Shirika la Fedha Duniani IMF limeidhinisha mkopo wa kiasi cha dola bilioni 2.5 kwa Sudan, na pia Benki ya Dunia imesaini makubaliano ya kihistoria ya kutoa unafuu wa punguzo la deni la karibu dola bilioni 50 kwa taifa hilo masikini.
Tangazo hilo linatolewa baada ya IMF kuhitimisha makubaliano ya mataifa wahisani 101, ambayo yameiruhusu Sudan kufuta kiasi cha deni cha takribani dola bilioni 1.4, hatua ambayo italifanya taifa hilo liweze kupata msaada mpya.

No comments:
Post a Comment