Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC imetangaza kuwa vikosi vyake vimefaulu kuwafurusha wanamgambo kaskazini mwa Msumbiji.
Lakini vikosi hivyo vitasalia nchini humo kwa muda usiojulikana ili kuendelea kudhibiti hali. Mkuu wa ujumbe wa jumuiya hiyo nchini Msumbiji Mpho Molomo amesema ugaidi ungali kitisho kikubwa kwa Msumbiji.
Ameongeza kuwa SADC itatuma wanajeshi zaidi wa ardhini japo wanamgambo wameshafurushwa na kutawanyika kutoka eneo lenye utajiri wa gesi na mafuta Cabo Delgado.
Jumuiya hiyo ya nchi 16 haijawahi kuweka wazi idadi ya wanajeshi waliopelekwa Msumbiji tangu operesheni yao ilipoanza mwezi Julai.
Machafuko hayo ya wanamgambo yamesababisha vifo vya watu 3,340 na zaidi ya watu 800,000 kulazimika kuyahama makwao.
No comments:
Post a Comment