Rais wa China Xi Jinping amesema "muungano" na Taiwan "lazima utimizwe", huku mvutano juu ya kisiwa hicho ukiendelea.
Bw. Xi alisema muungano unastahili kufikiwa kwa njia ya amani, lakini akaonya kwamba watu wa China wana "utamaduni mtukufu" unaopinga utengano.
Ikijibu tamko hilo, Taiwan ilisema hatma yake iko mikononi mwa watu wake.
Taiwan inajichukulia kama taifa huru, huku China ikitaja kuwa mkoa wake uliojitenga.
Beijing imefutilia mbali uwezekano wa kutumia nguvu kufikia muungano huo
Bw. Xi ameingilia suala hilo baada ya China kutuma idadi kubwa ya ndege za kijeshi katika eneo la ulinzi wa anga la Taiwan katika siku za hivi karibuni.
Baadhi ya wachambuzi wanasema hatua hiyo huenda ni onyo kwa rais wa Taiwan kabla ya kisiwa hicho kuadhimisha sikukuu ya kitaifa siku ya Jumapili.
Waziri wa ulinzi wa Taiwan amesema mvutano wao na China umekuwa mbaya zaidi katika miaka 40 iliyopita.
Lakini matamshi ya Jumamosi ya Bw Xi yalionekana kuwa ya maridhiano zaidi na Taiwan ikilinganishwa na tamko la Julai, ambapo aliahidi "kuvunja" jaribio lolote la uhuru wa Taiwan.
Akiongea katika hafla ya kuadhimisha miaka 110 ya mapinduzi ambayo yaliangusha nasaba ya mwisho ya ufalme wa China mnamo 1911, alisema umoja kupitia "njia ya amani" ni bora "zaidi kwa masilahi ya taifa ya Wachina, na wenzao wa Taiwan".
Lakini akaongeza: "Hakuna mtu anayepaswa kudharau uamuzi thabiti wa watu wa China, dhamira thabiti, na uwezo mkubwa wa kutetea himaya yake."
"Jukumu la kihistoria la kuungana tena nchi yetu lazima litimizwe, na hakika litatimizwa," alisema.
Bw. Xi alisema anataka kuona muungano ukifanyika chini ya "nchi moja, mifumo miwili" mpango, sawa na ule ulitumiwa Hong Kong, ambayo ni sehemu ya China lakini ina kiwango cha juu cha uhuru.
Lakini ofisi ya rais wa Taiwan ilisema kwamba maoni ya umma yalikuwa wazi dhidi ya sera ya nchi moja, mifumo miwili.
No comments:
Post a Comment