Search This Blog

Wednesday, July 31, 2019

Unaambiwa Wema Sepetu Akiongeza Fyuzi Moja tu ya Shilole Kichwani Ametoboa


UKITAKA kujua nguvu ya Madam, Wema Sepetu weka bando lako la kutosha kwenye simu yako janja, chukua picha ya mrembo huyo aliyetwaa Taji la Miss Tanzania 2006 halafu sindikiza na ujumbe wa kumsema vibaya uone balaa lake! Wema anapendwa bwana na bahati nzuri yeye mwenyewe anajua kwamba ana nyota ya kupendwa. Mara kadhaa ameshazungumza hilo pindi anapopewa nafasi ya kufanya hivyo na vyombo vya habari. Kupendwa kwake na watu ni fursa tosha.

Ushawishi alionao anaweza kutangaza jambo lake, wanaompenda wakimuunga mkono kwake ni utajiri. Mathalan anaweza kuandaa tamasha kubwa na kuingiza mapato mengi kupitia kiingilio cha mlangoni. Ukimtazama Wema kwa umaarufu wake lazima ujiulize anakwama wapi? Jina kubwa analo, rasilimali watu kwa maana ya ‘koneksheni’ anazo za kutosha lakini kwa nini hatoboi? Hapo ndipo kwenye msingi wa hoja yangu kwamba kuna kitu kimoja tu (fyuzi) anatakiwa kuwa nacho si kingine bali ni ‘akili ya ushindi’.

Zuwena Mohamed ‘Shilole’ hajawahi kugusa anga za Wema kwa maana ya umaarufu tangu anaanza kuigiza hadi alipobadili gia na kufanya muziki wa Bongo Fleva. Jina lake linapaa juu lakini ni levo ile ya kawaida tu lakini kichwani mwake kuna akili ya ushindi.

Siku zote mtu mwenye akili ya kusaka ushindi huwa anaangalia njia za kupita. Shilole ameshajaribu mambo mengi sana katika maisha yake, alishawahi kufungua saluni baadaye akafungua duka la nguo hadi sasa ameingia kwenye biashara ya chakula. Kwenye biashara ya chakula kumemlipa. Kwenye biashara ya chakula amekusimamia vizuri na kumfanya azidi kuboresha  kutoka kwenye mgahawa mdogo hadi kuwa nao mkubwa. Ametumia uwanja wa mashabiki wake (Milioni 4.5) katika ukurasa wake wa Instagram kuwavuta wateja.

Hii ni akili ambayo Wema akijiongeza kidogo tu anatoboa maana ana wafausi Milioni 5.4, ni dhahiri kwamba akiwatumia vizuri wanaweza kumpa faida kubwa. Wabadilishe hao watu milioni 5.4 kuwa hela. Inawezekana kabisa hao watu kuwa utajiri mkubwa kwako.

Wema unapaswa kuwa na msimamo katika mambo anayoyafanya. Kutofanya vitu kwa muda kisha kuviacha. Kama una biashara, isimamie hadi ikupe matokeo. Usiwe mwepesi wa kukata tamaa na kuanzisha biashara mpya kila wakati.

Isimamie, ulifungua duka basi hakikisha kweli linafanikiwa. Usiishie njiani, ulishawahi kuzungumza kwamba una moyo wa kusaidia sana marafiki na mwisho wa siku wakakuangusha basi safari hii usiruhusu hilo litokee. Kuwa na akili sasa ya ushindi, wekeza! Fungua miradi na uisimamie kikamilifu. Jijenge sasa kimaisha, jenga nyumba na usiwe tena mtu wa kuishi kwa kupanga. Mtazame Shilole amefanikiwa hilo na sasa anaishi kwake, amedunduliza lakini ameweza wewe ushindwe kwa nini?

Tumia tu kidogo fyuzi ya ushindi ya Shilole. Kuwa mwanamke shupavu, mwenye kuthubutu na kusimamia kile unachokiamini. Usichezee fedha hovyo, wekeza na mwisho wa siku maisha kwako yatakuwa rahisi. Sisi mashabiki wako tunataka kuona ustaa wako unaendana na mafanikio yako, kila lakheri Madam!

GPL

Samatta Azidi Kuwa Lulu KRC GENK Thamani ya Kumpata Yapanda


INAELEZWA uongozi wa klabu ya KRC Genk umeamua kuongeza tena dau kwa timu zinazomtaka mshambuliaji wake, Mtanzania Mbwana Samatta kutoka shilingi bilioni 40 hadi kufukia shilingi bilioni 53. Mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita alifunga mabao 23, katika Ligi Kuu ya Ubelgiji, amekuwa akitakiwa na timu nyingi za England zikiwemo Leicester, Middlesbrough na Aston Villa lakini wapo Galatasaray ya Uturuki.


Taarifa za uhakika kutoka nchini Ubelgiji, Genk wameamua kuongeza dau tena kwa mshambuliaji huyo kwa lengo la kutaka kubaki naye baada ya Galatasaray kuongeza fedha tena kutoka bilioni 26 hadi kufikia bilioni 40.


Inadaiwa Genk wamekuwa wagumu kumuachia Samatta kwa kuwa wanamhitaji kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hali ambayo imekuwa ikiwapa ugumu Galatasaray kumalizana nao licha ya Leicester na Aston Villa kuendelea kusubiri mwishoni.


“Suala la Samatta kuondoka sasa limeanza kubadilika kutokana na ugumu ambao umeanza kujitokeza baada ya Genk kuamua kuongeza dau la mchezaji husika kutoka lile la awali ingawa Galatasaray wameamua kukomaa kufuatia kuongeza pesa yao na kufikia bilioni 40.

“Kikubwa kinachoonekana kwa Genk ni kwamba hawataki kumuachia kwa ajili ya michuano ya UEFA ndiyo maana wamekuwa wakipandisha dau kila wakati ingawa Galatasaray ndiyo wamebaki kwenye meza ya mazungumzo hadi sasa na hao wengine wanasubiri kama kutakuwa na mabadiliko yoyote,” kilisema chanzo


Kampeni iliyoanzishwa ya Jiondoe Vodacom Yamuibua Tundu Lissu Asusia Huduma zao


Wanasiasa pamoja na wadau wengine akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wameendesha kampeni maalumu ijulikanayo kama jiondoe Vodacom kwa kitendo cha kuvujisha mawasiliano ya wateja wao.

Kampeni hiyo ambayo wameitangaza katika mitandao ya kijamii ikiwa imelenga kuwepo na udhibiti wa mawasilino ya mteja bila kutolewa kwa taarifa zake.

Lissu kupitia akaunti yake ya Twitter amesema anasusia huduma za mtandao wa Vodacom na rasmi anaachana nao.

“Nimesusia huduma za mtandao wa Vodacom Tanzania na rasmi anaachana nao,” aliandika Lissu.






Vanessa Mdee Amu Unfollow Rafiki wa Jux Cyrill Kamikaze "Sipendi Mwanaume Mwenye Tabia za Kike"



Malkia wa Bongo Fleva kwa sasa, Vanessa Mdee ameonekana akimrushia maneno aliyekuwa shemeji yake wa zamani Cyrill Kamikaze.


Wawili hao kwa sasa wamekuwa hawana mawasiliano mazuri baada ya kuvunjika kwa penzi la Jux na Vanessa, ambapo hadi sasa kila mtu amemu-unfollow mwenzake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Vanessa Mdee amesema sababu za kumu-unfollow Cyrill Kamikaze kwenye mtandao huo ni kutokana na maneno ambayo aliyaandika katika moja ya post zake baada ya kuachana na Jux, ambayo hakuyapenda.

“Kuna kitu alipost alinikera, sipendi mwanaume ambaye anatabia za kike Kuna post na maneno alikuwa anazungumza sikuyapenda kwahiyo nikamu-unfollow”, amesema Vanessa.

Cyrill Kamikaze aliwahi kusema kwa sasa akiambiwa achague kati ya Vanessa Mdee na Mpenzi mpya wa Jux aitwaye Nnayika, atamchagua Nnayika kwa sababu rafiki yake ndio yupo nae kwa sasa na wala hawezi kumpinga Jux kwenye uamuzi wake.

Tundu Lissu "Mimi na Timu Yangu Tutatinga Mahakamani Kuu Wakati Wowote Tupo Tayari"


Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema yeye na timu yake wako tayari kutinga Mahakama Kuu muda wowote  kuanzia leo maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika.

Lissu aliyasema hayo kupitia akunti yake ya Twitter kuwa kesi za ubunge ni kesi za kisiasa. Ni kesi nyeti na zinahitajika umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha.

“Mimi na timu ya mawakili wangu tupo tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania. Tutafanya hivyo muda wowote kuanzia leo maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika,” aliandika Lissu.

Lissu alieleza kuwa atawajulisha mara moja kesi hiyo itakaposajiliwa rasmi.

“Kama itawapendeza nitawaomba mtakaopata nafasi kuhudhuria mahakamani kwa niaba yangu wakati wowote kesi hiyo itakapokuwa inaendelea,” alieleza Lissu.

 Kesi za ubunge ni kesi za kisiasa. Ni kesi nyeti na zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha.

Mimi na timu ya mawakili wangu tuko tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania. Tutafanya hivyo muda wowote kuanzia leo. Maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika.


Tundu Antiphas Lissu
@TunduALissu
Nitawajulisheni mara moja kesi hii itakaposajiliwa rasmi. Kama itawapendeza, nitawaomba mtakaopata nafasi kuhudhuria mahakamani, kwa niaba yangu, wakati wote kesi hiyo itakapokuwa inaendelea.

21
5:26 PM - Jul 31, 2019
Twitter Ads info and privacy
See Tundu Antiphas Lissu's other Tweets
AMEHITIMISHA KUTUMIA DAWA

Aidha, Lissu ameeleza kuhitimisha matumizi ya dawa alizoanza kutumia tangu Septemba 7 mwaka 2017 na sasa yupo tayari kurudi Tanzania September 7 mwaka huu.




TOUFIQ: Tanzania Kinara Katika Udahili Wa Wanafunzi Elimu Ya Awali Barani Afrika.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni kinara katika suala la udahili wa wanafunzi katika elimu ya awali barani Afrika na hivyo kuifanya kupiga kubwa katika utekelezaji wa maelengo ya maendeleo endelevu(SDGs).  

Mafanikio hayo yanatokana na serikali kutoa elimu bure bila malipo ambao umechangia kuongeza udahili wa watoto wengi kupata fursa ya kupata elimu. 

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Viti maalum FATUMA TOUFIQ ambaye ni pia champion wa masuala ya SDGs bungeni wakati akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari kuhusu mkutano aliohudhuriwa wa ‘High level political forum’ uliofanyika Umoja wa Mataifa(UN) hivi karibuni. 

Amesema katika mkutano huo waliwasilisha malengo 6 ya SDGs ambayo kwa ujumla wake Tanzania imefanya vizuri ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kutoa wito kwa serikali. 

TOUFIQ ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika linalojishughulisha na wanawake na watoto(Wowap), amesema katika mkutano huo alipelekwa kwa ufadhili kutoka Shirika la Equal Measure 2030 la nchini Marekani  linalojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo hayo ili kuhakikisha kunakuwa kuna usawa kwenye mambo mbalimbali ikiwemo elimu. 

Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya utoaji taarifa jinsi nchi ilivyofanya katika utekelezaji wa SDGs na Tanzania ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kutoa ripoti yake iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Dk.Philipo Mpango.


EU Watoa Neno Kifo cha Mtumishi Wizara ya Fedha



Umoja wa Ulaya (EU) umesema umeshtushwa na kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhandisi Leopold Lwajabe, ambaye mwili wake ulikutwa ukining'inia juu ya mwembe katika kijiji cha Mgoza Wilayani Mkuranga siku ya Julai 26, 2019.


''Tumesikitishwa na taarifa za kifo cha Lwajabe, ni mwenzetu, ni rafiki yetu mzuri, kifo chake kimetustua sana'', imesema taarifa ya EU.

Aidha taarifa hiyo imebainisha kuwa utendaji na kujitoa kwake katika kazi kwa miaka kadhaa ni wa kuthaminiwa na wako bega kwa bega katika kutoa ushirikiano wao kwa ndugu na Wizara ya Fedha katika kipindi hiki kigumu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya DSM leo Julai 31, imeeleza kuwa Lwajabe alijinyonga huku akiacha ujumbe wa wosia ofisini juu ya meza yake akitoa mgawanyo wa mali kwa ndugu zake ikiwemo mashamba, nyumba, gari, ng'ombe na viwanja.

Wosia mwingine aliouacha ni wa kuchinjiwa ng'ombe takribani wanne wakati wa maombolezo ya msiba wake.

Polisi Yamkana Maalim Seif, Zitto Kabwe Azungumza


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Thobias Sedeyoka amesema jeshi hilo halijavunja kongamano lililoandaliwa na kamati ya maridhiano Zanzibar na kuhudhuriwa na Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT - Wazalendo, Maalim Seif Sharrif Hamadi pamoja na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe.


Sedeyoka amesema kilichotokea ni kwamba askari wa doria walipita eneo hilo na kubaini mkusanyiko wa watu na kutaka warejee kwenye shughuli zao za kila siku inavyokuwa, na kwamba hawakumuondoa Maalim Seif kama ilivyokuwa ikiripotiwa.

Kwa upande wa Zitto Kabwe akizungumza mara baada ya kongamano hilo kuzuiliwa amesema, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Malindi alifika eneo la Kongamano na kutoa amri mbili ikiwemo ya kutaka kumkamata Maalim Seif ama kusimamisha kongamano.

"Hamna mtu ambaye anaweza kuthubutu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumchukua maalim kwa nguvu, tuna wanasheria kuna taratibu za namna za kumhitaji kiongozi mwenye hadhi ya Maalim hawezi tu kuja Mkuu wa Kituo cha Polisi Malindi na kutoa amri. Maalim ni mtu ambaye amekuwa sehemu ya viongozi katika nchi hii, amekuwa Waziri Kiongozi na Makamu wa kwanza wa Rais'', amesema Zitto.

Aidha Zitto amesema kuwa huenda polisi walikuwa na lengo la kuvuruga mkutano na kuzuia Wazanzibar kujadiliana juu ya neema zilizokuwepo wakati wa maridhiano.

Kutana na Mtaalam wa Tiba Omari Mbwana Kutoka Bagamoyo


Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Sharifu Omar mbwana ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)

Sharifu Omar mbwana ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dua Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)

Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio? Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo.. Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.

Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Sharifu Omar mbwana Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Sharifu Omar mbwana Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN , Nyota NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI..  HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu.. Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
Mawasilinae kwa simu no: +255 718-209773 WhatsApp no: +255 762-568247

Serikali yanunua magari 12 ya huduma ya dharura na uokozi


Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imenunua magari kumi na mbili kwa ajili ya huduma za dharura nchini.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ukaguzi kwenye ofisi za Toyota jijini Dar es Salaam.

Dkt. Ndugulile amesema magari hayo yameletwa muda muafa ikiwa zimesalia siku chache kuanza mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo magari hayo pamoja na mabasi mawili ya uokozi yatatumika kutoa huduma za kiafya kwenye mkutano huo na baada ya hapo yatagaiwa kwenye maeneo yaliyoanishwa kwa uokoaji wa majeruhi wa ajali.





Picha: Simba SC waliporejea nchini


Mabingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL), Simba SC wamerejea nchini wakitokea Afrika Kusini alipokuwa wameweka kambi. Kikosi hicho kipo kwenye maandalizi ya mchezo wao watakaocheza kwenye tamasha la Simba Day.



Kumbilamoto achaguliwa kuwa Meya Ilala


Diwani wa Vingunguti (CCM), Omary Kumbilamoto, amechaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala baada ya kumshinda mpinzani wake katika Greyson Selestin aliyepata kura 14.

Uchanguzi huo umefanyika Jumatano hii, katika kikao cha baraza la madiwani ambapo Kumbilamoto ameshinda kwa kura 41 kati ya kura 55 zilizopigwa ambapo hakuna kura iliyoharibika.

Akizungumza na waandishi baada ya uchaguzi huo, Kumbilamoto amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopata na kila mmoja aliyempigia kura ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuomba ushirikiano ili waweze kufanikisha majukumu ya Manisapaa hiyo.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu  kwa nafasi hii nilioipata na kufanikisha zoezi hili la uchanguzi kufanyika na kuisha salama, nawashukuru madiwani wote mlioweza kunipigia kura za kutosha na hata msionipigia lakini mmefanikisha haki zenu za kidemokrasia.

“Kikubwa niwaombe umoja na ushirikiano katika kufanikisha majukumu ya Manispaa ya Ilala inafanya kazi na miradi yote ya mikakati ya Mh. Rais Magufuli inatekeleza kwa wakati, nitakuwa Meya wakawaida wa kutekeleza majukumu yangu kwenu ”anasema Kumbilamoto

Makusanyo ya kodi kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/19


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya TZS 15.9 trilioni kati ya lengo la TZS 18 trilion kwa mwaka wa Fedha 2018/19 kuanzia tarehe 1 Julai 2018 hadi 30 Juni 2019.

Aidha katika robo ya nne ya mwaka huo wa fedha yaani, mwezi Machi hadi Juni 2019, TRA ilikusanya TZS 1.1 trilioni, TZS 1.2 trilioni, na TZS 1.5 trilioni kwa mwezi Aprili, Mei, na Juni, mtawalia. Kwa namna ya kipekee kabisa, TRA inawashukuru walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kwa ushirikiano.

Ikumbukwe kwamba, katika mwaka huo wa fedha, Serikali ilianzisha Mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) ambao utekelezaji wake umefanyika kwa awamu mbili (2). Awamu ya kwanza, ilihusisha bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia na aina zote za vileo. Awamu hii ya kwanza iliyoanza kutekelezwa tarehe 15 Januari 2019 imeendelea vizuri na maandalizi ya awamu ya pili ya utekelezaji wa ETS inayojumuisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi, na CD/DVDs yamekamilika.

Hivo mfumo huu wa ETS kwa awamu hii ya pili, unatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 1 Agosti, 2019.

Lengo kuu la kubandika stempu hizi za kielektroniki ni kuongeza usimamizi na ufanisi wa ukusanyaji wa Ushuru wa bidhaa ikiwa ni pamoja na kupata taarifa sahihi za uzalishaji viwandani ili kukusanya mapato stahiki.

Ni matumaini ya TRA kuwa, wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, wauzaji wote wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa pamoja, na umma kwa ujumla wataendelea kutoa ushirikiano kwa TRA ili kufanikisha utekelezaji wa mfumo huu kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Waziri Mkuu akagua maandalizi ya Terminal III


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua jengo la tatu la abiria kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere ili kuona maandilizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC.

Akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja na Kamati ya maandalizi uwanjani hapo Jumatano jioni, Waziri Mkuu amesema maandalizi ni mazuri isipokuwa kwa kasoro chache zilizobakia.

“Nimepita VIP hakuna shida. Pale terminal 2, sehemu ya Uhamiaji iko vizuri, uchunguzi wa afya nayo iko vizuri, lakini vyoo inabidi vibadilishwe haraka sana. Vile vyoo pale nje vimechoka, vibadilishwe mara moja, siyo tu kwa ajili ya ugeni, bali ni kwa faida yetu pia,” amesema huku akimwagiza meneja wa uwanja huo, Bw. Paul Lugasha aharakishe zoezi hilo.

Katika jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo, Waziri Mkuu amekagua eneo ambalo viongozi wakuu wa nchi watashukia, watakagua gwaride la heshima na kuangalia vikundi vya ngoma. Pia amekagua vyumba ambavyo watapumzikia kabla ya kuelekea mjini.

Amesisitiza kuwa usafi wa barabarani bado hauridhishi sababu kuna mawe, udongo na michanga kwenye barabara kuu ya kutoka uwanja wa ndege hadi mjini. “Tulikubaliana kuwa zile bustani ziboreshwe, vyuma vya barabarani vitengenezwe lakini hata leo nimepita kwenye fly-over, bado kuna mawe na michanga, hata sijui vinatokea wapi,” alisema.

Amewataka wahusika waweke banners za kutosha za aina mbalimbali na picha za wanyama kutani, uwanjani hapo ili kuonesha kwamba kuna mkutano mkubwa unafanyika hapa nchini.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka Watanzania watumie fursa ya uwepo wa mkutano huo mkubwa kuendesha biashara zao na ujasiriamali.

“Ziko fursa nyingi za uwepo wa mkutano huu. Kila mmoja atumie nafasi hii kuweza kuongeza na kuboresha kazi yake inayomletea uchumi,” amesema.

Waziri Lukuvi atatua migogoro ya ardhi Dar


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefanya ziara katika maeneo ya Kigogo na Msimbazi Center jijini Dar es Salaami na kurejesha kiwanja cha Bwa. Ramadhan Sudi Balega  kilicho tapeliwa na mtu ajulikanaye kama Bw. Macha  katika eneo la Kigogo.

Waziri Lukuvi amerejesha kiwanja hicho kutokana na mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka Kumi kutokana na kuwepo na utapeli katika eneo hilo huku akisisitiza kuendeleo kupambana na matapeli wa ardhi popote walipo kwani Wizara yake haitokubali wanyonge kudhurumiwa katika kipindi chake chote cha uongozi.

Lukuvi amerejesha Hati ya jengo lake na kuchukua uamuzi wa kutengua uteuzi wa msajiri wa Hati ambaye alifanya makosa ya kubadili hati kutoka kwa Ramadhan kwenda kwa Bw. Macha huku akijua kufanya hivyo ni kunyume cha utaratibu na swala hilo linatafsiriwa kuwa ni kitendo cha utapeli.

"Nataka kuwapa matumaini wananchi wote walioonewa, haki yako itachelewa tu lakini ipo siku utarudishiwa haki yako nataka kuwapa onyo watu wote ambao wanafikiri wanaweza kunyan’ganya haki ya masikini yoyote alafu Serikali isiwaone watambuwe kwamba serikali ipo macho na inashughurikia migogoro yote’’. Amesema Waziri Lukuvi.

Hata hivyo Waziri Lukuvi amewataka wananchi kutoa ushirikianao kwa kuripoti matapeli  na wadanganyifu wote waliyomo ndani ya Serikali ama nje ya Serikali ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao kama ilivyofanywa kwa msajili wa Hati aliyetenguliwa kutokana na vitendo vya kujihusisha na utapeli wa ardhi.

Kwa upande mwingine Waziri Lukuvi ametembelea eneo la msimbazi center lenye mgogoro wa muda mrefu kati ya kanisa katoliki na mmiliki wa kituo cha mafuta cha Victoria Bw. Harod Exavel ambapo eneo hilo limeonekana kuwepo na Hati mbili katika eneo moja hali hii inatokana na Kanisa kuwa na Hati iliyoipata tangu Mwaka 1965.

Hali hii inatokana watendaji wa Halmashauri ya Ilala kupitia moja ya vikao vyake  walifanya makosa na kumpa Hati Bw. Huweli ambapo Mwaka 2009, hivyo Bw. Huweli alimuuzia mmiliki wa Victoria eneo ambalo tayari Wizara  ilishalifuta hati hiyo.

Aidha Waziri Lukuvi amefafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria ni kosa kumilikisha Hati juu ya hati nyingine au mchoro wa upimaji juu ya mchoro mwingine na kama ikitokea kufanya hivyo ni lazima Yule mwenye hati ya awali arurudishiwe kwani kuna fomu maalumu ya Serikali ( Surrender form) inajazwa na ndipo utaweza kuingia kwenye ardhi yenye hati kuipima na kuipanga matumizi.

Hata hivyo Waziri Lukuvi amewataka kukutana na pande zote mbili kati ya Kanisa Katoliki na Mmiliki wa kituo cha mafuta cha Victoria siku ya Ijumaa Septemba 2, 2019 saa tano asubuhi ofisini kwake Ilala Jijini Dar es Salaam ili kujadili namna bora ya kuweza kuutatua mgogoro huo.

Mkandarasi aagizwa kuwasaidia usafiri wafanyakazi


Na. Amiri kilagalila, Njombe

Naibu waziri wa ujenzi Elias kwandikwa ametoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga bara bara kwa kiwango cha lami Lot2 kutoka Moronga-Makete,kuwawezesha wafanyakazi usafiri ili waweze kufika kwa wakati katika  maeneo yao ya kazi.

Waziri ametoa maelekezo hayo wakati akikagua maendeleo ya mradi mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa waendashaji wa mitambo katika mradi huo kutokana na kutumia gharama kubwa ili kufika sehemu ya kazi.

“Nimeelekeza hawa wakandarasi walitazame tuweke mazingira mazuri kwasababu magari yapo,waweze kuwasafirisha kwenye sehemu za kazi na mfanye kazi vizuri”alisema Kwandikwa

Hata hivyo naibu waziri huyo amewataka wafanyakazi katika maeneo hayo kutengeneza uongozi ili waweze kufikisha matatizo yao badala ya kusubiri viongozi.

“Tengenezeni uongozi wenu wenye busara sio nia ya kugombana ili kurahisisha mawasiliano na matajiri wenu kwasababu  kila mmoja akizungumza itakuwa ni kelele,hii itasaidia bahati nzuri viongozi wenu ni wasikivu na watawasikilizeni kama kuna jambo mnalisema bila ugomvi”aliongeza Kwandikwa

Awali waendeshaji wa mitambo ya utengenezaji wa bara bara hiyo walisema wanahitaji kusaidiwa usafiri wowote ili kufika maeneo yao ya kazi kwani kwao imekuwa ni changamoto kubwa.

“Sisi kwakweli tutashkuru tukipata usafiri kwasababu tunatoka mbali na tunahama hama  huku tukitumia nauli kubwa sisi tunahitaji hata lori sio mbaka basi,na mda mwingine hata wenzetu wasafirishaji wa abiria huwa tunawachomoa wakikwama ila sisi kwetu sisi kufika hapa bado ni shida”alisema mmoja wa waongozaji wa mashine

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Ignatio Mtawa anasema kukamilika kwa bara bara hiyo mapema kutafungua kwa kiasi kikubwa fulsa za kiuchumi.

"Tunaamini kwamba barabara hii ikikamilika basi wananchi wa Makete watanufaika sana kwasababu fulsa za kiuchumi zitafunguka na miundombinu awali ili kuwa ni kikwazo na ukizingatia tunamazao ya viazi,mbuga ya kitulo na hospital kubwa hapa kwa hiyo tutanufaika kwa kiasi kikubwa,” alisema Mtawa.

Bara bara ya Moronga-Makete yenye urefu wa km 53.5 inayojengwa kwa gaharama ya bilioni 110. 446 ikiwa ni pamoja na ongezeko la VAT inasimamiwa na Simak international kutoka Australia pamoja na kampuni ya Mac consart ingenearing and transport service ya Kitanzania kwa gharama ya mkataba wa usimamizi wa shilingi bilioni 2.68 ikiwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani huku ukitegemewa kukamilika kwa miezi 29

MAGAZETI YA LEO 1/8/2019
































Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...