Habari njema. kutoka SUYUTI LINK TANZANIA tunatoa punguzo
la bei ya VIWANJA Vyetu kati ya VIWANJA 300 Vimebaki 100 TU.
Badala ya kulipia shs. 2,500,000 kwa AWAMU MBILI.
BASI USIWAZE utalipia shs. 2000,000 tu kwa AWAMU MBILI.
Awamu ya kwanza utalipia shs.1,000,000. baada ya hapo tutakupa Miezi miwili (2) KUMALIZIA NUSU ILIYOBAKIA.
mradi wetu upo VIKINDU mjini Mkoa wa PWANI/DAR ES SALAAM .
Mradi wetu upo kilometa moja (1) kutoka barabara kubwa(kilwa road).
HUDUMA ZA KIJAMII.
Huduma zote za kijamii zinapatikana kama vile.
1.Maji Tayari yapo ndani ya mradi wetu
2.Shule za serikalini na za binafsi(ibnu jazzary) zote zipo karibu na mradi wetu
3.Hospitali za serikali na za binafsi zipo karibu na mradi wetu
4.Umeme upo tayari ndani ya mradi ni kuwasha tu na kutumia.
5.Barabara zinapitika masaa 24 bila shida yoyo te
6.Sehemu za ibada zipo karibu na mradi.
7.Eneo lipo tambarare hakuna mabonde.
8.Viwanja vipo kwenye mpangilio mzuri,kwa mipango miji
UKUBWA WA VIWANJA.
1.Sqm 208(40futi & 50futi) bei yake 2,000,000/= Milioni MBILI tu (OKOA PUNGUZO LA LAKI TANO) , Hichi ni ukubwa wa kiwanja kimoja.
2.Sqm 416 (40futi & 100futi) bei yake 4,000,000/= Milioni nne (OKOA PUNGUZO LA MILIONI MOJA) , Hichi ni ukubwa viwanja viwili (2)
3.Sqm 832(80futi & 100futi) bei yake 8,000,000/= milioni nane (OKOA PUNGUZO LA MILIONI MBILI) . Hichi ni ukubwa wa Viwanja vinne(4).
HABARI NJEMA NI KWAMBA UNAWEZA KULIPA KWA AWAMU MBILI.
MAUZIANO.
Mauziano yote hufanyika ofisi za serikali ya mtaa/kijiji pamoja na kupata HATI ya mauziano ya AWALI kama utalipa CASH na kama utatoa Nusu Utapewa mkataba Yetu Tunayo Tayari. MTEJA wetu atachangia asalimia 5% na sisi 5% ya ushuru wa kijiji .
Habari njema Hakuna UDALALI kwenye biashara hii unanunua kwa wahusika .
Tunakitambulisha kichocheo madhubuti cha Nano kilichothibitishwa ubora wake na shirika la
viwango la kimataifa (ISO 9001:2015). Hii ni teknolojia ya kipekee na ya kimapinduzi kwenye tasnia ya magari na mitambo. kichocheo cha Nano kimetengenezwa na teknolojia ya kisasa duniani ya Nano (Nano technology) kwa ajili ya kuikarabati na kuipa ulinzi injini ya gari yako bila kuifungua. Kichocheo cha Nano huziba mikwaruzo yote ndani ya injini na kuirudisha nguvu ya injini kama ilivyokuwa mpya. Wasiliana nasi kupitia Namba 0715480174.
Kichocheo cha Nano kinaipa injini ganda au tabaka gumu la ceramic na platinum. Tabaka hili linafanya muunganiko wa kudumu na chuma cha injini (cylinder wall) na kina uwezo madhubuti wa kuhimili uchakavu na michubuko itokanayo na msuguano. Inarudisha uwezo wa kusukuma wa injini (compression ratio) kwa kuweka ganda gumu kwenye ukuta wa cylinder. FAIDA ZA KICHOCHEO CHA NANO.
Hupunguza matumizi ya mafuta kwa 8% - 21%.
Huongeza nguvu ya injini hadi kufikia 100%.
Hupunguza mlio na makelele ya injini na mtetemo hadi Mara 5 zaidi.
Inatoa ulinzi wa injini hadi kufikia 40000 km.
Husaidia Kuboresha uhai wa injini na vifaa vingine
.
Hulinda injini na kuirudisha kwenye ubora wake kama ilivyokuwa mpya.
Huongeza msukumo wa injini na kuboresha uunguaji wa mafuta.
Hulainisha usukani na gear box.
Hupatikana kwa magari ya aina zote, generator, compressor, pikipiki, bajaji na kila aina ya mtambo.
Hupunguza utoaji wa moshi kati ya mara 3 hadi 9.
Ina garantii ya utendaji kazi kwa 100%.
Haiharibiki kwa nanma yoyote ile.
Bidhaa bora kabisa iliyothibitishwa kimataifa na kitaifa.
Inakupa faida ya kutoifungua injini hivyo kuongeza thamani ya gari hata ukitaka kuiuza.
Inakupa faida ya kupata mafuta bure kila unapoweka kwa mara ya 9.
Faida isiyolinganishwa ya ulinzi wa gari lako hadi kufikia km 40000 kwa sh 60000 tu ukilinganisha na gharama za mafuta na services kwa kipindi hicho.
MATUMIZI
Injini inatakiwa iwe imetumika kwa km 3000.
Kichocheo cha Nano kinatumika kwa injini za aina yoyote inayotumia oili ya aina yoyote (mineral or synthetic oils).
Ili kupata matokeo bora zaidi weka unapofanya service.
Ipashe injini yako.
Tikisa kichocheo cha Nano kabla ya kuweka kwenye injini.
Fungua kifuniko cha injini oili halafu mimina kichocheo cha Nano.
Funga kifuniko. Hongera, umefanikiwa.
Baada ya kumimina kichocheo cha Nano usibadili oili ya injini mpaka kipindi cha matumizi yafuatayo (kilomita 400 kwa pikipiki na bajaji, kilomita 1200 - 1500 kwa magari madogo na kilomita 3000 kwa malori na mabasi).
MAPENDEKEZO.
Kichocheo cha Nano kimefanyiwa majaribio na kukubaliwa na taasisi zifuatazo.
Chuo kikuu cha Taifa cha Kyungpook - Korea.
Chuo Kikuu cha Taifa cha Seoul - Korea.
Taasisi ya Korea ya Mashine na Vifaa.
Chuo Kikuu cha Yeungnam - Korea.
Taasisi ya Korea ya Teknolojia ya magari.
Jeshi la ulinzi wa Taifa la Korea.
Kituo cha Jeshi la Anga la India.
UTHIBITISHO WA UBORA.
Kichocheo cha Nano kimefanyiwa majaribio maabara, kuthibitishwa, kukubalika na kutunukiwa vyeti vya ubora na taasisi zifuatazo.
Shirika la Ubora la Kimataifa ISO 9001:2015.
Shirika la viwango la Tanzania - TBS.
Mkemia mkuu wa serikali ya Tanzania - GCLA.
Maabara ya kimataifa ya SGS.
Maabara ya kimataifa ya TUV SUD Industrie Service GmbH.
USHUHUDA / MAPENDEKEZO.
Kichocheo cha Nano kimefanyiwa majaribio na makampuni ya kutengeneza magari, kimethibitishwa na kupendekezwa kutumika na makampuni yafuatayo.
MERCEDES BENZ
TOYOTA
GM DAEWOO
VOLVO
HONDA
HYUNDAI
AUDI
kichocheo cha Nano sasa kinapatikana Tanzania na kusambazwa na POWER ENERGY ENGINEERING COMPANY LTD. Tunakaribisha mawakala kutoka wilaya zote za Tanzania. Wasiliana nasi kupitia Namba 0715480174.
Kwa wafanyabiashara: usiikose fursa hii ya kibiashara.
Kwa wamiliki wa vyombo vya moto (Magari, pikipiki, bajaji nk): Tumia Kichocheo cha Nano kwa ulinzi madhubuti wa chombo chako.
WASAMBAZAJI WA NANO MIKOANI- TANZANIA DAR ES SALAAM
UBUNGO OIL COM Jengo la oil com juu kwenye bango la Bima 0715 480 174
RealMaps Mtaa wa sikukuu/mkunguni kariakoo 0755 366 658 0713 360 040
Dubai traders Livingston/mafia Kariakoo 0716 302 626
Luesha central Mtaa wa msimbazi/ mvita jingo la kisangani 0768 820 344
Japan auto spare parts Mwenge( karibu na Maryland bar) 0714 363 637
Bk japani auto spare parts Segerea stand karibu na Fantasy park 0653 519 653 0758 519 653
Darajani Geraji Darajani ubungo karibu na Land Mark Hotel 0765 447 803 0686 615 298
MOSHI KILIMANJARO
Mshiu 0714 229 079
MOROGORO
Jumbo Lubnzants Morogoro eneo la Fine Mazimbo Road 0715 003 738
Nuba auto Auto Accessories Mtaa wa Fine morogoro 0653 129 307
DODOMA
Temu auto parts Mtaa wa mji mpya chenja Dodoma 0754 265 211 0715 265 211
Nuba auto Accessories Eneo la CBE Dodoma 0653 746 907
MWANZA
GT. Sahara general supplies Pamba Road mwanza0754 560 284 0754 560284
Libety mkabala na Coconut Hotel mwanza 0626 450 450
GEITA
Kashakara auto spare parts Nyerere Road Geita
SHINYANGA
Green Star Expresses Stendi ya mikoani 0766 876 057 0759 933 290
Phanuel jeremia Machinjioni eneo la viwanda shinyanga 0755 042 505 0787 592 871
SINGIDA
Bingo spare Centre Standi ya zamani C Bomba la maji mkabala na Asma Hotel Singida 0755 961 679 0712 504 579
ZANZIBAR
Bengkok Accessories Kwa Biziredi mkabala na Bin Rashid Madawa 0779 959 850 0788 106 469
IRINGA
MAGELANGA – mtaa wa mahiwa, kibanda cha ccm no.6 stand kuu. 0684 025388
MAFINGA
LUMATO TELEPHONE SERVICES karibu na bank ya posta.
0753-105040/0655-105040
MAKAMBAKO
ALEX AUTO SPERE - mji mwema mkabala na stand mpya.
0769-252445 /0755-519246
NJOMBE
MANGULA AUTO PARTS -karibu na duka la Mama Widambe
0763-514771 / 0769-463911/0757-017321
MBEYA
KAPAGA -Mtaa wa Nyimbuko Kata ya Mwakibete
0789-889331/0754-306881
TUNDUMA
DUKANI KWA YUSTO ILOMO - Mtaa wa black kwa manyanya.
0753-353673/0653-188492
Kwa maelezo zaidi na kutaka uwakala katika wilaya na mikoa ya Tanzania piga simu no 0715480174 au Lira elites international Ltd no 0715 464310, waliopo ofisi za Acacia estates ghorofa ya kwanza plot no 84.
Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo amesema hana mpango wa kustaafu soka hivyo ataendelea kucheza kwa miaka mingi zaidi licha ya kukaribia umri wa miaka 36.
Ronaldo raia wa Ureno msimu wa 2020/21 ametupia kambani magoli 16 kwenye mechi 14 alizocheza katika mashindano yote, huku 12 akifunga kwenye ligi ya Serie A.
Ronaldo atakuwa na umri wa miaka 36 ifikapo mwezi Februari 2021 ana mkataba na timu ya Juventus hadi ifikapo mwaka 2021 na amesema anataka kusakata kabumbu hadi akitimiza umri wa miaka 40.
Vizuizi vimewekwa dhidi ya sherehe za mwaka mpya katika maeneo tofauti duniana wakati nchi nyingi zinajizatiti kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya coronaona.
Onyesho la fataki na mikusanyiko ya watu ilipigwa marufuku kuanzia Sydney hadi New York.
Sherehe pia zimezimwa hususan barani Ulaya baada ya aina mpya ya ugonjwa ambao maambukizi yake yanasambaa kwa kasi kugunduliwa
Ufaransa iliweka zaidi ya polisi 100,000 kushika doria katika barabara za mji mkuu mkesha wa mwaka mpya ili kuhakikisha amri ya kutotoka nje nyakati za usiku zinazingatiwa.
Zaidi ya watu milioni 1.8 wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona tangu janga hilo lilipoanza mwaka mmoja uliopita.
Nchini Ufaransa, serikali iliamuru uwepo wa usalama katika maeneo ya mijini kutoka 20:00 (19:00 GMT) Alhamisi, wakati amri ya kutotoka nje ilipoanza.
Katika mji wa Paris nusu ya usafiri wa metro ilifungwa.
Ufaransa ilikuwa imeweka amri ya kutotoka nje huku mabaa, migahawa na maeneo ya vivutio vya watu yakisalia kufungwa walipokaribisha mwaka mpya
Katika hotuba yake ya mwaka mpya, Rais Emmanuel Macron aliwaangazia wakosoaji wanaolalamikia kujikokota kwa mpango wa kutoa chanjo, na kuapa kushughulikia suala hilo katika "muda unaostahili".
Nchini Uingereza - ambako virusi vipya vya corona vinavyosambaa kwa kasi vimegunduliwa huku watu milioni 20 wakiathiriwa zaidi katika eneo hilo watu wamelazimika kusalia majumbani mwao - Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa wito wa watu kuzingatia masharti yaliyowekwa.
Barabara za mji wa London zilikuwa kimya mkesha wa mwaka mpya baada ya polisi kuomba watu washerehekee majumbani mwao.
Badala ya sherehe za kawaida zinazojumuisha mikusanyiko ya watu jijini London, onyesho la fataki lilifanywa katika maeneo tofauti jijini humo.
Ireland iliongeza vikwazo zaidi siku ya Alhamisi, kwa kupiga marufuku watu kutembeleana majumbani na kufunga maduka ambayo hayauzi bidhaa muhimu na kudhibiti usafiri wa hadi kilomita 5.
Ujerumani kwanza sasa imeweka amri ya kutotoka nje hadi Januari 10. Serikali imepiga marufuku uuzaji wa fataki na kuweka vikwazo vikali vya kudhibiti idadi ya watu wanaokusanyika pamoja.
Katika hotuba yake ya mwaka mpya inayotazamiwa kuwa ya mwisho kwake kama kansela wa Ujerumani, Angela Merkel aliwaangazia watu wanaopotosha umma kuhusiana na janga hilo.
Alisema anashangazwa na jinsi uwongo wa kijinga na wa kikatili unavyotumiwa bila kujali hisia za wale waliyopoteza wapendwa wao kutokana na ugonjwa wa corona
Nchini Italia, amri ya kutotoka nje iliwekwa saa 22:00 huku mabaa, migahawa na maduka mengi kufungwa. Huku hayo yakijiri Papa Francis hakuongoza ibada ya mwaka mpya mjini Rome badala ya kupata maumivu ya nyonga sugu.
Uholanzi pia iko nchini ya amri ya kutotoka nje ambayo itaendelea kudumishwa hadi Januari 19.
Uturuki imeanza kutekeleza amri ya kutotoka nje kwa siku nne
Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu wamelaani shambulizi lililoendeshwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Aden nchini Yemen na kulitambua kuwa "kosa baya la jinai."
Katika taarifa iliyotolewa na Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu, Katibu Mkuu Ali Muhyiddin al-Karadakh alisema, "Vitendo hivi ni dhambi na uhalifu kwa yeyote anayevifanya. Matukio haya yanastahili adhabu kali zaidi."
Akitoa wito wa kukomeshwa kwa vitendo vya kuhuzunisha na shida wanazopata wananchi wa Yemen, Karadakh alisisitiza kwamba kila mtu anapaswa kushiriki kutoa msaada wa maneno ya kibinadamu, kifedha, maadili na kisiasa ili kuiokoa Yemen kutokana na hali hii.
Wakati wajumbe wa baraza la mawaziri la serikali mpya ya Yemen walipowasili nchini hapo jana, milipuko 3 ilitokea katika kituo kimoja cha Uwanja wa ndege wa Aden.
Waziri wa Afya wa Yemen Kasim Buhaybeh alitoa maelezo kwenye akaunti yake ya Twitter na kutangaza kuwa watu 25 walipoteza maisha na wengine 110 walijeruhiwa kwenye milipuko hiyo iliyotokea katika uwanja wa ndege.
Waziri wa Habari na Utamaduni Muammar al-Iryani pia alitoa ujumbe kupitia akaunti yake ya Twitter na kusema, "Shambulizi hili la woga lililofanywa na wanamgambo wa Houthis wanaoungwa mkono na Iran kwenye Uwanja wa Ndege wa Aden halitatuzuia kutimiza wajibu wetu wa kitaifa."
Kwa upande mwingine, Mohammed al-Buhayti ambaye ni mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Houthis alisema, "Hatuna uhusiano wowote na shambulizi hilo."
Rais wa Iran Hassan Rouhani, amemfananisha Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa zamani wa Iraq aliyepinduliwa Saddam Hussein.
"Saddam alitupiga vita kwa miaka 8 na mwishowe aliangamizwa. Trump alituwekea vita vya miaka 3 vya kiuchumi, na atamaliza kuhudumu wiki chache zijazo. Atakumbukwa kama mtu asiye na heshima katika historia.’’
Rouhani, ambaye alishiriki katika hafla ya ufunguzi wa miradi kadhaa katika mkoa wa Magharibi ya Azerbaijan wa Iran kwa njia ya video, alifanya tathmini juu ya shambulizi la Marekani ambalo Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Qasim Soleimani aliuawa pamoja na sera ya Trump nchini humo.
Akisisitiza kwamba Trump amefanya mauaji mengi yasiyosahaulika kama vile ya Kamanda wa Kikosi cha Jerusalemu Soleimani na Rais wa Hashdi Shabi Mhandisi Abu Mahdi, ambayo yatalipiza kisasi, Rouhani alisema,
"Trump amefanya unyama mwingi. Mojawapo ya matendo yake yasiyosameheka ni mauaji ya Soleimani na Mhandisi. Hii imetuletea maumivu na uchungu ndani ya mioyo yetu. Watu wa eneo hilo na wananchi wa Iran watalipiza kisasi kwa wakati unaofaa. Adui hakika ataumia katika harakati hizi mbaya za mauaji ya kinyama. Watu wa Iran watachukua msimamo mkali katika hatua ya upinzani. Watu wote wameelewa kuwa maadamu Marekani iko katika eneo hili, hawatafikia malengo yao ya furaha zinazotarajiwa. Njia na mwelekeo wa Soleimani utaendelea."
Katika hotuba yake ya maelezo, Rouhani pia aligusia siasa za ndani ya nchi.
Akijibu kukosolewa kwa serikali ya ndani, Rouhani alisema,
"Wale wanaosema wanapingana na Marekani na kudhoofisha serikali wanadanganya. Serikali iko kwenye uwanja wa vita. Wale wanaodhoofisha serikali ni wafuasi na waliokuwa upande wa Marekani."
Hatimaye Uingereza imetamatisha kabisa uhusiano wake wa nusu karne na Umoja wa Ulaya kwa kujiondoa kutoka kwenye soko moja la Umoja huo na pia kwenye umoja wa forodha.
Uingereza sasa itafanya mambo yake kivyake, miaka minne baada ya kura yake iliyoishtua Ulaya ya kutaka kuondoka kwenye Umoja huo, Brexit.
Brexit ilitimia mara tu ilipogonga saa tano usiku kwa saa za Uingerezana saa sita usiku kwa nchi nyengine za Ulaya zilizokuwa zinaadhimisha mwaka mpya wa 2021. Waziri Mkuu Boris Johnson aliyeongoza kampeni ya nchi hiyo kujiondoa Umoja wa Ulaya, amesema hiki ni kipindi kizuri na akaendelea na usemi wake kwamba Uingereza itakuwa "Uingereza ya Dunia" ambayo haitotikiswa na sheria zinazotungwa katika makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels.
Kisheria Uingereza iliondoka kutoka kwenye Umoja wa Ulaya Januari 31 mwaka 2020 ila imekuwa katika kipindi cha mpito wakati wa mazungumzo ya kusaka makubaliano ya kibiashara na umoja huo ambayo yalipatikana mkesha wa Krismasi.
Na kwasasa kwa kuwa kipindi hicho cha mpito kimeshakwisha, sheria za Umoja wa Ulaya hazitumiki tena kwa Uingereza. Matokeo ya kwanza ya mchakato huo kukamilika ni kikomo cha usafiri huru wa watu milioni 500 kati ya Uingereza na nchi 27 za Umoja wa Ulaya.
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo kadhaa, ukaguzi wa forodha unarudi na licha ya makubaliano ya biashara huria yanayotoa nafasi kwa UIngereza kuendelea kufanya biashara na karibu wateja 450 wa Umoja wa Ulaya, kunatarajiwa milolongo mirefu na kutatizwa kwa huduma kutokana na stakabadhi zaidi zitakazohitajika.
Huko Calais, Ufaransa, maafisa wa Ufaransa walianza kutekeleza sheria hizo mpya saa sita usiku juu ya alama ambapo walianza kwa kulikagua trela moja lililokuwa linatokea Romania na lililokuwa limebeba barua.
Uingereza ndiyo mwanachama wa kwanza kuuhama Umoja wa Ulaya uliobuniwa kuleta umoja baada ya mabaya yaliyoshuhudiwa katika Vita vya Pili vya Dunia. Kura ya maoni ya mwaka 2016 ilileta mivutano mikali baina ya waliokuwa wanataka kubakia Umoja wa Ulaya na waliokuwa wanataka kuondoka na kusababisha miaka kadhaa ya kulemazwa kwa siasa nchini humo kabla Johnson kuchukua uongozi mwaka jana na kuapa kwamba ataifanya Uingereza iwe nchi yenye uvumbuzi wa kisayansi na ushirikiano na nchi mbalimbali.
Uingereza ni nchi yenye uwezo mkubwa wa kifedha na kidiplomasia na pia ni mwanachama mwenye nguvu kubwa katika muungano wa kujihami wa NATO na fauka ya hayo ni nchi iliyo na kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na pia katika nchi saba zilizostawi kiuchumi duniani G7.
Umoja wa Ulaya kwa sasa umpoteza watu milioni 66 na uchumi wa trilioni 2.85 na kuna majuto kwamba Uingereza ilitaka kujiondoa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema Uingereza itasalia kuwa "rafiki yetu" lakini akadai kwamba Brexit ni matunda ya mchakato uliokuwa na "hadaa na ahadi za uongo."
Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo kikamilifu shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili,homon,Neva,misuli,hisia na miriji ya damu
CHAZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
-kuwa na halemu (cholesterol) na shinikizo la damu( B,P,)au ugonjwa wa motorcycle
-ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
-kisukari,
-umri hasa wazee
-utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
-tabi za kujichua kwa mda mrefu ,kutopata usingizi
-ngiri,vidonda vya tumbo,
-tumbo kuunguruma na kukosa choo
-matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibu magonjwa Kama vile,kansa,vidonda vya tumbo,moyo,kisukari
DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
1kuwahi kufika kileleni,2kukosa hamu ya tendo 3kushindwa kurudia tendo la ndoa 4uume kusimama kwa uregevu au kushindwa kusimama 5 kuchoka Sana baada ya tendo la ndoa
TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME
Dawa ya MJN ni dawa ya asili isiyokuwa na mkemikali yoyote dawa hii ipo kwenye mfumo wa kunywa na kuchua pia dawa hii ni tamu Sana kwani imechanganywa na asari ni tofauti na ulizowahi kutumia usaidia ata wazee wenye miaka 80 pi uboresha uume wa mwanaume ulioingia ndani na kuwa mfupi
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE
1. kunywa maji mengi Sana Kila wakati
2. kwenda haja ndogo Mara kwa Mara
3. kuwa dhaifu ,kukosa nguvu na kijisikia mchovu kila wakati
4. kupunguza uzito au kukonda ata Kama unakula
5. kutoona vizuri
6. mwili kufa gazi hasa miguni
7. vidonda au majeraha sehemu ya mwili kutopona
8 kupungukiwa nguvu za kiume nk
MTN ndio dawa ya kisukari dawa hii inatibu tatizo mojakwamoja endipo ukidhingatia matumizi yake ni dawa isiyokuwa na masharti magumu kwa mtumiaji
Ndugu mteja epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahii kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO
WASILIANA NAMI TABIBU DITTU KWA SIMU 0714448999 AU Whatsapp +255714448999 ofisi ipo mbagara sabasaba walio nje ya mkoa utatumiwa sehemu yoyote ulipo
Karibu watu ishirini na sita wameuwawa baada ya miripuko katika uwanja wa ndege wa Aden huko Yemen muda mchache baada ya maafisa wa serikali mpya ya Yemen kuwasili nchini humo.
Duru za serikali na kimatibabu zimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa ingawa hakuna afisa yoyote wa serikali aliyeathirika zaidi ya watu hamsini wamejeruhiwa.
Kipindi moshi ulipokuwa unafuka kutoka uwanja huo wa ndege huku watu wakikimbia kuwanusuru waliojeruhiwa, kulisikika mripuko wa pili.
Ukanda wa video wa shirika la habari la AFP umeonyesha kile kilichoonekana kuwa kombora lililoulenga uwanja huo wa ndege.
Baadhi ya maafisa wamewalaumu waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran kwa shambulizi hilo.
Mwanachama wa Republican anasema kwamba atakuwa seneta wa kwanza kupinga wakati bunge la Congress litakapomuidhinisha rais mteule Joe Biden wiki ijayo.
Seneta wa Missouri Josh Hawley alisema kwamba alikuwa na wasiwasi wa maadili licha ya kutokuwa na ushahidi wa kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi uliopita.
Kundi moja la wanachama wa Republican katika bunge wawakiishi pia linapanga kupinga matokeo ya uchaguzi.
Lakini pingamizi hizo hazitarajiwa kubadilisha matokeo.
Baraza la wajumbe linaloidhinisha matokeo ya uchaguzi kwa kutoa pointi kwa kila jimbo lililoshindwa na wapinzani hao wawili mapema liliidhinisha ushindi wa rais mteule Joe Biden dhidi ya Trump kwa 306-232. Kura hiyo ni lazima zihakikiwe na bunge la Congress ifikiapo Januari 6 .
Siku ya kuapishwa kwa rais mteule na makamu wake itakuwa tarehe 20 Januari.
Tangu aliposhindwa katika uchaguzi, bwana Trump mara kadhaa amedai kwamba kulikuwa na udanganyifu wakati wa shughuli hiyo bila ya kutoa ushahidi.
Hatua za kisheria za rais huyo wa chama cha Republican kubadilisha matokeo zimekataliwa na mahakama.
Rais Recep Tayyip Erdoğan ameshauri majeshi ya Armenia yaliyokuwa yamevamia Nagorno-Karabakh, ambayo yana tabia ya kukiuka usitishaji vita, kuacha kufanya kosa kama hilo haraka iwezekanavyo.
Rais Erdogan, alihutubia vikosi vya pamoja vya Uturuki na Urusi vinavyotarajia kufanya kazi huko Karabakh.
HUtuba hiyo ilikuwa kwa njia ya simu.
"Uwepo huu una ishara ya heshima inayoonyesha mahali ambapo uhusiano kati ya nchi zetu umefikia." alisema Rais Erdoğan.
“Ninawatakia mafanikio wanajeshi wetu walioko kazini kusaidia usitishaji wa vita. Ninataka kituo kianzishwe kufanya kazi haraka iwezekanavyo. " aliongeza.
Akizungumzia mashambulizi ya maeneo ya Azerbaijan na vikosi vya Armenia, Erdoğan,
"Ninashauri wanajeshi wa Armenia, ambao wana tabia ya kukiuka usitishaji vita, waache tabia hii haraka iwezekanavyo."
Baada ya Waziri wa madini Dotto Biteko kutoa maagizo December, 17 2020 ya maneneja wa migodi kuwakagua wafanyakazi wao kabla yakutoka kwenye ukuta wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara,Wachimbaji wa madini maarufu kama wanaapolo wamekutana nakupeana mikakati ikiwemo kufuata utaratibu uliowekwa ili kukomesha utoroshaji wa madini.
Rose Njau katibu wa chama cha wachimbaji wa madini Mirerani amesema serikali inawatambua wachimbaji hao
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imeteketeza tani 52 za mchele ulioingizwa nchini na Mfanyabiashara Suleiman Abdalla mwezi Machi mwaka jana ukiwa umeshaharibika na haufai kwa matumizi ya binadamu.
Mchele huo ambao ulikuwa umo kwenye makontena mawili bandarini Malindi, ulitakiwa urejeshwe ulikonunuliwa ama uangamizwe kwa gharama za mfanyabiashara mwenyewe na alikubali kugharamia zoezi la kuuangamiza.
Mkurugenzi Idara za Huduma za Maabara wa Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar Nadir Khatib Hassan, ambae alisimamia uangamizaji huo katika jaa la Kibele, alisema uliingizwa nchini tarehe 15.3.2019 kutoka Pakistan.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, Fabian Manoza, ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani wenyeviti wa vitongoji 8, katika Kata ya Itinje wilayani humo, wanaodaiwa kula fedha za michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kata hiyo.
Mkurugenzi huyo ametoa amri ya kukamatwa kwa viongozi hao wa serikali za mitaa, kwenye ziara yake ya kukagua na kuhamasisha ujenzi wa vyumba vya madarasa, iliyoshirikisha kamati ya ulinzi na usalama pamoja na kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapo na kujionea kukwama kwa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kata ya Itinje.
"Hapa kuna mambo makubwa mawili ikiwemo ya hawa wenzetu waliokula hela zetu na hawataki kurejesha sisi tunachotaka ni majina yao wale ambao wanafedha zetu, OCD hawa tunaondoka nao itakapofika wakati wa kufungua shule wote waanze shule", amesema DED Manoza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Anthony Philip, amesema kuwa wiki ijayo halmashauri yake itatoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa sekondari hiyo.
Staa wa Tanzania aliyetangaza kuacha muziki Vanessa Mdee, amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Rotimi ambaye ni msanii wa filamu na mwanamuziki Rotimi ambao wanaishi wote kwa sasa nchini Marekani.
Kupitia 'videos clip' ambazo zimepostiwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha Rotimi akiwa amepiga magoti mbele ya Vanessa Mdee huku akimvalisha pete hiyo ya uchumba, kisha wakakumbatiana na kuanza ku-kiss.
Ikumbukwe tu mwanzoni mwa mwezi wa kumi mwaka 2020, Vanessa Mdee na Rotimi walishea picha mitandaoni zikiwaonyesha wamechorana 'tattoo' zenye majina yao kwenye miili yao.
Penzi la wawili hao lilianza Oktoba 2019, baada ya Vanessa Mdee kuachana na mkali wa RnB Bongo Juma Jux ambao walidumu kwa miaka 6.
Serikali imesema inatafuta namna ya kuwa na kituo kimoja cha kulipia tozo zote za mazao ya mifugo na uvuvi pamoja na kuondoa tozo ambazo zinakwamisha sekta hizo zisikue.
Akizungumza jana (30.12.2020) na baadhi ya wavuvi katika Kata ya Nyamikoma, iliyopo Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani humo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amesema wizara itaangalia tozo ambazo zitakuwa rafiki kwa wawekezaji, wafanyabiashara pamoja na wafugaji na wavuvi wa hali ya chini ili kuhakikisha sekta za mifugo na uvuvi zinachangia kwa sehemu kubwa pato la taifa.
“Tutaenda kuangalia ni tozo zipi na baadhi tayari mmeshazitaja zikiwemo za kusafirisha mazao ya mifugo na uvuvi nje ya nchi halafu tunatafuta namna ya kuwa na kituo kimoja cha kulipia hizi tozo zote.” Amesema Mhe. Ndaki
Waziri Ndaki ambaye amefuatana na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Pauline Gekul ameongeza kuwa uwepo wa tozo ambazo zitakuwa rafiki katika kukuza sekta za mifugo na uvuvi kutasababisha watu wengi kuwekeza katika sekta hizo na kuongeza pato la taifa kwa kuwa shughuli za kuchumi zitaongezeka.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul ameendelea kusisitiza kuwa watu wanaondelea kujihusisha na uvuvi haramu kuacha mara moja vitendo hivyo kwa kuwa wizara haitafumbia macho ambao bado hawataki kuacha kuharibu mazao ya uvuvi kupitia vitendo hivyo.
Amesema ni wakati sasa jamii kushirikiana na serikali kuwabaini watu wanaojihusisha na uvuvi haramu kwa kuwa wanaishi katika maeneo wanayofahamika ili serikali ichukue hatua na kwamba Wizara ya Mifugo na Uvuvi itazidi kutoa elimu juu ya athari ya uvuvi haramu kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Siku moja kabla ya kuanza ziara ya kikazi Mkoani Simiyu, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki wakati akihitimisha ziara ya siku mbili Mkoani Mwanza amefika katika Kijiji cha Kitongosima kilichopo Wilaya ya Magu mkoani humo na kuzungumza na jamii ya wavuvi na kuwasisitiza waanze kufuga samaki kupitia njia za vizimba na mabwawa ili kujiongezea kipato na kuongeza kuwa mahitaji ya soko la samaki kwa sasa ni makubwa.
Mhe. Ndaki amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah kuhakikisha anaanzisha utaratibu wa kuwepo kwa kizimba cha mafunzo kwa ajili ya kufugia samaki na kuhakikisha wataalamu kutoka wizarani wanafika katika kijiji hicho kuwafundisha wananchi namna ya kufuga na kulisha samaki ili jamii ya hapo iweze kupata mapato kupitia mazao ya uvuvi.
Waziri Ndaki amebainisha hayo baada ya kutembelea vizimba vya kufugia samaki katika kijiji hicho vinavyomilikiwa na Shamba la Konga na kufurahishwa na namna mwekezaji anavyofuga samaki kwa wingi kwa njia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria kwa kuwa ni sera ya serikali kuhakikisha katika kipindi cha miaka mitano ajira zaidi ya elfu arobaini na tano zinapatikana kupitia ufugaji wa samaki.
Katika kuhakikisha wananchi wa Kijiji cha Kitongosima wananufaika kupitia ufugaji wa samaki Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Bw. Lutengano Mwalwiba amewataka wanakijiji hao kujiunga katika ushirika ili halmashauri hiyo iweze kuwakopesha fedha kwa ajili ya shughuli za uvuvi huku Mwenyekiti wa Chama cha Wafuga Samaki Ziwa Victoria Bw. Cyprian Matembo amemuomba Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki kuangalia namna wizara inavyoweza kuwasaidia kupata vyakula vya samaki kwa bei nafuu kwa kuwa kwa sasa vyakula vingi vimekuwa vikiagizwa kutoka nje ya nchi na kuongeza gharama za uzalishaji.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki leo (31.12.2020) anahitimisha ziara ya kikazi katika mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa kwenye Mkoa wa Shinyanga, baada ya kufanya ziara kwenye mikoa ya Mwanza na Simiyu, akiambatana na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Pauline Gekul.
Wakulima kutoka Wilaya 25 zilizoko nchini wamepatiwa msaada wa mbegu tani 200 kutoka kampuni ya Bayer zitakazowasaidia kuongeza uzalishaji na kukuza vipato vyao .
Akizungumza katika uzinduzi wa Mpango wa “Mashamba Bora ,Maisha Bora” uliofanyika jijini Arusha ,Meneja wa Kampuni ya Bayer Nchini Tanzania, Frank Wenga alisema kuwa kwa kushirikiana na Tume ya Kilimo Tanzania (ACT) watasambaza takribani tani 200 kwa Wilaya 25 zilizoko nchini Tanzania mchango ambao una thamani ya shilingi bilioni 1.1
Meneja huyo amesema kuwa mpango huo umeshazinduliwa katika nchi za Kenya,Nigeria,Zambia,Malawi,Afrika Kusini na Msumbiji ambapo wakulima wadogo 700,000 barani Afrika watanufaika kati ya mwaka 2020 hadi 2022 huku nchini Tanzania Wakulima 100,000 watanufaika.
Akizindua Mpango huo na kukabidhi mbegu kwa wakulima wa Wilaya ya Meru ,Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara wa Mbegu Tanzania (TASTA) ,Bob Shuma amewataka Wakulima waliopokea mbegu hizo kuzitumia vizuri kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo ili waweze kupata mavuno mengi na kuwa mfano wa kuigwa kwa wengine.
“Tunashukuru serikali kwa kuweka miundombinu bora katika kilimo na vituo vya masoko ya mazao ili kuwasaidia wakulima ,kwa kushirikiana na sekta binafsi tunaweza kuinua kilimo na kuleta mabadiliko chanya” Alisema Bob
Mwakilishi wa Ofisi ya Kilimo Mkoa wa Arusha , Chisunga Jumanne amepongeza juhudi za kampuni ya Bayer katika kuwakumbuka wakulima na kuwarudishia sehemu ya faida wanayoipata kwa kuwapa msaada wa mbegu jambo ambalo linapaswa kuigwa na makampuni mengine.
Kwa upande wao Wakulima walipokea Mbegu hizo kutoka Wilaya ya Meru Ndetaiyo Nko na Anna Mbaga wameishukuru kampuni ya Bayer na kuahidi kutumia mbegu hizo kusaidia kuongeza uzalishaji katika kilimo hivyo kukuza vipato vyao.