Search This Blog

Monday, November 30, 2020

Ngorongoro Heroes kibaruani tena baada ya kufuzu Afcon


 USHINDI walioupata jana, Ngorongoro Heroes wa bao 1-0 dhidi ya Sudani Kusini umewapa nafasi ya kutinga michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Vijana chini ya miaka 20.(Afcon)

Bao pekee la Ngorongoro lilipatikana dakika ya 55 kupitia kwa Kassim Shaban baada ya kipa wa timu hiyo kutema mpira uliopigwa na Kelvin John.

Kesho Desemba 2 inatarajiwa kuwa fainali kati ya Ngorongoro Heroes ambao ni wenyeji dhidi ya Uganda ambao walishinda mabao 3-1 dhidi ya Kenya kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Black Rhino, Karatu.

Afcon ya vijana inatarajiwa kufanyika nchini Mauritania mwakani, ambapo kupitia michuano ya Cecafa inayoshirikisha timu za Afrika Mashariki na Kati Ngorongoro Heroes imepata tiketi hiyo.

Nahodha wa Ngorongoro Heroes, Kelvin John amesema kuwa ushindi ambao waliupata jana ni zawadi kwa mashabiki hivyo watapambana kesho kupata ushindi mbele ya Uganda kwenye hatua ya fainali.



Mwanasayansi wa Iran 'aliuliwa kwa silaha iliyoongozwa mbali na tukio


Mkuu wa masuala ya usalama Ali Shamkhani alisema kuwa washambuliaji walikuwa "wametumia kifaa cha kielekroniki " wakati gari la Fakhrizadeh lilipofyatuliwa mashariki mwa mji mkuu Tehran.

Alikuwa akizungumza katika mazishi ya mwanasayansi huyo ambaye Israeli ilimshutumu kwa kusaidia kisiri kutengeneza silaha za nyuklia.

Israel haijatoa kauli yoyote wazi kuhusu madai ya uhusika wake.

Iran inaamini kuwa Israel na kikundi cha upinzandi walitumia silaha ya kielektroniki (remote control)kumpiga risasi mwanasayansi wa ngazi ya juu wa nyuklia Mohsen Fakhrizadeh Ijumaa.


Iran yailaumu Israel kwa mauaji ya mwanasayansi wake wa nyuklia

Katika miaka ya 2000, Fakhrizadeh alikuwa na mchango mkubwa katika mpango wa nyuklia wa Iran, lakini mwanasayansi huyo wa serikali amekuwa akisisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia wote ni wa amani.

Iran imekuwa ikiwekewa vikwazo na mataifa ya magharibi kwa lengo la kuizuia kutengeneza silaha zaq nyuklia.



Wafungwa 8 wafariki kwenye ghasia zilizozuka ndani ya gereza la Mahara nchini Sri Lanka


Wafungwa 8 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 45 kujeruhiwa kufuatia ghasia zilizozuka ndani ya gereza moja lenye ulinzi mkali lililoko katika Jimbo la Magharibi mwa Sri Lanka.

Msemaji wa Idara ya Usalama Ajith Rohana,  alieleza kuwa wafungwa wa gereza la Mahara lenye ulinzi mkali lililoko umbali wa kilomita 15 kaskazini mwa mji mkuu wa Colombo, walisababisha ghasia na vurugu ndani.

Akifahamisha kuwa mamia ya wafungwa walijaribu kudhibiti hali ya gereza na kutoroka, Rohana alisema walinzi walifyatua risasi ili kukabiliana nao.

Rohana aliongezea kusema kuwa wafungwa 8 walipoteza maisha na wengine 45 kujeruhiwa kwenye ghasia zilizotokea ndani ya gereza la Mahara, ambalo ni moja ya magereza yenye wafungwa wengi zaidi nchini humo.

Wafungwa wengi pamoja na walinzi 2 wanaarifiwa kuwa kwenye hali mbaya, na vikosi vingi vya usalama vimepelekwa kwenye gereza hilo ili kudhibiti hali ya usalama.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya ndani, wafungwa hao walipinga ongezeko la kesi za maambukizi ya  virusi vya corona (Covid-19) gerezani, kudai waachiliwe mapema kwa dhamana na kutaka hali iboreshwe.

Wafungwa zaidi ya 2 wamepoteza maisha kwa covid-19 na wengine zaidi ya elfu moja kukutwa na kezi za maambukizi ya kwenye magereza 5 yenye idadi kubwa ya wafungwa katika miji tofauti ya nchi.



Rais Venezuela amechapisha nambari yake ya simu nambari yake ya simu mtandaoni


Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, amechapisha nambari yake ya simu mtandaoni kupitia akaunti yake ya Twitter, na kusema "Nialikeni kwenye vikundi vyenu."

Maduro alirekodi video na kutoa ujumbe uliosema,

"Venezuela, ninashiriki katika vita vya maoni kwenye vikundi vya WhatsApp na Telegram kwa nambari 04262168871. Nijumuisheni kwenye vikundi vyenu vyote na tupambane pamoja kutetea Venezuela."

Katika nambari hiyo aliyoitoa, ilionekana kuwa na picha yake Rais Maduro iliyobeba maneno yanayosoma "Rais wa Venezuela" kwenye profile ya WhatsApp na Telegram.

Maduro pia alichapisha video za ujumbe aliotumiwa kwake kupitia akaunti kituo rasmi cha Telegram.  

Maduro alimalizia kusema, "Mapokezi yamekuwa makubwa sana, maelfu ya vikundi vimenijumuisha."



Serikali yawataka waliohujumu mali za ushirika kurudisha kwa hiari


Serikali imewataka watu wote waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha na kurudisha malihizo kwa hiari kabla ya kuchukuliwa hatua za Kisheria. 

Kauli hiyo imetolewa  jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald  Kusaya  wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL).

 Kusaya amesema kuwa  mali zote za vyama vya ushirika zilizochukuliwa bila kufuata utaratibu zitarudi kwenye mikono ya serikali.

Aidha,amebainisha kuwa wamefanikiwa kurejesha mikononi mwa  serikali mali 59 za ushirika zilizochukuliwa bila kufuata utaratibu kuna viwanja,, majumba, mitambo na vingine vyote vina thamani ya bilioni 68.9 na zoezi ni endelevu.

“Kama kuna mtu ana mali za ushirika kwa njia zisizo sahihi azirudishe kwa hiari bila hivyo tuna nguvu nyingi za ziada haijalishi zipo wapi lazima tutazipata,” amesema Kusaya.

Kusaya ameendelea kubainisha kuwq serikali itakuwa bega kwa bega na benki hiyo ua ushirika ya Kilimanjaro ili kuhakikisha inazaa matunda kwa manufaa ya Watanzania.

“Kama tunaamini katika ushirika lazima tuuheshimu  na kulenga kufanya ushirika wa kibiashara katika kumkomboa Mtanzania tunataka kila mwanaushirika awe bilionea,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya KCBL, Dk Gervas Machimu amesema benki hiyo iko imara kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt.Machimu amesema kuwa wameweza kushirikiana na Benki ya CRDB na wana bodi ya pamoja kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.

Hata hivyo ameelezea kuwa Serikali inayo ndoto ya kuendeleza viwanda katika nchi na kutoa huduma katika kilimo na biashara na uwepo wa benki hiyo utasaidia kuendeleza  sekta za uzalishaji na kusaidia zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanaotegemea kilimo kunufaika.

Naye Mrajisi wa vyama vya ushirika Dk Benson Ndiege amesema kuwa KCLB ni chama cha ushirika kilichoandikishwa kama benki na kimepata leseni ya kuhudumu kama benki ya ushirika kwa wananchi wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga katika kilimo cha kahawa.

Amebainisha kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo, ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na benki ya CRDB wamefanya kila liwezekanalo ili benki isimame na kuhudumia makundi mbalimbali kama wakulima, wafugaji, wavuvi, wajasiriamali, wafugaji.

“Kama tukiamua leo kuikuza benki hii kwa kununua hisa tunaweza kuifikisha mbali, vyama vikuu vya ushirika viko 46  lakini vinavyofanya kazi vizuri viko 30,” amesema 

Amesema benki ya ushirika ya Kenya inafanya vizuri kutokana na uwezezaji uliofanyika na Tanzania ikiamua jambo hilo hakuna linaloshindikana.

“Kama tukifanya mabadiliko kwenye sekta ya kilimo, viwanda na uvuvi kama walivyofanya Kenya na kwenye benki ya ushirika wana uwekezaji ndio maana wamefanikiwa na benki yao ni ya tatu kwa ukubwa Kenya,” amesisitiza Dk.Ndiege

 Mwenyekiti wa Kilimanjaro Development Forum (KDF), Dk. Abubakar Ibrahim amevitaka vyama vya ushirika kuchangamkia fursa ya uwekezaji kwenye vyama hivyo.

Amesema  wanachama wengi wa KDF wamewekeza kwenye benki hiyo.

Ofisa Mkuu wa biashara wa CRDB, Dk. Joseph Witts amesema  kuwa CRDB iliundwa na ushirika na baadaye kuwa benki ya biashara.

Amesema wana kitengo cha kutoa mikopo kwa wakulima na wazalishaji mbalimbali.

“Mikopo yote tunayoitoa kwenye kwenye vyama vya ushirika   inalipwa vizuri,” alisema

Amebainisha wametoa bilioni saba kama mtaji kwenye benki ya KCBL.

Amesema CRDB ina menejimenti ndani ya benki hiyo na  wajumbe wa bodi ya CRDB wengine wako kwenye benki ya KCBL ili kuweza kuborsha utendaji



Tetesi za soka kimataifa

 


Inter Milan wanataka kumleta mshambuliaji Mfaransa kutoka Chelsea Olivier Giroud, 34, kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita mwezi Januari, wakiwa na chaguo la kumnunua . (Tuttosport via Mail)

Lakini Inter Milan wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka mahasimu wa Serie Juventus, kwani meneja Andrea Pirlo anataka kuwaleta wachezaji wake mwezi Januari, akiwemo Giroud. (Ilbianconero via Calciomercato- in Italian)

Chelsea wataanzisha mazungumzo na mlinzi wa Bayern Munich David Alaba, 28, Januari wanataka kumsaini mchezaji huyo wa Austria kwa mkataba utakaomruhusu kuhama bila malipo wakati mkataba wake utakapokamilika msimu . (AS via Sun)

Manchester United wanamatumaini kwamba Villarreal wanaweza kushawishika kumchua mchezaji wao wa zamani mlinzi Muivorycoast Eric Bailly, kama sehemu ya mpango wao kumnunua kiungo wa kati-nyuma wa Uhispania Pau Torres, 23, kwa pauni milioni 60. (Team Talk)

Liverpool wataweza kusaini mkataba na mlinzi wa Ajax Perr Schuurs kama watatoa pauni milioni 27 kwa kijana huyo mwenye umri wa maika 21. (De Telegraaf via Liverpool Echo)

Tottenham wanamfuatilia kwa karibu mchezaji wa safu ya kati-nyuma Sassuolo , Gian Marco Ferrari, 28, kabla ya uwezekano wa kuhamia Italia Januari . (90min)

Manchester United wanaweza kumnunua kiungo wa kati Inter Milan Christian Eriksen, 28, kama mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark international hatatakiwa na klabu yake ya zamani Tottenham. (Football Insider)

Barcelona walikataa dau la euro milioni 250 (£224m) kutoka Inter Milan kwa ajili ya Muargentina Lionel Messi, 33, mwaka 2006, kulingana na rais wa zamani wa klabu hiyo Joan Laporta. (Football Italia)

Mlindalango wa Ufaransa na Fulham Alphonse Areola, 27, anasema alikataa maombi ya kujiunga na klabu kadhaa ikiwa ni pamoja na Real Madrid na Paris St-Germain kwa kuwa alipendelea kujiunga na klabu ya Primia Ligi . (Canal+ via Football London)

Uamuzi wa winga wa Rangers Ryan Kent wa kubadili mawakala katika msimu huu wa soka unaweza kumpelekea kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijhusishwa na klabu ya Leeds msimu uliopita kuihama , kulingana na meneja wa zamani Gers boss Alex McLeish. (Glasgow Evening Times)

Mchezaji wa safu ya kati Bayern Munich Javi Martinez, 32, amedokeza kuwa ataondoka klabu hiyo ya Championi Ligi ya Ujerumani wakati mkataba wake utakapoisha mwezi Juni mwaka ujao, " kujaribu kitu kingine kipya ". (Reuters via Eurosport)

Kiungo wa kati wa AZ Alkmaar Mohamed Taabouni, 18, yuko tayari kuhamia Italia au Uhispania Januari, huku klabu kadhaa zikimfukuzia kijana huyo kutoka timu ya kimataifa ya vijana chipukizi ya Uholanzi . (Voetbal International - in Dutch)

Newcastle wanaangalia uwezekano wa kusaini mkataba wa kudumu na mchezaji wa klabu ya Ujerumani ya Eintracht Frankfurt Jetro Willems, 26 baada ya mlinzi wao Mholanzi kulazimishwa kuondoa kipengele chake cha kucheza kwa mkopo katika mkataba wake katika St James' Park mwezi Januari kwasababu ya jeraha baya la goti . (Shields Gazette)



MAGAZETI YA LEO 1.12.2020

 

























Mpambano wa Mike Tyson dhidi ya Roy Jones Jr umeshindwa kumpata mbabe


 Mpambano wa masumbwi ambao ulikuwa wa hisani, baina ya Bingwa wa zamani wa Ndodi, Mike ‘Iron’ Tyson dhidi ya Roy Jones Jr umeshindwa  kumpata mbabe baada ya majaji kutangaza kuwa ni droo, mpambano huo ambao ulikuwa wa raundi nane, ulipigwa mwishoni mwa wikiendi jijini Los Angeles Marekani.

Mike Tyson, (54) ambaye ubingwa wake wa kwanza aliupata Miaka 36 iliopita baada ya kumtwanga Trevor Berbick, Las Vegas mwaka 1986 na kuweka rekodi ya kuwa bingwa wa uzani wa juu (Heavy weight) mdogo kutwaa mkanda huo.

Muda mwingi wa pambano hilo #RoyJones alionekana kuzidiwa na makonde aliyokuwa anarushiwa na Tyson.

Majaji waliwashangaza wengi, baada ya kutangaza matokeo kuwa ni sare, kwani wengi walidhani Tyson ameshinda kwa jinsi alivyotawala pambano hilo ambalo halikuwa la Ubingwa.

Tyson mara baada ya pambano alisema alikuwa anaona dakika mbili ni nyingi hiyo ni kutokana kutopanda ulingoni kwa muda kwa muda mrefu  pambano lake mwisho lilikuwa mwaka 2005 ambalo alipoteza dhidi ya Kevin McBride kwa KO na kuamua kutangaza kustaafu.




TAMWA yatoa neno uteuzi wa JPM


Mkurugenzi Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania, (TAMWA), Rose Reuben amesema amefurahishwa na uteuzi uliofanyawa na Rais John Magufuli, kwani umezingatia usawa wa kijinsia.

Bi.Rose amesema uteuzi wa Rais Magufuli unadhihirisha kuwa yale yote waliyokuwa wanasema kuhusiana na wanawake yalikuwa mambo ya msingi.

"Nimeufurahia uteuzi wa Rais John Magufuli kwasababu umeweza kukumbuka na kuelewa yale tuliyokuwa tukishawishi kwamba  upo umuhimu wa kuwaweka wanawake katika ngazi mbalimbali" amesema Rose Reuben

"Rais Magufuli aliahidi kutekeleza kuhusiana na kuwapatia ngazi za maamuzi wanawake na hivi sisi ameanza kutekeleza kwasababu kati ya wawili aliowateuwa jana moja ni mwanamke na mwingine ni mwanaume hivyo amezingatia usawa wa jinsia" ameongeza Bi.Rose

Aidha Bi Rose amewataka viongozi walioteuliwa kuzingatia misingi ya uongozi kwani wamefika hapo kwa ajili ya kuwatumikia watanzania na nyuma yao yupo mwanamke. hivyo waende wakaendeleza sera zitakazo wasaidia wanawake na kutatua matatizo yao.

Kauli ya Bi Rose inafuatia baada ya uteuzi wa Rais Magufuli siku ya jana ambapo aliwateua Bi. Riziki Said Lulida na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi (CCM),Humphrey Polepole, kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Rais wa TFF aipongeza kamati ya chama cha mpira wa miguu Dar

 





Vijana kadhaa wachukuliwa mateka Libya

Vikosi vya Khalifa Hafter vimeripotiwa kubomoa baadhi ya nyumba na kuwachukuwa mateka vijana kadhaa baada ya kuvamia mji wa Ubari nchini Libya. 

Taarifa hizo za uvamizi zilizotolewa na Ofisi ya Mawasiliano ya Operesheni ya Volcano inayosimamiwa na serikali ya Libya. 

Vyanzo vya ndani pia vimefahamisha kuwa vikosi vya Khalifa Hafter vilivamia mitaa ya Al-Sharib ya mji wa Ubari ambapo viliwatishia raia kwa silaha na kuondoka wakielekea mji wa Sebha wakiwa pamoja na vijana kadhaa wa kabila la Tuareg waliowachukuwa mateka. 

Mji wa Ubari ambao ni mji wa pili kwa ukubwa baada ya Sebha katika kanda ya kusini mwa Libya, idadi kubwa ya wakazi wake inajumuisha watu wa Kabila la Tuareg. 

Kwa muda mrefu sasa nchi ya Libya ambayo imekosa utulivu, vikosi vya Khalifa Hafter vilianza kuvamia mji mkuu wa Tripoli na kudhibiti utawala baada kumarishwa na kiongozi wao Aprili 2019. 



Mradi wa Maji Songea kukamilika ndani ya siku 60


Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ametoa miezi miwili kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji kijiji cha Litisha katika Halmashauri ya wilaya ya Songea.

Mhandisi Sanga ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi huo.

“Nimefurahi kuona kisima kinatoa maji mengi sana na tenki tayari limekamilika lakini, bado miundombinu ya kuwafikishia wananchi maji haijakamilika; maelekezo yangu ni kuwa, ndani ya siku 60 mradi huu uwe umekamilika na wananchi wawe wamepata huduma ya maji,” amesema Sanga...



Azam FC kibaruani tena leo na Biashara


 Klabu ya Azam Fc itashuka dimbani jioni ya leo huko mkoani Mara itakapokaribiana na Biashara ikiwa ni muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Mshambuliaji wa Azam Fc, Prince Dube (Pichani) atakosekana katika mchezo wa leo dhidi ya Biashara kutokana na kuumia mkono na ameelekea Afrika Kusini kupata matibabu zaidi.

Kikosi cha Azam kitakuwa kikiongozwa na kocha Vivier Bahati ambaye amekabidhiwa mikoba iliyoachwa na Aristica Cioba ambaye alifutwa kazi kufuatia mwenendo mbovu wa kikosi hicho.

Azam Fc walio katika nafasi ya pili wakiwa na alama 25, watakuwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 walichoambulia dhidi ya Yanga, lakini vilevile wakiwa wametoka kufungwa mechi mbili mfululizo za VPL kwa hivi karibuni.

Kwa upande wa Biashara ambao walianza vyema msimu huu, hawajawa na matokeo mazuri lakini katika mechi tano za mwisho, wameshinda moja pekee , sare mbili na vipigo viwili.



Somalia yamuita nyumbani balozi wake na kumfukuza wa Kenya


Serikali ya Somalia imesema kuwa imemuita nyumbani balozi wake nchini Kenya Mohamud Ahmed Nur Tarzan, na kuishutumu nchi hiyo kwa kuingilia siasa za nchi yake.

Somalia pia imemtaka balozi wa Kenya nchini Somalia kufunga virago "kwa ajili ya majadiliano".

Somalia imeishutumu Kenya kwa kushinikiza serikali ya Jubbaland kukataa makubaliano ya uchaguzi yaliofikiwa Septemba 17, katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwezi ujao.

"Serikali ya Somalia ilichukua uamuzi huo kulinda eneo lake la utawala baada ya kujitokeza kuwa Kenya inaingilia kimaksudi masuala ya Somalia eneo la Jubbaland," Mohamed Ali Nur, Waziri wa mambo ya nje wa Somalia amesema katika taarifa iliyotolewa.

"Serikali] ya Somalia imeonesha kusikitishwa kwake na serikali ya Kenya kwa kuingilia moja kwa moja masuala ya ndani ya siasa za Somalia hatua ambayo inaweza kuchangia ukosefu wa uthabiti, usalama na maendeleo kwa eneo zima,” taarifa hiyo imesema.

Kenya inaunga mkono utawala wa Ahmed Mohamed Islam maarufu kama "Madobe" huko Jubbaland, kwasababu ya maslahi yake ya kiusalama na kieneo.



Museveni ashutumu wanasiasa wa upinzani kupotosha vijana

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameshutumu waandamanaji na wanasiasa wa upinzani kwa kuwapotosha vijana kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.

Bwana Museveni amesema wazo la kuwa mheshimiwa Bobi Wine akikamatwa kutakuwa na ghasia lisirejee tena.

‘’Hakuna mwanasiasa ambaye ana mamlaka kuliko sheria’’, Museveni alisema.

Aliongeza kuwa wanasiasa wanalipa magenge ya uhalifu ambao wametangaza baadhi ya sehemu za mji wa Kampala eti hazitawaliki na hata kuvamia maafisa wa polisi wanaoshika doria.

Bwana Museveniameshutumu watu waliorekodiwa wakivamia maafisa wa usalama na waliokuwa wamevaa mavazi ya rangi ya njano inayoashiria chama tawala.

‘’Hili, halitawahi kutokea tena, kwasababu waliotekeleza hayo wameona matokeo ya kucheza na moto’’, amesema rais Museveni.

Bwana Museveni pia alisema kuwa ajenda za wanasiasa wa upinzani ni kupata uungwaji mkono kutoka nje ya nchi ambao nia yao ni kukosesha uthabiti nchi ya Uganda.

Rais Museveni aliongeza kuwa makosa makubwa ni wagombea urais walikiuka hatua zilizowekwa za kukabiliana na virusi vya corona na kutojali utekelezaji wa sheria.

Pia, alitoa risala zake za rambirambi kwa raia wa Uganda waliopoteza wapendwa wao wakati wa ghasia hizo na kuongeza kwamba serikali itawalipa fidia.

Bobi Wine anatafuta kumuondoa madarakani Museveni ambaye ametawala nchi hiyo kwa miaka 34 - katika uchaguzi utakaofanyika Januari 2021.



Madaktari waliotoa figo na maini ya marehemu wahukumiwa


Watu sita wakiwemo Madaktari wamefungwa gerezani nchini China kwa kutoa viungo vya mwili kinyume cha sheria kwa watu waliofariki kutokana na ajali, vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti juu ya hukumu hiyo.

Kundi hilo lilikuwa limelaghai familia za waliofariki kuwa wanachangia rasmi viungo vya mwili katika mashirika husika.

Kati ya mwaka 2017 na 2018 walitoa maini na figo kutoka kwa watu 11 katika hospitali ya Anhui.

Watuhumiwa hao sita wakiwemo Madaktari wanaohusika na ulanguzi huo wa viungo vya binadamu walisomewa mashtaka yao Julai mwaka huu kwa kosa la “kuharibu miili ya wafu kimaksudi” na kuhukumiwa kifungo cha kati ya miezi 10 na 28 gerezani.

China inakabiliana na upungufu wa viungo vya mwili na imekuwa na wakati mgumu kukidhi mahitaji ya raia.



Mtanzania aliyefungwa maisha ajiua Kenya


Taarifa kutoka nchini Kenya zinasema, Mtanzania aliyehukumiwa kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi lililotokea mwaka 2015 katika chuo kikuu kimoja nchini humo na kusababisha watu 148 kufariki, amejiua mwenyewe akiwa gerezani.

Washambuliaji wanne waliuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Kenya katika chuo Kikuu cha Garissa, lakini Mtanzania huyo, Rashid Charles Mberesero na wenzake wawili walikamatwa na mwaka jana na kuhukumiwa kwa kuhusika katika ugaidi.

Hukumu hiyo ilimpa, Mberesero kifungo cha maisha gerezani.

Taarifa zinasema alikuwa na matatizo ya akili wakati akiwa gerezani na alikuwa anamuona mtaalamu wa afya akiwa gerezani.

Gazeti la Daily Nation linasema Mberesero alijinyonga mwenyewe akiwa gerezani kwa kutumia blanketi lake.



Ben Pol afunguka kuhusu kupaka rangi kwenye kucha

 


Mwimbaji Staa wa Bongofleva mmiliki wa ngoma mpya mbili za ‘hii ndio mbaya’ na ‘walimwengu’ Ben Pol ameongea baada ya Watu kuongea kuhusu yeye kupaka rangi kwenye kucha za mkononi.

Ben Pol amesema “zile rangi zilizopo kwenye bendera ya Tanzania, nafikiri kitu kikubwa kinachosumbua wengi ni mazoea, kitu cha muhimu zaidi ni roho ya Mtu, hivi vitu vya kuchora na kupaka sio vya muhimu na sidhani kama ni vitu vinaweza kum-define Mtu”





Spika Ndugai kuwaapisha Polepole, Lulinda leo

 


Spika wa Bunge, Job Ndugai leo Jumatatu, Novemba 30, saa 9.00 alasiri atawaapisha wabunge wateule, Humphrey Polepole na Riziki Lulinda katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Polepole na Lulinda waliteuliwa Jana na Rais Dk.John Magufuli kuwa wabunge ikiwa ni sehemu ya nafasi 10 alizonazo rais kwa mujibu wa Katiba.



Alichokisema Mzee Msekwa kuhusu Spika Ndugai


Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kuwa hakuna ugumu wowote anaoweza kukutana nao Spika wa Bunge la 12, Job Ndugai, mara baada ya wabunge 19 wa CHADEMA, kufukuzwa uanachama kwa kuwa yeye ni kama daktari tu anayepokea wagonjwa kuwatibu kisha kuondoka.

Msekwa ameoa kauli hiyo  kufuatia sakata la wabunge 19 wa viti maalum ambao wamefukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA baada ya kwenda kula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama, ambapo alisisitiza kuwa kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni basi hata ubunge wao umekoma.

"Spika Ndugai hapati ugumu wowote, hakupata ugumu walipoletwa hapati ugumu wowte wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, hana ugumu na wala hafaidiki na lolote ni kama mganga wa hospitali yeye anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka, wakifa wanaondoka yeye hana jukumu zaidi ya hilo", amesema Spika Mstaafu, Pius Msekwa.



WHO: Mapambano ya malaria yanakwamishwa na COVID-19, fedha


Shirika la Afya Duniani, WHO limeonya kuwa kutokana na kulishughulikia zaidi janga la virusi vya corona huenda kukawa na hadi vifo 100,000 zaidi vitokanavyo na ugonjwa wa malaria kwa mwaka huu.

Katika ripoti yake ya mwaka kuhusu ugonjwa wa malaria duniani iliyotolewa leo Jumatatu, WHO imesema maendeleo ya kupambana na ugonjwa huo yamekwama katika miaka ya hivi karibuni hasa katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako kuna visa vingi pamoja na vifo.

WHO imesema mwaka 2019 kulikuwa na takriban maambukizi milioni 229 ya malaria duniani, takwimu ambazo zilikuwa sawa na za miaka minne iliyopita na kwamba vifo vya malaria vinaweza kuzidi vile vitokanavyo na janga la COVID-19, huku wengi wao wakiwa watoto.

Kwa mujibu wa shirika hilo, watu 409,000 duniani walikufa kwa ugonjwa wa malaria mwaka 2019, wengi wao wakiwa kutoka maeneo masikini ya Afrika, ikilinganishwa na watu 411,000 kwa mwaka 2018.

Hata hivyo, ripoti hiyo imegundua kuwa kampeni nyingi za kupambana na malaria ziliendelea wakati huu wa janga la virusi vya corona, lakini kuna wasiwasi kwamba juhudi za kukabiliana na malaria zinaingiliana na mzozo wa COVID-19 ambao unakwamisha juhudi hizo na kurudisha nyuma zaidi mapambano.

Mkurugenzi wa WHO anayehusika na mpango wa malaria, Pedro Alsonso, amesema kutokana na mzozo wa corona, nchi nyingi zimefunga mipaka yake na viwanda hatua ambayo pia inazuia au inakwamisha kupelekwa kwa vyandarua vya kujikinga na mbu pamoja na dawa za malaria.

Aidha, serikali zimezielekeza rasilimali zake katika kupambana na janga la COVID-19, ambazo pia zilikuwa ni gharama za kupambana na malaria.

Mkurugenzi wa WHO barani Afrika, Matshidiso Moeti amesema virusi vya corona vinatishia kukwamisha juhudi za kupambana na malaria. Moeti amesema licha ya COVID-19 kuuathiri uchumi wa Afrika, washirika wa kimataifa wanahitaji kuongeza juhudi kuhakikisha kwamba rasilimali zinaongezwa katika miradi ya malaria ambayo inaleta mabadiliko.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Gebreyesus amesema ni muda kwa viongozi wa Afrika na dunia kwa ujumla kuamka tena na kupambana na malaria. WHO imesema upungufu wa fedha za kupambana na malaria unaleta kitisho kikubwa, huku ikiwa na dola bilioni 3 kati ya dola bilioni 5.6 zilizochangishwa 2019.

Zaidi ya asilimia 90 ya ugonjwa huo uko barani Afrika, ambapo watu 384,000 walikufa mwaka uliopita. Nigeria ilikuwa na asilimia 27 ya vifo hivyo, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo asilimia 12, Uganda asilimia tano na Msumbiji asilimia nne.

Ripoti ya WHO imesema nchi 21 zimefanikiwa kuutokomeza ugonjwa wa malaria katika kipindi cha miongo miwili iliyopita. Nje ya Afrika, India imeendelea kupata faida kubwa katika miaka miwili iliyopita, huku ikipunguza asilimia 18 ya maambukizi na asilimia 20 ya vifo.

Peter Sands, Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa dunia wa kupambana na UKIMWI, kifua kikuu na malaria amesema ripoti ya WHO imetolewa kwa wakati unaofaa.



Sunday, November 29, 2020

Tetesi za soka kimataifa


 Kiungo wa kati Mjerumani Sami Khedira, 33, anasema anaweza kuhamia katika Primia Ligi wakati mkataba wake na Juventus utakapoisha msimu huu.

Aliongeza kuwa anaendelea kuwasiliana na mameneja wa Everton Carlo Ancelotti na wa Tottenham Jose Mourinho. (ZDF, via Mail)

Mkataba wa mlindalango wa AC Milan Gianluigi Donnarumma katika Serie A unamalizika mwaka 2021 lakini kijana huyo wa kimataifa Muitaliano mwenye umri wa miaka 21- anasema wakala wake ataongea na klabu na anataka kuendelea kubakia nao kwa "muda mrefu". (Football Italia)

Liverpool wamekuwa wakihusishwa na mlinzi wa Ajax Perr Schuurs, 21, lakini the Reds hawajafanya dau lolote kwa ajili ya Mholanzi huyo . (Voetbal Primeur - in Dutch)

Celtic wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Crystal Palace na Jamuhuri ya Ireland James McCarthy, lakini Aston Villa na Burnley pia wanamtaka kijana huyo mwenye umri wa miaka 30. (Teamtalk)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema "hashiri sana kuhusu wale watakaoingina na kutoka " wakati wa dirisha la uhamisho la wachezaji la mwezi wa Januari . (Evening Standard)

Viungo wa safu ya kati Wahispania Riqui Puig, 21, na Carles Alena, 22, wanapijgania hali zao za baadaye katika timu ya Barcelona sawa na mshambuliaji Mdenmark Martin Braithwaite, 29, na kiungo wa nyuma-kushoto Muhispania Junior Firpo, 24. (Marca)

Winga wa Ufaransa Florian Thauvin anasema ali "ondolewa " na mkurugenzi wa masuala ya kiufundi wa AC Milan Paolo Maldini akisema timu hiyo ya Serie A side iliitaka kumsaini . Mkataba wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 27-katika timu ya Ufaransa ya Marseille unaisha msimu ujao wa soka wa mwaka 2021. (Football Italia)

Juventus wanaweza kumlenga kiungo wa safu ya kati-nyuma wa Atletico Madrid na kiungo wa kati -nyuma wa Montenegro Stefan Savic, 29,ili kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Calciomercato)

Kiungo wa zamani wa safu ya nyuma-kushoto wa Brazil Roberto Carlos amesema mpango wake wa kuhamia Chelsea ulio "afikiwa" mwaka 2007 na ulivunjwa tu katika "nyakati za mwisho ". (Goal)

Barnsley wanaangalia kwa makini uwezekano wa kurefisha mkataba wa mkopo wa Leicester City kumuhusu mchezaji wa safu ya kati Matty James katika klabu hiyo, huku mkataba wa Muingerezaq huyo mwenye umri wa miaka 29 ukitarajiwa kumalizika mwezi wa Januari . (Leicestershire Live)




Baada ya kufanya mauaji Nigeria Simba kutua nchini kesho

 


Baada ya mchezo wa jana uliowafanya imu ya simba kuiwakilisha vizuri anzania kwa  kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya  Plateau United ya nchini Nigeria kikosi cha wawakilishi wa nchi kimaaifa leo jumatatu kitaanza safari kurudi Tanzania kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi Plateau United.

Safari itaanza alfajiri kutoka Jos hadi Abuja, mchana kikosi kitaondoka Abuja kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo kitafika usiku na kupumzika hapo. 

Hata hivyo kikosi hiko  kitatua Tanzania kaika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro siku ya jumanne saa 10:00 jioni.



Museveni atangaza kupata dawa ya virusi vya Corona


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza kupata tiba ya Corona Virus ambayo imegunduliwa na Wanasayansi wa Uganda

Katika hotuba yake kwa Taifa jana Jumapili, Museveni amesema Madaktari wanatumia mchanganyiko wa vitu maalum ambavyo vinaongeza kinga mwilini

Dawa hiyo ambayo amesema itaanza kutumika Desemba 15, imejaribiwa kwa Wagonjwa kadhaa wa COVID 19 nchini humo na wamepona

Pia, Wanasayansi wamegundua namna ya kupima COVID19 kwa kutumia mate ambapo majibu hutoka ndani ya dakika 30




Ngorongoro Heroes kibaruani leo dhidi ya Sudan Kusini


KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes,  Jamhuri Kihwelo amesema kuwa anaamini vijana watafanya vizuri leo Novemba 30 kwenye mchezo dhidi ya Sudan Kusini.

Mchezo wa leo ni hatua ya nusu fainali michuano ya Cecafa ambayo inafanyika Arusha,Tanzania ikiwa ni wenyeji.

Khiwelo amesema :"Tulicheza mechi nyingi za kirafiki kwa ajili ya maandalizi na sasa tupo kwenye hatua ngumu tupo tayari kupata ushindi, imani yetu ni kwamba tutafikia lengo letu.

"Mashindano ni magumu licha ya kwamba tulifanikiwa kushinda mechi mbili mpaka kufika hapa, kikubwa ni kwamba tunajua tuna mzigo mkubwa na mzito kwa ajili ya kufikia kile ambacho tunakihitaji.

"Ushirikiano umekuwa mkubwa kutoka kwa viongozi mpaka mashabiki hili linatupa nguvu ya kufanya vizuri katika mchezo wetu," .

Mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Black Rhino, Karatu,Arusha.




Papa Diop afariki Dunia


Kiungo mkabaji wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal Papa Bouba Diop ,42, amefariki dunia leo Paris nchini Ufaransa baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Diop bado vyanzo vingi vya habari havijaweka wazi sababu za kifo chake lakini inaripotiwa alikuwa akiugia kwa muda mrefu.

Papa Diop umaarufu mkubwa aliupata 2002 katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Korea na Japan baada ya kufunga goli na kuipa ushindi 1-0 wa Senegal dhidi ya Ufaransa ambao ndio walikuwa Mabingwa watetezi lakini walifika pia hatua ya robo fainali katika michuano hiyo huku Diop akifunga magoli mawili katika sare ya 3-3 dhidi ya Uruguay.

Papa Diop amewahi kucheza vilabu mbalimbali England kama Fulham, Portsmouth, West Ham United na Birmingham City, Diop alistaafu timu ya taifa 2008 na soka kwa ujumla alistaafu 2013.



Aliyekuwa daktari wa Maradona achunguzwa kuhusiana na kifo cha nyota huyo


Waendesha mashitaka nchini Argentina wanamchunguza daktari wa Diego Maradona kwa uwezekano wa kuua kufuatia kifo cha nyota huyo wa soka kilichotokea siku nne zilizopita .

Polisi mjini Buenos Aires wameisaka nyumba na kliniki ya daktari huyo- Leopoldo Luque huku wakijaribu kubaini iwapo ulikuwepo uzembe katika matibabu baada ya upasuaji aliofanyiwa Maradona.

Maradona ambaye alikuwa na umri wa miaka 60 alifariki dunia kutoka na shinikizo la damu nyumbani kwake ambako alikuwa akiendelea kupona baada ya kufanyiwa upasuaji.

Dokta Luque bado hajashitakiwa. Anakana kufanya kosa lolote.

Maradona alifanyiwa upasuaji kwenye mshipa wa ubongo kutokana na kujganda kwa damu , uliofanikiwa mapema mwezi wa Novemba na amekuwa akipata matibabu kutokana na uraibu wa pombe.

Binti yake alikuwa amesisitizia kupata taarifa zaidi kuhusu matibabu ya baba yao.



31 wauawa, 24 wajeruhiwa kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa nchini Afghanistan


Watu 31 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 24 kujeruhiwa kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa kwa kutumia gari mjini  Ghazni nchini Afghanistan.

Kulingana na taarifa za "Tolo News", Msemaji wa Ofisi ya Gavana ya Gazne Wahidullah Jumazada alitangaza kuwa shambulizi hilo la kutumia gari la bomu lilitekelezwa karibu na jengo la usalama wa umma mjini humo.

Jumazada alibainisha kuuawa kwa watu 31, na kujeruhiwa kwa watu wengine 24 kwenye shambulizi hilo.

Katika taarifa hiyo, ilibainishwa kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa kwa kutumia gari aina ya Humvee, ambalo lilijazwa vilipuzi vilivyolipuliwa kwenye jengo hilo lililokuwa na kikosi cha makomando.

Hakuna yeyote aliyedaiwa kuhusika na shambulizi hilo hadi kufikia sasa.




MAGAZETI YA LEO 30.11.2020

 

























Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...