Search This Blog

Sunday, January 31, 2021

Utekelezaji miradi ya umeme mto Rumakali na Ruhudji, umefika patamu waziri wa nishati afika eneo la mradi

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Katika kutekeleza azma ya serikali ya kuhakikisha upatikanaji umeme nchini unakuwa wa uhakika na kuwapunguzia wananchi mzigo wa ghalama za umeme pamoja na kukuza uchumi wa viwanda,serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali ya kuzalisha umeme.


Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa Rumakali uliopo wilayani makete utakaozalisha megawati 222 pamoja na mradi wa Ruhudji uliopo mjini Njombe utakaozalisha megawati 358 na kufanya onezeko kubwa la nishati ya umeme huku mkoa wa Njombe ukiwa ni wa kimkakati huku ukiwa ni mkoa wa pili kwa uzalishaji mkubwa wa nishati ya umeme.


Waziri wa nishati Dkt,Medard Kalemani amebainisha hayo januari 30,2021 alipofika mkoani Njombe pamoja na kutembelea eneo la maporomoka yam to Rumakali uliopo kata ya Kipagalo wilayani Makete na kubainisha kuwa mradi huo utakaozalisha 222 MW ,tayari utekelezaji umeanza na serikali imeshatoa shilingi bilioni 899 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.


Kalemani amefafanua kuwa msukumo wanaoweke katika utekelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme ni kwasababu uzalishaji wake ni wa ghalama nafuu na kupelekea wananchi kupata bila changamoto kubwa ukilinganisha na aina nyingine ya umeme.


“Uzalishaji wa umeme kwa maji ni ghalama nafuu kulinganisha na vyanzo vingine,kuzalisha umeme kwa maji Unit moja inaghalimu kiasi cha sh.36 tu huku vyanzo vingine ni zaidi y ash.103 na kuendelea.Mradi wa Mwl,Nyerere utakapokamilika utawapunguzia wananchi mzigo wa bei za umeme na bei zitashuka sana”alisema Kalemani


Aliongeza “Utekelezaji wa mradi wa Rumakali na Ruhudji umekwishaanza,timu ya kutekeleza mradi huu imeshaundwa na kimsingi timu hiyo imenza na shughuli za matayarisho ya kuanza miradi tajwa na kufika Julai 02,2021 ujenzi rasmi wa miaradi ya Rumakali na Ruhudji utaanza”aliongeza Kalemani


Mbali na hayo amesema katika mradi wa Rumakali kitajengwa kituo cha kupokea umeme na utasafirishwa hadi Mwakibeta jijini Mbeya umbali wa kilomita 150 na vijiji vyote vitakavyopitiwa na njia ya kusafirisha umeme vitapatiwa nishati hiyo.


Aidha amesema bado mikakati ya ukamilishwaji wa kazi ya kupeleka umeme vijijini unaendelea na taratibu zote za kufikisha umeme vilivyosalia nchini zimekamilika ambapo februari 05 mwaka huu wakandarasi wataanza kuingia kazini ili kukamilisha vijiji vilivyosalia ndani ya miezi 18 kwa kuwa tayari serikali imeshatoa shilingi bilioni 851 kwa ajili ya kazi hiyo huku akiwataka wananchi ambao ambao bado vijiji vyao havijapatiwa huduma kuwa wavumilivu.


Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Rumakali,meneja uendelezaji wa vyanzo vya umeme kutoka shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mhandisi Toto Zedekia amesema,wamejiridhisha baaday kufanya utafiti na tathmini ya kina kuwa maporomoko yam to Rumakali una maji mengi na yakutosha kuzalisha umeme.


“Tumejiridhisha vya kutosha mto huu una maji mengi na kutosha kwa kuwa una mita za ujazo 13 kwa sekunde” na kuongeza kuwa


“Litajengwa bwawa lenye urefu wa mita 870 kutoka kingo moja kwenda nyingine na urefu wa kwenda juu utakuwa ni mita 70 na litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji takribani lita 280”


Awali akitoa tarifa ya hali ya upatikanaji wa umeme mkoani Njombe,kaimu meneja wa kanda ya Nyanda za juu kusini Maghalib Mhandisi Yusuph Salim amesema,hali ya umeme mkoani humo imeimarika zaidi tofauti na miaka ya nyuma na hali hiyo imechangiwa na kukamiilika kwa mradi wa Makambako hadi Songea.


Aidha mhandisi Yusuph amesema upatikanaji wa umeme mijini na vijijini ni wa uhakika na kupitia miradi ya umeme vijijini (REA),takribani vijiji 293 vya mkoa wa Njombe vimefikiwa na huduma ya nishati huku vikisalia 88 ambavyo vyote vimeingizwa katika mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili huku 90% ya miradi ya REA ikiwa imekamilika.


Baadhi ya wananchi wa kata ya kipagalo wamefurahishwa kuona mwanga wa kuanza kwa mradi wa umeme katika mto Rumakali kwa kuwa wamekuwa wakisubiri tangu miaka 40 iliyopita huku wakiamini kupta fursa za kiuchumi mradi huo utakapoanza rasmi.


Katika ziara hiyo waziri wa nishati Dkt,Medard Kalemani ameongozana na maafisa waandamizi kutoka wizara ya nishati na shirika la umeme Tanzania (TANESCO)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...