Search This Blog

Sunday, February 28, 2021

Mwambusi atangaza kurejea Yanga

 


ALIYEKUWA kocha msaidizi wa kikosi cha klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa kwa sasa yupo fiti kurejea ndani ya kikosi hicho, hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji wa jino.

Mwezi mmoja uliopita, Mwambusi alitangaza kujiuzulu wadhifa wake ndani ya kikosi cha klabu ya Yanga, hii ni baada ya kushauriwa na daktari kutokana na kuwa na matatizo hayo ya kiafya ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Nizar Khalfan.

Akizungumzia maendeleo yake Mwambusi amesema: “Tayari nimepata matibabu ya jino, na ni kama wiki mbili zimepita tangu nifanyiwe upasuaji, naendelea vizuri na sina maumivu kama ilivyokuwa mwanzo.

“Wanamichezo waniombee nipone ili niweze kurejea katika majukumu yangu kama ilivyokuwa awali, na endapo nitakuwa sawa basi naweza kurejea Yanga”



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...