
ALIYEKUWA Nahodha na beki wa kati wa Kagera Sugar, George Kavila amesema akirudi uwanjani basi anajipa mwaka mmoja tu ndipo atundike daruga rasmi.
Mkongwe huyo ambaye aliitumikia Kagera Sugar kwa zaidi ya miaka 15, msimu huu hajaonekana uwanjani baada ya kuachwa kikosi hicho chini ya Kocha Mecky Maxime huku na yeye akisema alihitaji kupumzika.
Kavila alisema kwa sasa anaendelea kujifua mdogo mdogo na msimu ujao anahitaji kuja kivingine na kubainisha kuwa bado hajafikia muda wa kustaafu soka.
“Msimu huu nimeamua kutocheza kutokana na changamoto za hapa na pale, lakini kwa sasa naendelea kujifua ili msimu ujao nirudi kivingine nikiwa na timu mpya ya Ligi Kuu,” alisema Kavila.
Beki huyo wa kati aliongeza kuwa anachojivunia hadi sasa ni historia na heshima aliyojiwekea kwa kipindi chote alipokuwa akikichafua hivyo hata msimu ujao anaamini ataendeleza moto wake.
Alisema kikubwa ni wadau na mashabiki wake kuendelea kumpa sapoti na kwamba anahitaji kucheza msimu mmoja tu ili aweze kutangaza rasmi kutundika daluga.
No comments:
Post a Comment