Kimbunga Ida, mojawapo ya vimbunga vyenye nguvu kabisa kuwahi kupiga katika Ghuba ya Pwani ya Marekani kimekata umeme kwenye zaidi ya nyumba milioni 1 katika jimbo la Louisiana hapo jana.
Kimbunga hicho kiliwasili mjini New Orleans siku ya Jumapili kikiwa na kasi ya kiwango cha nne. Tangu jana Jumatatu, juhudi za uokozi zimekuwa zikiendelea huku mamia ya boti na helikota kikitafuta watu waliokwama kwenye mafuro yaliyosababishwa na kimbunga hicho.
Hadi sasa kumeripotiwa vifo vya watu wawili. Kimoja cha mwendesha pikipiki aliyezama kwenye mafuriko na cha pili cha mtu aliyeangukiwa na mti.
Miaka 16 iliyopita katika wakati sawa na sasa Kimbunga Katrina kilisababisha janga lililoua zaidi ya watu 1,800 New Orleans.

No comments:
Post a Comment