Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

WAZIRI HASUNGA ATANGAZA MAZAO YATAKAYOUZWA KWENYE MFUMO WA STAKABADHI GHALANI I


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akitangaza msimamo wa serikali kuhusu Mazao yatakayouzwa kwa mfumo wa Stakabadhi Ghalani ofisini kwake Jijini Dodoma juzi tarehe 30 Mei 2020. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Serikali imetangaza rasmi mazao ya kuanzia yatakayouzwa kupitia mfumo maalumu wa uuzaji wa mazao wa Stakabadhi ghalani.

Mazao hayo ni pamoja na zao la Korosho ambalo limekuwa na mafanikio makubwa kupitia mfumo huo, mazao mengine ni Ufuta ambao utauzwa kwa mfumo huo katika baadhi ya maeneo nchini.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametangaza msimamo huo wa serikali wakati akizingumza ofisini kwake Jijini Dodoma juzi tarehe 30 Mei 2020 huku akiyataja mazao mengine yaliyoingizwa katika mfumo huo kuwa ni pamoja na Choroko, Pamba, Dengu n.k pamoja na Kahawa itakayotumia mfumo huo kwa baadhi ya maeneo.

Waziri Hasunga amesema kuwa mfumo huo tangu umeanza kutekelezwa umekuwa na faida kubwa hususani katika mikoa ya kusini kupitia zao la korosho lakini umeleta changamoto kubwa katika maeneo ambayo misingi ya kuanzishwa kwa mfumo huo haijatimizwa.

Amesema kuwa ili mfumo wa Stakabadhi ghalani uweze kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa ni lazima kuwa na vyama vya Ushirika vya mazao vilivyoanzishwa na wananchi wenyewe katika eneo husika.

Ameeleza kuwa lengo la kuwa na vyama hivyo ni kufanya kazi ya kukusanya mazao na kuyapeleka kwenye ghala kuu ambalo limesajiliwa na kuwa na viwango vinavyotakiwa.

Jambo jingine ni lazima kuwepo na muendesha ghala mwenye leseni anayetambuliwa na Bodi ya Maghala na lazima elimu ya kutosha itolewe kwa wananchi ya namna ya kutumia mfumo huo na ushiriki wao katika kufuatilia minada itakavyokwenda.

Amesisitiza kuwa ili mfumo huo uweze kufanya kazi vizuri wanunuzi lazima wawepo, Mfumo utangazwe na kuuzwa hadharani kadhalika kuwe na mzigo wa kutosha pamoja na ubora wa uhifadhi ili kuwavutia wanunuzi.

Ameeleza kuwa sio mazao yote yanaweza kutumika katika mfumo wa stakabadhi ghalani ni baadhi ya mazao kulingana na uwezo wake wa kutunzwa na kukaa muda mrefu bila kuharibika. Hivyo kwa mazao ya mboga na matunda haiwezi kuwa jambo jepesi kuzitunza muda mrefu hivyo sio rahisi kuingia katika mfumo wa stakabadhi ghalani.

“Ukichukua mazao kama karanga ukaweka kwenye mfumo huu, unaweza ukahifadhi lakini tatizo la karanga zinaweza zisiwe na unyevu unaokubalika hivyo kuna hatari ya kusababisha Sumu kuvu.

Waziri Hasunga amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa mfumo wa Stakabadhi ghalani ilikuwa ni kulinda maslahi ya wakulima kwani mazao hukusanywa pamoja, kuwekwa kwenye madaraja kisha kupanga bei kwa pamoja hivyo kuuza kwa bei nzuri.

Mfumo huo unamuwezesha mkulima kupata mkopo popote baada ya kuwa na risiti ya stakabadhi ghalani wakati akisubiri mazao yake kuuzwa kwa bei nzuri

Kwa utaratibu mfumo wa stakabadhi ghalani unasimamamiwa na Bodi ya Maghala ambayo ipo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara hivyo kuikabili changamoto hiyo serikali imeihamishia Bodi hiyo wizara ya kilimo ili kupunguza muingiliano uliopo wa kimajukumu katika Wizara hizo mbili.

Mhe Hasunga amesema kuwa katika mikoa ambayo tayari vyama vya Ushirika vimeanzishwa mfumo huo unafanya vizuri lakini kwa mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, Katavi ambapo vyama vya Ushirika havijaanzishwa mfumo huo hauwezi kufanya kazi.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga (Mb) ametoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wilaya katika maeneo ambayo hakuna vyama vya Ushirika vilivyoanzishwa na wananchi wenyewe, Hakuna maghala yaliyosajiliwa, na Hakuna wenye leseni wanaotambulika na Bodi ya Maghala kutowasumbua wananchi badala yake wauze kwa uhuru katika maeneo watakayo.

Kadhika, Waziri Hasunga amewataka wafanyabiashara watakaonunua mazao hayo kwa mzigo unaozidi Tani moja ni lazima Kodi za Halmashauri zilipwe kwa mujibu wa utaratibu wa kikanuni na kisheria.

Ameongeza kuwa moja ya majukumu ya wakuu wa Mikoa na Wilaya katika mfumo wa mazao ya Stakabadhi ghalani ni kusimamia biashara kwa kuzingatia taratibu bila wananchi kudhulumiwa ambapo wasimamizi ni vyama vya Ushirika, pamoja na Bodi ya Maghala.


Upinzani hupata mwamko vikiwa na mgombea wa Urais mwenye asili na CCM-Said Said Nguya





DC Morogoro atoa siku 14 wenye vibanda vya nyasi kuondoka Msamvu

Mji wa Morogoro umekumbwa na taharuki usiku wa kuamkia juzi baada ya moto kuzuka katika stendi kuu ya mabasi Msamvu na kuteketeza vibanda vya wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao katika stendi hiyo, ambapo Mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, ametoa agizo la siku 14 kubomolewa kwa vibanda vyote vilivyopo kituoni hapo.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro ameeleza hayo baada ya tukio la moto uliosababishwa na uunguwaji holela wa umeme katika vibanda hivyo na kusababisha kuteketeza mali zao. Zaidi ya vibanda viwili huku Mkuu wa Wilaya akimuagiza meneja wa tanesco morogoro kukata umeme unaongia katika vibanda hivyo.

Ofisi ya DC Lindi yaipa kongole halmashauri ya manispaa ya Lindi

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Kufuatia jitahada kubwa zilizofanywa na watendaji na madiwani wa halmashauri ya manispb ya Lindi. Serikali wilayani Lindi imepongeza halmashauri hiyo.

 Pongezi hizo zilitolewa juzi na katibu tawala wa wilaya(DAS) ya Lindi, Thomas Safari wakati wa kikao cha mwisho cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika juzi katika ukumbi wa mtakatifu Andrea Kagwa uliopo manispaa ya Lindi.

Safari alisema licha ya changamoto ndogondogo ambazo baadhi yake zimesababishwa na raslimali chache lakini inastahili kupongezwa.

 Alisema ushirikiano wa madiwani na watendaji wanaongozwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Joomary Satura umesababisha mabadiliko makubwa ya maendeleo.

 Alisema ushirikiano huo licha ya kubadilisha mandhari ya manispaa, hasa kwenye miundombinu ya barabara, lakini pia umeiletea sifa na heshima manispaa hiyo.

 Alisema barabara nyingi katika mitaa ya katikati ya manispaa hiyo zimejengwa barabara za kiwango cha lami.

Hali ambayo imebadilisha haraka muonekano kuliko miaka ya nyuma. '' Kwahakika ushirikiano wenu umesababisha mambo mazuri mengi licha ya barabara lakini halma mashauri hii imewahi kuchukua ushindi wa kwanza wa mbio za Mwenge wa Uhuru.

Hakika mmeiletea heshima manispaa na wilaya ya Lindi,'' alisema Safari.

Aidha katibu tawala huyo alitoa wito kwa madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo waendeleze mshikamano na ushirikiano huo hata baada ya madiwani hao kumaliza muda wao.

 '' Mpendane hata mkiwa nje ya uongozi, wapendeni watumishi hawa na watumishi wapendeni madiwani hawa ili hata watoto wenu wapendane,'' alisisitiza Safari.

Kwaupande wake meya wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Mohamed Lidume Lihumbo alitoa wito kwa watendaji waendelee kufanyakazi kwa juhudi na maarifa, huku wakiepuka kufanyakazi kwa mazoea.

 Alitoa wito kwa madiwani wenzake watoe ushirikiano kwa maslahi ya manispaa hiyo hata wakiwa nje ya uongozi walionao kwa kufichua vitendo vinavyoweza kusababisha halmashauri hiyo ikose na kupoteza mapato.

Ngasa: Tupo tayari kurejea kwenye ligi

MRISHO Ngasa, kiungo mkongwe ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kurejea kwenye mechi za ushindani baada ya kuanza mazoezi Mei 27.

Masuala ya michezo yalisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga dunia.Serikali imeruhusu masuala yamichezo kuanza Juni Mosi na tayari bodi ya ligi imetangaza kuwa Juni 13 ligi itaanza.

Ngassa amesema kuwa wanaendelea vizuri na mazoezi jambo linalowafanya wazidi kujiamini pale ligi itakapoanza.

“Kila kitu kinakwenda vizuri kwenye mazoezi na kila mchezaji anafurahi kwani tulikuwa nje kwa muda mrefu, kwa sasa tupo tayari kurejea uwanjani ili kuendelea pale ambapo tuliishia,” amesema.
Yanga ikiwa imefunga mabao 31, Ngasa amehusika kwenye mabao matatu, akifunga mawili na kutoa pasi moja ya bao.

Jafo atoa siku 17 ujenzi wa soko Morogoro kukamilika

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo ameagiza kukamilishwa kwa ujenzi wa soko la Manispaa ya Morogoro ifikapo Juni 17 mwaka huu.

Agizo hilo amelitoa leo mjini Morogoro katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyo chini ya Ofisi hiyo yake baada ya kuona kuwa limechelewa kukamilika ndani ya muda uliopangwa awali.

”Hili ni Soko  kubwa la bidhaa kupitia fedha za miradi ya kimkakati hapa nchini lilioanza kujengwa mwanzoni mwa mwaka wa jana ambalo litawezesha wafanya biashara kupata mazingira rafiki ya kufanyia biashara”amesema Jafo

Aidha Jafo ametembelea na kujionea  ujenzi wa stendi ya daladala ya Mafiga inayojengwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(Tarura)  kwa ajili matumizi ya Manispaa hiyo ya Morogoro huku akifurahishwa na kazi ya ujenzi wa stendi hiyo ambayo imefikia  wastani wa asilimia 98 ya ujenzi.

Jafo ameitaka Manispaa hiyo kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vikiwemo masoko na standi za mabasi ili kuongeza pato la Manispaa hiyo.



Yanga yaweka historia ya aina yake, yasaini mkataba na La Liga

Kutokana na janga la Corona viongozi wa La Liga na wale wa Sevilla wameshindwa kuhudhuria tukio la kusaini mkataba wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji la kihistoria iliyofanyika pale Serena Hotel.

Hata hivyo viongozi hao wametuma video clip wakielezea uzuru wao na kueleza mpango kazi wao nini watakifanya kuhakikisha Yanga SC inafanikiwa kisha mkurugenzi wa La Liga akasaini mkataba na kuutuma kisha Yanga SC kuupokea, Mshindo Msolla na Eng Hersi Said wameusaini na kukamilisha zoezi!

Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo amepongeza jitihada hizo zinazofanywa na viongozi hao hivyo amewataka kuendelea na uimarishaji katika sekta ya michezo.

“Niwapongeze kwa hili la leo, matamanio ya uendeshaji kwa Yanga ni ya muda mrefu toka kwa Castro Mponela. .alipokuja na Yanga kampuni , la pili alipokuwa Yusuf Manji alipokuja na dhana ya kukodisha hili litakuwa la tatu mengine yalikuwa kubadilisha katiba”. Amesema Dkt.Kikwete.



Wakili asema kifo cha George Floyd kilipangwa

Wakili wa familia ya George Floyd, ambaye kifo chake kiliibua maandamano ya hasira kote nchini Marekani , amemshutumu afisa wa polisi kwa "kupanga mauaji".

Polisi wa Minneapolis Derek Chauvin ameshitakiwa kwa mauaji , lakini wakili Benjamin Crump amekiambia kituo cha habari cha CBS news kuwa yalikuwa ni mauaji ya kiwango cha kwanza.

"Tunadhani kwamba alikua na nia … takriban dakika tisa aliendelea kushindilia goti lake kwenye shingo ya mwanaume ambaye alikua anamuomba amsamehe na kumwambia kuwa hawezi kupumua," alisema

matukio ya uporaji yameripotiwa katika jimbo la Philadelphia.

Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya polisi na kuiba katika duka moja .


Rais Donald Trump alituma ujumbe wake wa twitter uliosema: Sheria na amri vifuatwe Philadelphia, SASA! Wanapora maduka. Walete wanajeshi wetu waingilie kati ".

Tukio la Floyd limeibua ghadhabu miongoni mwa Wamarekani juu ya mauaji yanayotekelezwa na polisi dhidi ya watu weusi.

Hii inafuatia kesi maarufu ya mauaji ya Michael Brown mjini Ferguson, Eric Garner mjini New York na kesi nyingine zilizowasilishwa mahakamani na vuguvugu linalojulikana kama Black Lives Matters.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO JUNI 1,2020



  
 
 


MAGAZETI YA LEO 1/6/2020

















Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu June 1

















Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...