Search This Blog
Tuesday, March 31, 2020
Africa Is Two to Three Weeks Away From Height of Virus Storm!
(Bloomberg) -- Africa is two to three weeks away from the worst of the coronavirus storm and needs an emergency economic stimulus of $100 billion to bolster preventative measures and support its fragile healthcare systems, according to the United Nations Economic Commission for Africa.
Almost half of the funds could come from waiving interest payments to multilateral institutions. That would give countries the fiscal space needed to impose social-distancing measures, widen social safety nets and equip hospitals to treat the sick ahead of an expected surge in infections, UNECA Executive Secretary Vera Songwe said by phone from Washington.
“If we want to have a fighting chance, we need it immediately,” she said. “In the next two to three weeks, if we act really decisively, we may be able to flatten the curve and then when the storm comes it will be not be as brutal as we see in Europe.”
One measure that can provide some immediate relief is the creation of the special purpose vehicle requested by African finance ministers through which interest payments on sovereign bonds could be sequestered and provide all countries on the continent, regardless of income level, with support, she said.
Stressed Systems
A lack of resources and staff means authorities must work fast to limit the spread of the disease on a continent where hospitals have an average of just 1.8 beds per 1,000 people, UNECA data show. While Africa accounts for 1% of global health expenditure, it carries 23% of the disease burden, including hundreds of thousands of deaths each year from malaria, HIV/Aids and tuberculosis.
“Our hospital systems are so weak and so stressed already that another stress on them is going to break them,” Songwe said.
There are more than 3,000 Covid-19 infections in 46 countries across the continent, according to the Addis Ababa-based Africa Centres for Disease Control and Prevention.
The continent has never experienced a crisis of the scale and magnitude caused by the coronavirus pandemic, Songwe said. While its impact is likely to be felt for 12 to 18 months -- with a loss of lives, jobs and businesses as economies grind to a halt -- the potential loss of health care providers and schooling would also weigh on the continent’s health and education sectors for years to come, she said.
A coordinated global effort is required to assist countries and businesses, and support the recovery of economies across the world, she said.
“If there is one African country or one country anywhere in the world that still has the coronavirus, the whole world has it. We’ve seen the speed of contamination and how quickly it can re-spread,” Songwe said.
For more articles like this, please visit us at bloomberg.com
©2020 Bloomberg L.P.
Forewarned is forearmed!
Mwasika awashangaa Tshabalala, Jafary

BEKI wa kushoto wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Stephano Mwasika anashangazwa na kitendo cha wachezaji wa nafasi kama yake hawafungi mabao.
Mwasika alicheza beki ya kushoto kwa mafanikio katika timu hizo mbili pamoja na Tanzania Prisons ya Mbeya alikoanzia.
“Enzi zetu tulikuwa tunafunga mabao. Unacheza kulinda pembeni lakini wakati huo unaitafutia timu yako ushindi kwa kutafuta nafasi za kufunga mabao na unafanikiwa,” alisema Mwasika.
“Lakini, siku hizi mabeki wa pembeni hawafungi sijui tatizo, au kutofuata maagizo wanayopewa na walimu wao,” alisema.
Msimu ambao Mwasika alifunga mabao mengi ni 2007-2008 ambao Michael Katende raia wa Uganda akiwa Kagera Sugar alikuwa mfungaji.
Mwasika akiwa Tanzania Prisons, alimaliza na mabao saba na kushika nafasi ya nne.
Kocha wa JKT Tanzania, Abdallah Mohammed ‘Bares’ amesema katika kufunga inategemea na aina ya maagizo anayopewa na benchi la ufundi na kipaji cha mchezaji.
“Kabla ya yote kufunga ni kipaji kwa sababu kuna mabeki wa pembeni wazuri wanapanda juu vizuri lakini wanakosa umakini katika kufunga,” alisema Bares.
“Kufunga ni kipaji tena kwa beki ni kitu kikubwa kwa cha ziada si wote wanaweza kufunga. Ukija kwenye mipango ya mwalimu kuna aina ya mabeki hao wa pembeni wanapewa maagizo ya kucheza maeneo husika. Atembee na mtu fulani, akabe eneo lipi .”
Bares aliwataja mabeki wa pembeni ambao kama watajipanga wanaweza kufunga kitaalamu ni mabeki wa Azam FC, Nicholas Wadada raia wa Uganda na Mzimbabwe Bruce Kangwa wa Simba Mohammed Hussein na Shomari Kapombe, Juma Abdul wa Yanga na Michael Idan wa JKT Ruvu.
Kavila: Ninacheza mwaka mmoja tu

ALIYEKUWA Nahodha na beki wa kati wa Kagera Sugar, George Kavila amesema akirudi uwanjani basi anajipa mwaka mmoja tu ndipo atundike daruga rasmi.
Mkongwe huyo ambaye aliitumikia Kagera Sugar kwa zaidi ya miaka 15, msimu huu hajaonekana uwanjani baada ya kuachwa kikosi hicho chini ya Kocha Mecky Maxime huku na yeye akisema alihitaji kupumzika.
Kavila alisema kwa sasa anaendelea kujifua mdogo mdogo na msimu ujao anahitaji kuja kivingine na kubainisha kuwa bado hajafikia muda wa kustaafu soka.
“Msimu huu nimeamua kutocheza kutokana na changamoto za hapa na pale, lakini kwa sasa naendelea kujifua ili msimu ujao nirudi kivingine nikiwa na timu mpya ya Ligi Kuu,” alisema Kavila.
Beki huyo wa kati aliongeza kuwa anachojivunia hadi sasa ni historia na heshima aliyojiwekea kwa kipindi chote alipokuwa akikichafua hivyo hata msimu ujao anaamini ataendeleza moto wake.
Alisema kikubwa ni wadau na mashabiki wake kuendelea kumpa sapoti na kwamba anahitaji kucheza msimu mmoja tu ili aweze kutangaza rasmi kutundika daluga.
Uganda yathibitisha kuwa na wagonjwa 44 wa Covid 19
Kupitia matangazo ya televisheni, alisema kuwa wagonjwa wote wapya walikuwa karantini baada ya kurejea kutoa ughaibuni , ingawa hakueleza afya zao zikoje kwa sasa na walikuwa wametoka taifa gani.
Mara nyingi kwaya hiyo huwa inatumbuiza katika nchi za ughaibuni kama Marekani, Canada na Uingereza.
Mpaka sasa Uganda imethibitisha kuwa na wagonjwa wa Corona 44.
Katika hatua za kukabiliana na maambukizi ya corona, tayari rais wa Uganda Yoweri Museveni ametagaza masharti zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada ya kupiga marufuku usafiri wa Umma.
Katika hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni usiku wa Jumatatu Bw. Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku.
Mtu yeyote anayehitaji huduma za dharura za kiafya kama vile kujifungua au kufanyiwa upasuaji anatakiwa kupata idhini kutoka kwa maafisa wa serikali katika ngazi ya Wilaya kabla ya kutoka nyumbani
Wauzaji bidhaa za chakula sokoni watahitajika kuondoka maeneo yao ya biashara hadi pale serikali itakapokamilisha kushughulikia maeneo mapya ya wao kuuzia bidhaa zao .
Rais Museveni pia ameahidi msaada wa chakula kwa watu ambao hawafanyi kazi kutokana na vikwazo vya kukabiliana na covid-19 na hawana uwezo wa kujipatia bidhaa hiyo muhimu.
Bw. Museveni pia ametoa agizo kwa polisi kuwakamata wanasiasa watakaotoa misaada ya chakula kwa jamii na kushtakiwa kwa ''jaribio la mauaji ''
Uganda kufikia sasa imethibitisha kuwa na wagonjwa 33 wa corona na maafisa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.
Dkt. Mabula Awaka, Wakurugenzi Hawafuatilii Wadaiwa Sugu Kodi ya Pango la Ardhi.
Makazi, Dkt. Angeline Mabula akizungumza na Wakurugenzi pamoja na Wataalam wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri sita za Mkoa wa Simiyu kuhusu ukusanyaji kodi ya Pango la Ardhi pamoja utunzaji wa nyaraka za
sekta ya Ardhi.

Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula, Akikabidhi vitendea kazi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bariadi Mjini, Melikzedek Humbe kwa niaba ya Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuzungumza na Wakurugenzi pamoja na Wataalam wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri hizo kuhusu ukusanyaji kodi ya Pango la Ardhi pamoja utunzaji wa nyaraka za sekta ya Ardhi.

Mkuu wa Kitengo cha Kodi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami, akifafanua hali ya makusanyo ya kodi ya pango la Ardhi kwa nchi nzima, hadi sasa Serikali kupitia Wizara Ardhi inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu ulipaji wa kodi hiyo.
******************************
Mwandishi Wetu- SIMIYU
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula amesema anasikitishwa sana na Wakurugenzi katika Halmashauri za Mkoa wa Simuyu kutojishughulisha hata kidogo na ufuatiliaji wa kodi ya pango la Ardhi.
Naibu Waziri aliyasema hayo katika ziara yake Mkoani Simiyu, alipokutana na wakurugenzi pamoja na maafisa mbalimbali wa Sekta ya Ardhi mkoani humo kwa lengo la kugawa vifaa vya kusaidia ukusanyaji kodi ya pango la Ardhi, pamoja na kukagua utunzaji wa nyaraka katika masjala za Ardhi.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Dkt Mabula alipata nafasi ya kupokea taarifa ya hali ya makusanyo ya kodi ya pango la Ardhi kutoka katika Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu na baadae taarifa ya jumla ya makusanyo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi ndugu Denis Masami kabla hajagawa vifaa vya kusaidia kazi ya ukusanyaji.
Taarifa ya jumla iliyowasilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Kodi, ilionesha Mkoa wa Simiyu kuwa nyuma sana katika makusanyo. Ukilinganisha kiasi kilichokusanywa na Mkoa na lengo lililokusudiwa kukusanywa kwa mwaka,
bado hata nusu ya lengo haijafikiwa na muda uliobaki kumaliza mwaka wa fedha ni miezi miwili tuu.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi kutoka Wizara ya Ardhi alisema, kwa kuliona hilo la kuwa nyuma kimakusanyo kama changamoto, Wizara iliamua kuzipatia Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu vifaa kama vile Karatasi na Wino ili kuongeza kasi katika ufuatiliaji wa kodi ya Pango la
Ardhi.
Aliongeza kwamba, Wizara imesaidia kupatikana hivyo vifaa ikiamini sasa hati za madai zitaandaliwa na wadaiwa watapelekewa ili kodi stahiki ya Serikali ikusanywe.
Nae Naibu Waziri Dkt Mabula wakati anakabidhi vifaa hivyo alisema, hakuna sababu tena ya Wakurugezi kutokukusanya kodi ya pango la Ardhi kwa kuwa vitendea kazi vya msingi wamepewa na Serikali kupitia Wizara.
Aliongeza kwamba, Wakurengi waone kazi ya makusanyo ya kodi ya Pango la Ardhi katika umuhimu wake kwani Sekta ya Ardhi ina mchango mkubwa sana katika uchumi wa nchi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Msanii maarufu wa muziki wa Jazz Wallace Roney amefariki kwa corona
Msanii maarufu wa muziki wa Jazz Wallace Roney amefariki baada ya kuugua Covid-19, Msemaji wa familia amethibitisha hili nakusema,
'Wallace Roney amefariki akiwa ktk matibabu ya CoronaVirus ktk hospitali ya Chuo Kikuu cha St Joseph huko Paterson, New Jersey, Alikuwa na umri wa miaka 59'.
WANAWAKE HANANG' WANUFAIKA NA MRADI WA KILIMO KUTOKA SHIRIKA LA OXFAM & UCRT
Felista Giyam mhasibu wa kikundi cha hamasa ameiomba serikali kuona uwezekano wa kutafuta masoko kwa mazao ya wakulima kwani wamekuwa wakilima kwa muda mrefu lakini wanakosa masoko hivyo kuwakatisha tamaa licha ya kukiri kuwa wamekuwa na faida kwa wastani japo soko linaendelea kuwa kikwazo licha ya kwamba pia wakulima wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika pembejeo za kilimo
Anna Iselu mbaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake na vijana cha Gosanga anasema mradi huo utawafanya kutokuonekana mizigo ndani ya familia na kwa jamii kwa ujumla na kuleta mtazamo mwingine mpya na chanya miongoni mwa jamii
Albert Masuja muwakilishi kutoka shirika la UCRT wamewawezesha jumla ya wanawake 45 katika Kijiji Mureru kata ya Balangdalalu wilayani hanang kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji ili kuondokana na utegemezi wa asilimia 100 kwa wanaume zao.
Baadhi ya wakinanana wanufaika wa mradi huo wakibadilishana mawazo wakiwa sahambani kukagua mazao yanaendeleaje

Donath Fungu Meneja wa miradi ya Oxfam kanda ya kaskazini akitoa ufafafanuzi wa mradi huo unavyoendelea kwa sasa

Charles Kidaguwi mmoja wa wanaume walioshiriki katika mradi huo wa wanawake na vijana kwaajili ya kujikwamua kiuchumi katika kijiji cha Mureru wilayani Hanang' mkoa wa Manyara.
Anna Iselu mbaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake na vijana cha Gosanga akikagua mazao katika shamba la mradi wa wanawake na baadhi ya wanaume waliojiunga katika vikundi hivyo

Charles Kidaguwi ambaye ni mmoja wa wanakikundi na mlizi wa shamba la mradi akifurahia jambo
Baadhi ya wanakikundi wakitoka kukagua shamba la mradi wa mahidi waliowezeshwa na Oxfam pamoja na Acrt amabao wanatarajia kuvuna zaidi ya magunia 100-150 kwa mujibu wa wataalam wa kilimo.
Na Vero Ignatus,Manyara.
Katika kuhakikisha kuwa jamii inajikwamua kiuchumi shirika la Oxfam Tanzania kwa kushirikiana na Ujamaa community resources (UCRT wamewawezesha jumla ya wanawake 45 katika Kijiji
Mureru kata ya Balangdalalu wilayani hanang kuanzisha mradi wa kilimo cha
umwagiliaji ili kuondokana na utegemezi wa asilimia 100 kwa wanaume zao.
Wakieleza manufaa ya mradi huo kwao wanawake hao kwa nyakati tofauti wamesemakuwa mradi huo utawafanya kutokuonekana mizigo ndani ya familia na kwa jamii kwa ujumla na kuleta mtazamo mwingine mpya na chanya miongoni mwa jamii wilayani hapo kufuatia jamii ziishio Hanang kutokumpa nafasi mwanamke hivyo kuendelea kuwa na uchumi tegemezi kwa miongo yote.
“Huu mradi kwakweli kwanza tunawashukuru Oxfam na Ucrt kwa kutuletea mradi huu unajua huu mradi utatukwamua sana kiuchumi na hata kusaidia baadhi ya majukum kwenye Familia”alisema Felista Giyam ambaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake hao.
Ameongeza kuwa pamoja na mradi huu kulenga wanawake ndani yake kuna wanaume ambao tumeamua kushirikiana nao kwani sisi tunaamini “hapa ndani ya mradi kuna wanaume 12 kati yet una hapo tumeamua sana katika umoja.kushirikiana kwa sababu ni mwanzo” Alisema Felista
Mmoja ya wanakikundi mwingine Anna Iselu pia kwa niaba ya wanawake hao na kikundi hicho cha muungano ameiomba serikali kuona uwezekano wa kutafuta masoko kwa mazao ya wakulima kwani wamekuwa wakilima kwa muda mrefu lakini wanakosa masoko hivyo kuwakatisha tamaa licha ya kukiri kuwa wamekuwa na faida kwa wastani japo soko linaendelea kuwa kikwazo licha ya kwamba pia wakulima wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika pembejeo za kilimo.
“Unajua hapa tunatumia gharama kubwa wakati wa kununua pembejeo lakini tunakosa masoko jambo hili linaturudisha nyuma kwakweli serikali iangalie namna ya kuwawezesha wakulima hasa sisi wanawake ambao tumeamua kujiingiza katika kilimo” Alisema Anna Iselu mmoja ya wanakikundi.
Charles Kidaguwi ni kati ya wanaume ambao wameshiriki katika mradi huo amesema kwake una manufaa makubwa kwani utamsaidia kuwajibika vyema katika familia zaidi tofauti na awali kwani kwake ni chanzo kimojawapo cha mapatao ,pia kwa upande wa mwanamke itamsaidia kujikwamua kiuchumi,na kutoa mchango katika familia tofauti na awali walikuwa wanakaa nyumbani pekee.
Kwasababu sikuzote familia inalaliaga upande wangu lakini kama mama amepata mradi huu wa kilimo basi na mimi nitapata msaada mkubwa alisema Chalrles Kidaguwi kutoka Kijiji cha Mureru wilaya ya Hanang’ mkoa wa Manyara
Kwa upande wake Donath Fungu Meneja wa miradi ya Oxfam kanda ya kaskazini amesema mradi huo wanaufanya kwa kuwashirikisha wanawake na vijana lengo likiwa ni kuwajengea wanawake uwezo kiuchumi kipato kiuchumi kwani mwanamke anajishughulisha na mambo mengi ila jamii haimtambui
Ukimuwezesha mwanamke umeiwezesha familia ,jamii na Taifa kwa ujumla hivyo Oxfam Tanzania nzima mdau wetu mkubwa tunaesgughulika nae ni mwananmke,kitendo chake cha kutambulika kinatokana na nguvu yake ya kiuchumi kuwa ndogo tunaamini kwamba atakapopata nafasi ya kuinuka kiuchumi
Fungu amesema mwanamke atakapopata nguvu ya kuinuka
kiuchumi atapata nafasi ya kufanya maamuzi katika ngazi ya kifamilia Kijiji
hadi ngazi ya kitaifa,amesema pamoja na hayo pia wanawapatia mafunzo ya uongozi ,kujiamini ambapo hadi sasa wamefikia hatua kubwa
Amesema hapo awali katika wilaya hiyo mwanamke alikuwa haruhusiwi kusimamam mbele ya jamii na kuzungumza chochote ila baada ya mafunzo waliyowapatia wameweza kujiamini na baadhi yao wameweza kugombea nafasi mbalimbali katika ngazi za vijiji,kuwepokatika na kamati za vijiji na nafasi mbalimbali muhimu.
Naye Mratibu wa Mradi kutoka UCRT Masuja alisema kuwa malengo ni kumpa mwanamke fursa ili aweze kuboresha Maisha yake kiuchumi ambapo wameweza kuwaweka katika vikundi ili waweze kufanya kazi kwa pamoja na kuleta ufanisi Zaidi
Amesema katika kushirikiana na Oxfam wameweza kutoa
nafasi kwa mwanamke kumiliki ardhi wapatao 365 pamoja na kuwapatia hati miliki,pia wameweza kuwapatia wakinamama wa kikundi cha hamasa ng’ombe wapatao 9 na sasa wamepo 18 lengo ni kuwakwamua kiuchumi pamoja na vijana kujitambua na kujiandaa kuja kuwa na familia baadae.
Burundi imetangaza wagonjwa wawili wa kwanza wa corona
“Tuna uchaguzi mkuu May 20,2020, hali ikizidi kuwa tete tunaweza kuusogeza mbele”
May 20 mwaka huu, Burundi itaingia kwenye uchaguzi mkuu wa Urais ambapo Rais Nkurunziza ambaye ameitawala Nchi hiyo kwa miaka 15 sasa tangu mwaka 2005, ameahidi kutogombea tena.
Meneja wa Diamond apona Corona
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Sallam SK ameweka wazi kuwa sasa ni mzima baada ya siku 14 alizokuwa ametengwa kwa ajili ya matibabu kumalizika.
Sallam ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz amesema amefanyiwa vipimo mara kadhaa ya vyote vimeonesha kuwa hana tena maambukizi ya virusi vya corona.
Kupitia instagram ameandika hivi;
Nimshukuru Allah 🙏🏽 na pia niwashukuru wote mlionitumia msg, comments, DM na dua zenu. Bila kuwasahau Temeke Isolation Centre kwa kuwa bega na bega pamoja na mie bila kunichoka pale nilipokuwa nimezidiwa, na shukurani zangu zingine ziende kwa Madaktari bingwa kujua maendeleo yangu mara kwa mara na pia Serikali yangu na viongozi wake husika Wizara na Mkoa walikuwa hawana ubaguzi kutujulia hali na kutupa moyo na kutupa mahitaji tutakayo. Naomba niwape taarifa ndugu yenu, kijana wenu nimechukuliwa vipimo mara mbili na nimekutwa NEGATIVE na kwa sasa nipo huru. Ila naomba tuendelee kujikinga na kufata ushauri wa viongozi wetu na kuacha maelekezo ya utashi yasiyokuwa na uhakika. ALLAH IS GREAT 🙏🏽🙏🏽🙏🏽
Machi 19 mwaka huu alibainika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo vinavyosababisha homa ya mapafu, baada ya kutembelea nchi ambazo tayari zilikuwa na maambukizi.
Watoto 11 wa kwaya maarufu nchini Uganda wathibitishwa kuwa na corona
Kupitia matangazo ya televisheni, alisema kuwa wagonjwa wote wapya walikuwa karantini baada ya kurejea kutoa ughaibuni , ingawa hakueleza afya zao zikoje kwa sasa na walikuwa wametoka taifa gani.
Mara nyingi kwaya hiyo huwa inatumbuiza katika nchi za ughaibuni kama Marekani, Canada na Uingereza.
Mpaka sasa Uganda imethibitisha kuwa na wagonjwa wa Corona 44.
Katika hatua za kukabiliana na maambukizi ya corona, tayari rais wa Uganda Yoweri Museveni ametagaza masharti zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada ya kupiga marufuku usafiri wa Umma.
Katika hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni usiku wa Jumatatu Bw. Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku.
Mtu yeyote anayehitaji huduma za dharura za kiafya kama vile kujifungua au kufanyiwa upasuaji anatakiwa kupata idhini kutoka kwa maafisa wa serikali katika ngazi ya Wilaya kabla ya kutoka nyumbani
Wauzaji bidhaa za chakula sokoni watahitajika kuondoka maeneo yao ya biashara hadi pale serikali itakapokamilisha kushughulikia maeneo mapya ya wao kuuzia bidhaa zao .
Rais Museveni pia ameahidi msaada wa chakula kwa watu ambao hawafanyi kazi kutokana na vikwazo vya kukabiliana na covid-19 na hawana uwezo wa kujipatia bidhaa hiyo muhimu.
Bw. Museveni pia ametoa agizo kwa polisi kuwakamata wanasiasa watakaotoa misaada ya chakula kwa jamii na kushtakiwa kwa ''jaribio la mauaji ''
Uganda kufikia sasa imethibitisha kuwa na wagonjwa 33 wa corona na maafisa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.
Magari binafsi yatazuiwa kuingia barabarani baada ya maelekezo ya awali kutaka magari kubeba abiria watatu pekee kukiukwa, na baadhi ya watu kutumia magari binafsi kuwasafirisha wengine na kuongeza hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo. Limeandika gazeti la New vision la Uganda.
''Isipokuwa kwa ndege za mizigo, malori, magari aina ya pickups na treni, kuanzia siku ya Jumanne tarehe 31 mwezi Machi saa moja, amri ya kutotoka nje itatekelezwa katika nchi yote ya Uganda'' Meseveni aliesema.
Alisema kuwa siku 14 zitatumika kubaini na kuwafuatilia na kuwatenga wale wote waliokaribiana na watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Uganda kwa sasa imethibitisha kuwa na watu 13 walioambukizwa virusi vya corona, hakuna vifo na hakuna aliyepona mpaka sasa.
Kati ya nchi 54 barani Afrika, nchini ya nchi 10 hazijathibitisha kuwa na maambukizi.
Kikosi kazi cha taifa kinachoshughulikia janga la corona kitatoa taratibu siku ya Jumanne baada ya maelekezo ya rais, alieleza mmoja wa wanakikosi hao.
Museveni ameamuru pia kufungwa kwa maduka makubwa, njia tao, maduka ya vifaa, biashara zisizo za chakula, saluni, nyumba za kulala wageni na karakana za magari kwa siku 14, maeneo amayo amesema hukusanya watu wengi, limeeleza gazeti la Daily Monitor la Uganda.
Amri hiyo haihusu hospitali, maeneo yanayotoa huduma za kitabibu na mashirika yanayojihusisha na masuala ya afya.
Ulaya yaanza biashara ya mabadilishano na Iran
Iran na Umoja wa Ulaya zimekamilisha mauziano ya kwanza chini ya mfumo wa ubadilishanaji bidhaa na huduma uliowekwa ili kukikiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri hiyoya Kiislamu.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani ilisema hapo jana kwamba uundwaji wa kile kinachoitwa INSTEX umefanikisha usafirishwaji wa vifaa vya matibabu kutoka Ulaya.
Ikizungumza kwa niaba ya Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, wizara hiyo imesema kwamba mfumo huo utaruhusu manunuzi mengine kuendelea.
Mfumo huo ulibuniwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita baada ya Marekani kurejesha upya vikwazo vikali dhidi ya sekta ya mafuta ya Iran kufuatia hatua ya Rais Trump kujiondowa kwenye makubaliano ya kimataifa kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani juu ya mpango wake nyuklia.
Chini ya mfumo INSTEX, bidhaa na huduma zinabadilishwa badala ya kuuzwa kwa fedha, jambo linalokwepa matumizi ya moja kwa moja ya fedha na vikwazo vya Marekani.
Awali, kampuni za Ulaya hazikuwa na la kufanya zaidi ya kusitisha biashara na Iran na kufuta miradi ya pamoja kwa hofu ya kuadhibiwa na Marekani.
Kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia na Marekani, China, Urusi, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, mwaka 2015 Iran iliamuwa kuiunda upya programu yake ya nyuklia ili isiweze kutengeneza bomu la atomiki.
Matokeo yake vikwazo vingi vikaondolewa na biashara na Tehran ikarejea. Lakini mwezi Mei 2018, Trump aliiondoa kwenye makubaliano hayo, na mwaka mmoja baadaye, Iran ikaanza kujivua taratibu majukumu yake kwenye mkataba huo.
Mwanaume ajiandalia jeneza kisa mateso ya familia
Na Paschal Malulu, Kahama
Mkazi wa Ushirombo kitongoji cha Butambala Kata ya Igulwa wilayani Bukombe mkoa wa Geita Sylvester Mihayo (45) anaishi na jeneza ndani ya nyumba ambalo ameliandaa kwaajili ya mazishi yake pale atakapofariki kutokana na kile alichoeleza kuwa ni kuchoshwa na kunyanyaswa na familia yake.
Aidha mwanaume huyo akizungumza na waandishi wa habari alieleza kuwa kwa takribani miaka 3 sasa, anaishi bila furaha kutokana na unyanyasaji huo ikiwa ni pamoja na kipigo kutoka kwa mke na watoto wa kuwazaa mwenyewe hali iliyompelekea kuitelekeza nyumba na kuishi kwenye karakana ya ufundi anakochomelea kwa kutumia mitungi ya gesi.
Alisema kuwa chanzo cha mateso yake ni baada ya kuugua kwa muda mrefu tangu mwaka 2018 ambapo familia ilimtenga na kumzuia kuingia kwenye nyumba yake kwa madai kuwa siyo yak wake badala yake ni nyumba ya urithi kwa watoto wake.
“Ndugu zangu waandishi wa Habari mimi kujichongea jeneza siyo kwamba nitajidhuru, bali nimejitabilia kufa kutokana na manyanyaso na ukatili naofanyiwa na familia yangu na litatumika kama mauti yatanikuta, ninamiaka mitatu nateseka na ugonjwa na sina msaada wa familia katika matibabu walichokifanya wamenikimbia name nikarudi kuishi kwenye ofisi yangu ya karakana ya ufundi huu ugonjwa haueleweki,” alisema Mihayo kwa huzuni na kuongeza.
“Kwa sasa familia yangu, wamejenga nyumba nyingine eneo la Maghorofani Ushirombo ili waendeshe uganga wao kwa uhuru kwa kipindi chote hicho wakati huo nikiwa nasaka matibabu katika hospitali zote ambazo nazo zimekosa ugonjwa wakiwamo waganga wa jadi ndipo kipindi cha 2018 nikachongesha jeneza kwa maandalizi ikitokea nimefariki litatumika hilo,” alisema Mihayo huku akibubujikwa na machozi.
Hata hivyo, mke wake Vumilia John hakupatikana kuzungumzia hali hiyo baada ya kuondoka nyumbani kwake, na hata alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya kiganjani alikataa kwa madai ya kumuuguza mgonjwa mwingine wilayani Kahama.
Mama mzazi wa mwanaume huyo Veronika Kasase (86)mkazi wa kijiji cha Mwalo Kata ya Businda Halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani hapa akizungumza na waandishi wa Habari nyumbani kwake huku akimwaga machozi wakati akisimulia mkasa wa mwanaye alisema mwanaye amegeuzwa msukule kwa imani za ushirikina.
Alisimulia kuwa mwanaye anamiaka mitatu nateseka na ugonjwa usiofahamika na kwamba ametumia fedha nyingi na hospitali nyingi hapa nchini hadi kwa waganga wa jadi lakini hakuna nafuu badala yake aliambulia kutolewa maji mengi tumboni yenye ujazo wa lita nane pamoja na kunyofolewa nyama ubavuni ambayo ilipimwa na kukosekana kansa.
Hata hivyo mama alieleza kuwa alishitushwa na kitendo cha mwanaye kumweleza kuwa amechonga jeneza kwaajili ya kuhifadhi mwili wake pindi mauti yatakapomkuta kutokana na kushindikana matibabu kwa kipindi chote hali ambayo alimtaka alilete nyumbani kuliko kukaa nalo huko.
“Mimi nilijaribu kuwaita ili nijue chanzo cha wanangu kusambaratika kiaina ukilinganisha ni watu wazima sasa na wanafamilia kubwa ya watoto wanane kisha nipate nafasi ya kuwashauri wake pamoja na kuuguzana lakini mkamwana wangu alikataa kabisa jambo ambalo tumemwachia mungu,” alisema.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Said Nkumba akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alisema hajapata taarifa za Mihayo na kuahidi kumtafuta ili kupata maelezo ya kina kwaajili ya ufumbuzi wa suala hilo.
“Suala la kujiandalia jeneza siyo jambo la kushangaza sana ama kuleta taharuki kwa jamii lakini niwapongeze sana kwa kusaidia wananchi kama mkuu wa wilaya hii nimeletwa na rais kushughulikia na kutatua kero za wananchi na kama mwakilishi wake hili suala nitalishughulikia kwa kiwango kikubwa na nitawaita wote mke na mume tukae na wasaidizi wangu kwa maana ya ustawi wa jamii na ngazi zingine tulipatie ufumbuzi,” alisema Said Nkumba mkuu wa wilaya ya Geita.
Simbachawene: Kifungo cha nje suluhisho msongamano magerezani nchini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii kabla ya kuzindua Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo, ambayo itasimamia Utekelezaji wa Sheria ya Huduma kwa Jamii inayotoa fursa kwa wafungwa wa vifungo vidogo kutumikia adhabu hizo kwenye jamii. Pia Waziri huyo ameitaka Kamati hiyo, iweke mikakati zaidi ya kusimamia adhabu mbadala ya kifungo cha nje ili kuondoa msongamano magerezani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati meza kuu), akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii kabla uzinduzi wa Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Katibu wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Uangalizi, Aloyce Musika, alipokuwa anazungumza kabla ya kabla uzinduzi wa Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo. Waziri Simbachawene amezindua Kamati hiyo, ambayo itasimamia Utekelezaji wa Sheria ya Huduma kwa Jamii na kutoa fursa kwa wafungwa wa vifungo vidogo kutumikia adhabu hizo kwenye jamii. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji Zephrine Galeba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati meza kuu), akimsikiliza Mjumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, Isaac Nantanga (kushoto), wakati alipokuwa anajitambulisha kabla ya uzinduzi wa Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo. Watatu kulia ni Katibu Mkuu, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (wanne kushoto), Katibu Mkuu, Christopher Kadio (wanne kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, Jaji Zephrine Galeba (watatu kushoto), Katibu wa Kamati, Aloyce Musika (watatu kulia), Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (wapili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Minziro ndio basi tena Alliance FC

UONGOZI wa Alliance FC umefanya mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kumrejesha Kessy Mzirai kuwa kocha mkuu huku Fred Felix Minziro akipangiwa majukumu mengine.
Mapema msimu huu, timu hiyo ilianza kazi na Athuman Bilali ‘Billo’ ambaye hakudumu kufuatia matokeo ya mchezo mmoja dhidi ya Mbao FC uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Baada ya kuondoka Billo, majukumu yalibaki kwa Mzirai akisaidiana na Habibu Kondo ambaye kwasasa ni kocha msaidizi KMC na baadaye Minziro pamoja na Mathias Wandiba wakachukuwa nafasi huku Mzirai akijiengua.
Minziro akiwa Kocha Mkuu, amesimamia michezo 15 ikiwamo miwili ya Kombe la Shirikisho na ameshinda minne, sare nne na kupoteza saba na kuiweka timu nafasi ya 18 kwa pointi 29 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Jackson Mwafulango alisema Minziro hajafukuzwa isipokuwa kilichofanyika ni mabadiliko kwenye benchi la ufundi kwa lengo la kuboresha timu hasa kipindi hiki ligi imesimama.
Alisema Minziro atapangiwa majukumu mengine kutokana na klabu hiyo kuwa na timu nyingi, huku aliyekuwa Msaidizi wake, Wandiba akipewa kikosi cha Vijana (U-20).
“Mzirai tumemrudisha kuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Gilbert Dady na Minziro atapangiwa majukumu mengine na Wandiba amepewa timu ya vijana, lengo ni kuboresha” alisema Mwafulango.
Kwa upande wa Minziro alisema hajapata taarifa zozote za aidha kusimamishwa au kupangiwa majukumu mengine, hivyo atakapopata rasmi ndio ataweza kuzungumza.
Hata hivyo, licha ya uongozi kutoweka wazi kuachana na Minziro, habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa Minziro hana tena nafasi ya kuifundisha Alliance kwa maana ya kwamba ametupiwa virago.

Mfahamu Mrembo Kim Kardashian Kiundani zaidi na Jinsi Alivyoangukia Kweye Penzi la Kanye West

Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...