Maafisa wa Kaskazini mwa Nigeria wameiomba msaada serikali kuu baada ya miezi ya hivi karibuni watu wapatao 3,000 kujisalimisha wakiwemo wanamgambo wa Boko Haram. Jeshi la Nigeria limesema hiyo ni ishara kwamba limefanikiwa kuwazidi nguvu wanamgambo wa kundi hilo la kijihadi katika mgogoro unaoendelea kwa miaka 12.
Wanamgambo hao pamoja na familia zao walianza kujisalimisha kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau mnamo mwezi Mei wakati wa mapigano na wapiganaji wa Tawi la Magharibi mwa Afrika la Dola la Kiislam (ISWAP).
Gavana wa Jimbo la Borno Babagana Zulum amesema wengi waliojisalimisha ni wanawake, watoto na wakulima ambao walilazimishwa kufanya kazi katika eneo ambalo lilikuwa likidhibitiwa na Boko Haram.

No comments:
Post a Comment