Newcastle huenda wakatumia hadi pauni milioni 190 kumpata mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 28, na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, lakini "ndani ya uwezo wao". (Telegraph - subscription required)
Kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte angetaka sana kuchukua nafasi ya Steve Bruce katika klabu ya Newcastle. (Sun)
Philippe Coutinho, 29, huenda akatua uwanja wa St James' Park kutoka Barcelona mwezi Januari. (Sport - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandes, 27, amekuwa akiwasiliana na mchezaji nyota wa nyota wa Leeds Mbrazil Raphinha, 24, kuhusu uwezekano wa kuhamia Manchester United. (Mirror)
Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Demba Ba, 36, amejitolea kurejea tena kuchezea klabu hiyo baada ya kununuliwa. (Star)
Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, 28, ni chaguo la kwanza la Real Madrid mwakani, kandarasi yake na Chelsea ikitarajiwa kukamilika msimu huu wa joto. (ABC, via Mail)
Kiungo wa kati wa England Ainsley Maitland-Niles, 24, na kiungo wa kati wa Misri Mohamed Elneny, 29, huenda wakaondoka Arsenal kwenda kusaka nafasi ya kucheza soka ya safu ya kwanza mwezi Januari. (Sun)
Barcelona wanamsaka mchezaji wa safu ya kati mwezi Januari na wanamnyatia mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya Manchester United Donny van de Beek na Mfaransa Tanguy Ndombele, 24 ambaye anacheza soka ya kulipwa huko Tottenham. (Sport - in Spanish)
Ole Gunnar Solskjaer hayuko tayari kumwachilia Van de Beek aondoke Manchester United mwezi Januari na atazuia hatua yoyote ya kumsaini. (ESPN)
Mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 33, alikataa ombi la Juventus kutaka ajiunge nao kabla ya kwenda Barcelona okwa uhamisho wa bure baada ya kuondoka Manchester City msimu wa kiangazi. (Sport - in Spanish)
Juventus wanapanga kumuuza kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 30, Januari mwakani, huku West Ham na Everton wakionesha nia ya kutaka kumnunua. (Calcio Mercato - in Italian)
Leicester wanapania kumsajili mchezaji nyota wa Real Madrid na Uhispania Isco, 29,ambaye mahitaji yake ni mengi kwa klabu hiyo mji mkuu, Uhispania. (Fichajes - in Spanish)
No comments:
Post a Comment