Search This Blog

Friday, October 15, 2021

Marekani yarejea katika Baraza la Haki za Binadamu la UN


Marekani imerejea katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, miaka mitatu na nusu tangu ilipojiondoa kwenye baraza hilo. 
 
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilichagua wanachama wapya 18 kujiunga na baraza lake la Haki za Binadamu, na nchi hizo zitaanza kuhudumu Januari mosi kwa kipindi cha miaka mitatu.
 
 Kando na Marekani, mataifa mengine yaliyochaguliwa ni pamoja na Argentina, Benin, Cameroon, Eritrea, Finland, Gambia, Honduras, India, Kazakhstan, Lithuania, Luxembourg, Malaysia, Montenegro, Paraguay, Qatar, Somalia na Umoja wa Falme za Kiarabu.
 
 Hata hivyo kwa mara nyingine uchaguzi wa Eritrea uliibua maswali kuhusu kuwa na mataifa yenye utawala wa kimabavu kuhudumu kwenye baraza hilo. 
 
Baraza hilo limetwikwa jukumu la kutetea haki za binadamu kote ulimwenguni, kushughulikia ukiukaji wa haki hizo pamoja na kutoa mapendekezo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...