Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Frances na viongozi wengine wa kidini wametoa wito wa pamoja, kama suluhisho la kuiokoa dunia kutokana na mgogoro wa ikolojia usio na kifani, ambao utawasilishwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP26) mwezi ujao.
Mkutano huo wa jana uliopewa jina la "Imani na Sayansi", ulikutanisha viongozi wa dini tofauti zenye waumini wengu ulimwenguni. Papa Francis amesema mkutano wa COP26 utakaofanyika mjini Glasgow, unatoa matumaini kwa vizazi vijavyo.
Nyaraka hiyo alikabidhiwa Waziri wa Mambo ya nje wa Italia Luigi Di Maio na Alok Sharma wa Uingereza, ambae ni rais wa mkutano wa COP26.
No comments:
Post a Comment