Search This Blog

Saturday, October 9, 2021

Marekani kukutana rasmi na Taliban leo


Marekani itafanya mazungumzo rasmi na wanamgambo wa Taliban kwa mara ya kwanza, tangu Marekani ilipoondoa vikosi vyake nchini Afghanistan. 
 
Hayo yamethibitishwa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani mjini Washington, katika tangazo lililosema kwamba ujumbe wa nchi hiyo utakutana uso kwa uso na wawakilishi wa ngazi ya juu wa Taliban katika mji mkuu wa Qatar, Doha leo Jumamosi na kesho Jumapili. 
 
Marekani inataka kuwahimiza watawala hao wapya wa Afghanistan kuheshimu haki za binadamu na kuruhusu mashirika ya msaada wa kiutu kuwafikia wenye mahitaji
 
. Tangu kuchukuwa udhibiti wa nchi katikati ya mwezi Agosti, Taliban wamekuwa wakifanya kila juhudi kutambuliwa kimataifa. Marekani imesema kukutana nao haimaanishi kuuutambua utawala wao.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...