Search This Blog

Tuesday, December 31, 2019

Wabunge waliovuma mwaka 2019

MWAKA 2019 umekwisha. Ulikuwa na mambo mengi katika medani za siasa kwa baadhi ya wabunge wa upinzani na chama tawala kujichanganya na ‘kuvuna walichopanda.’

Kwa upande wa chama tawala, wapo waliojichanganya kwa kushindwa kutumia vizuri ‘nyama ya ulimi,’ wakazungumza bila breki, lakini baadaye, wakatambua kosa lao; wakajitambua kuwa ni wana wapotevu; wakarudi nyumbani kwa baba na kuomba radhi. Uchungu wa mwana ajuaye mzazi; Rais John Magufuli akawasamehe. Hao, ni January Mamba, Nape Nnauye na William Ngeleja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa upande wa upinzani, uwajibikaji ukapungua kwa baadhi ya wabunge; wakashindwa kufanya kazi kwa mfumo rasmi na badala yake, wakataka kufanya kwa mazoea, bila kujali kwamba zama za kutenda kwa mazoea zimekwisha. Hao wakajikuta wanajivua ubunge bila kujua. Hao ni Joshua Nassari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

MAGUFULI ANAWASAMEHE WABUNGE WALIOMSEMA VIBAYA
Mwaka ulioisha wa 2019 umekuwa na mambo mengi ambapo kati ya mambo hayo ni pamoja na kuvuja kwa sauti za wanasiasa vijana wabunge wa CCM zilizoaminika kuwa ni za Nape (Mbunge wa Mtama), January Makamba (Mbunge wa Bumbuli) na William Ngeleja (Mbunge wa Sengerema). Sauti za wanasiasa hao wa CCM zikasikika zikitoa maneno ya kumkejeli Rais John Magufuli ambaye pia licha ya kuwa ni rais wa nchi, pia Mwenyekiti wa chama chao (CCM).

Sauti hizo zilisambaa katika mitandao ya kijamii. Hata hivyo, Septemba 4,2019 wakati Rais Magufuli akahutubia katika mkutano wa wataalamu wa ujenzi nchini, alisema wabunge Makamba na Ngeleja walimuomba msamaha na kuwa amewasamehe.

Akasisitiza: “Kuna umuhimu wa kusameheana hasa mtu anapokukosea na mimi nimewasamehe.” Rais ambaye ni mwenyekiti wa kitaifa wa CCM akasema: ‘Nilizisikia zile sauti na nikasema kuwa hivi hawa wakipelekwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM adhabu si itakuwa kubwa, lakini wawili walijitokeza na kuniomba msamaha ambao ni Makamba na Ngeleja, nimewasamehe.”

Kwa kurejewa na busara kama walivyofanya wenzake, siku kadhaa baadaye, Nnape naye aliwasili Ikulu –Magogoni na kumuomba radhi Rais Magufuli na kisha wote wamesamehewa na kuendelea na kazi zao kama kawaida katika majimbo.

WABUNGE WA CHADEMA ‘WAJIPOTEZEA’ UBUNGE
Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ‘anakitia kitumbua mchanga’; anapoteza ubunge wake. Kivipi? Machi 14, 2019, Spika wa Bunge, Job Ndugai alimwandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage kumjulisha kuwa Jimbo la Arumeru Mashariki lililokuwa likiongozwa na Nassari lipo wazi kutokana na mbunge huyo kupoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge.

Ndugai akasema Nassari amekosa sifa za kuendelea na ubunge wake kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya bunge ambayo ni Mkutano wa 12 wa Septemba 4- 14, 2018, Mkutano wa 13 wa Novemba 6- 16 2018 na Mkutano wa 14 wa Januari 29 mpaka Februari 9, 2019.

Kwamba uamuzi wa spika umezingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 71(1)(c). Ibara hiyo inasema: “Mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake cha ubunge ikiwa ataacha kuhudhuria vikao vya mikutano ya bunge mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya spika.”

Ibara hiyo tena imefafanuliwa pia katika kanuni ya 146(1) na (2) za kanuni za kamati ya kudumu za bunge toleo la Januari 2016. Kanuni hiyo inaeleza: “Kuhudhuria vikao vya bunge na kamati zake ni wajibu wa mbunge, mbunge yeyote atakayeshindwa kuhudhuria mikutano ya bunge mitatu mfululizo bila ruhusa ya spika iliyotolewa kwa maandishi atapoteza ubunge wake na spika ataitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi.”

Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ‘ilibariki’ kuvuliwa ubunge kwa Nassari. Jaji wa mahakama hiyo, Latifa Mansour alikubaliana na uamuzi wa Spika kuwa Nassari amepoteza sifa za kuwa mbunge kutokana na utoro.

Katika utetezi wake kabla ya kwenda mahakamani, Nassari alidai kuwa alikuwa nje ya nchi akimuuguza mkewe na kuwa, aliwasiliana na Ofisi ya Spika kwa kuongea kwa simu na msaidizi wake pamoja na kutuma ujumbe kupitia barua pepe. Baada ya wanachama wa vyama vingine kushindwa kukidhi vigezo, mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, Dk John Pallangyo alipita bila kupingwa na akaapishwa Mei 22, 2019 bungeni jijini Dodoma.

Tundu Lissu wa Singida Mashariki Sikio la kufa halisikii dawa. Ingawa wahenga walisema mwenzio akinyolewa, wewe tia maji, Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, hakujifunza kwa Nassari.

Ndiyo maana Juni 28, 2019, Spika Ndugai akatangaza kumvua ubunge Lissu. Alitoa sababu mbili kubwa kuwa ni pamoja na Lissu kutotoa taarifa rasmi ya maendeleo yake huku akionekana ‘huku na kule’ pamoja na kutokujaza fomu za maadili ya viongozi za Tume ya Maadili, hivyo kupoteza sifa za kuwa mbunge. Ndugai akaliambia Bunge: “Nimemwandikia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kuwa Kiti cha Ubunge wa Singida Mashariki ambacho Mbunge wake ni Tundu Lissu, kipo wazi.” Nafasi ya Lissu katika jimbo hilo imeshikwa na Miraji Mtaturu aliyeapishwa Septemba 3, 2019 bungeni, Dodoma.

WABUNGE WALIOPATA UWAZIRI
Mwaka 2019 ulikuwa mwaka mzuri kwa baadhi ya wabunge baada ya kuuteuliwa na Rais kuingia katika kada ya uwaziri akiwamo Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene aliyeteuliwa Julai 21, mwaka jana kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Muungano na Mazingira), badala ya January Makamba ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Simbachawene anarejea kwenye baraza la mawaziri baada ya kujiuzulu uwaziri wa Nishati na Madini Septemba 2017. Mwingine ni Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyeteuliwa na Rais Magufuli kushika wadhifa wa Naibu Waziri wa Kilimo. Nafasi hiyo ilikuwa ikikaliwa na Innocent Bashungwa aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Makala haya yameandaliwa na Evance Ng’ingo na Tuzo Mapunda.


Aiba Kichanga Anusurika kifo

Mama mmoja, mkazi wa Kitongoji cha Mwanzugi wilayani Igunga Mkoa wa Tabora aliyejifanya mjamzito, Shija Mihambo (32) amenusa kifo baada ya kupigwa na wananchi kwa tuhuma za wizi wa kichanga.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk Deus Rutha alisema, tukio hilo wiki iliyopita muda wa saa moja asubuhi kwenye wodi ya wajawazito.

Dk Rutha alisema, akiwa nyumbani kwake, alipigiwa simu na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Dk Merchades Magongo akimjulisha kuna wizi wa kichanga.

Alisema alikwenda hadi hospitalini hapo ambapo alikuta wananchi wengi, huku mtuhumiwa akiwa tayari amekamatwa na mganga mfawidhi kwa kushirikiana na wananchi.

Alisema mama huyo, alikamatiwa maeneo ya stendi kuu ya mabasi saa 1:48 asubuhi akiwa na kichanga hicho chenye uzito wa kilo 3.3 cha jinsi ya kike akiwa kwenye pikipiki aliyokodi kwenda Kitongoji cha Mwanzugi.

Dk Rutha alimtaja mama aliyeibiwa mtoto kuwa ni Hoka Maganga, mkazi wa Kijiji cha Bulenya Kata ya Nanga ambaye alifika hospitalini hapo Desemba 13, mwaka huu, saa 2 usiku akiwa mjamzito ambapo alilazwa na ilipofika saa 6:00 usiku kuamkia Desemva 14, alijifungua mtoto wa kike.

Alisema tayari mtoto amekabidhiwa kwa mama yake na afya yake inaendelea vizuri na mtuhumiwa alifikishwa kituo cha polisi kwa hatua zaidi akaongeza kuwa hilo ni tukio la pili ndani ya miezi mitano kutokea hospitalini hapo.

Alisema wamejipanga kuimarisha ulinzi kwa kila mtu anayeingia na kutoka hospitalini hapo.

Mmoja wa kina mama waliolazwa hospitalini na mwanae, Joyce John walisema mama huyo aliingia wodi ya wazazi saa 8:00 usiku akiwa amejivingirishia nguo tumboni ili kuonesha yeye ni mjamzito, huku akiwa na beseni ambapo wao waliamua kunyamaza.

Mama wa mtoto, alisema mama aliyemuibia mtoto alimuomba amwangalizie aende kujisaidia na aliporudi alikuta kaondoka na mwanawe ndipo akaanza kuomba msaada.

“Uaminifu umekwisha, nilimuachia mwanamke mwenzangu aniangalizie mwanangu ili niende kujisaidia, kumbe ni mwizi, namshukuru Mungu na uongozi wa hospitali ulioongozwa na mganga mfawidhi kwa kumkamata mwizi wa mwanangu,” alisema.

Mtuhumiwa huyo alikiri kuiba kichanga hicho na kusema alifanya hivyo siyo kwa nia mbaya, kwani angeenda kumtunza.

Ofisa Mtendaji Kata ya Igunga, Robert Mwagala alithibitisha kutokea tukio hilo na kusema polisi walifika hospitali kuwatuliza wananchi waliojaa hasira.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Barnabas Mwakalukwa alipotafutwa ili aweze kuzungumzia swala hili alisema upelelezi ukikamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.


Waandamanaji wa Iraq wavamia ubalozi wa Marekani

Waombolezaji nchini Iraq wamekusanyika nje ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad kulaani mashambulio ya ndege za Marekani yaliyolenga vituo vya wanamgambo wa Kishia.

Waombolezaji hao walizingira ubalozi huo uliopo kwenye eneo lenye ulinzi mkali wakiwa wamebeba bendera za kundi la wanamgambo lenye ushawishi mkubwa.

Wakati huo huo, Saudi Arabia imewalaani wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran kwa kuyashambulia majeshi ya Marekani yaliyoko nchini Iraq ambapo mkandarasi mmoja wa Marekani aliuliwa.

Wanamgambo hao walifanya mashambulio hayo wiki iliyopita. Marekani ilijibu kwa kuwashambulia kwa ndege wanamgambo hao wa Kataib Hezbollah Jumapili iliyopita.

Wanamgambo hao wa Hezbollah walikishambulia kituo cha kijeshi cha Marekani nchini Irak Ijumaa iliyopita.

Hata hivyo Waziri Mkuu wa Iraq, Adel Abdul Mahdi ameilaani pia Marekani kwa kufanya mashambilio ya ndege yaliyolenga vituo vya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran.

Amesema hatua ya Marekani inaweza kuitumbukiza zaidi Iraq katika vita vya kiwakala baina ya Marekani na Iran.


Kigwangalla afunguka Baada ya Magufuli Kumpa Siku 5

Baada ya Rais John Magufuli kuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda kumaliza tofauti zao vinginevyo atawaondoa, Kigwangalla ameibuka na kudai kuwa tayari walishamaliza tofauti zao na sasa hali ni shwari.

Kupitia akaunti yake ya Twitter na Instagram  amesema walishafanya kikao na Katibu Mkuu, Prof. Adolf Mkenda cha kumaliza tofauti zao.

“Kazi ya Urais ni ngumu sana, tulioteuliwa na Rais kumsaidia utendaji/usimamizi wa maeneo mbalimbali hatupaswi kumuongezea frustrations nyingine zaidi, sisi kwenye Wizara yetu, baada ya kikao na Chief Secretary tulimaliza tofauti zilizokuwepo na sasa hali ni shwari,” amesema Kigwangalla.

Ni imani na heshima kubwa sana kwako kuteuliwa kuwa Waziri kwenye nchi yako. Kwenye nchi ya watu milioni 60, kwa nini Hamisi KIGWANGALLA? Sijui. Ni neema na baraka za Mungu tu. Maana siyo kila mtu kwenye maisha yake atapata fursa ya kuhudumu kwenye serikali kama Waziri ama kama Katibu Mkuu kwenye serikali. Siibezi wala siwezi kuichezea fursa hii adhimu.

Ni kwa kuelewa ukweli huu na ushauri, mwongozo na maelekezo ya wakuu wa kazi, na watendaji wazoefu kwenye utumishi wa umma, kama Katibu Mkuu Kiongozi, tulikaa mimi na Katibu Mkuu wangu na kukubaliana kufungua ukurasa mpya wa mahusiano mazuri zaidi kwa manufaa ya nchi yetu.

Kuondolewa kwenye nafasi ya Uwaziri unaweza kuondolewa kwa sababu mbalimbali lakini kuondolewa kwa sababu watu wazima, tena viongozi, ambao mmepewa fursa ya kushauriwa, mmeshindwa kuelewana, ni upumbavu! Mimi siyo mpumbavu.

Kuleta kiburi na jeuri kwenye mazingira Haya ni upumbavu. Kwanza sisi waislam tunafundishwa kuwa wanyenyekevu, maana ‘kiburi’ ni sifa ya Mungu, siyo yetu wanadamu. Kufanya kiburi na jeuri ni upumbavu. Hekima ya Mungu ni kujishusha na kumshinda shetani.

Sina jeuri wala kiburi sababu nimelelewa vizuri na bibi yangu Mama Bagaile, na pia naogopa hasira za Mungu. Tumalizie haya masaa kwa amani! Happy New Year Good People. Nitaendelea kutoa darasa la mambo niliyojifunza 2019, na mipango yangu ya 2020.

Nipo jimboni nachunga ng’ombe wangu kidogo. Ningekuwa Dar ningemtembelea Prof. Mkenda kwa ajili ya picha tukigonga glass ili mjue tuko sawa . Mhe. Rais yeye ana namna yake ya kupata taarifa zetu. Atazipata tu! . Limeisha hilo au niongeze volume? Wakatabahu Dkt. Hamisi KIGWANGALLA, MB., MNEC, WMU.


Magufuli AMPIGIA Simu Diamond Platnumz Katikati ya SHOW Kigoma Asema "Wewe ni Mwanaume"


MAGUFULI AMPIGIA SIMU DIAMOND KATIKATI YA SHOW KIGOMA ASEMA "WEWE NI BABA LAO"

FAHAMU: Usiku wa jana msanii wa muziki Diamond Platnumz alikuwa akitumbuiza katika kusherekea miaka 10 katika muziki wa Bongo Fleva. Wakati akiwa jukwaani alipigiwa simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt John Pombe Magufuli kisha kupongezwa kwa jitihada zake anazofanya katika sanaa na Taifa kwa ujumla. Nimekusogezea video hii itazame kisha nipe maoni yako

VIDEO:



Faida ya Kunywa Chai ya Tangawizi


Tangawizi ni moja ya kiungo ambacho husaidia kuleta ladha na harufu nzuri kwenye chai.

Miongoni mwa faida za kutumia tangawizi ni pamoja na kusaidia mfumo wa ummeng’enyaji wa chakula tumboni.

Tangawizi pia husaidia sana kwa wale wenye matatizo ya kuhisi maumivu mara kwa mara kwenye viungo, hivyo matumizi ya chai yenye tangawizi huwa na nafasi kubwa ya kutoa ahueni kwa wenye tatizo hilo.

Pia tangawizi husaidia sana kwa wale wenye kusumbuliwa na mafua, unapotumia chai yenye tangawizi husaidia kupunguza uwezekano wa tatizo hilo.

Kwa wale kinamama ambao husumbuliwa na kichefuchefu wakati wa kipindi cha ujauzito, tangawizi ina nafasi kubwa ya kuondosha hali ya kichefuchefu, hivyo si lazima kutumia ndimu katika kuondosha hali hiyo.

Pamoja na hayo, tangawizi pia hutumika kwa kutuliza maumivu ya tumbo yanayochangiwa na matatizo ya usagaji wa chakula, halikadhalika tangawizi husaidia sana kuongeza hamu ya kula.

Rais Magufuli Kuwatengua Waziri Kingwangalla na Katibu Wake Endapo Hawatamaliza Tofauti zao


Rais Magufuli amewapa siku 5 za kutekeleza agizo hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Adolf Mkenda

Rais Magufuli amesema kama watashindwa kufanya hivyo atatengua teuzi zao

Akiwa katika Hifadhi ya Rubondo amesema, Katibu Mkuu hataki kumheshimu Waziri na Waziri hataki kwenda pamoja na Katibu Mkuu. Rais Magufuli amesema anawatazama taratibu

Ameongeza kuwa, hawezi kuwa na watendaji aliowateua yeye halafu kila siku wanagombana na mambo ndani ya Wizara hayaendi
18h

Mtandao wa SIMU wa MTN Washutumiwa Kufadhili Magaidi


Shutuma hizo zilizotolewa katika Mahakama ya nchini Marekani siku ya Ijumaa zinadai Mtandao huo mkubwa wa simu Afrika unafadhili kwa kutoa fedha kwa Makundi ya Kigaidi Nchini Afghanistan

Katika shutuma hizo ambapo Kampuni nyingine tano zimehusishwa inadaiwa kuwa MTN ilivunja sheria ya kukabiliana na ugaidi ya Marekani

MTN inadaiwa kutoa rushwa kwa Al-Qaeda na Taliban ili wasiweze kuwekeza pesa nyingi kwa ajili ya kulinda mitambo yao nchini humo ambapo fedha hizo zinadaiwa kutumika kwenye mashambulio kati ya mwaka 2009 hadi 2017

Pia, inasemekana fedha hizo zilizotolewa na mtandao huo wa mawasiliano unaoshika nafasi ya 8 kwa duniani kote, ukiwa na Watumiaji zaidi ya milioni 240, zimetumika kununua silaha hivyo kuvunja sheria ya kupambana na ugaidi

Mwaka 2015, Kampuni hiyo ililipishwa fidia ya Dola Bilioni 5 na Serikali ya Nigeria baada ya kushindwa kudhibiti laini za simu ambazo hazikusajiliwa, ambapo fidia hiyo baadaye ilipunguzwa hadi kufikia Dola Bilioni 1.7

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu


Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dua Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.

Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN   Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA.  

Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...


Trump apandwa na hasira Baada Ya Waandamanaji Kuuvamia ubalozi wa Marekani nchini Iraq na Kutaka Kuuchoma Moto

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema anatarajia Iraq itatumia vikosi vyake vya usalama kuulinda ubalozi wa Marekani mjini Baghdad.

Kauli hiyo ameitoa wakati ambapo anailaumu Iran kwa kuchochea vurugu hizo dhidi ya eneo lake. 

Wananchi wa Iraq ambao ni wafuasi wa wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran waliandamana kwenye ubalozi wa Marekani siku ya Jumanne huku wakiimba nyimbo zinazosema ''Kifo cha Marekani,'' wakirusha mawe, wakivunja kamera za usalama pamoja na kulichoma moto eneo la mapokezi, wakilaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani.

Mashambulizi hayo yaliyofanyika Jumapili iliyopita yaliwaua wapiganaji wapatao 25 wa kundi la wanamgambo wa Kataeb Hezbollah. 

''Tunatarajia Iraq itavitumia vikosi vyake kuulinda ubalozi na tumearifiwa hivyo,'' ameandika Trump katika ukurasa wake wa Twitter. Trump amesema Iran itawajibika kikamilifu kwa machafuko hayo.

Mashambulizi ya Marekani yalikuwa ni kujibu shambulizi la roketi lililofanywa wiki iliyopita na kumuua mkandarasi mmoja wa Kimarekani katika kituo cha jeshi la Iraq, ambalo ni la karibuni kufnayika lililenga maslahi ya Marekani nchini Iraq. 

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini vikosi vya usalama vya Marekani vimelishutumu kundi la Kataeb Hezbollah.
 
Trump amesema Marekani imejibu vikali shambulizi ambalo limemuua mkandarasi huyo na skwamba siku zote itafanya hivyo. 

Uhusiano kati ya Marekani na Iran umekuwa ukizorota tangu Marekani ilivyojiondoa kwenye mkataba wa kihistoria wa nyuklia wa Iran mwaka 2018 na kuweka vikwazo vipya.

Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kadhaa kwa waandamanaji kufanikiwa kuufikia ubalozi wa Marekani mjini Baghdad, uliopo kwenye eneo lenye ulinzi mkali maarufu kama Green Zone. 

Vikosi vya usalama ndani ya ubalozi huo walifyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji nje ya ubalozi huo. Imeripotiwa kuwa zaidi ya watu 20,000 walikusanyika nje ya ubalozi huo.


Waandamanaji wa Iraq wavamia ubalozi wa Marekani mjini Baghdad

Waombolezaji nchini Iraq wamekusanyika nje ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad kulaani mashambulio ya ndege za Marekani yaliyolenga vituo vya wanamgambo wa Kishia.

Waombolezaji hao walizingira ubalozi huo uliopo kwenye eneo lenye ulinzi mkali wakiwa wamebeba bendera za kundi la wanamgambo lenye ushawishi mkubwa.

Wakati huo huo, Saudi Arabia imewalaani wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran kwa kuyashambulia majeshi ya Marekani yaliyoko nchini Iraq ambapo mkandarasi mmoja wa Marekani aliuliwa.

Wanamgambo hao walifanya mashambulio hayo wiki iliyopita. Marekani ilijibu kwa kuwashambulia kwa ndege wanamgambo hao wa Kataib Hezbollah Jumapili iliyopita. 


Wanamgambo hao wa Hezbollah walikishambulia kituo cha kijeshi cha Marekani nchini Irak Ijumaa iliyopita.

Hata hivyo Waziri Mkuu wa Iraq, Adel Abdul Mahdi ameilaani pia Marekani kwa kufanya mashambilio ya ndege yaliyolenga vituo vya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran. 


Amesema hatua ya Marekani inaweza kuitumbukiza zaidi Iraq katika vita vya kiwakala baina ya Marekani na Iran.


Rais Magufuli awatakia Watanzania heri ya mwaka Mpya 2020

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia Watanzania wote heri ya Mwaka mpya wa 2020 na kuwaomba waendelee kudumisha amani na upendo ili uwe mwaka wa maendeleo na ustawi kwa Taifa.

Mhe. Rais Magufuli ametoa salamu hizo jana  wakati akiagana na Maafisa na Askari Wanyamapori na Hifadhi ya Misitu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ambako alitembelea na kujionea vivutio vya utalii pamoja na wananchi wa Nyabugera na Muganza aliowasalimu wakati akiwa njiani kurejea nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amepokea salamu za heri ya Mwaka Mpya wa 2020 kutoka kwa wananchi, viongozi mbalimbali wakiwemo Marais Wastaafu, Maaskofu na Masheikh ambao wamempongeza kwa kazi nzuri ya kuongoza nchi kwa mafanikio makubwa na wamemuelezea matarajio yao ya kufanikiwa zaidi katika mwaka ujao.

“Mhe. Rais wangu, Dkt. Magufuli, Bwana Yesu Asifiwe. Ninakupa hongera sana kwa wajibu mzito ulionao. Kwa neema ya Mungu tumejaaliwa kufikia siku ya mwisho kwa mwaka huu wa 2019. Mimi nakupongeza kwa jitihada zako nyingi za kuleta maendeleo kwa nchi yetu. Ninakuombea na kukutakia Mwaka Mpya 2020 wa heri na mafanikio makubwa. Uso wa Bwana uende nawe popote utakapokuwa” amesema Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Frederick Shoo.

Kabla ya kuondoka katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi, Maafisa na Askari wote wa hifadhi hiyo kwa mapokezi mazuri na juhudi kubwa zilizowezesha hifadhi hiyo kuvutia na amewahakikishia kuwa pamoja na kutoa shilingi Bilioni 2 za ujenzi wa kivuko cha kwenda hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo, Serikali itatoa shilingi Milioni 200 za kuboresha barabara za hifadhi hiyo.

Baada ya kuvuka ziwa Victoria kwa kivuko cha MV Chato, Mhe. Rais Magufuli amekutana na wananchi wa Kasenda na kuelezea kutoridhishwa kwake na ukusanyaji wa mapato ya soko la dagaa na samaki la Kasenda baada ya kuelezwa kuwa makusanyo ya mapato ya soko hilo ni shilingi laki 5 kwa siku licha kuwa soko kubwa namba 2 kwa kuuza dagaa katika ukanda wa Ziwa Victoria.

Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Chato, kufuatilia ukusanyaji wa mapato katika soko hili na kuchukua hatua za kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato itakayobainika ili Halmashauri ya Wilaya ya Chato iweze kupata fedha zitakazosaidia kutatua kero za wananchi ikiwemo kuboresha mazingira ya soko hilo na ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyabugera ambayo amechangia shilingi Milioni 5.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Bw. Eliud Mwaiteleke kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya Kasenda - Muganza yenye urefu wa kilometa 2.2 ili ijengwe kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi, na kwamba Serikali itatoa fedha za ujenzi wa barabara hiyo.

Mhe. Rais Magufuli pia amewasalimu wananchi wa Muganza, ambapo amewapongeza kwa maendeleo yaliyopatikana katika eneo hilo na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma ili iendelee kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi.

“Nchi hii ilikuwa inaliwa sana na majizi na mpaka sasa bado wapo, namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kunipa uhai ili katika mwaka 2020 niendelee kuwatumbua majizi wote na fedha tutakazopata tuzipeleke kwenye miradi ya maendeleo kama ambavyo tumenunua ndege 11, tunajenga reli (standard gauge), tunatoa elimu bure na mengine mengi” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli pia amemuonya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Bw. Eliud Mwaiteleke kwa matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na halmashauri hiyo na ametaka dosari hizo zirekebishwe mara moja. “Nataka ujirekebishe, wananchi hawa wanateseka sana” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato


Nabii TITO Ageuza Kibao "Kwasasa Dini Yangu ni CCM"


"Ukitii amri za Serikali ni sawa na kutii amri za Mungu, naamini Mungu anaishi Ikulu Mimi Dini yangu ni CCM kanisa langu ni Serikali na Mungu wangu ni Raisi, CCM ni tunda la uzima imeandikwa ufunuo 22:2"-Nabii Titto.

Toa maoni yako kisha Share

Wakili Jebra Kambole Afunguka "Tayari Tumempa Taarifa za Msiba Erick Kabendera Gerezani"



Wakili Jebra Kambole  amesema tayari wamempa taarifa ya msiba wa Mama yake Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera ambae yupo Gerezani.

Wakili Kambole ambae anamtetea Kabendera kwenye kesi ya utakatishaji fedha iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu amesema wanafanya utaratibu kuona kama atashiriki maziko "kuna Logistic za kufanya ili Kabendera aweze kushiriki msiba ila tunazungumza na Ndugu tuone wanasemaje"

"Kabendera amezipokea kwa masikitiko sana taarifa hizi sababu Marehemu ni Mtu ambaye alikuwa anamtegemea, amewashukuru Watanzania kwa mchango na pole wanazompatia" - Wakili Jebra Kambole


Binti wa Advaced Level Ananikosesha RAHA Ndani ya Ndoa Yangu


Wajumbe mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 33 Ni Mwajiriwa wa Serikali, nimeoa na nina mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 3.
Licha ya kwamba niko kwenye ndoa, lakini ilitokea siku moja asubuhi nikiwa barabarani na gari langu nikitokea nyumbani kwangu Mitaa ya Kihonda Magorofani nikielekea kazini Morogoro mjini.Nilikutana na Mwanafunzi kavaa sare za shule na alikuwa akielekea shuleni nae.Nilisimamisha gari na kumuuliza kama anaenda shuleni maana baada ya kuona sare alizovaa niliweza kutambua ni shule gani anasoma.Baada ya kumuuliza kama anaenda shule aliitikia kwamba anaenda shuleni, nilitoa Lock ya Milango ya gari nikamwambia apande nimsogeze kidogo.

Cha kushangaza niliona akifungua mlango wa mbele na kuingia maana nilikuwa peke yangu.Niliondoa gari tayari kuendelea na safari,tukiwa njiani niliweza kumuuliza jina lake, wazazi wake kadharika tulipeana hadi namba za simu.

Baada ya siku mbili alinitumia msg iliyosomeka hivi."Shikamoo, Habari ya kazi?Nimeona sio vizuri kukaa kimya wakati juzi ulinisaidia nikawahi shuleni.Jioni Njema na karibu nyumbani." Bahati mbaya hiyo msg sikuweza kuijibu maana nilikuwa niko na wife na zaidi niliifuta baada ya kuisoma.Baadae nilitafuta nafasi nikampigia kumjulisha msg yake nimeipata akadai amefurahi sana kusikia sauti yangu.Na mimi kama mwanaume nikamuomba atafute muda japo siku moja tukutane tena tuongee.Alikubali na kuniahidi nimtafute siku za Ijumaa jioni, Juma mosi na jumapili maana hizo siku anakuwa free.

Ilipofika Ijumaa nilimtafuta tukaenda Hotel moja nje kidogo ya Mji tukaongea sana na ikafikia hata mimi nikamwambia namtaka, alionekana mpole na akakubali ombi hilo pia akaomba tukutane siku inayofuatia ambayo ni Juma Mosi.Tuliingia kwenye gari nikamuacha jirani na nyumbani kwao na mimi nikarudi kwangu

Jumamosi mida ya saa 8 alinibeep nikampigia then nikamwambia ajiandae ndani ya nusu saa nitampitia. Time ilipofika nilimpitia sehemu tuliokubaliana tukaelekea sehemu husika, huko huko ndio tulipeana mapenzi(Nilimgegeda effectively). Baada ya siku hiyo kugegeda ikawa Continuously.

Ila shida imekuja sasa huyu binti anadai nimpeleke nyumbani kwangu ili nikamtambulishe kwa Mke wangu ili wafahamiane. Nimejaribu kumshauri kwamba yeye bado ni mwanafunzi hivo atulie kwanza amalize masomo yake lakini hanielewi

Anadai kila siku asubuhi niwe nampeleka shuleni na jioni kumrudisha kwa gari langu.Hilo nalo nikamshauri kwamba isiwe kila siku ila pale tukapoona inafaa bado haelewi.

Nimemkataza kunipigia simu au kutuma msg hasa mida ya usiku maana mke wangu atanielewa vibaya hilo nalo haelewi

Amechukua namba ya simu ya mke wangu kwenye simu yangu bila mimi kujua na kumpigia simu mke wangu nae akiwa kazini kwake akimtaarifu kuwa yeye ni mke mwenzie na baadae kurusha msg kibao akidai huo ni utambulisho tosha.Kwa ujumla siku hiyo hayo yote yalipotendeka mimi na mke wangu hatukulala kwa amani kabisa,Wife alilia karibu akataka kukesha.

Nilimfuata yule Binti nikamuonya vikali nusura kuchapa makofu na nikamwambia simuhitaji tena ila yeye kakomaa kwamba kama nataka kumpiga sababu ya mke wangu basi na nikimuacha anajiua na kuacha ujumbe.Ameenda mbali kuniambia kwamba nimemuharibia akili zake maana toka nifanye nae mapenzi hana hamu kabisa ya kusoma au kwenda shuleni.

Wakuu nifanye hapo, Kuna hatari mbili ambazo ni:
1. Ndoa kuvunjika (Wakati tayari tuna mtoto)
2. Kwenda Jera (ukizingatia huyu ni Mwanafunzi)

Maalim Seif Afungula "2020 ni Mwaka wa Kuing'oa CCM Mazima"



Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amesema mwaka 2020 ni mwaka wa kuing'oa CCM madarakani na kuwataka wananchi kuweka pembeni tofauti zao ili kufanikisha uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akitoa salamu za mwaka mpya Maalim Seif amesema wanatarajia kujenga maisha ya raha na furaha kwa wananchi watakaposhika dola na kukuza uchumi wa nchi.

TIMU ya Simba Yaufunga Mwaka 2019 Kwa Furaha Kubwa


Klabu ya Simba imefanikiwa kuufunga mwaka vizuri baada ya kuitandika Ndanda FC bao 2-0 katika dimba la Taila jijini Dar es Salaam.

Magoli ya Simba yaliwekwa nyavuni na Francis Kahata dakika ya 12 na Deo Kanda dakika ya 87.

FT: Simba SC 2-0 Ndanda FC

Kwa Nini Wanawake Wanapenda Wanaume Masharobaro aka Bad Boys


Wanawake kuchagua wanaume masharobaro aka badboys kuwaliko wanaume wa kawaida si jambo geni na hutokea mara kwa mara. -aidha katika vyuo, vilabuni, sinema, maktabani ama sehemu yeyote ile. Wanaume masharobaro, kama wanaume wengine, wao pia wanamaumbo ya kila aina, shepu na mvutio wa kijinsia. Kama wewe ni mwanamume wa kawaida ambaye humaliza wa mwisho ama ushawahi kupoteza mpenzi wako kwa sharobaro fulani, hapo chini kuna nadharia ambazo zitasaidia kueleza kwa nini  wanawake wanapenda sana kuvutiwa na wanaume masharobaro.

1. Hamu ya kufuata
Kufuata kitu ambacho unakipenda huwa kuna msisimko fulani mtu hupata. Lakini msisimko zaidi hutokea wakati ambapo mtu anajaribu kufuata mtu ambaye hataki kujulikana mienendo yake ya kimaisha, kufuatwa ama kueleweka kimaisha. Haya ndio maisha anayoishi mwanamume sharobaro. Wanawake wanapenda sana wanaume ambao hawaeleweki kimaisha (yaani hawatambuliki) ama kutaka kujua maisha yao. Na wewe kama mwanamume unataka kutumia huu udhaifu kwa manufaa yako, wakati mwingine unafaa kumfanya mwanamke abaki na maswali chungu nzima kutaka kukujua zaidi. Kama unampenda, jaribu kadri iwezavyo kutojaribu kumuonyesha.  Badala yake mpe pia yeye changa moto kwa kuweka ujanja wa kutoeleweka mara kwa mara. Hii ni njia moja murua ya kuhakikisha utaingia katika akili yake.

2. Kutaka kuwafunga fundo
Kitu kingine ambacho wanawake huvutiwa kwa sharobaro ni kutaka nafasi ya kuwafunga fundo ama kuwajeuza tabia zao. Mwanamke, amezaliwa naturally na hisia za uzazi, yaani kutaka kujeuza mtu mwenye tabia ovyo kuwa na tabia nzuri. Hii huibua hisia halizi za uzazi ndio maana kama mwanamume unapaswa wakati mwingine kumsumbua mwanamke hikisia, kimawazo na kadhalika. Unafaa kuwa mpinzani lakini usiwe mhalifu. Unafaa kuwa hatari lakini usipitishe kiwango ambacho kitamwogopesha. Kimtazamo, unafaa kumfanya mwanamke auonyeshe uke wake wote ili kujaribu kukubadilisha, mpe nafasi ajaribu kuubadilisha upande wako wa kiza na mwishowe kukufanya uwe mwanamume thabiti katika mchakato mzima.

3.Uanaume uliothabiti
Wanaume masharobaro (na si wale feki) karibu nyakati zote huwashinda wanaume wa kawaida kwa sababu ya mambo mawili makuu. Kwanza ni kuwa ni wanaume majasiri na pili wanaudhibiti uanaume wao kwa kuwa ngangari kimaisha. Kutoogopa kwao kwa jambo lolote ndiko kunawafanya wanawake kuvutiwa nao. Wanawake wengi wanavutiwa na wanaume ambao ni hatari, ngangari na wenye nguvu kwa sababu si rahisi kuchezewa au kufanyiwa masihara. Ukismama  kumtetea mwanamke kuhusu mahitaji yake na uovu, hii inamaana ya kuwa una uwezo wa kusimama kando yake na jambo lolote lile.  Kuweza kuonyesha level ya kuwa wewe ni mtu usiekuwa na woga wowote, unafaa kumwonyesha mwanamke wako kuwa una uwezo wa kuwa ngangari mahali popote pale ili mradi kumlinda yeye tu.

4. Uoga wa kujitwika majukumu
Wanaume masharobaro hupenda kuhepa majukumu yanayohusiana na mahusiano. Kwa wanawake ambao wana uoga huo huo wa kuwa na majukumu, masharobaro huwavutia sana na kuwaona kama hakuna wanaume wazuri kama hao. Kwa kuwa wanawake hawatajitweka majukumu, huwa hawana haja ya kujishughulisha na hisia za kipenzi ambazo ni stress. Pia ni habari njema kwa wanawake ambao wako tayari kwa uhusiano wa kimapenzi wa muda mfupi pekee. Lakini kama kawaida, mwisho wa siku lazima mwanamume sharobaro au mwanamke mtundu lazima kuna sehemu fulani ndani ya mawazo yake anatamani kuwa na mahusiano ya kudumu na pia kupendwa. Hivyo siri hapa ni kuipima miondoko yake na uangalie level yake ya kujitwika majukumu katika mapenzi halafu sasa uanze na hapo.


Upende usipende, wanaume masharobaro watakuwa na nafasi kubwa katika moyo wa mwanamke. Kuna kitu ndani yao ambacho kinawasababisha wanawake kuangua mwili mzima kihisia na kimapenzi kwao. Lakini hii haimaanishi kuwa lazima kila mwanamume ajeuke na kuwa sharobaro ili aweze kuwa na nafasi rahisi ya kutongoza mwanamke aliye kwa ndoto zako. Kile unachotakiwa kufanya ni kucheza mchezo mzima kiwastani. Daima unafaa kuwa vile ulivyo huku ukiingiza tabia flani za usharobaro hivi katika miondoko yako. Kama kuna kitu nzuri kati yenu wawili, basi pia kuna sehemu mbaya ambayo unaweza kuitumia ili ukajinufaisha nayo


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano January 1, 2020


















Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano January 1, 2020


Alichokisema Kigwangalla Baada Ya Rais Kumpa Siku 5

Baada ya Rais John Magufuli kuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda kumaliza tofauti zao vinginevyo atawaondoa, Kigwangalla ameibuka na kudai kuwa tayari walishamaliza tofauti zao na sasa hali ni shwari.

Kupitia akaunti yake ya Twitter na Instagram  amesema walishafanya kikao na Katibu Mkuu, Prof. Adolf Mkenda cha kumaliza tofauti zao.

“Kazi ya Urais ni ngumu sana, tulioteuliwa na Rais kumsaidia utendaji/usimamizi wa maeneo mbalimbali hatupaswi kumuongezea frustrations nyingine zaidi, sisi kwenye Wizara yetu, baada ya kikao na Chief Secretary tulimaliza tofauti zilizokuwepo na sasa hali ni shwari,” amesema Kigwangalla.

Ni imani na heshima kubwa sana kwako kuteuliwa kuwa Waziri kwenye nchi yako. Kwenye nchi ya watu milioni 60, kwa nini Hamisi KIGWANGALLA? Sijui. Ni neema na baraka za Mungu tu. Maana siyo kila mtu kwenye maisha yake atapata fursa ya kuhudumu kwenye serikali kama Waziri ama kama Katibu Mkuu kwenye serikali. Siibezi wala siwezi kuichezea fursa hii adhimu.

Ni kwa kuelewa ukweli huu na ushauri, mwongozo na maelekezo ya wakuu wa kazi, na watendaji wazoefu kwenye utumishi wa umma, kama Katibu Mkuu Kiongozi, tulikaa mimi na Katibu Mkuu wangu na kukubaliana kufungua ukurasa mpya wa mahusiano mazuri zaidi kwa manufaa ya nchi yetu.

Kuondolewa kwenye nafasi ya Uwaziri unaweza kuondolewa kwa sababu mbalimbali lakini kuondolewa kwa sababu watu wazima, tena viongozi, ambao mmepewa fursa ya kushauriwa, mmeshindwa kuelewana, ni upumbavu! Mimi siyo mpumbavu.

Kuleta kiburi na jeuri kwenye mazingira Haya ni upumbavu. Kwanza sisi waislam tunafundishwa kuwa wanyenyekevu, maana ‘kiburi’ ni sifa ya Mungu, siyo yetu wanadamu. Kufanya kiburi na jeuri ni upumbavu. Hekima ya Mungu ni kujishusha na kumshinda shetani.

Sina jeuri wala kiburi sababu nimelelewa vizuri na bibi yangu Mama Bagaile, na pia naogopa hasira za Mungu. Tumalizie haya masaa kwa amani! Happy New Year Good People. Nitaendelea kutoa darasa la mambo niliyojifunza 2019, na mipango yangu ya 2020.

Nipo jimboni nachunga ng’ombe wangu kidogo. Ningekuwa Dar ningemtembelea Prof. Mkenda kwa ajili ya picha tukigonga glass ili mjue tuko sawa 😀. Mhe. Rais yeye ana namna yake ya kupata taarifa zetu. Atazipata tu! 😀. Limeisha hilo au niongeze volume? 🤷🏾‍♂️ Wakatabahu Dkt. Hamisi KIGWANGALLA, MB., MNEC, WMU.

 


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano January 1, 2020





















Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...