Search This Blog

Thursday, April 30, 2020

Breaking: Waziri Wa Katiba Na Sheria Mahiga Afariki Dunia -Video



Waziri wa Katiba na Sheria , Balozi Dkt Augustine Mahiga amefariki dunia alfajiri ya leo baada ya kuugua ghafla akiwa mjini Dodoma.

Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kumuelezea Balozi Mahiga kuwa ni mchapakazi, mzalendo na mwanadiplomasia mahiri.





NEWZ ALERT: Rais DKT Magufuli atangaza kifo cha Waziri Augustine Mahiga






Pichani ni aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mbunge)  aliyefariki leo tarehe 01 Mei, 2020 Jijini Dodoma. 








VIDEO: Waziri wa katiba na sheria DKT. Augustine Mahiga afariki dunia


Rais Magufuli anasikitika kutangaza kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt.Augustine Mahiga(Mbunge) kilichotokea leo alfajiri Mei 01,2020 Dodoma, Balozi Mahiga ameugua ghafla akiwa nyumbani kwake Dodoma na amefikishwa Hospitali akiwa tayari ameshafariki.

“Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa, Marehemu Balozi Mahiga, alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nililompa”-JPM

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..USISAHAU KU SUBSCRIBE



Breaking News: Waziri Augustine Mahiga afariki dunia baada ya kuugua ghafra

Rais Magufuli anasikitika kutangaza kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt.Augustine Mahiga(Mbunge) kilichotokea leo alfajiri Mei 01,2020 Dodoma, Balozi Mahiga ameugua ghafla akiwa nyumbani kwake Dodoma na amefikishwa Hospitali akiwa tayari ameshafariki.

“Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa, Marehemu Balozi Mahiga, alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nililompa”-JPM

TANZIA: Waziri wa Katiba na Sheria , Mh. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amefariki dunia ......Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anasikitika kutangaza kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mbunge) kilichotokea leo alfajiri tarehe 01 Mei, 2020 Jijini Dodoma.

Mhe. Balozi Mahiga ameugua ghafla akiwa nyumbani kwake Jijini Dodoma na amefikishwa hospitali akiwa tayari ameshafariki dunia.

Mhe. Rais Magufuli ametoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Wabunge, Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria na wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kuondokewa na mpendwa wao, na amesema anaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Mhe. Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Balozi Mahiga kuwa alikuwa mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na Mwanadiplomasia mahiri aliyeiwakilisha na kuipigania Tanzania katika njanya za Kimataifa kwa miaka mingi.

“Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa, Marehemu Balozi Mahiga alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nililomtuma” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.




MAGAZETI YA LEO 1/5/2020

















Rais Magufuli Awapongeza Wafanyakazi na Kuwatakia Heri katika Siku ya Leo ambayo ni Mei Mosi ( Siku ya Wafanyakazi)




Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa May 1




















BMT kuandaa muongozo kuhusu ukomo wa wachezaji wa Nje nchini.

Na Shamimu Nyaki, WHUSM-Dodoma
Serikali haijatoa ukomo wa wachezaji kutoka nje kushiriki michezo hapa nchini bali imeibua mjadala kwa wadau ili watoe maoni yao.
 
Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa ni hatua ya kuboresha na kuimarisha sekta ya michezo nchini. 
 
Ili kutekeleza mjadala huo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limepewa jukumu la kuendelea kuandaaa mwongozo utakaotumika kukusanya maoni kutoka kwa wadau kuhusu ukomo wa wanamichezo wa nje hapa nchini.
 
“Katika Hotuba ya Bajeti iliyosomwa hivi karibuni Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, hakuongolea idadi ya wachezaji kutoka nje wanaotakiwa kucheza nchini, bali aliagiza BMT kuandaa mjadala mpana katika kukusanya maoni kwa wadau wa michezo kuhusu namna bora ya kusajili wachezaji wa kigeni katika michezo yote hapa nchini” alisema Bw. Singo.
 
Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo ambainisha kuwa Mhe.Waziri Dkt. Mwakyembe alisisitiza kuwa wanamichezo wote kutoka nje ya nchi wanaosajiliwa hapa nchini ni lazima wawe na ubora pamoja na viwango vinavyotakiwa.
 
Akifafanua suala hilo Bw. Singo amesema kuwa michezo yote ya kulipwa kwa sasa imeendelea kukua duniani kote na nchi yetu pia inayo wachezaji wengi wanaocheza michezo hii ikiwemo Mpira wa Kikapu (Basketball), Kriketi, Mpira wa Miguu na michezo mingine, hivyo, Serikali haijatoa maelekezo ya ukomo wa usajili wa idadi ya wachezaji bali inataka kuwepo kwa mjadala wa wazi utakaotoa mwongozo wa ukomo wa idadi ya usajili wa wachezaji wa kigeni.
 
Aidha, Mkurugenzi huyo alitoa rai kwa wadau wa michezo nchini watakapopata fursa ya kuchangia au kutoa maoni katika mjadala huo wasiegemee katika timu wanazoshabikia, bali watoe maoni ambayo yatasaidia kuendeleza michezo na kuendeleza vipaji vya wanamichezo wetu pamoja na kukuza michezo nchini.
MWISHO






NAIBU WAZIRI MGALU AMTAKA MKANDARASI KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Na Ripota wetu – Morogoro
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amefanya ziara mkoani Morogoro na kumwagiza Mkandarasi, Kampuni ya State Grid, anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, mkoani humo kumaliza kazi kwa wakati.
Mgalu alilazimika kufanya ziara hiyo baada ya kupokea malalamiko ya kusuasua kwa Mradi husika ambapo aliwaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kumsimamia Mkandarasi huyo ili kuhakikisha anakamilisha kazi kwa muda ulioainishwa kwenye Mkataba.
Wakati wa ziara hiyo iliyofanyika Aprili 25 mwaka huu, Naibu Waziri alitembelea baadhi ya vijiji vya Wilaya za Gairo na Mvomero kujionea maendeleo ya kazi husika.
Vijiji vilivyotembelewa ni Ukwamani na Nguyami (Gairo) pamoja na Komtanga (Mvomero). Kadhalika, Naibu Waziri alitembelea Yadi ya Mkandarasi iliyopo Gairo Mjini.
Naibu Waziri aliwaasa viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Covid – 19 unaosababishwa na virusi vya Corona huku wakiendelea kufanya shughuli zao.
Pia, aliwataka TANESCO Mkoa wa Morogoro kuhakikisha wananchi wote wanaolipia ili kuunganishiwa umeme, wanapatiwa huduma hiyo kwa wakati.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati-mwenye ushungi), akikagua kazi ya kuunganisha umeme vijijini inayoendelea katika eneo la Ukwamani, wilayani Gairo hivi karibuni.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), akikagua maendeleo ya kazi ya usambazaji umeme vijijini katika kijiji cha Komtanga, wilayani Gairo, akiwa katika ziara ya kazi, Aprili 25 mwaka huu.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye ushungi), akikagua Yadi ya Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, wilayani Gairo, akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni.


UGONJWA WA CORONA (Covid-19) WAIHIRISHA SHEREHE ZA MEI MOSI 2020 ZANZIBAR



TAMKO LA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI ZANZIBAR KUPITIA VYOMBO VYA HABARI  KATIKA KUADHIMISHA SIKU SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI 2020
Ndugu Viongozi, Wafanyakazi na Wananchi  

Kama wengi wetu tunavyoelewa kwamba  leo ni  tarehe 01-05-2020 ambayo pia hujulikana kama Siku ya Mei Mosi. Siku ambayo Wafanyakazi wa Zanzibar kila Mwaka hushirikiana na Wafanyakazi wenzao Duniani kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani

Kwa msingi huo hatunabudi  kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na Mwenye kurehemu kwa kutufikisha siku ya leo tukiwa wazima na amani ya nchi yetu. Aidha tunawapongeza Viongozi wetu wa Serikali hususan Mhe. Rais kwa uongozi wake uliobora , Waajiri na wananchi kwa kushirikiana nasi katika maadhimisho haya 

Ndugu Viongozi, Wafanyakazi na Wananchi  
Siku hii ni miongoni mwa Siku maarufu Duniani ambayo kihistoria inaadhimishwa kutokana na tukio lililotokea huko Marekani siku nyingi zilizopita ambako Wafanyakazi waliandamana kwa amani kwa Madhumuni ya  kupinga madhila waliyokuwa wakifanyiwa katika sehemu zao za kazi.

Kama sote tunavyokumbuka  kwamba, Maadhimisho haya kila mwaka huadhimishwa kwa ratiba ndefu inayojumuisha shughuli mbali mbali, hata hivyo kwa mwaka huu tumelazimika kuakhirisha Ratiba yote kutokana na Mripuko ya Maradhi ya CORONA yaliyoingia nchini mwetu katikati ya Mwezi wa Tatu.

Badala yake tumeamua kutowa tamko hili la wafanyakazi kwa lengo kuadhimisha tukio hilo na kutathmini haki na mazingira ya kazi kwa kipindi cha Mwaka mmoja uliopita kama ilivyo lengo kuu la Maadhimisho ya Mei Mosi kila mwaka.

Ndugu Viongozi, Wafanyakazi na Wananchi  
Kwa vile Mwaka huu 2020 unatarajiwa kuwa wa mwisho wa Uongozi wa Awamu ya Saba (07) inayoongozwa na Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Shirikisho limekusudia kufanya tathmini kwa uchache juu ya uongozi wa Awamu hii ili kutambua mchango wake katika maendeleo ya sekta ya ajira pamoja na changamoto zilizojitokeza ambazo  kwa maoni yetu zinahitaji kufanyiwa kazi
Kwa msingi huo, na kwa niaba ya Wafanyakazi wa Zanzibar nachukuwa fursa hii kuainisha baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya ajira kwa kipindi cha Awamu ya Saba ya Uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ambayo miongoni mwa mengine ni

1.      Kutunza amani na utulivu wa nchi na kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao za kawaida
2.      Kuimarika kwa fursa za ajira nchini ambapo zaidi ya vijana 11, 000 wameajiriwa katika Wizara na taasisi za Serikali katika kipindi hicho
3.      Kuundwa kwa Sheria ya Utumishi na ya Mwaka 2011 na Kanuni za Utumishi za 2014 kwa lengo la kuweka mifumo bora ya utumishi Nchini pamoja na kuundwa kwa Wizara na taasisi maalum zinayoshughulikia Utumishi wa Umma
4.      Kuimarishwa kwa maslahi ya wafanyakazi katika sekta ya umma, binafsi na Sekta isiyo rasmi hasa mishahara pamoja na kurekebishwa mifumo ya utumishi na uwajiri
5.      Kuimarishwa kwa Miundombinu ya Nchi na sehemu za kazi hasa za utowaji wa huduma kulikozingatia afya na usalama sehemu za kazi na utowaji wa huduma bora nchini
6.      Serikali kuendelea kuimarisha mifumo ya hifadhi ya jamii kwa wananchi hasa wazee kwa kutunga Sheria na Sera za kuwalinda na kuimarishwa, kutoa pencheni na kuimarisha viwango vya chini vya pensheni za wastaafu.
7.      Utayari wa Serikali kuzungumza na wafanyakazi na viogozi wa Vyama vya wafanyakazi yanapotokea matatizo ya kikazi au mambo yanayohusu haki za wafanyakazi
8.      Kuondoa michango katika  huduma za afya kwa wajawazito na watoto wadogo na katika sekta  za elimu kuanzia Msingi hadi sekondari ili kupunguza mzigo kwa wafanyakazi na wananchi
Ndugu Viongozi, Wafanyakazi na Wananchi  
Kama tunavyoelewa kwamba kama ilivyo mifumo ya maisha kila ambapo kunamafanikio hapakosi changamoto kwa hivyo baadhi ya changamoto ambazo kwa maoni yetu zikifanyiwa kazi mafanikio zaidi yatapatikana ni kama ifuatavyo
1.      Kuwepo kwa Uwakilishi wa wafanyakazi katika vyombo vilivyoundwa kwa mujibu wa sheria ya utumishi kama vile Kamisheni na Tume za Utumishi
2.      Vyombo vilivyoundwa kwa mujibu wa sheria za kazi na Utumishi wa umma vifanyekazi zake vilivyopangiwa kikamilifu  ikiwemo kukutana kama vile Bodi ya Ushauri ya mambo ya kazi, bodi ya mishahara, kamati za DHU  na OSH pamoja na Chombo cha Majadiliano cha Kitaifa
3.      Kuchukuliwa hatua kwa Waajiri wasilipa  mishahara kwa mujibu wa amri ya Serikali au kulipa kinyume na kima cha chini kilichoamriwa na serikali
4.      Kulipwa kwa Malimbikizo makubwa ya madeni ya haki za wafanyakazi ikiwemo tofauti za Mishahara ya mishahara na stahiki nyengine na wafanyakazi wa Serikali na taasisi za Serikali
5.      Kufanyiwa kazi Changamoto za marekebisho ya mishahara katika mashirikika ya umma na taasisi zinazojitegemea ambazo hadi sasa zinaendeleza manung’guniko kwa baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hizo
6.      Kurejeshwa kwa Kikokotoo cha mishahara ya Watumishi wa Umma kilichowekwa 2012 ambacho kiliondoa kabisa malalamiko ya wafanyakazi katika mishahara yao na kuweka uwazi katika malipo ya Mishahara
7.      Taasisi za serikali kuajiri kampuni za utowaji wa huduma (outsourcing) zenye uwezo , viwango na zenyekuzingatia sheria za kazi na za nchi katika haki na maslahi ya wafanyakazi
8.      Serikali za mitaa kuwa na watumishi wenye kujali taaluma za wafanyakazi zao kitaaluma (Walimu, madaktari) na kutoruhusu kuwepo wafanyakazi wengi wa muda  (part time ) kinyume na miongozo ya Serikali

Ndugu Viongozi, Wafanyakazi na Wananchi 
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Mei Mosi kwa mwaka huu ni kama ifuatavyo
“WAFANYAKAZI TUNAWAJIBU KUPAMBANA NA JANGA LA KORONA NA KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI MKUU KWA AMANI”

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) kwa niaba ya  wafanyakazi limeamua kuweka ujumbe huu kutokana na hali halisi iliyopo hapa nchini juu ya mripuko wa maradhi hatari ya CORONA ambayo hadi sasa imeonekana kwamba hayana Kinga wala dawa

Kwa upande wa wafanyakazi kupitia Shirika la kazi duniani linahesabu maradhi haya kama ni maradhi ya sehemu za kazi yaani “Occupational disease” kwa vile limeathiri zaidi wafanyakazi katika sehemu zao za kazi na athari  kubwa ya maradhi haya ni kwa ajira, uchumi na ustawi wa wafanyakakazi  na vipato vyao

Hivyo basi, ujumbe una lengo la kuwakumbusha wananchi hasa wafanyakazi kuchukuwa kila aina ya hatua kuhakikisha janga hili linaondoka nchini kwa kufuata maelekezo yote yanayotolewa na viongozi na wataalamu wa afya juu ya namna ya kujikinga na kuwakinga wenzetu makazini na majumbani juu ya janga hili kwa vile ni hatari kwa Ajira zetu, fursa za ajira za vijana wetu, kipato chetu, haki na maslahi yetu pamoja uchumi na ustawu wa taifa letu

Kwa upande mwengine Taifa letu mwaka huu linakabiliwa na Uchaguzi mkuu ambapo tukichukulia uzowefu wa siku zilizopita inapofika muda kama huu kunajitokeza baadhi ya Viongozi wa kisiasa, na kidini na wafuasi wao kupandikiza chuki na kushajiisha uvunjifu wa amani. Jambo ambalo huvuruga mifumo ya maisha ya wafanyakazi, kuathiri tija na kuzorotesha utowaji wa huduma

Kwa msingi huo na kwa kupitia ujumbe huu tunakusudia kuwakumbusha wananchi hasa wafanyakazi kwamba tunawajibika kikamilifu katika kuilinda amani ya nchi yetu kwa kupiga kura kwa amani, kwani huo ndio msingi wa utawala bora katika jamii. Kinyume chake tunaweza kuvuruga maendeleo mengi yaliyopatikana nchini kwetu kwa kufanya mzaha na amani

Ndugu Viongozi, Wafanyakazi na Wananchi 
Kwa kumalizia tumapenda kutoa maoni yetu katika siku hii muhimu kwetu kwa wadau kutokana na hali inavyoendelea katika sekta ya ajira nchini kwetu kama ifuatavyo:-

1.      Serikali
Tunaipongeza sana Serikali kwa namna ya hatua ilizochukuwa kupambana na janga la Corona hata hivyo tunaelewa kwamba sio rahisi kuhibiti ugonjwa huu ambao hauna kinga. Hata hivyo pamoja na hali iliyojitokeza tunaiomba Serikali yetu kuyafanyia kazi mambo yafuatayo :

a)       Kuendelea na jitihada  kutimiza ahadi za Mhe.Rais ya kuongezwa kwa Mishahara na mafao mengine inatekelezwa kabla ya kuondoka kwake madarakani yanafanyiwa kazi
b)       Kuendelea kuhakikisha watumishi wa afya, wanaotoa huduma kwa wagonjwa na waandishi wa habari ambao wapo katika mstari wa mbele kupambana na janga la  CORONA wanapatiwa kinga, motisha na bima ya maisha kutokana na mazingira wanayofanyia kazi
c)        Kuendelea kufanya udhibiti wa maeneo ambayo bado inaonekana hayajadhibitiwa ya uingiaji wa watu kutoka nje na kuwachukulia hatua bila ya muhali wanaokiuka taratibu zilizowekwa na Serikali
d)       Kuendelea kuhakikisha kwamba maeneo ya kazi ya umma yanawekewa hatua za tahadhari ikiwemo vifaa vya usafi,  vipima joto, uvaaji wa barkoa na kuondoa mkusajiko sehemu za huduma
e)       Kuendelea kuhakikisha kwamba waajiri wanapohitaji kufanya hatua zozote za kiajira kwa wafanyakazi ambao ajira zao zimeathirika na janga hili, ni lazima wapitie taratibu za kisheria ikiwemo majadiliano na mashauriano ya pamoja na wafanyakazi kwa mujibu wa Sheria katika hatua wanazochukuwa
f)          Serikali ifanye utafiti wa kiwango cha wafanyakazi walioathirika na janga hili kwa kupoteza kazi kupitia au kupunguwa kwa kipato chao ili iwasaidie kupitia mifumo ya hifadhi ya jamii
g)       Kwa vile janga hili kwa kiasi kikubwa linaathiri ajira na mazingira yake, Serikali ihakikishe inazishirikisha Jumuiya za ajira ikiwemo Vyama vya Wafanyakazi katika mapambano haya ikiwemo kamati za Kitaifa

2.      Waajiri

a)     Kuhakikisha kwamba maeneo yao ya  kazi yanawekewa hatua zote za  tahadhari ikiwemo vifaa vya usafi na  vipima joto ili kudhibiti maambukizi zaidi ya COVID-19
b)     Kuhakikisha watumishi wao wanapata huduma za dharura na sehemu za dharura endapo kutajitokeza wanaoshukiwa kuwa na dadili za maradhi yenye ishara zinazolingana na maradhi ya CORONA
c)      Kuhakikisha kwamba hakuna mfanyakazi atakaekosa haki yake na maslahi yake kwa kisingizio cha CORONA bali wafuate Sheria katika kuchukuwa hatua yoyote kwa wafanyakazi ikiwemo kuwasiliana na ofisi ya Kamishna wa kazi kabla hawajachukua hatua yoyote
d)     Kuhakikisha kwamba wafanyakazi wao wanajikinga na maradhi hayo kwa kuepuka mikusanyiko kazini na wanachukua hatua zote za tahadhari ya maradhi hayo

3.      Wananchi

a)     Kukubaliana na kufuata maagizo ya Serikali na wataalamu wa afya kuhusu  kujikinga sisi wenyewe na na familia zetu na janga hili
b)     Kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika kuhakikisha janga hilo linaondoka nchini iwe kwa kujitolea hali zao na mali zao kuongezea nguvu za serikali katika mapambano hayo
Ndugu Viongozi, Wafanyakazi na Wananchi 
Mwisho kabisa Kwa kumalizia tunapenda kutoa shukurani za dhati kwa uongozi wa Serikali kuu hususan Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uongozi wake ulio mwema ambao umeleta maendeleo mengi nchini na manufaa kwa wafanyakazi ,
Aidha tunawapongeza viongozi wa wizara ya kazi hususan Mhe. Waziri, katibu Mkuu na Kamishna wa Kazi kwa mashirikiano yao kwa Vyama vya Wafanyakazi. Kwa uzito huo huo tunawapongeza waajiri na wafanyakazi wote kwa ujumla kwa mashirikiano wanayotoa kwa wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi katika  kufanikisha shughuli zatu
Tunaomba tushirikiane kumuomba Mwenyezi Mungu atuondoshee janga hili ili tuweze kurudi katika mfumo wa maisha yetu ya kawaida huku tukichukua tahadhari zinazotolewa na Viongozi wa Serikali na wataalamu wa Afya juu ya kujuikinga sisi binafsi na kuwakinga wengine dhidi wa janga hili la CORONA

Kwa niaba ya Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar Nawashukuru sana kwa kunisikiliza

KWA MSHIKAMANO TUTASHINDA
SOLIDARITY FOR EVER -Mshikamano Daima


KOKA AIPATIA JUMUIYA YA WAZAZI KIBAHA MIZINGA YA NYUKI

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini, Slyvestry Koka, amekabidhi Mizinga kumi ya Nyuki Yenye Thamani ya Shilingi Milioni 1.5 kwa Umoja wa Wazazi(CCM) Kibaha Mjini kwa Ajili ya Mradi wa Ufugaji wa Nyuki.

Akizungumza Wakati wa Makabidhiano Hayo, katika Ofisi za CCM Kibaha Mjini, Jana, Mbunge Koka Aliipongeza Jumuiya Hiyo kwa Kupata Mwenyekiti Mwenye Maono Makubwa ya Kuiendeleza Jumuiya Hiyo kwa Kuitafutia Miradi Mbalimbali.

"Niwapongeze Jumuiya ya Wazazi Kibaha Mjini kwa Kupata Mwenyekiti Shunda Ambaye Anajitambua,Mbunifu na Mckarikaji katika Kutaka Kuacha Alama kwa Muda Aliopo Madarakani katika Utawala Wake;

Aidha Mbunge Koka, Alisema kwa Hamasa ya Maendeleo ya Jumuiya ya Wazazi Imempelekea Yeye Kama Mwakilishi katika Jimbo Hilo la Kibaha Mjini Kutoa Mizinga 10 Kwa Ajili ya Kuchagiza na Kutunisha Mradi wa Ufugaji wa Nyuki Ambao Baada ya Uvunaji wa Asali Utaipatia Jumuiya Hiyo Kipato.

Akizungumza Baada ya Kupokea Mizinga Hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya CCM, Edwin Shunda, Alimshukuru Mbunge Koka kwa Kuipatia Jumuiya Hiyo Mizinga 10 na Kusema Awali Walikuwa na Mizinga 30 kwa Kuongezewa Mizinga 10 Sasa Mizinga imefika 40.

"Kwa Niaba ya Jumuiya ya Wazazi Kibaha Mjini Tunamshukuru Mbunge Koka kwa Kutupatia Mizinga 10 ya Nyuki Tayari Tuna Mizinga 30 Ambayo Tumeshatundika Kwenye Shamba Letu na Hii 10 Jumla 40" Alisema Mwenyekiti Shunda.

Pia Mwenyekiti Shunda Alitumia Nafasi Hiyo Kuwashukuru Meneja wa Kanda wa Wakala wa Misitu Tanzania na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti wa Miti Dawa Kutoka Muhimbili kwa Kuipatia Jumuiya Hiyo ya Wazazi Shamba Ekari 5 na Maji kwa Ajili ya Ufugaji wa Mradi wa Nyuki Utakaozalisha Asali Baada ya Uvunaji na Kuiletea Fedha Jumuiya Hiyo.
 



Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...