Search This Blog

Sunday, January 31, 2021

Urusi yajiandaa kwa maandamano makubwa ya mpinzani utawala wa Urusi Alexei Navalny

 


Mamlaka nchini Urusi zimefunga vituo vya treni na basi vya abiria na kuzuwia shughuli za watu katika mji mkuu wa nchi hiyo Moscow kabla ya mkutano maandamano makubwa yakiyopangwa kwa ajili ya kumuunga mkono kiongozi wa upinzani na mkosoaji wa utawala Urusi Alexei Navalny.


Migahawa mingi na maduka katikati ya mji huo vitafungwa na usafiri wa treni wa chini ya ardhi utabadilishwa.


Zaidi ya watu 4,000 walikamatwa kote nchini Urusi wakati wa mikutano wiki iliyopita.


Bw Navalny alifungwa jela aliporejea nchini Urusi baada ya kupona jaribio la kumuua kwa sumu inayoua neva.


Mpinzani huyo wa serikali ya Urusi alitakamtwa tarehe 17 Januari kwa kutotimiza masharti ya hukumu iliyoahirishwa dhidi yake. Alikuwa ndio amewasili tu kutoka mjini Berlin, ambako aliishi kwa miezi kadhaa akiendelea kupona shambulio la sumu ambalo nusura limuue.


Mamlaka nchini Urusi zinasema kuwa alipaswa kuripoti polisi kwasababu ya kesi yake ya ubadhilifu wa mali ya umma iliyoahirishwa.


Bw Navalny alipinga kukamatwa kwake jambo ambalo anasema "ni ukiukaji wa sheria ", na kuongeza kuwa mamlaka zinafahamu fika kwamba alikuwa akitibiwa mjini Berlin kutokana na sumu ya Novichok , ambayo alipewa Urusi mwezi Agosti mwaka jana.


Maandamano makubwa ya kumuunga mkono Bw Navalny yameanza kufanyika nchini Urusi , licha ya onyo jipya kutolewa na polisi kuhusu mikusanyiko ya watu ambapo polisi wanawashikilia watu zaidi ya 250 , kwa mujibu wa kikundi cha maandalizi ya maandamano hayo OVD-Info protest monitoring group. Maandamano katika mji mkuu Moscow yanatarajiwa kufanyika baadae leo.


Washirika kadhaa wa Bw Navalny wamekuwa wakifungwa tangu juma lililopita na wengine , akiwemo kaka yake na mwanaharakati wa kikundi cha Pussy Riot Maria Alyokhina, ameweka katika kifungo ha ndani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...