Polisi wamepiga risasi na kuwaua waandamanaji 18 nchini Myanmar, ofisi ya Umoja wa Kimataifa ya kutetea haki imesema katika siku ambayo maandamano ya kupinga mapinduzi yamekumbwa na mauaji mabaya.
Vifo vimeripotiwa katika miji kadhaa ikiwemo Yangon, Dawei na Mandalay baada ya polisi kutumia risasi halisi na vitoa machozi.
Vikosi vya usalama vilianza msako uliokumbwa na vurugu siku ya Jumamosi baada ya wiki kadhaa za maandamano ya amani kupinga mapinduzi ya kijeshi ya Februari mosi.
Viongozi wa serikali, miongoni mwao Aung San Suu Kyi, waliondolewa madarakani na kuzuiliwa.
Kanda za video katika mitandao ya kijamii zinaangazia matukio ya siku ya Jumapili zikiwaonesha waandamanaji wakitoroka huku polisi wakiwakimbiza, vizuizi vya muda vya barabarani vikiwekwa, na watu kadhaa waliokuwa wamelowa damu wakielekezwa kwingine.
Oparesheni hiyo iliimarishwa siku ya Jumapili huku viongozi wa mapinduzi wakipambana kuvunja uasi wa raia ambao haujaonesha dalili ya kumalizika.
Mshauri wa Usalama wa Umoja wa Mataifa Jake Sullivan amesema utawala wa Biden unaandaa "hatua za ziada" dhidi ya wale waliyohusika na msako huo wa vurugu.
"Tutaendelea kushirikiana kwa karibu na washirika wetu kuratibu yanayoendelea katika eneo la the Indo-Pacific na ulimwengu mzima kuwawajibisha wanaohusika na vurugu," alisema katika taarifa siku ya Jumapili.
Marekani tayari imewawekea vikwazo viongozi wa kijeshi wa Myanmar tangu jeshi lilipochukuwa madaraka.

No comments:
Post a Comment