Mmiliki mwenza wa klabu ya Inter Miami David Beckham anasema kwamba angependa kuwasajili katika klabu yake wachezaji kama vile Lionel Messi wa Barcelona na washambuliaji wa Portugal na Juventus Cristiano Ronaldo katika klabu yake katika ligi ya Marekani ya MLS. (Mirror)
Bayern Munich wamewasilisha ombi la £39m kumnunua beki wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 29. (Tuttomercatoweb, via Caught Offside)
Mkurugenzi wa kiufundi katika klabu ya AC Milan Paolo Maldini anataka kufanya mazungumzo na Chelsea kuhusu mbadala wa kubadilisha uhamisho wa mkopo wa beki wa kati Fikayo Tomori katika klabu hiyo ya Serie A kuwa wa kudumu . (Sky Sports)
Real Madrid wamejiunga na Manchester City pamoja na Juventus katika kuonyesha hamu ya kiungo wa kati wa Sassuolo na Itali Manuel Locatelli, 23. (Calciomercato - in Italian)
Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp anasema kwamba mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah ni mchezaji muhimu wa klabu hiyo na anatumai kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atasalia katika klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi. (Liverpool Echo)
Burnley na Newcastle United wanachunguza beki wa Portugal Nuno Tavares huku klabu ya Itali Napoli ikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 wa Benfica. (O Jogo - in Portuguese)
Meneja wa Everton Carlo Ancelotti anasema kwamba klabu hiyo ilimsaini kiungo wa kati Abdoulaye Doucoure, 28, kutoka Watford kutokana na pendekezo lililotoka kwa mkurugenzi wa soka, Marcel Brands. (Liverpool Echo)
Klabu ya Carlisle hujipatia £10,000 kila mara Manchester United inapomtumia kipa Dean Henderson, 23,ikiwa ni pamoja na makubaliano ya kandarasi yake wakati klabu hiyo ya daraja la pili ilipomuuza kipa huyo katika klabu hiyo ya Old Trafford akiwa na umri wa miaka 14. (Sun)

No comments:
Post a Comment