Search This Blog
Tuesday, March 31, 2020
Meneja wa Diamond apona Corona
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Sallam SK ameweka wazi kuwa sasa ni mzima baada ya siku 14 alizokuwa ametengwa kwa ajili ya matibabu kumalizika.
Sallam ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz amesema amefanyiwa vipimo mara kadhaa ya vyote vimeonesha kuwa hana tena maambukizi ya virusi vya corona.
Kupitia instagram ameandika hivi;
Nimshukuru Allah ππ½ na pia niwashukuru wote mlionitumia msg, comments, DM na dua zenu. Bila kuwasahau Temeke Isolation Centre kwa kuwa bega na bega pamoja na mie bila kunichoka pale nilipokuwa nimezidiwa, na shukurani zangu zingine ziende kwa Madaktari bingwa kujua maendeleo yangu mara kwa mara na pia Serikali yangu na viongozi wake husika Wizara na Mkoa walikuwa hawana ubaguzi kutujulia hali na kutupa moyo na kutupa mahitaji tutakayo. Naomba niwape taarifa ndugu yenu, kijana wenu nimechukuliwa vipimo mara mbili na nimekutwa NEGATIVE na kwa sasa nipo huru. Ila naomba tuendelee kujikinga na kufata ushauri wa viongozi wetu na kuacha maelekezo ya utashi yasiyokuwa na uhakika. ALLAH IS GREAT ππ½ππ½ππ½
Machi 19 mwaka huu alibainika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo vinavyosababisha homa ya mapafu, baada ya kutembelea nchi ambazo tayari zilikuwa na maambukizi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment