Search This Blog
Monday, September 30, 2019
Kamanda Aeleza, Jambazi wa Muda Mrefu alivyouawa
Mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni jambazi, ameuawa kwa kupigwa risasi katika majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi, tukio lililotokea majira ya saa 7:30 mchana eneo la Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Ilala, Zuberi Chembela amesema kuwa mhalifu huyo alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu na kwamba alianza kufukuzwa kuanzia eneo la Magomeni.
''Hilo tukio naomba mmpigie Afande Mambosasa kwasababu huyo mhalifu alikuwa anakimbizwa kutokea Magomeni, kwahiyo alivyofika hapo akazingirwa na ndipo kikatokea hicho kilichotokea na hilo tukio limehusisha mikoa miwili, Ilala na Kinondoni hivyo ni vyema mkamtafuta Mambosasa atalizungumzia vizuri zaidi'', amesema Chembela.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa, amethibitisha kupokea taarifa ya tukio hilo akisema, ''ni kweli tukio hilo limetokea, askari wetu walikuwa wanapambana na huyo jambazi, alikuwa anafuatiliwa na hiyo milio iliyosikika walikuwa wanapambana naye na tumefanikiwa kupata Bastola moja'', amesema SACP Mambosasa.
Aidha Kamanda Mambosasa amesema kuwa atatoa undani wa tukio hilo, punde tu atakapopokea vielelezo vyote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment