Search This Blog

Sunday, January 31, 2021

Maandalizi ya uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Manyara yapambana moto

 


Na John Walter- Manyara

Kamati ya maandalizi ya Uchaguzi wa marudio wa Chama cha Soka mkoa wa Manyara (MARFA) imetangaza majina yaliyopitishwa kugombea nafasi za mbalimbali za uongozi wa chama hicho.


Majina hayo yamepatikana baada ya usaili uliofanyika kwa wagombea hao januari 23,2021.


Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji. 


Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa  na Katibu wa Kamati Mussa Rehani, imetaja majina ya wagombea na nafasi ya mwenyekiti ni Gerald Mtui na Fratern Kwahhison, Makamu Mwenyekiti yupo Victor Kijazi.


Katika nafasi ya Katibu mkuu, mgombea ni  Wilhelmon Mayo na mgombea  katibu msaidizi ni Denis Bakuza.


Mweka hazina aliechukua fomu ya kugombea ni mtu mmoja pekee Jumanne Dotto.


Mjumbe Mwakilishi Vilabu Albert Ferdinand, mjumbe mwakilishi mkutano mkuu TFF Hassan China na mjumbe mwakilishi soka la wanawake Rose Mkindi.


Nafasi nyingine ni wajumbe Kamati ya utendaji ambao ni Charles Mligo, Wilfred Mwanyika, Charles William pamoja na Nuru Mkireri.


Katibu wa Kamati ya maandalizi ya uchaguzi wa marudio wa chama cha soka mkoa wa Manyara Mussa Rehani amesema uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Februari 13,2021 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...