Search This Blog
Wednesday, July 31, 2019
Kumbilamoto achaguliwa kuwa Meya Ilala
Diwani wa Vingunguti (CCM), Omary Kumbilamoto, amechaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala baada ya kumshinda mpinzani wake katika Greyson Selestin aliyepata kura 14.
Uchanguzi huo umefanyika Jumatano hii, katika kikao cha baraza la madiwani ambapo Kumbilamoto ameshinda kwa kura 41 kati ya kura 55 zilizopigwa ambapo hakuna kura iliyoharibika.
Akizungumza na waandishi baada ya uchaguzi huo, Kumbilamoto amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopata na kila mmoja aliyempigia kura ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuomba ushirikiano ili waweze kufanikisha majukumu ya Manisapaa hiyo.
“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu kwa nafasi hii nilioipata na kufanikisha zoezi hili la uchanguzi kufanyika na kuisha salama, nawashukuru madiwani wote mlioweza kunipigia kura za kutosha na hata msionipigia lakini mmefanikisha haki zenu za kidemokrasia.
“Kikubwa niwaombe umoja na ushirikiano katika kufanikisha majukumu ya Manispaa ya Ilala inafanya kazi na miradi yote ya mikakati ya Mh. Rais Magufuli inatekeleza kwa wakati, nitakuwa Meya wakawaida wa kutekeleza majukumu yangu kwenu ”anasema Kumbilamoto
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment