Search This Blog

Thursday, December 31, 2020

Seneta wa Republican kupinga kuidhinishwa kwa kwa Joe Biden


Mwanachama wa Republican anasema kwamba atakuwa seneta wa kwanza kupinga wakati bunge la Congress litakapomuidhinisha rais mteule Joe Biden wiki ijayo.

Seneta wa Missouri Josh Hawley alisema kwamba alikuwa na wasiwasi wa maadili licha ya kutokuwa na ushahidi wa kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi uliopita.

Kundi moja la wanachama wa Republican katika bunge wawakiishi pia linapanga kupinga matokeo ya uchaguzi.

Lakini pingamizi hizo hazitarajiwa kubadilisha matokeo.

Baraza la wajumbe linaloidhinisha matokeo ya uchaguzi kwa kutoa pointi kwa kila jimbo lililoshindwa na wapinzani hao wawili mapema liliidhinisha ushindi wa rais mteule Joe Biden dhidi ya Trump kwa 306-232. Kura hiyo ni lazima zihakikiwe na bunge la Congress ifikiapo Januari 6 .

Siku ya kuapishwa kwa rais mteule na makamu wake itakuwa tarehe 20 Januari.

Tangu aliposhindwa katika uchaguzi, bwana Trump mara kadhaa amedai kwamba kulikuwa na udanganyifu wakati wa shughuli hiyo bila ya kutoa ushahidi.

Hatua za kisheria za rais huyo wa chama cha Republican kubadilisha matokeo zimekataliwa na mahakama.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...