Search This Blog

Wednesday, June 30, 2021

IGP Sirro afanya mabadiliko madogo ya Makamanda wa Polisi


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP),  Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo kwa makamishna na makamanda wa Polisi watatu kwa lengo la kuongeza ufanisi kwenye mikakati ya kubaini, kuzuia na kukabiliana na uhalifu.

Taarifaimetolewa Msemaji wa Jeshi hilo,  David Misime imeeleza kuwa kamishna msaidizi wa polisi  (ACP) Joseph Konyo amehamishwa kutoka kitengo cha maadili makao makuu ya polisi Dodoma na kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma .

Kamanda Konyo anachukua nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma (ACP) Simon Maigwa ambaye anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro

Taarifa hiyo inaeleza kuwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (ACP) Amon Kakwale amehamishwa katika kamisheni ya operesheni na mafunzo makao makuu ya polisi Dodoma.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...