Search This Blog

Thursday, September 30, 2021

Mwigulu Aagiza Halmashauri Nne Zichunguzwe


WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), azikague na kuzichunguza halmashauri nne za wilaya na taasisi ya serikali kwa tuhuma za kukiuka Sheria za Ununuzi wa Umma.


Dk Mwigulu alitoa agizo hilo jijini Dodoma baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Utendaji ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ya Mwaka wa Fedha 2020/2021.


Alisema lazima ufanyike uchunguzi hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaobainika kukiuka taratibu za ununuzi ikiwa ni pamoja na kutoa zabuni nje ya mfumo wa kielektroniki wa TANePS unaotumika kuchakata zabuni.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi (PPRA), Profesa Ninatubu Lema kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA,  Profesa Marten Lumbanga, taasisi tano zilipata wastani hafifu wa kufuata sheria taratibu na kanuni za ununuzi wa umma.


Nazo ni Halmashauri ya Mji Kondoa, Halmashauri ya Mbogwe, Halmashauri ya Biharamulo, Halmashauri ya Chato na Taasisi ya Utafiti wa Wanyama.


Dk Mwigulu pia alimuagiza Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba, aziandikie waraka taasisi 172 zilizounganishwa TANePS zijieleze kwa nini hazitumii mfumo huo kufanya ununuzi.


Alizitaka taasisi nunuzi zote zitumie asilimia 30 ya gharama zao za zabuni zinazotangazwa katika mpango wa ununuzi wa mwaka kwa ajili ya kuwezesha makundi maalumu yakiwemo ya vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.


"Nimesikitika sana baada ya kusikia kwamba kati ya taasisi 86 mlizozikagua ni taasisi mbili tu ndizo zilitenga asilimia 30 katika mpango wao wa ununuzi wa mwaka kwa ajili ya makundi maalumu," alisema Dk Mwigulu.


Tutuba alisema atazingatia maelekezo aliyopewa na kuwawajibisha wote watakaobainika kuhusika na ukiukaji wa sheria ya ununuzi.


Alizitaka taasisi za umma zizingatie sheria, kanuni na taratibu za ununuzi wa umma ili kuthaminisha miradi ya maendeleo na fedha zinazotumika.


Kwa mujibu wa Tutuba, katika mwaka wa fedha 2020/2021 bajeti ya ununuzi ilikuwa shilingi trilioni 25 sawa na zaidi ya asilimia 75 ya bajeti yote ya serikali.


Profesa Lema alisema katika mwaka wa fedha 2020/2021 walifanya ukaguzi wa mikataba 8,838 ya ununuzi yenye thamani ya Sh trilioni 9.2 kutoka taasisi 86.


 



Ni asilimia mbili pekee ya watu Africa waliopata chanjo za Covid

 


Shirika la afya duniani limesema Alhamisi kwamba ni takriban asilimia mbili pekee ya watu barani Afrika ambao wamepokea chanjo za covid.


Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mataifa 15 kati ya jumla ya mataifa 54barani yamechanja takriban asilimia 10 ya watu wake na kwa hivyo kufikia vingango vilivyo kusudiwa kufikia mwisho wa Septemba.


Mratibu wa chanjo barani Afrika kutoka shirika la afya dunia Richard Mihingo amesema kwamba kuna hatua zilizopigwa ingawa kuna safari ndefu kuelekea kuchanja asilimia 40 ya watu wake kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Muhingo ameongeza kusema kwamba upelekaji wa chanjo barani humo umeongezeka lakini mifumo hafifu ya usambazaji ni changamoto kubwa.


Jumla ya chanjo milioni 23 zimewasili Afrika Septemba, ikiwa ni ongezeko mara 10 kulinganishwa na mwezi Juni. Nusu ya mataifa 52 ya kiafrika yaliopokea chanjo hizo ndiyo pekee yaliotoa chanjo kamili kwa asilimia 2 ya watu wake. Hata hivyo visiwa vya Mauritius na Seychelles vimefaulu kuchanja asilimia 60 ya watu wake kulingana na data za WHO.


Morocco imetoa chanjo kamili kwa asilimia 48 ya watu wake. Mataifa mengine ambayo yamepita asilimia 20 ni Tunisia, Comoros na Cape Verde.



UN kubaki Libya hadi Januari

 


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi limekubaliana kuendelea na shughuli za kisiasa nchini Libya hadi Januari 31, mwaka ujao. 


Wakati huo utakuwa muda mfupi baada ya taifa hilo kufanya uchaguzi wa rais. Baraza hilo lenye wanachama 15 limekuwa likishauriana kuhusu kuongeza jukumu lake la kisiasa nchini humo hadi Decemba 24 ambapo uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika.


Hata hivyo kulitokea mvutano mkali kati ya Uingereza na Russia kuhusiana na pendekezo hilo. Moscow ililamamikia lugha iliyokuwa kwenye rasimu ya mapendekezo, na ilioandikiwa London ikisema kwamba vikosi vya kigeni pamoja na mamluki nchini Libya waondoke pamoja na sehemu inayoeleza jukumu la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo.


Jumatano Russia ilitishia kupinga pendekezo hilo lakini baadaye ikaamua kuongeza maandishi yake kwenye rasimu hiyo. Baada ya mkutano wa dharura kati ya wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo Alhamisi, makubaliano yalifikiwa ya kuongeza ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Libya hadi Januari 31. Wanachama hao ni Uingereza, China, Ufaransa, Russia na Marekani.



Rais Samia azidi kuwakosha UWT


 Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mwenyekiti wa jumuiya  ya wanawake ya Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe Bi, Scholastica Kevela amesema hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwataka viongozi wa dini kuzungumza na waumini wao kuhusu umuhimu wa chanjo ya Covid-19 ni jambo la kupongezwa kwa kuwa limelenga kulinda Afya za watanzania.


Akizungumzia suala hilo,kwa niaba ya UWT Njombe, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Scolastika Kevela alisema Rais Samia alishawahi kusema kuwa Tanzania haipaswi kujitenga dhidi ya juhudi zinazofanywa na Dunia nzima kupambana na ugonjwa huo.


Alisema hata alipolihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UN na kutoa hotuba ya kuvutia na yenye kuliheshimisha Taifa, Rais Samia pia hakuacha kugusia  pia suala la Covid-19,  kutokana na kutambua umuhimu wa kujilinda


"Rais  Samia hivi karibuni amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye makao makuu ya umoja huo jijini New York ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia mapambano ya ugonjwa huo, hilo ni suala ambalo viongozi wa dini wanapaswa kumuunga mkono" alisema Mama Kevela


Awali akihutubia Baraza la UN lenye makazi yake New York nchini Marekani ikiwa ni mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo  Machi mwaka huu, Rais Samia alimulika masuala mbalimbali kuanzia uchumi, siasa, tabianchi, COVID-19 na usawa wa jinsia. 


Hata hivyo kutokana na hotuba hiyo,   Mwenyekiti huyo wa UWT alisema hotuba ya Rais Samia iliwagusa siyo tu watanzania, bali watu wa mataifa mbalimbali  hasa kwa namna alivyogusia masuala muhimu yanayoendelea kigubika dunia na hasa namna alivyohimiza nguvu ya pamoja katika kuyatafutia majawabu masuala hayo.


"kauli yake ya kuitaka dunia kutoyaacha nyuma mataifa yanayoendelea katika vita ya kukabiliana na janga la maambukizi ya virusi vya corona kwa kuwa inaweza kusababisha kurudi nyuma kwa maendeleo ya Dunia kwa kasi ya ajabu  iwapo kila nchi itajichukulia njia yake katika kulishughulikia janga hilo, imeionyesha dunia kweli Tanzania ipo mstari wa mbele katika kukabiliana na janga hilo" alisema Mama Kevela.


" Ukweli na hakika Rais Samia aliipangilia vizuri hotuba yake mbele ya Baraza hilo la Umoja wa Mataifa, ameanza na mguu sahihi ndani ya chombo hicho cha kimataifa hivyo kuonyesha ubora katika nafasi yake  kama kiongozi wetu katika Taifa hili" alisema Scolastika 


Mbali na hilo alisema hatua ya Rais Samia kugusia pia hatua anazochukua katika kumwezesha mwanamke kupanda katika ngazi mbalimbali za uongozi na hatimaye kufikia shabaha ya uwiano sawa na mwanamme ni jambo lililoonyesha dhamira yake ya dhati mbele  ya Baraza hilo la kutekeleza matakwa ya kufikia malengo ya mkutano wa Beijing uliotaka uwiano sawa wa 50/50 kati ya mwanamme na mwanamke. 


"Kwetu sisi wana Jumuiya ya UWT Mkoa wa Njombe amezidi kutufanya tuendelee kujivunua nafasi yake kama Rais wetu, mbali na mambo mengi na mazuri aliyoyafanya katika Taifa hili kwa kipindi kifupi tangu aapishwe amevuka na kwenda mipaka ya mbali kuionyesha Dunia kuwa Tanzania ni nchi ya namna gani" alisema Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono  Auction Mart


Aidha wao kama wana Jumuiya hiyo kutoka Njombe watasimama naye pamoja wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake na kusisitiza kuwa Mwaka 2025 watampa miaka mingine mitano ya kuliongoza Taifa kwa kaulimbiu yao ya 'Samia mitano tena'



S-400: Ifahamu silaha inayozua hofu kati ya Marekani kwa Uturuki

 


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema katika mahojiano na runinga ya Marekani ya CBS kwamba serikali yake ina mpango wa kununua silaha nyengine aina ya S-400 kutoka kwa Urusi.


Lakini msemaji mmoja wa Idara ya serikali mara moja alijibu: Tunaionya Uturuki dhidi ya kununua silaha zaidi za kijeshi kutoka kwa Urusi.


Serikali ya Ankara inaonekana kupuuza onyo la Marekani kama ambavyo imekuwa ikifanya hapo awali.


Je Rais Erdogan alisema nini?

Akizungumza katika runinga hiyo ya CBS katika hotuba yake kwa taifa, mtangazaji Margeret Brennan alimuuliza swali hili .


"Inaonekana kana kwamba bado unataka kununua silaha nyengine aina ya S-400, je ni kweli?.


Akijibu Erdogan alisema: Tutanunua hivi karibuni . Hakuna mtu anaweza kuingilia masuala ya nchi nyengine .. "


Mtangazaji huyo alirejelea tena suali hilo akisema: Je unamaanisha ndio?. Erdogan alijibu mara moja: Unamaanisha nini? Ndio.


Jibu la Marekani

Kulingana na chombo cha habari cha Reuters , msemaji huyo wa idara ya masuala ya kigeni aliulizwa mara moja kuhusu jibu la serikali yake kufuatia matamshi hayo ya Erdogan.


"Tunaionya Uturuki, tunaonya kupitia viwango mbalimbali e kwamba kwasababu tayari anamiliki silaha hiyo hana haja ya kununua nyengine na hatutaki anunue silaha nyengine aina ya S-400 kutoka kwa Urusi.


Tutaweka vikwazo

"Tutaendelea kuiambia Uturuki kwa maelezo kwamba silaha yoyote itakayonunuliwa kutoka kwa Urusi itasababisha vikwazo zaidi mbali na vikwazo vilivyowekwa Disemba 2020'', alisema.


Msemaji huyo alisema kwamba Marekani inaichukulia Uturuki kama mshirika wake na kwamba inatazama njia za kuimarisha uhusiano wake zaidi na taifa hilo licha ya kwamba kuna tofauti ya maono.


Mwezi Disemba mwaka uliopita , wizara ya fedha nchini Marekani iliiwekea vikwazo Uturuki kuhusu hatua ya taifa hilo kununua silaha aina ya S-400 kutoka kwa Urusi.


Mwezi Aprili 2021, azimio la CAATSA lilianza kutumika na Uturuki ikapigwa marufuku kununua silaha kutoka Marekani.


Uturuki hutengeneza silaha za kisasa ambazo awali Ujerumani ilikuwa imezikataa.


Je ni aina gani ya silaha zilizonunuliwa na Uturuki ambazo zinahatarisha maisha ya Marekani?


Na ni kwanini Uturuki inataka kuongeza uwezo wake wa silaha za kijeshi?


Mataifa hayo mawili ni wanachama wa muungano wa NATO , ijapokuwa yana tofauti kubwa za kijeshi.


Uturuki kwa sasa ipo katika mazungumzo kununua silaha kutoka kwa Urusi , na inaonekana kwamba Ankara haitajali hatua ya Marekani kupinga uamuzi huo.


Erdogan alisema katika mahojiano na CBS kwamba alikuwa akituma ujumbe kwa rais Joe Biden.


"Namwambia Biden, hii ni muhimu. Tayari tumenunua ndege aina ya F35. Tuliwalipa Marekani $1.4b lakini haijaturudishia fedha hizo licha ya kuwalipa kununua ndege hizo. "


Siku ya Jumatano , rais Erdogan anatarajiwa kukutana na rais wa Urusi Vladmir Putin ambapo watazungumzia ununuzi wa silaha hizo pamoja na masuala mengine ikiwemo hali ilivyo kaskazini magharaibi mwa Syria.


Je silaha aina ya S-400 inafanya kazi vipi?





MAGAZETI YA LEO 1/10/2021

















 

Wanaume kabla ya kuoa huangalia mwanamke mwenye sifa hizi

 


Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.

Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.

Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.

Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.

1. Mwenye mapenzi ya kweli.

Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto hao ndio furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.

Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingiutamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.

Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.

Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.

Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.

2. Wenye tabia nzuri

Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja sualana kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya.

Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.

Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.

3. Mwenye uchu wa maendeleo

Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani ‘golikipa’. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini.

Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.

4. Wasiopenda makuu.

Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia “leo tunakwenda wapi dear?”

Akimuona rafiki yake kanunua simuya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia,”mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.

Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’

Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.

Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leoamemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.

Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitajiupo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulaniwakati inawezekana uwezekano haupo.

5. Wavumilivu.

Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.

Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?

Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.

Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.



Baba yake Britney Spears azuiwa kusimamia mali yake- Mahakama


Jaji amemsimamisha baba wa Britney Spears kutoka kwa utaratibu wa kisheria ambao ulimpa udhibiti wa maisha yake baada ya Spears kumshtaki kwa kumnyanyasa kwa miaka kadhaa.

Jamie Spears aliteuliwa kuwa mlezi wake mnamo 2008, wakati kulikuwa na wasiwasi juu ya afya yake ya akili. Siku ya Jumatano, jaji alimpa jukumu hilo mtu aliyeteuliwa na Spears.

Bwana Spears, ambaye anakanusha unyanyasaji wowote, alikuwa amewasilisha la kuwa na nguvu zaidi katika udhibiti wa fedha za binti yake baada ya Spears kuomba mtunzaji mwingine.

Masjabiko kutoka maeneo tofauti duniani wamekuwa wakimuunga mkono kupitia kampeni ya #FreeBritney.

Uhifadhi hutolewa na mahakama kwa watu ambao hawawezi kufanya maamuzi yao, kama wale walio na matatizo ya akili au magonjwa mengine ya akili.

 



Waziri wa Afya azindua kiwanda cha kuzalisha Barakoa




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk Dorothy Gwajima amezindua Kiwanda cha Vifaa Tiba Mony Industries chenye uwezo wa kuzalisha Barakoa 100 kwa dakika Moja.

Katika uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo Uvumba Street-Kigamboni, Waziri Gwajima amesema
Alisema..“ Nipende kuwajulisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia ipo katika kuunga mkono juhudi hizi kwani imeweka kipaumbele katika sekta ya afya,

“Vile vile nitoe wito kwa wanachi wa Tanzania kuzingatia umuhimu wa afya zao binafsi kwani takwimu zinaonesha kuwa magonjwa yasiyoambukiza yanachangia asilimia 27 ya vifo vyote vinavyotokea nchini,”- Waziri wa Afya

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mony Industries, Violet Mordichai alielezea kwa kina ubora wa bidhaa zinazotokana na kiwanda hicho zinazofanya kiwanda hicho kuwa na uwezo wa kuhimili ushindani wa ndani na nje ya nchi

“Tuna mashine 7 za kisasa zenye uwezo wa kuzalisha barakoa 100 kwa dakika 1 huku kikiwa na uwezo wa kuzalisha Barakoa za Hospitalini (Surgical Masks), Viwandani (KN 95) na za Umma kwa Ujumla (Medical Masks). Na hivi karibuni kitaanza kutengeneze glavu za (Surgical na Medical), kwa hivyo kuweza kuhimili soko la ndani na la kimataifa ikiwa ni mpango wa hivi karibuni”- Mkurugenzi

 



Samia: Tutaliangalia hili la matokeo masomo ya dini


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inakwenda kuliangalia suala la kutotambuliwa kwa vyuo vinavyofundisha masomo ya Biblia na theolojia katika mabadiliko ya sera ya elimu yanayofanyika sasa.

Ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Kanisa la Anglikana Tanzania yaliyokwenda sambamba na kongamano la maaskofu na wachungaji wa kanisa hilo.

Kauli hiyo ilitokana na ombi la Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania, Dk Maimbo Mndolwa la kutaka Serikali kutambua elimu ya dini inayotolewa katika vyuo vinavyomilikiwa na kanisa hilo nchini.

Dk Mndolwa alibainisha mambo mbalimbali ambayo kanisa lake linafanya katika sekta za afya, elimu na ulinzi, huku akiiomba Serikali pia iangalie suala la kodi katika huduma zinazotolewa na taasisi za dini.

Rais Samia alisema Serikali imelichukua suala la kutotambuliwa kwa vyuo vya kufundishia Biblia na Theolojia na baadaye watatoa mrejesho wa suala hilo.

“Niseme tunayachukua, tutayaangalia na tutaleta mrejesho. Hii siyo kwa Anglikana pekee, ni kwa taasisi za dini zinazofundisha dini zote, bado hatujaziweka kuzitambua kwenye mitaala yetu au tunapofanya tathmini ya kuhitimu watoto wetu wa Kitanzania.

“Kwa hiyo tunapokwenda kuiangalia sera ya elimu ambayo tunaiangalia sasa, tutakwenda kuliangalia tuone uzito wake halafu tutaleta mrejesho kwa dini zote na madhehebu yote,” alisema kiongozi huyo.

Wakati huohuo, Rais Samia aliwataka viongozi wa dini kuwahimiza wananchi kwenda kupata chanjo ya Uviko-19 sambamba na kushiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwakani.

Alisema imezoeleka Serikali ikitoa matamko ya shughuli kama hizo, anatokea kiongozi wa dini anaanza kupinga wakati mafundisho ya kwenye kitabu chake hayamtumi kufanya hivyo.

“Naomba sana, nendeni mkatuhimizie zoezi la sensa, lakini pia mpige kampeni ya kutosha kwenye suala la Uviko-19. Ukweli ni kwamba chanjo zinapunguza vifo, lakini pia inapunguza makali ya lile gonjwa,” alisema Rais Samia.

Alisisitiza kwamba viongozi wa dini wawaelimishe waumini wao ili wakubali kuchanja kwa hiari yao baada ya kuelimishwa na kuelewa kwamba wakichanja watapata nini na asipochanja anakosa nini.

Hata hivyo, kauli hii ya Rais inakuja ikiwa ni siku mbili tu kupita, alipotoa maelekezo ya kuanza kufanyika kampeni ya kitaifa ya kuelimisha jamii kuhusu chanjo ya Uviko-19 alipokuwa akizindua mkutano mkuu maalumu wa ALAT jijini Dodoma.

Rais alisema kwa kufanya hivyo, kutasaidia wananchi wahamasike kuchanja.

Alitaka ushirikishwaji wa makundi mbalimbali upewa kipaumbele kwenye kampeni hiyo.

Lakini pia jana watumiaji mbalimbali wa simu za mkononi walianza kupokea ujumbe mfupi unaohamasisha watu kuchanja.

Ujumbe huo unasomeka, “Chanjo ya Uviko-19 itakukinga na ugonjwa, kulazwa na hatari ya kifo. Fanya uamuzi wa kupata chanjo. Wahi sasa okoa maisha”.


Usawa wa kijinsia

Kuhusu usawa wa kijinsia, Rais Samia alilitaka Kanisa la Anglikana kuwekeza nguvu katika kujenga heshima ya mwanamke wa Kitanzania.

Alisema Serikali imedhamiria kwa dhati kuwainua wanawake kijamii, kiuchumi na kisiasa na pia kupambana na ukatili, kejeli na manyanyaso dhidi ya wanawake na watoto.

“Tunafanya hivyo siyo kwa ajili mimi ni Rais mwanamke, la hasha. Tunafanya hivyo kwa sababu mwanamke ni kiumbe mwenye haki sawa na kiumbe mwingine anayezaliwa na mwanadamu.

“Wote tunazaliwa sawa, kinachotutofautisha ni makuzi na imani katika makabila yetu na imani mbalimbali. Kwa hiyo mwanamke ana haki sawa na mwanamume katika jamii,” amesema Rais Samia.

Awali akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Dk Mndolwa aliitaka serikali kwenda kuangalia suala la kodi kwa taasisi za dini kwa jicho la huruma kwa sababu inatishia baadhi yao kutaka kufunga huduma.

Pia, aliitaka serikali iboreshe mifumo ya utoaji vibali vya huduma mbalimbali, mathalani vibali vya kuanzishwa kwa dayosisi na vibali vya kuanzisha vituo ili viendelee kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi.

“Kuna changamoto ya kanisa kutakiwa kulipa kodi kiasi zinazotishia kufunga baadhi ya huduma zetu. Sisi tunafanya ni ibada, mfano hospitali na shule za jamii, pamoja na kwamba zinatoa huduma, lakini zinatakiwa kulipa kodi kwa serikali na kodi nyingine ambazo haziendani kabisa na mapato ya hospitali.

“Tunafurahi kwamba Serikali yako inayaangalia masuala haya, lakini tukuombe utuangalie kwa jicho la huruma kwa sababu inapelekea baadhi ya taasisi hizi kustruggle sana katika kujiendesha,” alisema Askofu Mndolwa.

Akijibu hoja hiyo, Rais Samia alisema ameagiza watu wake kufanya tathmini upya ili kubaini taasisi za dini zinazotoa huduma na zile zinazofanya biashara.

Alisema taasisi zinazofanya biashara lazima zilipe kodi katika sehemu ya faida wanayoipata.

 



TAMBUA DALILI ZA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME NA TIBA YAKE, PIA TAMBUA DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE

  


Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo kikamilifu shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili,homon,Neva,misuli,hisia na miriji ya damu


DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


1kuwahi kufika kileleni,2kukosa hamu ya tendo 3kushindwa kurudia tendo la ndoa 4uume kusimama kwa uregevu au kushindwa kusimama 5 kuchoka Sana baada ya tendo la ndoa


TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME


Dawa ya MJN ni dawa ya asili isiyokuwa na mkemikali yoyote dawa hii ipo kwenye mfumo wa kunywa na kuchua pia dawa hii ni tamu Sana kwani imechanganywa na asari ni tofauti na  ulizowahi kutumia usaidia ata wazee wenye miaka 80 pi uboresha uume wa mwanaume ulioingia ndani na kuwa mfupi


DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE


1. kunywa maji mengi Sana Kila wakati

2. kwenda  haja ndogo Mara kwa Mara

3. kuwa dhaifu ,kukosa nguvu na kijisikia mchovu kila wakati

4. kupunguza uzito au kukonda ata Kama unakula

5. kutoona vizuri

6. mwili kufa gazi hasa miguni 

7. vidonda au majeraha sehemu ya mwili kutopona 

8 kupungukiwa nguvu za kiume nk


MTN ndio dawa ya kisukari dawa hii inatibu tatizo mojakwamoja endipo ukidhingatia matumizi yake ni dawa isiyokuwa na masharti magumu kwa mtumiaji,pia zipo dawa za vidonda vya tumbo,presha,ngiri,chango la uzazi, miguu kuuma na mgongo nk


WASILIANA NAMI TABIBU DITTU KWA SIMU 0743362017  AU Whatsapp +255714448999 ofisi ipo mbagara sabasaba walio nje ya mkoa utalipia nauri ya mzigo tu sh elfu 12 ukipokea mzigo wako ndio utume pesa



MAFUNZO YA UJASIRIAMALI, JIFUNZE KUTENGENEZA VITU MBALIMBALI.

 


Star Entrepreneur General Inawaalika Wakazi Wote Wa Mkoa Wa Njombe Kwenye Kongamano la Mjasiriamali Supaa Litakalo Fanyika  Tarehe 4-8/10/2021 Katika ukumbi Wa Milimani Motel Muda Saa  2:00Asubuhi Mpaka saa 8:00 Mchana.


Mafunzo yatakayotolewa Ni :


Utengenezaji wa Sabuni Aina Zote


Batik Aina Zote Kuprint Tsheet na Mashuka


Utengenezaji Wa Keki za Sherehe, Tambi, Tomato Cause, Biscuit, Tea Masala


Ufugaji Wa Kuku Wa Aina Zote Na Samaki.


Ufungashaji na Uandaaji Wa Lebo.


Usimamizi Wa Biashara na Utafutaji Wa Masoko


Mafunzo Haya yote yatatolewa Kwa Gharama ya Shillingi 10,000/ Tuu


USAJILI UNAANZA IJUMAA TAREHE 1-4/10/2021 Saa 2:00 Asubuhi Mpaka Saa 11:00 Jioni.


WALENGWA NI WATU WOTE.


KWA MAWASILIANO PIGA NAMBA 0717656531 / 0753343335.


WATU WOTE MNAKARIBISHWA.
















RAO HEALTH TRAINING CENTRE RORYA YATANGAZA NAFASI ZA MASOMO

         


MKUU WA CHUO CHA RAO HEALTH TRAINING CENTRE RORYA ANATANGAZA KUPOKEA MAOMBI KWA MWAKA WA MASOMO 2021/2022 INTEK SEPTEMBER / OCTOBER.

 KATIKA KOZI ZIFUATAZO:
 1. ORDINARY DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE (AFISA TABIBU) MIAKA 3 SIFA ZA MWOMBAJI:

AWE NA UFAULU WA KIDATO CHA NNE KWA ANGALAU ALAMA 'D' IKIWEMO FIZIKIA'D' BIOLOJIA'D' KEMIA’D’ NA IKIWEMO HESABU NA ENGLISH NI KWA NYONGEZA KWA MASOMO MOJAWAPO.

 2. CETIFICATE IN IN CLINICAL MEDICIN (AFISATABUBU MSAIDIZI) MIAKA MIWILI

SIFA ZA MWOMBAJI:
AWE NA UFAULU WA KIDATO CHA NNE KWA MASOMO ANGALAU ALAMA 'D' IKIWEMO MASOMO YA FIZIKIA'D' BIOLOJIA 'D' CHEMIA'D' NA IKIWEMO HESABU NA KINGEREZA KWA MASOMO MOJAWAPO


FOMU ZINAPATIKANA CHUONI RAO MKOA WA MARA WILAYA YA RORYA AU KWENYE WEB SITE YETU www.raocoop.org

au wasiliana nasi kwa Email raohtc@raocoop.org au 0789232430 / 0621614530 / 0753624780 / 0753908726 / 0685085757

WAHI SASA NAFASI NI CHACHE!!!!!! ALL COREESPONDENCES BE ADDRESS TO THE DIRECTOR GENERAL.






Ole Nasha kuzikwa leo


Mwili wa aliyekuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), William Ole Nasha utazikwa Jumamosi kijijini kwake wilayani Ngorongoro, Arusha.

Ole Nasha, ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, na Elimu, Sayansi na Teknolojia alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi jijini Dodoma.

Akizungumza jana, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema: “Familia imeomba ndugu yao azikwe Jumamosi na sisi tumelipokea hili, tumeona halina shida na mwili utaagwa kitaifa leo saa tano asubuhi katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma”.

Wakati huohuo, mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Arusha yamepokea kwa mshtuko kifo cha Ole Nasha, yakisema alikuwa na mchango mkubwa.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Mashirika ya Wafugaji, Wawindaji na Waokota Matunda (PINGOs Forum), Edward Porokwa alisema mara ya mwisho kuwasiliana naye ilikuwa Jumapili iliyopita.

“Katika maisha yake Nasha nitamkumbuka kwa uchapakazi, alipenda kuona maendeleo katika jamii yake na Tanzania kwa ujumla,” alisema Porokwa.

Mratibu wa Mtandao wa Mashirika ya Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa alisema watamkumbuka Nasha kwa kuwaunganisha wananchi wa Ngorongoro na kuwapa taarifa za maendeleo ya jimbo hilo katika kundi WhatsApp.

Ofisa miradi wa shirika la Wanahabari la Watetezi wa Jamii za Pembezoni (Maipac), Andrea Ngobole alisema Ole Nasha alikuwa kiungo muhimu cha shirika hilo na wananchi na muda mwingi alishauri.

Mkurugenzi wa shirika la Utafiti, Maendeleo na Huduma kwa Jamii (Cords), Lilian Looloitai alisema kifo cha Ole Nasha ni pigo sio kwa wana-Ngorongoro pekee, bali jamii nzima, kwani alikuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya wananchi anaowawakilisha.

 



Kenya yatangaza msako dhdi ya wahamiaji haramu


Serikali ya Kenya imetangaza msako dhidi ya raia wa kigeni walio nchini humo kiharamu.

Hii ni baada ya hofu kuzuka juu ya ongezeko la makundi ya raia wa kigeni- wengi wao kutoka bara Asia ambao wameonekana katika maeneo ya makazi jijini Nairobi.

Takwimu iliyotolewa na wizara mambo ya ndani zinaonesha kuwa zaidi ya raia wa kigeni 20,000 wameinga nchini tangu mwezi Juni. Karibu 8,000 kati yao wameondoka.

Katibu katika Wizara ya Mambo ya ndani, Karanja Kibicho, alisema wageni hao wako njiani kuelekea Saudi Arabia kwa kazi.

Saudi Arabia imejumuisha nchi kadhaa za Asia katika orodha nyekundu, ambayo ilibuniwa kuzuia kusambazwa kwa virusi vya corona.

Bw. Kibicho hata hivyo amesema Kenya inakabiliwa na tishio la kuenea zaidi kwa virusi vya Covid-19 ndiposa inataka kudhibiti idadi ya watu wanaopita nchini hiyo.

Raia hao wa kigeni wanaishi Nairobi na jimbo jirani la Machakos.

Vyama vya wakaazi vimekuwa vikihoji ikiwa wageni hao wanazingatia kanuni zilizowekwa za kudhibiti maambukizi ya Covid-19 kama vile kuvaa barakoa.

 



Mbunge Ndejembi afanikisha upatikanaji wa Sh Milioni 103 za ujenzi wa Sekondari


NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma, Deo Ndejembi amefanikisha upatikanaji wa kiasi cha Sh Milioni 103 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa manne na matundu 10 ya vyoo kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Kata ya Zajilwa.

Kiasi hicho cha fedha kitakamilisha ujenzi wa Madarasa hayo pamoja na samani zake kwa maana ya madawati na ambapo pia matundu hayo 10 nane yatakua ya wanafunzi na mawili ya walimu.

Ndejembi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Zajilwa akiwa kwenye ziara yake ya kuzungumza na wananchi ambapo amewahakikishia kuwa ukamilishaji wa umeme kwa baadhi ya vijiji vya Kata hiyo utaanza Oktoba mwaka huu.

"Nichukue fursa hii kwa niaba yenu kumshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TASAF kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha hizi ambazo zitakwenda kukamilisha madarasa haya manne, matundu 10 ya vyoo na haya madarasa siyo majengo tu yatakua na Viti na Meza, haya yote nimefanya kama Mbunge wenu kuwatua mzigo wa kuchangishana kila siku kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari.

Kupitia fedha hizi tunakwenda kukamilisha ujenzi wa Shule hii ambayo niliahidi kipindi cha kampeni na sasa tunatekeleza, hii ndio kazi ambayo niliwaomba na ni lazima niitekeleze kwa nguvu na kasi," Amesema Ndejembi.

Kuhusu changamoto ya miundombinu ambayo kwa kipindi kirefu imekuepo kwenye Kata hiyo, Ndejembi amesema tayari washapokea Sh Bilioni 1.5 kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Barabara hivyo fedha hizo zimeshafika kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Wilaya ya Chamwino na tayari mkandarasi ameshaanza kazi.

"Kipekee nimpongeze Rais Samia kwa kutupatia kiasi hicho cha fedha ambacho alitoa kwa majimbo yote nchini, hivyo Mimi baada ya TARURA kunishirikisha nikasema sasa ni wakati Tarafa hii ya Itiso ambayo Zajilwa Iko ndani yake kumaliza changamoto hiyo ya Barabara.

Kwa kusema hivyo tayari mkandarasi yupo kazini tunaanza kutengeneza njia panda,itapita hapa Zajilwa kuelekea Gwandi na kutokea Haneti ni Barabara nzuri ambayo itapitika kwa nyakati zote haya yote ni matokeo ya fedha ambazo tumepatiwa na Rais wetu Samia tunamshukuru sana," Amesema Ndejembi.



Mahakama ya juu ya Ulaya yafuta mikataba na Morocco


Mahakama ya juu ya Umoja wa Ulaya imeifuta mikataba miwili ya biashara na Morocco, ambayo ilikuwa inairuhusu nchi hiyo kufanya biashara zake kutoka Sahara Magharibi. Uamuzi huo unaweza kuharibu uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Morocco.
 
 Mahakama ya Haki ya Ulaya, ECJ imesema hatua ya kufuta mikataba ya kilimo na uvuvi imechukuliwa baada ya vuguvugu la kisiasa la Polisario linalodai uhuru wa Sahara Magharibi, kufungua kesi kuipinga mikataba hiyo iliyosainiwa mwaka 2019. 
 
Morocco inalidhibiti eneo la Sahara Magharibi, lakini Algeria imekuwa ikiiunga mkono Polisario. Mahakama hiyo imebaini kuwa chama cha Polisario kilikuwa kinatambuliwa kimataifa kama mwakilishi wa watu wa Sahara Magharibi na Umoja wa Ulaya haukuhakikisha kuwa umepata idhini ya watu wa Saharawi kabla ya kufikia makubaliano na Morocco.

 



Merkel ampongeza Olaf Scholz


Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amempongeza mgombea wa ukansela wa chama cha Social Democratic, SPD Olaf Scholz kwa kushinda uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili. 
 
Taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya Merkel imeeleza kuwa kansela huyo anayeondoka madarakani, aliwasiliana binafsi na Scholz waziri wake wa fedha, siku ya Jumatatu.
 
 Ofisi hiyo pia imesema Merkel na mawaziri wataendelea na majukumu yao hadi serikali mpya ya shirikisho itakapoundwa na kuchukua rasmi madaraka. 
 
Kansela Merkel ataendelea kutekeleza majukumu yake ikiwemo kufanya ziara za nje na kuhudhuria mikutano ya viongozi wa serikali wa nchi nyingine. 
 
Aidha, shirika la habari la Ufaransa, AFP limeripoti kuwa kiongozi wa CDU, Armin Laschet pia amempongeza Scholz.

 



Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...