Search This Blog

Thursday, October 31, 2019

MLEMAVU WA MACHO ATAMANI KUWA MFANYABIASHARA MKUBWA

Na Woinde Shizza, Globu ya jamii Arusha
KIJANA Baraka Imanuel ni kijana mwenye umri wa miaka (24) mkazi wa ngaramtoni halmashauri Arusha iliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, kijana huyu ni mlemavu wa macho (kipofu ) na ni mfanyabiashara ndogomdogo na malengo yake ya kutoka kumiliki biashara ndogo anayoifanya na kuwa mfanyabiashara mkubwa.

Gazeti hili lilipata nafasi ya kuzungumza na kijana huyu na alikuwa na
mengi yakueleza kuhusiana na namna anavyofanya biashara yake

Baraka anafanya biashara ya kuuza viberiti ndani ya jiji la Arusha, kila
asubuhi amekuwa akiamka na kwenda kununua viberiti na kuvitembeza kwa watu mbalimbali na kuuza ili apate chochote kitu kitakacho msaidia kutumia yeye na familia yake.

Baraka ni mtoto wa kwanza katika familia ya mama Beatrice Imanuel
akiwa na wadogo zake wawili mmoja wa kike alimtaja kwa jina la Jackile
Imanuel ambaye yeye yupo nyumbani tu hafanyi kazi yoyote pamoja na
wakiume aliyemtaja kwa jina la Steven Imanuel ambaye yeye ni
anajitolea kufanya kazi ya kusaidia mafundi wa ujenzi ili apate
chochote kitu cha kuwasukuma katika maisha.

Anafafanua kuwa mama yake mzazi anafanya bishara ya mamantile huku
baba yake aliemzaa aliikimbia familia na kutelekeza na kukimbili
pasipo julikana kwa kipindi cha mda mrefu.

Kwanini alianza biashara ilihali ni mlemavu wa macho?
Anaeleza kuwa kitu halisi kilichomsukuma mpaka akaamua kufanya
biashara ya kutembeza viberiti ni kuondokana na utegemezi, kitu
ambacho alisema anakichukia kuliko vitu vyote katika maisha yake japo
kuwa yeye ni kipofu.

Alisema kuwa aliamua kumuomba mama yake mtaji wa kuanza biashara hali kuwa mama yake alikuwa mgumu wa kumpa kutokana na hali yake lakini alimbembeleza hadi mama yake akaamua kumpa mtaji wa shilingi elfu 30, hela ambayo aliamua kwenda kununua nusu katoni ya viberiti na kuanza
kutembeza.

“Mama alinipa mtaji wa shilingi elfu 3o tu na niliamua kuanza
biashara bila kujali hali yangu na mpaka leo nafanya, nilianza na nusu
katoni ya viberiti na sasa hivi naweza nunua katoni moja nzima mbali na
hivyo pia nashukuru Mungu mtaji wangu umekuwa na umefikia kiasi cha
shilingi elfu 70 na hii inatokana na mimi kujali kazi yangu na
kuipenda na pia kuafanya maamuzi ya kutokuwa tegemezi”alibainisha
Baraka.

Anatambuaje Fedha anapopewa na mteja ?
Baraka alifafanua kuwa alibahatika kusoma hadi kidato cha nne ambapo
alisema kuwa elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya msingi Longido mkoani Arusha, huku elimu ya sekondari akiipata katika shule ya Shaibushe iliopo mkoani Shinyanga ambapo walikuwa wakifundishwa na walimu wenye uzoefu wa kutoa elimu kwa wanafunzi wenye uhitaji.

“Nikipewa ela najua hii ni shilingi ngapi kutokana na elimu niliopewa
darasani pia nakisia na kutambua hii ni kiasi gani, pia nashukuru Mungu
maana wateja wengi nao wauzia viberiti wananionea huruma hivyo
hawawezi kunirusha kwani wanaona kabisa hali yangu ilivyo”,alisema

Alibainisha kuwa amekuwa anaamuka kila siku asubui na kwenda kununua
viberiti hivyo katika maduka ya Jumla na amekuwaanatembeza katika
maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha ikiwemo standi, masokoni na hata
katika maeneo ya majumbani kwa watu.

Nini ombi lake kwa serikali na wadau ?
Baraka ameiomba serikali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza katika
kumsaidia kumuongezea mtaji na ikiwezekana kumfungulia sehemu moja
ambayo atakuwa anafanya biashara yake kwa kutulia na kuaachana na
kutembeza barabarani anavyofanya hivyo anahatarisha maisha yake
kwani anaweza kupata ajali kugongwa na hata kuibiwa mtaji wake mdogo
ambao ameukusanya kwa ajili ya kumkimu kimaisha.

Kwa upande wa mama yake Beatrice Imanuel alisema kuwa mtoto wake
Baraka alizaliwa na ulemavu wa macho lakini anashukuru Mungu
amejikubali na anajitambua pia anaweza kujituma hata kufanya biashara
tofauti na walemavu wengine ambao wengi wao wanaombamba omba tu
barabarani na hawana mawazo wa kugundua mradi wowote au biashara
yeyote ambayo inaweza kuwasaidia katika maisha.

Anaongeza kuwa kijana wake amekuwa ni mtu wa kumsaidia katika baadhi
ya maitaji hapo nyumbani kwani amekuwa akinunua vitu mbalimbali na
hata mda mungine wadogo zake wakiumwa na yeye anafedha za kuwapeleka hospitali amekuwa akimega sehemu ya mtaji wake na kuutumia kwa jili ya kuwapeleka hospitali.

Beatrice ametoa wito kwa baadhi ya watu wenye ulemavu na kuwaambia
wasijizarahu pindi wanapokuwa walemavu bali wajaribu kuangali kitu cha
kufanya ambacho kitawakwamua kimaisha na kuachana na biashara ya kukaa na kuomba omba barabarani, pia aliwataka wazazi ambao wanawatoto ambao wanaulemavu wasiwafiche watoto wao ndani bali wawatoe nje wakapate elimu kama vile watoto wengine wanavyopata elimu kwani iwapo watapata elimu itawasaidia kujiongeza katika maisha.

“Nina imani mtoto wangu kama angekuwa hajapata elimu basi asingeweza
kuniomba hela ya mtaji na kujiamini na kwenda kuanzisha biashara
ya kuuza viberiti hii imetokana na kujiamini kwakwe na ndio maana
akaamua kujitoa na kwenda barabarani kufanya biashara naimani huu
wote ni ujasiri ambao alijengewa na walimu wake wakati alipokuwa
shuleni, na kwakweli ananisaidia sana katika maitaji madogo madogo
hapa nyumbani “Alisema Beatrice.

Baadhi ya wananchi ambao wanamshuhudia kijana
Baraka walimpongeza jinsi anavyofanya kazi na kusema kuwa ni vijana
wachache wenye ulemavu ambao wanaweza kujiongeza na kuanza kufanya
biashara kama vile kijana Baraka anavyofanya biashara, huku wengine
wakisikika wakisema ni bora angetafuta biashara ya kukaa sehemu moja
na kufanya na sio kutembeza kwa ajili ya usalama wa maisha yake.


Picha zikionyesha kijana Baraka Imanuel akiendelea kufanya biashara yake ya viberiti katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha.


Twitter yapiga marufuku matangazo ya kisiasa

Jukwaa la mtandao wa kijamii Twitter limetangaza kwamba halitatangaza tena matangazo yenye muelekeo wa kisiasa.

Kiongozi mkuu ( CEO) wa Twitter, Jack Dorsey amearifu kwamba shirika hilo halitatoa tena matangazo yenye muelekeo wa kisiasa.

Dorsey amearifu kwamba uamuzi huo mpya utaanza kutumika mwishoni mwa mwezi Novemba.

Washindani wa mtandao wa kijamii wa Facebook hivi karibuni walifutilia mbali mpango wa kupiga marufuku matangazo ya siasa ya kibiashara.

Taarifa ya marufuku hiyo imeibua mgawanyiko katika kambi za kisiasa nchini Marekani zinapojiandaa katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Brad Parscale,meneja wa kampeni ya Raisi Donald Trump, kugombea muhula wa pili, amesema marufuku hiyo ni jaribio jingine la kumnyamazisha Trump


Spika Ndugai awasihi Wakenya kujifunza zaidi Kiswahili


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewasihi Wakenya kuongeza juhudi katika kujifunza lugha ya Kiswahili kwani kwa sasa ni moja ya lugha rasmi katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kwamba itawasaidia kufanikiwa katika mambo mbalimbali.

Ndugai ametoa kauli hiyo nchini Kenya wakati akizindua Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya kwa lugha ya Kiswahili na matangazo ya moja kwa moja ya bunge.

“Ukitaka kujifunza lugha fulani ni lazima utumie kamusi ya lugha yenywe, kwahiyo ninawatia moyo muendelee kujifunza Kiswahili kwasababu sasa hivi kinatumika kama alugha mojawapo muhimu na rasmi katika Jumuiya ya SADC, Umoja wa Afrika, Bunge la Afrika lakini pia kwenye Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki kiswahili ni moja ya lugha rasmi inayotumika.

“Ili uweze kupata mafanikio ni vizuri ukajua lugha ya kiswahili hata kama ni kile cha kuombea maji, sio vibaya kuzungumza kiingereza lakini ili uweze kufanikiwa katika mambo yako unayoyafanya ni vyema ukajifunza Kiswahili pia,” amesema Ndugai.

Aidha amewapongeza kwa taarifa za kamati walizoziandaa na kwa hatua waliyoifikia ya kurusha mubashara matangazo ya kamati za bunge kwaajili ya wananchi wa Kenya kuona kinachoendelea.

RC Singida akabidhi Gari kikosi cha Zimamoto na Uokoaji


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wananchi kujiepusha na majanga ya moto yanayotokana na uzembe au makusudi kwa kigezo cha kutegemea uwepo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Dkt. Nchimbi aliyasema hayo wakati akikabidhi gari aina ya‘Land Lover Defender’kwa Jeshi la Zima moto na Uokoji mkoani hapa litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za utawala.

“Natarajia gari hili liitasaidia kurahisisha majukumu ya kijeshi kwa Jeshi hili, hususan kwenye eneo la utoaji elimu na kujenga maarifa kwa jamii katika kuhakikisha suala la kinga linapewa kipaumbele ili kuepusha maafa na ajali zozote huko mbeleni,” alisema Nchimbi.

Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi hilo mkoani hapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella, alisema gari hilo litatumika kwa shughuli zote za dharula ndani ya jeshi hilo chini ya uratibu wa idaraya utawala.

“Ifahamike kuwa Jeshi la Zima moto na Uokoaji linahusika nadharula zote ikiwemo majanga ya moto, tetemeko la ardhi, mafuriko na uzazi isipokuwa jinai pekee,” alisema Ombella

Aidha, aliwatahadharisha wananchi kuwa makini kwa kujiepusha na majanga ya moto hasa nyakati za utayarishaji wa mashamba kwa kuzingatia usalama na utunzaji mzuri wa mazingira kulingana na eneo husika.

Tanzania kuanzisha kituo cha Kimahakama na usuluhishi wa migogoro ya Kimataifa


Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimekubaliana kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) hususani katika kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya Kimataifa katika maeneo ya madini, biashara na usuluhishi na makampuni ya Kimataifa pamoja na mafuta na gesi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo mara baada ya majadiliano na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) Bwana Stephen Karangizi mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory Coast.

Prof. Kabudi amesema kuwa lengo la majadiliano hayo ni kuisaidia Tanzania kuweka mikakati kuimarisha sekta ya Sheria ikiwa ni pamoja na kuiongezea uwezo ofisi ya mwanasheria mkuu wa Tanzania hasa baada ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa ya muundo mpya wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ili kuiwezesha kutoa ushauri wa kina na wa kitaalam kwa serikali lakini pia kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya Kimataifa.

Ameongeza kuwa maombi ya Tanzania kwa taasisi hiyo kwa ajili ya kuisaidia ofisi ya mwanasheria na wakili mkuu wa serikali yamekamilika na kinachosubiriwa hivi sasa ni kuwasilisha maombi hayo kwa kikao cha bodi ili utekelezaji uanze.

Ameongeza kuwa eneo jingine ambalo Tanzania inahitaji msaada kutoka kwa  Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ni kuhusu kuisaidia Tanzania katika hatua iliyoichukua ya kutunga sheria mpya ya usuluhishi wa migogoro ya kimataifa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo kipya cha kusimamia usuluhishi wa migogoro.

Katika eneo hilo Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itatoa wataalamu kusaidia Tanzania kupitia  miswaada ambayo imeandaliwa na serikali pia kuandaa andiko la namna kituo hicho kitawekwa Tanzania na kukidhi matakwa ya kimataifa.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika Bw Stephen Karangizi amesema wamepokea ombi hilo na kwamba wanasubiri maamuzi ya kikao cha bodi ili kuweza kuanda program maalum kwa ajili ya kuimarisha na kuendeleza ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.

Ameongeza kuwa nchi nyingi za Kiafrika zimeshindwa katika usuluhishi wa migogoro hususani ya kibiashara,madini,mafuta na gesi na maeneo mengine na kuongeza kuwa suala hilo linapaswa kuwekewa mkakati maalum na kutekelezwa kwa haraka ili kuepuka makosa yaliyokwisha kufanywa katika siku zilizopita.

Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyo chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ilianzishwa kutokana na ombi la Mawaziri wa fedha kutoka Afrika kwa lengo la kuzisaidia Nchi za Afrika kujijengea uwezo katika masuala ya kisheria hususani katika  madini,mafuta na gesi pamoja na madeni ili kuziwezesha nchi za Kiafrika kuwa na uwanda sawa wa majadiliano katika ngazi za Kimataifa kuhusu masuala ya kisheria yanahusu biashara na makampuni ya Kimataifa.

TANECU yauza tani 13,181 za Korosho


Na. Ahmad Mmow, Newala

Chama kikuu cha ushirika cha Tandahimba and Newala Co-operative Union( TANECU) mkoani Mtwara, jana kiliuza korosho za wakulima zenye uzito wa tani 13,181 katika mnada wa kwanza kwa msimu wa 2019\2020 uliofanyika mjini Newala.

 Katika mnada huo ambao ulihudhuriwa na kushuhudiwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa bei ya juu ilikuwa shilingi 2,526 kwa kilo moja huku bei ya chini ikiwa shilingi 2,468.

Taarifa ya makusanyo ya Korosho na kiasi kilichoingizwa katika mnada iliyosomwa na meneja mkuu wa TANECU Ltd ,Mohammed Nassoro  ilibainisha kuwa Korosho zilizouzwa zilikuwa kwenye maghala makuu ya TANECU yaliyopo Newala na Tandahimba na Agrofocus Newala.

 Ilieleza kwamba katika ghala la Agrofocus ziliuzwa tani 194, ghala la TANECU Newala ziliuzwa tani 6,303 na ghala la TANECU Tandahimba ziliuzwa tani 6,682.

Baada ya kaimu mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania, Frances Alfred  kutoa taarifa ya bei ya korosho katika soko la Dunia hadi kufikia jana  kuwa Korosho zinauzwa kwa kati ya shilingi 2,440 hadi shilingi 2,740. Wakulima walikubali ziuzwe kwa bei zilizofikiwa na wanunuzi.

Aidha mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa  aliwasisitiza viongozi wa chama kikuu hicho na bodi ya korosho Tanzania kuharakisha mchakato wa malipo ili wakulima walipwe fedha zao kwa muda muafaka.

Katika mnada huo kampuni 28 zilijitokeza kuomba kununua, ambapo hitaji la kampuni hizo lilikuwa ni tani 40,000. Hatahivyo  korosho  zilizokusanywa hadi tarehe 29, mwezi huu( Oktoba),mwaka 2019 na kuuzwa kwenye mnada huo ni hizo tani 13,181.



Serikali imeweka mkazo katika sekta ya Michezo - Naibu Waziri Ole Nasha


Na. Ezekiel Mtonyole

Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele katika kuimarisha michezo kama eneo muhimu la mtaala wa mafunzo ya ualimu kutokana na ukweli kwamba michezo inaimarisha stadi za kujifunza, nidhamu na ni ajira pia.


Hayo yamesemwa Mkoani Mtwara na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati wa kufunga Mashindano ya Kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu Tanzania Bara (UMISAVUTA).

Amesema pamoja na kuwepo kwa mchepuo wa michezo katika baadhi ya vyuo vya Ualimu ni vizuri Vyuo hivyo kupitia Ofisi ya Kamishna wa Elimu wakaweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ufundishaji na ujifunzaji wa michezo na sanaa unalenga kuwawezesha vijana kufanya vizuri katika eneo hilo kwa maendeleo yao na Taifa.

Ametaja Vyuo ambavyo kwa sasa vinatoa mchepuo wa michezo kuwa ni Chuo cha Ualimu Tarime, Butiama, Butiama Mtwara Kawaida na Ilonga na kwamba Wizara itahakikisha kuwa michezo inaimarishwa katika vyuo vyote vya ualimu nchini.

Naibu Waziri Ole Nasha amevitaka vyuo vya ualimu kuhakikisha vinaendeleza michezo chuoni  kutokana na faida zitokanazo na michezo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha  wahitimu wa mafunzo ya ualimu wanapata mafunzo ambayo wakihitimu wanakwenda kuwa walimu mahiri wa michezo katika shule za msingi na sekondari ambapo ndipo wanamichezo na wasanii wanaandaliwa.

“Nimefarijika kuona mashindano ya michezo na sanaa kwa vyuo vya ualimu imerudi tena baada ya kutokuwepo kwa miaka 20 iliyopita, hatuna budi kuwekeza katika michezo kwa sababu ni fursa za kuweza kusaidia kukua kiuchumi. Nchi nyingi duniani michezo imekuwa sehemu kubwa ya kusaidia kukua kiuchumi,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambae pia ni Afisa Elimu Mkoa Germina Mng’aho amesema kufanyika kwa michezo hiyo ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo inataka kuwepo kwa mashindano ya michezo kwa shule na vyuo ili kuwezesha kuinua vipaji ambavyo vitaleta mafanikio katika michezo ya kitaifa na kimataifa.

Nae Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Seksheni ya Mafunzo ya Ualimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Agusta Lupokela amesema anaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutambua faida zinazopatikana katika michezo ikiwemo stadi za kujifunza na kuamua kurejesha mashindano ya michezo kwenye Vyuo vya Ualimu.

Akitoa taarifa ya mashindano hayo kwa  Naibu Waziri Mwenyekiti wa UMISAVUTA Taifa Agustine Sahili amesema kuwa michezo hiyo imeendeshwa kulingana na taratibu za michezo na matokeo yameamuliwa kwa weledi na haki katika kupata washindi.

Sahili ameiomba  Wizara  kuimarisha kozi ya michezo na fani mbalimbali za ndani katika vyuo vya ualimu ili wataalamu waweze kupatikana shuleni ambako ndiko chimbuko halisi la vipaji linapatikana lakini pia kuwajengea uwezo wasimamizi na waamuzi wa michezo kwa kuendesha kozi fupi na ndefu kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Pia ameiomba Wizara kuongeza wakufunzi wa michezo na Sanaa vyuoni kwani kwa sasa vyuo vingi havina wakufunzi wa aina hiyo hali inayodunisha uendeshaji wa michezo na ukuzaji wa vipaji kwa vijana chuoni ambapo pia inasababisha shule za msingi na sekondari kukosa walimu mahiri katika michezo na Sanaa.

Nae Mshiriki wa Mashindano ya Michezo na Sanaa  Albert Thomas kutoka Kanda ya Ziwa ameishukuru Serikali kwa kurejesha mashindano ya UMISAVUTA kwani inawasaidia kujenga  afya na akili lakini pia inawasaidia kuwa na uelewa wa masula ya michezo na kutoa elimu ya michezo kwa wanafunzi ambao watakwenda kuwafundisha  baada ya kumaliza masomo yao. Ameiomba Serikali kuendeleza vipaji vya wanamichezo wanaoshinda katika mashindano ya ngazi ya shule na vyuo ili visiishie kwenye ngazi ya kitaifa bali katika ngazi za kimataifa.

Ufungaji wa mashindano ya Kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa vyuo vya ualimu yaliyoanza Oktoba 25, 2019 na kuhitimishwa Oktoba 31, 2019 yamepambwa na mechi kati ya Kanda ya ziwa na Kanda ya kusini ambapo Kanda ya ziwa wameibuka kidedea baada ya kuwafunga Kanda ya Kusini goli moja kwa sifuri.



VIDEO: Aggrey Mwanri auwasha moto viongozi wa Hospitali hali tete

\
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameutaka uongozi wa hospitali ya wilaya ya ya Uyui ifikapo tarehe kumi November mwaka huu iwe imekamilika ili iweze kutoa huduma ka wananchi.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE



UZINDUZI WA KITABU NA FILAMU KUHUSU HISTORIA YA RELI YA TAZARA WAFANYIKA JIJINI BEIJING CHINA

Uzinduzi wa Kitabu na Filamu kuhusu historia ya Reli ya TAZARA umefanyika leo Beijing. 

Hafla hiyo ni sehemu ya matukio yanayoendelea ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanayofanywa na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University. 

Ujenzi wa Reli ya TAZARA ni moja ya ‘legacy’ ya Baba wa Taifa inayoenziwa nchini China ikiwa ni alama ya urafiki kati ya China na Bara la Afrika.

Katika hafla hiyo Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University kimetangaza dhamira yake kuanzisha kozi ya lugha ya Kiswahili. Vilevile, wameeleza mpango wa kuanzia kituo cha mafunzo ya uongozi kitakachojulikana kama Julius Nyerere Study Centre.  

Kituo hicho kitashughulika na tafiti mbalimbali juu ya falsafa za Uongozi Barani Afrika.  Rais wa Zhejiang Normal University na  Balozi wa Zambia Mhe Winnie Chibesakunda, Mabalozi na Wanazuoni pia wameshiriki hafla hii. Habari/Picha kwa hisani ya Phelista Wegessa
 Balozi wa Tanzania nchini China,Mhe.Mbelwa Kairuki akizungumza kwenye hafla ya Uzinduzi wa Kitabu na Filamu kuhusu historia ya Reli ya TAZARA uliofanyika jijini Beijing. Hafla hiyo ni sehemu ya matukio yanayoendelea ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanayofanywa na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University. 
Picha ya pamoja wakati wa uzinduzi 
 Wadau mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo






RC DKT. REHEMA NCHIMBI AKABIDHI GARI KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI MKOA WA SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akipeana mkono na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani hapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella wakati akikabidhi gari aina ya‘Land Lover Defender’ kwa Jeshi hilo katika hafla iliyofanyika jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragili.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella akizunguza baada ya kukabidhiwa gari hilo.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella (wa pili kulia) akiwa na maofisa wa jeshi hilo katika hafla ya kukabidhiwa gari hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa huo katika hafla ya kukabidhi gari hilo.
Gari aina ya ‘Land Lover Defender’ lililokabidhiwa kwa Jeshi la Zima moto na Uokoji mkoani hapa. 


Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wananchi kujiepusha na majanga ya moto yanayotokana na uzembe au makusudi kwa kigezo cha kutegemea uwepo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Dkt. Nchimbi aliyasema hayo jana wakati akikabidhi gari aina ya‘Land Lover Defender’kwa Jeshi la Zima moto na Uokoji mkoani hapa litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za utawala.

“Natarajia gari hili liitasaidia kurahisisha majukumu ya kijeshi kwa Jeshi hili, hususan kwenye eneo la utoaji elimu na kujenga maarifa kwa jamii katika kuhakikisha suala la kinga linapewa kipaumbele ili kuepusha maafa na ajali zozote huko mbeleni,” alisema Nchimbi.

Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi hilo mkoani hapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella, alisema gari hilo litatumika kwa shughuli zote za dharula ndani ya jeshi hilo chini ya uratibu wa idaraya utawala.

“Ifahamike kuwa Jeshi la Zima moto na Uokoaji linahusika nadharula zote ikiwemo majanga ya moto, tetemeko la ardhi, mafuriko na uzazi isipokuwa jinai pekee,” alisema Ombella

Aidha, aliwatahadharisha wananchi kuwa makini kwa kujiepusha na majanga ya moto hasa nyakati za utayarishaji wa mashamba kwa kuzingatia usalama na utunzaji mzuri wa mazingira kulingana na eneo husika.


WANANCHI MAKUNGU WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI NA KINGU KUWACHIMBIA MAJI

 Mbunge Kingu akiwahutubia wananchi hao katika mkutano wa hadhara.

 Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Makungu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida juzi,  wakati akikagua mradi wa maji waliowezeshwa na Rais John Magufuli.
 Katibu Muenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Iyumbu, Lameck Maguni akizungumza kwenye mkutano huo.
 Wananchi wa Kijiji cha Iyumbu wakiwa kwenye mkutano.
 Katibu wa CCM Kata ya Iyumbu, Mohammed Itambu akizungumza.
 Mbunge Kingu akiserebuka katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM Tawi la Makungu, Weja Ng'waya akizungumza.
 Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Iyumbu, Njile Gasamalu akizungumza.
 Diwani wa Kata ya Iyumbu, Peter Gwiligwa akizungumza.
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Iyumbu, Juma Okumu akizungumza.
 Wananchi wa Kijiji cha Iyumbu wakiwa kwenye mkutano.
Kingu akiwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha.

Na Dotto Mwaibale, Singida
WANANCHI wa Kijiji cha Makungu Kata ya Iyumbu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamemshukuru Rais John Magufuli na Mbunge wao Elibariki Kingu kwa kuwachimbia kisima cha 
maji.

Shukurani hizo walizitoa juzi katika mkutano wa hadhara aliouandaa mbunge huyo wakati akikagua miradi ya maendeleo pamoja na kuwahamasisha kujiandikisha kwa wingi ili waweze kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mwishoni mwa mwaka jana wananchi hao walizuia msafara wa mbunge huyo na kumuonesha mabango yenye kero mbalimbali kubwa ikiwa ni kukosa maji ambapo aliipeleka kwa Rais Magufuli ambaye amewachimbia kisima hicho ambacho kitasambaza maji katika kijiji hicho na vitongoji vingine vya jirani.

Kingu alisema wanamshuru Rais John Magufuli kwa kusikia kilio chao hivyo kutokana na heshima hiyo aliowapa watahakikisha  viongozi wote katika uchaguzi wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji wanatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)" Ndugu wananchi heshima pekee ya kumshukuru Rais wetu kwa kutuletea mradi huu wa maji ni  kuhakikisha tunakipa ushindi mkubwa chama chetu naombeni twendeni tukajiandikishe kwa wingi na siku ikifika ya kupiga kura basi tuwachague viongozi watakaounda serikali kupitia CCM" alisema Kingu.

Alisema serikali imewapendelea sana Jimbo la Singida Magharibi kwa kuwapelekea miradi ya  maji 24 na sasa hivi kuna magari mawili yenye mitambo ya kuchimba maji yapo maeneo mbalimbali ya jimbo hilo ambapo katika kijiji hicho maji yaliyopatikana yatakuwa yakitoka lita 11,000 kwa saa na kuwa sh.350 milioni zimetengwa kwa ajili ya miundo mbinu ya kusambaza maji kwenye kijiji hicho na kufunga DP.


SERIKALI KUWEKA KIPAUMBELE MICHEZO KWENYE MTAALA WA MAFUNZO YA UALIMU

Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele katika kuimarisha michezo kama eneo muhimu la mtaala wa mafunzo ya ualimu kutokana na ukweli kwamba michezo inaimarisha stadi za kujifunza, nidhamu na ni ajira pia.

Hayo yamesemwa Mkoani Mtwara na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati wa kufunga Mashindano ya Kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu Tanzania Bara (UMISAVUTA).

Amesema pamoja na kuwepo kwa mchepuo wa michezo katika baadhi ya vyuo vya Ualimu ni vizuri Vyuo hivyo kupitia Ofisi ya Kamishna wa Elimu wakaweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ufundishaji na ujifunzaji wa michezo na sanaa unalenga kuwawezesha vijana kufanya vizuri katika eneo hilo kwa maendeleo yao na Taifa. 

Ametaja Vyuo ambavyo kwa sasa vinatoa mchepuo wa michezo kuwa ni Chuo cha Ualimu Tarime, Butiama, Butiama Mtwara Kawaida na Ilonga na kwamba Wizara itahakikisha kuwa michezo inaimarishwa katika vyuo vyote vya ualimu nchini.

Naibu Waziri Ole Nasha amevitaka vyuo vya ualimu kuhakikisha vinaendeleza michezo chuoni  kutokana na faida zitokanazo na michezo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha  wahitimu wa mafunzo ya ualimu wanapata mafunzo ambayo wakihitimu wanakwenda kuwa walimu mahiri wa michezo katika shule za msingi na sekondari ambapo ndipo wanamichezo na wasanii wanaandaliwa.

“Nimefarijika kuona mashindano ya michezo na sanaa kwa vyuo vya ualimu imerudi tena baada ya kutokuwepo kwa miaka 20 iliyopita, hatuna budi kuwekeza katika michezo kwa sababu ni fursa za kuweza kusaidia kukua kiuchumi. Nchi nyingi duniani michezo imekuwa sehemu kubwa ya kusaidia kukua kiuchumi,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha. 

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambae pia ni Afisa Elimu Mkoa Germina Mng’aho amesema kufanyika kwa michezo hiyo ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo inataka kuwepo kwa mashindano ya michezo kwa shule na vyuo ili kuwezesha kuinua vipaji ambavyo vitaleta mafanikio katika michezo ya kitaifa na kimataifa.

Nae Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Seksheni ya Mafunzo ya Ualimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Agusta Lupokela amesema anaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutambua faida zinazopatikana katika michezo ikiwemo stadi za kujifunza na kuamua kurejesha mashindano ya michezo kwenye Vyuo vya Ualimu.

Akitoa taarifa ya mashindano hayo kwa  Naibu Waziri Mwenyekiti wa UMISAVUTA Taifa Agustine Sahili amesema kuwa michezo hiyo imeendeshwa kulingna na taratibu za michezo na matokeo yameamuliwa kwa weledi na haki katika kupata washindi.

Sahili ameiomba  Wizara  kuimarisha kozi ya michezo na fani mbalimbali za ndani katika vyuo vya ualimu ili wataalamu waweze kupatikana shuleni ambako ndiko chimbuko halisi la vipaji linapatikana lakini pia kuwajengea uwezo wasimamizi na waamuzi wa michezo kwa kuendesha kozi fupi na ndefu kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Pia ameiomba Wizara kuongeza wakufunzi wa michezo na Sanaa vyuoni kwani kwa sasa vyuo vingi havina wakufunzi wa aina hiyo hali inayodunisha uendeshaji wa michezo na ukuzaji wa vipaji kwa vijana chuoni ambapo pia inasababisha shule za msingi na sekondari kukosa walimu mahiri katika michezo na Sanaa.

Nae Mshiriki wa Mashindano ya Michezo na Sanaa  Albert Thomas kutoka Kanda ya Ziwa ameishukuru Serikali kwa kurejesha mashindano ya UMISAVUTA kwani inawasaidia kujenga  afya na akili lakini pia inawasaidia kuwa na uelewa wa masula ya michezo na kutoa elimu ya michezo kwa wanafunzi ambao watakwenda kuwafundisha  baada ya kumaliza masomo yao. Ameiomba Serikali kuendeleza vipaji vya wanamichezo wanaoshinda katika mashindano ya ngazi ya shule na vyuo ili visiishie kwenye ngazi ya kitaifa bali katika ngazi za kimataifa.

Ufungaji wa mashindano ya Kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa vyuo vya ualimu yaliyoanza Oktoba 25, 2019 na kuhitimishwa Oktoba 31, 2019 yamepambwa na mechi kati ya Kanda ya ziwa na Kanda ya kusini ambapo Kanda ya ziwa wameibuka kidedea baada ya kuwafunga Kanda ya Kusini goli moja kwa sifuri.
Naibu waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akitoa kombe la ushindi wa mpira wa miguu kwa wachezaji wa kanda ya ziwa wakati wa ufungaji wa mashindano ya kitaifa ya Michezo na Sanaa ya Vyuo vya Ualimu UMISAVUTA yaliyomalizika leo mkoani Mtwara.

 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akisalimiana na wachezaji kabla ya kuanza mechi wakati wa ufungaji wa Mashindano ya Kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu Tanzania Bara ,yaliyofanyika Mkoani Mtwara.



MRADI WA MAJI WA KISARAWE KUANZA KUTOA MAJI MWEZI UJAO

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi wa Uwekezaji na Miradi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Ramadhani Mtindasi katika kituo cha kusukumia maji Kibamba, wilayani Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) pamoja na Mkuu wa Wilaya za Ubungo, Kisare Makori (kulia) na Mkuu Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (kushoto) katika ziara ya kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Kisarawe, katika Kata ya Kibamba, wilayani Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa na mkandarasi alipotaka maelezo kuhusu utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwake jana ya kukamilisha utaratibu wa malipo na kazi ya kuvuta umeme.
Tenki la maji la Kibamba lenye ujazo wa lita milioni kumi litakolotumika kuhifadhi maji yatakayo hudumia wakazi wa Kisarawe kupitia Mradi wa Maji wa Kisarawe.



Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa na Msimamizi wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kisarawe, Mhandisi Ishmaeli Kakwezi wakati akikagua tenki la maji la Kibamba lenye ujazo wa lita milioni 10.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa kwenye eneo palipo na maunganisho ya bomba la tenki la Kibamba na bomba linalopeleka maji katika Mji wa Kisarawe.
…………………….

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ametembelea na kukagua utekelezaji wa kazi ndogo zilizobaki katika ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kisarawe katika Kata ya Kibamba, wilayani Ubungo.

Ziara imelenga kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa jana kwa mkandarasi kukamilisha utaratibu wa malipo na kazi ya kuvuta umeme ifanyike haraka ili mradi uanze kufanya kazi mwezi ujao.

Malipo ya Shilingi milioni nane kwa TANESCO yameshafanyika na kazi ya kufunga umeme huo itaanza mara moja tayari kwa kufanya majaribio ya kusukuma maji (pump test) wiki ijayo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Aweso ameambatana na Wakuu wa Wilaya za Ubungo, Kisare Makori na Kisarawe, Jokate Mwegelo akiwasisitiza umoja na ushirikiano katika kufanikisha zoezi la utekelezaji wa mradi huo kwa maslahi mapana ya wananchi wa Kisarawe. 

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori ametoa rai kwa viongozi na watendaji wa wilaya za Ubungo na Kisarawe kujitoa na kusimamia miradi ya maendeleo inayotumia fedha nyingi, hatua itakayosaidia juhudi za Serikali kuzaa matunda.


RC SINGIDA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TATU WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA (SIFACU LTD)

 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi, akihutubia wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama Kikuu cha Ushirika (SIFACU Ltd) mkoani hapa juzi. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Uzalishaji Mkoa wa Singida, Beatus Choaji,  Mkuu wa Wilaya ya Singida,  Mhandisi Paskasi Muragili, Mwenyekiti wa  chama kikuu cha ushirika mkoa wa Singida,  Khamis  Mwanjowa na  mrajisi msaidizi wa  vyama vya ushirika mkoa wa Singida,  Thomas Nyamba.
 Mrajisi msaidizi wa  vyama vya ushirika mkoa wa Singida,  Thomas Nyamba, akizungumza katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa  chama kikuu cha ushirika mkoa wa Singida,  Khamis  Mwanjowa, akizungumza.
 RC Nchimbi na wajumbe wa mkutano huo wakiserebuka.
 RC Nchimbi na wajumbe wa mkutano huo wakiserebuka.
 Mkutano ukiendelea.
 Mkutano ukiendelea. 
 RC Nchimbi akikagua bidhaa za wajasiriamali.
 Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja. 

Na Waandishi Wetu, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi ametoa miezi miwili kwa Mrajisi wa Vyama vya Ushirika mkoani hapa kuhakikisha anafanya ukaguzi kwa vyama vyote ambavyo bado havijakaguliwa, na kinyume chake hataruhusu mchakato wowote wa mikopo kufanyika.

Dk.Nchimbi aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa tatu wa Chama Kikuu cha Ushirika (SIFACU Ltd) mkoani hapa juzi.

“Ukaguzi kwenye vyama hivi ni lazima na sio hiari, nakuagiza mrajisi ndani ya miezi miwili vyama vyote  vilivyobaki viwe vimekaguliwa na  chama kisichokaguliwa kisipewe mkopo wowote,” alisema Nchimbi
Alisema kwa mkoa wa Singida inasikitisha kuona takwimu zinaonyesha kati ya jumla ya vyama 320 vilivyopo ni vyama 70 pekee ndivyo vilivyokaguliwa jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali chanya  wa uhai wa ushirika na wanaushirika wenyewe.

Alisisitiza kuwa, ushirika pamoja na mambo mengine ni lazima utembee na ajenda ya mshikamano, nguvu, heshima na uhai endelevu sanjari na kuweka kando masuala yote yanayoweza kuufifisha ikiwemo ubinafsi na migogoro isiyokoma.

“Utakuta kila siku  vitu vinavyoleta utapiamlo kwenye vyama hivi vya ushirika ni ubinafsi…watu wamesahau kabisa kuwa ushirika ni utumishi ndio maana rushwa imetamalaki na matokeo yake ni kufifisha matarajio yake chanya,” alisema Nchimbi.

Alisema anatamani moja ya ajenda kubwa ya wanaushirika wote iwe ni kutafuta suluhisho la lishe bora kwa watoto waliopo mashuleni ili hatimaye kuwawezesha kujenga utulivu wa akili kuweza kumsikiliza vizuri mwalimu na kumudu masomo yao.

Dkt. Nchimbi aliwakumbusha wana ushirika wote nchini, hususan wale wa mkoa wa Singida kutambua kwamba wao ni nguzo na mkono wa serikali katika kushauri, kuongoza, kuelekeza na kuifikisha jamii na taifa kwenye uchumi wa viwanda kama ishara na tunda la serikali iliyopo madarakani kwa sasa.

Kwa upande wake, Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoani hapa, Thomas Nyamba, alisema hali ya vyama vya ushirika ndani ya mkoa wa Singida inaendelea kuimarika ikilinganishwa na huko nyuma, huku idadi ya vyama hivyo ikifikia 320.

“Tuna jumla ya vyama vya ushirika mia tatu na ishirini, kati ya hivyo sitini na tisa ni vile vya mazao hususan pamba, huku upande wa saccos hali sio ya kuridhisha kutokana na vingi kati yake kukabiliwa na madeni,” alisema Nyamba.

Makamu Mwenyekiti wa SIFACU, Yahaya Ramadhan Khamis alibainisha pamoja na mambo mengine lengo la mkutano huo mkuu ni kutathmini shughuli zote zilizofanywa kwa mwaka uliopita na kupanga mipango ya mwaka unaoanza.

“Mwaka uliopita tumefaulu kuunganisha vyama na wanachama wakekutoka idadi ya vyama thelathini na sita hadi sitini na sita, tumeweza pia kutafuta masoko ya uhakika, kuwaunganisha wakulima kuweza kupata mikopo kwenye taasisi mbalimbali za fedha,” alisema Khamis


Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...