Kulingana na takwimu zisizo rasmi, watu wasiopungua 1,643 walizuiliwa katika maandamano yaliyoendelea nchini Urusi wakitaka kuachiliwa huru kwa mpinzani wa Urusi Aleksey Navalny.
Maelfu ya watu, haswa wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu, walihudhuria maandamano yaliyopigwa marufuku katika miji mingi ya nchi, licha ya tahadhari za polisi.
Kulingana na mashirika ya haki za binadamu nchini Urusi, watu 1,643 pamoja na mke wa Navalny, Yuliya Navalnaya, walikamatwa, ambapo 338 kati yao walikuwa katika mji mkuu wa Moscow.
Wakati huo huo, waandamanaji wengine walikusanyika karibu na Gereza la Matrosskaya Tishina, ambapo Aleksey Navalny alizuiliwa, na kupiga kelele wakitoa wito kwa serikali.

No comments:
Post a Comment