Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo ameagiza kukamilishwa kwa ujenzi wa soko la Manispaa ya Morogoro ifikapo Juni 17 mwaka huu.
Agizo hilo amelitoa leo mjini Morogoro katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyo chini ya Ofisi hiyo yake baada ya kuona kuwa limechelewa kukamilika ndani ya muda uliopangwa awali.
”Hili ni Soko kubwa la bidhaa kupitia fedha za miradi ya kimkakati hapa nchini lilioanza kujengwa mwanzoni mwa mwaka wa jana ambalo litawezesha wafanya biashara kupata mazingira rafiki ya kufanyia biashara”amesema Jafo
Aidha Jafo ametembelea na kujionea ujenzi wa stendi ya daladala ya Mafiga inayojengwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(Tarura) kwa ajili matumizi ya Manispaa hiyo ya Morogoro huku akifurahishwa na kazi ya ujenzi wa stendi hiyo ambayo imefikia wastani wa asilimia 98 ya ujenzi.
Jafo ameitaka Manispaa hiyo kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vikiwemo masoko na standi za mabasi ili kuongeza pato la Manispaa hiyo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment