kumsajili Mjerumani Mesut Ozil msimu huu lakini mchezaji huyo wa Arsenal, 31, hana nia ya kuondoka London. (Telegraph)

Tottenham imeanzisha mazungumzo ya mkataba mpya wa mlinda lango wa Ufaransa Hugo Lloris, 33, licha ya kumsajili Joe Hart kwa uhamisho wa bure. (Football Insider)

Spurs inafanya mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Joshua King na pia inamnyatia mshambuliaji Mwingereza wa Cherrie, Callum Wilson, wote wakiwa na umri na 28. (Talksport)

Aston Villa pia imeonesha nia ya kumsajili Wilson kutoka Bournemouth. (Mail)

Schalke inamkodolea macho mlinda lango wa Arsenal Emiliano Martinez, 27, raia wa Argentina ambaye pia amehusishwa na Aston Villa. (Sky Sports)

Arsenal imekubali kumtoa beki wa kati Rob Holding, 24, Newcastle United kwa mkopo na makubaliano hayo yanatarajiwa kukamilika wiki hii. (Talksport)

Inter Milan huenda ikamuuza kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 28, miezi minane baada ya kumsajili kutoka Tottenham. (Corriere dello Sport - in Italian)

Crystal Palace inaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Conor Gallagher, 20, kwa mkopo. (Sun)



Macron aishinikiza Lebanon kuunda haraka serikali mpya



Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amerejea Lebanon, nchi ambayo ipo katikati ya mgogoro usio wa kawaida, kwa ziara ya siku mbili iliyosheheni shughuli nyingi na mazungumzo ya kisiasa yanayolenga kuipa ufumbuzi nchi hiyo

Macron alitua jana usiku mjini Beirut lakini mkutano wake wa kwanza haukuwa na waziri mkuu mpya aliyeteuliwa saa chache kabla, wala wanasiasa wanaozozana wa nchi hiyo au wanaharakati wa mashirika ya kijamii. Macron badala yake aliamua kumuona mwanamuziki nambari moja wa kike nchini Lebanon, Fairouz, ambaye ni alama ya kitaifa na mmoja wa vigogo wa nadra sana nchini Lebanon wanaopendwa na kuheshimiwa kote nchini humo. Mwanamuziki huyo maarufu katika ulimwengu wa Kiarabu, sasa ana umri wa miaka 86 na hajaonekana hadharani katika miaka ya karibuni. Mkutano na Fairouz ni ishara ya kibinafsi ya Macron.

Kisha akakutana na waziri mkuu wa zamani Saad Hariri katika makazi ya balozi wa Ufaransa. Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Beirut, Macron alitoa wito wa kuundwa haraka serikali mpya ya Lebanon kufuatia kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya." Nimeona mchakato umeanza katika saa chache zilizopita ambao umewezesha kupatikana kwa waziri mkuu. Sio jukumu langu kumuidhinisha au kumbariki - ni uhuru wa Walebanon ambao ndio suala la msingi hapa - Lakini uhakikishe kuwa serikali yenye lengo inaundwa haraka iwezekanavyo ili kutekeleza mageuzi ambayo tunatambua kuwa yanahitajika kutoa huduma kwa Walebanon." Amesema Macron  

Macron aliwasili saa chache tu baada ya viongozi kumteuwa Mustapha Adib, mwanadiplomasia mwenye umri wa miaka 48, kuwa waziri mkuu mpya na mwenye jukumu la kuukabili mgogoro mkubwa wa nchi hiyo wa kisiasa na kiuchumi.

Rais Michel Aoun mwenye umri wa miaka 85 na mshirika wake wa kisiasa, kiiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah, wameeleza kuwa tayari kubadilisha namna Lebanon inavyoongozwa. Hata amependekeza kutangazwa kwa taifa lisiloongozwa kwa misingi ya kidini. Chini ya mfumo wa sasa wa kisiasa wa Lebanon, waziri mkuu lazima atoke katika madhehebu ya Sunni, urais unaachiwa Mkristo na wadhifa wa spika wa bunge unatengewa madhehebu ya Shia.

Macron alikuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kuitembelea Lebanon, siku mbili baada ya mlipuko wa Beirut uliowauwa watu 188 na kuwajeruhi maelfu ya wengine. Aliahidi kurejea Septemba mosi kushiriki katika matukio ya kuadhinimisha miaka 100 ya uhuru wa Lebanon kutoka kwa Ufaransa.



CCM Yafanya Uteuzi wa Wagombea Uwakilishi katika Baraza la Wawakilish Zanizbar

Kamati  Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanya uteuzi wa wagombea Uwakilishi katika Baraza la Wawakilish  Zanizbar katika majimbo 50 kwa kuzingatia uwezo, umahiri na utendaji wao.
Kikao cha kamati kuu kimefanyika jana Jumatatu tarehe 31 Aagosti 2020 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole alitangaza majina ya walioteuliwa.

Polepole aliwataja waliopitishwa na majimbo kwenye mabano kuwa ni Zawadi Aamour Nasoro (Konde), Shamata Shahama Khamisi (Micheweni), Saidi Sale Salim (Tumbe), Tunu Mwalimu Masoud (Wingwi), Maliam Dhani Juma (Gando), Makame Said Juma (Kojani) na Othman Ali Khamis (Mtambwe).

Wengine ni Khamis Dadi Khamis (Pandani), Harus Said Suleiman (Wete), Shaibu Hassan Kaduara (Chake) Suleiman Masoud Makame (Chonga) Masoud Ali Mohammed (Ole), Bakari Hamad Bakari (Wawi), Suleiman Makame Ali (Ziwani), na Bahati Khamis (Chambani).

Mussa Kombo Mussa (Kiwani), Abdul Hussein Kombo (Mkoani), Mohammed Mgaza Jecha (Mtambile), Nadir Yussuf (Chaani), Juma Mkungu Juma (Kijini) na Mkwajuni ni Sulubu Kidongo Amour.

Pia wamo Abdul Abbas Wadi (Nungwi), Haji Omar Kheri (Tumbatu), Mtumwa Peya Yussuf (Bumbwini), Khalid Salum Mohammed (Donge), Asha Abdallah mussa (Mahonda), -Issa Haji Gavu (Chwaka), Haroun Ali Suleiman (Makunduchi), Paje- Dk. Soud Nahoda Hassan (Paje) na Mwanaasha Khamis Juma (Dimani).

Wengine ni Yussuf Hassan Iddi (Fuoni), Suleiman Haroub Suleiman (Kiembe Samaki), Ameir Abdallah Ameir (Mwanakerekwe), Ali Suleiman Ameir (Pangawe), Mudrik Ramadhan Soraga (Bububu), Machano Othman Said (Mfenesini), Hussein Ibrahim Makungu (Mtoni), Mihayo Juma Nhunga (Mwera), Hassan Khamis Hafidh (Welezo) na Rukia Omar Mapuri (Amani).

Miraji Khamis Mussa (Chumbuni), Jamaal Kassim Ali (Magomeni), Shaaban Ali Othman (Mpendae), Hamza Hassan Juma (Shaurimoyo), Ali Gullam Hussein (Jang’ombe), Nassor Salum Ali (Kikwajuni), Yahya Rashid Abdallah (Kwahani) na Malindi ni Mohammed Ahmada Salum


Polepole alisema Kamati Kuu imepitisha majina ya wawakilishi kundi la wanawake kwa Mkoa wa Kaskazini Pemba ambao ni Bihindi Hamadi Khamis, Chumu Kombo Khamis, na Farida Hamad Juma na Kaskazini Unguja ni Panya Ali Abdalah, Mwanajuma Kasim Makame na Fatma Hamza Mohamed.

Mkoa wa Kusini Pemba waliopitishwa ni Shadia Mohamed Suleimani, Zuhura Mgeni Othman na Zainab Omar Amir wakati Mkoa wa Kusini Unguja ni Salma Juma Bilal, Rahma Kasim Ally na Arafa Ali Yusuph.

Katika mkoa wa Magharibi Unguja, waliopitishwa ni Fatma Ramadhani Mandoba, Mwanaidi Kassim Mussa na Fatma Ali Akhmed na Mkoa wa Mjini Magharibi ni Saada Ramadhani Mwendwa, Mgeni Hassan Juma na Salma Abdi Ibada.

Kadhalika, Polepole alisema Kamati Kuu imewapitisha wawakilishi wanawake kwenye kundi la wenye ulemavu, ambao ni Mwantatu Mbaraka Khamis na Zainab Abdallah Salum na kundi la wasomi ni Riziki Pembe Juma,

Kwenye kundi la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) waliopitishwa ni Salha Mohamed Mwinjuma na Rahma Mbaraka Tahir na kwa upande wa wazazi ni Sabiha Filfili na Aza Januari Joseph.


CCM Wamuonya Maalim Seif...."Aache Kuchafua Viongozi Wetu"

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole  amemtaka Maalim Seif Sharif Hamad kuacha kuchafua viongozi wa chama hicho, vinginevyo atashughulika naye.

Bila ya kumtaja jina, Polepole amesema ‘Mzee Yule’ amekuwa na tabia ya kuchafua viongozi wa chama hicho.

Polepole ametoa kauli hiyo jana  Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020, wakati akitaja orodha ya wagombea uwakilishi visiwani humo.

"Lakini nataka kutoa rai mzee yule (ambaye hakumtaja jina) aache kutaja majina ya viongozi wetu, aache na leo nimetoa heshima kubwa , nimeambatana hapa na wajumbe wenzangu wa Halmashauri Kuu Taifa Bara na Zanzibar ili haya ambayo ninawaeleza ifahamike ndio msimamo wa Chama chetu,"alisema Polepole.

Alisisitiza ni vema akaacha na anajua Chama Cha Mapinduzi wamepiga hatua na itakuwa ngumu kwa vyama vingine kupiga siasa ya kueleweka ,wajipange sio kutengeneza hoja ya kubumba bumba zisizo na mashiko.

",Nimehuzunika sana mzee yule kwasababu anasema uongo kabisa tena hadharani na sina hakika huenda anatafuta namna tumshitaki ili apate kiki kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu, hakuna kitu kingine anachotaka zaidi ya kuvuta hisia za watu.

"Anataka kutengeneza kitu hivi, kutengeneza umaarufu sisi hatutafanya hivyo lakini tunamuonya afanye siasa yake,mambo ya CCM atuachie  , ziko kauli ambazo Chama Cha Mapinduzi hatuna tatizo nazo zilishakwisha atuache,ni vizuri ajifakari afanye kazi ambazo zitakuwa na tija .

"Wapiga kura wengi ni vijana zaidi na wazee ni wachache ,tunasema kwa mkiki huu tunaokwenda nao miaka mitano ya kutekeleza ilani tunakwenda mara tatu zaidi  ya miaka mitano iliyopita.Basi ni vizuri tukamaanisha watu, tumekwenda kule Pemba eneo la Mtambwe Taya ambako ndiko anatoka hajawahi kufanya kitu chochote hata kujenga mnara wa mita moja hajawahi.

"Pale Mtwambwe Taya kimejengwa chuo cha ufundi stadi na pale wanafunzi watasoma ,kuna shule ya bweni , ziko bweni za kutosha watoto karibu 200 watakaa pale watadundishwa ufundi wa aina mbalimbali.Na mambo hayo yote yamefanyika pale lakini huyu mzee hakufanya chochote, huyu ameshika nafasi ya uandamizi katika serikali hakufanya chochote.

"Sasa anatupotezea muda anamsema mgombea wetu , tunasema acha, hii ni mara ya mwisho,tutashulika na wewe katika namna ambayo inaweza kuleta habari nyingine, fanya kampeni za kistaarabu na sisi tumezindua kampeni juzi nzuri kabisa hatutaki kusema watu, tunasema hoja, tunajenga sababu kwa watanzania,tumepewa heshima kubwa sana katika miaka mitano tumefanya kazi kubwa, kazi imefanyika kule Zanzibar."  Alisema Polepole


Maofisa Benki, BRELA Kizimbani Kwa Kughushi Dola 300,000

Raia wawili wa kigeni, wafanyakazi wawili wa benki ya Equity na Msajili Msaidizi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 13 likiwemo la kughushi na kutakatisha  USD 300,000.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa jana mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon imewataja washtakiwa hao kuwa ni,  Mohammed Nur (48) raia wa Afrika Kusini, Umulkher Mohammed (34) raia wa Somalia, wote wafanyabiashara na Noel Shani (44) mfanyakazi Brela.

Wengine ni wafanyakazi wa Benki, Alex Ndondole (33) na Emma Chikaonda ambaye hakuwepo mahakamani.

 Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu imedaiwa kati ya Machi 2011 na Mei 30, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wote walikula njama kufanya kosa la kujipatia fedha kwa udanganyifu.

Katika shtaka la pili, mshtakiwa Nur na Mohamedi, wanadaiwa kughushi maamuzi ya bodi ya Kampuni ya Alliance Cargo Handling ltd ya February 8,2014 kuonyesha kuwa Kampuni hiyo imekubaliana kufungua akaunti katika Benki ya Equity tawi la Prestige wakati si kweli.

Wakili Wankyo amedai katika shtaka la tatu kuwa, Aprili 12, 2015 washtakiwa Nur na Mohamedi, walighushi maamuzi ya bodi ya Aprili 12, 2015 wakionyesha kwamba bodi imekubali kufungua akaunti Benki ya Amana tawi la Nyerere Road huku wakijua kuwa siyo kweli.

Pia inadaiwa, Aprili 18 mwaka 2011 washtakiwa hao walighushi barua kuonesha kuwa imetolewa na Brela kwa kuonesha kwamba Mohammed ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance huku akijua si kweli.

Aidha katika shtaka la tano mshtakiwa hao hao, Nur na Mohamed, wanadaiwa kughushi maamuzi ya bodi ya Machi 5, 2016 wakionesha Kampuni ya Alliance inabadili jina kutoka Alliance Cargo kwenda Africa Flight Service Tanzania wakati si kweli.

 Februari 8, 2014 mshtakiwa Nur aliwasilisha nyaraka ya uongo ya maamuzi ya bodi kuonesha kwamba wamekubali kufungua akaunti Equity benki huku katika shtaka la saba mshtakiwa huyo aliwasilisha nyaraka  Amana benki kuonesha kuwa kampuni imekubaliana kufungua akaunti.

Aidha mshtakiwa Nur anadaiwa kuwasilisha Brela  nyaraka kuonesha wamekubaliana kubadilisha jina la kampuni huku wakijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la tisa, inadaiwa Februari 10,2014 maeneo ya Equity Benki , mshtakiwa Nur na Mohamed  kwa nia ya kufanya udanganyifu katika akaunti ya Kampuni ya Cargo iliyopo Equity , kwa udanganyifu walichukua mkopo wa USD 300,000.

Wankyo alidai shtaka la 11, mshtakiwa tatu akiwa Msajili Msaidizi Brela anadaiwa kushindwa kuzuia uhalifu huku katika shtaka la 12 na 13 washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha  USD. 300,000.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Pia wakili Wankyo aliomba washtakiwa hao warudishiwe polisi kwa kuwa bado hawajapimwa Corona, ombi ambalo mahakama iliridhia kwa ajili ya vipimo na kesi itatajwa Septemba 7 mwaka huu.


Wakazi 'Kuwa Mbunifu ni Sawa na KUWA Mhalifu Kwa Tanzania


Webiro Wassira maarufu Wakazi ambaye ni Msanii na Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya ACT-Wazalendo amesema Serikali ya Tanzania haipo katika kukuza ubunifu kutokana na Sheria ya Maudhui iliyopitishwa

Amesema kumtaka msanii ambaye amefanya ubunifu kuwa na Tsh. Laki tano ili kuiweka kazi yake YouTube itafanya wabunifu wadogo kushindwa au kuonekana wahalifu kwa kukiuka sheria

Wakazi ametambua umuhimu wa uwepo wa Sera ya Sanaa na Wasanii ili kuwaweka wasanii katika mazingira mazuri na kukuza ubunifu

Webiro Wassira (Wakazi), ameyasema haya leo wakati wa uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha ACT-Wazalendo

Wafahamu Wanandoa Waliovunja REKODI ya Kuishi Pamoja Kwa Muda Mrefu zaidi


Julio Mora (110) na Waldramina Quinteros (104) wameweka rekodi ya dunia baada ya kudumu kwa muda wa miaka 79 katika ndoa tangu walipooana mwaka 1941

Wazee hao raia wa Ecuador walioana kwa siri nchini Uhispania kwa kuwa familia zao hazikukubaliana na uhusiano wao. Wote ni Walimu wastaafu na wana watoto walio hai 4, wajukuu 11, vitukuu 21 na kilembwe 1

Aliyefanya watambulike na kitabu cha rekodi cha Guinness ni mtoto aliyetuma maombi ya kuwatambua na wakavunja rekodi ambayo awali ilishikiliwa na Texas Charlotte na John Henderson



Lady Gaga, Ariana Grande na BTS Waongoza Kushinda TUZO za VMA'S 2020

Usiku wa kuamkia leo ulikuwa wa kipekee kwani Tuzo za MTV VMA's zilitolewa katika jiji la New York na kushereheshwa na Keke Palmer.

Mwimbaji Lady Gaga ameweka rekodi ya aina yake kwa kuondoka na Tuzo 9 usiku wa kuamkia leo, akifuatiwa na Ariana Grande pamoja na kundi la BTS.

HII HAPA ORODHA YA BAADHI YA WASHINDI

MTV Tricon Award
Lady Gaga

Video of the Year
The Weeknd - Blinding Lights

Artist of the Year
DaBaby

Song of the Year
Lady Gaga with Ariana Grande - Rain On Me

Push Best New Artist
Doja Cat

Best Pop BTS - On

Best R&B
The Weeknd - Blinding Lights

Best Hip Hop
Megan Thee Stallion - Savage

Best Music Video
Ariana Grande & Justin Bieber - Stuck with U

Best Collaboration
Lady Gaga with Ariana Grande - Rain On Me

Best Group
BTS

Majibu ya Harmonize Kuhusu Tuhuma za Kuanguka


Suala ambalo lipo trending kwa sasa mitandaoni na midomoni mwa wapenzi wa burudani ni kuhusu tuhuma za kuanguka kwenye kamba kwa msanii Harmonize wakati anafanya show siku ya Wananchi ya Uwanja wa Benjamin William Mkapa.


Baada ya tukio hilo kutokea limegusa hisia za watu wengi na kila mtu kusema lake ambapo yeye mwenyewe ametumia 'freestyle' na kuachia mistari ambayo inalenga  kuwachana wale wote waliomdiss baada ya kuanguka kwake.

"Wanasambaza eti Konde ameanguka kamba haishukwi kama baiskeli, wanaona donge hao wanyonge, tunavyoua kwenye show wao wanaona donge, Konde akishuka na kamba wanaona donge hao"

Baadhi ya wasanii wengine waliofanya show kwenye kilele cha siku ya Wananchi kwa timu ya Yanga ni Madee, Maarifa, Billnass, G Nako , Shilole, Baba Levo na Mzee wa Bwax.

Polepole Awaonya Wagombea na Siasa za Kusemana



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole, amewaonya viongozi na wagombea wa nafasi mbalimbali katika chama hicho wajiepushe na siasa za kusema watu badala yake wajikite kufanya siasa zenye kuzingatia ustaarabu.

Amesema hayo leo Agosti 31, 2020, wakati akitaja majina ya wagombea wa uwakilishi kwa upande wa Zanzibar na kusema kuwa kwa upande wa Tanzania Bara wamezindua kampeni zao vizuri kwa kuwasilisha hoja zao kwa Watanzania.

"Tufanye siasa za kistaarabu,na sisi tumezindua kampeni juzi vizuri kabisa hatutaki kusema watu ,tunasema hoja tunaziwekea sababu na tunaeleza tunachotaka kupeleka kwa watanzania", amesema Polepole

Akimzungumizia mgombea Urais kwa upande wa Zanzibar Polepole amesema, "Tumempata mtu mmoja mpole,mtaratibu, mtu wa watu, mwenye nidhamu ya hali ya juu ambaye amehudumu kwenye dhamana ya uongozi kama kiongozi mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ni Mzanzibari kwelikweli ndugu yetu Hussein Mwinyi”.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 1,2020


  


Mgombea Urais wa CCM Dr Magufuli Kutua Singida Leo

Maandalizi ya kumpokea mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida Dkt John Pombe Magufuli yamekamilika.

Akizungumza jana  na waandishi wa habari juu ya maandalizi hayo Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu alisema maandalizi yamekamilika ambapo leo  wanatarajia kumpokea Mgombea huyo mkoani hapo.
 
Alisema pamoja na maandalizi yote mgombea huyo atahutubia wanachama na wananchi pamoja na kunadi ilani ya chama hicho ya mwaka 2020-2025 ambayo alisema imejaa shehena ya vitu vizuri,pia atapata fursa ya kuwatambulisha na kuwanadi wagombea nafasi ya ubunge katika majimbo nane ya mkoa huo.


Watu Wanne Mbaroni Kwa Tuhuma Za Makosa Ya Kupanga Tukio La Mauaji Ya Mtu Mmoja Jijini Mwanza

Jeshi  La  Polisi  Mkoa  Wa  Mwanza  Linawashikilia  Watu  4  Kwa  Tuhuma  Za  Makosa    Ya Kupanga Tukio  La  Mauaji  Ya  Mtu  Mmoja Wilayani  Ukerewe.

Tarehe 25.08.2020 Majira Ya 02:00hrs Usiku Eneo La Mission, Kata Ya Nyamanga, Kisiwa Cha Ukara, Wilaya Ya Ukerewe, Mkoa Wa Mwanza, Andrew Magai, Miaka 48, Mkara, Mkristo, Mkulima Wa Kijiji Cha Chibasi, Aliuawa Kwa Kupigwa Sehemu Mbalimbali Za Mwili Na Kukatwa Na Vitu Vinavyodaiwa Kuwa Na Ncha Kali Kwa Madai Kuwa Marehemu Kabla Ya Kifo Chake Aliwasafirisha Watu Ambao Hawakutambulika Kwenda Kuvunja Nyumba Ya Magesa Simon @ Wile.

Uchunguzi Wa Awali Umebaini Kuwa Tukio La Kuvunja Nyumbani Kwa Magesa Simon @ Wile Lilikua Ni La Kutengenezwa Ili Kuhalalisha Mauaji Yaliyotokea Eneo Hilo. 

Uchunguzi Wa Kina Unaendelea Ukihusisha Wataalamu Mbalimbali. Mwili Wa Marehemu Ulifanyiwa Uchunguzi Na Daktari Katika Kituo Cha Afya Bwisya Na Kukabidhiwa Kwa Ndugu Kwa Mazishi.

Waliofikishwa Mahakamani Leo 31/08/2020 Ni:-

1.Magesa Simon @ Wile, Miaka 50, Mkala, Mkulima, Mkazi Wa Nyamanga.

2.Makanje Mgeta, Miaka 28, Mkara, Mkazi Wa Kijiji Cha Chibasi.

3.Mkapa Magesa@simon, Miaka 24, Mkara, Mkulima, Nyamanga.

4.Selestini Datusi, Miaka 22, Mkerewe, Mkristo, Mkulima, Nyamanga.

Watuhumiwa Wote Wamefikishwa Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kujibu Tuhuma Zinazowakabili.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawataka Wananchi, Wanasiasa Wa Vyama  Vyote  Kutojiingiza Katika Mambo Ambayo Yanaweza Kuhamasisha Uvunjaji Wa Sheria Na Kuvuruga Amani Na Utulivu Wa Nchi, Limeapa Kuendelea Kuchukua Hatua Kali Kwa Kila Atakayekiuka Sheria.

Imetolewa Na:-
Muliro Jumanne Muliro – Acp
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza
31 August, 2020


Aibu! Askofu Anayetuhumiwa UZINZI Avamiwa Madhabahuni na Kuvuliwa Kofia



ZANZIBAR: Timbwili kuzuka baa si hoja; lakini askofu kuvamiwa madhabahuni, kusukwasukwa mpaka kuvuliwa kofia, ni jambo la aibu kufanywa kanisani.


Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Mjini Zanzibar, Michael Henry Hafidh, Jumatatu wiki hii alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya baadhi ya waumini wake kumvamia kanisani wakimtuhumu kwa ufisadi na mambo mengine.


 


DOKEZO MUHIMU


Askofu Hafidh hivi karibuni ameburuzwa Mahakama Kuu ya Vuga mjini humo, akikabiliwa na tuhuma za uzinzi.


Kesi hiyo Namba 21/2020 ilianza kutajwa mahakamani hapo Juni 29, mwaka huu mbele ya Mheshimiwa Jaji, Dkt. Yessaya Kayange, huku mlalamikaji mkuu akitajwa kuwa ni Saburi Khamis mkazi wa Visiwani humo.


WAUMINI WANA NINI TENA?


Ikiwa shauri la uzinzi wa askofu huyo liko mahakamani kutafutiwa haki kisheria, waumini wana lipi tena la kumsumbua mtumishi huyo wa Mungu?


Majibu ni kwamba, Askofu Hafidh anadaiwa kuwaengua baadhi ya watumishi wenzake ambao hawamuungi mkono na kutaka kuwasimika mapadri wapya ambao wanamsapoti.


Kitendo hicho kimeleta mpasuko mwingine mkubwa ndani ya kanisa hilo ambapo kundi linalompinga askofu Hafidh, linasema “haiwezekani” na lile linalomuunga mkono likipigania “inawezekana.”




IKAWAJE SASA?


Sakata hilo lilianza kutimua vumbi mapema Jumatatu iliyopita siku ambayo Askofu Hafidh alikuwa ameandaa ibada ya kuwasimika mapadri wake wapya, lakini zoezi hilo lilivurugwa kwa nguvu na waumini wanaompinga.


Mapema siku ya tukio mwandishi wetu alifikia kanisani hapo na kuwakuta waumini wa kanisa hilo wakiwa wamefunga milango ya kanisa hilo pamoja na ofisi ya askofu huyo.


Akiwa kanisani hapo, mwandishi wetu aliwashuhudia waumini hao wakiwa na mabango yaliyoandikwa tuhuma mbalimbali za askofu Hafidh, huku mengine yakiwa yamebandikwa kwenye milango iliyokuwa imefunga.


Baadhi ya mabango hayo yalisomeka: “Umekiuka viapo vyako vyote, katiba huifuati, ondoka.”


“Umemaliza pesa za dayosisi, sasa umefuata za mtaa.”




WAIMARISHA ULINZI


Baada ya kufunga milango, kubandika mabango na mengine kuyashika mikononi, waumini hao ‘waasi’ wa askofu, waliweka ulinzi na kujiapiza kuwa hawatamruhusu askofu huyo na waumini wake kuingia kanisani.


Ikumbukwe kuwa, ibada hiyo ya kuwasimika mapadri hao iliyotakiwa kuanza saa tisa kamili jioni.


Punde si punde, washika doria hao waliokuwa wakiimba nyimbo za mapambio, walishuhudia umati wa watu waliowasindikiza ndugu zao waliokuwa wakitakiwa kusimikwa daraja hilo la upadri wakiingia kwenye viwanja vya kanisa hilo na hapo mzozo ukaanza.


Wakati vurugu mechi zikiwa zimeshika kasi, askofu Hafidh alifika kanisani hapo lakini alijibanza sehemu kupima hali ya hewa.


Mshikemshike kanisani hapo ulipozidi kati ya wanaosema “inawezekana” na wale wa “haiwezekani”, polisi wakatinga na kuzima vuguvugu hizo kisha kuzikutanisha pande mbili kwa lengo la kuleta mwafaka.


Hata hivyo, lakuvunda huwa halina ubani, kikao hicho cha pande hizo mbili na polisi, hakikuweza kuzaa matunda.


Mtiti wa waumini uliendelea hadi usiku, ambapo baadhi yao waliamua warudi majumbani kulala, huku wengine wakiweka doria kanisani hapo lengo likiwa ni lilelile kutimiza “haiwezekani yao.”


Mawazo ya waumini hao ambao ndiyo walioonekana kuwa na nguvu kuliko wanaomuunga mkono askofu, yalikuwa ni kama machale, kwani ni kweli kesho yake asubuhi (Jumanne) askofu Hafidh na mapadri wake walidamkia kwenye kanisa hilo na kutaka kufanya ibada hiyo.


VURUGU ZAZUKA KWA MARA NYINGINE


Kabla ya kuanza kwa ibada hiyo, waumini wanaompinga askofu huyo waliokesha doria, walianza kuwapigia simu wenzao za “ongezeni nguvu jamaa wamefika huku.”


Dakika chache baadaye, kusanyiko jingine la waasi wa askofu lilifurika kanisani na kuivamia ibada hiyo kwa ujeuri.


Nyumba ya ibada ikageuka kuwa uwanja wa fujo, Askofu Hafidhi akawa siyo muongoza ibada tena, bali mtu aliyekunjwa na kuvuliwa kofia na waumini hao akiwa madhabahuni, tayari kuongoza ibada aliyokusudia kuifanya ambapo polisi kwa mara nyingine walifika na kutuliza ghasia.


TUWASIKILIZE WAASI WA ASKOFU


Kufuatia sakata hilo, mwanahabari wetu alizungumza na mmoja wa wazee wa kanisa hilo aliyeko kundi la uasi aliyejitambulisha kwa jina la Bi. Lili Sudi, ambaye alisema:


“Huyu askofu anachofanya ni kukiuka kiapo alichokula kwa kuwa hapa kanisani sasa hivi pamekuwa na kashfa kibao ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo kufuja fedha na kashfa ya ngono inayomkabili mahakamani.


“Lakini cha ajabu, malalamiko yetu yameshafika kwa Askofu Mkuu Maimbo William Mndolwa, lakini tunamshangaa naye anashindwa kuyachukulia maamuzi malalamiko ya waumini ambao tuko wengi kwa sasa.”


Mwingine aliyezungumza maneno kama hayo, ni James Daudi ambaye naye alitoa malalamiko yanayofanana na Bi. Lili.


Waumini wengine nao kwa nyakati tofauti, walitoa malalamiko yao wakimtuhumu askofu huyo kwa makosa mbalimbali.




ASKOFU HAFIDH ATAFUTWA


Baada ya kukusanya data za kutosha na kuondoka eneo la tukio, RISASI JUMAMOSI liliwasiliana kwa njia ya simu na askofu Hafidh ili kujua undani wa tukio hilo na nini mwisho wa mvutano wao, alipopokea simu alisema:


“Ahaa nakupata ndugu yangu, ila sasa nipo kwenye kikao cha amani na mashehe, hivyo naomba nitafute baadaye au nitumie ujumbe.”


Hata hivyo, licha ya kutumiwa ujumbe na kuelezwa juu ya sakata hilo, askofu huyo hakujibu chochote.


KAMANDA WA POLISI ASEMA YAKE


Baada ya kuachana na askofu huyo, mwanahabari wetu alimtafuta Kamanda wa Polisi wa Mjini Magharibi, Kamishna Msaidizi (ACP) Mohamed Haji Hassan ambaye alikiri kuufahamu mgogoro ndani ya kanisa hilo na kusema suala hilo wamemwachia mkuu wa mkoa huo (Hassan Khatib Hassan) ambaye anaendelea kuziweka sawa pande hizo zinazopingana.


Mwanahabari wetu alimtafuta mkuu huyo wa mkoa kwa njia ya simu ambapo simu yake iliita bila kupokelewa kila ilipopigwa.



Shilole Kaona Isiwe TABU Aamua Kuyapa Mapenzi Kisogo


Msanii na mmiliki wa Shishi Food anayefanya poa kwenye miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, kwa sasa ameyapa kisogo mapenzi na badala yake, yuko bize na kazi ili heshima yake isitetereke.


 


Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Shilole au Shishi Baby ambaye siku chache nyuma alimwagana na aliyekuwa mumewe; Ashraf Uchebe, amesema kuwa, ameona akiyaweka tena mapenzi mbele, hayatamzalishia matunda yoyote mazuri, lakini akikazana katika kazi yake, inamletea mafanikio makubwa kuliko mapenzi.


 


“Jamani kwa usawa huu mtu usipobadilika na kuangalia kitu cha maana cha kufanya, ni shida sana.


“Mimi mambo ya mapenzi sasa hivi yanisubirie kwanza nifanye kazi zangu ili nipate maendeleo na siyo mapenzi ambayo kila kukicha wanafaidi mashabiki wa Instagram kukuangalia maisha yako,” anasema Shilole ambaye kesi yake na Uchebe inaendelea mahakamani.



MAGAZETI YA LEO 1/9/2020




















Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...