Search This Blog

Tuesday, August 31, 2021

MAGAZETI YA LEO 1.9.2021
















 

Ukitaka kuwa mwanaume wa shoka, epuka kula vyakula hivi

 

Katika makala hii hii utajifunza vyakula mbalimbali ambavyo wanaume hawatakiwi kula ili kubaki na afya bora wakati wote. Kuna vingine unaweza kuwa unavitumia kila siku bila mwenyewe kujuwa.

Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele
Moja ya matatizo makubwa upande wa urembo kwa wanaume ni kupoteza nywele (upala). Lakini kama unatafuta kitu cha kukilaumu dhidi ya tatizo lako la kunyonyoka nywele basi ni hiyo sahani yako ya chipsi unayokula kila siku.  Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana kwenye fast foods na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile vyote vya kwenye maboksi.

Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno cha lehemu (cholesterol) na lehemu hii hupelekea kile huitwa kwa kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na kupelekea kiasi kikubwa cha ‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye kupotea kwa nywele kichwani a.k.a upara.
Kunyonyoka kwa nywele kunaweza kuwa ni jambo la kurithi (genetics) lakini vile vile aina ya chakula unachokula kinaweza kuwa kinahusika moja kwa moja.

Punguza kunywa pombe 
Wanaume wengi wanaokunywa bia kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na tatizo la kuota matiti kama wamama tatizo lijulikanalo kwa kitaalamu kama ‘gynecomastia’.

Kwenye bia au pombe mara nyingi hakuna lishe ya moja kwa moja na hivyo hukufanya ujisikie njaa au hata kuongzeka kwa njaa zaidi na ndiyo sababu unaambiwa kama huna uhakika utakula wapi ni bora usinywe pombe ili kulinda afya yako.

Kwenye bia kuna kitu kama homoni ya oestrogen ya kupandikizwa na hivyo unywaji pombe kupita kiasi kuna uhusiano wa moja kwa moja na matokeo ya wanaume kuwa na matiti kama wanawake.

Acha kutumia mafuta ya mboga mboga kuepuka saratani ya tezi dume
Mafuta yatokanayo na mboga mboga au mimea yamekuwa yakipigiwa debe kwa miaka mingi na watu wanaojihusisha na lishe na wale wenye hasira sana na mafuta yatokanayo na wanyama. Hata hivyo leo nakujulisha mafuta hayo si salama sana kutumika na mwanaume kila siku. Hili limekuja hasa kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ya moyo na lehemu na watu walazishwawa kutumia mafuta ya namna hiyo.

Lakini mafuta haya ya mboga mboga ndiyo kitu kibovu kabisa unatakiwa kukiepuka ili usipatwe na saratani ya tezi dume.  Linapokuja suala la kujilinda saratani ya tezi dume basi mafuta yenye omega 3 ndiyo suluhisho la kudumu na siyo omega 6 kama ilivyo kwenye vyakula vingi vya kwenye makopo, mafuta ya alizeti, maharage ya soya, mafuta ya  canola na mafuta ya corn na mengine yote yenye omega 6.

Popcorn
Popcorn au bisi ni chakula kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa kutumia mafuta yasiyo na afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya kansa. Kuna kitu kinaitwa ‘Diacetyl’ kinachopatikana kwenye popcorn ambacho kinahusika na kusababisha kansa na kuna kingine kiitwacho ‘Perfluorochemicals’ ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati huo huo husababisha ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa kiingereza kama ‘Attention-deficit/hyperactivity disorder (ADHD)‘.Ni vizuri kuacha kula popcorn.

Mkate mweupe
Mkate mweupe una wanga mwingi zaidi usio na faida. Kwenye hatua za kutengeneza mkate mweupe vitamini zote za kundi B hupotea, hupotea pia nyuzinyuzi (fiber). Siyo hivyo tu mkate mweupe umesemekana kuwa ni sababu ya ugonjwa wa kisukari na kuongeza uzito zaidi mwilini wakati huo huo ukisababisha tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

Vingine vinavyofanana na na hilo ni ugali wa sembe, tambi nyeupe, chai ya rangi na kahawa. Kula mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa dona na chai unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya chai.

Chumvi ya mezani
Chumvi ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume. Kila mmoja amesikia chumvi hii husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na hayo bado sehemu kubwa ya watu wanatumia chumvi hii.

Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini, madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile ‘aluminium silicate’ huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi kwa afya ya mwanaume.



Rais wa Iraq Barham Salih ahimiza uchaguzi wa mapema na marekebisho ya katiba nchini


Akielezea kuwa nchi haiwezi kutawaliwa na mfumo wa sasa, Rais wa Iraq Barham Salih alisema kuwa uchaguzi wa mapema utakuwa tarehe 10 Oktoba na marekebisho ya katiba yatafanyiwa mabadiliko.

Berhem Salih alitaja uchaguzi wa mapema utakaofanyika Oktoba 10 katika hotuba ya ufunguzi wa Fomu ya Rafideyn inayoitwa "Suluhisho" huko Baghdad.

Kuelezea kwamba anataka katiba ibadilishwe licha ya mambo mazuri ya nguvu za kisiasa na sehemu muhimu ya jamii, Salih alisema,

"Haiwezekani tena kutawala Iraq na katiba hii na mfumo wa sasa. Uchaguzi wa mapema na marekebisho ya katiba yanapaswa kuwa hatua ya kugeuza kuongeza ubora wa huduma nchini na kuboresha hali. Uchaguzi pia ni tukio la kutatua migogoro iliyokusanywa."

Akisisitiza kuwa katika miaka 100 iliyopita, mauaji na ukatili wa misingi ya madhehebu na makabila yametokea nchini Iraq, Salih alibainisha kuwa baada ya 2003, walikabiliwa na shida za ugaidi na uingiliaji wa kigeni nchini.

 



Kamati ya Maadili: Askofu Gwajima kukataa vitu vilivyoandaliwa ni ujeuri


Kamati ya Maadili imetafsiri kitendo cha Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima kukataa vitu alivyoandaliwa kama ujeuri

 
Gwajima alikataa kutumia kiti na kipaza sauti siku ya kwanza na siku ya nyingine alikataa kukaa chini kama alivyoelekezwa


Aidha alikataa kujibu maswali kadiri yalivyoulizwa bali aling'ang'ania kuwa alizungumza kama kiongozi wa dini



Rais Hichilema awaapisha Wakuu wapya wa Jeshi na Polisi, IGP atetemeka ashindwa kuapa


Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amewaapisha Wakuu wapya wa Jeshi na Polisi aliowateua Agosti 29, 2021 baada ya kuahidi kukomesha ukatili wa Polisi uliokuwa ukifanywa wakati wa utawala wa Rais aliyepita.

Miongoni mwa walioapishwa ni Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi Zambia (IGP) Remmy Kajoba ambaye hata hivyo alishindwa kusoma kiapo hadi mwisho baada ya kuanza kutetemeka mikononi ambapo Rais alimuomba Mtu mwingine amsomee kwa niaba yake na kukamilisha kiapo.

 



Dirisha la usajili kufungwa leo


NI masaa tu kwa sasa yamebaki kabla ya dirisha la usajili kwa msimu wa 2021/22 kufungwa. Leo Agosti 31 milango iliyokuwa wazi inafungwa.


Sarakasi zimekuwa zikionekana kwenye timu zote kuhusu usajili hilo ni sawa. Ipo hivyo duniani kote hasa pale ambapo usajili unapofunguliwa ni asili ya mpira na mara nyingine bila hayo ule umakini unapungua kidogo.


Haina maana kwamba haya makosa yanapaswa kuwepo hapana ni mbaya kujirudia mara kwa mara kwa kuwa itafika wakati kunakuwa na muda mwingi wa kusikiliza kesi kuliko kufanya maendeleo kwa ajili ya timu zetu kusaka mafanikio.


Kwa namna soka letu la Bongo lilivyo nina amini kwamba zipo timu ambazo mpaka sasa hazijakamilisha usajili. Unaweza ukashangaa lakini huu ni ukweli na ipo wazi kabisa zipo timu wakati huu zinaanza kuingia sokoni kusaka wachezaji.


Viongozi wengine kwa sasa wanaanza kuwavutia waya wachezaji wao ili kujua kuhusu hatma yao kwa kuboresha mikataba yao. Kawaida na watakaoanza kumalizia leo nadhani watajipongeza kwamba wakikamilisha mpango kazi wao.


Kawaida kabisa pale usajili unapokaribia kufungwa wanaanza kuhangaika na wachezaji wapya na mtandao ukisumbua kidogo basi watasubiri huruma kutoka Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuwaongezea muda.


Ukizunguka kote duniani ni soka la Bongo tupo kivyetuvyetu kuanzia staili ya uendeshaji na namna ya kumaliza mambo ambayo tunayafanya.


Wakati wenzetu wa Ulaya wakiwa wanaratiba yao kamili ya msimu mzima na kuanza mechi za ushindani hapa kwetu bado mambo hayajawa sawa kwa upande wa ratiba.


Pongezi kwa TFF kwa kuja na ile kalenda ya matukio tunaona kwamba wamekuwa tofauti kidogo kwa msimu huu basi inapaswa wawe tofauti katika kila jambo kwa msimu ujao kuanzia usimamizi mpaka umaliziaji wa yale ambayo wanayafanya.


Kwa wachezaji ambao wanaanza maisha mapya hao nina amini wanajua kile ambacho wanatakiwa kukifanya. Kuanza kwa ligi msimu wa 2021/22 kupo karibu na ni wakati mzuri kwa waliojiandaa na wakati mbaya kwa wale ambao bado hawajajiandaa.


Kazi ile ya kujua nani alisajiliwa kwa pendekezo la benchi la ufundi ama ilikuwa ni kwa pendekezo la kiongozi fulani inakuja pale ligi itakapoanza muhimu kujipanga kisaikolojia na kukubali matokeo yatakayotokea.


Pale watakapoanza kazi wanapaswa kufanya kazi kwa juhudi ili kuona kile wanachokihitaji kinatokea.


Juhudi isiyo kuwa ya kawaida katika kusaka matokeo pamoja na nidhamu ndani ya uwanja ni mambo ya kuzingatia. Muhimu ni kwamba hakuna ambaye anaweza kufikia malengo ikiwa hatakuwa na nidhamu.


Pia kwa TFF mbali na kuwekeza nguvu kubwa kwenye Ligi Kuu Bara basi kwa msimu ujao ni muhimu pia kuwekeza nguvu kubwa kwenye Ligi Daraja la Kwanza ambayo kwa sasa inaitwa Championship.


Endapo jicho kubwa litakuwa ndani ya ligi pekee na kuacha huku kwenye kiwanda cha kutengeneza timu shiriki bila kujali maisha yao itakuwa ni hatari kwa afya ya soka letu.


Ili soka liendelee ni lazima kuwe na misingi makini ambayo inaanzia huku chini na haijengwi kwa kubahatisha bali mipango makini na hesabu zenye uhakika.


Timu shiriki ndani ya Championship ni lazima zitambue namna gani zinaweza kufikia malengo yao hasa ukizingatia kwamba siku zinakwenda kasi na hazisubiri kwa yale makosa ambayo yalionekana msimu uliopita.


Njia ya kupata ushindi kwao ni moja tu kupambana na kufanyia kazi makosa yao ambayo waliyafanya kwenye mechi zao za mwanzo ikiwa walipata matokeo wana kazi ya kuendeleza rekodi ya kucheza bila kupoteza.



 



Kamati ya maadili ya Bunge yamtia hatiani Gwajima, apewa adhabu


Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima kwa makosa ya kudhalilisha na kushushsa nafasi ya Bunge, wabunge na viongozi, kuchonganisha mhimili wa bunge dhidi ya mhimili wa serikali na wananchi na kuonesha dharau na kushusha heshima ya bunge, shughuli za bunge na uongozi wa bunge.

Baada ya kumtia hatiani, kamati hiyo imeazimia Askofu Gwajima apewe adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge.


Maafisa wa Nigeria wanaomba msaada, wapiganaji wa Boko Haram wakijisalimisha


Maafisa wa Kaskazini mwa Nigeria wameiomba msaada serikali kuu baada ya miezi ya hivi karibuni watu wapatao 3,000 kujisalimisha wakiwemo wanamgambo wa Boko Haram. Jeshi la Nigeria limesema hiyo ni ishara kwamba limefanikiwa kuwazidi nguvu wanamgambo wa kundi hilo la kijihadi katika mgogoro unaoendelea kwa miaka 12. 
 
Wanamgambo hao pamoja na familia zao walianza kujisalimisha kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau mnamo mwezi Mei wakati wa mapigano na wapiganaji wa Tawi la Magharibi mwa Afrika la Dola la Kiislam (ISWAP). 
 
Gavana wa Jimbo la Borno Babagana Zulum amesema wengi waliojisalimisha ni wanawake, watoto na wakulima ambao walilazimishwa kufanya kazi katika eneo ambalo lilikuwa likidhibitiwa na Boko Haram.

 



Bunge lapunguza muda wa vikao kujinga na Uviko-19


Bunge limepunguza muda wa kuanza kwa vikao vyake ambapo sasa litaanza vikao vyake kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 1:00 usiku huku kukiwa hakuna kipindi cha maswali na majibu asubuhi ikiwa ni jitihada za kujikinga na ugonjwa wa Uviko-19.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Agosti 31, 2021 na Spika wa Bunge, Job Ndugai mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika bungeni.

“Lengo ni kupunguza muda wa kukaa pamoja. Kuanzia kesho kikao kitaanza saa 8:00 mchana na kumalizika saa 1:00 jioni, hii itatufanya tutumie saa tano badala ya saba na nusu ambao ni utaratibu wa kawaida,”amesema.

Amesema pia kipindi cha maswali na majibu kitakuwa cha dakika 60 badala ya dakika 90 unaotumika kwa kawaida bungeni.

Wabunge wakiwasili katika viwanja vya Bunge Dodoma kwa ajili ya kuanza kwa kikao cha Bunge.Picha na Said Khamis

Ndugai amesema kwa lengo la kupunguza msongamano bungeni watatumia kumbi mbili wakati wa vikao bungeni ikiwa ni ukumbi wa Bunge na ule wa Pius Msekwa.

“Ukumbi wa Msekwa utawawezesha kuwafanya wabunge watakaoshiriki katika kikao cha Bunge kushiriki sawa na wale waliopo katika ukumbi wa Bunge,”amesema Ndugai.

Amesisitiza wabunge kuvaa barakoa katika kipindi chote wanachokuwa katika viwanja vya Bunge hususan katika kumbi za Bunge.

Hata hivyo, amesema wale wenye tatizo la kiafya linalowafanya wasivae barakoa wataruhusiwa baada ya kupata idhini yake.

Kuhusu wageni, Ndugai amesema hawataruhusu wageni wanaofika kutembelea Bunge wala mafunzo na kwamba watakaoruhusiwa ni wale wenye shida za kiofisi, maofisa wa Serikali wanaofuatilia shughuli za Bunge na waandishi wa habari.



TAMBUA DALILI ZA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME NA TIBA YAKE, PIA TAMBUA DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE

                                          


TAMBUA DALILI ZA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME NA TIBA YAKE, PIA TAMBUA DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE

Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo kikamilifu shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili,homon,Neva,misuli,hisia na miriji ya damu


CHAZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


-kuwa na halemu (cholesterol) na shinikizo la damu( B,P,)au ugonjwa wa motorcycle

-ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi

-kisukari,

-umri hasa wazee

-utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili

-tabia za kujichua kwa mda mrefu ,kutopata usingizi

-ngiri,vidonda vya tumbo,

-tumbo kuunguruma na kukosa choo

-matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibu magonjwa Kama vile,kansa,vidonda vya tumbo,moyo,kisukari


DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


1kuwahi kufika kileleni,2kukosa hamu ya tendo 3kushindwa kurudia tendo la ndoa 4uume kusimama kwa uregevu au kushindwa kusimama 5 kuchoka Sana baada ya tendo la ndoa


TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME


Dawa ya MJN ni dawa ya asili isiyokuwa na mkemikali yoyote dawa hii ipo kwenye mfumo wa kunywa na kuchua pia dawa hii ni tamu Sana kwani imechanganywa na asari ni tofauti na  ulizowahi kutumia usaidia ata wazee wenye miaka 80 pi uboresha uume wa mwanaume ulioingia ndani na kuwa mfupi


DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE


1. kunywa maji mengi Sana Kila wakati

2. kwenda  haja ndogo Mara kwa Mara

3. kuwa dhaifu ,kukosa nguvu na kijisikia mchovu kila wakati

4. kupunguza uzito au kukonda ata Kama unakula

5. kutoona vizuri

6. mwili kufa gazi hasa miguni 

7. vidonda au majeraha sehemu ya mwili kutopona 

8 kupungukiwa nguvu za kiume nk


MTN ndio dawa ya kisukari dawa hii inatibu tatizo mojakwamoja endipo ukidhingatia matumizi yake ni dawa isiyokuwa na masharti magumu kwa mtumiaji,pia zipo dawa za vidonda vya tumbo,presha,ngiri,chango la uzazi, miguu kuuma na mgongo


Ndugu mteja epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahii kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO 


WASILIANA NAMI TABIBU DITTU KWA SIMU 0755028097  AU Whatsapp +255714448999 ofisi ipo mbagara sabasaba walio nje ya mkoa utatumiwa sehemu yoyote ulipo



ST.DAVID TRAINING COLLEGE AND OPEN SCHOOL


TUPO DAR ES SALAAM: MBEZI (KWA MSUGURI) NA PIA TUPO KIBAHA-KONGOWE


USAJILI: IAE/OS/0742(Full registration)


TUNATOA ELIMU YA SEKONDARI  NA  UJUZI KATIKA KOZI MBALIMBALI KAMA IFUATAVYO:-


1. Ualimu NA MALEZI WATOTO WADOGO (EARLY CHILDHOOD DEVELOPMENT AND EDUCATION)-Mwaka 1


2. ICT (Computer maintance, Networking, Website Design, Software engeenearing na Graphic Design)


3. BOA- BUSINESS OPERATING ASSISTANT(MAFUNZO YA UENDESHAJI WA BIASHARA)


4. UUGUZI-Kwa wale wanaotaka kusoma kozi za afya wakati wanasafisha vyeti vyao wataanza na kozi ya FOUNDATION ili kupata ujuzi na uelewa na baadae kuunganishwa katika vyuo vya afya hapa nchini ili kujiendeleza hadi ngazi ya Diploma!


SIFA: Muombajia awe amemaliza amemaliza kidato Cha nne na ufaulu wa angalau D moja tu na kuendelea. 


Kwa uuguzi awe amefaulu somo la Biologia kwa agalau D moja tu na kuendelea!


KOZI FUPI( Miezi 3 tu )


1. COMPUTER COURSE

2. ENGLISH COURSE

3. USHONAJI

2. UDEREVA   WS MAGARI


SIFA: Muombaji awe amemaliza angalau Darasa la saba na kuendelea..


ELIMU YA SEKONDARI

1. Qualifying Test (Seco dary miaka 2 )

2. Ressitters- Wanaorudia mtihani/NECTA ya Form FOUR/SIX


Aply now:-

PROGRAM MAALUM

1. Tunapokea WANAFUNZI wa KIDATO CHA KWANZA ambao hawakuchaguliwa kwenda sekondari ili kujiunga na FORM ONE Hadi fomu FOUR chini ya Taasisi ya elimu ya Tanzania!


2. Wanaotaka kujiunga kidato Cha TANO NA SITA kwa mwaka mmoja tu.


_Ada zetu Ni nafuu sana na unalipa kidogokidogi..._🙏


TUPIGIE: 0718 455002/0767 521231















Ditopile aiomba Serikali kuwezesha upatikanaji wa Mbegu Bora za Alizeti

MBUNGE wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha bei ya zao la Alizeti kupanda hadi Sh 1600 kwa Kilo Moja lakini akaihoji Serikali imejipangaje kuwawezesha wakulima wa zao hilo kupata mbegu bora na za kisasa.

Ditopile ameuliza swali hilo leo Bungeni wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu ambapo Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema tayari Serikali ishaingia mkataba na wasambazaji wa mbegu kwa ajili ya kusambaza mbegu bora za zao hilo.

" Niipongeze sana Serikali yetu kwa muda mfupi tu imeweza kupandisha thamani ya Zao la Alizeti ambapo bei imepanda hadi Sh 1600 kwa Kilo Moja, hii haijawahi kutokea kwenye Nchi yetu, kupanda huku kwa bei kumesababisha muamko uwe mkubwa kwa watu kwenda kulima Alizeti, Je Serikali imejipangaje kuhakikisha inawezesha upatikanaji wa mbegu bora kwa ajili ya msimu mpya wa Kilimo hasa kwa wakulima wetu wa Dodoma,"?

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kwa sasa Serikali imeanza kuchukua mahitaji ya Mikoa wanayoleta wenyewe kutokana na uwezo wa Mkoa husika katika suala la uzalishaji ambapo katika Mkoa wa Dodoma wanashirikiana kwa karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupitia Katibu Tawala wa Mkoa.

" Kwa sasa tunashirikiana na Ofisi ya RAS kutuletea mahitaji ya Wilaya zote ili sisi kama Wizara tuweze kuwapatia mbegu, nataka niwahakikishie wakulima tutahakikisha wakulima wa Alizeti wanapata mbegu bora ambazo zitaweza kuwasaidia mwaka huu wakati ambao sisi Serikali tunajipanga kwa mwaka mwingine," Amesema Bashe.



Sakata la Askofu Gwajima na Jerry Silaa latua bungeni


Sakata la wabunge Askofu Josephat Gwajima na Jerry Silaa limetua bungeni na leo Jumanne mchana mbivu na mbichi itajulikana kuhusu hukumu yao.

 
Mbunge wa Viti Maalum, Shally Raymond amewasilisha taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu wabunge hao.

 
Hii ni mara ya kwanza katika Bunge la 12 kamati kutoa taarifa yake mbele ya Bunge kwa wabunge waliohojiwa ingawa mbunge wa kwanza kuitwa mbele ya kamati hiyo alikuwa mbunge wa viti maalum, Felista Njau lakini taarifa yake haijawahi kusomwa hadharani.

 
Kanuni za Bunge zinatoa nafasi kwa Bunge kupokea taarifa kwanza kabla ya kuisoma na kuijadili kwa wabunge wote, hivyo baada kamati hiyo itawasilisha taarifa kamili na kujadiliwa bungeni.

 
Shally ameanza kuwasilisha taarifa ya Mbunge wa Kawe, Askofu Gwajima ambaye alisema anatuhumiwa kwa makosa ya kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge.

 
Kwa upande wa Silaa amesema miongoni mwa tuhuma zake ni kuchonganisha wananchi na Bunge.
Wawili hao waliitwa mbele ya kamati mwanzoni mwa wiki iliyopita ambao kila mmoja alihojiwa kwa siku mbili tofauti huku kukiwa na vioja vya kukataa viti walivyopangiwa na wakati mwingine kuhojiwa wakiwa wamesimama.

 
Hukumu ya kamati hiyo huwa ni mapendekezo ya mbunge kusimamishwa vikao kadhaa na kutolipwa posho.

 
Katika Bunge la 11, miongoni mwa waliopitiwa na adhabu hiyo walikuwa Godbles Lema, Halima Mdee, Zitto Kabwe na Ester Bulaya



Marekani yaharibu ndege na vifaa vyake vya kijeshi walivyoviacha Afghanistan


Jeshi la Marekani lilihakikisha linalemaza ndege zao na magari ya silaha waliyoyaacha kwenye uwanja wa ndege mjini Kabul kabla ya kuondoka usiku wa Jumatatu. Maafisa wameeleza.

Kamanda wa majeshi ya Marekani Jeneralo Kenneth McKenzie amesema vikosi ''vililemaza'' ndege zake 73, na magari 70 ya silaha na magari mengine ya kijeshi ili Taliban wasiweze kuyatumia.

''Ndege hizo hazitaweza kuruka tena.....Hakuna mtu yeyote atakayeweza kuyaendesha,'' alisema.

Video iliyotumwa na mwandishi wa habari wa Los Angeles imes ilionesha Taliban wakiingia kwenye uwanja wa ndege eneo ambalo ndege za Marekani zimeegeshwa wakionekana kukagua vifaa hivyo.

Pia Marekani imelemaza mfumo wa roketi wa teknolojia ya juu-ulioachwa uwanja wa ndege. Mfumo wa C-RAM ulifanya kazi Jumatatu kudhibiti shambulio la roketi la wanamgambo wa IS lililolenga uwanja wa ndege.

Kama tulivyoripoti awali, wapiganaji wa Taliban katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita wameonekana wakiwa na vifaa vya kijeshi vya Marekani na vyombo vya moto. Vifaa hivyo vilikuwa vimegawiwa kwa jeshi la Afghanistan, lakini baada ya jeshi la Afghanistan kuweka silaha chini, vifaa hivyo viliingia mikononi mwa Taliban.


 



Mwana FA aeleza kilichotokea ajali aliyopata


Mbunge wa jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA, amepata ajali ya gari eneo la Mkambalani mkoani Morogoro jana Agosti 31, 2021 usiku. 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Fortunatus Muslim na kueleza kuwa mbunge huyo yupo salama.

Kwa upande wake Mwana FA alipopata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari alieleza kuwa kabla ya ajali waliona gari mbele yao inataka kupita gari (Overtake) na ilikuwa mwendokasi sana hivyo hawakuweza kuikwepa ndio ikawaparamia.

Aidha amesema kiafya yeye na mwenzake aliyekuwa naye kwenye gari ni wazima ila alikuwa anasikia maumivu kidogo kifuani mwake.

 



Kimbunga Ida kimekata umeme Louisiana


Kimbunga Ida, mojawapo ya vimbunga vyenye nguvu kabisa kuwahi kupiga katika Ghuba ya Pwani ya Marekani kimekata umeme kwenye zaidi ya nyumba milioni 1 katika jimbo la Louisiana hapo jana. 
 
Kimbunga hicho kiliwasili mjini New Orleans siku ya Jumapili kikiwa na kasi ya kiwango cha nne. Tangu jana Jumatatu, juhudi za uokozi zimekuwa zikiendelea huku mamia ya boti na helikota kikitafuta watu waliokwama kwenye mafuro yaliyosababishwa na kimbunga hicho. 
 
Hadi sasa kumeripotiwa vifo vya watu wawili. Kimoja cha mwendesha pikipiki aliyezama kwenye mafuriko na cha pili cha mtu aliyeangukiwa na mti. 
 
Miaka 16 iliyopita katika wakati sawa na sasa Kimbunga Katrina kilisababisha janga lililoua zaidi ya watu 1,800 New Orleans.

 



Wanasayansi Afrika kusini wanachunguza aina mpya ya virusi vya corona


Wanasayansi nchini Afrika Kusini wanafuatilia aina mpya ya kirusi cha corona ambacho polepole kinazidi kusambaa katika miezi ya hivi karibuni, kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Magonjwa ya Kuambukiza NICD.

Aina hiyo, inayojulikana kama C.1.2., iliripotiwa wiki iliyopita na Kituo cha Utafiti cha KwaZulu-Natal.

Ingawa maambukizi mengi Afrika Kuisini yanatokana na kirusi cha aina ya Delta chenye chimbuko lake nchini India, lakini wanasayansi wameanza kutiwa wasiwasi na aina hiyo ya C.1.2 kutokana na kwamba kasi yake ya mabadiliko ni mara mbili ya aina nyingine za virusi ulimwenguni.

Hata hivyo wanasema kasi yake ya maambukizi bado ni ndogo.

Wakati wa mkutano wa mtandaoni na waandishi wa habari, mtafiti Penny Moore kutoka NIDC amesema hadi hivi sasa hakuna data za kutosha zinazotokana na utafiti kuthibitisha jinsi gani aina hiyo ya kirusi inaweza kuushambulia mwili wa binadamu. Lakini ameongeza kuwa wana uhakika wa kutosha kuwa chanjo zinazotolewa Afrika Kusini zitaendelea kuwalinda watu dhidi ya ugonjwa huo pamoja na kifo.

Hadi hivi sasa aina hiyo mpya ya virusi vya corona ya C.1.2 imeguduliwa katika majimbo tisa ya Afrika Kusini, pamoja na sehemu nyingine ulimwenguni ikiwa ni pamoja na China, Mauritius, New Zealand na Uingereza.

Hata hivyo hakijasambaa sana hadi kuweza kutangazwa kuwa nia aina yenye hatari zaidi ya kirusi cha corona kama zilivyo aina za Delta na Beta zilizozuka Afrika Kusini mwaka uliopita.

Afrika Kusini ni nchi iliyoathirika zaidi na virusi vya corona barani Afrika. Tangu janga hilo kuanza ulimwenguni, Afrika Kuisni imeripoti maambukizi ya watu milioni 2.7 na vifo 81,830.

Kirusi aiana ya Beta kilisababisha wimbi la pili la maambukizi mnamo mwezi Desemba na Januari, na taifa hilo hivi sasa linapambana na wimbi la tatu lilosababishwa na aina ya Delta ambalo linatarajiwa kuendelea kuwepo na kugongana na wimbi lijalo la nne.

Richard Lessells, mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza na mmoja ya waandishi wa utafiti juu ya C.1.2, amesema kuibuka kwake kunatudhihirishia kwamba janga hili halijakwisha na kwamba virusi hivi bado vinatafuta njia bora za kuendelea kutuambukiza.

Wakati huo huo kampeni ya kutoa chanjo ya nchini Afrika Kusini bado inaendelea kwa kasi ndogo, kwani ni asilimia 14 ya idadi jumla ya watu waliochanja hadi sasa.

 



Taliban wawazuia Wamarekani wanaoingia uwanja wa ndege-Ripoti


Wakati Ndege ya Marekani inaondoka Afghanistan bado kulikuwa na raia wa Marekani na Waafghani waliokuwa wakitarajia kuondoka, wakijaribu kuingia kwenye uwanja wa ndege, maafisa wameeleza.

Katika mkutano wa waandishi wa habari awali, Jeneali McKenzie, Mkuu wa vikosi vya Marekani alithibitisha kuwa kuna Wamarekani 100-250 ambao wameshindwa kufika uwanja wa ndege au wameshindwa kuingia kwenye ndege.

Mwanajeshi wa zamani wa Marekani ambaye amesema kuwa alikuwa akisaidia kuratibu shughuli za uokoaji akiwa katika makazi yake Connectcut amesema Taliban waliwazuia wengi kupita. Alikuwa akiwasiliana na wengi, aliandika katika ukurasa wa twitter.

''Taliban walikuwa hawawezekani kuratibu nao mpaka mwiho. Walikataa kutoa ushirikiano nje ya milango ya kuingilia,'' alisema.

BBC haijathibitisha madai haya.

Alex Plitsas, Mwanajeshi wa zamani amesema bado anawasiliana na Wamarekani wanaotaka kuondoka Afghanistan, lakini baadhi hawajajisajili kwenye mamlaka za Marekani ''Hatuwezi kuwaokoa watu ambao hatujui kama wako huko,'' alisema.

 



Monday, August 30, 2021

Pakistan yapeleka msaada wa dawa Afghanistan


Wizara ya ulinzi ya Marekani yasema bado kuna kitisho kikubwa cha mashambulio Afghanistan

Ndege ya Pakistan iliyobeba shehena ya dawa na vifaa vya huduma ya afya imewasili alasiri ya leo ikifikisha mzigo huo kwa mara ya kwanza Afghanistan,tangu ilipoangukia mikononi mwa kundi la Taliban.

Ndege ya Pakistan yenye shehena ya dawa na vifaa vingine vya matibabu iliwasili katika mji wa Kaskazini mwa Afghanistan wa Maza-I Sharif na balozi wa Pakistan mjini Kabul akitangaza kuhusu hatua hiyo ya nchi yake amesema ni sehemu ya kutoa msaada wa kibinadamu wa mahitaji muhimu nchini Afghanistan kwa uratibu wa mashirika ya kimataifa.

Shirika la afya duniani WHO katika taarifa yake limesema ni ndege ya kwanza kati ya tatu za Pakistan zilizopangwa kupeleka msaada wa haraka wa dawa na vifaa tiba katika nchi hiyo inayoshikiliwa hivi sasa na kundi la Taliban. Msaada huo wa  Pakistan unatosha kuwasaidia zaidi ya watu 200,000 wenye matatizo ya kiafya.

Kwa upande mwingine kundi linalojiita dola la kiislamu limedai kuhusika na shambulio la bomu la hivi karibuni huku kundi la Taliban likisema litawashughulikia wanamgambo hao. Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid amesema watakapomaliza kuondoka wanajeshi wa kigeni nchini humo, watayashughulikia mashambulizi yanayopangwa na dola la kiislamu na kutarajia kundi hilo litakomesha mashambulio yao.

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga alhamisi wiki iliyopita alishambulia nje ya uwanja wa ndege wa Kabul na kuuwa watu chungunzima wakiwemo wanajeshi 13 wa Marekani waliokuwa wakitarajia kurudi kwao. Marekani ilianzisha mashambulio ya kulipiza kisasi dhidi ya ngome za IS katika siku chache zilizopita hatua ambayo imewaudhi Taliban.

Kundi hilo limesema hawajatoa idhini kuruhusu oparesheni ya aina hiyo na uhuru wa nchi yao unapaswa kuheshimiwa. Kimsingi zoezi la kuwaondoa maelfu ya wageni na waafghanistan walioko hatarini chini ya utawala wa Taliban linatarajiwa kukamilika kesho Jumanne ikiwa ni pamoja na kukamilika hatua ya kuondoka kabisa wanajeshi wote wa Marekani na Jumuiya ya kujihami ya Nato.

Lakini wakati huohuo mjini Brussels Umoja wa Ulaya unajitahidi kuzuia kuwaachia wakimbizi kutoka Afghanistan kuingia katika nchi za Umoja huo bila ya kudhibitiwa. Hayo yamebainika kwenye taarifa iliyoandaliwa kutangazwa katika mkutano maalum utakaofanyika Jumanne, kuhusu Afghanistan. Umoja wa Ulaya umepania kuepusha marudio ya kile kilichotokea mwaka 2015 ambapo wimbi kubwa la kumiminika wakimbizi na wahamiaji lilishuhudiwa katika nchi za Jumuiya hiyo ambazo zilikuwa hazijajipanga na kuzusha mgawanyiko mkubwa miongoni mwao, hali ambayo vile vile ilisababisha kuwapa nguvu vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia katika nchi kama Ugiriki, Italy na kwengineko.

 



Kiungo wa Azam FC aondoka kambini Zambia


KIUNGO wa kimataifa wa Kenya na Klabu ya Azam, Kenneth Muguna leo ameondoka kwenye kambi ya Azam FC iliyopo Zambia kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa ya Kenya.

 

Azam ipo Ndola, Zambia kwa ajili ya maandalizi ya kabla ya msimu ya takribani wiki moja na nusu, ambapo wakiwa huko wamepanga kucheza michezo minne ya kirafiki kabla ya kurejea Tanzania Septemba 5, mwaka huu.

 

Watakaporejea Azam watakuwa kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed ya Somalia, unaotarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 10 hadi 12, mwaka huu.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Kikosi chetu kinaendelea vizuri na maandalizi ya kabla ya msimu ‘Preseason’ hapa Ndola Zambia.

 

“Tunatarajia kuwa kiungo wetu wa kimataifa wa Kenya Kenneth Muguna ataondoka kambini kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa ya nchi yao.”


Mchezo wa pili Azam FC ilicheza na Kabwe Warriors ambapo ilishinda kwa bao 1-0 lilifungwa na Prince Dube hivyo kiungo.

 



Afghanistan: Ndege ya mwisho ya Marekani yaondoka, ikiashiria tamati ya operesheni yake


Ndege ya mwisho ya jeshi la Marekani imeondoka Kabul, ikiashiria mwisho wa uwepo wa nchi hiyo nchini Afghanistan.

Kamanda mkuu wa jeshi la Marekani katika eneo hilo, Jenerali Kenneth McKenzie, amesema ndege ya mwisho ya C17 iliondoka Kabul ikiwa na balozi wa Marekani baada ya saa sita usiku saa za eneo hilo.

Aliongeza kuwa ujumbe wa kidiplomasia kusaidia wale ambao hawakuweza kuondoka kabla ya tarehe ya mwisho utaendelea.

Milio ya risasi ya sherehe za Taliban ilisikika baada ya ndege ya mwisho kuondoka.

Kuondoka kwa ndege hiyo ya mwisho kunaashiria kumalizika kwa vita virefu kabisa vya Marekani, na juhudi kubwa ya uokoaji ambayo ilianza tarehe 14 Agosti mara tu baada ya Taliban kuchukua nchi.

Jenerali McKenzie alisema kuwa kwa jumla, ndege za Marekani na nato ziliwaondoa zaidi ya raia 123,000 - wastani wa zaidi ya raia 7,500 kwa siku wakati huo.

Akiongea baada ya tangazo hilo, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken alizungumza huko Washington, akiita uhamishaji huo "jukumu kubwa la kijeshi, kidiplomasia na kibinadamu" na moja wapo ya changamoto kubwa kwa kazi ambayo Marekani imewahi kutekeleza.

"Ukurasa mpya umeanza," alisema. "Ujumbe wa kijeshi umekwisha. Ujumbe mpya wa kidiplomasia umeanza."

Lakini alisema kuwa Taliban ilihitaji kupata uhalali wake na itahukumiwa kwa kiwango ambacho ilitimiza ahadi na majukumu yake ya kuruhusu raia kusafiri bure kwenda na kutoka nchini, ilinde haki za Waafghan wote wakiwemo wanawake, na ilizuia vikundi vya ugaidi kutokana na kupata nafasi nchini.

Aliongeza kuwa wakati Marekani ikisitisha uwepo wake wa kidiplomasia huko Kabul, na kuhamisha operesheni zake kwenda Doha, itaendelea na "juhudi zake" za kuwasaidia Wamarekani, na Waafghan na pasi za Marekani, kuondoka Afghanistan ikiwa wanataka.

Bwana Blinken alikuwa waziri wa kwanza wa baraza la mawaziri la Biden kuzungumza kuhusu kujitoa.

Rais Joe Biden alitoa taarifa fupi kuwashukuru wale wote waliohusika katika operesheni ya uokoaji kwa siku 17 zilizopita na kusema kuwa atalihutubia taifa baadaye Jumanne.

Wakati huo huo, Marekani bado haijaelezea ripoti kwamba shambulio la ndege isiyo na rubani dhidi ya mtu anayeshukiwa kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga nchini Afghanistan liliwaua raia kadhaa, wakiwemo watoto sita na mtu ambaye alifanya kazi kama mtafsiri wa vikosi vya Marekani.

Jamaa wa watu hao walisema shambulio hilo, kwenye gari karibu na uwanja wa ndege wa Kabul, lilitokana na taarifa isiyo sahihi. Pentagon ilisema ilikuwa ikitathmini na kuchunguza ripoti hizo.

 



Vikosi vya Israel vyawajeruhi Wapalestina 18


Watu 18 walijeruhiwa wakati wa uingiliaji wa Wapalestina wanaopinga uvamizi wa Israel katika eneo la Gaza.

Kukabiliana na kizuizi cha Israel, Wapalestina wamekuwa wakifanya maandamano katika eneo la mpakani. Walakini, vikosi vya Israel vilijibu tena kwa kutumia nguvu kwa maandamano hayo ya amani.

Wapalestina 18 walijeruhiwa katika uingiliaji mkali wa wanajeshi wa Israel wanaotumia risasi za moja kwa moja na gesi ya kutoa machozi.

Katika mji wa Haifa, Israel, Wapalestina, ambao ni raia wa Israel, walifanya maandamano mbele ya gereza hilo na kutaka wafungwa wa kike wa Kipalestina waachiliwe.

Kuna takriban wafungwa 4,850 wa Kipalestina, 41 kati yao ni wanawake, katika magereza ya Israel.

Wakati wa kuongezeka kwa mvutano huko Gaza, mkutano wa kiwango cha juu ulifanyika kati ya vyama vya Palestina na Israel.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alijadili uhusiano wa Israel na Palestina na Waziri wa Ulinzi wa Israel Benny Gantz. Ilibainika kuwa wakati wa mkutano uliofanyika Ramallah, Ukingo wa Magharibi, mambo yote ya uhusiano yalizungumziwa.

Tangu mashambulizi ya mnamo Mei, Israel imezuia kwa kiasi kikubwa kuingia kwa bidhaa Gaza. Hali hii ilisababisha hali ya uchumi huko Gaza kuwa mbaya zaidi.

Israel imekuwa ikizuia uingiaji kwa njia ya nchi kavu, baharini na angani tangu 2006 katika Ukanda wa Gaza wenye idadi ya watu takriban milioni 2.1



Tetesi za soka kimataifa


Real Madrid imejiondoa katika mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kutoka Paris St-Germain kwasababu vilabu haviwezi kukubali ada.(RMC Sport - in French)

Hata hivyo, klabu hiyo ya Uhispania inatarajia kuipiku PSG katika mbio za kumsajili kiungo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 18 Eduardo Camavinga kutoka Rennes. (Canal+ via Get French Football News)

Manchester City hawatarajii yeyote zaidi ama kuingia au kuondoka kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa baada ya kumfungia kipa wa Brazil Ederson, 28, kwa mkataba mpya. Kiungo wa Ureno Bernardo Silva, 27, alikuwa ndiye gumzo katika ofa kutoka AC Milan, lakini hakufurahishwa na hatua hiyo. (Times - subscription required)

Barcelona watajaribu kumsajili beki wa kulia wa Arsenal na Uhispania Hector Bellerin, 26, ikiwa mlinzi wa Brazil Emerson Royal, 22, ataondoka Nou Camp na kujiunga na Tottenham. (Mundo Deportivo - in Spanish)

West Ham wamefikia makubaliano ya maneno na Ajax kumsaini beki wa kushoto Nicolas Tagliafico, ingawa kukamilisha makubaliano hayo kabla ya tarehe ya mwisho uhamisho , Jumanne itakuwa vigumu na mchezaji huyo wa miaka 28 ambaye sasa hivi yuko katika jukumu la kimataifa na Argentina. (Telegraaf - in Dutch)

Hata hivyo, kuna wasiwasi wa Hammers kuendeleza mpango wa kutafuta makubaliano na Tagliafico licha ya beki huyo kutolewa kwa klabu hiyo na mawakala wengi. (Athletic)

Chelsea wamemuambia ajenti wa beki wa kati wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde watafanya jaribio la mwisho kumsajili mchezaji huyo wa miaka 22. (ABC Sevilla, via Sport Witness)

Leicester City wameonyesha nia kwa winga wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 20, ambaye pia amehusishwa na Borussia Dortmund. (football.london)

Blues pia wanataka kumchukua kiungo wa Atletico Madrid raia wa Uhispania Saul Niguez, 26, kwa mkopo lakini mabingwa wa La Liga wanataka kujumuisha kifungu ambacho kitaifanya kuwa mkataba wa kudumu kwa £ 34m. (Goal)

Burnley wapo kwenye mazungumzo ya kumleta mlinzi wa Swansea City na Wales Connor Roberts, 25, Turf Moor. (WalesOnline)

Mshambuliaji wa Wolves Adama Traore, 25, amemuajiri wakala Jorge Mendes kumsaidia kupata uhamisho Tottenham. Mchezaji huyo wa Uhispania anataka kuungana tena na kocha wake wa zamani Nuno Espirito Santo. (Footballer Insider)

Wolves wamewasilisha dau la pauni milioni 8.6 kumsajili mlinzi wa Marseille na Croatia Duje Caleta-Car lakini timu hiyo ya Ligue 1 inataka pauni milioni 12.9 kabla ya kumruhusu mchezaji huyo wa miaka 24 aondoke. (Foot01 - in French)

Juventus wameamua kutotafuta mkataba kwa kiungo wa kati wa Barcelona na Bosnia-Herzegovina Miralem Pjanic, 31, huku kilabu cha Serie A kikikaribia kumsajili Mholanzi Mohamed Ihattaren mwenye umri wa miaka 19 kutoka PSV Eindhoven. Pjanic, ambaye alikaa Juventus kwa miaka minne kabla ya kujiunga na Barca mnamo mwaka 2020, ni mmoja wa wachezaji kadhaa ambao kilabu hicho cha Kikatalani wanajaribu kumuuza kabla ya tarehe ya mwisho ya Jumanne. (Goal)

Brentford imetoa ofa ya pauni milioni 13 kwa beki wa Gremio, Mbrazil Vanderson, 20, ambaye pia amevutia AC Milan msimu huu. (Goal)

Kiungo wa kati wa Chelsea Tino Anjorin anakaribia kujiunga na Lokomotiv Moscow katika mkataba wa mkopo ambao unajumuisha chaguo la pauni milioni 17 kumnunua Mwingereza mwenye umri wa miaka 19. (Goal)

 



Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...