Search This Blog
Friday, April 30, 2021
Yanga kuwakosa nyota watatu dhidi ya TZ Prisons leo
Msemaji klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amethibitisha kuwakosa wachezaji nyota watatu wa kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa mtoano wa 16 bora wa kombe la Shirikisho dhidi ya TZ Prisons utakaochezwa saa 10:00 jioni ya leo kwenye uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.
Wachezaji hao watakaokosekana ni viungo wa kati,Tonombe Mukoko, Feisal Salum “Fei Toto” na mshambuliaji Michael Sarpong baada ya wachezaji hao kuoneshwa kadi za manjano tatu mfululizo hivyo kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja.
Benchi la ufundi la Yanga linaloongozwa na kocha wake mpya, Mtunisia, Mohammed Nasruddine Nabi linatazamiwa kuwageukia viungo Zawadi Mauya kuchukua nafasi ya Tonombe Mukoko,Carlinhos kucheza nafasi ya Fei Toto na Ditram Nchimbi kama mbadala wa Sarpong.
Kwa upande wa nahodha wa Prisons, Benjamin Asukile amejinasibu kuwaondoa Yanga na kutinga robo fainali kwasababu wamejiandaa vya kutosha ukizingatia na kusema wana uwezo wa kufanya hivyo tena kwenye dimba lao la nyumbani.
Ikumbukwe kuwa, kwenye michezo miwili ya VPL msimu huu, Yanga na TZ Prisons wametoka sare ya bao 1-1 kwenye michezo hiyo huku ikishuhudiwa kuwa yenye upinzani huku moja ya sababu ikiwa ni TZ Prisons kucheza mchezo wa mabavu.
Ben Pol afunguka kuhusu shauri lake la kudai talaka
Mkali wa muziki wa RnB Bongo Ben Pol ametoa taaifa ya kile kinachoendelea kuhusu shauri lake la kudai talaka Mahakamani dhidi ya mke wake Anerlisa Muigai ambaye ni Raia wa Kenya.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram taarifa hiyo inaeleza kuwa "Ben Pol angependa kuthibitisha uwepo wa shauri la talaka dhidi ya mke wake linaloendelea katika Mahakama ya mwanzo hapa Dar es salaam, Mahakama bado haijatoa talaka/maamuzi yoyote mpaka pale litakaposikilizwa na kukamilishwa"
"Masuala haya ni binafsi sana na kwa kuwa shauri linaendelea Mahakamani Ben Pol asingependa lizungumzwe zaidi kwa heshima ya pande zote na kwa kuheshimu kazi ya Mahakama"
Aidha imeendelea kueleza "Pia anaomba nafasi na faragha kwake na kwa familia katika kipindi hiki kigumu, anawashukuru wote kwa uelewa na pia kwa familia, marafiki na mashabiki wote kwa support mnayoendelea kuionesha".
Kuhusu chanzo cha Ben Pol kudai talaka hiyo Mahakamani bado hakijatajwa, wawili hao walifunga ndoa ya siri na picha za siku ya hurusi yao zilionekana Oktoba 2020.
Waziri Mchengerwa aongoza mkutano wa pili wa Mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Na.8 ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati Na. 8 inayoshughulika na masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala leo ameongoza Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala Afrika kwa njia ya mtandao.
Mhe. Mchengerwa ameongoza Mkutano huo ili kupitia na kuidhinisha ajenda mbalimbali zilizowasilishwa na Mkutano wa Wataalamu uliofanyika tarehe 27 na 28 Aprili, 2021.
Miongoni mwa ajenda zilizopitiwa na kuidhinishwa ni rasimu ya Nyenzo ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Miiko na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala Afrika; ambapo iliridhiwa kuwa Tanzania, Afrika ya Kusini, Namibia, Cameroon na Kenya zitahusika katika kufanya majaribio ya Utekelezaji wa Nyezo husika.
Ajenda nyingine ni kuchagua Wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba; ambapo walioidhinishwa ni Mwenyekiti kutoka Afrika Kusini, Makamu Mwenyekiti wa Kwanza kutoka Algeria, Makamu Mwenyekiti wa Pili kutoka Cameroon, Makamu Mwenyekiti wa Tatu kutoka Benin na Katibu kutoka Tanzania.
Pia mkutano ulitathmini hali ya utiaji saini na uridhiwaji wa Mkataba wa Umoja wa Afrika na kupendekeza mbinu za kukuza uridhiaji wa pamoja wa Mkataba huo kwa nchi wanachama ambapo ilibainishwa kuwa, mpaka sasa mwenendo wa utiaji saini na uridhiwaji wa Mkataba miongoni mwa nchi wanachama, nchi 38 zimeshasaini, wakati nchi 19 tu zimeridhia na 19 zimewasilisha Nyaraka za kuidhinisha.
Aidha, Mkutano uliridhia juu ya kuhimiza Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kusaini na kuridhia Mkataba wa Umoja wa Afrika na Kuziomba AAPAM na AMDIN na Taasisi zingine kuutangaza Mkataba huu kupitia mijadala na tovuti mbalimbali.
Sanjali na hilo, wajumbe walipitia na kuridhia Azimio la Mkutano wa Pili wa Nchi Wanachama kwa kuwasilisha taarifa ya kwanza ya utekelezaji wa Mkataba kwa Kamishna wa Umoja wa Afrika ifikapo mwezi Januari, 2022, na kuiomba Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuandaa taarifa ya jumla kuhusu Utendaji wa Utumishi wa Umma katika Afrika ikiwa ni pamoja na kudumisha ushirikiano na mshikamano baina ya Nchi Wanachama.
Mkutano kazi huo, ulihudhuriwa na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika walioridhia Mkataba huu ambao ni Algeria, Benin, Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Mali, Namibia, Rwanda, Afrika ya Kusini, Mali, Ivory Coast, na Tanzania. Mkutano wa Tatu wa Nchi Wanachama utafanyika mwezi Aprili, 2022.
TABIBU AGU NI BINGWA WA KUTIBU MAGONJWA SUGU KAMA VILE UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME KULEGEA,TEZI DUME, KISUKARI
tatizo hili la kuishiwa nguvu za kiume lime asili watu wengi,sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine, kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo zipo , sababu nyingi zinazosababisha, tatizo hilo baadhi ni
(i) upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN ambazo mwanaume, anapobarehe vichocheo hivi, HORMONES hizo, husaidia ukuaji wa uume
(MIZIZI 29) ni dawa bora, ya kurudisha nguvu, za, kiume inatibu ,kabisa na kutoa tatizo hilo, na kukupa , hamu ya , kurudia tendo, la ndoa zaidi, ya mala nne 3 ,bila kuchoka atakama unaumli ,wa mika 80,!
WA TEZI DUME , MADHARA YAKE NA TIBA YAKE
Tezi dume ni Nini na kazi yake ni Nini?
Tezi dume ni kiungo kidogo na ni sehem moja ya uzazi wa wanaume.hupatikana chini ya kibofu na mbele ya mwanzo cha njia itokayo mkojo hupitia ndani ya tezi dume.tezi dume ndiyo hutoa maji yabebayo mbegu (manii) ya mwanaume
DALILI ZA AWALI ZA TEZI DUME
.kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu
.maumivu kwenye mfumo wa mkoji
.homa
.kukojoa mala kwa mala
.kuhisi kipofu kimejaa mkojo mda wote
MADHARA YA TEZI DUME
.kipofu cha mkojo kuuma na kupelekea mkojo kurudi juu na ,kuharibu figo,Ini n,k
.kufunga kwa njia ya mkojo kabisa
.figo kushindwa kufanya kazi
.kushindwa kumudu tendo la ndoa
.ugumba
.kutokea kwa majipu sehemu za tezi dume
Sasa hii hapa tiba sahihi MDOSHI ni dawa ya asiri inatibu kabisa tatizo la tezi dume dawa hii imeonyesha mafanikio makubwa kwa wateja waliotumia
ISENYE hii ni dawa ya kisukari dawa hii ni ya mimea asili ipo ya vidonge na unga dawa hii imeonyesha matokeo mazuri Sana kwa wagonjwa wa kisukari jaribu Leo hakika uweze kuona utofauti wake na dawa ulizowah kutumia, pia ana ,dawa za ,kutibu, presha ya kupanda ,na kushuka, kuondoa, mafuta , mwilini ,na maumivu ya, mgogo kiuno, dawa zipo, vidonda ,vya, tumbo , huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa hata Kama hupo nnje ya nchi ofisi ipo mbagara sabasaba MWANZA yupo wakala
Wasiliana nami kwa simu 0782794980 Whatsapp +255782794980
Breaking News: Rais Samia Suluhu achaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM
Rais Samia Suluhu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kura zote 1862 za ndio za Mkutano Mkuu Maalum sawa na asilimia 100.
Rais Samia Suluhu Hassan kuweka rekodi ya tatu kwenye historia ya Tanzania
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Philip Mangula amesema kazi kubwa iliyofanywa na wagombea wao wa Urais na Umakamu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ndio iliyosabisha chama hicho kipate heshima kwa wananchi.
Kupitishwa kwa Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa CCM kunamfanya kuweka rekodi tatu muhimu katika historia ya Nchi yetu toka kupata kwa Uhuru Desemba 9, 1961.
Rekodi hizo ni za kuwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke mwaka 2015 hadi 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo aliapishwa Machi 19 mwaka huu na sasa leo anathibitishwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza Mwanamke wa CCM.
Mangula ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano maalum wa chama hicho wenye ajenda moja tu ya kulipitisha jina la Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Sita wa CCM.
Rais Mama Samia anapigiwa kura za kupitishwa kuwa Mwenyekiti wa CCM kufuatia kifo cha aliyekua Rais na Mwenyekiti wa chama hicho, Hayati Dk John Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu.
Wajumbe 1876 kutoka kila Wilaya ya Tanzania wamefika jijini Dodoma tayari kulithibitisha jina la Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho.
TANGAZO: TUNAAGIZA MAGARI NAKUKOPESHA
Kampuni yetu inaitwa Bin Khalifa motors company limited.
Tunahusika kuuza gari used, Pia tunaagiza gari kutoka japan na uingereza.
Pia tunakopesha magari unalipa asilimia 60% nyingine unalipia kwa miezi minne.
Vile vile tunatoa ushauri wa kitaalam kuhusu magari.
Ofisi zetu zipo magomeni mapipa nyuma ya bank ya diamond trust bank
Tunapatikana kwa namba 0718228825 / 0758228825 / 0784228825 instagram @bin khalifa motors co ltd
Mizengo Pinda amuombea kura za Uenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan "Amepangwa na Mungu"
WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mizengo Pinda amewataka wajumbe 1876 wanaoshiriki mkutano mkuu maalum wa Chama cha Mapinduzi kumchagua kwa kishindo Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Sita wa CCM.
Pinda amesema uzoefu wa miaka 34 wa kuwa Mwanachama wa CCM na uzoefu wa miaka 44 akiwa mtumishi wa Serikali vinatosha kumfanya kuwa mwenye sifa na uwezo wa kukiongoza Chama hicho.
Amesema uwezo wake aliouonesha wa kufanya kazi kama Makamu wa Rais chini ya Dk John Magufuli vimemfanya amuamini kwamba anatosha kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kinachotawala.
" Ameondoka Dk Magufuli akiwa na miaka 61 na Mama Samia ameapishwa Machi 19 kuwa Rais akiwa na miaka 61 kumbe hili jambo limepangwa na Mungu, tumpigie kura zote za ndio ili tumpe moyo na nguvu ya kuendeleza kazi iliyoachwa na Dk Magufuli.
Alivyofariki Dk Magufuli yakazuka maneno ya hapa na pale lakini Mama mwenyewe akasema yeye na Hayati ni kitu kimoja, hivyo niwasihi wote tumpigie kura Rais Samia kuwa Mwenyekiti, nitashangaa kama baada ya kazi yote hiyo tutapata matokeo tofauti na asilimia 100," Amesema Pinda.
MAGONJWA NINAYO TIBU NI KISUKARI, TEZI DUME, NGUVU ZA KIUME
DOCTOR MBOJE,
NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA
MAGONJWA NINAYO TIBU NI
A,_DOCTOR MBOJE,
NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA
MAGONJWA NINAYO TIBU NI
A,_KISUKARI na tibu kwa miti shamba kunywa na kupona kabisa
B,_TEZI DUME_natibu kwa miti kunywa na kupona kabisa bila kufanyiwa upasuaji
C,_NGUVU ZA KIUME
Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa natibu kwa miti shamba na kupona kabisa
D,_kutibu magonjwa mbalimbali Kama uzazi) (miguu kuvimba na kuwaka Moto) (Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu) (mgongo, kiuno)
MHERA JIGURHU ni dawa ya miti shamba inatibu kisukari na kupona kabisa kwa mda wa siku 16
Sukari iwe kubwa kabisa lakini iwe normal 5.1
NNKOROBHIJE ,ni dawa ya miti shamba inayotibu TEZI DUME bila kufanyiwa operation na kupona kabisa kwa siku 14 na kibaki history
NHUNGHU MAPANDO Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa au kama unahisi kupungukiwa tumia nhunghu mapando ni dawa inatibu na kupona kabisa tatizo kwa mda wa siku 4 tu
NTURURU ni dawa ya miti shamba inayotibu uzazi chango kwa wakina mama wasio kua na watoto inatibu na kumaliza tatizo kabisa na mfumo wako wa Heath Kama umevulugika inatibu kwa mda wa siku 18
MWICHE,ni dawa ya miti shamba inayotibu Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu kurunguia kiuno kuuma mgongo na kupona kabisa kwa mda wa siku 7
PIIA UNAWEZA KUNIPATA KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA
CALL AND WHAT SAAP
+255744922982
+255737585753
HUDUMA ZANGU ZINAPATIKANA DUNIA NZIMA KWA OFISI NI DAR ES SALAAM NA MOROGORO KWA ULIE MBALI DAWA NAKUSAFIRISHIA MPAKA INAKUFIKIA KWA WALE WA DAR NA MOROGORO KAMA HUWEZI KUFIKA OFISINI NAKUAGIZIA DAWA INAKUFIKIA MPAKA ULIPO na tibu kwa miti shamba kunywa na kupona kabisa
B,_TEZI DUME_natibu kwa miti kunywa na kupona kabisa bila kufanyiwa upasuaji
C,_NGUVU ZA KIUME
Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa natibu kwa miti shamba na kupona kabisa
D,_kutibu magonjwa mbalimbali Kama uzazi) (miguu kuvimba na kuwaka Moto) (Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu) (mgongo, kiuno)
MHERA JIGURHU ni dawa ya miti shamba inatibu kisukari na kupona kabisa kwa mda wa siku 16
Sukari iwe kubwa kabisa lakini iwe normal 5.1
NNKOROBHIJE ,ni dawa ya miti shamba inayotibu TEZI DUME bila kufanyiwa operation na kupona kabisa kwa siku 14 na kibaki history
NHUNGHU MAPANDO Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa au kama unahisi kupungukiwa tumia nhunghu mapando ni dawa inatibu na kupona kabisa tatizo kwa mda wa siku 4 tu
NTURURU ni dawa ya miti shamba inayotibu uzazi chango kwa wakina mama wasio kua na watoto inatibu na kumaliza tatizo kabisa na mfumo wako wa Heath Kama umevulugika inatibu kwa mda wa siku 18
MWICHE,ni dawa ya miti shamba inayotibu Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu kurunguia kiuno kuuma mgongo na kupona kabisa kwa mda wa siku 7
PIIA UNAWEZA KUNIPATA KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA
CALL AND WHAT SAAP
+255744922982
+255737585753
HUDUMA ZANGU ZINAPATIKANA DUNIA NZIMA KWA OFISI NI DAR ES SALAAM NA MOROGORO KWA ULIE MBALI DAWA NAKUSAFIRISHIA MPAKA INAKUFIKIA KWA WALE WA DAR NA MOROGORO KAMA HUWEZI KUFIKA OFISINI NAKUAGIZIA DAWA INAKUFIKIA MPAKA ULIPO
UNDP yatoa kompyuta zenye thamani ya zaidi ya milioni 40/=
WALIMU wa shule mbalimbali wametakiwa kuwafundisha wanafunzi wao elimu ya natharia na vitendo ili pindi wanapomaliza masomo yao na kwenda mtaani waweze kujiajiri kirahisi na sio kutegemea kuajiriwa
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa Taha Jackline Mkindi jana wakati akikabibidhi komputa kumi na vifaa vyake venye thamani ya Shilingi milioni 48 vilivyotolewa na washirika wao ambao ni UNDP kwa ajaili ya kuwapatia wanafunzi wa shule ya sekondari Shepherds iliopo katika Kijiji cha Manyire kilichopo katika kata ya Mlangarine
Alisema kuwa kazi ya TAHA ni kuhamasisha na kutangaza sekta ya horticulture nchini ,lakini vilevile pia sekta hii inapendwa sana na vijana,na katika kuhamasisha huku sasa hivi hatuangalii tu vijana ambao wanatoka vyuoni lakini tunataka wale vijana ambao wanatoka kwenye msingi vijana ambao wapo katika levo ya shule za msingi hadi wale waliopo katika shule za sekondari pamoja na wale ambao kabla hawajafika vyuoni.
Alisema kuwa wao kama TAHA wameanzisha mikakati mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule mbalimbali hapa nchini ,ambapo katika kuwagusa hawa vijana ili waweze kuelewa kabisa na kupenda sekta ya kilimo kuanzia wakiwa wadogo.
‘’chanzo cha komputa hizi kuletwa hapa kama zawadi ni kwamba sisi kama Taha tulikuja kutoa elimu ya kilimo cha mboga na matunda kwa wanafunzi hawa wa shule hii ya sekondari ya shepherds baada ya kutoa elimu ,tulikuwa tunawafatilia mara kwa mara n ahata mmoja wa washirika wetu alipokuwa kututembelea ambaye ni UNDP tuliamua kumleta hapa ,alivyokuja na kuona namna wanafunzi hawa wanavyofanya kilimo na kukielezea ,namna uhamasishaji wa watoto hawa ulivyo ndio akaadi kuwapa komputa hizi wanafunzi hawa ili waendelee kujifunza zaidi maswala ya kilimo “alisema Mkindi
Alisema kutokana na mambo ambayo wanayona wanafunzi hawa wanayafanya yamewapa motisha zaidi ya kuendelea kutoa elimu kwa shule zingine na vijana wengine kwani wanafunzi hawa wameonyesha wanauelewa mkubwa wa masomo ya sanyansi na teknolojia jambo ambalo limewashangaza sana pia wana uelewa wa mazao mbalimbali ya kilimo .
Aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa namna wanavyoendelea kuwafundisha wanafunzi hao na kusema kuwa wanawafundisha watoto hao jinsi ya kujiajiri pindi wanapotoka shuleni hapo kwani wanakuwa na elimu ya maarifa na vitendo kwa kilimo na jinsi wanavyoendelea kupewa elimu zaidi ndio itawasaidia wao kuwa wadau wazuri wa kilimo hapo baadae,kwani kilimo ni mti wa mgongo kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu ya Tanzania .
Kwa upande wake mmoja wawanafunzi wa shule hiyo Kennedy Lomboi aliishukuru Taha kwa kuwapa elimu ya kilimo ambapo alisema kuwa wanaimani kabisa pindi watakapo maliza elimu yao ya sekondari wanapoenda nyumba kusubiri matokeo wataendelea kujiajiri kwa kufanya kilimo.
Aidha aliishukuru UNDP kwakuona umuihimu wao na kutambua kazi wanazifanya za kilimo wanapokuwa shuleni hadi wakaamu kuwapatia zawadi ya komputa ambazo alisema kuwa zitawasaidia kuendelea kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo kupitia mitandao mbalimbali
Kwa upande wake meneja wa shule ya shepherds sekondari Lucy Moses aliwashukuru Taha kwa kumleta mshirika wao ambaye ni UNDPaliyeweza kuwapatia komputa kwa ajili ya wanafunzi waliopo hapo shuleni ambapo aliwahaidi kuzitunza na kuzifanyia kazi wa lengo lililokusudia huku akaiwasihi walimu wa shule zingine kujitahidi kutembelea TAHA na kupata ujuzi ambao utawasadiia vijana kujifunza mbinu mbalimbali za kujiajiri pindi wanapo maliza shule na sio kutegemea ajira za serikalini.
Sheria ya uhujumu uchumi kufumuliwa
Hatua ya Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria kufanyia tathmini sheria sita, ikiwamo ya uhujumu uchumi, imepokelewa kwa furaha na wadau wa sheria ikielezwa kuwa ni kilio cha muda mrefu cha kuondoa sheria kandamizi za muda mrefu.
Hatua hiyo imetangazwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi jana, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022, akisema lengo ni kufahamu kama sheria hizo zinaweza kutumika katika kupunguza msongamano magerezani.
Mbali na uhujumu uchumi, Profesa Kabudi alizitaja sheria nyingine zinazofanyiwa tathmini kuwa ni pamoja na Sheria ya Magereza, Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na Sheria ya Huduma za Jamii, Sheria ya Bodi ya Msamaha na Sheria ya Kikomo cha Adhabu.
“Madhumuni ya tathmini hii ni kubainisha kama sheria zilizopo zinaweza kutumika kupunguza msongamano magerezani na hivyo kupunguza gharama za kuendesha magereza,” alisema.
Profesa Kabudi alisema kwa upande wa uboreshaji wa sekta ya utalii, sheria zinazofanyiwa tathmini ni pamoja na Sheria ya Utalii na Sheria ya Wanyamapori.
Nyingine ni Sheria ya Mbuga za Wanyama, Sheria ya Makumbusho ya Taifa, Sheria ya Hifadhi ya Eneo la Mamlaka ya Ngorongoro na Sheria ya Malikale.
Kenya kufunga kambi za Kakuma, Dadaab kufikia Juni 2022
Kenya imethibitisha kuwasiliana rasmi na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na kutaarifu kuwa itafunga kambi za wakimbizi ya Dadaab na Kakuma ifikapo Juni 30, 2022.
Waziri wa mambo ya nje wa nchini Kenya bwana Fred Matiangí ametangaza hayo baada ya kufanya mkutano na Filippo Grandi, mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia wakimbizi.
Dkt. Matiangí amesema kuwa timu ya maafisa wa serikali ya Kenya na Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa watafuatilia mchakato huo uliopangiwa kuanza Mei, 5, 2022.
Mchakato wa sasa hivi unajumuisha kurejea katika nchi zao kwa hiari au kutoa kibali cha kufanyakazi au cha makazi bila malipo kwa wakimbizi kutoka jamii ya Afrika Mashariki.
Wakati huo huo, Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limefurahishwa na mpango wa kupitiwa tena kwa mpango wa kufunga kambi hizo za wakimbizi.
‘’Sio kambi za kudumu za wakimbizi au kufungwa kwa haraka kwa kambi hizo au kukiuka kanuni ya kimataifa inayokataza nchi inayopokea wakimbizi kuwarejesha nchini mwao ambako wanaweza kuwa katika hatari ni suluhisho ya hili’’, UN imesema.
Katika taarifa iliyotolewa na shirika hilo, imesema kuwa inaamini serikali ya Kenya na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa katika kubaini machaguo mengine ya kuwahifadhi au kurejea kwa hiari kwa wanaotaka kwa namna heshima.
Mnamo mwezi Machi, serikali ya Kenya ilikuwa imeipatia UN makataa ya mwisho ya kutafuta njia kwasababu inataka kufunga kambi hizo mbili ambazo ni makazi kwa wakimbizi 400,000.
Muda mfupi baadae, Shirika la Amnesty International likajibu kwa kusema kuwa hatua ya kufungwa kwa kambi za Dadaab na Kakuma bila mpangilio unaoheshimu haki za wakimbizi, kutasababisha janga la kibinadamu wakati tayari dunia inakumbana na janga la virusi vya corona.
Kenya imekuwa ikitoa makazi kwa wakambizi kwa zaidi ya miaka 30 na sasa hivi serikali inasema uwezo wake kuendelea kuwatunza hata kwa kuzingatia viwango vya chini kabisa vya kibinadamu vinavyokubalika imekuwa changamoto kwa nchi hiyo kuvifikia.
Katibu Mkuu nchini Kenya Karanja Kibicho, aliongeza kuwa uamuzi wake wa kufunga kambi za Dadaab na Kakuma kufikia Juni 30, 2022 ‘ni kwa maslahi ya raia wa nchi yake’.
Malkia wa Zulu afariki dunia mwezi mmoja baada ya kuchukua majukumu ya kifalme
Familia ya kifalme ya Zulu nchini Afrika Kusini imetangaza kifo cha Malkia wake aliyekuwa anaongoza eneo hilo Shiyiwe Mantfombi Dlamini Zulu, mwezi mmoja tu baada ya kutawazwa kuchukua majukumu ya kifalme.
Malkia Mantfombi, 65, alikuwa kiongozi wa mpito wa kabila la Zulu ambalo ndilo kubwa zaidi nchini Afrika Kusini baada ya kifo cha mume wake, Mfalme Goodwill Zwelithini.
Waziri mkuu wa malkia huyo amesema kifo chake kimeshutua familia ambayo ipo kwenye masikitiko makubwa kwa kumpoteza.
Mrithi kama mtawala wa eneo la Wazulu lenye watu milioni 11 bado hajatajwa.
"Ni huzuni na masikitiko makubwa kwamba Familia ya Kifalme inatangaza kifo ambacho hakikutarajiwa cha Malkia Shiyiwe Mantfombi Dlamini Zulu, wa Wazulu," Mwanamfalme Mangosuthu Buthelezi, waziri wake mkuu amesema kwenye taarifa.
Aliongeza kuwa anataka kuhakikishia watu kwamba hakutakuwa na "ombwe la uongozi kwa eneo la Wazulu".
Malkia Mantfombi alilazwa hospitalini wiki moja iliyopita baada ya kuuguwa ugonjwa ambao haukujulikana, kulingana na vyombo vya habari vya Afrika Kusini.
Alikuwa ameteuliwa kuchukua nafasi hiyo Machi 24, baada ya mume wake, 72, Mfalme Zwethilini, kufariki dunia akiwa hospitalini kwa ugonjwa wa kisukari na matatizo mengine.
Mfalme huyo alikuwa ametawala eneo la Wazulu kwa karibu miaka 50 – na kumfanya kuwa mfalme aliyetawala kwa kipindi kirefu zaidi Afrika.
Malkia MaDlamini Zulu alikuwa ameshikilia nafasi ya juu zaidi ya uongozi miongoni mwa wake wa mfalme kwasababu anatoka familia ya kifalme.
Alikuwa dada ya Mfalme wa Eswatini, Mswati III – nchi pekee Afrika ambayo yote inaendeshwa kwa mfumo wa kifalme.
Malkia MaDlamini Zulu na marehemu muwe wake walijaaliwa watoto wanane – ikiwa ni pamoja na vijana 5 wa kiume.
Kijana wao mkubwa, 47, Mwanamfalme Misuzulu, ndiyo mwenye uwezekano mkubwa wa kuchukua uongozi kama mfalme, taarifa zinasema
Thursday, April 29, 2021
Damien Duff ampa makavu Eden Hazard
Duff amekosoa mwenendo wa Eden Hazard tangu alipohamia Real Madrid mwaka 2019, akisema kuwa kamwe hawezi kulinganishwa na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kwa sababu hajawahi kuwa na kiwango bora cha hali ya juu duniani.
Maneno hayo mazito aliyasema baada ya mchezo wa sare ya bao 1-1 wa mchezo wa nusu fainali ligi ya mabingwa ulaya Jumanne usiku Madrid chidi ya Chelsea ambao ulikuwa ni mchezo wa 16 kwa Hazard akiwa na Los Blancos msimu huu.
Duff ambaye aliwahi kucheza misimu mitatu Chelsea na kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu, anaamini kwamba Hazard amekuwa akipambana sana na uzito wake kila wakati, na anapaswa kuweka bidii zaidi aweze kukaa sawa.
Eden Hazard alihamia Real Madrid kutoka Chelsea mwaka 2019 kwa dau la paund milioni 130 na amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara kitendo ambacho kimemfanya kucheza michezo michache.
Shomari Kapombe aongeza mkataba Simba
Beki wa pembeni wa Simba, Shomari Kapombe amesaini dili jipya baada ya kukubaliana na uongozi kuongeza mkataba.
Beki huyo mzawa chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Didier Gomes mkataba wake ulikuwa unafika ukingoni mwishoni mwa msimu wa 2020/21.
Alikuwa anatajwa kuingia rada za FAR Rabat ya Morocco pamoja na timu nyingine nchini Afrika Kusini ambazo zilikuwa zinahitaji saini yake.
Baada ya makubaliano mazuri na mabosi wake wa sasa nyota huyo amesaini dili jipya na inaelezwa ni kandarasi ya miaka miwili.
Tetesi za soka Kimataifa
Borussia Dortmund imeingia kwenye kinyanganyiro cha kumsajili mlinzi wa Uingereza Ben White, 23, huku Paris St-Germain, Manchester United na Arsenal zikimnyatia mchezaji huyo. (Sun)
Aston Villa ipo kwenye tahadhari baada ya kujitokeza kuwa Chelsea iko tayari kukubali ofa ya takriban pauni milioni 40 kwa ajili ya mshambuliaji Tammy Abraham, 23. (Mirror)
Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, aliyeondoka Barcelona kujiunga na Atletico Madrid msimu uliopita amemtaka mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, kusalia Nou Camp. (TV3, via Sport)
Rais Mwinyi afuturisha Dodoma
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, leo amejumuika na mamia ya waislamu katika Iftari aliyoiandaa kwa ajili yao na kufanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Conversion centre, Jijini Dodoma.
Katika hafla hiyo viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) walihudhuria, akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya saba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Mama Maryam Mwinyi na Mama Mwanamwema Shein .
Wengine ni pamoja na Makamo wa Pili Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Serikali za SMZ na SMT, Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Said Ahmeid, Wabunge, Wawakilishi, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na wageni mbali mbali.
Akitoa shukran kwa waalikwa, Dk. Mwinyi amesema amefarikijika sana na muitikio wa waumini hao, mbali na mialiko kutolewa katika kipindi kifupi.
Amesema ameamua kuandaa futari hiyo Jijini Dodoma kwa kuzingatia uwepo wa vikao vya Bunge na vikao vya Chama cha Mapinduzi wakati huu, akibainisha kuwa ni wakati muafaka wa kukutana na kufutari pamoja na waumini hao.
Aidha, Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha waumini hao kutekeleza vyema ibada hiyo muhimu ya funga, na kusema kukutana kwao huko ni jambo la kheri.
Nae, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Mustafa Rajab Shaaban amemuombea dua Rais Dk. Mwinyi pamoja na kumtakia kheri nyingi kwa Mwenyezi Mungu kwa maandalizi mazuri ya iftari hiyo.
Alitumia fursa hiyo kumtakia rehma yeye na familia yake , akibainisha wema mkubwa aliowafanyia waumini waliotikia mwaliko wake.
Akinukuu hadithi ya Mtume Muhamad (SAW), Sheikh Rajab amesema Mtume ameelekeza kuwalipa wema watu wanaofanyia wenzao mambo wema na pale wasipokuwa na cha kuwalipa, basi ni vyema wakawaombea dua, hivyo dua hiyo ni jambo lililosadifu.
Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi, yuko Jijini Dodoma kwa vikao mbali mbali vya Chama cha Mapinduzi, ambapo kesho April 30, 2021, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama hicho watapiga kura ya kumthibitisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho kufuatia kifo cha Mwenyekiti wake, Rais Dk. Joseiph Pombe Magufuli.
Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi 2021 yakamilika
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...





















































