Venezuela itafungua mpaka wake na Colombia hii leo baada ya kuufunga kwa zaidi ya miaka mitatu kutokana na mivutano ya kisiasa.
Taariga hiyo imetolewa jana na Makamu wa Rais wa Venezuela Delcy Rodriguez kupitia televisheni ya taifa. Venezuela iliufunga mpaka huo Februari 2019, baada ya upande wa upinzanu ukisaidiwa na Colombia na Marekani kujaribu kuingiza misaada ya kiutu nchini humo bila ya ridhaa ya Rais Nicolas Maduro
. Serikali ya Venezuela ilidai kwamba uingizaji huo wa misaada ulikuwa ni kisingizia cha kutaka kumpindua Maduro. Upinzani wa Venezuela na washirika wake wanamshutumu Maduro kwa wizi wa kura katika uchaguzi wa marudio wa mwaka 2018.
Maduro, anaeegemea siasa za ujamaa, anasema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, badala yake anadai vikwazo vya kiuchumi alivyowekewa na Marekani ndiyo sababu ya mgogoro wa kiuchumi wa Venezuela.
No comments:
Post a Comment