Search This Blog

Thursday, September 30, 2021

UN kubaki Libya hadi Januari

 


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi limekubaliana kuendelea na shughuli za kisiasa nchini Libya hadi Januari 31, mwaka ujao. 


Wakati huo utakuwa muda mfupi baada ya taifa hilo kufanya uchaguzi wa rais. Baraza hilo lenye wanachama 15 limekuwa likishauriana kuhusu kuongeza jukumu lake la kisiasa nchini humo hadi Decemba 24 ambapo uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika.


Hata hivyo kulitokea mvutano mkali kati ya Uingereza na Russia kuhusiana na pendekezo hilo. Moscow ililamamikia lugha iliyokuwa kwenye rasimu ya mapendekezo, na ilioandikiwa London ikisema kwamba vikosi vya kigeni pamoja na mamluki nchini Libya waondoke pamoja na sehemu inayoeleza jukumu la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo.


Jumatano Russia ilitishia kupinga pendekezo hilo lakini baadaye ikaamua kuongeza maandishi yake kwenye rasimu hiyo. Baada ya mkutano wa dharura kati ya wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo Alhamisi, makubaliano yalifikiwa ya kuongeza ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Libya hadi Januari 31. Wanachama hao ni Uingereza, China, Ufaransa, Russia na Marekani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...